Pamoja na kuwa mkongwe chamani na Serikalini, lakini nami ni mjuzi na msomi wa sheria. Nilimaliza sheria miaka ya themanini na kuifanyia kazi hadi miaka ya mwishoni mwa tisini. Najua ninachokiandika hapa. Nina hakika na nikiandikacho hapa.
Amini nawaambia, Lengai Ole Sabaya 'ameshaachiwa' kisheria. Punde tu atakuwa mtu huru na atatamba na kubamba kuliko pamba. Hataachiwa kutokana na udhaifu wa ushahidi wa mashtaka. Hataachiwa kwakuwa utetezi wake una mashiko kama mwiko.
Sote tumeshuhudia jinsi kesi nzito na yenye mashiko ilivyojengwa na akina Kweka wa Jamhuri. Tumeshuhudia na kusikia jinsi utetezi wa Sabaya ulivyokuwa mwepesi kama karatasi. Lakini, Sabaya ataepuka kukutwa na hatia kama si Mahakama inayomsikiliza sasa basi ni ambayo watakata rufaa.
Sabaya ataachiwa kwa suala la kisheria. Baada ya kutokea mabishano ya kisheria kuhusu jina la Sabaya kukosewa, iliamriwa kuwa Sabaya asomewe maelezo yake upya. Akasomewa. Utetezi ukaendelea. Kuna kitu muhimu cha kisheria hakikufanyika. Mashahidi wa Jamhuri walipaswa kuitwa tena na kutoa ushahidi wao tena. Haikuwa hivyo.
Mashahidi walipaswa kuitwa upya kwakuwa Mshtakiwa 'amebadilishiwa' jina lake. Hawakuitwa na kesi inaendelea. Wao walitoa ushahidi dhidi ya Sayaba na si Sabaya. Kutoitwa tena kutatumika 'kumchomoa' Sabaya hapo au baada ya hapo. Ni suala la kisheria. Subirini mshuhudie jambo hili.
Askofu Gwajima hakamatiki?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma Mjini)