Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee humjui huyo, na usomi wake wote anazungumza jina la Kiislam, mwambie hilo ni jina la Kiarabu
Mwana,Ya wapi matusi kwenye matamshi yangu?
Waarabu hawakuwa wakoloni?
Kila kitabu ni msahafu?
Wajukuu wa Kleist Sykes hawajui nasaba yao hadi waambiwe na wewe?
Culture,Sasa Mzee wangu Saidi, huyo Mkwawa au Songea hayo majina ya kiarabu walipewa kabla waarabu hawajaja au baada ya waarabu kuja???
Kama ilikua baada ya waarabu kuja ni wazi kua walikua na majina yao ya asili ambayo ndio hayo tunayoyaona na kama walipewa kabla hapa lazima tuhoji wao majina ya kiarabu waliyapata wapi angalau hapo tunaweza kuongea kiundani.
Fogoh2,je majina yao halisi ya kiasili ya kiafrika yalibaki?
James,MM
Umenipa changamoto kiasi. Katika kupitia vitabu vya historia hasa " Oral Histories of Tanzania" ambayo imeandika historia ya Majimaji from "First Hand" lakini sijawai ona kuhusu suala la uislam wala ukristo kwa wapiganaji wake, wala motisha ya kupigana haijabainishwa kuhusiana na imani yoyote iliyotoka nje ya mipka ya Tanganyika. Hii ni kwa historia hata ya Mkwawa. Sidhani kama watafiti tena kutoka mbali (siyo) mmoja wanaweza kuplan kupotosha historia kama hiyo. Ndiyo maana nasema umenipa changamoto. Either side of you, researchers mna hidden agenda.
Sheikh Ilunga angemuuliza muumini yeyote wa kikatoliki angepata majibu sahihi.Fogoh2,
Majina ya majemadari wa Majimaji hayo hapo chini:
![]()
Baada ya kusoma hayo majina sasa soma hii makala ya Sheikh Ilunga:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.
Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.
Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.
Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.''
Raph,Sheikh Ilunga angemuuliza muumini yeyote wa kikatoliki angepata majibu sahihi.
Wakatoliki huamini kuwa jambo bora kuliko yote la kumfanyia mtu aliyeko katika hatari ya kufa ni kumwitia padri ampatie sakramenti za mwisho, na kama mtu huyo hakuwahi kubatizwa, ni kumbatiza ili ajipatie uhakika wa uzima wa milele aendako.
Kwa hiyo si kweli kuwa padri huyo aliwahadaa hao mateka kuwa eti wakikubali kubatizwa wataachiwa huru. Ni kwamba hukumu ya kuwanyonga watu hao ilishapitishwa na watu ambao padri huyo hakuwa na mamlaka yoyote juu yao. Yeye alichoitiwa ni kuwasalisha sala ya mwisho, na kwa waliokubali kubatizwa aliwabatiza, akawaacha wasubirie hatima yao. Na hii hufanyika sehemu nyingi duniani hadi leo, hata wale wafungwa waliohukumiwa kifo hupewa nafasi ya kutubu na kupata mwongozo wa viongozi wa dini ikiwemo ya uislamu. Kuna wafungwa wengi magerezani huko Marekani waliamua kusilimu wakiwa magerezani, hata bondia Mike Tyson alisilimu akiwa gerezani. Watu wanaobadilisha dini katika hali ya kufani, ima ni kutafuta faraja ama kutarajia miujiza ya kuokoka kutoka katika hatari hiyo au kujihakikishia hatima njema kwa jinsi walivyoshawishika na mahubiri, yote huwa ni maamuzi yao wenyewe wanapokuwa katika hali hiyo ya kukata tamaa.
Si halali hata kidogo kutengeneza tafsiri za kutunga, ni busara kutafiti upate ukweli ndipo uongee, hiyo ndiyo hekima.
Barikiwa Sheikh wangu.Raph,
Ahsante kwa maelezo haya.
mbona sasa unataka kutudanganya wewe ni mwanahistoria wakat kwa maandishi yako haya unaonekana wewe ni mwanaharakati unaelazimisha kuandikwa kwa historia mpya za kiislam humu nchini. umekuwa unajiona kwamba mambo unayopresent ni muhim kias kwamba unahudhuria kwenye makongamano na vyuo mbali mbali kutoa mihadhara jambo moja hujui ni kuwa wazungu hawapuuz kitu wanasikiliza kila kitu na kukaa kuchambua na ndio maana hata mashoga kwao wanawaruhusu madhali hawaingilia na kila mtu mambo yake.Lukubuzyo,
Sijui kwa nini umetumia neno, ''kulalamika.''
