Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Ndugu zangu wana Jf habari zenu.

Unajua kwenye haya maisha tunapitia mengi sana hasa katika utafutaji kwa upande wa Wanaume. Tunakutana na mambo mengi sana ya aibu, kukatishwa tamaa, kuachwa na tuwapendao na mauzauza mengi sana.

Nakumbuka mzee mmoja alinambia mapambano ya kupata maisha mazuri sio rahisi inatakiwa ujasiri, kujitoa na kuwa na maamuzi magumu sana. Kila aliyefanikiwa ana siri nyingi ambazo sio rahisi kushare na mtu mwingine, sometimes tunakutana humu jf, tuna marafiki zetu wote hapa duniani tuna matatizo lakini matatizo yetu yametofautiana.

Mimi INSIDER nimepitia mambo mengi sana kiasi kwamba nilikata tamaa ya maisha unaweza ukasoma huu uzi wangu “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu”

Sitaomba kazi tena, wacha niwe jeuri tu!!

https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/Sitaomba-kazi-tena%2C-wacha-niwe-jeuri-tu%21%21.1619876/ , na story yangu itaanzia hapa, ilikuaje mpaka nikaingia kwenye biashara ya uber??.
Hii ni story ya kweli na siyo ya kutunga, lengo langu nataka ndugu zangu mpate ujumbe kuhusu haya maisha. Kiufupi usikubali kukata tamaa hata kidogo, no matter what you fall, keep fighting, God has plans for all of us. Kwa wale ndugu zangu wa Uber/Bolt ambao mnataka kuingia kwenye hii biashara utaweza kupata mwanga mzuri kuhusu hii biashara maana nina experience ya kutosha. Tusichoshane acha nianze kumwaga asalii……..,,

…….wakati naandika ule uzi wa “ Sitaomba kazi tena wacha niwe jeuri” , nilikua nimerudi mkoani kwa wazazi kuwasalimia. Ofcourse maisha ya mkoani na niko home sikua na wasiwasi kabisa wazungu wanasema “HOME SWEET HOME””. Chuo mimi nimemaliza moja ya chuo kikubwa hapa Dsm, baada ya kumaliza chuo sikutaka kurudi home kabisa. Maana niliwaza hata nikienda home kule nitafanya nini? Nikakae na mama tu? Niwe nakula na kulala? nikakukumbuka ule msemo unaosema mtoto kwa mama hakui bali analemaa akili.
Niliamua kwenda kwa Uncle wangu kukaa huku nikiendelea kutafuta kazi hapa mjini, alikua anaishi Mikocheni. Kipindi cha weekend nilikua natoka chuo nakwenda Mikocheni nashinda kule kwa Uncle then jumatatu narudi chuo, pale palikua kama home tu.

Nikaanza kusambaza CV kwenye mataasisi, makampuni, NGO’s kwenye mabank na sehem nyingi tu hapa Dsm lakini patupu sikufanikiwa kupata sehemu hata ya kujitolea. Kuna siku nilikuwa nimekaa na Uncle tunaongea akaniuliza umemaliza chuo sasa una mpango gani?. Nikamwambia abc zote kwamba nimepeleka maombi yangu sehemu mbalimbali nasubiri majibu kama nitafanikiwa ama laah. Akanambia kuanzia jumatatu tutaanza kwenda wote kazini, lakini utaweza mikiki ya Kariakoo?, nikamwambia ni bora nishinde huko kuliko kubaki hapa home, I hate that.

Kweli jumatatu ikafika tukaenda huko kwa Wachina, ile siku sikutaka kuuliza ni kazi gani lakini nilikua najua Uncle anafanya kazi kiwanda cha mabag. Tulivyofika pale kiwandani Uncle akanitambulisha kwa Mchina.

UNCLE: Hey Mr ping that is my Uncle, My sister’s son. Call him INSIDER.

MCHINA: Ooh you look alike I thought is your son, akacheka. huyu mchina alikua hajui kiswahili hata ngeli alikua anaibia kwa mbali. Mchina akanambia hey “Rafiki” karibu.

MIMI: Thank you.

Uncle akaniita niingie store akanambia kazi yangu itakua ni kusupply mabag kule Kariakoo. Hii kampuni yeye alikua ni Sales and Operation manager. Kampuni ilikua inatengeneza journey bags na backpack bags na pilot bags. Canter ilikua imefika pale tayari kwa upakizi, so tukaanza kupakia mabag mle kwa gari na kuyapanga kuyapeleka Kariakoo kwa wateja. “Ipo hivi pale kiwandani sio kwamba ndo wanaanza kutengeneza hapana wanafanya assembling tu, material zote zinatoka China, pale ni kuassemble na kuyapeleka sokoni”.

Ile siku nilipiga sana kazi nakumbuka tulipiga trip 2 ila kila tripu ilikua na bag 200, sio poa kupakua bag pale Kariakoo ni mtihani yaani foleni za watu zilikua zinakera sana. Uncle akawa ananilipa cash kwa siku 10,000/=, wakati naanza alikua ananinulia chakula ila baadae akaanza kunikataa so nikawa najilipia, kuhusu kwenda kazini tulikuwa tunaondoka wote kwa gari asubuhi.

Nikaimasta kazi kwa muda mfupi sana ikafika stage akawa ananiacha niende peke yangu na dereva mitaa ya Kariakoo na wateja nikawa nimewajua tayari haikuwa ngumu kwangu. Uncle akanambia upo vizuri ikafika stage hata madeni nikawa nakwenda kukusanya then napeleka bank, yaani unakuta nimekusanya madeni mpaka 80million, hiki ndo kipindi nilikua nashika pesa nyingi sana.

