Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Tunajua mna mkakati wa kusilimisha NCHI,Hamtaweza.Tangu huyu mzee apewe AZIMIO LA ABUJA.Kaleta MAJANGA.

Abu Jahal,
Kuna mahali nilionya hapa kuwa "Azimio la Abuja," si document ya kutegemea
kwa sababu chanzo chake (source) ni kitabu cha Walokole wa Kimarekani:
"The Two Headed Dragon" ambaho kilisambazwa kwa wingi Nigeria.

Si kitabu cha maana.
 
Kila nikiona malalamiko ya waislamu juu ya Nyerere najiuliza kama mikakati yakuipatia uhuru taifa hili liliratibiwa na waislamu je
1.Ilikuwaje Nyerere akawazidi ujanja?
2.Je walitaka taifa hili liwe la kiislamu?
3.Nyerere kusema taifa hili halina dini wao wameathirika na nini
NB:matokeo yametoka mwanzo walilalamika kuwa ndelichako nikikwazo sasa kaondoka matokeo yametoka kumi bora hampo kumi za mwisho mpo je tatizo nini
 
Babuwaloliondo,
Angalia nimeanza lini kuandika.

Soma kwanza ndipo useme.
 
Mazoko,
Hayo mengine watajibu wengine.

Naomba nikuulize hili moja.
Katoka Ndalichako kaingia nani?
Mazoko,
Hayo mengine watajibu wengine.

Naomba nikuulize hili moja.
Katoka Ndalichako kaingia nani?

Mohamed
Nijibu maana nategemea kuelimishwa nasio kulumbana
Pia aliyeleta mada hii nadhani katoa kwenye gazeti la RAIA MWEMA wiki hii nimesoma hekaya za mwandishi chaajabu nilichoshidwa kuelewa na hasa ndiyo chuki aliyoisema mwandishi nikuwa Nyerere aliwaleta wakristo wagombee uongozi na mwandishi anakiri kuwa wakoloni waliweka sheria ya wagombea wawe wewna elimu ambayo kwa bahati mbaya shekhe na wenzake hawakuwa nayo
Nikajiuliza swali je tulitaka tusipate uhuru mpaka waislamu wasome? Tena anakiri ushindi ulipatikana mkubwa sana kwa mtu mweusi je huyu mkristo alichaguliwa na nani sina dini zote tena akaendelea kusema baada ya ushindi Nyerere akampinga sasa huyu mweshimiwa kwakutaka kuleta udini je kosa la Nyerere nilipi?
 
Nimekupa swali ili nikugutue na utazame lile ambalo mimi nimeona
limekupita.

Kingine ambacho napenda uzingatie ni kuwa hayo ambayo umeandika
ya TANU kupata ushindi mkubwa kwa kuchaguliwa na watu ndiyo
niliyoandika mimi.

Si wengi walikuwa wanaijua historia hii na mimi nimeileta hapa na
sasa inafahamika.

Katika hali kama hii ni juu ya msomaji mwenyewe kufanya uchambuzi
wake mwenyewe kama ulivyofanya wewe.

Hii ndiyo kazi kubwa ya mwandishi yoyote.
Kuiletea jamii kile ambacho hakikuwa kinafahamika.

Mimi sikulazimishi kuiona historia hii katika jicho langu.

Una uhuru wa kuchambua mambo kama akili yako inavyokuelekeza.

Ila umenisikitisha kusema kuwa historia hii ya TANU hasa kipande
hiki kuelekea uhuru kuanzia 1958 ni "hekaya."

Naelewa moyo unakuuma kwa kuwa kwako historia hii imekuletea
mshtuko wa moyo.

Hauko peke yako.

Watu wengi wameumizwa na hizi taarifa mpya katika historia ya
nchi nchi yetu zaidi kwa kugundua kuwa historia waliyoizoea
haikuwa imekamilika.

Mazoko,
Mimi siandiki hekaya.
Usiwe na haraka katika kunihukumu.

