Tunakoelekea ni wazi kabisa kuwa serikali yetu ,viongozi wa dini na jamii Kwa ujumla imeamua kuwa suala la ndoa ni la mtu binafsi na tamaa zake Mwenyewe hakuna kanuni Wala SHERIA ya kulinda ndoa za watu waliloapa na kupewa hati au shahada ya Ndoa na serikali. Wanaoumia Kwa sasa ni watoto.
Ni wazi kabisa kuwa wahanga wengine ni wanaume kwani jamii haiweki mkakati wa kulinda watoto waliozaliwa kwenye ndoa zaidi ya kuweka SHERIA kali za mirathi lakini mirathi isiyo na wazazi wenye maelewano . Hapa anayeumia ni Mwanaume. Wanawake wengi Kwa Sasa wanatengeza migogoro kutokana na Hali ngumu ya kimaisha huku wao wakiwa wanamahitaji makubwa kuliko vipato vyao.
Maumivu yatakua makubwa sana Kwa wanaume kwani Mwanamke akiachana na mume wake hata kama yeye ndio alikua Malaya kwenye familia Bado jamii inasema Fulani kamuacha mkewe na kumtelekezea watoto. Kinachofuata ni watoto kujenga Chuki dhidi ya baba yao. Na Kwa hali ya Sasa mwanaume akisema anaoa mke Mwingine ndio hatari zaidi kwani huyo mwingine anakua amewaza mambo yake binafsi na sio familia Tena.
Inakua ni mzunguko wa uhasama na migogoro kutokana na SHERIA ya Ndoa kuwa dhaifu Sana na sijui SHERIA hiyo mbovu iliyoungwa miaka sabini kipindi ambacho asilimia 98 ya watoa maamuzi walikua ni wanaume Huko Bungeni na serikalini Bado inaendelea kutumiaka.
Wakati huo sharia ya Ndoa inatungwa Hali ya wanaume kuchepuka na wake za watu sio TU ilikuwa Kwa hiyari Bali pia ilikua ni Kwa lazima na hapakua na sharia Kali ya ubakaji.
Wakati huo ndio wakati ambaoa mabosi wengi walikua wanazaa na masekretari bila kujali kuwa ni wake za watu. Miaka hiyo ni ilikua ni miaka ya zama za giza kweli kweli. Wanawake walikua wanabakwa maofisini bila kulalamika kokote mana bosi atawasiliana na bossi Mwenzake waliyekuwa naye Jana kwenye pombe au waliyesoma naye na atampigia simu ya mezani na kutanguliza Taarifa zako mbaya kabla hujafika kutoa malalamiko yako kwake.
Miaka hiyo huwezi kuona Nesi anaolewa , mana muda wowote atahitajika na bosi wake , hata walimu wa kike wale Wazuri zuri Kwa sura na maumbo ilikua ni chakula Cha wakurugenzi ,maofisa Elimu na wakaguzi, Miaka hiyo ilikua sio rahisi kumwona Polisi wa kike anaolewa kirahisi hasa na raia kwani mabosi walikua wanaona ni halali kwao apende asipende halikadhalika mwanajeshi wa kike akiolewa kirahisi labda awe ni mtoto wa mkubwa na aolewe na mkubwa lakini akiolewa na mdogo basi anakuwa ni WA mabosi apende asipende. Hata wakubwa wengine Huko juu Hali ilikua ni hiyo hiyo. Wanaume walitunga sheria NYEPESI sana ya Ndoa iliyowabeba zaidi Wazinifu na kutupilia mbali uadilifu kwenye NDOA. Mwanaume maskini akiporwa mke wake au mchumba wake anaambiwa nenda mahakamani ukafungue kesi ya madai. Au kama huwezi njoo nikulipe pesa utulie kimya na kama hutaki basi nitakupoteza. Yaani mwanaume mwenye mke halali yeye ndio anatishiwa na kuambiwa akae kimya. Sasa mwanaume Mwingine maskini na anakubali kupewa pesa ili akatafute naye mchepuko wake maisha yaendelee.