Nilikua nimejenga urafiki na baadhi ya wafanyakazi wa pale kiwandani, siku katika kupiga story jamaa akanambia naona sikuhizi umepanda cheo unapeleka mabag mwenyewe Kariakoo. Nikamwambia nimemasta kimtindo akanambia safi inabidi mzee wako majukumu yapungue maana umri unakwenda huko Kariakoo atuachie vijana. Jamaa akaniuliza posho si unapewa ukienda kupeleka mzigo?? nikamwambia sio haba kuliko kukaa bure, akauliza kwani unalipwa kiasi gani? nikamjibu 10,000. Jamaa akasema Uncle wako anakupiga atlist angekupa hata 50,000/= nikamwuuliza kwanini?, jamaa akanambia posho ya kwenda kupeleka mabag kwa siku ni 100,000/=

Jamaa akasema mzee wako anakuonea sio haki ile kazi ni risk, “hii kazi kama jamaa anavyosema kweli ni risk sababu unaweza kuibiwa kweupe, Kariakoo si mnaijua? “Kuna siku tulikua tunapakua mabag nilikua na moja ya wafanyakzi wa pale sasa jamaa alichanganya mafile akampa bag muhuni mwingine. Ilibidi akatwe kwenye mshahara, ni hivi tukikaribia Kariakoo tunawapanga wateja mapema. Kama mnavyojua maduka ya kariakoo yako barabarani plus yale mafoleni ni kichefuchef so huwa tunapakua mabag mlemle kwenye foleni. Mhusika anakuja na vijana wake wabebaji, inatakiwa uwakariri vzr maana ukizingua tu unaweza mpa mzigo mtu mwingine.”

Jamaa baada ya kufunguka hayo pia akanambia mzee wako kila bag anapata commision kwa bag la set 3 analipwa 1,000 na set 2 analipwa 700 (Zile bag za safari, set 3 ndani zinakuwa mbili yaani ukifungua zipu za bag kubwa ndani kuna kuwa na bag 2. Na hizi set 2 ukifungua zip ndani kunakuwa na bag 1). Nikawaza hata lunch najilipia, uncle anaplay fouls sio haki. Nikakumbuka matukio mengi tu mfano sometimes nikipeleka mzigo before sijaondoka atanambia ukifika Kariakoo piga simu kwamba TRA wamekukamata risiti sio sahihi, then utasema wanataka million 2, so mchina alikua anatuma hela. Nilikua nafanya hayo yote afu atanipa 50,000 tu au asinipe kabisa, nikikusanya madeni kama na million 30 atanambia ingiza kwa account ya kampuni maybe million 27 then million 3 nampelekea. Zile ndo zilikua commission zake, Uncle wangu alikua anapiga sana hela shida alikua na madem wengi sana.

Kufupisha hii story, Mchina akaanza kunikubali sababu nilikua nampa ushauri baadhi ya mambo, akawa close sana mimi. Hiki kitendo Uncle hakupenda aliona kama nataka kumpokonya ugali wake, nikaona anaanza kunikataa mara anipe kazi ya kwenda kuangalia madogo shuleni, sababu zikawa nyingi mara biashara imekua ngumu sijui mambo yakikaa sawa ataniita. Kama msomi nikajua hapa sina changu, maana jamaa kule kazini alikua ananipa mkanda mzima kinachoendelea. Ukweli hii kazi ilikua inanisaidia sikosi hata pesa za vocha na matumizi yangu binafsi.

Nikaanza kukaa home na Aunt yangu, yeye alikua ni mama wa home tu. Hakuna kitu kigumu kama kuishi na ndugu inahitaji moyo na uvumilivu sana. Aunt yangu ni mvivu sana hata kwenye masuala ya mausafi hayuko active, nafikir ni moja ya sababu Uncle akawa na michepuko mingi. Ubaya sasa Uncle alikua anamsikiliza sana Aunt kwa lolote alilokua anasema yaani ni shida. Sasa hapa home tulikua tunabaki mimi na Aunt, madogo 2 wako boarding mmoja wa kike ndo alikua mdogo ansoma anatoka asbh anarudi jioni.

Nikaanza kuwa house boy wa mle ndani naamka Asubuhi sa12 nimpikie mtoto chai, baada ya hapo nitafanya usafi na kuosha vyombo, mchana nitapika chakula, jioni ninakazi ya kupikia mbwa chakula na kumwagilia miti na maua. Hizo kazi zote nilikua nafanya mwenyewe kila siku na nilikua nafanya kwa moyo wote. Unaweza kushangaa mwanaume nawezaje kufanya hizo kazi lakini nilifunzwa nikiwa mdogo na mama yangu mzazi pamoja na dada yangu. Ikafika stage akaanza kunipa kufua nguo za Uncle na mdogo wangu ambaye ni mtoto wa mwisho (ambaye huwa naamka asubuhi kumpikia chai), nikaona haya mazoea yamezidi sasa.

Kuna siku nilikua natoka pale home Asubuhi kwenda mjini kwaajili ya interview na kusaka fursa, wahenga wanasema fursa haikufuati nyumbani unatakiwa ukaitafute. Sasa nikiondoka pale asubuhi mara nyingi anakua amelala na uncle wangu huwa anatoka sa11 au 12. Sometimes kuepusha makazi kama hayo nilikua nakwenda mjini au kwa washikaji kupoteza muda tu. Aunt wangu akawa anampa taarifa Uncle kwamba huwa naondoka bila kuaga afu narudi usiku. Kuna siku Uncle alinikaripia sana nikamwambia Uncle navyotoka huwa anakua kalala kumwamsha sio busara, napia nikitoka sio naenda kuzurura nakwenda kutafuta kazi. Uncle akasema kama umekua mkubwa humu ndani nenda kapange ili uwe huru. Kama mwanaume niakanza kufikiri namna ya kutoka pale ikiwezekana nikapange nianze maisha yangu ya kujitegemea.

