Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

mbona sasa unataka kutudanganya wewe ni mwanahistoria wakat kwa maandishi yako haya unaonekana wewe ni mwanaharakati unaelazimisha kuandikwa kwa historia mpya za kiislam humu nchini. umekuwa unajiona kwamba mambo unayopresent ni muhim kias kwamba unahudhuria kwenye makongamano na vyuo mbali mbali kutoa mihadhara jambo moja hujui ni kuwa wazungu hawapuuz kitu wanasikiliza kila kitu na kukaa kuchambua na ndio maana hata mashoga kwao wanawaruhusu madhali hawaingilia na kila mtu mambo yake.
Kitali,
Niseme uongo nimdanganye nani katika ulimwengu huu uliojaa wasomi?

Mimi sijalazimisha kitu ila kile nikisemacho huwa ni elimu mpya inayoongeza maarifa.

Hakika kitabu changu cha Abdul Sykes kimebadili historia nzima ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hakika Wazungu hawapuuzi kitu lakini si kuwa watamwalika kila mtu kutoa mhadhara Northwestern University Evanston, Chicago wamsikilize.
 
Hivi kweli we Mzee huoni Tatizo lilipo?

1: Waarabu na tuseme Waislam wamekaa Tanganyika kwa zaidi ya Karne tano kwa nini hawakujenga shule Tanganyika nzima mpaka nyie wa baada ya uhuru?, Huoni tatizo lilipotokea?

2: Waarabu Waliwakuta machifu nchi nzima, lakini wameficha hiyo historia, na wewe wala ulalamiki kwa hilo, kwa sababu Waarabu waliwapa majina ya ya Kiarabu kKitukowako roho kwatu kabisa, wapi historia ya Wanzanzibar iliyoandikwa na Waarabu?, Waarabu hawakuwakuta watu na machifu wao Zanzibar? wao walipoingia hawakuwakuta watu waliojipanga kwenye utaratibu na uongozi unaoeleweka? Hiyo historia kwa sababu imechafuliwa na Mwarabu/Mwislam kwako haina shida
Kituko,
Nafahamu tatizo lako la shule.

Kwako wewe shule lazima ziwepo kuta nne na kibao kiwekwe nje kuwa hii
ni shule.

Kwa Waislam shule ni madras na Uislam mzima umesimama katika elimu bila
elimu hakuna Uislam.

Shule ni neno la Kijerumani ''schule'' na Wajerumani walipofika pwani ya Afrika
Mashariki walikuwakuta Waislam tayari wanazo zile 3Rs, yaani Reading, Writing
and Arithmetic.

Waalimu wa kwanza wa shule za Kijerumani na watendaji serikalini walikuwa
Waislam na herufi zilizokuwa zikitumika zilikuwa za Kiarabu.

Johann Krapf alipofika kwa Chief Kimweri Vuga alimkuta anajua kusoma, kuandika
na kupiga hesabu yeye na watoto wake wote.

Hii ilimshangaza Krapf na pia ikamjaza hasad katika moyo wake kuwa kawakuta
Waislam wamestaarabika si kama alivyokuwa anafikiri kuwa kaja kwa watu washenzi.

Waingereza walipoichukua Tanganyika kama watawala kitu cha kwanza wao kufanya
ilikuwa kupiga marufuku matumizi herufi za Kiarabu.

Watu ambao kwa karne na karne walikuwa wameelimika wakawa kwa amri ile ghafla
wamekuwa watu wasiojua kusoma wala kuandika.

Nadhani umeelewa hili la ujenzi wa shule.

Lakini wamishionari wao wanataka watu waaamini kuwa ni wao ndiyo walileta elimu
huku kwetu ilhali watu wakijua kuandika na kusoma kabla yao.

Nataka nikupe mfano mmoja.

Haidar Mwinyimvua (1905 - 1987) ni katika watu wa mwanzo katika TANU na walikuwa
na tawi lenye nguvu sana Kisutu kisha likahamia Kariakoo Mtaa wa Mvita.

Haidar Mwinyimvua yeye alikuwa hajui kuandika kwa hizi herufi za Kirumi siku zote akiandika kwa herufi za Kiarabu.

