Pre GE2025 Jina la Dkt. Samia latamkwa mara 40 kwenye Hotuba ya Bajeti ya Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ametumia dakika 127 sawa na saa 2 na dakika saba kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25 huku jina la Rais Samia Suluhu Hassan akilitamka mara 40.

Dk Mwigulu ameanza kusoma bajeti hiyo leo Alhamisi, Juni 13, 2024 bungeni jijini Dodoma kuanzia saa 10:04 hadi 12:11 jioni.

Mbali na Dk Mwigulu kulitaja jina la Samia Suluhu Hassan wakati akiwasilisha bajeti hiyo yenye kurasa 173, pia ametaja jina la ‘Mama’ mara 15 wakati akinogesha hotuba yake mathalani amesema: “Ni dhahiri Mama hasemi tu, bali anatekeleza!”

Pia, Dk Mwigulu akielezea mafanikio makubwa ya awamu ya sita amesema: “Hii inadhihirisha kuwa Mama anawapenda sana Watanzania, hivyo basi na sisi Watanzania tusimame na Mama.”

Zaidi soma: Waziri Mwigulu awasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
 
Amelitaja mara chache sana.Maana ningekuwa mimi ningelitaja kila baada ya mstari mmoja. Hii ni kutokana na uchapakazi wa Mama yetu na kazi kubwa alizozifanya kwa Taifa letu zilizogusa maisha ya watanzania na kuinua matumaini kwa wengi.

Rais Samia ameleta nuru na Mwanga katika maisha ya watanzania. Kwa hakika ningelitaja Jina la Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa unyenyekevu mkubwa sana.
 
Na ungelitaja huku ukibubujikwa na machozi🤣🤣🤣
 
Kwa sababu wewe hujui Sayansi ya namba

40 ndiyo namba ya Ukamilifu

Wana wa Israel walisafiri Jangwani miaka 40

Hitma Yako wewe ukidedi ni 40

Za mwizi ni 40

Sasa wewe na elimu Yako ya Memkwa ni kweli ungetaja mara 10000 ila Mwigulu ni Daktari wa Falsafa anaelewa Sayansi ya namba

Ulale unono 😂😂😂😂
 
Unadhihirisha utaahira wako tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…