Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Mzee humjui huyo, na usomi wake wote anazungumza jina la Kiislam, mwambie hilo ni jina la Kiarabu

Pengo alikuambia utoe pesa za mchango wa mafuta ya mwenge . Jee umeshatoa ???
 
Sasa Mzee wangu Saidi, huyo Mkwawa au Songea hayo majina ya kiarabu walipewa kabla waarabu hawajaja au baada ya waarabu kuja???
Kama ilikua baada ya waarabu kuja ni wazi kua walikua na majina yao ya asili ambayo ndio hayo tunayoyaona na kama walipewa kabla hapa lazima tuhoji wao majina ya kiarabu waliyapata wapi angalau hapo tunaweza kuongea kiundani.
 
Ya wapi matusi kwenye matamshi yangu?

Waarabu hawakuwa wakoloni?

Kila kitabu ni msahafu?

Wajukuu wa Kleist Sykes hawajui nasaba yao hadi waambiwe na wewe?
Mwana,
Ikiwa huoni matusi katika kauli zako hapana neno.
Ili tuwe na mjadala mzuri itakuwa vyema kama tutajikita katika yale tunayojadili.

Mathalan umetumia lugha kali kwangu kwa kuniita mdini sina haja ya kuweka
maneno yako hapa.

Mimi nikakuuliza kama umemsoma Sivalon (1992).

Nimekuwekea jalada la kitabu ukifahamu na maneno aliyosema mle ndani katika
moja ya kurasa.

Naamini kabisa maneno yale yamekushtusha sana.
Ukija na ''Waarabu,'' na ''misahafu,'' haya siyo tunayojadili hapa.

Wala hatujadili nasaba.
Hapa tunajadili kwa nini walitangulia kuandika historia hizi wamezitia mikono?
 
Sasa Mzee wangu Saidi, huyo Mkwawa au Songea hayo majina ya kiarabu walipewa kabla waarabu hawajaja au baada ya waarabu kuja???
Kama ilikua baada ya waarabu kuja ni wazi kua walikua na majina yao ya asili ambayo ndio hayo tunayoyaona na kama walipewa kabla hapa lazima tuhoji wao majina ya kiarabu waliyapata wapi angalau hapo tunaweza kuongea kiundani.
Culture,
Ushauri wangu kwako ni kuwa fanya utafiti lau kidogo kwa kusoma hicho
unachotaka kujadili.
 
Blaa blaa za historia bhana..ndio maana matoto yanapata zero kila kukicha..sasa hii inatusaidia nini
 
je majina yao halisi ya kiasili ya kiafrika yalibaki?
Fogoh2,
Majina ya majemadari wa Majimaji hayo hapo chini:
DSC02264.jpg

Baada ya kusoma hayo majina sasa soma hii makala ya Sheikh Ilunga:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudumu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.''
 
MM
Umenipa changamoto kiasi. Katika kupitia vitabu vya historia hasa " Oral Histories of Tanzania" ambayo imeandika historia ya Majimaji from "First Hand" lakini sijawai ona kuhusu suala la uislam wala ukristo kwa wapiganaji wake, wala motisha ya kupigana haijabainishwa kuhusiana na imani yoyote iliyotoka nje ya mipka ya Tanganyika. Hii ni kwa historia hata ya Mkwawa. Sidhani kama watafiti tena kutoka mbali (siyo) mmoja wanaweza kuplan kupotosha historia kama hiyo. Ndiyo maana nasema umenipa changamoto. Either side of you, researchers mna hidden agenda.
James,
Soma hayo hapo chini kisha nisikilize ukimaliza nipe fikra zako:
Mwandishi katika video hii anaanza kuzungumza katika dakika ya 40:40

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955:

Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018
 
Fogoh2,
Majina ya majemadari wa Majimaji hayo hapo chini:
DSC02264.jpg

Baada ya kusoma hayo majina sasa soma hii makala ya Sheikh Ilunga:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.''
Sheikh Ilunga angemuuliza muumini yeyote wa kikatoliki angepata majibu sahihi.
Wakatoliki huamini kuwa jambo bora kuliko yote la kumfanyia mtu aliyeko katika hatari ya kufa ni kumwitia padri ampatie sakramenti za mwisho, na kama mtu huyo hakuwahi kubatizwa, ni kumbatiza ili ajipatie uhakika wa uzima wa milele aendako.
Kwa hiyo si kweli kuwa padri huyo aliwahadaa hao mateka kuwa eti wakikubali kubatizwa wataachiwa huru. Ni kwamba hukumu ya kuwanyonga watu hao ilishapitishwa na watu ambao padri huyo hakuwa na mamlaka yoyote juu yao. Yeye alichoitiwa ni kuwasalisha sala ya mwisho, na kwa waliokubali kubatizwa aliwabatiza, akawaacha wasubirie hatima yao. Na hii hufanyika sehemu nyingi duniani hadi leo, hata wale wafungwa waliohukumiwa kifo hupewa nafasi ya kutubu na kupata mwongozo wa viongozi wa dini ikiwemo ya uislamu. Kuna wafungwa wengi magerezani huko Marekani waliamua kusilimu wakiwa magerezani, hata bondia Mike Tyson alisilimu akiwa gerezani. Watu wanaobadilisha dini katika hali ya kufani, ima ni kutafuta faraja ama kutarajia miujiza ya kuokoka kutoka katika hatari hiyo au kujihakikishia hatima njema kwa jinsi walivyoshawishika na mahubiri, yote huwa ni maamuzi yao wenyewe wanapokuwa katika hali hiyo ya kukata tamaa.
Si halali hata kidogo kutengeneza tafsiri za kutunga, ni busara kutafiti upate ukweli ndipo uongee, hiyo ndiyo hekima.
 
Raph,
Ahsante kwa maelezo haya.
 
Lukubuzyo,
Sijui kwa nini umetumia neno, ''kulalamika.''

Kitu ambacho tumekifanya na ndicho kilikuwa na umuhimu mkubwa sana baada ya kujua
kuwa historia yetu ilikuwa imefutwa ni kuhakikisha kuwa historia ya Waislam inaandikwa
na kuhifadhiwa ili ibaki kuwa historia ya nchi yetu.

Ukiwa unataka historia ya BAKWATA fungua uzi tuchangie lakini hapa hoja iliyoko mezani
ni kwa nini wanahistoria waliitia mkono historia ya kweli ya Vita Vya Majimaji kwa kubadilisha
majina ya wapiganaji.

Unauliza hatua gani mimi nimechukua.
Hatua niliyochukua mimi ni kuandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nimeandika vitabu na paper na nimezungumza katika Vyuo Vikuu Afrika Ulaya, Marekani.

Kuna mengine umeandika kwa kejeli ni tabu kwangu kujibu kejeli na khasa ikiwa na hilo
jambo lenyewe halituhusu.

Katika sekta ya elimu Waislam wamepata vipingamizi vingi sana kutoka serikalini.
Nakupa ''chronology,'' fupi labda itaweza kukufikirisha:

1. 1929 African Association founded in Dar es Salaam
2. 1933 Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika founded
3. 1947 East African Muslim Welfare Society founded
4. 1940 Sheikh Hassan bin Amir relocates to Dar es Salaam from Zanzibar and sets up prominent Madrasas and Zawiyya in Tanganyika, Malawi, Rwanda, Burundi and Eastern Congo
5. 1950 Dr. Kyaruzi and Abdulwahid Sykes elected as TAA President and Secretary respectively
6. 1953 Julius Nyerere and Abdul Sykes elected TAA President and Vice President respectively
7. 1954 TANU founded in Dar es Salaam with Nyerere and John Rupia as President and Vice President respectively
8. 1962 First Muslim Congress
9. 1963 Second Muslim Congress
10. 1963 TANU Elders Council dissolved by TANU
11. 1964 EAMWS delegation led by Sheikh Hassan bin Amir pays visit to Muslim countries in Middle East. President Gamal Abdel Nasser of Egypt agrees to build a fully fledged university for Muslims in Tanganyika
12. 1968 Foundation Stone is laid for the EAMWS Muslim University
13. 1968 EAMWS is declared ‘’illegal society’’ and banned
14. 1968 BAKWATA founded by the government to replace EAMWS Muslim University Project is scrapped off.
15. 1970s Government refuse permission to allow Organisation of Islamic Conference (OIC) to build a Muslim University in Tanzania. OIC builds the university in Mbale, Uganda.
16. 1981 Government refuse to register four Muslim Schools as seminaries
17. 1982 Government refuse to register Masjid Quba Muslim School
mbona sasa unataka kutudanganya wewe ni mwanahistoria wakat kwa maandishi yako haya unaonekana wewe ni mwanaharakati unaelazimisha kuandikwa kwa historia mpya za kiislam humu nchini. umekuwa unajiona kwamba mambo unayopresent ni muhim kias kwamba unahudhuria kwenye makongamano na vyuo mbali mbali kutoa mihadhara jambo moja hujui ni kuwa wazungu hawapuuz kitu wanasikiliza kila kitu na kukaa kuchambua na ndio maana hata mashoga kwao wanawaruhusu madhali hawaingilia na kila mtu mambo yake.
 
