Jinsi awamu ya 5 ilivyoua ajira za Vijana wazawa

Jinsi awamu ya 5 ilivyoua ajira za Vijana wazawa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Utawala wa awamu ile uliamini kwenye Umasikini, Shida na Mateso . Kwamba umasikini ni baraka .

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania 2015 , alikuwa akihutubia kwao Chato na alizungumzia ufaulu wa Darasa la 7 baada ya wanafunzi wengi kufeli kwenye shule aliyosoma , aliwalaumu wazazi kwa kuwalea watoto wao kimayaimayai , aliendelea kusema kwamba enzi zao walitembea umbali mrefu kwenda shule kwa miguu ( TZ 11 ) na walishinda njaa lakini walifaulu , yaani kiongozi anaamini dhiki italeta ufaulu! Hakika haya yalikuwa mawazo duni sana .

Uongozi wa awamu hii uliamini kwamba matajiri ni maadui na ni wezi , na kwamba hela zao hazikuwa za halali, kwamba huwezi kuwa na hela bila kuiba, Bilionea Mbowe na Club yake ya Bilicanas wakashughulikiwa na kufilisiwa , serikali ikapora hadi Spika na waya za club hiyo , kwenye uharamia huu Jiwe alishirikiana kikamilifu na Nehemia Mchechu, Yusuph Manji na matajiri wengine kadhaa wakadhibitiwa na kusingiziwa kila uchafu , hela zao zikaporwa .

Matokeo yake ajira zikafa , na ufadhili kwenye kila sekta hadi kwenye michezo zikayeyuka , Panya Road wakaibuka.

FB_IMG_1698682350017.jpg
 
Mimi naamini bado matajiri ni maadui. Hebu fikiria mtu mmoja anaagiza matairi nje alafu anayauza hapa nchini yeye na familia yake ambapo kiwanda kinachoajiri zaidi ya watu 2000 kinaachwa kife. Hivi viwanda vya aina hii vikiwa vinne nchini watu wangapi watapata ajira?

Viwanda kama Tanganyika Packers, Urafiki, UFI, Mwatex, Mutex, Morogoro shoes tena kule morogoro viwanda kibao hivi vyote serikali iliwekeza jee hakuna mtu mwenye mawazo ya kuvifufua? Nchi yetu iligeuka nchi ya wachuuzi tu yaani kwenda Dubai, China, Singapore , Thailand na kuleta mitumba toka nje!

Hapo hakuna maendeleo. Nchi yetu ni kubwa population ni kubwa hatuna shida ya soko. Matajiri wa mabasi na malori sasa hivi wanashugulikia SGR isifanye kazi hata Morogoro tu haijafika.

Ufadhili wa michezo waliofadhili wameambiwa tena hadhalani kwamba wasisumbuliwe na TRA maana yake mizigo yao wanayoingiza nchini hawalipi kodi..
 
Mimi naamini bado matajiri ni maadui. Hebu fikiria mtu mmoja anaagiza matairi nje alafu anayauza hapa nchini yeye na familia yake ambapo kiwanda kinachoajiri zaidi ya watu 2000 kinaachwa kife...
Huo ni uzembe wa serikali yako
 
Unataka kujenga Uhasama kati ya Serikali na Wananchi wake?

Huo Uharamia ulioubandika huko juu umeshindwa kuuwekea -Ushahidi na Vielelezo-yaani ni Kalas. ni siasa taka. Badilikeni, wananchi wanahitaji kujua mtakacho weka mezani.

Jibuni hoja za Makonda na sio kuleta hizi Siasa chafu za Uhasama, Nongwa na Kufukuzana na makaburi.

CHADEMA mmekosa Hoja na Dira.

Badilikeni
 
Utawala wa awamu ile uliamini kwenye Umasikini , Shida na Mateso .

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania 2015 , alikuwa akihutubia kwao Chato na alizungumzia ufaulu wa Darasa la 7 , aliwalaumu wazazi wanaowalea...
Kumbe unaamini kuna awamu bora chini ya utawala wa ccm!
 
Utawala wa awamu ile uliamini kwenye Umasikini , Shida na Mateso .

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania 2015 , alikuwa akihutubia kwao Chato na alizungumzia ufaulu wa Darasa la 7 , aliwalaumu wazazi wanaowalea watoto wao kimayaimayai...
Ndo maana kwa sasa Mama amerekebisha anaupiga mwingi. Hakuna tena kama yeye mpaka 2035. Mambo mazuri kwa sasa.
 
Unataka kujenga Uhasama kati ya Serikali na Wananchi wake?


Huo Uharamia ulioubandika huko juu umeshindwa kuuwekea -Ushahidi na Vielelezo-yaani ni Kalas. ni siasa taka. Badilikeni, wananchi wanahitaji kujua mtakacho weka mezani.

Jibuni hoja za Makonda na sio kuleta hizi Siasa chafu za Uhasama, Nongwa na Kufukuzana na makaburi.

CHADEMA mmekosa Hoja na Dira.

Badilikeni
Bila shaka hujui kusoma
 
Porojo tupu !
Kwaiyo sasa hivi ndiyo tatizo la Ajira ndiyo limekwisha?

Watanzania hawana ajira za uhakika tangu awamu ya pili ya Utawala wa CCM leo unamnanga Marehemu aliyeamasisha Uchumi wa viwanda Ili tuondokane na Uchumi wa uchuuzi wa K/Koo wa kuuza bidhaa feki za Mchina!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna formula ya kuendeleza uchumi kwa kuwakandamiza wenye mitaji. Magufuli alikosea sana..

Na laiti kama angekuwa anakubali kushauriwa na kushaurika angekuwa kiongozi bora wa mfano kuwahi kutokea.

Ninachoamini hii nchi mtu akiwa kiongozi anakuwa anazungukwa na smart brain na atapata ushauri wote mzuri anaoutaka, shida itaanza kama kiongozi akiwa na ego na kukataa ushauri, hicho ndo kilimponza Magufuli... Kuona kwamba alikuwa anajua kila kitu lilikuwa ni kosa kubwa sana
 
Kwaiyo sasa hivi ndiyo tatizo la Ajira ndiyo limekwisha?
Watanzania hawana ajira za uhakika tangu awamu ya pili ya Utawala wa CCM leo unamnanga Marehemu aliyeamasisha Uchumi wa viwanda Ili tuondokane na Uchumi wa uchuuzi wa K/Koo wa kuuza bidhaa feki za Mchina!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Cherehani 4 haziwezi kuwa kiwanda
 
Mimi naamini bado matajiri ni maadui. Hebu fikiria mtu mmoja anaagiza matairi nje alafu anayauza hapa nchini yeye na familia yake ambapo kiwanda kinachoajiri zaidi ya watu 2000...
Fanya bidii na wewe utakuwa kama hao unaosema matajiri, matajiri wanawaona nyie ni wajinga fursa zipo kazi kulialia
 
Back
Top Bottom