666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,700
- 3,921
Wadau kikawaida kila mtu ana haki ya usiri wa taarifa zake na mambo yake, hakuna mtu au taasisi yoyote inayoruhusiwa kuingilia haki hio na kuivunja haki hio.
Hii imekuwa tofauti kwa baraza la mitihani ya taifa NECTA, ambalo kwa makusudi kabisa na kwa kujua kuwa haki ya faraja ya wasomi waliopitia katika mikono yake inavunjwa, baraza hili mpaka leo bado limeacha taarifa za Watanzania hadharani.
Ukigombana na mtu, itakulazimu kumjua jina lake lote hata kwa kuangalia tu kwenye huduma za simu, then utamgoogle kwa ilo jina na miongoni mwa taarifa utakazoziona ni matokeo yake ya kidato cha nne au cha sita, kitakachofuata ni kumrudia huyo mtu na kumkshifu sana "hata kwambia nini kwanza form four alikula zero".
Matokeo ya watahiniwa waliomaliza miaka ya 2013 kushuka chini kwa ngazi zote za form four na form six bado yapo Google yamejaa tele, kwa majina yote, sasa hii ni kinyume na haki ya faragha za watu, ajabu yake watu wa NECTA wapo tu wala hawaoni kama hii ni kasoro.
Je wamedhalilika wangapi? Wangapi bado wanaendelea kudhalilika? Mpaka lini? Imefikia hatua mpaka wakwe na mashemeji wanajua kabisa muoaji aliwahi kupata zero form four na dunia nzima uvunjwaji huu mkubwa wa haki ya faragha uko Tanzania tu chini ya kivuli cha NECTA.