Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Ila kwenye zile part za mizagamuano na prisca Mkuu anatubania sana angechimba chimba ndani kidogo story ingenoga zaidi hii stori
Kwamba insider alipofika room akamvuta prisca kifuani akajionea uumbaji wa Mungu maana alichomwa na kitu chenye incha kali kama mshale, kumbe zilikuwa chuchu za mrembo Pili. Baada ya hapo zikapigwa romance za hapa na pale kisha oil ikapimwa kama ipo, baada ya hapo gari ikawashwa kwaajiri ya safari😎😎. Ndo unataka awe anaweka na hizo kachumbari?
 
Haya si ndio mambo Sasa.....popote ulipo Mkuu agiza kinywaji bills on me!!!.......alafu Kuna watu wanakataa....pilau bila kachumbari hainogi bhana...sisi wazee wa mizagamuano pale kwenye sekta yetu hatutendei hakii angeenda deep kidogo.... haiwezekani unakula PISI kali alafu tusijue hata alifurahije tendo
 
EPISODE 33

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Baada dakika kadhaa nilisikia mlango ukigongwa na nikaenda kufungua muda uleule, na mimi nilihisi anayegonga ni Muajemi. Na kweli baada ya kufungua alikuwa ni yeye na Iryn alikuwa bado kalala kitandani vilevile kama hana habari na mtu anayegonga mlango.

CONTINUE.

Niliingiwa na wasiwasi muda huu nikiwa pale mlangoni.

MIMI: “Bro! karibu ndani.”

MUAJEMI: “Ahsante nimegonga kwa Iryn nikaona kimya nahisi kalala nilitaka nimpe ratiba ya kesho kuondoka……”

Nilimkatisha na mazungumzo yake,

MIMI: “Kesho muda gani kwahiyo.”

MUAJEMI: “Tutaondoka na Private jet jioni.”

Na muda huu tulikuwa bado mlangoni kwa jinsi chumba kilivyokuwa kimedizainiwa ni ngumu kuona kitanda labda uingie ndani.

MIMI: “Bro karibu ingia ndani tuongee.” Lakini kimoyomoyo nilikuwa naomba asiingie kabisa.

MUAJEMI: “Bro mimi na haraka natoka kuna demu naenda kumwona tutaonana kesho.” Aliingiza mkono kwenye kanzu yake na akatoa pesa akanikabidhi pale.

“Bro na hii ni ile ishu uliyoomba, mimi nawahi tutawasiliana kesho, make sure Iryn hajui kama nimetoka Bro!.”

MIMI: “Bro usiwe na wasiwasi, Ahsante na Mungu akubariki sana.”

MUAJEMI: “Inshallah.”

Na Muajemi aliondoka eneo hili na mimi nilihakikisha anapotea kabisa ndo nikafunga mlango.

Baada ya kumalizana na Muajemi ofcourse mwili ulianza kuwa mwepesi muda huu na kwa upande mwingine nilifurahi sana maana asingenielewa kabisa. Hata kama Iryn ni Bossy wangu kuonekana kwake room yangu muda ule na akiwa amevaa night dress tena za kutia hamasa kwa haraka mtu angehisi ni demu wangu.

Nilishusha pumzi kwa nguvu na kurudi ndani nikiwa nimeshika bahasha mkononi. Nilimwangalia Iryn na yeye akanizomea kwa ishara ile ya mkono ( yooh).

IRYN: “Insider umeshika nini?”

MIMI: “Pesa hizi kuna mtu kesho asubuhi nitaonana naye, Muajemi kaomba nimpe kwa niaba yake maana yeye kachoka na atachelewa amka na amesema kesho tutaondoka na Private jet.” Ilibidi nimdanganye na nimbadilishie mada juu kwa juu.

IRYN: “Hajaniulizia?”

MIMI: “Amesema kagonga mlango hufungui anahisi utakuwa umelala.”

IRYN: “He lied, hivi unajua reason ya mimi kuondoka mapema muda ule?”

MIMI: “Hapana why?”

IRYN: “Sikutaka usumbufu kabisa, toka jana ananitongoza niende room yake na mimi namwona anataka kunifvck tu hana lolote.“

MIMI: “Mimi nilimwona smart sana kwani kakukera nini mummy?”

Na muda huu nilimsogelea na kukaa mbele yake na nilizungusha mkono wangu kumshika bega lake la kushoto nikiwa kama nambembeleza, nadhani mnaelewa.

IRYN: “Jana wakati umetuacha alikuwa anaforce tulale wote na mimi nilimwambia yale so makubaliano yetu.”

MIMI: “Pombe alizokunywa zitakuwa zilikuwa zinamuendesha.”

IRYN: “Insider mimi nakuamini sana ujue, Muajemi pia hakutaka wewe uje huku Zanzibar unatambua hili?”

MIMI: “Aiseee kumbe.”

Niliwaza pale kumbe Muajemi hakupenda ujio wangu kabisa.

IRYN: “Nilimwambia bila Insider mimi siwezi kuja, hili pia lilinipa mashaka. Hata jana nimemwambia bora nilale na wewe naamini nitakuwa salama, mimi naondoka byee”

MIMI: “Sasa umeghairi kulala na mimi?”

IRYN: “Si ulinifukuza wewe?, tutaonana asubuhi.”

MIMI: “Kesho utaniamsha bhasi.”

Baada ya kuondoka nilifunga mlango na nilitoa zile pesa kwenye bahasha na zilikuwa bunda 5 ya noti za 10,000/=. Nilifurahi sana lakini niliwaza hizi pesa Muajemi anatoa sababu anashida ya kumpata Iryn, bila Iryn sidhani kama tungekuwa tunajuana.
********

Saa 3 asubuhi Iryn aliniamsha kwa kunipigia simu na niliingia kuoga pamoja na kujiandaa haraka. Baada ya hapo tulitoka na tulikwenda restaurant kupata breakfast.

Baada ya breakfast tulikwenda moja kwa moja mpaka swimming pool na yeye aliingia kuswim na mimi muda huu nilikuwa kama mpenzi mtizimaji. Sio kwamba nilikuwa sitaki kuingia ila nilikuwa nataka kwanza kuyaangalia maungo yake vizuri.