Nikapata wazo tangu nimalize chuo sijawai kwenda home mkoa kusalimia acha niende home nikasalimie wazazi wanipe na baraka. Kuna siku Aunt alinitia hasira sana, ilikua usiku inakwenda saa 2 nikatoka kwenda dukani kununua vocha niliacha simu chumbani. Kumbe wakati nimetoka Uncle alirudi akaniulizia hakunikuta ikabidi apige simu ikawa haipokelewi. Wakati nimerudi nikaona gari ipo uwanjani nikajua mzee karudi naingia ndani namkuta seblen kavimba hatari. Nikamsalimia Uncle shikamoo pole na kazi hakujibu, akaniuliza ulikuwa wapi usiku huu? Maana simu hupokei, kabla sijajibu Aunt akaropoka “huyu alikua kwa kidem chake kule bondeni taarifa zake zote ninazo kazi umalaya tu”. Nikaona hizi dharau sasa nakua kama mtoto nikamwambia Aunt mimi tayari ni mtu mzima hupaswi kunipangia mambo ya kufanya, mimi kama kijana pia nahitaji kuwa na mpenzi na haki yangu naomba uwe na mipaka, nikaenda zangu chumbani. Aunt akasema kama umekua mkubwa si uende ukapange ili uwe huru??, nikajua hapa nishachokwa sipaswi kuendelea kung’ang’ania, akufukuzaye hakwambii toka.

Huyu mwanamke ambaye Aunt alikua anasema kidem changu ndo mama junior wangu mpaka sasa. Ni mke wangu japo sijafunga ndoa ila taratibu zote nimekamilisha kama kulipa mahari, bado ndoa ya kanisani tu. Niseme tumetoka mbali sana from Nothing to something, ni mwanamke anayenipenda sana na kunijari anasifa zote za kuitwa mke. Namshukuru Mungu kwa kuniletea huyu mwanamke kwenye maisha ni moja ya mtu ambaye ameplay part kubwa kwenye mafanikio niliyonayo. Tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa tumwite Junior.

Nilikua kwenye dimbwi kubwa la mawazo sana. Wakati niko room nikawaza jumamosi acha niondoke niende home mkoa kusalimia na pia niongee na wazazi juu ya mustakabali wa future yangu. Kesho yake nikamwaga mama Junior alishtuka sana mbona ghafla? something wrong? Nikamwambia NO! nataka nikawasalimie wazazi lakini nitarudi ASAP. Mama Junior akaomba tusex ilikua ni miez 5 toka tuanze mahusiano hatujawai kukutana. Ile jioni nikaona acha niwaage na hawa akina Uncle wanaweza kufikiri vibaya, nikategea Uncle amekaa seblen nikamsalimia, then nikamwambia Uncle Jumamosi mimi nitakwenda home kusalimia then nitarudi. Uncle akashtuka mbona haraka hivyo kulikoni? nikamwambia ni muda sijakwenda huko ni vizuri kwenda kuwajulia hali wazazi. Uncle akanambia bhasi kesho uende hata Kariakoo ununue vitenge vya mama, nikamwambia kesho ambayo ni “ijumaa” nitakwenda chuo kufuatilia cheti changu hivyo sitoweza kwenda Kariakoo. “Kumbe nilikua na timetable na mama Junior”, uncle akatoa hela akanipa kuhesabu ilikua 100,000 cash.

Jumamosi kweli nikaondoka kwenda home jioni nikiwa na bashasha nikafika mkoa nikashangaa jinsi mji ulivyojengeka maana ni miaka 3 ilipita bila kukanyaga. Nikachukua bajaji mpaka home kushuka mama akaja akanikumbatia….

MAMA: waaoohh mwanangu nilikumisi sana jamani, naona umepungua sana shida nini?
MIMI: Mama maisha haya na stress za ajira nitanenepaje?
MAMA: umerudi sasa ule kwa bidii, maziwa, mayai yapo yakutosha akatabasamu, twende ndani. “Maana wakati tunaongea haya tulikua nje getini”.

Kiukweli nilivyofika home nilifarijika sana moyo wangu ulijawa na furaha sana. Bhasi ile jioni tukala dinna as family, wakati tunakula mama akaongea huyu mdogo wako anasoma science lakini hesabu hawezi zero kabisa, itabidi uangalie namna ya kumsaidia. Nikamwambia mama haina shida kesho nitakaa naye chini tuongee vizuri. Baada ya dinna nikakaa na wazee tukaongea sana kuhusu maisha, wakanitia moyo sana, tukafanya maombi tukaenda kulala.

Kipindi naandika ule uzi “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu” nilikua nimeridhika na maisha tayar sina stress niko home. Ilikua ni kucheza PlayStations na masela wa huku home full raha niko home kwa mama stress za maisha natolea wapi!?. Naamka asubuhi chai ya maziwa, mayai 2 ya kuchemsha ya chienyeji, mkate umejaa blue band. Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana.

Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.