Kitu ambacho tumekifanya na ndicho kilikuwa na umuhimu mkubwa sana baada ya kujua
kuwa historia yetu ilikuwa imefutwa ni kuhakikisha kuwa historia ya Waislam inaandikwa
na kuhifadhiwa ili ibaki kuwa historia ya nchi yetu.
Ukiwa unataka historia ya BAKWATA fungua uzi tuchangie lakini hapa hoja iliyoko mezani
ni kwa nini wanahistoria waliitia mkono historia ya kweli ya Vita Vya Majimaji kwa kubadilisha
majina ya wapiganaji.
Unauliza hatua gani mimi nimechukua.
Hatua niliyochukua mimi ni kuandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nimeandika vitabu na paper na nimezungumza katika Vyuo Vikuu Afrika Ulaya, Marekani.
Kuna mengine umeandika kwa kejeli ni tabu kwangu kujibu kejeli na khasa ikiwa na hilo
jambo lenyewe halituhusu.
Katika sekta ya elimu Waislam wamepata vipingamizi vingi sana kutoka serikalini.
Nakupa ''chronology,'' fupi labda itaweza kukufikirisha:
1. 1929 African Association founded in Dar es Salaam
2. 1933 Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika founded
3. 1947 East African Muslim Welfare Society founded
4. 1940 Sheikh Hassan bin Amir relocates to Dar es Salaam from Zanzibar and sets up prominent Madrasas and Zawiyya in Tanganyika, Malawi, Rwanda, Burundi and Eastern Congo
5. 1950 Dr. Kyaruzi and Abdulwahid Sykes elected as TAA President and Secretary respectively
6. 1953 Julius Nyerere and Abdul Sykes elected TAA President and Vice President respectively
7. 1954 TANU founded in Dar es Salaam with Nyerere and John Rupia as President and Vice President respectively
8. 1962 First Muslim Congress
9. 1963 Second Muslim Congress
10. 1963 TANU Elders Council dissolved by TANU
11. 1964 EAMWS delegation led by Sheikh Hassan bin Amir pays visit to Muslim countries in Middle East. President Gamal Abdel Nasser of Egypt agrees to build a fully fledged university for Muslims in Tanganyika
12. 1968 Foundation Stone is laid for the EAMWS Muslim University
13. 1968 EAMWS is declared ‘’illegal society’’ and banned
14. 1968 BAKWATA founded by the government to replace EAMWS Muslim University Project is scrapped off.
15. 1970s Government refuse permission to allow Organisation of Islamic Conference (OIC) to build a Muslim University in Tanzania. OIC builds the university in Mbale, Uganda.
16. 1981 Government refuse to register four Muslim Schools as seminaries
17. 1982 Government refuse to register Masjid Quba Muslim School
SijakuelewaPengo alikuambia utoe pesa za mchango wa mafuta ya mwenge . Jee umeshatoa ???
Du! We inawezekana ikawa kilaza mwenzangu,yaani waarabu wamemkuta akiwa kijana kivipi ungefafanuwa zaidi maana historia hadi ya shule za msingi inasema waarabu waliingia ktk karine ya tisa
Kiswahili kinakupiga chenga ??
Sijaona ulipoandika Kiswahili cha kunishinda, sijaelewa ulichoandika,
mbona sasa unataka kutudanganya wewe ni mwanahistoria wakat kwa maandishi yako haya unaonekana wewe ni mwanaharakati unaelazimisha kuandikwa kwa historia mpya za kiislam humu nchini. umekuwa unajiona kwamba mambo unayopresent ni muhim kias kwamba unahudhuria kwenye makongamano na vyuo mbali mbali kutoa mihadhara jambo moja hujui ni kuwa wazungu hawapuuz kitu wanasikiliza kila kitu na kukaa kuchambua na ndio maana hata mashoga kwao wanawaruhusu madhali hawaingilia na kila mtu mambo yake.
Luggy,
Inaelekea hujui historia ya Waislam wa Tanzania.
Ungekuwa unajua usingekuja na kauli hiyo.
Baada ya uhuru Waislam waliitisha Muslim Congress 1962 na 1963 na waliamua kujenga shule nchi nzima na Chuo Kikuu.
Nawaachie wengine wakueleze nini kilitokea.
AminBarikiwa Sheikh wangu.