Baadae sana ndipo alipokuja kujifunza kuandika na kusoma kwa hati za Kirumi.

Nina mada hii hapa nimeeleza haya yote kwa kirefu:

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika
(Tanzania Mainland) 1800 – 2000’
(Paper presented at International Symposium on Islamic
Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research
Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in
Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Nashindwa kusema lolote kuhusu hayo mengine na nisamehe kwa kusema haya ni kuwa wewe
una mengi hujui na ndiyo maana unakuja na hizi hoja.

Soma kwanza historia ndipo urejee hapa barzani kufanya mjadala.

CHIEF%2BKIMWERI%2BWA%2BVUGA.jpg

Mtoto wa Chief Kimweri
 
Mzee wangu Mohammed SAID wakati mwengine ni vizuri kuandika jambo bila kuweka mrengo wowote unaouamini wewe,hii mada ingelikuwa nzuri sana kama usingeingiza hiki kipengele kwamba hawa machifu walikuwa waislam au walikuwa kinanani!ktk ukoo wangu ninao baba zangu,babu zangu na wadogo zangu Abdallah,Salim pia wadogo zangu Halima,Iddi na Shaban ila wote hawa ni wakristo.my point is,kuitwa kwao majina hayo hakuwafanyi wao kuwa waislam na naamini hata wewe kulithibitisha hilo huwezi may be ilikuwa trick ya wao kupata msaada kutoka kwa hao waarabu ndio maana wakajibadilishia hayo majina ili kuendana nao ninani anayejua?hao machifu ndiyo waliokuwa wanaongoza watu kuabudu miti huwezi kututhibitishia hapa kwamba Mkwawa kuna siku amehudhuria madrassa kujifunza dini za kuja,obviously huu ni uongo mkubwa sana!
 
Sir...
Hofu ya Uislam ndiyo iliyotufikisha hapa.
Chuo Cha Kivukoni wakati kinaandika historia ya TANU iliogopa kueleza historia ile kwa ukweli wake kwa kuogopa Uislam.

Wasomi wanahistoria bingwa kama Kimambo walipoandika historia ya TANU wamekwepa ukweli kwa kuogopa Uislam.

Kumbukumbu ya Majimaji historia yake imetiwa mkono kwa kuogopa Uislam.

Wewe nawe unaniambia ati nisiwataje Waislam.

Mbona sijasikia mkiseme wasitajwe Wamishionari?

Kila jamii itatambuliwa kwa kile walichofanya.

Hilo la Mkwawa fika katika makumbusho yake uone barua alizokuwa akiandika.
 
