Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

mzee kasome vizuri historia ya wangoni mimi ni mngoni najua in and out ya kabila langu sijui abdala sijui raufu hatulifahamu hilo
acha upotoshaji
 
HATA KAMA UTAINGIZWA UDINI CHA MSINGI UKWELI UFAHAMIKE ILI KUWEKA SAWA HISTORIA.MIMI PIA NI MGONI NA BABU YAKE NA BABA ALIKUWA NA JINA LA KIISLAM JAPO SIJUI ALILITOA WAPI.
 
HATA KAMA UTAINGIZWA UDINI CHA MSINGI UKWELI UFAHAMIKE ILI KUWEKA SAWA HISTORIA.MIMI PIA NI MGONI NA BABU YAKE NA BABA ALIKUWA NA JINA LA KIISLAM JAPO SIJUI ALILITOA WAPI.
ukweli upi mkuu hao machifu baada ya kunyongwa na kuzikwa walindikwa majina yao ya asili sasa huyu mzee anavyodai Chifu songea haitwi songea mbano bali abduli nani
hao machifu walihojiwa kabla ya kunyongwa na majima yalioandikwa vibaoni ni yale yale waliotumia hawa machifu enzi ya utawala wao na hadi vita ya maji maji
 

Sasa kama ukimuuliza hilo swali akafafanua kuwa waliyapataje hayo majina itapendeza kwa sababu ukweli ndio tunaoutaka.Japokuwa walikuwa na majina ya kiafrika lakini kupewa majina ya kiarabu ni sehemu ya historia.Sasa si vibaya tukijua mapito yao yote hadi pale walipoishia,mimi siongelei udini bali ninasapoti mtiririko mzima wa historia hasa kama kuna ukweli ndani yake.
 
Bagamoyo,
Mohamed Said Salum Abdallah Muyukwa Samitungo...

Itapendeza ukitumia majina yako yote ili watu wako wote wajivunie kuona ukijitambulisha kwa Watanzania na walimwengu kama Mohamed Said Salum Abdallah Muyukwa Samitungo.

Na baada ya hapo kama mwanahistoria nguli Mohamed Said Muyukwa Samitungo, kwa pamoja tuwashawishi na wengine kuiga mfano wa kujivunia asili yao na mengineyo yaendayo na utambulisho walioishi nao kitamaduni, kimila na kiimani ili kutunza historia kamilifu.
 

Bagamoyo ni jina lako au utokako?
 
aende maktaba ya mkoa pale songea kila kitu kipo pale atakuna na mengine yatamfunga mdomo
maana ameandika haya kama anaijua historia ya wangoni
kuna mahali nilimuuliza swali je hawa wazee walikuwa waislamu before/after mfecane war hajanijibu
 
Bagamoyo,
Wala hilo halina shida kwangu hayo hapo ni majina yangu lakini kwa
utaratibu huwa tunaandika majina matatu.

Ikiwa nitatakiwa kuandika zaidi ya matatu hayo yatatokeza.

Wanangu wote wanayajua majina haya na historia ya wenye majina
hayo - Mohamed Said Salum Abdallah Muyukwa Samitungo Mwekapopo.

Unaweza kusoma historia ya babu yangu Salum Abdallah hapo chini:
Mohamed Said: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Mohamed Said: SIKU BABU YANGU SALUM ABDALLAH ALIPOMKABILI FREDERICK MCHAURU KATIKA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TANGANYIKA RAILWAYS TABORA 1947
 
Ktk hili nakubaliana nawewe ila panaponishangaza nyumba nyingi zawenyeji wairinga mjini zile kongwe nizawaislam,nisaidie hapo we mnyalu
 
aende maktaba ya mkoa pale songea kila kitu kipo pale atakuna na mengine yatamfunga mdomo
maana ameandika haya kama anaijua historia ya wangoni
kuna mahali nilimuuliza swali je hawa wazee walikuwa waislamu before/after mfecane war hajanijibu
Mack...
Nimekujibu lakini ulitegemea jibu unalolitaka wewe na hapo ndipo kuna tatizo.

Nakuwekea hapo chini hayo ya Songea uyasome na mimi nategemea utaniwekea
hayo yako ya kunifunga mdomo:
Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
 

Ndivyo inavyotakiwa kuwa, majina siyo kitu kidogo huwezi juu huko siku za usoni vijana wakataka kujua asili yao ni wapi mbali ya majina yetu ya kuasili toka mabara mengine.

Kuna rafiki yangu maruhani kichwani mwake yalidai akatambike ktk sehemu aliyolazwa babu wa babu yake na kilichomnusuru ni wazee wake kama wewe pia walihifadhi historia yao na tukaweza kuyafikia makaburi.

Na sasa jamaa yangu baada ya kujigaragaza ktk makaburi ya wahenga yupo fresh amerudia hali yake ya kawaida.

Mimi kama kijana baada ya kuyaona yaliyomfikia kijana mwenzangu nikiona watu wana majina ya asili ya kigeni bila umatumbi ndani yake wananikumbusha tafarani ya jamaa yangu. Tudumishe historia kamilifu.
 
Mack...

Hii ndiyo hatari ya kujadili jambo usilolijua.

Hebu soma hapo chini:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007.

Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo.

Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam.

Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam.

Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.''
 
Mkuu nitajie mpigania uhuru mmoja tu ktk kila mkowa wa tz bala.naukitaja nakununulia kinywaji
 
Unalazimishia udini, hao wazee hata madini yenu walikuwa hawayajui, kama huyo mzee kwa ndumba nasikia alikuwa balaa, au uisilamu na ndumba zimo.
Du! Kwanini sasa makabuli yakawa yakiislam?[emoji12] [emoji13] [emoji14]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…