Jina la Sabaya lasimamisha kesi kwa muda

Jina la Sabaya lasimamisha kesi kwa muda

Kutokea Arusha Kesi Na 105 inayomuhusu Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Ya Hai

SERIKALI yakiri kuwa Aliyeshtakiwa Ni Lengai Ole SAYABA badala ya Lengai Ole SABAYA hivyo wameiomba Mahakama kubadili Hati ya mashtaka

Mawakili wa utetezi wamepinga kwa hoja kuwa Serikali ilishafunga zoezi la kutoa ushahidi kwa Kuleta mashahidi 11 na Mawakili Wasomi 4 waliothibitisha hati ya mashtaka yenye jina la LENGAI OLE SAYABA

Wamedai huu ni muda wa mshtakiwa kujitetea baada ya kukutwa na Kesi ya kujibu

Habari Leo
Wanasheria ni wasanii na wanabishaji sana

Imagine all these days wanapiga show ya yondo sister kwenye misa ya kwanza

mbaafff
 
Unachoelezea ni kweli kabisa. Hata hii habari kuna sehemu ukisoma unashindwa kupata mtiririko mzuri. Habari za mahakama zinapaswa kuandikwa vizuri na kwa usahihi mkubwa
Ila Tanzania kwa kukosa umakini tuko kwenye kiwango kingine. Hawa watu dizaini hii ndiyo huwa hata sehemu kama JF hawajui kuandika baadhi ya maneno na ukiwasahihisha wanatukana
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yaridhia ombi la kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ya kesi ya unyang`anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake 2 baada ya kubaini kulikua na makosa ya uchapishaji wa jina la tatu la mshatakiwa wa kwanza lililokua likisomeka kama 'Sayaba' badala ya Sabaya.

Zaidi endelea kufuatilia taarifa zetu Itv
 
Hayo mabishano hayana maana.

Kama kuna tatizo la SAYABA kwamba siyo Lengai Sabaya aliyepo mahakamani; basi ilikuwa ni nafasi ya Wakili wa Utetezi kuiambia Mahakama kwenye "submission" kwenye "Prima facies Case" (A Case to Answer submission) ili aishaiwishi Mahakama kwamba aliyeshtakiwa kwenye Hati ya Mashtaka siyo Mteja wake aliyopo mahakamani.

Hivyo angeomba Mahakama itoe uamuzi kwamba Lengai Ole Sabaya hana kesi ya kujibu, bali Jamhuri imtafute huyo SAYABA aletwe mahakamani hapo.

Hatua hiyo imepita, na Mahakama imemkuta Sabaya anayo kesi ya kujibu. Maana yake ni kwamba makosa ya jina hilo ni makosa madogo sana ambayo Mahakama ikayafumbia macho kwa kukubaliana kwamba Sayaba aliyeandikwa kwenye Hati ndiye huyu aliyepo mahakamani akijitambulisha kuwa ni Sabaya.
Safi kabsa maelezo yako.
 
Hata mfanyeje..Sabaya kashakiri makosa na mahakama imemkuta na hatia
Alifanya ujinga wakati wa kujitetea.kashakiri kafanya yote ila aliona utetezi ni kutumwa.alijikaanga
We kibaka kakamatwa huko kajeruhi kapelekwa mahakamani,ushahidi mahakamani ikamkuta na hatia.anaambiwa ajitetee anaanza ooh ni kweli nilikaba na kujeruhi ila nilitumwa na mzee A,waulizeni B na C wanajua..
Hiko ni nini?
Fuatilia utetezi wake, Hajakiri kutumwa kufanya uhalifu.

Amekiri kuwa na shughuli za kiusalama alizotumwa na mamlaka ya juu ya serikali nje ya eneo lake la kazi na ndo maana watuhumiwa aliwapeleka polisi pia akasema kuna shughuli nyingine za kukamata mitambo ya fedha feki alishawahi kutumwa ambazo makamu wa sasa anafahamu.

Alikakataa tuhuma za ujambazi uliohusishwa na shughuli hizo za kiusalama za serikali.