Wakati yuko swimming Wanaume kama watatu hivi walimfata kumtongoza lakini Iryn alikuwa hana habari nao. Kwa upande mwingine alikuwa akikodolewa sana macho na mafisi, walikuwa wakimtani tu na wengi pale walikuwa ni foreigners.

Iryn alisogea mpaka upande niliokuwepo na akaanza kuniita

IRYN: “Insider…….., njoo bhasi au unapenda navyosumbuliwa?”

MIMI: “Ok nakuja.”

Muda huu nilivua nguo nikabaki na boxer nikaliunga tukaanza michezo kama kawaida, muda huu nilikuwa free kucheza na Mrembo Iryn maana Muajemi hakuwepo.

Ukweli hii siku nili enjoy sana maana nilikuwa namshika sana makalio yake mle kwenye maji, na yeye hakuwa na pingamizi lolote.

Baada ya kuchoka tulikaa kwenye ki-ukuta pembeni ya swimming na tukaanza story pale.

IRYN: “Hivi mama Junior anajua uko Zanzibar?”

MIMI: “Kwanini unauliza hivyo au umeyakanyaga tayari?”

IRYN: “Nimekuuliza tu na maana yangu.”

MIMI: “Ndio anajua ila hajui kama tumekuja wote, ulikuwa unamaana gani?”

IRYN: “What if aki-found out tulikuja wote huku?”

MIMI: “Sio rahisi kujua otherwise uwe umemwambia uko Zanzibar hapo ndo atajua tuko wote.”

IRYN: “Insider mimi mtu mzima naelewa siwezi fanya ujinga kama huu, unaoneka unamwogopa sana Mama Junior.”

MIMI: “Sio namuogopa ila ninamuheshimu.”

IRYN: “Have you ever cheated your wife?”

MIMI: “Iryn sijui unataka kugundua nini but the answer is YES.”

IRYN: “Why?”

MIMI: “Iryn sisi wanaume ndo tulivyoumbwa lakini ilikuwa bahati mbaya. Hivi wewe unajiskiaje kudate na mme wa mtu? Unaona sawa kabisa?”

IRYN: “I don’t feel good, lakini Insider naomba utambue kwamba Griezmann ana msaada mkubwa sana kwangu, sijawai kwambia tu.”

MIMI: “Msaada gani?”

IRYN: “Nitakwambia siku nyingine tukiwa home.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

Tulitoka pale Swimming na tulikwenda mpaka beach, ukweli ni kwamba huku njiani kila tunayekutana naye alikuwa lazima ageuke au atutizame. Iryn alikuwa kavaa short pant iliyokuwa imemchora shepu vizuri na ule weupe wake uwiii alikuwa kivutio kule beach.

Beach ilikuwa na watu tofauti tofauti na wengi walikuwa ki-couples, tulipiga picha nyingi sana za ukumbusho hapa beach.

Tuliongea mambo mengi sana na Iryn huku beach na moja kubwa alisema atabadili muundo wa maisha yake.

Tulikaa beach mpaka saa 9 mchana ndo tukarudi zetu hotelin ili tujiandae kwaajili ya safari ya kurudi Dar.

Baada ya kurudi hotelini na kujiandaa nilifanya mawasiliano na Muajemi na yeye alisema yuko around kuna mtu ana mazungumzo naye hivyo atakuja kutufata. Haikuchukua muda Iryn alikuja room yangu na akalala kitandani na tulikuwa tukipiga story muda huu.

Muajemi baada ya kurudi aligonga na baada ya kumfungulia mlango nilimkaribisha ndani na alivyoingia alimwona Iryn kalala kitandani. Walisalimiana na Iryn na akasema anakwenda kuchukua bag lake ili tuondoke.

Ofcourse Muajemi alionekana kama hana furaha baada ya kumwona Iryn pale kitandani, dizaini kama alihisi something fishy is going on. Maana Iryn alionekana kujiachia sana hapa kitandani na hakuwa na wasiwasi wowote.

MIMI: “Iryn utakuja kunipa case wewe.”

IRYN: “Case gani?”

MIMI: “Hivi unafikiri Muajemi anajiskiaje kukuona upo room yangu na umejiachia hivi?”

IRYN: “Insider kwani kuna tatizo mimi nikilala hapa? Una Agenda gani na Muajemi maana siwaelewi kabisa.”

MIMI: “Ulisema amekutongoza na ulimgomea kwenda room yake, kukuona hapa huoni atajiskia vibaya?”

IRYN: “I told him wewe ndo Mwanaume nayekuamini baada ya Grizmann so don’t stress yourself”

Na muda huu Muajemi alipiga simu tuanze safari, usafiri ushawasili unatusubiri sisi tu.


Saa 12 jioni tulikuwa tumewasili Airport kwa ajili ya safari ya kurudi Dar na ndege iliondoka 18:30.

Saa 1 usiku tulikuwa tumeshawasili pale JNIA Terminal 1 na muda ule hatukuona umuhimu wa kurudi home mapema, tulikubaliana twende sehemu tupumzike tupate na Dinna.

Nilifanya kurequest usafiri na break ilikuwa pale Hyatt Hotel na tulikwenda moja kwa moja mpaka level 8. Tuliagiza chakula na vinywaji kila mtu alitoa odda yake, kwa upande wangu kwa kinywaji niligaiza wine na Iryn aliagiza wine pia, Muajemi aliagiza Jagermaister.

Tulikaa pale Hyatt mpaka saa 4 usiku na tukaondoka, Muajemi alifatwa na Dereva wake na sisi tulirequest Uber mpaka Kijitonyama.

Baada ya kufika Kijitonyama, mimi sikutaka kuendelea kubaki maeneo haya maana muda ulikuwa umekwenda tayari, hivyo nikachukua key ya gari nikamuaga Iryn na nikaondoka pale.

Na muda ule niliwaza nitafute zawadi kwaajili ya wife, niliwaza kurudi mikono mitupu na nilikuwa Zanzibar asingeelewa, hivyo nilipitia sinza madukani nikafanya shopping ya kununua nguo za wife, Junior pamoja na dada.

Nilimnunulia wife track 2, skin jeans 2, raba ya nike, shati ya jeans na kikoti cha jeans pamoja na jaz ya Barcelona, maana ni mshabiki wa hii team, bila kumsahau Junior nilimnunulia zawadi ya Ipad zile za watoto za kuchezea na dada yake Junior naye nilimnunulia nguo na mazaga mengine.