ITAENDELEA...
Uko kwa wachina nikonektie ndugu yangu anatafuta kazi
 
Wanawake wapo complicated sana

Binafsi sijaona ulipokosea kwa hao Wanawake wote na huyo iryn umefanya vizuri kitomla mana mngesumbuana huko mbele ya safari na alivokununia ni wivu tu wa Wanawake na kwakuwa ashakupenda au usikute baada ya kuona simu aliyokupa umempa mkeo au akawa na sababu zake binafsi tu ambazo hutakiw zikuhangaishe nawewe

Kwahy akitaka kuvunja we mkubalie tu bila kinyongo kisha endelea na maisha yako huyo asitake kujipa umuhimu kwako kias cha kutaka uishi anavyotaka yeye
 
Wanawake wapo complicated sana

Binafsi sijaona ulipokosea kwa hao Wanawake wote na huyo iryn umefanya vizuri kitomla mana mngesumbuana huko mbele ya safari na alivokununia ni wivu tu wa Wanawake na kwakuwa ashakupenda au usikute baada ya kuona simu aliyokupa umempa mkeo au akawa na sababu zake binafsi tu ambazo hutakiw zikuhangaishe nawewe

Kwahy akitaka kuvunja we mkubalie tu bila kinyongo kisha endelea na maisha yako huyo asitake kujipa umuhimu kwako kias cha kutaka uishi anavyotaka yeye

Mkuu naona kama unakwenda vizuri na movie [emoji1544]
 
Ni ama Iyrn alikutwa na wivu, huu with time huisha tu na pindi alipokumiss naamini alirudisha majeshi...

Au mama Liam na Iryn waliongea mambo ambayo Iryn aliona ajiweke kando kuepusha balaa

Kingine Iryn itakua alijisikia vibaya kwamba amemwambia mambo yake mengi sana Insider wakati yeye anavitu vikubwa na vizito japo vya kawaida kama kuwa na Mke na mtoto hajamwambia. Akaona jamaa sio kama alivyomwamini na kumchukulia.

Kama nakuona ulivyoshikwa hasira jamaa alivyoitwa chumbani kwenda kupanga simu na vitu vingine wakati Mzee ulishajua maandiko yanatimia😄
 
Hii story siipendi natoa sababu.
1.unataka tujue umepiga hatua sijui unawatu wakubwa sijui wa njee yaani kuna vitu vinaonyesha unajionyesha au upo kwenye matangazo,either ya kibiashara au yakinini. Yaani haupo real kuhadithia story ya huyu demu ,jingine kwenye hii story lazima ujue hili haihiitaji utuanzie undani wa maisha yako sana ingekuwa imeisha unatoa na prove yanini siuende kwenye point ya huyo msichana na baadhi ya vitu vyako vya muhimu pale mwanzo ni sawa katikati ulipoanza kujielezea undani wa biashara basi hujanivutia tena inaboa
Acha makasiriko,anajionesha wapi sasa na mtu anahadithia stori yakw?? Umasikini mbaya sana,kila mtu anachofanya unahisi anakulingishia[emoji13]
 
EPISODE 23

Iryn alikuwa akionesha picha ambayo nilikuwa nimeipost whatsapp status nikiwa na Junior.

TUNAENDELEA….


Sikutaka mkatalia maana mimi na Junior tumefanana sana ni ngumu kukataa na pia sikutaka kukataa damu yangu. Ni dhambi kubwa sana hii ningefanya kumkana mwanangu.

Baada ya kutambua amefind out sikutaka kuendelea kuhide,

MIMI: “Yeah is my son.”

IRYN: “Why didn’t you tell me before?”.

MIMI: “Remember nilikwambia nitakusaprize, niliplan nikupeleke home sasa umeshajua mapema.”

IRYN: “Insider suala la mtoto la kunificha? Ni mambo mangapi mimi na share na wewe?

MIMI: “Iryn kumbuka nilikuahidi kukwambia siri zangu zote ilikuwa ni suala la muda tu, na nilipanga nikupeleka home kabisa ukapajue.”

IRYN: “Ni muda sana umeahidi Insider, ni mambo mangapi umeniahidi na je umeyatimiza?”

MIMI: “Sorry”

IRYN: “Mtoto yuko wapi?”

MIMI: “Yuko home”

Na muda huu Iryn aliinuka kwenye kiti kwa hasira na kuingia ndani chumbani.

Kwa upande wangu sikujua nifanyaje na pia nilijiona na hatia sana kwa kitendo cha kutomwambia hili jambo mapema, pia nilijilaumu kwa kitendo cha kupost ile picha.

Ilimchukua dakika 5 Iryn kutoka chumbani na alitoka akiwa amevaa surual ya track yenye vifungo pembeni na kishati cha kubana cha njano na mkononi alikuwa kashika card ya bank.

Na mimi nilishangaa sana kuona katoka vile akiwa amebadilika haraka sana.

IRYN: “Insider tunakwenda kwako right now.”

MIMI: “Kwangu? Now?”

IRYN: “Ndio maana yake.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

Na mimi sikuweza kumkatalia sababu Mama J alikuwa home, sikuona tatizo kwenda naye home na niliona ni jambo jema tu, Iryn alishakuwa familia tayari kwa upande wangu.

“Insider tunapitia kwanza Mlimani city maramoja.”

Tulitoka pale kwake muda ule na hatukuweza kuzungumza kabisa njiani mpaka tunafika pale Mlimani city.

Nilipark gari na tukaelekea ndani mimi nilikuwa namfuata tu anakokwenda, na tuliingia moja kwa moja mpaka Shoppers.

Iryn alianza kununua vitu pale, alinunua maziwa ya kopo makubwa, alinunua sukari, diapers, na mazaga mengi ya kutosha. Na baada ya kumaliza pale Shoppers tulikwenda moja ya duka la watoto mle ndani na alinunua nguo za Junior za kutosha mpaka viatu.