Du! We inawezekana ikawa kilaza mwenzangu,yaani waarabu wamemkuta akiwa kijana kivipi ungefafanuwa zaidi maana historia hadi ya shule za msingi inasema waarabu waliingia ktk karine ya tisa

Inawezekana wewe ndio Kilaza, Waarabu ndio waliingia mapema sana, lakini hawakuzunguka sehemu kubwa ya Tanganyika, walikaa karne nyingi Pwani kabla ya kuanza kuingia ndani tena kwenye specific routs, so inawezekana kabisa Waarabu walimkuta Mkwawa kijana, kwani waarabu walianza kuingia kwa wahehe wakati wa mkwawa
 
Sijaona ulipoandika Kiswahili cha kunishinda, sijaelewa ulichoandika,

HIKI SI KICHINA au damu ya yesu imekuzidi ??

Pengo alikuambia utoe pesa za mchango wa mafuta ya mwenge ?? . Jee umeshatoa ???
 
mbona sasa unataka kutudanganya wewe ni mwanahistoria wakat kwa maandishi yako haya unaonekana wewe ni mwanaharakati unaelazimisha kuandikwa kwa historia mpya za kiislam humu nchini. umekuwa unajiona kwamba mambo unayopresent ni muhim kias kwamba unahudhuria kwenye makongamano na vyuo mbali mbali kutoa mihadhara jambo moja hujui ni kuwa wazungu hawapuuz kitu wanasikiliza kila kitu na kukaa kuchambua na ndio maana hata mashoga kwao wanawaruhusu madhali hawaingilia na kila mtu mambo yake.

Kumbe wazungu huruhusu hata mashoga ?? Hivi kanisa lako linawaruhusu mashoga kuwa Wachungaji ??
 
Luggy,
Inaelekea hujui historia ya Waislam wa Tanzania.

Ungekuwa unajua usingekuja na kauli hiyo.

Baada ya uhuru Waislam waliitisha Muslim Congress 1962 na 1963 na waliamua kujenga shule nchi nzima na Chuo Kikuu.

Nawaachie wengine wakueleze nini kilitokea.

Hivi kweli we Mzee huoni Tatizo lilipo?

1: Waarabu na tuseme Waislam wamekaa Tanganyika kwa zaidi ya Karne tano kwa nini hawakujenga shule Tanganyika nzima mpaka nyie wa baada ya uhuru?, Huoni tatizo lilipotokea?

2: Waarabu Waliwakuta machifu nchi nzima, lakini wameficha hiyo historia, na wewe wala ulalamiki kwa hilo, kwa sababu Waarabu waliwapa majina ya ya Kiarabu kwako roho kwatu kabisa, wapi historia ya Wanzanzibar iliyoandikwa na Waarabu?, Waarabu hawakuwakuta watu na machifu wao Zanzibar? wao walipoingia hawakuwakuta watu waliojipanga kwenye utaratibu na uongozi unaoeleweka? Hiyo historia kwa sababu imechafuliwa na Mwarabu/Mwislam kwako haina shida
 
Back
Top Bottom