Conservative3,
Lililopo mezani si hilo unalozungumza.
Hapa ni tatizo la kuandika historia rasmi na kukwepa ukweli.
HONGERA MZEE
NAOMBA NIKUKUMBUSHE MAENEO MENGI WATU WALIPEWA JINA KWA AJILI YA KUMBUKUMBU INAWEZEKANA SULTAN ALITEMBELEA HAPO KWA AJILI YA MIKATABA YA KIBIASHARA NK
,KUNA HAJA YA KUFANYA TAFITI TENA ILA INAFAHAMIKA KWA WATU WENGI KUWA WARABU NA WAZUNGU WALIKUTA WAAFRIKA WANA DINI ZAO NA HATA BAADA YA KUWABATIZA NA KUWASILIMISHA ILA HAWAKUWA WAKRISTU WALA WAISLAM,YAANI MTU ANAITWA JUMA AU JOHN HAJUI MSIKITI WALA KANISA ILA ANATAMBIKA NA KUTEGEMEA RAMLI ZA WASAIDIZI WAKE. AU MTU ANARITHI JINA ,ILA SI DINI HIYO
SASA INAWEZA MWANDISHI ALIAMBIWA KUWA HUYU JAMAA ALIKUWA SULTAN HUO NI MTAZAMO WA MTOA HISTORIA NA MWANDISHI
PIA KWENYE GAZETI LENGO LA MWANDISHI NAHISI NI KUKUZA UNGONI NA SI USULTANI AU UCHIFU KWA MAANA INAJULIKANA ALIKUA KIONGOZI.
WAPO VIONGOZI WENGI WALIBATIZWA NA KUSILIMISHWA ILA HOJA ILIYOKO MEZANI KWA SIKU HUSIKA NI USHUJAA WA KIJADI
MFANO :AGUSTINO RAMADHANI,SI WAKATI WOTE MAGAZETI YANAANDIKA NI KASISI WA IMANI FULANI AU JENERALI MSTAAFU ,JAJI NK, HAIMAANISHI WANAPOSEMAA JAJI BILA KUTAJA MENGINE HAWATAMBUI VINGINE AU WANAFICHA UKWELI HAPANA ,LA MSINGI NI DHIMA YA TUKIO HUSIKA,INAWEZEKANA UCHIFU WA KIMILA UNA HADHI KUBWA KITANZANIA KWA SIKU YA MASHUJAA KULIKO USULTAN AU HADHI INGINE,
MFANO:CHIFU KIMWERI WA USAMBAA WENGI WANAPENDA AITWE ZUMBE AU KIONGOZI MKUU AU CHIFU KULIKO SULTAN,UKIENDA KITALA KUULIZA WANAKILI KUWA ALIKUWA NA UKARIBU NA WAFANYA BIASHARA WA KIARABU JAPO HAWATHIBITISHI ALIKUWA MUISLAM JAPO HAO WAZEE NI WAISLAMU,JAPO WARABU WALIMPA USULTAN NA WAJERUMANI WALIMPA LAO,HAIMAANISHI KWA KUITWA SULTANI YEYE BINAFSI NA FAMILIA AU UKOO WALIKUWA WAISLAM.AU HAKUWA MUISLAM AU WANAPOTOSHA HISTORIA LA HASHA LENGO KUU NI UONGOZI THABIT WA KIMILA NA WENGI WALIFUATA MILA KULIKO IMANI NA MAJINA YA KIMILA YALIJULIKANA NA WOTE KULIKO YALE YA KIIMANI.
NAFASI YA WAANDISHI NA WATAFITI:WENGI WALIJARIBU KUFANANISHA NA USULTAN AU AINA NYINGINE KUTOKANA NA MAVAZI AU MFUMO WA UTAWALA WAKE AMBAPO MWANDISHI AU MTAFITI,INAWEZEKANA HIZO NGUO HUYO CHIFU ALIPEWA ZAWADI AU KUIGA NK
HITIMISHO:TUNAOTAMBIKA TUNATAMBIKA KWA MAJINA YA KIMILA HATA KM TUMEBATIZWA AU KUSILIMISHWA SI YA KIGENI HIVYO BUSARA ILITUMIKA KUANDIKA MAJINA YA KIMILA KUKUZA JADI ILA KWA WALE WANOTAKA KUBOBEA KUANDIKA THESIS WANAWEZA KUTUMIA MAJINA YOTE
 
Conservative shida ni kuwa wengi wenu hamna ujuzi wa historia hivyo ni rahisi kudanganyika.

Sikiliza historia hii kisha jiulize iweje watu hawa ikawa wakafutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika:

Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018
Mwandishi katika video hii anaanza kuzungumza katika dakika ya 40:40
Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955.
 
Mimi maswali yangu ni haya

1. Katika uislamu kuna kitu kinaitwa shirki ... ukiangalia jina majimaji limetokana na shirki ya kuamini risasi ya mjerumani kugeuka maji je,kama hawa washiriki waliuamini uislamu zaidi kuliko njia zao za kiasili ilikuwaje wakahadaika na kuingia katika vita huku wakiamini watalindwa na shirki na sio Allah ???......
Na hili swali pia linatokana na hiyo barua ambayo umeionesha maana inaonekana kama hawa watu walikuwa ni waislamu wazuri

2. Kuna haja ama umuhimu gani wa kuiandika historia ya nchi yetu ikiegemea katika udini na si utaifa !!!!!!....
Je , huoni kama unataka kutengeneza diversity na sio unity ambayo kwa kiasi flani tunayo

Je,huoni hiyo ni mbegu ambayo haina tofauti kubwa na ile iliyopandikizwa rwanda na matokeo tunayajua

3. Wewe ni mfuasi wa historia ya Tanzania au ni mfuasi wa historia ya waislamu ndani ya Tanzania maana ni mara chache kuona unatoa historia isiyo na mlengo wa uislamu
 
Eyce,
Hilo swali la kwanza wanaoweza kulijibu ni wao wenyewe.