Baada ya kumaliza shopping tuliondoka maeneo yale ya Mlimani na kuelekea home sasa. Na nilikuwa nimemtumia text Mama J aweke mazingira mazuri ya mtoto pamoja na yeye, maana narudi home na mgeni.

Kwenye mambo kama haya Mama Junior hajawai niangusha kwakweli anakuwaga chap sana kuweka mazingira vizuri.

Tulifika home mapema kabisa tulishuka kwenye gari, nikamkaribisha na nikatoa vitu kwa gari.

Niligonga mlango na dada alitoka kufungua tukaingia ndani. Baada ya dakika 3 Mama J alitoka chumbani na mtoto wakasalimiana na Iryn. Na mimi bila kupoteza muda nikafanya utambulisho, maana Mama J alikuwa kama haamini anachoona machoni mwake.

“Mama Junior huyu anaitwa Iryn ni Bossy wangu na anaishi Kijitonyama.”

Baada ya kumaliza utambulisho wa Iryn nilihamia upande mwingine,

“Iryn huyu ndo Mama Junior mke wangu na huyu ndo Junior mwenyewe uliyeona picha yake na huyu ni dada yake Junior.” Na muda huu nilikuwa nikimchukua Junior kwa mama yake.

MAMA J: “Wow Ahsante kwa kukufahamu Iryn karibu sana na jisikie uko nyumbani. Dada mletee mgeni juice kwenye glass sawa?.”

IRYN: “Ahsante sana Mama Junior kwa kukufahamu, Insider alikuwa ananificha sana, bila kuona status ya Junior leo nisingekuwa hapa kabisa. Naomba nimshike Junior mme wangu mpya kwa sasa.”

“Wow Junior is so Handsome, very charming…… eti Junior tunaondoka leo wote sindio?”

Na muda huu Junior alikuwa anatabasamu tu, Junior hanaga noma kabisa tena anapenda sana wadada. Junior alionekana kumfurahia sana Iryn wakati huu.

Story ziliendelea pale kwa muda mrefu na ndani ya muda mfupi Iryn na Mama J walikuwa kama wamefahamiana muda mrefu sana.

IRYN: “Mama Junior unajishughulisha na nini?”

MAMA J: “Mimi nasoma bado dear.”

IRYN: “Unasomea nini mpenzi?”

MAMA J: “Business Administration”

IRYN: “Wow safi sana komaa mpenzi hata mimi nimesoma hiyo course.”

MAMA J: “Napambana sana kwakweli.”

Na mimi muda huu sikutaka kuendelea kukaa seblen hivyo niliamua kuondoka kwenda chumbani ili niwaachie uwanja, wawe huru kuongea.

Baada ya dakika 10 nilitoka chumbani na Mama J akaniuliza,

MAMA J: “Baba J tunatoka kweli leo? Maana nina hamu sana.”

MIMI: “Ndio tunatoka out ngoja nimpeleke mgeni afu nikirudi tunaondoka.”

IRYN: “Guys tunatoka wote out, I’m not going anywhere.”

MIMI: “Sawa haina shida, Mama J kajiandae tutoke.”

Na muda huo Mama J alikwenda chumbani na akatuacha mimi na Iryn pale seblen.

IRYN: “Insider una mtoto mzuri sana hata mama yake pia, hongera.”

MIMI: “Thank you, ila saprize ya leo sijaipenda kabisa.”

Na muda huu Iryn alicheka kwa kimbea

IRYN: “Insider bhana huoni kama mimi leo nafuraha atlist nimeonana na familia yako. Ona Junior anavyonifurahia hapa.”

MIMI: “Sawa bhana leo umeshinda bhana.”

Na muda huo Mama J alitoka na tukaondoka pale home. Na muda huo ilikuwa saa 3 kasoro za usiku. Mama J na Iryn walikuwa wamekaa seat za nyuma kwenye gari wakiendelea kuongea na hawakuwa na habari na mimi kabisa.

Niliendesha gari mpaka pale Makonde “25 Lounge” ndo nikapark gari pale nje, tuliingia ndani na tukapiga vinywaji mpaka saa 7 usiku ndo tukaondoka pale. Kuhusu Iryn nilifanya kurequest Uber ili impeleke kwake na sisi tukarudi home kulala na Mama J.

**********

Asubuhi kama kawaida niliamka mapema na niliendelea na ratiba zangu zilezile. Nilikwenda kwa Mama wa2 kumchukua maana alikuwa amemaliza likizo yake. Nilifika pale kwake asubuhi na nikampakia, Rachel mwanaye alikuwa bado anaendelea na likizo.

MIMI: “Hivi na wewe ilikuwaje ukaomba likizo March badala ya April?”

MAMA WA2: “Insider unafikiri nilipenda sema walinipangia tu.”

MIMI: “Pole hata hivyo hii likizo imekufanya kunawiri huko ofisn wanakutolea macho sana mafisi.”

MAMA WA2: “Hahahaha Insider huishiwi vituko wewe. Afu Mke wako Pili anarudi weekend hii”

MIMI: “Akirudi nambie nije nimsalimie mke wangu.”

Na muda huo tulikuwa tushafika kwa Maggy na kumpick na tuliendelea na safari ya kwenda Posta. Mama wa2 na Maggy walikuwa washazoena na njiani walikuwa wakipiga sana story.

Niliwapeleka kila mmoja kwenye ofisi yake pale Posta na mimi nikaendelea na kazi yangu ya Uber, japo biashara ilianza kuwa ngumu kiaina sababu ya kupanda kwa nauli za Uber, maana hata wese bei ilikua ishaanza kupanda kwa kasi na ilikua kwenye 2,800 kipindi kile cha April.