Haya ya kukiri kufanya uhalifu na kusingizia alitumwa naona ni ya mtandaoni. Hata hivyo Still bado ana wakati mgumu sana mtu huyu.
 
ila wanaJF kama vitu hamvijui ni bora kupita tuu haina shida, sasa hakimu kashasema wana kesi ya kujibu wewe unategemea nini?

Hapo sasa ndiyo mtuhumiwa anaanza kusema ana watoto 10 wake saba wanaomtegemea anasomesha ndugu, anaumwa ukimwi ili apunguziwe miaka, lakini dogo amekalia bomu akisimama linamlipukia.
 
Fuatilia utetezi wake, Hajakiri kutumwa kufanya uhalifu.

Amekiri kuwa na shughuli za kiusalama alizotumwa na mamlaka ya juu ya serikali na ndo maana watuhumiwa aliwapeleka polisi pia akasema kuna shughuli nyingine za kukamata mitambo ya fedha feki alishawahi kutumwa ambazo makamu wa sasa anafahamu.

Alikakataa tuhuma za ujambazi uliohusishwa na shughuli hizo za serikali.

Haya ya kukiri kufanya uhalifu na kusingizia alitumwa naona ni ya mtandaoni. Hata hivyo Still bado ana wakati mgumu sana mtu huyu.
Refer kesi ya zombe, wale wauwaji walisema pia walitumwa na boss wao. zombe sasa hivi anajipigia chimpumu kilaina na kubeba wamama wauza.
 
Taifa la kipumbavu na tumekubali kukumbatia ujinga. Matokeo yake hata ujinga tunaona ndiyo akili zenyewe hizo.
 
ila wanaJF kama vitu hamvijui ni bora kupita tuu haina shida, sasa hakimu kashasema wana kesi ya kujibu wewe unategemea nini?

Hapo sasa ndiyo mtuhumiwa anaanza kusema ana watoto 10 wake saba wanaomtegemea anasomesha ndugu, anaumwa ukimwi ili apunguziwe miaka, lakini dogo amekalia bomu akisimama linamlipukia.
Ata Kenyata alikuwa na kesi ya kujibu kule ICC lakini mwisho wa siku uyooo anakula bata hapo Kenya
 
Hata mfanyeje..Sabaya kashakiri makosa na mahakama imemkuta na hatia
Alifanya ujinga wakati wa kujitetea.kashakiri kafanya yote ila aliona utetezi ni kutumwa.alijikaanga
We kibaka kakamatwa huko kajeruhi kapelekwa mahakamani,ushahidi mahakamani ikamkuta na hatia.anaambiwa ajitetee anaanza ooh ni kweli nilikaba na kujeruhi ila nilitumwa na mzee A,waulizeni B na C wanajua..
Hiko ni nini?
Sheria ulisomea chuo gani mkuu.
 
Hayo mabishano hayana maana.

Kama kuna tatizo la SAYABA kwamba siyo Lengai Sabaya aliyepo mahakamani; basi ilikuwa ni nafasi ya Wakili wa Utetezi kuiambia Mahakama kwenye "submission" kwenye "Prima facies Case" (A Case to Answer submission) ili aishaiwishi Mahakama kwamba aliyeshtakiwa kwenye Hati ya Mashtaka siyo Mteja wake aliyopo mahakamani.

Hivyo angeomba Mahakama itoe uamuzi kwamba Lengai Ole Sabaya hana kesi ya kujibu, bali Jamhuri imtafute huyo SAYABA aletwe mahakamani hapo.

Hatua hiyo imepita, na Mahakama imemkuta Sabaya anayo kesi ya kujibu. Maana yake ni kwamba makosa ya jina hilo ni makosa madogo sana ambayo Mahakama ikayafumbia macho kwa kukubaliana kwamba Sayaba aliyeandikwa kwenye Hati ndiye huyu aliyepo mahakamani akijitambulisha kuwa ni Sabaya.

Sasa kama yeye sio sayaba all this time yeye Sabaya kwanini alikuwa akijibu maswali??
Mimi sijui am confused [emoji52]
 
Back
Top Bottom