Hivi kweli we Mzee huoni Tatizo lilipo?
1: Waarabu na tuseme Waislam wamekaa Tanganyika kwa zaidi ya Karne tano kwa nini hawakujenga shule Tanganyika nzima mpaka nyie wa baada ya uhuru?, Huoni tatizo lilipotokea?
2: Waarabu Waliwakuta machifu nchi nzima, lakini wameficha hiyo historia, na wewe wala ulalamiki kwa hilo, kwa sababu Waarabu waliwapa majina ya ya Kiarabu kKitukowako roho kwatu kabisa, wapi historia ya Wanzanzibar iliyoandikwa na Waarabu?, Waarabu hawakuwakuta watu na machifu wao Zanzibar? wao walipoingia hawakuwakuta watu waliojipanga kwenye utaratibu na uongozi unaoeleweka? Hiyo historia kwa sababu imechafuliwa na Mwarabu/Mwislam kwako haina shida
Kituko,
Nafahamu tatizo lako la shule.
Kwako wewe shule lazima ziwepo kuta nne na kibao kiwekwe nje kuwa hii
ni shule.
Kwa Waislam shule ni madras na Uislam mzima umesimama katika elimu bila
elimu hakuna Uislam.
Shule ni neno la Kijerumani ''schule'' na Wajerumani walipofika pwani ya Afrika
Mashariki walikuwakuta Waislam tayari wanazo zile 3Rs, yaani Reading, Writing
and Arithmetic.
Waalimu wa kwanza wa shule za Kijerumani na watendaji serikalini walikuwa
Waislam na herufi zilizokuwa zikitumika zilikuwa za Kiarabu.
Johann Krapf alipofika kwa
Chief Kimweri Vuga alimkuta anajua kusoma, kuandika
na kupiga hesabu yeye na watoto wake wote.
Hii ilimshangaza
Krapf na pia ikamjaza hasad katika moyo wake kuwa kawakuta
Waislam wamestaarabika si kama alivyokuwa anafikiri kuwa kaja kwa watu washenzi.
Waingereza walipoichukua Tanganyika kama watawala kitu cha kwanza wao kufanya
ilikuwa kupiga marufuku matumizi herufi za Kiarabu.
Watu ambao kwa karne na karne walikuwa wameelimika wakawa kwa amri ile ghafla
wamekuwa watu wasiojua kusoma wala kuandika.
Nadhani umeelewa hili la ujenzi wa shule.
Lakini wamishionari wao wanataka watu waaamini kuwa ni wao ndiyo walileta elimu
huku kwetu ilhali watu wakijua kuandika na kusoma kabla yao.
Nataka nikupe mfano mmoja.
Haidar Mwinyimvua (1905 - 1987) ni katika watu wa mwanzo katika TANU na walikuwa
na tawi lenye nguvu sana Kisutu kisha likahamia Kariakoo Mtaa wa Mvita.
Haidar Mwinyimvua yeye alikuwa hajui kuandika kwa hizi herufi za Kirumi siku zote akiandika kwa herufi za Kiarabu.
Baadae sana ndipo alipokuja kujifunza kuandika na kusoma kwa hati za Kirumi.
Nina mada hii hapa nimeeleza haya yote kwa kirefu:
Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika
(Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic
Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research
Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in
Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
Nashindwa kusema lolote kuhusu hayo mengine na nisamehe kwa kusema haya ni kuwa wewe
una mengi hujui na ndiyo maana unakuja na hizi hoja.
Soma kwanza historia ndipo urejee hapa barzani kufanya mjadala.
Mtoto wa Chief Kimweri