Nilitumia kama dakika 20 kuendesha gari mpaka home na baada ya kupark gari Mama junior alitoka na kuni-hug na nikampa ule mfuko wa zawadi.

Ukweli baada ya kwenda na hizi zawadi wife hakuwa hata na maswali mengi kabisa na mimi, niliwaacha pale seblen na nikaenda kulala maana nilikuwa nimechoka sana.
 
EPISODE 34

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

ENDELEA……


Jumatatu mchana niliweza kumit na Dullah Posta
na story kubwa zilikuwa kuhusu ugumu wa biashara kwa kipindi hiki.

DULLAH: “Insider unajua Bolt sipati request kabisa afu hawa Lokito wanaharibu biashara.”

Lokito ni App ambayo inatumiwa na madereva wa Uber katika kuongeza nauli au kusaidia kupata request haraka. Hii inafanya kazi hivi unakuta umerequest Bolt maybe kutoka Posta mpaka Mbweni, nauli unakuta ilikuonesha 15,000-20,000/= sasa unafika destination nauli dereva anakuonesha 35,000/= na hakukuwa na foleni kabisa, kama ulishawai kutana na hii bhasi jua ulifanyiwa lokito.

Upande mwingine unakuta dereva wa Bolt yuko pale Sinza makaburini ila kupitia Lokito anaweza ipeleka gari yake mpaka Mlimani city na mtu akirequest tu usafiri, anapata ile request kwa haraka, so atatoka Makaburini mpaka Mlimani city atachukua mteja anawaacha nyie mkiendelea kuzubaa. Huu mchezo ulikuwa sana kwa Madereva wa Bolt ila kwa Uber ulikuwa huwezi kuta huu ushenzi maana walikuwa serious na smart.

MIMI: “Sasa tunafanyaje Senior maana wewe ndo mkongwe huku.”

DULLAH: “Mzee mimi sahivi mikataba ndo itakayoniweka mjini na Private, ila leo kuna mzee katerminate mkataba maana nilimpamndishia nauli.”

MIMI: “Aisee acha tupambane mimi nashukuru Mungu yule dada mrembo (IRYN) amenipa mkataba mpya sio haba.”

DULLAH: “Atakuwa anakulipaje kwasasa? na wale wengine vipi bado unaendelea nao?”

MIMI: “Mzee now nakuwa Operation manager masuala yote ya logistic yatakuwa chini yangu, mshahara million 2, wale wengine bado tunaendelea.”

DULLAH: “Daah mzee umelamba bingo hapo ukitoa mafuta na service hukosi 1.2m kama faida na hao wengine hukosi mia sita mzee kwa mwezi upo vizuri. Ningekuwa mimi ningeachana na Bolt tu nikoamae na contract maana kwasasa unachosha gari tu, nauli za kis*nge afu request hakuna.”

MIMI: “Hata mimi nafikiria hivyo.”

DULLAH: “Fanya hivyo acha kuchosha gari yako au komaa weekend upate pesa ya kula na service.”

MIMI: “Leo umeongea point sana.”

DULLAH: “Afu yule dada wa Bank wa CRDB uliyeniconnect naye nishamweka tayari ila naona analeta mapenzi, hahahaha!.”

MIMI: “Hahaha wewe jiroge uanze kumleta Posta bure shauri zako.”

DULLAH: “Sema ni wife material nitamuangalia kwa jicho la 2.”

MIMI: “Sawa bhana all the best bro ila usilete mapenzi na kazi.”

DULLAH: “Niko makini kaka, mimi ndo Senior.”

Tuliagana na Dullah na mimi nilielekea Masaki kuwachukua madogo ili niwapeke makwao.

Baada ya kumalizana na madogo Muajemi alinipiga simu akasema jioni tuonane ana maongezi deep na mimi nisikose, na alionekana kuwa serious sana.

Na mimi nilipatwa na wasiwasi muda huu maana nilianza kuogopa, Muajemi alikuwaga ananinyenyekea sana why leo awe mkali hivi?. Muda huu nilipata wazo navyokwenda kuonana na Muajemi niwe na Prisca lengo langu ajue nina demu. Nilimpigia simu Prisca kumwambia badae kuna sehemu tutakwenda kupata dinna na alikubali akasema atakuwa around chuo.

Niliendesha gari mpaka Mikocheni ndo ilikuwa break yangu pale lengo kubwa ni kuongea na Lucy kuhusu mipango ya kazi.

Na tulikubaliana tuonane pale Mikocheni mitaa ya Scott Pizza “Lucy Lameck Road”. Na wakati nimefika hapa nilimpigia simu Prisca kumwambia atachukua boda afu tutakutana hapa.

Baada ya dakika 20 Lucy aliwasili maeneo haya na tulikaa kwenye kamgahawa kanatizamana na Barabara ya Mwaikibaki.

Baada ya kumaliza kuongea masuala ya kikazi tulianza kupiga story zingine.

LUCY: “Insider nina habari zako”

MIMI: “Habari gani?”

LUCY: “Si ulikuwa Zanzibar na Bossy?”

MIMI: “Aliyekwambia nani?”

LUCY: “Naamini huko Zanzibar umefanya kweli.”

MIMI: “Afu Lucy ujue unazingua sana, suala lako naona kama halitowezekana.”

LUCY: “Insider umepata opportunity lakini unashindwa itumia.”

MIMI: “Hivi unajua mimi na mke? na Iryn anatambua hili, hata kipindi kile hunioni alinisimamisha kazi sababu ya kumficha hili suala. Hii siri nimekupa wewe tu ole wako uitoe.”

Ilibidi nimpe story nzima Lucy kuhusu hili sakata lilivyokuwa.

LUCY: “Now nimeelewa, Iryn anakupenda ameshindwa kukaa mbali na wewe. Kama unaona huwezi date naye fanya kumla iwe friend with benefits, na hakikisha unamgonga kisawasawa, mtoto laini yule sidhani kama anakutana na mapigo ya kibabe.”

MIMI: “Lucy naona hauko serious yule namchukulia kama Bossy ujue.”

LUCY: “Angalia usije ukakosa vyote, au unataka nikupe mbinu?”

MIMI: “Unazingua sana.”

LUCY: “Naomba hata elfu 10 bhasi.”

MIMI: “Hii hela nakupa ila utakuja kuilipia siku.”