Soma kazi zangu na baadhi zimechapwa na wachapaji wenye sifa
ulimwenguni kama Oxford Univeristy Press.

Soma mada zangu nilizowasilisha katika vyuo tofauti ndani na nje
ya nchi yetu.

Baada ya hapo ndiyo unaweza ukanihukumu ikiwa unao uwezo huo.
 
scan0026.jpg

Kutoka Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, Mbutta Milando, JohnRupia na Julius Nyerere Hao Waliowazunguka na Silaha za Jadi ni Bantu Group Kundi la Vijana wa TANU lililokuwa linatoa Ulinzi kwa Viongozi wa TANU. Picha Hii Ilipigwa Mwaka wa 1955.

Jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU. Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na sidhani hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa. Lakini naamini viongozi hawa walio madarakani hivi sasa ambao wakati wa kudai uhuru walikuwa watoto wadogo lazima watakuwa wamesikia jina hili likitajwa na wazee wao. Sheikh Suleiman Takadir hutajwa kila linapotokea jambo ambalo Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali kwani ilikuwa Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyeweka agenda ya hali ya baadae ya Waislam na Uislam katika Tanganyika huru mwaka 1958. Jambo hili alipolileta lilitishia kuigawa TANU katika misingi ya dini katika wakati amabo umoja wa Waafrika ulikuwa unahitajika sana. Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imeenea nchi nzima na tayari iko katika barabara ya kuelekea kuchukua madaraka ya ndani na kisha Tanganyika kupata uhuru wake kamili.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa nani na nini ulikuwa umaarufu wake? Sheikh Suleiman Takadir kwanza alikuwa ‘’alim,” mwanazuoni kisha alikuwa Mwenyekiti muasisi wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia TANU ilipoundwa mwaka 1954 hadi “alipotoswa” mwaka 1958 kwa kosa la “kuchanganya dini na siasa.’’ Sheikh Takadiri alishiriki vilivyo ndani ya Baraza la Wazee wa TANU katika kutayarisha safari ya Nyerere kwenda UNO mwaka 1955. Wapenzi wake katika harakati za kupigania uhuru walimpachika jina la utani wakimwita “Makarios,” wakimlinganisha na Askofu Makarios wa Cyprus na Ugiriki aliyekuwa anapambana na ukoloni wa Waingereza wakati yeye alipokuwa anapambana na Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Sasa kwa kuwa Suleiman Takadir alikuwa sheikh na mpambanaji ndipo walimpa jina hilo la “Makarios” na kwa hakika jina hili lilimkaa, likamwenea vyema na yeye akalipenda.

WAZEE%2BWA%2BTANU.jpg

Baraza la Wazee wa TANU
Sheikh Suleiman Takadir wa Pili Chini Kulia, Wa Pili Waliosimama Dossa Aziz,
Wa Sita Julius Nyerere, Wa Saba John Rupia, Wa Tisa Said Chamwenyewe,
Anaefuatia Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate

