Jinsi Ambavyo Ningefanya Baada ya Kuishika Milioni 100 za haraka

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Kuna wakati mtu unapata pesa za haraka alafu unashindwa kuwaza ufanye nini kwa haraka ili pesa yako isiishe bila kufanya cha maana. Wengine wanapata kutoka kwenye kiinua mgongo, mafao fulani, wengine mkopo, wengine ni mgao fulani, wengine wanagawiwa kama zawadi n.k

Kama mimi ningebahatika kuishika milioni 100 kwa haraka, ningeivunja katika vipande kwa umakini mkubwa sana, nikihakikisha kila senti inatumika ipasavyo🤣:

1. Milioni 30 ningewekeza katika soko la hisa hususan hisa ya CRDB. Ingekuwa imekuja hii hela 2022 basi hela yote ningetupia NICOL na 2024 ningekuwa nimetengeneza milioni 200 (maana kwa miaka 2 NICOL ilikua mara 2 yake toka bei ya hisa 380 hadi 810 Julai/Agosti).

2. Milioni 30 nyingine ningetupia hatifungani za miaka 25 na kisha gawio lake lote lingekuwa linaelekea UTT AMIS.

3. Milioni 10 ningeacha katika akiba dharura na nayo ingekuwa katika mfuko wa Ukwasi inayoendelea kukua mdogo mdogo.

4. Milioni 10 nyingine ningeiweka katika biashara kuendeleza kukuza biashara kidogo kidogo.

5. Milioni 10 nyingine ningeweka katika ununuzi wa vito kama sehemu ya akiba.

6. Milioni 5 ningeweka katika akiba ya uwekezaji binafsi katika maarifa kwa miaka 2 juu ya uwekezaji na biashara.

7. Milioni 3 inayobakia iendelee kuwa sehemu ya ustawi wa kijamii.

8. Milioni 2 kwa ajili ya kupata nafasi ya kusafiri nchini kutafuta fursa za kibiashara.

Ningefanya hayo

Lakini pia wanaopenda mambo ya biashara tuna vitabu viwili tumeviandika vinaweza kukusaidia sanasana. Kitabu cha kwanza ni kwa wale wanaopenda kuchukua bidhaa kariakoo kitabu kimewarahisishia ili waweze kufika kiurahisi kwa wauzaji wa jumla. Na kitabu cha pili ni kwa ndugu zetu wanaopenda kujenga na kufungua vituo vya mfuta vijijini na mjini. Kimewaongoza hatua zote za kufanya.

IMG-20241129-WA0000.jpg

IMG-20241022-WA0010.jpg

Unataka kujifunza biashara na unahitaji hivyo vitabu karibu Whatsapp: 0612607426
 
Wewe mleta mada si ndio Kuna siku ulikuja humu na Uzi ukiitaka serikali ipandishe nauli kwe treni ya SGR hili kulinda biashara ya usafiri wa mabasi isife???

Halafu leo hii uko hapa eti unataka kuwauzia watu maarifa ya kibiashara?

Wewe, Kwa ule Uzi wako tu wa kipumbavu na kipuuzi haufai kuchukuliwa serious na mtu yeyote mwenye akili timamu, maana kwanza hauna akili za biashara Bali una akili za kulihujumu taifa na na uhakika hata kwenye hicho kitabu chako itakuwa kimejaa upuuzi mtupu, hakuna Cha maana huko.
 
Boss kama kuna mahala tulikukwaza kwa makala zetu tunazo andika hapa jamii forums tunaomba utuwie radhi.

Lakini pia kuandika ni sawa na ufundi sio rahisi ukaandika makala ikamfurahisha kila mtu lazima kuna mmoja isimfurahishe na ndio maana wakaweka sehemu ya kutoa maoni (comment) lengo ni kuipima makala.

Na kwa upande wa biashara kila mmoja ana mtazamo wake wa kibiashara. Lakini mwisho wa siku ushauri unapo tolewa hubakia kuwa ushauri tu wala sio utekelezaji au maamuzi ya mwisho.

Kwa hiyo boss kila ushauri unaondikwa hapa jamii forum sio maamuzi ya mwisho ya watoa maamuzi. Viongozi wetu wamechaguliwa ili kutuongoza, sisi tunapotoa ushauri huuchukua na kuupima kwanza ndipo huufanyia maamuzi.

Zaidi tunakuomba radhi kwa kukwazika boss.
 
