Jinsi Baraza la Mitihani la Taifa 'NECTA' linavyotudhalilisha na kutuacha uchi Watanzania

Jinsi Baraza la Mitihani la Taifa 'NECTA' linavyotudhalilisha na kutuacha uchi Watanzania

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Wadau kikawaida kila mtu ana haki ya usiri wa taarifa zake na mambo yake, hakuna mtu au taasisi yoyote inayoruhusiwa kuingilia haki hio na kuivunja haki hio.

Hii imekuwa tofauti kwa baraza la mitihani ya taifa NECTA, ambalo kwa makusudi kabisa na kwa kujua kuwa haki ya faraja ya wasomi waliopitia katika mikono yake inavunjwa, baraza hili mpaka leo bado limeacha taarifa za Watanzania hadharani.

Ukigombana na mtu, itakulazimu kumjua jina lake lote hata kwa kuangalia tu kwenye huduma za simu, then utamgoogle kwa ilo jina na miongoni mwa taarifa utakazoziona ni matokeo yake ya kidato cha nne au cha sita, kitakachofuata ni kumrudia huyo mtu na kumkshifu sana "hata kwambia nini kwanza form four alikula zero".

Matokeo ya watahiniwa waliomaliza miaka ya 2013 kushuka chini kwa ngazi zote za form four na form six bado yapo Google yamejaa tele, kwa majina yote, sasa hii ni kinyume na haki ya faragha za watu, ajabu yake watu wa NECTA wapo tu wala hawaoni kama hii ni kasoro.

Je wamedhalilika wangapi? Wangapi bado wanaendelea kudhalilika? Mpaka lini? Imefikia hatua mpaka wakwe na mashemeji wanajua kabisa muoaji aliwahi kupata zero form four na dunia nzima uvunjwaji huu mkubwa wa haki ya faragha uko Tanzania tu chini ya kivuli cha NECTA.
 
666 chata, Hili nilishawahi kulifikiria. Ni uvunjaji wa faragha za mtu binafsi.

Kimsingi inavunja spirit ya ibara ya 16 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
 
wee unadhani vi mitihani vya siku moja ndio vinaweza kupima akili za mtu kwa maisha yake yote yaliobakia?
Inaonekana wewe ni muhanga, ndiyo maana unalaani na kujipa moyo vyote viwili kwa wakati mmoja.
 
Mh!! Hichi unachokiongelea mbona nimejaribu kimeshindikana mkuu? Nimejaribu kuangakia ya kwangu mimi kwa kutumia jina langu na bado sijayaona
 
Nakuunga mkono kwa hoja yenye msingi.NECTA wanavunja haki ya faragha ya mtainiwa.

Wenyewe NECTA hawakubali mtahiniwa apate nafasi ya kupitia karatasi ya majibu ya mtihani aliofanya akilalamika kuwa matokeo haridhishwi nayo. Wanalinda faragha yao.

Muda umefika NECTA kulinda faragha ya mtahiniwa. 666 chata,
 
We Mbona unawananga sana madreva wenzako wamepewa lesen na wajomba
 
Ofisi yetu ya Kata mpaka ninapoandika muda huu bado hawajabandua Matokeo ya uchaguzi uliopita 2015, Udiwani, Ubunge na Urais.
 
666 chata,
Ngoja nikaangalie jina langu.

Ila wacha yaendelee kuwepo hadharani, wakitoa nyie wajomba mtajuaje kama shule yangu ilikuwa ya kwanza kitaifa miaka hiyo?
 
Tanzania iachane na mfumo wa Ranking na kutangaza Wanafunzi bora. Huu mfumo husababisha watu na shule kuiba mitihani ili wapate wanafunzi Wengi. Ikitungwa sheria ya kutojitangaza itasaidia shule zifundishe vizuri
 
Dawa ya kupata zero NECTA ni kupata DIV 1 kwenye life otherwise utaprove wewe ni kilaza wa muda wote.
 
Inaonekana wewe ni muhanga, ndiyo maana unalaani na kujipa moyo vyote viwili kwa wakati mmoja.
binafsi sijawai kufeli kitu chochote kinachoitwa mtihani, generally, elimu niliyo nayo leo uenda hata Chief Executive wa Necta hana.
 
Wanazalilishwa wapi? Sindo matokeo waliyopata? Mimi nawapongeza maana madoctor walizidi kuwa wengi mno, ukiwa mbunge au napesa watu walitafta cheti , eti kasomea nje! Nacte safi sana
 
binafsi sijawai kufeli kitu chochote kinachoitwa mtihani, generally, elimu niliyo nayo leo uenda hata Chief Executive wa Necta hana.
Hata Kiswahili sanifu unashindwa kuandika. Labda uwe na elimu ya kukariri Korani. Kwa taarifa, Marekani unaweza kwenda kwenye tovuti za mahakama au jela/magereza uka search jina la mtu yoyote kama unataka kufahamu historia ya uhalifu ya mtu yoyote. Mimi naona hii ya NECTA kuweka wazi matokeo ya mitihani mtandaoni ni sawa ukizingatia utamaduni uliokithiri wa watu ku forge vyeti. Na wadaiwa sugu HESLB nao majina yao huanikwa vilevile. Unweza kukuta mtu anamiliki BMW X6 wakati bado ana deni HESLB.
 
Back
Top Bottom