Mikutano ya mwanzo ya TANU ilikuwa ikifanyika Mnazi Mmoja mbele ya baadae ilipojengwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Wakati ule pale palikuwa hakuna jengo lolote, palikuwa na kiwanja kitupu na ardhi ile ilikuwa mali ya Mzee John Rupia Makamu wa Rais wa TANU. Kiwanja hiki baaadae Mzee Rupia aliwapa TANU na TANU wakaanzisha Chuo Kikuu pale mara baada ya uhuru. Mikutano ya kwanza ya TANU ikifanyika pale Mnazi Mmoja na kabla Nyerere hajapanda juu kwenye jukwaa kuzungumza na wananchi alikuwa kwanza anatangulia Sheikh Suleiman Takadir kusawazisha uwanja na kuwaweka wananchi tayari kumsikiliza kiongozi wao. Kama alivyokuwa Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri alikuwa na kipaji cha kuongea. Leo hii huenda baadhi ya wasomaji wangu wasiamini lakini ukweli ni kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabla hajazungumza lolote alikuwa akipiga “fatha,” wananchi wakaitika na kwa umoja wao wakasoma, “Surat Fatha,” sura ya ufunguzi katika Qur’an Tukufu, kisha Sheikh Takadir akaomba dua na wananchi wakawa wanaitika kwa pamoja, “Amin,” Amin,” “Amin.” Baada ya hapo ndipo atapanda Nyerere na kuanza kuhutubia. (Picha za mwanzo za mikutano hii zipo na zilipigwa na Mzee Shebe ambae katika miaka ile ya 1950 alikuwa na studio yake Mtaa wa Livingstone na Kipata. Picha hizi baadhi nimepata kuziona. Mzee Shebe ndiye alinipiga picha yangu ya kwaza nikiwa na umri wa mwaka mmoja au miwili hivi na picha hii ninayo hadi hii leo. Inaaminika Mzee Shebe ndiye mpiga picha wa kwanza wa TANU na Nyerere).

002_2.JPG

Mwandishi Akiwa na Mwaka Mmoja Au Miwili Picha Aliyopigwa na Mzee Shebe
1952/53 Kwenye Studio Yake Mtaa wa Livingstone na Kipata

scan0027-1.jpg

Nyerere Akihutubia Mkutano wa TANU Siku za Mwanzo

Huyu ndiye Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954.Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA. Sheikh Takadir alimpenda sana Nyerere kiasi kuwa mwaka 1957 katika hotuba aliyotoa katika tafrija moja ya taarab Mtaa wa Mvita, alimwita Nyerere, “Mtume wa Afrika,” aliyetumwa na Mungu kuwaokoa Waafrika. Maneno yale ya Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kama anamtabiria Nyerere makubwa katika mustabali wa Afrika, kwani miaka mingi baadae Nyerere alikuja kusimama mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika kutoka makucha ya wakoloni. Nyerere akawa hapungui nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Swahili. Nyumba hii iko jirani na kilabu ya mpira ya Pan Africa. Kutembelewa na Nyerere pale nyumbani kwake ikapelekea baba mwenye nyumba, Jumbe bin Jumaa wa Digosi amuhamishe nyumba Sheikh Takadir asije kumponza kwa kwani Nyerere alijulikana kama adui mkubwa wa Waingereza. Hii kwa muhtasari ndiyo historia ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere. Lakini usuhuba huu ulikuja kuvunjika na watu wawili hawa wakawa mahasimu wakubwa, Sheikh Suleiman kafa hasemi na Nyerere na Nyerere kwa upande wake hakupata hata siku moja kumtaja Sheikh Takadir popote hadi anaingia kaburini. Inaaminika Sheikh Takadir alikufa kihoro baada ya kupigwa pande na TANU na wakazi wote wa Dar es Salaam na wanachama wa TANU kwa kosa la “kuchanganya dini na siasa.” (Ikiwa msomaji wangu ulisoma makala yangu ya juma lililopita utakuwa umeona kuwa TANU ikiongozwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir ilipitisha azimio la kupiga vita hisia zozote na chembechembe za Uislam ndani ya TANU). Hakika Uislam ulikuwa na nguvu ndani ya TANU lakini haukuachiwa uvuke mipaka kuwabagua wengine waliokuwa si Waislam.

