Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ametumia dakika 127 sawa na saa 2 na dakika saba kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25 huku jina la Rais Samia Suluhu Hassan akilitamka mara 40.
Dk Mwigulu ameanza kusoma bajeti hiyo leo Alhamisi, Juni 13, 2024 bungeni jijini Dodoma kuanzia saa 10:04 hadi 12:11 jioni.
Mbali na Dk Mwigulu kulitaja jina la Samia Suluhu Hassan wakati akiwasilisha bajeti hiyo yenye kurasa 173, pia ametaja jina la ‘Mama’ mara 15 wakati akinogesha hotuba yake mathalani amesema: “Ni dhahiri Mama hasemi tu, bali anatekeleza!”
Pia, Dk Mwigulu akielezea mafanikio makubwa ya awamu ya sita amesema: “Hii inadhihirisha kuwa Mama anawapenda sana Watanzania, hivyo basi na sisi Watanzania tusimame na Mama.”
Zaidi soma: Waziri Mwigulu awasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025