Umuhimu wa.kuandika historia hii kwa usahihi wake ni kuwa waliotangulia kuiandika hawakuwa wakweli.

Kubadilisha historia hakuwezi kuimarisha umoja halikadhalika kuisahihisha historia hakuvunji umoja.

Historia ya wazee wangu ina mvuto wa pekee na imependwa na wengi.
 

Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Kibao kimeandika jina lake kama ''Lwafu'' Nduna Mbano


Kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano

Kwa miaka mingi sana na hadi leo jina la Sultani wa Wangoni Abdulrauf Songea Mbano Jemedari wa Wangoni katika Vita ya Majimaji, jina lake la ‘’Abdulrauf’’ moja ya sifa za Allah ikiwa na maana ‘’Mwenye Huruma,’’ lilikuwa halifahamiki kwa wengi na wanahistoria kwa sababu zao hawakutaka kulisema lijulikane kama vile wengi hawajui kuwa Sultani Mkwawa jina lake ni ''Abdallah.''

Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''




Kaburi la Kleist Sykes

Tunaweza tukasema kuwa haya yote ni matatizo ya ukoloni. Lakini swali linakuja iweje hata baada ya ukoloni kutoweka ikabakia historia yetu hatuiweki sawa?

Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.

Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.

Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
  1. Mohamed Said: SULTAN ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
  2. Mohamed Said: KUTOKA JF: MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI - SULTAN SONGEA BIN RAUF NA SHEIKH SULTAN MATAKA BIN HAMIS MASSANINGA
  3. Mohamed Said: KUTOKA JF: UCHAKACHUAJI WA MAJINA YA KIISLAM KATIKA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI
  4. Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
Umejitahidi kuandika vizuri, Ila umesahau hakuwa Mwarabu! nashukuru waliondika majina yake halisi...kwa kifupi ata wareno wangeingia Tanganyika Leo hii pengine ata wewe ungeitwa Pereira n.k. Majina asili yametoweka/ yanatoweka sababu ya ukoloni..miaka si mingi dunia inavyoendelea utakutana na akina Cheng,Xi na Lee weusi..Haya si majina ya asili zetu!
 
Leo hii MTU akiitwa hadharani Masawe Ndesamburo watu wajifanya hawamwelewi bila akiwa na jina eti Abubakar Hassan au Josephat Michael wajifanya kumjua kesho si watakuja kina Morata Morales, Xi Cheng Chou, Nemanja Ludovic hahahahaha!
 
Leo hii MTU akiitwa hadharani Masawe Ndesamburo watu wajifanya hawamwelewi ila akiwa na jina eti Abubakar Hassan au Josephat Michael wajifanya kumjua wanamuona mjanja..kesho si watakuja kina Morata Morales, Xi Cheng Chou, Nemanja Ludovic hahahahaha! saikolojia na majina!
 
Hawa wote Milambo, Mkwawa nk ndio walikuwa mawakala wakuu wa biashara ya utumwa. Historia pia inaficha sana hili jambo ovu kabisa!
 
Hawa wote Milambo, Mkwawa nk ndio walikuwa mawakala wakuu wa biashara ya utumwa. Historia pia inaficha sana hili jambo ovu kabisa!
Ndugu zangu napenda kuwakumbusha nini mimi nimekiona katika historia ya Majimaji.

Nilichogundua ni kuwa kumekuwepo na juhudi za makusudi za kupotosha historia hiyo.

Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano lakini walioandika hustoria hiyo jina hili hawakulipenda wakaliondoa.

Hii mosi.

Pili ni kuwa wale majemadari wa Majimaji walionyongwa majina yao ya Kiislam yaliyokuwepo awali nayo yakafutwa.

Someni makala ya Sheikh Ilunga inayoeleza aliyoshuhudia majina hayo kwa macho yake mara ya kwanza alipofika Kumbukumbu ya Majimaji Mahenge, Songea na aliporudi akakuta yote yamebadilishwa.

Nini mukusudio ya haya yote?
 
Eyce,
Hilo swali la kwanza wanaoweza kulijibu ni wao wenyewe.