Kilitokea nini hadi kupelekea Sheikh Suleiman Takadir agombane na Nyerere? Chanzo cha mtafaruku huu ni Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka 1958. Waingereza waliweka masharti ambayo kwa hakika yalikuwa ya kibaguzi na yalifanya wananchi wengi wasiweze kukidhi sifa zilizowekwa za kuweza mtu kupiga au kupigiwa kura. Kulikuwa na sifa ya elimu, kipato na kazi ya kukubalika na kupiga kura kwa tabaka za rangi. Mpiga kura Mwafrika alitakiwa ampigie kura Mzungu, Muasia na Mwafrika. Masharti haya yalikuwa kisiki kigumu kwa uongozi wa TANU na wanachama wake kutimiza. TANU na viongozi wake wengi hawakuwa na hiyo elimu iliyokuwa ikitakikana wala kipato cha maana. Ili mtu asimame kama mgombea kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria au awe angalau mpiga kura ilibidi azikusanye sifa zote hizo mahali pamoja. Wapiga Kura na wagombea walitakiwa wawe na kisomo cha darasa la 10 au kipato cha pauni 400 kwa mwaka na kuwa na kazi ya maana. Waafrika waliokuwa na sifa hizi hawakuwa wengi katika TANU. Wengi katika TANU kama walivyokuwa wakipenda kujiita wenyewe walikuwa, “Baba Kabwela.” Ikawa sasa ili TANU iweze kuweka wagombea ilibidi iwatafute watu nje ya uongozi wa TANU. Hapa ndipo lilipokuwa tatizo.

scan0023.jpg

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyerere Akitia Sahihi Azimio la Tabora[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ilibidi TANU sasa iwalete watu wenye sifa nje yake na wengi wa watu hawa walikuwa Wakristo waliosomeshwa na wamishionari. Jambo hili lilimkera sana Sheikh Takadir na wanachama wengi wa TANU kwa ujumla wao na kwa hakika TANU nzima hawakutaka kabisa kuingia uchaguzi ule kwa masharti yale waliyoyaona ya kibaguzi. Wanachama wa TANU walikuja na kauli mbiu isemayo, “Kuingia Kura Tatu ni sawa na kujipaka kinyesi.” Ilikuwapo minong’ono kuwa Wakristo wataichukua nchi lakini kwa muda mrefu hofu hii ilizuiwa kwenye vifua hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kulisema hilo waziwazi kwani jambo la dini lilikuwa mwiko mkubwa katika TANU. Ikawa tatizo lile la kushiriki kwa TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu lijadiliwe kwenye Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka 1958 uliopangwa kufanyika Tabora. Mpinzani mkubwa wa Kura Tatu alikuwa Zuberi Mtemvu, Katibu Mwenezi wa TANU kwa wakati ule. Ukweli ni kuwa Kura Tatu ilitishia uhai wa TANU na zilikuwapo dalili za chama kumeguka pande mbili. Kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Zuberi Mtemvu na Sheikh Takadir wangelikuwa upande mmoja na wangeweza kuja na chama kingine ingawa agenda zao zilikuwa tofauti. Mtemvu yeye alisimama kwenye Afrika kwa Waafrika na Sheikh Takadir kwenye Uislam. Mkutano wa Tabora ni kisa kirefu In Sha Allah tutakitafutia wakati wake makhsusi tukizungumze. (Nimekiandikia kitabu kizima “Uamuzi wa Busara,” Abantu Publishers 2007, Dar es Salaam) Sheikh Suleiman Takadir na baadhi ya wazee katika Baraza la Wazee wa TANU walikuwa wajumbe katika mkutano wa Tabora. Kufupisha kisa TANU ilipiga kura kukubali kuingia kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu na manusruna kura zifungane kati ya wale wanaounga mkono na wale waliokuwa wakipinga. TANU iliingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu na ikapata ushindi mkubwa.

Hofu aliyokuwanayo Sheikh Takadir ilikuwa kuwa watu walioingia katika TANU kuchukua uongozi ni Wakristo. Sheikh Takadir alikuwa anajua nguvu ya madaraka waliyokuwa wanakabidhiwa akawa na hofu kama uongozi huu mpya utakuja kutoa haki kwa Waislam uhuru utakapopatikana. Sheikh Takadir alitaka uhakika wa hali ya baadae ya Waislam katika Tanganyika huru. Katika mkutano wa Halmashauri Kuu Makao Makuu ya TANU, New Street Sheikh Takadir alimkabili Nyerere akamshutumu kuwa hakuwa na nia nzuri na Waislam, atakuja wapendelea ndugu zake Wakristo katika Tanganyika huru. Sheikh Takadir akawageukia wenzake katika Baraza la Wazee wa TANU akasema, “Tuzibe ufa tusije tukajenga ukuta.” Jambo lile lilikuwa zito. Nyerere alijiinamia na aliponyanyua uso wake machozi yalikua yanambubujika. Mkutano haukuweza kujadili jambo lile na kikako kile kikavunjika pale pale na wajumbe wakawatawanyika.

