Jinsi Ambavyo Ningefanya Baada ya Kuishika Milioni 100 za haraka

Jinsi Ambavyo Ningefanya Baada ya Kuishika Milioni 100 za haraka

Mleta mada, fafanua zaidi hapo kwenye NICOL.

Pia, kati ya Hisa za CRDB na UTT, ipi ni option nzuri zaidi?
 
Mleta mada, fafanua zaidi hapo kwenye NICOL.

Pia, kati ya Hisa za CRDB na UTT, ipi ni option nzuri zaidi?
NICOL au (National Investments Company Limited)
Ni kampuni ya uwekezaji ambayo imeonyesha ukuaji mzuri wa thamani ya hisa kwa miaka ya hivi karibuni.

Mfano, kati ya mwaka 2022 hadi 2024, bei ya hisa za NICOL iliongezeka mara mbili, kutoka shilingi 380 hadi 810 (Julai/Agosti 2024).

Ukuaji huu unatokana na uwekezaji wake wa kimkakati kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mabenki na kampuni nyingine zenye msingi thabiti. NICOL pia inalipa gawio la kila mwaka, jambo linalovutia wawekezaji wa muda mrefu.

Uwekezaji kwenye NICOL ni mzuri kwa wale wanaotafuta ukuaji wa thamani ya mtaji kwa muda mrefu. Lakini ni muhimu kutambua kuwa soko la hisa lina mabadiliko, hivyo unapaswa kuwa tayari kuvumilia changamoto za muda mfupi ili kufikia faida za muda mrefu.

Hisa za CRDB
CRDB ni benki imara na moja ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini Tanzania. Hisa zake zimekuwa na rekodi nzuri ya ukuaji wa thamani na hutoa gawio linalovutia kwa wawekezaji.

Lakini kama hisa zingine, bei zake zinaweza kushuka au kupanda kulingana na hali ya soko, hivyo zinafaa kwa wawekezaji wa muda mrefu wanaoweza kuvumilia mabadiliko ya bei.

UTT AMIS
UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaotoa usalama wa mtaji na mapato thabiti ya kila mwaka kupitia gawio. Haufanyi kazi kama hisa, bali kama mfuko wa uwekezaji wenye hatari ndogo.

Faida zake ni za wastani na haziwezi kufikia ukuaji mkubwa wa mtaji kama hisa za CRDB au NICOL.

Uwekeze wapi?
Sasa basi, kama unalenga ukuaji wa mtaji wa muda mrefu na unaweza kuvumilia mabadiliko ya bei ya soko, basi hisa za CRDB au hata NICOL zinafaa zaidi.

Kama unahitaji usalama wa mtaji na mapato ya uhakika ya kila mwaka, basi UTT AMIS ni chaguo bora.
 
Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri bwana Muhimbu.

Hoja zako nimezisoma kwa kina na nimezichambua nimegundua jambo ambalo pengine umeshindwa kulichakata na kuling'amua mapema.

Bwana Muhimbu serikali yetu pendwa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania haingozwi na mawazo ya mtu binafsi. Zinapo tolewa hoja mbalimbali na watu mbalimbali haimaanishi kwamba zinachukuliwa bila kuchambuliwa na kuchujwa. Kuna jopo la wataalam mbalimbali ambao hukaa chini na kuchambua mawazo yote yanayo fikishwa mezani kisha huchujwa kwa kinaa, na kama yakifaa ndipo huchukuliwa kwaajili ya utekelezaji.

Hivyo bwana Muhimbu ondoa shaka juu ya mawazo yanayo tolewa na wadau mbalimbali hapa jamii forums. Hayo ni mawazo tu sio utekelezaji.

Zaidi bwana Muhimbu nazidi kukushukuru kwa mawazo yako mazuri unayo endelea kuyatoa hapa jukwaani hicho ndicho kipimo cha ukomavu wa kiakili

Asante sana na karibu kwa mawazo mengine.
Kwa hiyo kuwaambia serikali kwamba wapandishe nauli ya SGR kwa kiasi ambacho wanainchi wengi watashindwa ku-afford wewe unaona yalikuwa ni mawazo sahihi?

Kwanini usingependekeza kwamba serikali itafute namna ya kufanya subsidization Kwenye biashara ya usafiri wa mabasi halafu wakati huo nyie wamiliki wa mabasi mnashusha nauli kama competitive strategy ya kufanya biashara yenu iendelee kishamiri?

Halafu Bado unakomaa tu eti yalikuwa ni maoni yako, wewe akili huna kabisa.
 
NICOL au (National Investments Company Limited)
Ni kampuni ya uwekezaji ambayo imeonyesha ukuaji mzuri wa thamani ya hisa kwa miaka ya hivi karibuni.

Mfano, kati ya mwaka 2022 hadi 2024, bei ya hisa za NICOL iliongezeka mara mbili, kutoka shilingi 380 hadi 810 (Julai/Agosti 2024).

Ukuaji huu unatokana na uwekezaji wake wa kimkakati kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mabenki na kampuni nyingine zenye msingi thabiti. NICOL pia inalipa gawio la kila mwaka, jambo linalovutia wawekezaji wa muda mrefu.

Uwekezaji kwenye NICOL ni mzuri kwa wale wanaotafuta ukuaji wa thamani ya mtaji kwa muda mrefu. Lakini ni muhimu kutambua kuwa soko la hisa lina mabadiliko, hivyo unapaswa kuwa tayari kuvumilia changamoto za muda mfupi ili kufikia faida za muda mrefu.

Hisa za CRDB
CRDB ni benki imara na moja ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini Tanzania. Hisa zake zimekuwa na rekodi nzuri ya ukuaji wa thamani na hutoa gawio linalovutia kwa wawekezaji.