Hii siku pia niliongea na Muajemi kupitia telegram na alikuwa na furaha sana ya kukutana na Iryn ile weekend. Muajemi aliniomba niendelee kumshawishi Iryn waende Zanzibar na mimi nilimuhakikishia kwamba watakwenda Zanzibar.

Ukweli ni kwamba, Muajemi alikuwa tayari kashaoza kwa Iryn, maana alikuwa anamkubali sana Iryn kupita maelezo.

Nilipiga kazi mpaka saa2 usiku nikasema acha nirudi zangu home nikalale. Wakati niko njiani nilimpigia simu Prisca ili nikirudi home asisumbue, na Prisca alikuwa kashaoza kwangu maana alikuwa haelewi.

MIMI: “Prisca naomba usajili namba nyingine maana hii wife anaijua na sitaki tugombane tena, tunaelewana?”

PRISCA: “Sawa haina shida nitafanya hivyo baba watoto.”

MIMI: “Naomba Usijaribu hata kunipigia simu usiku labda nikupigie mimi, tutakuwa tunachati kwa whatsapp.”

PRISCA: “Nimekuelewa Insider”

MIMI: “Ukivunja haya makubaliano yetu mimi na wewe tunaachana na niko serious kabisa na naomba umuheshimu Mama Junior wangu.”

PRISCA: “Insider siwezi kuvunja ahadi yangu ila naomba nimjue mama Junior hata kukutana naye, please.”

MIMI: “Suala la kuonana na Mke wangu haliwezekani Prisca tafadhali sana.”

PRISCA: “Please Insider I’ll pray smary and I promise you.”

Prisca alikuwa tayari kaoza kwa Insider maana hakuna ambacho nilimwambia akanipinga, maana alikubali mwenyewe kuwa mchepuko bila kulazimishwa.

Tuliagana na Prisca na muda huu nilikuwa nishafika home tayari, nilipark gari na nikaingia ndani.

Upande mwingine tangu Iryn aje home mimi na Mama Junior tulikuwa hatujakaa chini wala kuongea lolote maana tulirudi usiku sana na tukalala, na mimi asubuhi niliamka mapema sana na niliondoka yeye akiwa bado kalala.

Nilingia ndani na seblen alikuwa dada na mtoto nikamsalimia, nikaelekea moja kwa moja chumbani na nilimkuta wife akisoma muda ule.

MIMI: “Swahiba nakuona upo busy unakula msuli.”

WIFE: “Afu Baba J yule dada mmefahamiana wapi?”

MIMI: “Kupitia kazi hii tulifahamiana.”

WIFE: “Mhhh ulisema ni Bossy wako kivipi?”

MIMI: “Tumeingia mkataba wa kazi namsaidia mambo yake kama kuchukua mizigo bandarini na kupeleka kwenye saloon zake.”

WIFE: “Aya bhana, toka uanze hii kazi sikuelewi kabisa naona mabadiliko yako taratibu. Baba J nakuomba sana ukumbuke una mke na mtoto wana kuhitaji sana, hii kazi ni ngumu sana na huwezi kukwepa mishale yote, kuwa makini shetani yuko kazini.”

MIMI: “Mke wangu naomba uwe na amani na mimi na utoe mawazo yako mabaya kichwani, jana mlikuwa mnaongea nini?”

WIFE: “Haya kuhusu.”

Na mimi nilikwenda kuoga muda huo baada ya hapo nikaenda zangu seblen kucheza na Junior.

******

Hii week niliweza kuonana na Mary pia, maana alisema kuna jambo la kazi anataka tuzungumze jioni. Pia sikuona sababu ya kuwa mbali na Mary maana ni mteja wangu, sikuona kosa lake lolote sababu Prisca bado hajataka kumfungukia dada yake na mimi nilisema sitoweza kumwambia Mary kinachoendelea.

Niliwasiliana na Mary na tukakubaliana tuonane pale Target na hii sehem ipo nyuma kidogo upande wa kushoto kabla hujafika Roundabout ya kwenda Whitesand, kama unatokea kwa Zena.

Wakati natoka kwenye mishe zangu nilipitia pale na yeye alikuwa akinisubiri na ilikuwa ni usiku tayari. Nilifika mpaka alikokaa, tulisalimiana na muda huu mhudumu alikiwa amefika kutusikiliza tayari.

MARY: “Insider unaweza agiza kwanza.”

MIMI: “Dada niletee Pepsi ya baridi sana na portion ya mbuzi choma tu.”

“Mbuzi choma bila kitu?” Dada aliuliza

MIMI: “Ndio dada tena ufanye haraka.”

MARY: “Insider si ungekula kabisa? Ili ukifika home unalala tu.”

MIMI: “Nitakuta home wamepika haitakuwa busara na sijatoa taarifa mapema.”

Sikutaka kula kabisa pale maana ningerudi home nimeshiba ningeenda gombana na Mama J.

MARY: “Sawa haina shida, mambo yako yanakwendaje kwa ujumla?”

MIMI: “Salama nashukuru Mungu, Mary nambie exactly unajambo gani? Maana sitaki kupoteza muda hapa.”

MARY: “Insider mwezi ujao tunakwenda Mikumi National Park mimi na friends wa chuo, nataka utupeleke kule na kuturudisha.”

MIMI: “Mnakwenda lini?”

MARY: “Mwezi ujao, nimeamua kukwambia mapema ili ujipange.”

MIMI: “Sawa haina shida nitalifanyia kazi na tutaendelea kuwasiliana.”

MARY: “Insider please, Don’t let me down.”