Ukishibq mihogo mawazo ya ajabu huwa mengi sana
Hayo ni mawazo yetu boss, kama una mawazo mazuri zaidi unaweza kuyaandika hapa kwa faida ya wengi. Jamii forums kila makala inayo andikwa ina umuhimu mkubwa sana.
 
Boss kama kuna mahala tulikukwaza kwa makala zetu tunazo andika hapa jamii forums tunaomba utuwie radhi.

Lakini pia kuandika ni sawa na ufundi sio rahisi ukaandika makala ikamfurahisha kila mtu lazima kuna mmoja isimfurahishe na ndio maana wakaweka sehemu ya kutoa maoni (comment) lengo ni kuipima makala.

Na kwa upande wa biashara kila mmoja ana mtazamo wake wa kibiashara. Lakini mwisho wa siku ushauri unapo tolewa hubakia kuwa ushauri tu wala sio utekelezaji au maamuzi ya mwisho.

Kwa hiyo boss kila ushauri unaondikwa hapa jamii forum sio maamuzi ya mwisho ya watoa maamuzi. Viongozi wetu wamechaguliwa ili kutuongoza, sisi tunapotoa ushauri huuchukua na kuupima kwanza ndipo huufanyia maamuzi.

Zaidi tunakuomba radhi kwa kukwazika boss.
Pamoja na kwamba kila mtu ana uhuru WA kutoa maoni yake juu ya jambo fulani haijalishi maoni hayo yako vipi, ila Kuna maoni mengine ukitoa yanakupaka mavi kiasi Kwamba hata ukioga vipi Bado utaendelea kunuka tu.

Ninachomaanisha ni kwamba Kwa Uzi ule hata uongee jambo Gani jema Bado watu kama Mimi nitaendelea kukuona ni mtu WA ajabu sana na haustahili kutiliwa maanani kwenye jambo lolote la maana.

Kitendo tu Cha wewe kusema eti serikali ipandishe nauli ya SGR hili watanzania wengi washindwe kusafiri na SGR na hatimae warudi kutumia usafiri wa mabasi kilionesha ni jinsi Gani ulivyokuwa mbinafsi,roho mbaya sana, muhujumu na hauna mawazo shindani ya kibiashara ambayo ni chanya Kwa jamii na taifa letu Kwa ujumla.

Wewe ni aina ya wale watu ambao mnapenda serikali iendelee kutoa huduma mbovu za umaa hili nyie mtake advantage ya kufanya biashara, na endapo serikali iliboresha huduma zake na kuwa sawa na zinazotolewa na nyie watu binafsi, basi mnachofikiria ni kuikwamisha serikali na sio kuboresha huduma zetu ziwe maradufu hili watu waendelee kutumia huduma zetu.

Ndio maana nasema wewe hauna maarifa yoyote ya kibiashara ya kumpa mtu, maana ungekuwa nayo ungekuja na mawazo mazuri zaidi yenye mvuto hata kwenye ule Uzi wako WA kutaka serikali ipandishe nauli ya SGR.

Wewe labda ufundishe watu fitina za kibiashara na Wala sio njia Bora za wao kufanikiwa kibiashara.
 
Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri bwana Muhimbu.

Hoja zako nimezisoma kwa kina na nimezichambua nimegundua jambo ambalo pengine umeshindwa kulichakata na kuling'amua mapema.

Bwana Muhimbu serikali yetu pendwa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania haingozwi na mawazo ya mtu binafsi. Zinapo tolewa hoja mbalimbali na watu mbalimbali haimaanishi kwamba zinachukuliwa bila kuchambuliwa na kuchujwa. Kuna jopo la wataalam mbalimbali ambao hukaa chini na kuchambua mawazo yote yanayo fikishwa mezani kisha huchujwa kwa kinaa, na kama yakifaa ndipo huchukuliwa kwaajili ya utekelezaji.

Hivyo bwana Muhimbu ondoa shaka juu ya mawazo yanayo tolewa na wadau mbalimbali hapa jamii forums. Hayo ni mawazo tu sio utekelezaji.

Zaidi bwana Muhimbu nazidi kukushukuru kwa mawazo yako mazuri unayo endelea kuyatoa hapa jukwaani hicho ndicho kipimo cha ukomavu wa kiakili

Asante sana na karibu kwa mawazo mengine.
 
Back
Top Bottom