Wakati huo fumanizi live liliwekwa kama kigezo Cha kufungua kesi za madai. Lakini pia fumanizi live lilimpa mtu unafuu mahakamani endapo angefanya mauaji dhidi ya mgoni wake.
Wakati wanatunga SHERIA hiyo walijua wazi kuwa hapakuwa na teknolojia ya kubaini Kwa uwazi matukio yanayofanywa Kwa Siri labda mtu aone barua ya mapenzi na pia anaweza akaikana na ushahidi ukawa mdogo.
Mchezo ukawa ndio huo Kwa muda mrefu mpaka lilipikuja suala la Beijing na Haki za Wanawake na usawa wa kijinsia. Kwa kweli mabadiliko hayo yalibadili Kwa kiwango kikubwa unyanyasaji wa kijinsia na masuala ya ubakaji uliokuwa unaofanywa na mabosi maofisini na wenye vyeo kunyanyasa Wanawake bila kujali kuwa ni wake za watu au laa.
Mafanikio hayo yaliendana na mabadiliko ya SHERIA za ubakaji na udhalilishaji kwenye masuala ya mapenzi.
SHERIA Kali ikawa muarobaini na Wanawake wakawa na ahueni ya kufanya ngono na mabosi wao Kwa hiyari sio Kwa kulazimishwa Kwa manyanyaso.
Mabadiliko ya teknolojia yanafanya suala la mahusiano kuwa Tete sana Kwa jamii isiyo na watu waadilifu. Mtu anaweza akawa Ulaya akatongoza Wanawake au wanaume kumi Kwa wakati mmoja na akapata apointimenti tofauti tofauti na wakati huo huo yupo kitandani na mkewe au Mumewe huku akiwa anampa maneno mazuri ya kumwaminisha kuwa anampenda na hakuna kama yeye Mbinguni na Duniani. Jamii zetu za Kiafrika hazikuandaliwa kwenye suala la kujizuia na tamaa za macho ,Mali,fedha na Mwili pia. Ukimweka ofisini mwafrika bila SHERIA Kali ataiba mpaka afikisi kampuni. Ukimwachia Shamba au mifugo ataiuza ,ukimkaribisha kwako hata kama alikua na shida hafai kumwacha na mkeo au mumeo ataanza kumtongoza. Kesi ya masuala la kindoa au kifamilia ikifika kwenye vyombo vya SHERIA inaangukia Kwa watu wale wale waliojaa tamaa na inakua kama kesi ya mbuzi kapelekewa fisi.
Matokeo yake ni watu kuuana na kufanyiana jeuri na kudhalilishana mitandaoni kama njia Moja wapo ya kulipa kisasi.
Na ifahamike kuwa kisasi huwa ni njia mbadala ya kusamehe. Mtu akilipa kisasi au akilipiwa kisasi na vyombo vya kisheria Kwa kumwadhibu mkosaji basi nafsi yake inaondokana na machungu. Mfano mtu anapomuua mtu Mwingine bila kisasi Kwa muuaji jamii au familia ya muhanga inabaki na machungu makubwa sana hasa inapimuona muuaji akiwa anatanua na kutamba mitaani na kama ana pesa anasema "Njooni niwalipe pesa kama mnataka ".
Lakini endapo ikatokea muuaji anashambuliwa na watu Wenye hasira Kali na kuuawa on the spot au ana kamatwa na kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kunyongwa au kifungo Cha Maisha basi kisasi kinalipwa kisheria na jamii inapata matumaini na furaha inarejea.
Ni wajibu Wa serikali Sasa Kubena jukumu la kutoa adhabu Kali Kwa wakosaji wanaoiangamiza jamii Kwa kuvuruga ndoa za watu. Watoto wengi wanaokua bila baba halali wanakua mashoga mitaani na Wengine wanakuwa watu wasio na huruma.