MIMI: “Usijali kuna lingine nje na hili? Maana nataka nirudi home mapema nikalale.”

MARY: “Ni hilo tu na pia nili miss kukuona.”

MIMI: “Ahsante mimi mzima wa afya kama unavyoniona hapa. Twende nikudrop pale kwa Zena afu utachukua boda kwenu mimi siendi.”

MARY: “It’s okay, lets go.”

Tuliondoka pale na nilimshusha Mary pale kwa Zena akachukua boda bodaboda kwenda kwao. Kutoka kwa Zena mpaka kwao hata sio mbali ni ni karibu sana.

Baada ya kurudi home wife aliomba nimpeleke Junior clinic yeye angekua chuo na dada bado mgeni hamwamini kumuachia mtoto kwenda naye clinic, hivyo nilimwambia nitampeleka mimi asiwe na wasiwasi.

Ijumaa asubuhi niliwapeleka Maggy na Mama wa2 Posta na baada ya hapo nilirudi home mapema ili nimpeleke Junior clinic. Baada ya kurudi nyumbani tuliondoka na dada kwenda clinic na tulikwenda Rabininsia hospital ya kule Tegeta.

Tuliwasili pale hospital sababu taratibu zote za pale nazifahamu hata sikupata shida, maana haikuwa mara yangu ya kwanza kumpeleka mtoto clinic. Niliambiwa na nurse Junior alikuwa na sindano ya kuchoma na baada ya kumaliza taratibu zote za clinic tulirudi home. Lakini tulipitia pale Tegeta Sokoni na nikanunua baadhi ya mahitaji ya nyumbani.

Hii siku mimi sikutoka kabisa nilishinda home nikicheza na Junior wangu. Nilisema nitulie ili badae nitoke na Iryn maana alisema kuanzia weekend hii tungeanza kazi.

Nilimpigia simu Iryn ili kumwuliza kama ratiba zinaendelea ama laah!, lakini hakupokea simu yangu, nikampigia tena kwa mara ya pili lakini haikupokelewa, bhasi nikasema atakuwa busy na atanirudia.

Ukweli ni kwamba toka ile jumapili tuachane na Iryn pale 25 lounge hatukuwa na mawasiliano yoyote na mimi nilikuwa najua kama kungekuwa na kazi lazima angenicheki tu.

Nilikaa mpaka jioni pale home lakini sikuweza kupata taarifa yoyote kutoka kwa Iryn na mimi sikutaka kumpigia simu tena muda ule, maana niliona dharau simu mbili hajaziona?. Na siku ikaisha kihivyo bila kufanya kazi kabisa.

Jumamosi pia sikutoka kwenda mzigoni maana nilikuwa na mgeni ambaye ni Tyna alikuja kunisalimia na familia yangu na alisema angeshinda siku nzima na sisi nyumbani. Nilimpasha taarifa Mama J kuhusu ugeni na yeye alikuwa na bashasha ya kumjua mgeni atakaye kuja.

Saa 3 asubuhi Tyna aliwasili pale home maana nilimtumia location kwa whatsapp, nilimkaribisha ndani na alikuwa kaja na zawadi za Junior za kutosha.

Pale seblen nilifanya utambulisho na nilimtambulisha Tyna kwa Wife kuwa ni rafiki kipenzi wa dada yangu, na upande mwingine Tyna alifurahi sana kumjua wifi wake, na mimi niliwaacha waendelee na mazungumzo yao.

Mchana Msomali alinipigia simu akanambia tuonane jioni kuanzia saa 11 pale Seacliff Hotel na alisisitiza sana niwe on-time. Na mimi nilimwambia baada ya lisaa nitakuwa na majibu, lengo langu ni comfirm kama kuna kazi kwa Iryn.

Kwenye saa 10 jioni nilimpigia simu Iryn lakini hakupokea simu yangu, nilipiga tena baada ya dakika 20 lakini hakupokea. Niliamua kumtumia text lakini pia haikujibiwa kabisa, bhasi nikasema something wrong.

Niliwaza pale Iryn hajawai kuwa na tabia ya kutopokea simu zangu na kama akikuta missed call lazima anirudie, toka jana hajanirudia na leo hapokei simu zangu kuna nini?.

“Au hajapenda kujua mimi nina mke na mtoto?”

Upande mwingine niliwaza maybe anaweza kuwa na matatizo hivyo nikaplan nitakwenda kwake kumwona. Na muda huu nilimpigia simu Msomali kwamba nitakwenda kuonana naye na akasema yeye yupo nikifika nimjulishe.

Tulikaa na Tyna mpaka jioni saa 11 ndo akaaga na kabla hajaondoka alifanya maombi pale na akaomba next time sisi twende kwake tukatembee na tulimuhakikishia tutakwenda kumtembelea.

Tuliondoka pale home tukiwa tumeongozana barabarani mpaka mwenge ndo tukaachana, maana mimi niliendelea na Bagamoyo road na yeye alikata kwenda na Sam nujoma Road.

Nilifika Seacliff Hotel saa 12 jioni na nilimpigia simu Msomali baada ya kufika lakini hakupokea na akanitext chap,

“Have you arrived yet?”

“Yes Bossy”

“Wait for me I’m coming soon.”

Niliendelea kumsubiri pale na muda huu nilikuwa nimekaa kwenye kibench mitaa ileile nikipiga story na wamasai. Nilikuwa nimeshazoeana nao sana Wamasai wa eneo lile na ni marafiki zangu mpaka sasa.

Nilisubiri sana pale lakini Msomali hakuwa na dalili za kutoka na muda huo ilikuwa saa2 na nusu tayari. Niliwaza pale nimtext? maana niliona Msomali ananichomesha mahindi tu afu hatokei na kaniweka masaa 2 tayari.

