Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 36

“A TRUE STORY BY INSIDER”

Muda huu nilianza kujilaumu kwa kutotilia maanani hili suala, niliwaza pale hata Police wangeniona mimi ni mzembe sana. Nilivuta pumzi ndefu sana na nilijikuta macho yangu yakiwa yamejaa machozi na mapigo ya Moyo yalianza kuongezeka spidi.

CONTINUE….

Mtoto wa kiume nilitokwa na machozi muda huu na mawazo yalikuwa yananiambia Iryn atakuwa ametekwa. Nilitafakari pale, Muajemi ameondoka jumanne kwenda Iran na alisema kaongea na Iryn Jumatatu. Niliwaza huenda Muajemi kafanya jambo, haiwezekani iwe harakaharaka hivi, na muda huu Rose alitoka ndani akiwa amevaa skin jeans.

ROSE: “Jiran niko tayari tunaweza kuondoka.”

MIMI: “Sidhani kama Police ni muhimu kwa sasa nafikiri tuendelee ku-buy time kwanza, I have a plan.”

ROSE: “Jiran hivi hujui kwamba utajiweka kwenye matatizo? Maana mpaka sasa wewe ndo first suspect.”

MIMI: “I know, Iryn ana mama yake mlezi nadhani utakuwa unamjua, nafikiri tuwasiliane naye kwanza.”

ROSE: “Sijakuelewa Jiran unamaanisha nini?”

MIMI: “Kuna Mama Mzungu anakujaga hapa mwenye hizi apartments.”

ROSE: “Yule mama Mzungu ambaye anaongea kiswahili vizuri ni ndugu na Iryn?”

MIMI: “Exactly yule ni Mama mlezi wa Iryn na alikuwa rafiki wa mama yake kipenzi.”

Ilibidi nimpe historia kidogo kuhusu maisha ya Iryn mpaka kifo cha mama yake na mpaka Mama Janeth kuwa mama mlezi wake.

ROSE: “Jiran mimi sijawai kufaham kama yule Mama mzungu (Mama Janeth) ana undugu na Iryn, ila nilishawai kumwona mara 2 lakini sikujua kama ndo mwenye nyumba.”

MIMI: “Plan yangu kabla hatujakwenda Police ni bora niwasiliane naye kwanza huenda anajua kinachoendelea.”

ROSE: “Umewaza jambo zuri.”

Nilitoa simu yangu kwenye gari na nilitafuta namba za mama Janeth ambazo Iryn alinitumiaga kipindi kile napeleka mzigo kwake na nikazipata. Nilipiga ile namba lakini ilikuwa haipatikani na nilirudia kama mara 5 lakini ilikuwa haipatikani.

MIMI: “Jiran hapatikani acha niende Masaki kwake.”

ROSE: “Unajua anakoishi? Twende wote.”

Tuliondoka pale Kijitonyama na tulikwenda Masaki moja kwa moja mpaka kwa Mama Janeth. Baada ya kufika pale kwake nilipiga honi na baada ya dakika kadhaa alitoka mlinzi ambaye ndo nilikuwa namwona kwa mara ya kwanza na alikuja upande wangu, na mimi nikashusha kioo.

MLINZI: “Bro habari nikusaidie nini?”

MIMI: “Kaka nashida na Mama Janeth sijui nimemkuta?”

MLINZI: “Mama Janeth ni nani? Usije ukawa umekosea nyumba.”

MIMI: “Bro anaishi hapa hata week iliyoisha nilikuwa hapa, unaonekana ni mgeni hapa ndomana humjui, ana watoto wa2 wa kizungu wakiume na kike.”

MLINZI: “Kaka sasa nimekuelewa kama ulikuja week iliyopita huyo sijui mama Janeth atakuwa amehama, maana sisi tumehamia hapa Ijumaa na tunaweek tayari tuko hapa na huyu Tajiri nimeanza naye kazi muda mrefu sana.”

ROSE: “Kaka tusaidie kama yupo maana tumekuja kuonana naye kuna jambo muhimu sana tafadhali.”

MLINZI: “Hata mimi nawaona mmekuja kwa mazuri nayowambia nikweli kabisa, sisi tuna week hapa toka tuhamie.”

Ukweli nilikosa cha kusema na sikuielewa hii movie kabisa inavyokwenda, kitendo cha Iryn kupotea kimaajabu na kutopatikana na bado mama Janeth hapatikani na ninaambiwa amehama kilinipa maswali sana muda huu.

MIMI: “Jiran hii movie siielewi naona kama sina maamuzi kwa sasa.”

ROSE: “Hauna Plan B ya kumpata Mama Janeth?”

MIMI: “Ipo twende saloon huenda dada wa pale atakuwa na mawasiliano naye.”

ROSE: “Let’s go.”

Tulindoka maeneo yale na tulikwenda saloon yao ya kulekule Masaki na baada ya kufika pale nilikwenda moja kwa moja ndani.

Baada ya kuingia ndani niliwakuta wafanyakazi wakiwa busy sana na niliwasalimia pale.

“Sumaiya nimemkuta?”

“Yupo alikuwa around hapa ngoja nimpigie simu.”

Dada alitoa simu yake mfukoni akapiga simu na wakaanza kuongea pale,

“Anakuja unaweza msubiri pale kwenye coach.”

“Dada mimi niko nje parking namsubiri.”

Nilitoka ndani na nikaenda parking nilikokuwa nimepark gari.

ROSE: “Jiran what is going on?”

Na muda huu Rose alishuka kwenye gari na akasogea karibu yangu. Rose alionesha kuguswa sana na hili jambo na alionesha kunionea huruma sana.

ROSE: “Jirani pole sana najua unapitia wakati mgumu sana kwasasa ila tutampata akiwa mzima kabisa, hata mimi hili jambo limenigusa sana, kwa kipindi tulichoishi na Iryn, nimetokea kumpenda sana.”

MIMI: “Ahsante sana Jiran ngoja huyu dada aje tuone atakuwa na jambo gani.”

Baada ya dakika 10 Sumaiya alitoka na alikuja moja kwa moja mpaka Parking nilikokuwa nimepark gari. Sumaiya alikuwa ni msimamizi wa Saloon kwa upande wa Masaki kama alikvyokuwa Lucy msimamizi wa Mikocheni na Sinza.

SUMAIYA: “Hi Insider za wewe? Dada mambo?”

ROSE: “Safi za kwako?”

MIMI: “Umetuweka sana hapa ujue.”

SUMAIYA: “Sorry nilikuwa nina mteja nisingeweza kumwacha katika mazingira yale.”

MIMI: “I know usijali, nimekuja hapa kwa jambo moja tu.”

SUMAIYA: “Jambo gani Insider?”

MIMI: “Mama Janeth simpati kwa simu na nimekwenda kwake naambiwa amehama.”

SUMAIYA: “Mara ya mwisho tumeongea Jumapili na sijampigia tena maana sahivi hatuja pungukiwa na kitu na tukitaka kutoa mzigo si tunakucheki wewe?. Kidogo kumpigia simu kumepungua afu mauzo tunatuma report kwa Queen (Iryn).”

ROSE: “Na alikohamia unakujua?”

SUMAIYA: “Hapana hata alikokuwa anaishi before sikujui na sijawahi fika, mara nyingi mazungumzo yetu yanafanyika hapahapa ofisini. Si uwasiliane na Queen akupe namba zake?”

MIMI: “Mpaka nimekuja kwako kutafuta namba za Mama Janeth ni kwamba Iryn hajulikani aliko toka jumatatu, Mama Janeth ndo mtu pekee aliyebaki wa kuokoa hili jahazi maana tunataka kureport Police.”

SUMAIYA: “Insider acha kupoteza muda wako, unahangaika kumbe amejifungia Hotelini na Bwana wake. Acha kupoteza muda amini maneno yangu hata uko Police usiende kabisa.”

Na muda huu Rose alimkata jicho kali sana Sumaiya.

ROSE: “Naona unaleta masikhara kwenye vitu serious mtu zaidi ya week asipatikane? haimake sense.”

SUMAIYA: “Nachoongea ni kweli, Insider jaribu kumpigia Bossy au mtext kwenye whatsapp.”

MIMI: “Sawa Ahsante miss.”

SUMAIYA: “Insider trust maneno yangu, ukimpata Queen nijulishe.”

Sumaiya hakuonesha kujali kabisa na alikuwa akileta matani sana muda huu. Na sisi tuliondoka eneo hili kurudi Mikocheni na muda huu Lucy alinipigia simu na tukakubaliana tukutane palepale kwa Iryn.

ROSE: “Jirani usipompata Mama Janeth Whatsapp tunafanyaje?.”

MIMI: “Nafikiri turudi home pale tuonane na jirani mwingine na pia kuna dada atakuja anasimamia saloon za Sinza na Mikocheni tutapata majibu.”

ROSE: “Sawa, zote ni saloon zake?”

MIMI: “Yeah zake.”

ROSE: “Yuko vizuri sana nilikuwa namchukulia poa sana.”

Tuliwasili pale Kijitonyama na tulimkuta Lucy kafika tayari anatusubiri sisi, na muda huu giza lilikuwa lishaanza kuingia.

LUCY: “Insider vipi umefanikiwa kuonana na huyo Mama Janeth?”. Lucy alikuwa hamfaham Mama Janeth.

MIMI: “Hapana kwakweli Mama Janeth hapatikani na pale kwake kahama.”

LUCY: “Amehama toka lini?”

MIMI: “Hata mimi sielewi kwakweli maana last week jumanne nilikuwa pale kwake, leo tunaambiwa amehama.”

ROSE: “Mimi nahisi mlinzi hajataka tu uonane na Mama Janeth.”

LUCY: “Hata mimi nahisi hivyo.”

Na muda huu tulisikia geti likifunguliwa na alikuwa ni yule jamaa Jirani. Baada ya kuingia ndani na kupark gari alishuka na alivyotuona tumesimama pale kwa Iryn ilibidi asogee.

JAMAA: “Habari zenu Majirani, vipi kuna usalama hapa leo?.”

Na wote tuliipokea salamu yake

ROSE: “Jirani hapa hakuna usalama, ndugu yetu Iryn hajulikani aliko na mara ya mwisho kupatikana kwenye simu ilikuwa jumatatu.”

MIMI: “Labda Jirani mara ya mwisho ulimwona Iryn lini?”

JAMAA: “Nilimwona jumatatu jioni wakati narudi kazini na alikuwa amesimama hapo kibarazani, tulipungiana mikono na mimi nikaingia ndani.”

Na muda huu Jamaa alikwenda kusimaa eneo alilokuwa Iryn.

MIMI: “Mpaka sasa tuna uhakika Iryn Jumatatu alikuwa maeneo haya, sasa nini kimetokea asipatikane kwa simu na bila kuwa na taarifa yoyote?”.

JAMAA: “Bro! Wanawake wana siri nyingi sana labda nikuulize toka mkutane na shem mna muda gani?”

MIMI: “Tuna miez mi-nne sasa.”

ROSE: “Mimi nafikiri tu ripoti Police hili jambo mapema, naona hili suala linazidi kuwa gumu sana.”

JAMAA: “Unakuta huyu mtu amekufa huko ndani au alitekwa kwa maelezo yanayotolewa hapa mimi nafikiri hivyo.”

ROSE: “Guys twendeni Police jamani!”

LUCY: “Police hapana mimi Roho inaniambia Iryn yupo somewhere, Insider huwezi kutafuta means ya kumpata mama Janeth kama whatsapp hapatikaniki?”

MIMI: “Itabidi Jumatatu sasa niende ofisini kwake.”

JAMAA: “Bro mara ya mwisho ulikuwa na shem lini?”