LUCY: “Umemshindwa Iryn utaniweza mimi?”

Na muda huu nilimwona Prisca akishuka kwenye boda na alikuwa amesimama pembeni akitoa simu yake kama anataka kumpigia mtu. Na baada ya sekunde kadhaa simu yangu ilianza kuita, na nikaipokea.

“Insider uko wapi naiona gari ila wewe sikuoni.”

“Niko kwa ndani hapa wewe sogea hapo kwa gari nakuja tuondoke.”

Lucy alikuwa anashuhudia kinachoendelea maana alikuwa anamwona Prisca.

LUCY: “Insider ile ni pisi yako? We fala una nyota aiseee.”

MIMI: “Ndo ujue huna hadhi ya kutembea na mimi, fala wewe.”

Lucy aliishia kunifyonza na tukaanza kutoka eneo lile ili tuondoke. Na baada ya kufika kwa gari nilim-hug Prisca na wakasalimiana na Lucy, tukaondoka eneo hili.

“Insider utaniacha kwa Mwalimu hapo mimi narudi ofisini.”

Baada ya kumdrop Lucy, niliendesha gari mpaka Masaki na nilipark gari pale “The tribe” ndo tulikubaliana tungeonana pale na Muajemi, muda huu ilikuwa ni jioni tayari. Kwa upande wangu nilikuwa na wasiwasi sana na Muajemi maana nilikuwa nawaza sana muda huu.

Baada ya mhudumu kufika kwenye meza yetu, dada alianza kumsikiliza Prisca na mimi nikaagiza juice.

“Bae si umesema tunatoka kwaajili ya dinna kwanini unaagiza juice?”

“Kuna mtu na mazungumzo naye kwanza afu nitaagiza food.”

“Okay let me wait ukimaliza maongezi tutakulaa wote, dada niletee juice for now.”

Ilimchukua dakika 10 Muajemi kufika eneo hili na alikuja moja kwa moja mpaka kwenye meza yetu. Tulisalimiana na nikamtambulisha Iryn kama mpenzi wangu, na Muajemi alifurahia sana utambulisho huu.

Tulitafuta meza nyingine tukakaa na tukaanza mazungumzo yetu pale.

MUAJEMI: “Bro nina dakika 10 tu za kuongea na wewe maana kesho nasafari ya Iran.”

MIMI: “Mbona haraka hivyo?”

MUAJEMI: “Nahitajika huko ndomana ni urgent.”

MIMI: “Na unarudi lini?”

MUAJEMI: “Sijajua bado kwakweli ila tutakuwa tunawasiliana Bro!”

MIMI: “Nambie Bro! ulisema una mazungumzo na mimi.”

MUAJEMI: “Bro Nashukuru nilipata muda wa kukaa na kuzungumza na Iryn kule Zanzibar ila nimegundua anakuamini sana. Kaka hivi hujawai shawishika kumtamani kabisa Iryn?”

MIMI: “Kaka hapana kwakweli yule ni Bossy wangu na tumetokea kuelewana sana ndomana unaona anakuja hata room yangu analala, sababu ananiamini.”

MUAJEMI: “Bro! nimegundua wewe ndo unayeweza kunisaidia kumpata Iryn ama laah! Na mimi nataka wewe ndo unisaidie kwa hili.”

MIMI: “Bro mimi naona kwasasa kama unatumia hisia na sio akili, ukitumia hisia utafeli. Suala la mahusiano sio la kuforce linahitaji muda na akili pia. Iryn ni msomi, mtu mzima na hana shida na pesa kama wanawake wengine unatakiwa utambue haya.”

MUAJEMI: “Kweli Bro!”

MIMI: “Labda nikuulize kule Zanzibar ulimgusia suala la mahusiano?”

MUAJEMI: “Nilimgusia kidogo na hakuonesha sign yoyote mbaya.”

MIMI: “You have to be patient, nikuulize swali la mwisho unataka nini exactly kutoka kwa Iryn? Mahusiano au Sex?”

MUAJEMI: “Bro nataka mahusiano awe mke wangu kabisa, Bro nataka wewe ndo unisaidie hili na kama utafanikisha nitakupa pesa ya mtaji unaotaka kufungua duka la Lubricants na nitakununulia gari nzuri kabisa ya Kutembelea. Bro sina muda hapa maana na mtu naenda kuonana naye Posta tutawasiliana kwa simu”

Na muda huu alitoa Pesa na kunikabidhi.

“Bro hii itakusaidia na shem, Bro unajua kuchagua shem yuko vizuri sana.”

Na muda huu tuliishia kucheka na tukasogea mpaka meza aliyokuwepo Prisca, alimuaga na akaondoka.

Muda huu tulimuita dada na tuliagiza chakula, ukweli ni kwamba toka nianze mahusiano na Prisca nilikuwa sijawai kumtoa out tukapata Dinna kama leo. Na hii siku Prisca alionekana kufurahia sana.

PRISCA: “Insider yule mwarabu ni nani?”

MIMI: “Sio mwarabu ni Muajemi.”

PRISCA: “Okay na mna ajenda gani? Maana niliwaona mpo deep sana kimazungumzo.”

MIMI: “Prisca sisi ni wanaume sio kila kitu lazima ujue ni masuala ya kazi tu.”

PRISCA: “Sawa bhana.”

MIMI: “Afu kwanini jana umenipigia simu usiku? Unasahau makubalino yetu?”

PRISCA: “Kama nimekumiss nafanyaje?”

MIMI: “Nilikwambia nitext kwa Whatsapp na sio kupiga simu.”

PRISCA: “Wewe simu zangu ulikuwa hupokei, pia nimesajili namba mpya anajuaje kama mimi?”

MIMI: “Hiyo sio sababu naomba uelewe nachomaanisha, tafadhali Prisca.”

PRISCA: “Insider mimi siwez kwakweli kwasasa nawivu mkubwa na wewe.”

MIMI: “Una ny*ge wewe huna lolote.”

Tuliondoka Masaki saa 2 kasoro kurudi Mbezi Beach na tulivyokaribia kuna lodge tuliingia na tulimaliza hamu zetu pale.

Nilirudi home na baada ya kuoga nilikaa kitandani na nikaanza kuwaza yale maneno ya Muajemi, ni kama yalikuwa yakiniingia vizuri muda huu.