Vingine basi Kuna agenda ya Siri ya kuimarisha Ndoa za jinsia Moja na kuvuruga jamii na familia. Mana matukio ya MICHEPUKO yanahusisha Zaidi masuala ya kuingiliana kinyume na maumbile. Na inatangazwa kuonyesha kuwa Nje ya Ndoa huduma hiyo ni muhimu na inapatikana sana. Binadamu alivyo anapenda kujaribu kile kinachosifiwa bila vikwazo.
Vijana wengi sana Hawana Imani kabisa na masuala ya Ndoa . Kwa Sasa Hata masuala ya kufunga ndoa ni machache sana. Udanganyifu ni Mkubwa sana. Watoto wengi hawawajui baba zao halisi. Ni jambo baya sana. MTOTO anamjua mama tu Lakini baba hamjui. Watoto kama Hao ndio MAANA wanazidi kuwachukia akina baba na kutoheshimu juhudi Kubwa wanazofanya wanaume hapa Duniani.Chanzi ni tamaa za baadhi ya wanandoa kuzaa Nje ya Ndoa.
Waislam wapaze sauti kuhamasisha Ndoa za wake wengi na kukemea Vijana Kukaa bila kuoa. Lakini pia Sheria Ndoa za Kiislam ziingizwe kwenye Sheria za Ndoa rasmi Ili Wanandoa Wanaofunga Ndoa za Kiislam wawe wanafuata Kanuni za uadilifu Ili wasije wakaona kuwa suala la Talaka linawaumiza kwenye mirathi.
Mana Siku hizi wanawake wengi wanapenda kuvunja Ndoa kama chanzo Cha mapato na kujitafutia nafasi ya kupata mali Huku wakiachwa Watoto wakiwa wanateseka kulingana na Sheria ya mirathi ilivyokaa.
Lakini pia Mapadri waendelee kusisitiza suala la kutii kiapo Cha ndoa. Vinginevyo Sheria ya ibadilike iruhusu wake wengi.Ili kupunguza suala la NYUMBA ndogo na MICHEPUKO kuwa nyingi Kwa wakristo Wakati wameapa kuwa na MKE mmoja na Mume Mmoja.
Wachungaji nao Wahubiri Kwa wazi na kukemea dhambi ya uzinzi bila woga Wa kupoteza waumini mana Siku hizi hasa wanawake wanapenda kwenda FREE CHURCH ambapo wanahubiriwa mambo ya kupata pesa. Kuwa na Maisha ya Juu na starehe za Duniani zaidi Huku wakiwa washirikina na viburi Kwa waume zao.
Manabii Feki nao waache kutembea na wake au waume za watu mana Kwa nyakati hizi Biblia ilishasema kuwa Kila linalofanyika gizani litawekwa kwenye mwanga kweupe. Teknolojia itawaumbua na kuzidi kulichafua Kanisa na Yesu Kristo mwokozi.
Manabii Wa kweli waliopo Kwa uchache wao wazidi kuombea Ndoa na familia Kwani Tangu mwanzo shetani alivuruga Ndoa ya Adamu na Hawa waliokua wanapendana na kuaminiana Lakini ghafla wakajikuta hawaaminiani na wanatupiana lawama. Adamu anasema ni huyu mwanamke uliyenipa. Hawa Naye akashindwa kuheshimu Amri ya Mungu na kumtupia lawama Nyoka.
Jamii ikikubali Mawakala Wa shetani Duniani wanaotumia mbinu zote kuharibu ndoa basi ni wazi kuwa Dunia itapata ánguko kubwa sana. Watu wasio waadilifu kwanye ndoa wanakosa uaminifu karibu Kila Mahali. Wezi Wa Mali za umma mara nyingi wanatafuta pesa kugharamikia zinaa na matokeo yake. Kuna Wakati Hata uhasama Wa kisiasa unasababishwa na visasi kwenye mambo ya mapenzi.
Hivyo shetani anajua wazi kuwa Dunia haiwezi kuwa na utulivu kama watu watakua Wana migogoro ya kimahusiano.