Sheikh Takadir ‘’akatoswa,’’ kwani alikuwa amevunja mwiko mkubwa katika TANU. Mzee Iddi Tulio akachaguliwa kushika nafasi yake. Huku ‘’kutoswa’’ na kutengwa na jamii ndiko kulikosababisha kifo cha Sheikh Takadir. Alikuwa hata akitoa salamu hakuna aliyeitika. Akienda sokoni Kariakoo kununua chochote kile hakuna aliyekuwa tayari kupokea hela yake. Haikuchukua muda mrefu Sheikh Takadir akaaga dunia. Kabla Sheikh Takadir hajafa TANU ilifanya mkutano mkubwa sana na Nyerere akamshambulia Sheikh Takadir kwa kutaka kuwagawa Watanganyika katika misingi ya dini. Baada ya mkutano kundi kubwa lilikwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kuzomea huku wakiimba, “Takadir Mtaka Dini.” Sheikh Takadir alitoka nje akasimama kizingitini akasema maneno haya, “Ndugu zangu In Sha Allah iko siku mtakuja kunikumbuka.” Haukupita muda mrefu Sheikh Takadir akatangulia mbele ya haki na kwa kipindi kirefu katika historia ya uhuru wa Tanganyika hakuna aliyemkumbuka Sheikh Suleiman Takadir, Askofu Makarios wa Tanganyika. Hivi sasa Sheikh Suleiman Takadir anatajwa sana na kizazi cha leo. Utabiri wake kuwa ndugu zake watakuja kumkumbuka umetimia. Swali la kujiuliza ni iweje hii leo baada ya miaka 57 kupita Sheikh Suleiman Takadir anarejeshwa upya katika historia ya kupigani uhuru wa Tanganyika? Hiki ni kitendawili kinachongoja kuteguliwa.

3ngq7mfoNBkDsGoTihZVXo4ZzngGhTG3i5TneJ6bQLk=w409-h207-p-no

Cc watanzania cku zote ni bendera fuata upepo. Tunakurupuka na kufanya maamuzi mapema pasi na kufikiria consequence, alafu baadae watu wa majuto na kulalama. Rest in peace Takadir.oo
 
Plo Lumumba Jr.
Usiseme adui.

Yapo matatizo ambayo viongozi wetu wanaogopa kuyakubali.

Mfano BAKWATA.

Hii taasisi haikuundwa na Waislam na Waislam hawaitaki lakini ipo kwa kuwa serikali inataka iwepo ifanye kazi ya upawa.

Upawa kazi yake ni kupakua vitu vya moto.

mzee wangu usiishie kutonyesha vidonda, nimekua nikifuatilia haya mambo naona umejitoa kutetea ulichokiona kimepindishwa. endelea kutafuta historia na ushahidi wa kutosha endelea kuandika vitabu ambavyo vitakua urithi kwa watakao endeleza harakati zako mwisho kabisa ni vyema ukawapelekea malalamiko yako vyombo husika.
 
