Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU. Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na sidhani hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa.
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kwa kisa hiki cha Mzee wako, Sheikh Suleiman Takadir, ila sio kweli kuwa Mzee huyu hatajatwa popote kwenye historia ya Tanu, kwa sababu mimi nimelisikia jina la Sheikh Suleiman Takadir siku nyingi, kabla sijakusoma wewe, hivyo lazima kuna mahali alitajwa hadi mimi kumjua!, na sio kutajwa tuu, nadhani ia kuna namna alienziwa, sikumbuki vizuri, lakini nahisi niliwahi kulisikia jina la Mtaa fulani ukiitwa Takadiri japo sikumbuki vizuri!.
Kama hii ndio ilikuwa sifa kuu ya Sheikh Takadir, "kuongea sana na kupiga 'fatha' kwenye mikutano ya Tanu!, connotation meaning ya para hii ni kuwa Mkiristo Nyerere, alikuwa hawezi kupanda jukwaani kuwahutubia Waislamu wa Tanu, mpaka kwanza Sheikh Takadir atangulie kuwapooza kwa 'fatha'!, jambo ambalo sii kweli!, ili ukweli ni kuwa Maeneo mengi ya Uswahilini, walijaa Waislamu, hivyo hizo 'fatha' ni kikolezo tuu cha kujengea hamasa, kama alivyoakifanya Salum Tambalizeni kwenye mikutano ya CCM, yaani kazi ya uhamasishaji, hivyo inawezekana kwa sasa, usimsikie Tambalizeni ekienziwa popote!, kama ambavyo alivyotoswa Sheikh Takadir!, msingi wa mtu yeyote kuenziwa ni mchango wake kuthaminiwa kwenye jambo fulani!, kama mchanga wake ni uhamasishaji tuu, then alivyothaminiwa hata kwa kutajwa tuu hadi mimi kumfahamu, ni thamani tosha!. Wako wengi walioisaidia sana Tanu, na wengine hadi kufungwa gerezani kuipigania Tanu kama kina Robert Makange na Kheri Bagdelalah lakini sikumbuki kuwasikia ni wapi walienziwa!. Kuna mamia wengine huko mikoani, wamefanya makubwa kwa Tanu, lakini sikupata kuwasikia mfano Dr. Kyaruzi, mimi ndio nimemsikia juzi juzi tuu baada ya kufariki kimya kimya huko kwao Bukoba!. Hivyo kuna wengi waliofanya makubwa kwa Tanu, hawajatajwa, ila wewe unajenga picha kwa Wazee wako tuu kuwa hawajatajwa kwa Uislamu wao!, kitu ambacho sii kweli, na haitakuwa kweli hata siku moja!.[/QUOTE]Mikutano ya kwanza ya TANU ikifanyika pale Mnazi Mmoja na kabla Nyerere hajapanda juu kwenye jukwaa kuzungumza na wananchi alikuwa kwanza anatangulia Sheikh Suleiman Takadir kusawazisha uwanja na kuwaweka wananchi tayari kumsikiliza kiongozi wao. Kama alivyokuwa Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri alikuwa na kipaji cha kuongea. Leo hii huenda baadhi ya wasomaji wangu wasiamini lakini ukweli ni kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabla hajazungumza lolote alikuwa akipiga fatha, wananchi wakaitika na kwa umoja wao wakasoma, Surat Fatha, sura ya ufunguzi katika Quran Tukufu, kisha Sheikh Takadir akaomba dua na wananchi wakawa wanaitika kwa pamoja, Amin, Amin, Amin. Baada ya hapo ndipo atapanda Nyerere na kuanza kuhutubia.
Huu pia ni urongo, hapa unataka kujenga picha kuwa eti ni Sheikh Takadir ndie aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza kwa watu wa Dar es Salaam!, sii kweli!, kwenye utambulisho wa Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, naamini unaujua vilivyo!, labda ungesema, Sheikh Takadir pia alipiga ile 'fatha' yake maarufu kwenye mkutano wa kwanza wa kumtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, ningekukubalia, lakini siye yeye aliyemtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam!.Huyu ndiye Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954.Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA.
