Jingu: Lissu anazungukwa na watu wasiokuwa na uwezo

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Jackson Jingu, ameibua hoja nzito dhidi ya uongozi wa juu wa chama hicho, akidai kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa (bila kumtaja jina moja kwa moja) amezungukwa na watu wasiokuwa na uwezo wa kisiasa wala kiuongozi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Jingu amesema baadhi ya watu waliomzunguka Mwenyekiti huyo wamekuwa wakitoa ushauri usio na tija, na kwamba ushauri huo umekuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa chama, ikiwemo maamuzi ya kufukuza wanachama muhimu.

"Wanampelekea ushauri kama yaliyotokea kwenye uchaguzi, wanamwambia mfukuze fulani, na yeye anakubali. Kwa sababu gani? Kwa sababu hana watu sahihi wa kumshauri katika mambo ya ujenzi wa chama," amesema Jingu.
 
Msikilize Dr shala Ndio utajua lissu amezungukwa na watu gani!!
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Jackson Jingu, ameibua hoja nzito dhidi ya uongozi wa juu wa chama hicho, akidai kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa (bila kumtaja jina moja kwa moja) amezungukwa na watu wasiokuwa na uwezo wa kisiasa wala kiuongozi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Jingu amesema baadhi ya watu waliomzunguka Mwenyekiti huyo wamekuwa wakitoa ushauri usio na tija, na kwamba ushauri huo umekuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa chama, ikiwemo maamuzi ya kufukuza wanachama muhimu.
Hata jinga nae afukuzweee TU maana hakuna namnaa.
 
Msikilize Dr shala Ndio utajua lissu amezungukwa na watu gani!!
Unamaanisha yule aliyekuwa anatuaminisha kuwa Bandari imeuzwa milele ama mwingine? Umeona wapi msomi anaongea kwa hasira hasira hivi? Kuna wakati Harvard huwa wanapitiwa kwenye kuchukua kudahili.
 
Back
Top Bottom