Mohamed Said nasikitika kwanini unakwepa maswali nijibu kwa manufaa ya wengine maana yawezekana unajambo zuri kuliko nijuwavyo mimi maana wakati wakugombea uhuru nilikuwa na miaka19 na kila mmoja wetu tulikuwa tunapigania kupata uhuru nasio kutawaliwa na dini ipi sasa nijibu maswali yangu nadhani unaweza kuyaona nyuma
Nijuavyo mimi nikuwa umeleta mada hii ili kutuelimisha sasa mbona unaleta hadithi badala ya majibu
Ingawa yawezekana ukawa unaniweka kwenye kundi fulani ila siku huko nijibu kwa faida yangu na wengine
 
Kama shekhe takadir alitengwa na wengi ambao ni waislamu kama simulizi inavyosema,maana ake waislamu wenzie waliona umuhimu wakuwa wamoja katika kuikomboa tanganyika na siyo fikra za takadir kuwa anaikomboa dini ya kiislamu,..
 
Very true hakuna sababu ya sisi Watanganyika kumkumbuka hata kidogo
 
Mohamed Said nasikitika kwanini unakwepa maswali nijibu kwa manufaa ya wengine maana yawezekana unajambo zuri kuliko nijuwavyo mimi maana wakati wakugombea uhuru nilikuwa na miaka19 na kila mmoja wetu tulikuwa tunapigania kupata uhuru nasio kutawaliwa na dini ipi sasa nijibu maswali yangu nadhani unaweza kuyaona nyuma
Nijuavyo mimi nikuwa umeleta mada hii ili kutuelimisha sasa mbona unaleta hadithi badala ya majibu
Ingawa yawezekana ukawa unaniweka kwenye kundi fulani ila siku huko nijibu kwa faida yangu na wengine

Mazoko,
Swali gani unataka nikujibu.
Nifahamishe.

Makala ya Sheikh Suleiman Takadir imewagusa watu wengi sana.

Toka ilipotoka katika gazeti la Raia Mwema nimepongezwa na pia
kulaumiwa na wengi.

Wengi sana walikuwa hawakijui kisa hiki na kimewasisimua sana.

Nadhani wasomaji wangu wengi watataka kujua nini nitakujanacho
toleo lijalo In Sha Allah.

Sikutii katika kundi lolote.

Mimi nifanyapo utafiti kisha nikaa kitako kuandika huwa nazungumza
na dunia nzima.

Mtu mmoja au kundi la watu lina manufaa au tija gani?

Ndiyo maana naandika na Oxford University Press kisha kwa
Kiingereza ili niufikie ulimwengu.

Kuhusu kuleta, "hadithi."
Allah hakunijaalia kipaji hicho ingawa mie ni mpenzi wa riwaya.

Ujanani nikiwasoma James Hadley Chase, Irving Wallace, Peter
Cheyney
nk.
 
Inaonekana umejitoa ufahamu maswali unayajuwa na unakwepa kwepa

Naona unajivunia kuchapicha Oxford University press mimi nimefanyanao kazi ila kwa sasa ninakampuni yangu mimi nimejikita zaidi kwenye UCHUMI na Upatanishi kuliko dini nawengi wamefaidika na mimi pia nimetembea bara la Ulaya kwenye nchi zaidi 15 Afrika zaidi ya nchi 20 America asia na kwingineko
Huko kote nimealikwa kwenye midahalo yakuikomboa Dunia hasa mwafrika kutoka kwenye utumwa wakimawazo nakujenga uchumi imara

Dunia yaleo sio kuzungumzia dini fulani au utawala wa dini fulani maana hauna tija
Kunachi zinaongozwa kwa imani za kidini kama
Misri,Irak,Iran,Libya nanyinginezo hakuna utulivu zaidi ya ugomvi

Nadhani ifike sehemu dini zibaki misikitini na makanisa huku tuubiri upendo amani basi
 
Great thinker
 
Sijui kwa nini hii makala ya Sheikh Suleiman Takadir imekukasirisha.

Hapa tulipofika panatosha.
 
Nashukuru kwa kutupa taarifa nani hasa alianzisha chokochoko za kidini Tanzania/Tanganyika. Yalikuwa makosa makubwa sana kutokujua chanzo hasa cha mambo haya ya kidini hapa nchini. Kujua chanzo cha tatizo ni mwanzo wa kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom