INSIDER MAN
JF-Expert Member
- Nov 7, 2018
- 2,005
- 19,579
- Thread starter
- #3,321
EPISODE 31
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
CONTINUE……
“Kwahiyo umeamua twende Zanzibar?
“Ndiyo Insider nimeona tukatembee tubadili mazingira, afu kingine nataka nipate connection za Dubai kupitia Muajemi ili niwe nasimamia show mwenyewe hizi ndo target zangu.”
“Sawa bossy wangu mimi sina tatizo.”
“Bye Insider uwe na usiku mwema msalimie Junior wangu.”
“Usijali zimefika.”
Na muda huu niliwaza kuanza kumpanga Mama J mapema hili suala la mimi kwenda Zanzibar. Baada ya wife kuingia chumbani nilianza naye mazungumzo,
MIMI: “Swahiba njoo hapa tuongee bhasi, na leo nimekumiss sana itabidi umalize mambo yako mapema.”
WIFE: “Nambie unataka tuongee nini?”
MIMI: “Unajua nimeongezewa majukumu ya kiofisi kwa sasa nitakuwa na deal na mizigo kuichukua bandarini.”
WIFE: “Jambo zuri ufanye kazi kwa bidii sasa.”
MIMI: “Ijumaa pia nitakwenda Zanzibar kuchukua mizigo.”
WIFE: “Kama kikazi haina shida uwe makini sana na mizigo ya watu.”
MIMI: “Lazima niwe makini.”
WIFE: “Na unarudi lini?”
MIMI: “Inategemea na process zitakavyokwenda ila haiwezi zidi siku 2, si unajua bado sina experience ya kutosha na connection.?”
WIFE: “Utakwenda na nani?”
MIMI: “Sijajua bado ila nahisi peke yangu.”
WIFE: “Sawa nakuja ngoja nikampe Junior chakula.”
Suala la Mama J nilikuwa nimelimaliza kihivyo na aliyekuwa amebaki ni mzee tu kumpanga maana nilikuwa na gari yake angeweza kulihitaji afu mimi sipo.
Asubuhi Mzee Pama alinipigia simu na akanipa taarifa kuwa mchupuko wake anarudi hivyo nikawapokee Airport kama nitakuwa na nafasi. Na mimi sikuweza mkatalia nikamwambia nitakwenda kumpokea na alisema niwapeleke nyumba mpya ya kule Mbweni, na baada ya hapo niandae logistic ya kwenda kutoa vitu kule Kigamboni.
Mchana saa8 ndo muda ambao nilikwenda kumpokea mchepuko wake na nilipark gari pale Terminal 2.
Saa 9 kasoro ndo muda ambao waliwasili pale JNIA na alikuwa na Mama yake na dada mdogo. Tulisalimiana na tukaanza safari ya kwenda Mbweni.
Mchepuko wa Mzee alikuwa anaitwa Jane (CODE).
MIMI: “Mzee amesema niwapeleke Mbweni.”
JANE: “Kuna vitu kule?”
MIMI: “Kila kitu kipo na amesema jioni nikatoe vitu kule Kigamboni baadhi lakini sio vyote.”
JANE: “Sawa haina shida.”
Tulitumia saa moja na nusu na tuliwasili pale Mbweni, baada ya kuingia ndani Mchepuko wa Mzee alikuw akishangaa jinsi nyumba ilivyopendeza ni kama ilikuwa inamsubiri yeye tu.
Nilifanya mazungumzo na Mzee kuhusu kwenda kufata vitu kule Kigamboni na akanambia nitoe kitanda, nguo na vyombo vya ndani tu, vitu vingine nitajua mimi navipeleka wapi maana havina haja.
Jioni nilikwenda Kigamboni na nilingia ndani nikakagua vitu vya kubeba na nikaona canter ingetosha kabisa. Muda huu nilikuwa ninayapigia hesabu kabati la nguo, makochi na fridge maana ni vitu ambavyo vilikuwa muhimu kwangu.
Na wakati bado nikiwa napiga hesabu zangu jinsi ya kuchomoka na vile vitu Mchepuko alinipigia simu na nikapokea simu yake.
“Insider hivyo vitu vinavyobaki kuna best yangu anakuja kuvichukua na funguo utamwachia Jirani yangu hapo anayefuatia.”
Daah! nilimind sana nilitamani kumwambia Mzee amenipa ila nikavunga, niliamua kupotezea.
“Sawa haina shida.”
Baada ya Mchepuko kusema hivyo niliona Kirikuu ndo ingetosha kubeba mzigo unaokwenda Mbweni. Baada ya kupakia vitu vya kuondoka navyo niliamua kuondoka na fridge kibishi maana lilikuwa ni kubwa kampuni ya LG. Fridge lilikuwa kwenye hesabu zangu maana pale home nilikuwa na fridge dogo, hili kubwa lingesaidia kuweka mazaga ya Junior na matumizi mengine.
Baada ya kumaliza kupakia vitu niliacha funguo kwa jirani na tukaondoka pale Kigamboni. Nilipitia kwanza home nikaacha fridge then nikapeleka vile vitu Mbweni.
Tuliingiza vitu ndani na baada ya kumaliza nilifanya malipo kwa jamaa na akaondoka, muda huu mimi nilibaki nikimsaidia mchepuko kupanga vitu.
JANE: “Mzee Pama kanambia utanipeleka Driving school.”
MIMI: “Ndiyo sijui ni lini utaanza.”
JANE: “Nafikiri jumatatu nianze, au unaonaje maana nimetoka safari sijaweka mambo sawa.”
MIMI: “Vyovyote sawa pia hongera kwa mjengo na kijacho.”
JANE: “Hahahaha ahsante Insider.”
MIMI: “Mzee anakupenda sana huu mjengo ni hatari.”
JANE: “Nashukuru pia nimepata taarifa ulisimamia ujenzi ndomana nimehamia leo mapema.”
Baada ya kumaliza kuweka mambo sawa nilimpigia simu Mzee na nilimwuliza kuhusu gari akasema iendelee kubaki kwangu kwanza. Baada ya maongezi Mzee aliniingizia Pesa kiasi cha tsh 600,000/= kwaajili ya kulipia mafunzo ya mchepuko wake na pesa nyingine iikuwa yangu.
Nilirudi home maana ilikiwa usiku tayari na baada ya kupata dinna Muajemi alinipigia video call.
MIMI: “Bro habari za huko South Africa.”
MUAJEMI: “Bro huku salama, nashukuru kwa Effort yako.”
Muajemi angejua hata sikuhusika na suala la Iryn asingethubutu kunishukuru.
MIMI: “Kaka usijali tuko pamoja nafikiri ni hatua nyingine nzuri zaidi.”
MUAJEMI: “Kweli kaka Ijumaa mimi nitapitiliza Zanzibar hope nitawapokea Airport.”
MIMI: “Haina shida Bossy wangu ila endelea kuplay smart, don’t force her to do anything acha aamue mwenyewe.”
MUAJEMI: “Bro ushauri wako upo makini sana.”
MIMI: “Sisi ni wanaume lazima tukumbushane, ukiendelea kuplay smart na uhakika utampata kilaini kabisa.
MUAJEMI: “Siwezi fanya terrible things bro, maendeleo yako yakoje?”
MIMI: “Bro! mimi niko salama ila kuna mambo nimekwama kidogo nitahitaji msaada wako, lakini tutaongea tukionana.”
MUAJEMI: “Sawa Bro! anytime and be free.”
Tuliagana na Muajemi kwa makubaliano ya kuonana Zanzibar Ijumaa. Kwa upande mwingine Muajemi alikuwa na furaha sana, uzuri wa Iryn ulikuwa ukimpagawisha sana.
Kesho yake ambayo ni Alhamis hii siku sikufanya kazi ya Uber kabisa maana nilikuwa na kazi ya kusupply mizigo kwenye saloon za Iryn.
Baada ya kupeleka mzigo Mikocheni nilimkuta Lucy na tukaanza story na alikuja akakaa siti ya mbele.
LUCY: “Insider wewe ni balaa nakupa nyota zangu tano.”
MIMI: “Kwanini unasema hivyo dear?”
LUCY: “Hivi uliwezaje kumkamata bossy wetu?, akiwa na wewe anakuwa na furaha sana ila kwetu ni kauzu balaa.”
MIMI: “Hahahaa hujui kwamba wewe na yeye wote ni ke? Mafahali wawili hawakai zizi moja.”
LUCY: “Insider unadate na Bossy usinidanganye.”
MIMI: “Hapana hata sijawai mtongoza kabisa.”
LUCY: “Bhasi anakupenda acha uoga, hivi unamwachaje mrembo kama yule?”
