Jinsi Ambavyo Ningefanya Baada ya Kuishika Milioni 100 za haraka

Mleta mada, fafanua zaidi hapo kwenye NICOL.

Pia, kati ya Hisa za CRDB na UTT, ipi ni option nzuri zaidi?
 
Mleta mada, fafanua zaidi hapo kwenye NICOL.

Pia, kati ya Hisa za CRDB na UTT, ipi ni option nzuri zaidi?
NICOL au (National Investments Company Limited)
Ni kampuni ya uwekezaji ambayo imeonyesha ukuaji mzuri wa thamani ya hisa kwa miaka ya hivi karibuni.

Mfano, kati ya mwaka 2022 hadi 2024, bei ya hisa za NICOL iliongezeka mara mbili, kutoka shilingi 380 hadi 810 (Julai/Agosti 2024).

Ukuaji huu unatokana na uwekezaji wake wa kimkakati kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mabenki na kampuni nyingine zenye msingi thabiti. NICOL pia inalipa gawio la kila mwaka, jambo linalovutia wawekezaji wa muda mrefu.

Uwekezaji kwenye NICOL ni mzuri kwa wale wanaotafuta ukuaji wa thamani ya mtaji kwa muda mrefu. Lakini ni muhimu kutambua kuwa soko la hisa lina mabadiliko, hivyo unapaswa kuwa tayari kuvumilia changamoto za muda mfupi ili kufikia faida za muda mrefu.

Hisa za CRDB
CRDB ni benki imara na moja ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini Tanzania. Hisa zake zimekuwa na rekodi nzuri ya ukuaji wa thamani na hutoa gawio linalovutia kwa wawekezaji.

Lakini kama hisa zingine, bei zake zinaweza kushuka au kupanda kulingana na hali ya soko, hivyo zinafaa kwa wawekezaji wa muda mrefu wanaoweza kuvumilia mabadiliko ya bei.

UTT AMIS
UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaotoa usalama wa mtaji na mapato thabiti ya kila mwaka kupitia gawio. Haufanyi kazi kama hisa, bali kama mfuko wa uwekezaji wenye hatari ndogo.

Faida zake ni za wastani na haziwezi kufikia ukuaji mkubwa wa mtaji kama hisa za CRDB au NICOL.

Uwekeze wapi?
Sasa basi, kama unalenga ukuaji wa mtaji wa muda mrefu na unaweza kuvumilia mabadiliko ya bei ya soko, basi hisa za CRDB au hata NICOL zinafaa zaidi.

Kama unahitaji usalama wa mtaji na mapato ya uhakika ya kila mwaka, basi UTT AMIS ni chaguo bora.
 
Kwa hiyo kuwaambia serikali kwamba wapandishe nauli ya SGR kwa kiasi ambacho wanainchi wengi watashindwa ku-afford wewe unaona yalikuwa ni mawazo sahihi?

Kwanini usingependekeza kwamba serikali itafute namna ya kufanya subsidization Kwenye biashara ya usafiri wa mabasi halafu wakati huo nyie wamiliki wa mabasi mnashusha nauli kama competitive strategy ya kufanya biashara yenu iendelee kishamiri?

Halafu Bado unakomaa tu eti yalikuwa ni maoni yako, wewe akili huna kabisa.
 

Shukrani mkuu. Umesomeka vyema.

Na vipi kuhusu Hati fungani za Serikali/BOT, upatikanaji wake Una ushindani sana? ama ni rahisi kwa yeyote (hata beginners) kupata?
 
Ina pendeza, ila hizo biashara hapo juu zina hitaji uwe una vuta fegi kwenye yatcht😆.

Intelligent Businessman... eneo lako mujarabu kabisa hili. Business mentality.

Hebu nawewe tupe mawaidha kwenye million 100, mtu kaipata ghafula paaa, na ni penati ya mwisho, utamshaurije ili kuizalisha?
 
Ina pendeza, ila hizo biashara hapo juu zina hitaji uwe una vuta fegi kwenye yatcht😆.
Kuwekeza kwenye Hisa sio mbaya ila kama mtu au watu wana kiwanda na wanataka watu wa kuwekeza sawa
Unaweza ukawekeza humu na kama msataafu aidha unakuwa sehemu ya team au unakula faida taratibu huku ukikimbizana na wajukuu
 
Bwana Muhimbu unaonekana una mawazo mazuri sana. Haya ndio mambo serikali yetu inapenda kuyasikia. Ukiwa na mawazo juu mradi fulani hili jukwaa lipo wazi muda wote yaandike kwa faida ya wengi.
 
Mkuu hii mbona umekopi linkedin kwa Dk.Raymond mgeni?

Credit him kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…