Saa 3 ndo alinipigia simu akaniuliza niko wapi na mimi nikamwambia niko nje kabisa ya parking karibu na bango la Casino, Msomali akanambia niingize gari kwenye parking ndani. Nilisikiliza anachosema na nikaingiza gari parking za ndani, na baada ya dakika 10 alikuwa amefika nilikokuwa nimepark gari, na aliingia akakaa siti za nyuma.

MSOMALI: “Bro kwanza niombe Samahani kwa kukuweka sana hapa.”

MIMI: “Umeniweka masaa 3 hapa bora hata ungenambia nichelewe kuja aseee.”

MSOMALI: “Nilikuwa na kikao na ndugu zangu, ndo hao wanatoka hata wewe umechelewa kuja.”

Muda huu nilliziona gari mbili za Landcruiser VX zikitoka maeneo yale, ambao ndo alikuwa nao.

MIMI: “Sawa haina shida, what kind of deal you wanted to share with me?”

MSOMALI: “Insider unajua wewe Nyota yako ni kali sana.”

Maneno ya Msomali yanifanya nishtuke kidogo maana ndo nilikuwa nasikia kwa mara ya kwanza kutoka kwake.

MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”

MSOMALI: “Bro una nyota nzuri sana ila sema hujajua namna ya kuitumia tu, pia una kismart cha kupendwa na watu. Nambie hapa kama nadanganya Insider.

Niliamua kunyamaza tu maana maneno aliyokuwa anaongea ni kama yalikuwa na ukweli, maana kwenye kazi hii nilikuwa nakutana na watu wengi sana na walikuwa wanakubali sana mpaka sasa. Nilikuwa napata wateja wengi sana ambao walikuwa wanataka niwe nawafata asubuhi na kuwapeleka kazini, na wapo ambao walikuwa wanataka niwe nawafata kazini na kuwarudisha nyumbani. Lakini kutokana na kuwa na wateja wawili (2) wa asubuhi deals nyingi nilizipiga chini na zingine nilikuwa wanaunganishia watu wengine.

Ukija pale Posta nilikuwa nafanya kazi na wafanyakazi wengi sana hasa wa bank na wengi walikua Ma-loan officer, walikuwa wananipigia simu na wanaweka order mapema, nimezunguka nao sana kule Kariakoo kwenye makampuni mbalimbali na sehemu nyingi sana. Haya ni matukio ambayo sikutaka kuyaandika maana ni mengi sana, na nilizoeana na watu wengi kwa muda mfupi kupitia Uber.

Sikutaka kubishana naye maana najua Wasomali haya mambo ya Nyota wanayajua vizuri. Lakini mimi niliamini sana kwenye kusali na kumtanguliza Mungu kwenye kila jambo.

MIMI: “Unavyosema sijui namna ya kuitumia nyota yangu unamaanisha nini?”

MSOMALI: “Insider wewe endelea kumwomba Mwenyezi Mungu akuongoze atakuonesha njia sahihi.”

MIMI: “Ni kweli unachosema Mungu ndo kila kitu. Naona muda unakwenda kuna ishu gani?”

Muda huu Msomali alitoa bahasha kwenye bag lake “Duffel bag” na akanikabidhi muda ule. Ndani ya bahasha kulikuwa na kibox cha mstatili chenye ukubwa wa A4 na upana wa nchi nne hivi tena kilikuwa cheusi.

MIMI: “Bro ni nini hiki?”

MSOMALI: “Bro deal lenyewe ndo hilo sasa, nataka utajirike na wewe, hapa duniani hakuna anayefanikiwa bila kuvunja sheria, hawa matajiri unaowaona hakuna asiyefanya “shady dealings” au “Contrabands”. (Alinitamkia hayo maneno vivyo hivyo, unaweza kugoogle maana zake)

MIMI: “Unataka kusema hili ni bomu?”

MSOMALI: “Exactly nataka upeleke hilo bomu Posta haraka na urudi tuje tuongee mipango mingine.”

Na muda huu Msomali alitoa card kwenye gari ambayo ilikua na taarifa zote (Location Details) za mzigo unakotakiwa kwenda ambapo ni Posta na akatoa noti za dollar 100, baada ya kuzi hesabu zilikuwa ni noti 30 ambazo ni sawa na $3,000.

“Nataka upeleke huu mzigo haraka ukifika hapo wewe gonga mlango kuna mtu atapokea na navyoongea hapa na wewe yuko anasubiri huu mzigo now. ARE YOU IN OR OUT?.”

Muda huu nilikuwa sijui niseme nini maana nilikuwa nahitaji pesa kwa njia yoyote ile na nilikuwa nashida na pesa tena sana. Japo sikujua ndani kuna Bom gani ila nilikuwa bado niko Dilemma nilikubali lile Bom au nilikatae.

Na muda huo huo nikiwa kwenye mawazo ni maamuzi gani niyachukue dhidi ya Msomali nilipokea text kutoka kwa Iryn….

“Insider mambo I was very busy ila naomba kuterminate mkataba na wewe mwisho wa mwezi huu.”

Na muda huu nilihisi kuchanganyikiwa mara 2 hata Msomali aliona mabadiliko yangu pale, nilijikuta niko kwenye wakati mgumu sana.”

TO BE CONTINUED
&
GOOD NIGHT FANS.
Nimepata stress na hiyo message ya Iryn utasema mimi ndio Insider! Haya tunangoja muendelezo Ijumaa Inshallah [emoji120]
 
Back
Top Bottom