Mkuu sio hivyo unavyofikia,historia ya maarufu walioipigania nchi lazima iwekwe wazi ili vizazi vijavyo wajue nini kimetokea wakati wa utawala wa kikoloni,..
Mtoto wangu wa miaka saba alikuwa anasoma nchi moja ya ulaya,siku moja katika maongezi ya simu akanambia "baba leo tumesoma historia ya zamani ya wafalme na vitu walivyofanya,mfano majenzi ya makanisa vita walivyopigana nk " ....yani alikusudia hiyo nchi anayosoma,sasa swali likaja akataka nimuelezee historia ya wafalme wetu Tanzania na mambo waliyofanya,....kwa ukweli nilishindwa,nilijaribu kumuelezzea kidogo kuhusu vita vya maji maji sio zaidi..
Hapa Tanzania historia nyingi za machifu hazipendwi kuongelewa au kufundishwa shuleni kwasababu za Kidini au Kikabila,watawala wanaona wakianza kufundisha watakuwa wanakuza baadhi ya makabila au watazikuza baadhi ya dini,...Lakini kwa kweli Tanzania ina historia nzuri sana ya machifu wake,...
Kule Marekani na hata nchi nyengine za ulaya wanaamini kuwa wafrika wamezaliwa kuwa watumwa,wafrika walikuwa ni watu wanaozagaa zagaa porini kama wanyama,...
Kama historia yetu hatujailezea sisi wenyewe nani ataielezea nani atajua kama na sisi tulikuwa na wafalme wenye nguvu walioweza kupigana na mataifa makubwa makubwa..