MIMI: “Tuliondoka Ijumaa kwenda Zanzibar na tukarudi Jumapili usiku.”

JAMAA: “Mlitoka wawili tu?”

MIMI: “Hapana tulikuwa watatu afu Iryn sio mpenzi wangu kama mnavyofikiri ni mtu wangu wa karibu.”

Ilibidi niwape mkanda mzima wa kule Zanzibar tangu tunakwenda na kurudi na sikutaka kuficha suala la Muajemi.

JAMAA: “Kwa maelezo yako inaonesha huyo Muajemi anamtaka Iryn kwa njia yoyote ile na hatuwezi jua mpaka Iryn anakubali offa yake kwenda Zanzibar alipewa nini. Bro hawa wanawake sometimes wanasiri nyingi sana huenda amekula Pesa za jamaa nyingi sana. Kama dada alikuwa anamkazia huenda jamaa kaamua kumfanyia kitu mbaya wanasema usishindane na tajiri. Swali langu lingine kwanini akuage haraka anakwenda Iran?, something crazy is going on, kama alimwekea sumu huko Zanzibar ambayo itamwuua taratibu utajuaje?”

Maneno ya Jamaa yalituingia vizuri kila mmoja alikuwa anaguna tu muda huu, jamaa aliongea point sana.

ROSE: “So what’s next?”

JAMAA: “Tufungue mlango tuangalie ndani kwanza kwa suala la Police inaweza kuwa msala zaidi, Bro wewe ndo utakuwa kikaangoni na msala wote utabaki kwako ujue, sisi wengine tutakuwa mashahidi tu.”

ROSE: “Una maanisha tuvunje geti na mlango?”

JAMAA: “Yeah atleast tutapata picha nzuri ya kuanzia.”

ROSE: “Huoni kama tutasababisha majanga zaidi kama Police wakitambua kuwa mlango umevunjwa?”

JAMAA: “Vitasa vinarudishika vizuri hili lisikupe shida kabisa, idea ya kwenda Police mimi sikubaliani nayo.”

LUCY: “Hata mimi naunga mkono huko Police tutaenda kukuza mambo tu.”

Lucy alikuwa hataki kabisa kusikia masula ya Police na alikuwa akipinga waziwazi.

Muda huu wote tuliunga wazo la Jamaa kuhusu kubomoa geti ili tujue ndani kuna nini. Na muda huu jamaa alifanya mawasiliano ili kumpata mtaalamu wa kufungua pale na baada ya nusu saa fundi alikuwa amefika na mashine ya kazi.

Ilimchukua fundi dakika 30 kuweza kufungua lile geti pamoja na ule mlango wa kuingilia sebleni na alifungua kitaalamu sana.

Baada ya jamaa kumaliza kazi yake tulifanya malipo na tukamwambia aende ila kesho tutampigia kwaajili ya kufunga vitasa. Lengo letu asijue kinachoendelea pale.

Muda huu milango ilikuwa wazi ikitusubiri sisi kuingia ndani ili tujihakikishie kama Iryn yuko ndani ama laah. Kila mmoja alionekana kuwa na wasiwasi sana na hofu ilitawala mahali hapa, Rose alikuwa anatetemeka na alianza kusali muda huu. Mimi ndo niliyekuwa wakwanza kufungua mlango na kuingia ndani.

TO BE CONTINUED

Kudadekii kama utuonjesha ganda la embe halafu ukatupokonya… mzigo umesimama [emoji91][emoji91] wacha tusubiri
 
Kila nikisoma iriny naweka shepu ya hamjsa sura uwoya miguu lulu
Ni yeyeee
FB_IMG_16927419746346834.jpg
 
Nilipokuwa katika harakati za kutafuta mwenza, Mama aliwahi niambia "huko mjini nenda taratibu mshaija, hii dunia ina mambo mengi si mchezo, sio kila king'aacho ni dhahabu."
For sure hasa uku pwani majini siku hizi hadi social netwok yapo
 
Back
Top Bottom