Jinsi awamu ya 5 ilivyoua ajira za Vijana wazawa

Jinsi awamu ya 5 ilivyoua ajira za Vijana wazawa

Hakuna formula ya kuendeleza uchumi kwa kuwakandamiza wenye mitaji. Magufuli alikosea sana..

Na laiti kama angekuwa anakubali kushauriwa na kushaurika angekuwa kiongozi bora wa mfano kuwahi kutokea.

Ninachoamini hii nchi mtu akiwa kiongozi anakuwa anazungukwa na smart brain na atapata ushauri wote mzuri anaoutaka, shida itaanza kama kiongozi akiwa na ego na kukataa ushauri, hicho ndo kilimponza Magufuli... Kuona kwamba alikuwa anajua kila kitu lilikuwa ni kosa kubwa sana
Nyie mnazo sababu zenu binfsi zinazowafanya muwe na chuki,chuki hazijengi na hupofusha fikra na kuotesha kutu kwenye akili.uwezo wa kupambanua ukweli na uongo hupotea.nyie mnachuki binafsi na awamu ya tano.
 
Hao matajiri wa Tanzania ambao hawakupata utajiri kutokana na rushwa na wizi wa mali ya umma tutajie hapa
 
Utawala wa awamu ile uliamini kwenye Umasikini, Shida na Mateso . Kwamba umasikini ni baraka .

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania 2015 , alikuwa akihutubia kwao Chato na alizungumzia ufaulu wa Darasa la 7 baada ya wanafunzi wengi kufeli kwenye shule aliyosoma , aliwalaumu wazazi kwa kuwalea watoto wao kimayaimayai , aliendelea kusema kwamba enzi zao walitembea umbali mrefu kwenda shule kwa miguu ( TZ 11 ) na walishinda njaa lakini walifaulu , yaani kiongozi anaamini dhiki italeta ufaulu! Hakika haya yalikuwa mawazo duni sana .

Uongozi wa awamu hii uliamini kwamba matajiri ni maadui na ni wezi , na kwamba hela zao hazikuwa za halali, kwamba huwezi kuwa na hela bila kuiba, Bilionea Mbowe na Club yake ya Bilicanas wakashughulikiwa na kufilisiwa , serikali ikapora hadi Spika na waya za club hiyo , kwenye uharamia huu Jiwe alishirikiana kikamilifu na Nehemia Mchechu, Yusuph Manji na matajiri wengine kadhaa wakadhibitiwa na kusingiziwa kila uchafu , hela zao zikaporwa .

Matokeo yake ajira zikafa , na ufadhili kwenye kila sekta hadi kwenye michezo zikayeyuka , Panya Road wakaibuka.

Msaidizi wa Tundu Lisu amekatwa mapanga
 
Mimi naamini bado matajiri ni maadui. Hebu fikiria mtu mmoja anaagiza matairi nje alafu anayauza hapa nchini yeye na familia yake ambapo kiwanda kinachoajiri zaidi ya watu 2000 kinaachwa kife. Hivi viwanda vya aina hii vikiwa vinne nchini watu wangapi watapata ajira?

Viwanda kama Tanganyika Packers, Urafiki, UFI, Mwatex, Mutex, Morogoro shoes tena kule morogoro viwanda kibao hivi vyote serikali iliwekeza jee hakuna mtu mwenye mawazo ya kuvifufua? Nchi yetu iligeuka nchi ya wachuuzi tu yaani kwenda Dubai, China, Singapore , Thailand na kuleta mitumba toka nje!

Hapo hakuna maendeleo. Nchi yetu ni kubwa population ni kubwa hatuna shida ya soko. Matajiri wa mabasi na malori sasa hivi wanashugulikia SGR isifanye kazi hata Morogoro tu haijafika.