“Biashara nahitaji na gari pia nahitaji, yaani nikose hivi vitu kisa Iryn? Hapana nitahakikisha nalifanikisha hili jambo vizuri kabisa.”

Kwa upande mwingine nilianza kuyakumbuka maneno ya Lucy aliyosema nisipokuwa makini naweza kosa vyote. Ofcourse nilianza kupatwa na kawivu fulani muda huu na nilikosa maamuzi, nilikuwa Dilemma.
 
EPISODE 35

ENDELEA…

Jumanne nilimpeleka Mchepuko wa Mzee kuanza mafunzo ya Udereva pale Posta na alianza kuendesha kwa kutumia mashine za kisasa (SEDIRO). Nilimwacha pale na nikaenda kuonana na Maggy maana nilikuwa nataka kuongea naye suala la kutafuta apartment kwaajili ya Iryn.

Nilimkuta Maggy ofisini kwake na tukaanza maongezi ya kunitafutia apartment nzuri ya kisasa maeno ya msasani mpaka Mbezi beach na iwe full furnished.

MAGGY: “Insider hilo halina shida, hii apartment kwaajili ya nani?”

MIMI: “Kuna dada mteja wangu anahitaji.”

MAGGY: “Kama ya wifi unasema bhana usifiche maana maisha yako ya mahusiano siyajui”

MIMI: “Maggy au unafikiri nampangia mtu? Hizo dolali mimi natoa wapi?”

MAGGY: “Anaweza kuwa demu wako, maana yule dada (Mbotswana) na wasiwasi.”

MIMI: “Hahahaa afu atakuja soon alinambia utamtafutia apartment pia.”

MAGGY: “Haina shida, Insider kuna jambo nataka kukushirikisha rafiki yangu.”

MIMI: “Nambie Mummy ni jambo gani hilo?”

MAGGY: “Insider nimepata kazi Taasisi “X” na nina kwenda kuwa Mkuu wa Idara.”

MIMI: “Hongera Mummy nimefurahi sana kusikia hivyo jamani.”

MAGGY: “Nitakwenda Dodoma makao makuu ya Taasisi.”

MIMI: “Lini unaondoka?”

MAGGY: “Bado sijajua ila utaratibu ukikamilika nitakujulisha. But nitakumiss sana Insider ujue.”

MIMI: “Haya mambo tutaongea ukiwa unaondoka, mimi naumia mteja wangu unaondoka but sina jinsi. Kila jambo ni mipango ya Mungu.”

MAGGY: “Kweli Insider, sasa ishu ya apartment nitaanza ifanyia kazi then nitakujulisha.”

MIMI: “Sawa jitahidi kabla ya mwisho huu wa mwezi mambo yawe yamekaa sawa.”

MAGGY: “Na bajeti yake ikoje?”

MIMI: “Budget sidhani kama tatizo sana ila nitaongea naye afu nitakupa majibu.”

Baada ya kumalizana na Maggy nilimpigia simu Iryn nimpe taarifa kwamba nimeanza mchakato wa kutafuta apartment na pia nimuulize kuhusu bajeti aliyopanga. Lakini simu yake ilikuwa haipatikani nikapiga kwa mara nyingine tena ikawa haipatikani. Na muda huu mchepuko wa Mzee alinipigia simu kwamba yuko tayari nikamchukue nimrudishe Mbweni.

Baada ya kumchukua nilimwambia tunapitia Masaki ili miwachukue madogo na yeye hakuwa na pingamizi. Ndani ya masaa 2 tulikuwa tuko pale Mbweni tayari na baada ya kumshusha, Jane alisema niingize gari ndani.

“Insider usindoke bila kula tafadhali.”

Na mimi nilingia ndani kupata lunch na baada ya kushiba nilikaa seblen na nilikuwa naongea na mama yake Jane. Muda huu nilipata ujumbe kwa Whatsapp na ulionekana umetoka kwa Maggy na niliufungua palepale. Maggy alikuwa kanitumia picha za apartment nzuri sana na ilikuwa furnished, nikampigia simu chap

MIMI: “Maggy hiyo Apartment ni nzuri sana ipo wapi?”

MAGGY: “Ipo Msasani hiyo ni nzuri kama inawezekana aseme niishikilie maana kuna watu wanaitaka pia.”

MIMI: “Ngoja nimpigie simu afu nitakurudia, gharama zikoje?”

MAGGY: “$1,200 tu.”

Nilimpigia tena simu Iryn lakini ilikuwa haipatikani ikabidi nimcheki kwa whatsapp lakini alikuwa hayuko online pia, nikaplan kwenda kwake badae.

Jioni nilitoka pale Mbweni na lengo langu lilikuwa kwenda kwa Iryn, lakini wakati natoka pale Mbweni Mzee alinipigia simu akanambia badae niende kwake. Sababu nilikuwa karibu na Mzee nikamwambia niko around na sio muda mrefu nitakuwa pale nyumbani.

Niliwasili Ununio kwa Mzee Pama na nikapiga honi pale getini na alitoka kaka kufungua geti ambaye ni mfanyakazi wa pale.

Nilipark gari na nikaingia ndani seblen na nilimkuta Mzee akiwa amekaa seblen yuko na bint wanaongea.

MZEE PAMA: “Kijana huyu ni Bint yangu wa mwisho na amemaliza form 6 mwaka huu.”

Bint yake alinisalimia na akaondoka eneo hili,

MIMI: “Mzee hongera sana kama huyu ni Bint wa mwisho bila shaka wengine watakuwa ni wakubwa sana.”

MZEE PAMA: “Bint yangu wa kwanza yuko Canada na anafanya kazi huko, anayefuatia yuko chuo Australia, kabla ya huyu wa mwisho kulikuwa na mwingine ambaye alitangulia mbele za haki.”

MIMI: “Aisee pole sana.”

MZEE PAMA: “Nimebarikiwa kuwa na Mabint tu, ila Jane atanizalia dume la kuendeleza ukoo.”

MIMI: “Hongera sana bila shaka kwasasa unafuraha.”

MZEE PAMA: “Nafuraha sana, kijana mwanaume unatakiwa usikose mtoto kwa Kiume, huwa nawashangaa sana watu hasa mwanaume anakwambia nataka mtoto wangu wa kwanza awe wa kike, nawaonaga wamekosa akili kichwani.”