Umuhimu wa.kuandika historia hii kwa usahihi wake ni kuwa waliotangulia kuiandika hawakuwa wakweli.

Kubadilisha historia hakuwezi kuimarisha umoja halikadhalika kuisahihisha historia hakuvunji umoja.

Historia ya wazee wangu ina mvuto wa pekee na imependwa na wengi.
Kama hilo swali wanaweza kulijibu kwa maana ilihusu imani yao je, inakuwaje wewe uwasemee au uwatwishe imani kwa sababu ya majina ambayo sijaona pahala popote kama yalitumika kama utambulisho wao katika jamii zao ???.....

Wazungu waliuleta ukoloni lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa waarabu walikuja na utumwa ... wote walikuwa na lengo la unyonyaji wa waafrika na waliwatumia hata wenyeji katika hila zao

Wageni wote hao walikuwa na taratibu za kuwapa majina yenye asili yao ,wenyeji wote waliowakuta na pengine kuwapa elimu ambayo ilitumia maandishi ya lugha zao kama kiarabu, kireno au kiingereza lakini si kwamba sehemu zote waliweka pandikizi ya imani zao hususani katika sehemu ambazo zilikuwa kama transit tu ...

Nimeishi songea hivyo kwa kiasi fulani napaelewa... kulikuwa na biashara ya utumwa ambapo wangoni walikuwa wakiyauza makabila mengineyo hususani wayao na hata leo kuna utani baina ya wangoni na wayao kutokana historia hiyo ..
Je , huoni kuwa biashara hii pengine iliweza kuleta ustaarabu wa kiarabu kwa wangoni kama lugha ya kimaandishi na majina ili kurahisha shughuli hiyo pasipo kuihusisha dini ya kiislamu maana uarabu si uislamu !!!!.....

Kuna mji wa peramiho ambao upo songea ambao utaona ustaarabu wa kikatholiki na wala hutopaswa kuuliza kama kulitokea ukristo pale je, huko songea mbali na kuwa na majina hayo ,kuna ushahidi gani mwingine wa kudhihirika kuwako kwa uislamu kama ilivyo kwa mikoa ya pwani ama tabora .....
 
Kama hilo swali wanaweza kulijibu kwa maana ilihusu imani yao je, inakuwaje wewe uwasemee au uwatwishe imani kwa sababu ya majina ambayo sijaona pahala popote kama yalitumika kama utambulisho wao katika jamii zao ???.....

Wazungu waliuleta ukoloni lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa waarabu walikuja na utumwa ... wote walikuwa na lengo la unyonyaji wa waafrika na waliwatumia hata wenyeji katika hila zao

Wageni wote hao walikuwa na taratibu za kuwapa majina yenye asili yao ,wenyeji wote waliowakuta na pengine kuwapa elimu ambayo ilitumia maandishi ya lugha zao kama kiarabu, kireno au kiingereza lakini si kwamba sehemu zote waliweka pandikizi ya imani zao hususani katika sehemu ambazo zilikuwa kama transit tu ...

Nimeishi songea hivyo kwa kiasi fulani napaelewa... kulikuwa na biashara ya utumwa ambapo wangoni walikuwa wakiyauza makabila mengineyo hususani wayao na hata leo kuna utani baina ya wangoni na wayao kutokana historia hiyo ..
Je , huoni kuwa biashara hii pengine iliweza kuleta ustaarabu wa kiarabu kwa wangoni kama lugha ya kimaandishi na majina ili kurahisha shughuli hiyo pasipo kuihusisha dini ya kiislamu maana uarabu si uislamu !!!!.....

Kuna mji wa peramiho ambao upo songea ambao utaona ustaarabu wa kikatholiki na wala hutopaswa kuuliza kama kulitokea ukristo pale je, huko songea mbali na kuwa na majina hayo ,kuna ushahidi gani mwingine wa kudhihirika kuwako kwa uislamu kama ilivyo kwa mikoa ya pwani ama tabora .....
Eyce swali ninalouliza mimi ni kwa nini pamekuwa na juhudi za kufuta majina ya Kiislamu?

Ikiwa hujui sababu basi si lazima ujadili.
 
Back
Top Bottom