Ufadhili wa michezo waliofadhili wameambiwa tena hadhalani kwamba wasisumbuliwe na TRA maana yake mizigo yao wanayoingiza nchini hawalipi kodi..
Mawazo kama haya ndio yanafanya taifa hili lizidi kuwa masikini. Kiwanda ulichotolea mfano hakikuuawa na matajiri uliowazungumzia, na kingekuwa kinamilikiwa na hao matajiri hakingekufa. Hatuwezi kurudi nyuma mahali ambapo tulishaangukia serikali ilipokuwa inaendesha biashara na uzalishaji mali. Serikali inapaswa kuacha (na kuwezesha) sekta binafsi ifanye biashara na uzalishaji. Kazi ya serikali ibaki kutunga na kusimamia sera wezeshi, kukusanya kodi kikamilifu, kutoa huduma ikiwepo ulinzi na usalama na kujenga miundombinu mbalimbali.
Mpaka hapa tulipofika wakubeba lawama ni nani? Ni ccm ambao hawataki tuwe na katiba mpya itakayowathibiti wanasiasa wake ambao ndio waliuwa mashirika na viwanda vya umma, hawawajibiki ipasavyo kwenye ukusanyaji kodi bali wanasaidia wafanya biashara kukwepa kodi. Wanasiasa wa ccm ndio walarushwa wakubwa nchi hii. Mwingine alifanya ujuha kujaribu kumfilisi mwanasiasa wa upinzani kwa kuvuruga biashara zake, hata kuharibu miundombinu ya shamba lake. Kama alikuwa na hatia yoyote kwanini njia za kimahakama hazikutumika kumshughulikia? Nani alikuwa biashara ya mbaazi? Nani alivuruga soko la korosho? Nani aliuwa mashamba ya maua? Ajira ngapi zilipotea hapo? Badala ya kukusanya kodi, unafilisi walipa kodi eti huko nyuma walikwepa kodi. Maofisa wa serikali ambao waliwashawishi wafayabiashara kukwepa ili wapate rushwa mbona hawakuchukuliwa hatua? Then baada ya kumfilisi mlipa kodi utapata wapi kodi? No wonder hakuna mzunguko wa pesa mtaani- haya ni matokeo ya sera za ccm na yule 'shujaa' wao.
Suluhisho? Tupate KATIBA mpya itakayo wathibiti hawa wanasiasa na watumishi wa umma ambao ndio wezi wakubwa wa rasilimali za nchi hii. Na mambo mengine ya kijinga kama kinga ya mtu kutoshtakiwa na kuwajibishwa kwa makosa aliyotenda akiwa madarakani tuyafutilie mbali.
 
Wewe huwa ni mtu mwenye fikra mbirikimo na akili zenye matege,haujawahi kupumzika juu ya awamu ya tano,kila mada una andika ni awamu ya tano,unaviza akili yako kwa kuruhusu chuki iutawale moyo na akili zako,utaendelea kuteseka sana kwa ajiri ya huo upumbavu wako.
Basi nikajua unapinga
 
Mwezi wa Mungu ndio unaishia hivyo , Tuendelee au tusiendelee ?
 
Wapinzani ni mzigo kwa Taifa hili maana hawatambui wanatakiwa kusimami mambo gani.

Ni wahuni tu wamejazana huko kula ruzuku za bure bure kwa kuwapa matumaini hewa wananchi.

Siwaamini hata chembe.
 
Mbowe kama Mbowe binafsi hajawahi kuwa na mali zake.

Mpaka hivi tunavyoandika Mbowe anatembea chini ya kivuli cha mali za Urithi pekee!
Kama ni mali anayomiliki kama yake basi ni hii nyumba aliyojenga kupitia Ruzuku ya serikali kwenda Chadema.
Na ieleweke hivyo.
 
Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Mama huyu hapa...fursa kibao na uhuru umetamalaki.
 
Ukiachilia michango hii,

  • Fedha za join ze chain zilipatikana bei gani na ziko wapi?
  • Ruzuku ya Tsh. 2.7/- Mbowe umekula na nani? Hii fedha mtakuja kusema hapa kama sio hisani ni haki yenu, lakini mkumbuke kwamba baada ya uchaguzi mkuu 2020 mkatamka wazi kwamba, hamtochukua ruzuku kwani kufanya hivyo ni kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu 2020, ila 2023 mmefanya hivyo na mmekaa kimya..

- Fedha za matibabu ya Prof. J hamkuwahi kusema mlipata bei gani na hata siku moja hatukuona mkitoa msaada kwa mgonjwa huyo!
Fedha za Michango ya wahanga wa Mafuriko kule HANANG mtaziwakilisha na kuzikabidhi lini kwa wahanga?
Je!inakuwaje mnatumia RUZUKU kulipana posho za kujikimu kwenye Maandamano ambayo kimsingi ni ya Hiari?

Inakuwaje mwenyekiti wa Chadema ambacho kinajinasibu kuwa mtetezi wa watanzani, ana wadhurumu waandishi wa habari wa "Tanzania Daima" Gazeti ambalo ndio hasa lolikuwa msingi wa Propaganda za Chadema na kusaifia kwa kiasi kikubwa kuipaisha Chadema had kufikia hapo ilipo?

Je tukisema kwamba Mbowe hafai kuwa kiongozi wa kariba ya uongozianaojinasibu kuwa nao mtatuona wabaya?

Maswali hayo hapo juu ukiwa ndani ya chadema kama utayauliza, utakuwa au naweza kuwa ume sign your death warranty!
 
Back
Top Bottom