MIMI: “Kwanini Mzee?”

MZEE PAMA: “Mtoto wa kiume ndo aneyekuza na kueneza ukoo, mtoto wa kike akishakuwa na kuolewa sio wako tena, maana hata watoto wanakuwa ukoo wa baba.”

MIMI: “Mzee upo sahihi hata mimi mara yakwanza nilitamani sana kupata mtoto wa kike ila kwasasa najivunia kupata dume.”

MZEE PAMA: “Una mtoto?”

MIMI: “Ndiyo mzee pamoja na mke sema hatukawahi kukaa na kuongea mambo ya kifamilia ndomana, ila nilipanga kukwambia.”

MZEE PAMA: “Hongera sana Kijana ndomana upo serious kumbe una familia.”

MIMI: “Na mtoto mmoja na mwezi ujao atakuwa anatimiza mwaka.”

MZEE PAMA: “Mama yake ndo yule ambaye tulikuwa naye siku ile?”

MIMI: “Hahahaaa hapana Mzee yule ni mchepuko tu.”

MZEE PAMA: “Hahahahahaahha Kijana una mambo sana, kwasisi wanaume ni kawaida ila nikwambie jambo, kuwa makini sana na hawa michepuko wanaweza kukuharibia furaha yako. Unavyokuwa na mchepuko hakikisha anajua una mke ili asikusumbue pia ijali familia yako kwanza, yeye awe wa mwisho. Kumbuka wewe umemfata kimasilahi akutimizie haja zako hata yeye kwako atakuwa kimaslahi, uwe makini sana.”

MIMI: “Ahsante sana Mzee kwa ushauri, namchepuko sababu nakosa mambo fulani tu kwa kipindi hiki, maana wife yuko busy na kulea na anasoma pia.”

MZEE PAMA: “Naelewa sana na tunafanya hivi ili kuepusha ugomvi.”

MIMI: “Mzee ulinambia kuna jambo muhimu la kuongea.”

MZEE PAMA: “Hali yangu kiafya kwa sasa haiko vizuri nataka kwenda India kufanya vipimo na nitakuwa kule kwa week 2, nimekuita ili unisaidie kuhakikisha Jane anakuwa dereva mzuri na good news leo amenipa report kuwa ameanza mafunzo.”

MIMI: “Mzee kwa hili ondoa shaka nakuhakikishia utafurahi.”

MZEE PAMA: “Sina shaka na wewe nakuamini sana. Nitakupa pesa kwaajili ya mafuta ya ile gari na pesa zako za usafiri wa kumpeleka Posta. Nauli ya kwenda na kurudi ni tsh ngapi?”

MIMI: “Ni kama 30,000 kwenda na kurudi itakuwa 60,000/=.”

MZEE PAMA: “Haina shida vipi kuhusu gari performance ikoje barabarani? Kama kuna shida sema tuirudishe mapema.”

MIMI: “Mzee gari ipo vizuri sana na ile rangi imependeza kwelikweli.”

MZEE PAMA: “Endelea kuiendesha usiipark ndani, nataka uendeshe kama kuna tatizo turudishe hili ndo lengo la kukuachia, usiogope sawa?”

MIMI: “Haina shida Mzee.”

Mzee aliingia ndani na alitoka akiwa ameshika bahasha ya kaki mkononi ikiwa imekunjwa.

MZEE PAMA: “Hizi ni 2,500,000/= utakata pesa yako ya nauli kwa mwezi 1 inayobaki ni kwaajili ya mafuta na mambo mengine yatakayojitokeza kule mwenye mafunzo ya Jane. Nataka hiyo gari uende nayo hata Morogoro na kurudi ili ujue ulaji wa mafuta na hapa sasa utaisoma na kuielewa gari vizuri.”

MIMI: “Mzee haina shida nitakwenda nayo Dodoma mwisho wa mwezi huu.”

MZEE PAMA: “Hapo safi, sasa acha mimi nikapumzike maana kesho ninasafari naomba utanipeleka Airport maana jioni ndo naondoka.”

MIMI: “Haina shida mzee ahsante sana.”

Muda huu ilikuwa usiku tayari umeingia hivyo nikaamua kurudi zangu home mapema. Usiku huu Prisca alinipigia simu, tena alikuwa anapiga kwa fujo nikaamua kuizima simu na mimi nikalala.
*********

Kesho yake asubuhi wakati niko Posta na Maggy alinisisitiza sana kabla ya mchana niwe nimempa majibu kuhusu ile apartment maana nikichelewa kuna mtu atailipia. Na mimi nilimwambia kama mpaka mchana ikiwa kimya ampe mtu mwingine sababu anayetaka hapatikani.

Na muda huu nilipiga simu kwa Iryn tena mbele yake na ilikuwa haipatikani.

MIMI: “Maggy sijui atakuwa na shida gani maana hapatikan toka jana ujue.”

MAGGY: “Kwani mara ya mwisho mmewasiliana lini?”

MIMI: “Jumapili tulikuwa wote nikamdrop kwake baada ya hapo hatukuwasiliana jana ndio nilimpigia simu nimwambie kuhusu apartment na simu yake ikawa haipatikani.”

MAGGY: “Huenda kaibiwa simu au kapatwa na matatizo, umejaribu kwenda kwake kuangalia?”

MIMI: “Hapana sijaenda bado ila leo nakwenda.”

MAGGY: “Fanya hivyo mimi nahisi atakuwa kaibiwa simu.”

Tuliagana na Maggy na mimi nilikwenda Mbweni kwaajili ya kwenda kumchukua Jane na mapema nilikuwa nimefika pale kwake.

Baada ya kuwasili pale kwa Jane nilikaribishwa ndani ili nimsubiri maana alikuwa anajiandaa. Na muda huu nilikaribishwa Dining kupata breakfast.

Jane alitumia dakika 30 kujiandaa na baada ya kutoka tuliondoka kuelekea Posta. Na wakati tukiwa njiani alikuwa akiniangalia sana nikiwa naendesha gari.

“Naona unatizama kwa makini sana.”

“Yaani! najifunza hapa taratibu niko makini sana.”

“Soon tu utamasta cha muhimu wewe concentrate tu.”

Nilimshusha pale Posta kituo anachojifunzia na mimi nikaenda zangu kwa Maggy. Kipindi hiki nilikuwa navyorudi na Jane Mbweni naunganisha na watoto wa kule Masaki hivyo nilikuwa napiga ndege wawili kwa jiwe moja.

