Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir


M Mbabe,

Tafadhali sana na mimi nakuomba kwa unyonge, umasikini, kokosa elimu
kwetu na fursa zote hebu nasi tusikize juu ya hii hali yetu.

Naamini nawe una uwezo wa kuelewa historia ya wazee wangu na nini
walifanya, na shida walizobeba kwa matumaini mema ya baadae.

Tuijue historia yetu itatusaidia.

Tafadhali sana ikiwa hujasoma kitabu changu soma na uwaone wazee
wangu.

Ukiwajua wazee wangu utanijua na mimi na ninaposimamia.

Kalamu yangu naamini siku zote inaandika ambayo yanastahili kusikizwa
na watu wakatafakari.

Nasikitika kuwa badala ya jibu kutolewa na wahusika.
Jibu unatoa wewe.

Mimi niko chini ya miguu yako.
Msitupuuze.

Tusikizeni kilio chetu.
 

Kaka inaonekana kuna mengi ambayo watu hawayajui hivyo nakuomba sana ukipata nafasi ebu tupe kiundani juu ya hii EAMWS maana itatusaidia kuelewa mambo mengi na juhudi binafsi za muslim kujiendeleza katka elimu.

Asante kaka .
 
nilimsoma kwenye raia mwema, huyo sheikh na ilivyoelezewa ni waislam wenzie walimtenga na kumgwaya na akanyong'onyea sana kwa mawazo na akabaki akiwa mpweke, BAKWATA ambalo ni baraza kuu walimuona hafai pia, hivyo harakati zake zote zilizimwa, lakini muda upo, Mzee Said bado una nafasi ukishirikiana na barubaru na wenzio msiwe wazee wa kutoa mada yemen na kwingineko, kaeni chini tafuteni wafadhili muanzishe vyuo vyenu, mimi tarehe 19th nimenunua kadi ya milioni moja kuchangia upanuzi wa chuo kikuu cha Tumaini, mgeni rasmi ni Mheshimiwa JK, so nawausia ndugu zangu mnaolilia usawa, usawa unaanza na kuchukua hatua thabiti za kusimamia mambo yenu kupitia resources zenu ............................ sasa sina hakika ni kwanini hivi vyuo hamkuvianzisha basi wakati wa Mwinyi, mpaka mkaja kunyang'anya chuo cha TANESCO Morogoro, mkapewa nyie, sijui tuanzishe mada huku kudai kile chuo kirudi ?? usawa upi mwautaka hata mahakama itayojadili mambo yenu nayo kodi yangu iwalipie thubuttttttuuuu !!!
 
Kaka inaonekana kuna mengi ambayo watu hawayajui hivyo nakuomba sana ukipata nafasi ebu tupe kiundani juu ya hii EAMWS maana itatusaidia kuelewa mambo mengi na juhudi binafsi za muslim kujiendeleza katka elimu.

Asante kaka .

muwache kupora vyuo kama cha TANESCO muanzishe vyenu EMWAS bado ina nafasi, pale mtaani kwetu kuna kijidaftari cha ujenzi wa msikiti, nikasema hebu na mie nichangie, maana kwakweli wanaswalisha vizuri na sina ugomvi kabisa na maendeleo kama hayo kuangalia kidaftari salalalaaaaa michango mnaandikisha shs 200 nikaona hapa nikiweka nyekundu itaishia mfukoni kwa ustaadhi, hebu jaribuni kufanya mambo yenu vizuri sio kututisha na majambia na kupora vituo vya polisi
 

If you are such miss informed or Ignorant why this had been going on for the last 50 years you better shy away from commenting please. I bet you are not iin calibre to Mr. Mohammed Said.
 

= wakisubiri
 
Leo hii Tanzania tuna rais mwislamu, Mmakamu wa Rais pia ni mwislamu (tena yule conservative mwenyewe ambaye pale UDSM alikuwa ameifanya Masjid kama ofisi yake ndogo); yaani mkiristo wa juu kimadaraka ni Waziri mkuu tu ambaye anaweza kuondolewa madarakani wakati wowote na rais lakini unakuta kuna watu wanaohubiri kuwa "Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali" ni jambo la kushangaza sana. Wahubiri wa aina hii ni wale ambao hata uwape nini hawataridhika mpaka pale nchi nzima itakapokuwa ni ya waislamu tupu tena wa aina wanayotaka wenyewe kama ISIS inavyotaka. Je wasiokuwa waislamu hawana haki ya kuishi nchi hii? Tunaelekea wapi?
 

= tuzikabili
 

Maswali:

1) Hiyo "interior" ya Tanganyika / Tanzania ni ipi ambayo ilikuwa haina Waislam na wala haiwajui Waislam mpaka 1970? mbona huweki wazi? au kuzimu?

2) Kwanini Nyerere asidai Uhuru kutokea huko huko "interior" na akaja Dar? kwa wazee wa Kiislaam?

3) Mbona wwe hujatuletea msimamo wako wa Kihistoria ya Tanganyika ya huko "interior" iwe ya Uhuru au yoyote ile, ili tufaidike?
 

Kusikia tu? kila mtu wa Dar kalisikia hilo.