Lakini kama hisa zingine, bei zake zinaweza kushuka au kupanda kulingana na hali ya soko, hivyo zinafaa kwa wawekezaji wa muda mrefu wanaoweza kuvumilia mabadiliko ya bei.

UTT AMIS
UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaotoa usalama wa mtaji na mapato thabiti ya kila mwaka kupitia gawio. Haufanyi kazi kama hisa, bali kama mfuko wa uwekezaji wenye hatari ndogo.

Faida zake ni za wastani na haziwezi kufikia ukuaji mkubwa wa mtaji kama hisa za CRDB au NICOL.

Uwekeze wapi?
Sasa basi, kama unalenga ukuaji wa mtaji wa muda mrefu na unaweza kuvumilia mabadiliko ya bei ya soko, basi hisa za CRDB au hata NICOL zinafaa zaidi.

Kama unahitaji usalama wa mtaji na mapato ya uhakika ya kila mwaka, basi UTT AMIS ni chaguo bora.

Shukrani mkuu. Umesomeka vyema.

Na vipi kuhusu Hati fungani za Serikali/BOT, upatikanaji wake Una ushindani sana? ama ni rahisi kwa yeyote (hata beginners) kupata?
 
Ina pendeza, ila hizo biashara hapo juu zina hitaji uwe una vuta fegi kwenye yatcht😆.

Intelligent Businessman... eneo lako mujarabu kabisa hili. Business mentality.

Hebu nawewe tupe mawaidha kwenye million 100, mtu kaipata ghafula paaa, na ni penati ya mwisho, utamshaurije ili kuizalisha?
 
Ina pendeza, ila hizo biashara hapo juu zina hitaji uwe una vuta fegi kwenye yatcht😆.
Kuwekeza kwenye Hisa sio mbaya ila kama mtu au watu wana kiwanda na wanataka watu wa kuwekeza sawa
Unaweza ukawekeza humu na kama msataafu aidha unakuwa sehemu ya team au unakula faida taratibu huku ukikimbizana na wajukuu
 
Kwa hiyo kuwaambia serikali kwamba wapandishe nauli ya SGR kwa kiasi ambacho wanainchi wengi watashindwa ku-afford wewe unaona yalikuwa ni mawazo sahihi?

Kwanini usingependekeza kwamba serikali itafute namna ya kufanya subsidization Kwenye biashara ya usafiri wa mabasi halafu wakati huo nyie wamiliki wa mabasi mnashusha nauli kama competitive strategy ya kufanya biashara yenu iendelee kishamiri?

Halafu Bado unakomaa tu eti yalikuwa ni maoni yako, wewe akili huna kabisa.
Bwana Muhimbu unaonekana una mawazo mazuri sana. Haya ndio mambo serikali yetu inapenda kuyasikia. Ukiwa na mawazo juu mradi fulani hili jukwaa lipo wazi muda wote yaandike kwa faida ya wengi.
 
Kuna wakati mtu unapata pesa za haraka alafu unashindwa kuwaza ufanye nini kwa haraka ili pesa yako isiishe bila kufanya cha maana. Wengine wanapata kutoka kwenye kiinua mgongo, mafao fulani, wengine mkopo, wengine ni mgao fulani, wengine wanagawiwa kama zawadi n.k

Kama mimi ningebahatika kuishika milioni 100 kwa haraka, ningeivunja katika vipande kwa umakini mkubwa sana, nikihakikisha kila senti inatumika ipasavyo🤣:

1. Milioni 30 ningewekeza katika soko la hisa hususan hisa ya CRDB. Ingekuwa imekuja hii hela 2022 basi hela yote ningetupia NICOL na 2024 ningekuwa nimetengeneza milioni 200 (maana kwa miaka 2 NICOL ilikua mara 2 yake toka bei ya hisa 380 hadi 810 Julai/Agosti).

2. Milioni 30 nyingine ningetupia hatifungani za miaka 25 na kisha gawio lake lote lingekuwa linaelekea UTT AMIS.

3. Milioni 10 ningeacha katika akiba dharura na nayo ingekuwa katika mfuko wa Ukwasi inayoendelea kukua mdogo mdogo.

4. Milioni 10 nyingine ningeiweka katika biashara kuendeleza kukuza biashara kidogo kidogo.

5. Milioni 10 nyingine ningeweka katika ununuzi wa vito kama sehemu ya akiba.

6. Milioni 5 ningeweka katika akiba ya uwekezaji binafsi katika maarifa kwa miaka 2 juu ya uwekezaji na biashara.

7. Milioni 3 inayobakia iendelee kuwa sehemu ya ustawi wa kijamii.

8. Milioni 2 kwa ajili ya kupata nafasi ya kusafiri nchini kutafuta fursa za kibiashara.

Ningefanya hayo

Lakini pia wanaopenda mambo ya biashara tuna vitabu viwili tumeviandika vinaweza kukusaidia sanasana. Kitabu cha kwanza ni kwa wale wanaopenda kuchukua bidhaa kariakoo kitabu kimewarahisishia ili waweze kufika kiurahisi kwa wauzaji wa jumla. Na kitabu cha pili ni kwa ndugu zetu wanaopenda kujenga na kufungua vituo vya mfuta vijijini na mjini. Kimewaongoza hatua zote za kufanya.

View attachment 3199439

View attachment 3199440
Unataka kujifunza biashara na unahitaji hivyo vitabu karibu Whatsapp: 0612607426
Mkuu hii mbona umekopi linkedin kwa Dk.Raymond mgeni?

Credit him kwanza
 
Back
Top Bottom