Baada ya kumrudisha Jane kwake, Mapema kabisa nilikuwa pale Ununio kumchukua Mzee nikiwa na Dualis na nilimkuta yuko tayari ni kama alikuwa ananisubiri mimi tuondoke. Nilichukua bag lake la nguo nikaweka kwenye buti na tukaanza safari ya kwenda JNIA.

MZEE PAMA: “Familia haijambo?”

MIMI: “Nashukuru Mungu iko salama kabisa.”

MZEE PAMA: “Maendeleo ya Jane unayaonaje?”

MIMI: “Kwasasa kutoa neno inakuwa ngumu tumpe muda kwanza.”

MZEE PAMA: “Nikishuka Airport nitaikagua gari vizuri ila kwa ndani nimeridhika.”

Tulitumia kama Lisaa na nusu kuwasili pale JNIA Terminal 3 na baada ya kushuka Mzee alitumia muda huu kuikagua gari na akaridhika.

Niliagana na Mzee kwa miadi ya kuonana akirudi na aliniomba sana nihakikishe ulinzi kwa mke wake.

Baada ya kuachana na Mzee niliondoka JNIA na plan zangu kichwani ni kwenda Kijitonyama kwa Iryn. Niliwasili kwa Iryn saa 12 jioni na nilipark gari nje na nikaingia ndani na nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye apartment yake.

Nilijaribu kufungua geti na mlango lakini alikua kafunga, nilijaribu kugonga lakini hakukuwa na majibu yoyote. Mazingira yalionesha hakuna mtu pale, kwa upande wa jirani naye alikuwa hayupo maana hata gari yake haikuwepo eneo hili, hivyo nilijua bado hajarudi kutoka kazini.

Nilikaa pale nje kibarazani kama lisaa hivi na hapakuwa na dalili za Iryn kurudi wala majirani zake. Na muda huu nilipata wazo la kumpigia simu Lucy kama atakuwa na mawasiliano na Iryn lakini hakupokea simu yangu, na mimi nikawasha gari kuondoka eneo hili.

Wakati niko mataa ya Mwenge niliwasiliana na Mama wa2 nikampa taarifa napitia kwake na yeye akasema yupo.

Ndani ya dakika 20 nilikuwa pale kwake mitaa ya Rainbow na nilikaribishwa ndani.

MAMA WA2: “Mkwe unaendeleaje.”

MIMI: “Salama kabisa pole na kazi.”

MAMA WA2: “Aaaah Ahsante sana na wewe pia.”

MIMI: “Mama mkwe mimi sina mambo mengi ila nimekuja kupunguza mkopo wa lile deni letu.”

Na muda huu nilitoa bahasha mfukoni ambayo ilikuwa na zile pesa, na nikamkabidhi.”

“Mama mkwe hizo ni million 5 nimeziotea sehemu hivyo nimeona bora nipunguze deni.”

MAMA WA2: “Insider usinambie umepata lishangazi mara hii umeipata million 5 na ulikuwa unalalamika biashara ni ngumu.”

MIMI: “Mama mkwe wewe unaona mimi wa kulelewa? na hustle kila kona kupata hela.”

MAMA WA2: “Nakutania Mkwe, Insider itabidi nikufahamu na kwako hata kama unakaa geto.”

MIMI: “Hili ondoa shaka utapafahamu tu usiwe na wasiwasi.”

Nilimuaga Mama wa2 na wakati niko kwa gari mawazo ya kifisi yalinijia kichwani ya kuonana na Prisca. Nilichukua simu na kumpigia simu na ndani ya sekunde kadhaa alipokea na akanambia yuko Shoppers anafanya shopping, nikamwambia anisubiri nakuja.

Nilifika Shoppers na nikapark gari vizuri na nikaingia ndani supermarket, sikutaka kumpigia simu na nilivyoingia ndani nilianza kumsaka kwenye mashelfs na nilimwona mdogo wake Ivy na nikampa ishara ya “shhh” [emoji2958]. Nikazunguka upande wa pili ndo nikamwona Prisca nikamziba macho, na muda huu Ivy alikuwa anacheka sana.

Prisca na mdogo wao wa mwisho Ivy walikuwa wanapatana sana.

PRISCA: “You must be Insider.”

MIMI: “Hahahaa umemaliza shopping?”

PRISCA: “Ndo namalizia hapa.”

MIMI: “Fanya chap niwapeleke.”

Tulitoka pale Shoppers na tulielekea kwao na mimi nilipark gari nje kabisa getini. Prisca alishuka na Ivy akanambia anakuja, na haikuchukua muda Prisca alirudi na akaingia ndani ya gari.

PRISCA: “Insider umenunua gari mpya?”

MIMI: “Hapana hii sio yangu.”

Na muda huu nikawasha gari

PRISCA: “Vipi tunakwenda wapi? Mbona sikuelewi Insider.”

Muda huu mimi akili ilikuwa inawaza ngono tu.

Sikumjibu kitu na mimi nikakanyaga mafuta mpaka lodge tuliyokwenda mara ya kwanza kule whitesand.

PRISCA: “Insider muda huu unanileta huku na mama yuko home.”

MIMI: “It won’t be long, just an hour.”

Tulitumia kama lisaa na nusu kupeana utamu na baada ya hapo tukaondoka na nilianza kumrudisha Prisca kwao, na wakati tuko pale kwao nje getini alionekana Mary naye alikuwa ndo anarudi. Sikutaka kumsalimia, kwanza nilikuwa na gari mpya hivyo ingekuwa ngumu kunijua kwa muda ule na niliwaacha na Prisca wakiongea pale nje getini.

Ukweli ni kwamba nilianza kuwa addicted na Prisca kwenye suala la ngono hata yeye alikuwa vivyohivyo. Maana kila nikimkumbuka Prisca nawaza sex tu, nilikuwa kama nimerogwa.

Prisca ni aina ya mwanamke ambaye kama unamla unatamani hata ukeshe naye maana alikuwa ananyumbulika vizuri sana kitandani, hata ukitoa wafilipino unajikuta mnara unasimama tena kwa kasi ya 5G.

Baada ya kurudi home niliingia bafuni kuoga na baad ya kuoga simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Lucy na nikaipokea.