Tuoneshe lilipotajwa kihistoria, kama hauna kaa kimya ujisomee.

Usituletee porojo, kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.
 
Sasa Mzee Mbona Maandiko yako hayana hitimisho, tuwafanyie nini hawa waislaam ili kuwalipa fadhira za kupigania uhuru. Tuwafanyie nini ili wao waridhike maana mchango wao ni mkubwa

= fadhila
 

Mwaka gani? maana Uhuru kutokana na historia ulianza kugombewa zamani sana, tumemsoma Al Alama Mohamed Said akitupa historia ya maji maji, jinsi mababu zetu walivyopigania Uhuru wao.

Jee, vita ya majimaji ulikuwa na miaka 19?
 
Last edited by a moderator:
Mwaka gani? maana Uhuru kutokana na historia ulianza kugombewa zamani sana, tumemsoma Al Alama Mohamed Said akitupa historia ya maji maji, jinsi mababu zetu walivyopigania Uhuru wao.

Jee, vita ya majimaji ulikuwa na miaka 19?
Wakati wa vita ya Majimaji Tanganyika haikuwepo na akina Sykes walikuwa bado ni raia wa Africa Kusini.
 
Kusikia tu? kila mtu wa Dar kalisikia hilo.

Tuoneshe lilipotajwa kihistoria, kama hauna kaa kimya ujisomee.

Usituletee porojo, kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.
Sasa Faiza mtu MDINI wa aina ya Sheikh Takadir unamtaja kwenye HISTORIA ya nchi ipi? Mbona hakuna hata msikiti uloopewa jina hili pamoja kuipenda DINI yake sana?
 
Mkuu Mazoko hili kashaambiwa sana sijui kwanini hataki kutoka kwenye kichaka cha udini.
Mzee Mohamed Said kajihalalisha kwa udini. Hawezi kutoka humo. Kawaingiza na marehemu wengi kwenye UDINI huo ili kujijengea ka-legitimacy ka aina flani hivi. Hawezi kubadilika.
 
Last edited by a moderator:
Kusikia tu? kila mtu wa Dar kalisikia hilo.

Tuoneshe lilipotajwa kihistoria, kama hauna kaa kimya ujisomee.

Usituletee porojo, kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.
Mhamasishaji wa kupiga fatwa tuu ataje wapi kwa lipi?.
Endeleeni tuu kupiga mikelele humu, huku shule zetu zikiendelea kutesa kwenye top ten, huku zenu zikiendelea kuzungusha kule mkiani!. Chuo kikuu hicho mmepewa sadaka, kimewashinda, na mahakama za kadhi mtapewa na zitawashinda!, wengine hawana wajuacho, ama wachangiacho zaidi tuu ya kupiga adhana!.

Kama Sheikh Takadir alikuwa muhimu kihivyo wa kustahili kuenziwa, then si mumuenzi nyinyi mnaoujua umuhimu wake!.
Pale Arusha tunao uwanja wa Sheikh Amri Abeid, sijamsikia Sheikh Kassin Bin Jumaa anaenziwa vipi?, Sijamsikia Sheikh Hemed Bin Jumaa bin Hemed, anaenziwa vipi!, sijamsikia Sheikh Nurdeen Husein anaenziwa vipi!, sijamsikia Sheikh Said Comorean anaenziwa vipi, sijamsikia Sheikh Omar Jabir anenziwa vipi, why only Sheikh Takadir?!.

Hizi lugha za porojo, kuhororoja na kubwabwaja, nazo kakufunza Maalim Al Alama Mohamed Said?!.

Pasco
 

Pasco,
Imam Shaffi alikuwa akisema kuwa yeye anaweza kusimama kwa hoja hata
na watu mia lakini akitokea mjinga mmoja tu basi yeye huwa keshashindwa.
 
Wakati wa vita ya Majimaji Tanganyika haikuwepo na akina Sykes walikuwa bado ni raia wa Africa Kusini.

WildCard,
Unapenda mjadala lakini hufanyi maandalizi ukasoma kile unachotaka kujadili.

Isome historia ya Tanganyika vizuri.
Baada ya Berlin Conference Wajerumani wakaja Tanganyika kuja kuifanya koloni.

Wananchi walikataa uvamizi huu wakaamua kupigananao.
Bushiri bin Salim alisimama Pangani kupinga uvamizi huu na Mkwawa pia.

Wajerumani wasingeweza kupata jeshi Tanganyika ambalo lingepigana dhidi
ya ndugu zao hivyo Wissman akenda Mozambique kwenye kijiji cha Kwalikunyi
huko ndiko alipoweka mkataba na Chief Mohosh ndipo wakaja hawa Wazulu
kama jeshi la mamluki.

Ndani ya jeshi hili alikuwapo Sykes Mbuwane.

Wajerumani wakenda Sudan huko nako wakachukua askari mamluki wa Kinubi
wakawaleta Tanganyika.

Jeshi likawa limekamilika na vita ikaanza dhidi ya Bushir na Mkwawa.
Bushiri akakamatwa akanyongwa na historia ya Mkwawa ni mashuhuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…