MIMI: “Hujui ni Bossy wetu yule unataka nile kibuti afu nitakula wapi?”
LUCY: “Mimi ni mwanamke amini nachokwambia, unajua kwanini nasema hivyo? Kwanza ulikuwa wapi mwezi uliopita?
MIMI: “Nilikuwa mkoani niambie.”
LUCY: “Kuna siku alikuja ili nimtengeneze nywele zake na kila alichokuwa anafanya kwenye simu mimi nilikuwa naona live, alikuandikia message kama mara 3 hivi na alikuwa anafuta, akaamua kuweka simu pembeni.
MIMI: “Uliona alichokuwa anaandika?”
LUCY: “Mhh hapana ila nilimwona kama hayuko sawa kabisa, nilihisi something wrong kati yenu. Unajua toka urudi namwona anafuraha sana sikuhizi tofauti na wakati haupo. Insider unabaraka zangu zote fanya kweli, kula mrembo yule, Pisi kali ile acha ufala au wewe ni domo zege?”
Maneno ya Lucy yalinichoma sana ni kama alikuwa anaona dizaini kama nazingua hivi, Lucy aliona kama nachezea sarafu chooni. Na muda huu Lucy aliendelea kunichamba,
LUCY: “Insider ningekuwa mimi ndo wewe yule mrembo nisingemwacha kabisa, unazurura na mwanamke mzuri kama yule hakuna unachofanya? what kind of Man are you???”
MIMI: “Hivi unajua Iryn anamtu wake na ni Mfaransa, nakupa hii siri wewe.”
LUCY: “Yuko hapahapa Tanzania?”
MIMI: “Anakujaga mara moja moja ila anaishi Ufaransa.”
LUCY: “Insider hakuna mapenzi ya mbali the way navyomwona Bossy naona kabisa ana mapenzi na wewe, ila wewe ni kama unazingua, angalia utakosa vyote.”
MIMI: “Sawa bwana naona leo umeamua kunichamba kisawasawa.”
Katika maongezi yetu sikutaka kumwambia ukweli kwa kile kilichokuwa kinaendelea baina yetu mimi na Iryn.
MIMI: “Hivi Lucy unaishi wapi?”
LUCY: “Makongo juu.”
MIMI: “Iryn anakukubali sana make her more proud of you, usimuangushe naamini utakula mema mengi kutoka kwake.”
LUCY: “Sawa Insider maisha yenyewe magumu haya lazima niwe serious.”
Na muda huu nilimwaga Lucy na nilikwenda kwa Iryn kwaajili ya mipango ya safari ya Zanzibar. Njiani nilikuwa nikiyafikiria sana maneno ya Lucy ni kama yalikuwa yakijirudia Kichwani.
Baada ya kuwasili pale kwa Iryn nilipark gari nje getini nikaingia ndani na nilimkuta jiran akiwa nje kibarazani amekaa ikabidi nimsogolee,
MIMI: “Jirani nakuona umetulia unawaza jinsi ya kutumia hela.”
JIRANI: “Jamani kutumia hela tena? wakati hata hela zenyewe sina.”
MIMI: “Nambie lakini za siku? nilikumiss sana.”
JIRANI: “Sijakuona muda sana ulikuwa wapi?”
MIMI: “Mishemishe tu si unajua mtoto wa kiume?”
JIRANI: “Hata mimi naona, mliamua kunichinjia baharini.”
MIMI: “Hamna jiran sahivi nipo tutapanga hili na tutatoka.”
JIRANI: “Sema Jiran upo vizuri una miliki pisi kali sana hongera zako, leo nimeamua kukwambia ukweli, una bahati sana.”
MIMI: “Hahahahaaa jiran acha nikukimbie maana umeanza kunitukana.”
JIRANI: “Ni kweli, msalimie wifi yangu Iryn.”
Nilingia ndani na Iryn alikuwa seblen akichezea laptop yake. Tulisalimiana na mimi nikakaa kwenye coach,
IRYN: “Insider una agenda gani na Rose?” (Jirani)
MIMI: “Si jirani yako? nilikuwa namsalimia ni kitambo hatujaonana.”
IRYN: “Kumsalimia unatumia muda wote huo?”
MIMI: “Tulikuwa tunaongea masuala mengine pia alikuwa anakumbushia ile ahadi.”
IRYN: “Mhhh sawa, ushajiandaa kwaajili ya kesho?”