MIMI: “Ndo unaamua kunipigia muda huu.”

LUCY: “Insider sorry nilikuwa na mteja ndo tumemalizana naye hapa na simu ilikuwa chaji.”

MIMI: “Ok haina shida hata kama umeamua kunidanganya.”

LUCY: “Kweli jamani.”

MIMI: “Bossy wako mnawasiliana?”

LUCY: “Mmhh hapana mara ya mwisho tumewasiliana Jumapili mkiwa Zanzibar.”

MIMI: “Iryn hapatikani kwenye simu toka jana, nimekwenda kwake pamefungwa.”

LUCY: “Mmh sasa atakuwa amekwenda wapi? na bila taarifa? Mbona huwa anatoaga taarifa hata kama amepata emergence.”

MIMI: “Mimi toka tuachane Jumapili ndo jana nilimpigia simu ikawa haipatikaniki nahisi kuna shida.”

LUCY: “Insider endelea ku-buy time kwanza huwezi kujua yule ni mwanamke pia.”

MIMI: “Yeah uko sahihi, usiku mwema.”

LUCY: “Goodnight.”

Niliwaza pale huenda labda kaondoka na Muajemi kimyakimya hajataka kutoa taarifa, na mimi nilikwenda kupata Dinna na nikarudi zangu kulala.
********

Alhamisi na Ijumaa nilizitumia vizuri kwa kumsimamia Jane kwenye mafunzo yake ya udereva. Kwenye upande wa kuendesha gari kwa kutumia mashine ya SEDIRO mwalimu alisema yuko vizuri hivyo jumatatu ataanza kuingia barabarani.

Nilikuwa nampeleka Posta na kumrudisha Mbweni kwa Dualis yake na hata alikuwa hajui kama ile gari ni yake, japo alikuwa akiisifia sana. Mzee alisema nisimwambie mchepuko wake chochote kuhusu ile gari, na mimi sikutaka kuongea jambo lolote kwa Jane.

Jumamosi nilifanya kuingia naye barabarani na nilikuwa na Ist, nilimfundisha kuendesha kwenye barabara za mitaani na alikuwa kidogo anajitahidi alionesha kujua kuendesha gari mapema.

Tulitumia masaa 3 kuendesha mitaani na tulirudi nyumbani. Jane alishaanza kuwa karibu sana na mimi maana tulikuwa tumezoeana vizuri na tulikuwa tunapiga story sana.

Pale Mbweni nilikuwa nishapazoea tayari na baada ya kuingia ndani nilipata lunch na nikaenda kupumzika kwenye sofa pembeni nikiwa na glass ya juice ya Pineapple.

Na muda huu Muajemi alinipigia simu kupitia whatsapp call na niliipokea simu yake kwa haraka sana.

MIMI: “Bro habari yako.”

MUAJEMI: “Salama sana za huko Dar es salaam.”

MIMI: “Bro! salama sijui wewe huko Iran.”

MUAJEMI: “Salama pia, Iryn hapatikani kabisa kwa whatsapp toka jumatatu anashida gani?”

MIMI: “Bro! sio wewe tu hata mimi, na kwake hayupo.”

MUAJEMI: “Unasema? sasa atakuwa wapi?”

MIMI: “Bro! I don’t know nimejaribu kila njia lakini sijafanikiwa kumpata bado.”

MUAJEMI: “Wasije wakawa wamemteka fanya kureport Police.”

MIMI: “Bro! Police sidhani kama ni jambo jema, soon nakwenda kwake pia nitaongea na majirani zake, ikishindikana ndo nitatafuta Plan B.”

MUAJEMI: “Bro! I’ll call you later.”

Muajemi alionekana kuchanganyikiwa sana na mimi nilianza kuingiwa na wasiwasi muda huu maana niliwaza sana pale.

“Kwasasa mimi na Iryn tuko close sana kama anasafari au jambo lolote lazima angenijulisha tu. Nilihisi huenda kuna jambo baya limemtokea na sio kawaida yake kutopokea simu au kutokupatikana, something fishy is going on.”

Niliaga pale Mbweni na nikaondoka kuelekea Kijitonyama kwa Iryn. Niliwasili pale Kijitonyama saa 11 jioni na baada ya kupark gari niliingia ndani na kwenda kwenye apartment yake. Niligonga tena mlango lakini hakukuwa na majibu hivyo ikabidi nifanye ujasusi wa kuikagua nyumba vizuri.

Nilizunguka kote na nilikuwa najaribu kufungua madirisha lakini yalikuwa yamefungwa na nikarudi kugonga mlango kwa Jirani maana gari yake ilikuwepo nje.

JIRANI: “Wow karibu jirani, karibu ndani.”

MIMI: “Acha leo niingie nitie baraka, lakini namazungumzo na wewe.”

JIRANI: “Jirani unataka kunambia nini?”

Na muda huu nilikuwa niko seblen tayari

MIMI: “Mara ya mwisho umemwona lini Iryn?”

JIRANI: “Last week ile siku uliyokuja tukaongea ndo tulionana, I remember kitu kama Alhamis.”

MIMI: “Toka ile siku hamjaonana tena?”

JIRANI: “Yes! kwani kuna nini?”

MIMI: “Jiran Iryn toka jumatatu hapatikani kwa simu wala whatsapp na hakuna taarifa yoyote aliyoacha, ndomana nikasema nije kwako labda kuna ujumbe amekuachia.”

JIRANI: “Hapana kwakweli na haiwezekani mtu asipatikane kwa simu from nowhere, Jiran something wrong. Iryn ni mwanamke mrembo na mzuri kupotea kwake kimazingara hivi lazima kuna shida, wasije kuwa wamemteka wahuni.”

MIMI: “Jiran tunafanyaje?”

JIRANI: “Twende Police kureport toka jumatatu ni parefu sana.”

Na muda huu Jirani (Rose) aliingia ndani na mimi nilibaki pale nje nikiwa na mawazo sana.

Muda huu nilianza kujilaumu kwa kutotilia maanani hili suala, niliwaza pale hata Police wangeniona mimi ni mzembe sana. Nilivuta pumzi ndefu sana na nilijikuta macho yangu yakiwa yamejaa machozi na mapigo ya Moyo yalianza kuongezeka spidi.

EPISODE 36[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Hayaaa ndio mambo sasaaa thank you brooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…