Hili pia ni kujazilizia tuu kile Nyerere alichoandikiwa, kama Sheikh Takadir aliyasema haya 1957, alicopy tuu utabiri uliotangulia na kuja kuwa paste hapo kwenye hiyo tafrija ya Taarab, nyota ya Nyerere iliisha anza kung'aa siku nyingi tangu yuko Tabora School, Makerere, Edinburg hadi St. Francis (Pugu) siku nyingi kabla, hivyo utabiri huu wa Sheikh Takadir ilikuwa ni kujazia tuu yaliomo yamo!, usitaka kudanyanga humu eti aliyemtabiria Nyerere ukuu ni Sheikh Takidir!, is just one of them!.Sheikh Takadir alimpenda sana Nyerere kiasi kuwa mwaka 1957 katika hotuba aliyotoa katika tafrija moja ya taarab Mtaa wa Mvita, alimwita Nyerere, Mtume wa Afrika, aliyetumwa na Mungu kuwaokoa Waafrika. Maneno yale ya Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kama anamtabiria Nyerere makubwa katika mustabali wa Afrika, kwani miaka mingi baadae Nyerere alikuja kusimama mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika kutoka makucha ya wakoloni.
Huu utakuwa ni urongo mwingine, unless wewe ulikuwa bennet na Mwalimu, 24/7 hadi anaingia kaburini, ndio uweze kulisema hili kwa hakika!.Lakini usuhuba huu ulikuja kuvunjika na watu wawili hawa wakawa mahasimu wakubwa, Sheikh Suleiman kafa hasemi na Nyerere na Nyerere kwa upande wake hakupata hata siku moja kumtaja Sheikh Takadir popote hadi anaingia kaburini.
Hapa sasa ndio the Best of Maalim Mohamed Said!, muogope Mola wako!, huwezi kudaid kuwa Sheikh Takadir alikufa kwa kihoro cha kutoswa!, yaani kisababishi cha kifo chake ni kule kutenwa na jamii!. Uhai umeumbwa, na kifo pia kimeumbwa, Sheikh Takadir alijifia natural death siku yake aliyopangiwa na Mungu ilipowadia!. Kwa msio jua!, Malaika mtoa roho, Israel, anampitia kila mmoja wetu mara sabaini fii sabaa kwa siku, ili kuhakikisha muda wake ukifika asizidishe hata sekunde moja!. Hili ni moja ya bandiko jingine la Maalim Mohemed Said lenye kutoa ilmu adimu, but with "ill motive" behind!, ili ilionekane hata kifo cha Shekh Sulemain Takadir, msababishi ni fulani!.Inaaminika Sheikh Takadir alikufa kihoro baada ya kupigwa pande na TANU na wakazi wote wa Dar es Salaam na wanachama wa TANU kwa kosa la kuchanganya dini na siasa.
Sheikh Takadir akatoswa, kwani alikuwa amevunja mwiko mkubwa katika TANU. Mzee Iddi Tulio akachaguliwa kushika nafasi yake. Huku kutoswa na kutengwa na jamii ndiko kulikosababisha kifo cha Sheikh Takadir. Alikuwa hata akitoa salamu hakuna aliyeitika. Akienda sokoni Kariakoo kununua chochote kile hakuna aliyekuwa tayari kupokea hela yake. Haikuchukua muda mrefu Sheikh Takadir akaaga dunia. Kabla Sheikh Takadir hajafa TANU ilifanya mkutano mkubwa sana na Nyerere akamshambulia Sheikh Takadir kwa kutaka kuwagawa Watanganyika katika misingi ya dini. Baada ya mkutano kundi kubwa lilikwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kuzomea huku wakiimba, Takadir Mtaka Dini. Sheikh Takadir alitoka nje akasimama kizingitini akasema maneno haya, Ndugu zangu In Sha Allah iko siku mtakuja kunikumbuka. Haukupita muda mrefu Sheikh Takadir akatangulia mbele ya haki na kwa kipindi kirefu katika historia ya uhuru wa Tanganyika hakuna aliyemkumbuka Sheikh Suleiman Takadir.
Pamoja na "the ill motive behind", asante kwa simulizi nzuri,
endelea tuu kuipalilia na kuimwagilia na kuitilia mbolea hii "mbegu", soon itamea vilivyo na tutapata mavuno stahiki muda stahiki ukiwadia, wakati huo huo mimi naendelea kufanya research yangu kwenye urais wa Tanzania, rais akiwa ni Mkristo ni kwanini lazima awe ni Mkatoliki?.
Pasco.