Jimbo la Tigray Ethiopia limeonesha ubaya wa utawala wa majimbo Tanzania

Jimbo la Tigray Ethiopia limeonesha ubaya wa utawala wa majimbo Tanzania

Melesi Zenawi alikosea kuweka majeshi kwenye hayo majimbo. China na USA na Germany mbona zimendelea kwa Sera ya majimbo?
 
Melesi Zenawi alikosea kuweka majeshi kwenye hayo majimbo. China na USA na Germany mbona zimendelea kwa Sera ya majimbo?
Zenawi aliwaamini sana watigray kwakuwa alikuwa ni sehemu yao. Watigray walikuwa na jeshi maalum lenye silaha imara la kuulinda mpaka wa tigray/ethiopia dhidi ya eritrea
 
Jimbo la Tigray Ethiopia kuna vita wanasiasa wakora wanataka kujitenga, jimbo la Kaduna kule Nigeria wakora wanataka kujitenga, kule Kabregado Msumbiji wanataka kujitenga, Katalunha Hispania wahuni wanataka kujitenga.

Kumbe hata Tanzania tukianzisha utawala wa majimbo huenda kutakuwa na majimbo ambayo yanaweza kutamani kujitenga kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kikabila, kidini na za kilevi tu. Maana zipo dini, makabila ambayo yana malalamiko yao hadi sasa.

Mfano, yako makabila makubwa yanayohoji kwanini Kiswahili kiwe lugha ya taifa.

Nadhani tuko sahihi bado mpaka sasa kuwa hivi tulivyo, tuboreshe tu mapungufu.
Sio kweli kinachoangaliwa ni katiba usika na vipengele vilivyoanzisha utawala wa majimbo. Majimbo ni utawala bora zaidi duniani. Unawapa watawaliwa uamuzi wa kumchagua wamtakaye. MAREKANI wamekuwa na mfumo huo kwa miaka zaidi ya 200 na hajawai teteleka. Chukulia jimbo la uchaguz lenye watu elf 60 linachagua mwakilishi wake bungeni. Dar es salaam yenye watu mil 6 mnatawaliwa na mtu ambaye hamjamchagua na hamuzi kumuondoa. Chini ya majimbo haiwezekan
 
Sawa, lakini unapousifia uzuri wa majimbo ya Merekana usisahau kuulaumu ubaya wa majimbo ya Ethiopia (Tigray), Somalia(Portland), Nigeria (Kaduna, delta), Msumbiji (Cabo delegado), DRC (Katanga, Kivu), Sudani Kusini, Ivory coast (English speaking province), nk wanaotarajia kujitenga. Usiilinganishe Marekani na Tanzania kwenye haki za binadamu na demokrasia utakuwa hujui unachokisema. Hivi Ni kiongozi gani Afrika anayeweza kusema uchaguzi umeibiwa lakini akaendelea kujiandaa kuiachia Ikulu bila hata mtu mmoja kung"olewa jino?

Ukiruhusu serikali ya majimbo Tz, iko siku utasikia kiongozi wa jimbo akiwaambia wenzake kuwa "sisi ndio tuliostaarabika kuliko kuliko wengine nchini, hatuna utamaduni wetu wala waganga wa kienyeji, hivyo hatuwezi kutawaliwa Rais kutoka makabila ya kichawi na kishenzi, hivyo tujitenge" wataomba wakoloni wawasaidie kujitenga kwa malipo ya kuwapa zawadi ya mlima fulani au mbuga.
 
Back
Top Bottom