MIMI: “Hata bado vipi wewe tayari?”
IRYN: “Mimi sina mambo mengi maana jumapili tutarudi.”
MIMI: “Na muda wa kuondoka?”
IRYN: “Alisema atatuma ticket za ndege lakini nimemwambia sisi tutakwenda na boat, tutaondoka na boat ya mchana saa6”
MIMI: “So ushafanya booking tayari?”
IRYN: “Tayari”
MIMI: “Acha mimi nikukimbie bhasi ili kesho niwahi kuja hapa.”
IRYN: “Insider subiri.”
Na muda huu Iryn alinyanyuka na kwenda chumbani na alirudi akiwa ameshika kimfuko na akanikabidhi.
MIMI: “Thank you.”
IRYN: “Byee see you tomorrow.”
Alinisindikiza mpaka kwenye gari na tukaagana pale na mimi sikutaka kuchelewa kuangalia vilivyokuwa mle ndani. Maana nilikuwa naham ya kujua Iryn ameweka nini, baada ya kutoa vitu vya mle ndani, kulikuwa na T-shirt nyeupe, pensi na perfume ilikuwa kwenye chupa nyeusi imeandikwa Tom Ford.
*********
Ijumaa tarehe 13/05/2022 hii ndo siku tuliyokwenda Zanzibar na Iryn. Niliwasili pale kwake mapema kabisa na baada ya kuingia ndani nilikaa seblen nikimsubiri.
Ndani ya dakika 10 alikuwa ametoka na alikuwa kapendeza balaa, alikuwa kavaa kitop chekundu, skin jeans nyeusi, raba ya nike nyekundu, Sunglasses nyeusi, mkononi alikuwa na saa pamoja na bracelet bila kusahau necklace alizopewa na Muajemi.
Kwa upande wangu nilivaa zile nguo alizonipa jana kama zawadi, chini nilikuwa na raba ya nike na nilipulizia ile perfume aliyonipa na ilikuwa ikinukia vizuri sana.
Wakati nikiendelea kumshangaa Iryn alinianza,
IRYN: “Insider you look great today.”
MIMI: “Thank you ila wewe umefunika na hio miwani utafanya Muajemi azimie.”
IRYN: “Hahahaa Insider umeanza vituko, sasa itabidi tufanye kurequest usafiri gari yako si unaiacha hapa?”
MIMI: “Itabidi ibaki hapahapa tu”
Nilifanya kurequest usafiri na ndani ya muda mfupi usafiri ulikuwa umefika na tukaondoka kuelekea Posta.
Tulitumia dakika 20 kufika pale Azam marine na baada ya ukaguzi tulielekezwa kwenye boat yetu ambayo ilikuwa ni Kilimanjaro 7 na tulikwenda moja kwa moja mpaka Royal seats.
“Umelipia kiasi gani hapa?”
“Laki moja per seat.”
Na muda huu tuliendelea na story mpaka boat ikaanza safari ya kwenda Zanzibar.
Saa 9 mchana tulikuwa tayari Zanzibar na muda huu tulikuja kupokelewa na gari, tulikwenda moja kwa moja mpaka Hotel-Verde ndo tulishushwa pale.
Tulikaribishwa na moja kwa moja mpaka ndani tukakutana na Muajemi pale reception “Hotel lobby”. Tulisalimiana naye, akatupa pole ya safari na muda huu wahudumu walipeleka mabag kwenye rooms zetu na sisi tukaenda restaurant kupata lunch.
Ukweli kwa ambao hamjabahatika kufika kwenye hii Hotel, Verde ni Hotel nzuri aisee yaan ni balaa ni nzuri na inavutia sana. Humu ndani sura za Pesa ndo zilikuwa zikionekana, bado warembo na mimi macho yangu muda wote yalikuwa yakizunguka kama goroli kila angle.
Baada ya lunch tulitoka ili twende kwenye rooms zetu lengo ilikuwa tuoge ili tupumzike kidogo afu badae tungeanza kuzurura ili kusurvey eneo la hotel.
Tuliingia kwenye lift na tulipanda mpaka floor ya 3, kimbembe nilishangaa kuona kila mtu ana room yake. Muajemi alibook rooms 3 kwaajili yake,mimi na Iryn na zote zilikuwa floor moja, room ya Iryn ilitizamana na ya Muajemi na room yangu ilikuwa next baada ya Muajemi.
EPISODE 32[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu