EPISODE 39
ANONYMOUS : “Hi Insider.”
MIMI: “Iryn?”
ANONYMOUS: “Yes It’s me, I have Missed you so much.”
CONTINUE……..
MIMI: “Ni wewe kweli? Mbona kama siamini?.”
IRYN: “It’s me Insider, Ijumaa narudi naomba uje kunipokea Airport na tutaongea vizuri but am safe and ok.”
MIMI: “Sawa mummy, I’m happy you’re alive.”
Iryn alionesha kuwa mpole sana na sauti yake ilikuwa ya utulivu sana, sikutaka kumuuliza maswali muda huu maana Ijumaa anarudi hivyo tungeongea. Kwa upande mwingine nilikuwa na hasira kwa kitendo cha kuondoka bila kunipa taarifa kilinikera sana, niliona ni dharau yaani muda wote huo ndo ananitafuta leo?.
Na muda huu Mama J aliingia chumbani na akaanza kulalamika
MAMA J: “Baba J hivi kwanini hautaki kula chakula cha nyumbani?”
MIMI: “Nakuja kula ni lini sijala?”
MAMA J: “Mara nyingi tu, kama hauli uwe unatoa taarifa sio tunapika chakula kingi afu kinaharibika sio vizuri.”
MIMI: “Sawa Mummy, Iryn best yako kanipigia sio muda hapa.”
MAMA J: “Weeh, yuko wapi? Na kwanini atutese hivi?”
MIMI: “Amesema Ijumaa anarudi, ndo tutajua alikuwa wapi.”
MAMA J: “Labda alikuwa kwa Bwana wake”
MIMI: “Maybe itakuwa hivyo.”
Na muda huu niliweza kuwasiliana na Lucy na nikampa taarifa juu ya kuwasiliana na Iryn, na alifurahi sana kusikia Iryn kanitafuta.
********
Jumatatu nikiwa Posta baada ya kumshusha Jane pale shuleni, niliwasiliana na Mzee pama kupitia whatsapp na akasema yeye yuko Egypt anategemea kurudi weekend hii. Nilimwambia maendeleo ya mke wake Jane jinsi anavyojitahidi kwenye mafunzo ya udereva na Mzee alifurahi sana kuzisikia habari hizi.
“Mzee unaonaje tukimpa gari yake ili awe na hamasa zaidi?”
“Kijana naona mapema sana subiri nirudi weekend tuone progress yake.”
“Sawa haina shida.”
Baada ya kuwasiliana na Mzee ilibidi nimpigie simu Rose na kumpa taarifa juu ya kuwasiliana na Iryn na aliripuka na furaha kubwa sana.
“Jiran hajasema yuko wapi na hana tatizo lolote?”
“Hajasema ila yuko sawa kabisa na sehemu salama tusiwe na wasiwasi.”
“Na anarudi lini?”
“Mmh hapana hajasema bado ila nafikiri soon.” Sikutaka kumwambia Rose kama Iryn anakuja Ijumaa.
Niliamua kwenda kwa Maggy ofisini kwake ili tukazungumze suala la apartment maana nilijua Iryn akirudi lazima atauliza tu. Nilimkuta Maggy ofisini kwake na alivyoniona alionesha kufurahi na akanikaribisha nikae kwenye coach.
MAGGY: “Insider karibu sana nimefurahi kukuona.”
MIMI: “Nashukuru sana Maggy kazi zinakwendaje?”
MAGGY: “Ndo kwanza mapema vipi nikupe kahawa?”
MIMI: “Yeah itapendeza kama ipo.”
MAGGY: “Afu nilisahau kukuuliza kuhusu yule dada vipi amepatikana?.”
MIMI: “Ndio yaani jana kanipigia whatsapp call, amesema Ijumaa anarudi.”
MAGGY: “Bora amepatikana kwakweli.”
MIMI: “Nimekuja kwaajili ya lile suala la Apartments inabidi uanze kuziandaa ili akija tukacheki.”
MAGGY: “Sawa ila alikosa apartment nzuri sana ile siku. Yaani! ungeiona ilivyokuwa nzuri afu very cheap.”
MIMI: “Tafuta zingine nzuri kwa yale maeneo niliyokwambia. Mimi sikai sana hapa nataka nikukimbie mamaa.”
MAGGY: “Insider tunaweza kutoka out this weekend? kama utakuwa na nafasi.”
MIMI: “Vipi ndo unataka kuniaga nini? washakupigia simu?”
MAGGY: “Hapana bhana, nitakwambia wakinipigia simu.”
MIMI: “Sawa unanirusha Roho ujue, tutawasiliana cha muhimu ni uzima tu.”
MAGGY: “Byee Insider.” Huku ananipungia mkono.
Niliondoka na kwenda kumchukua Jane maana alikuwa kanipigia simu yuko tayari. Baada ya kumchukua tulikwenda moja kwa moja Masaki na nilimwambia tunapitia kwanza sehemu. Lengo langu nipitie pale Saloon ili niangalie kama mambo yanakwenda vizuri, nilikuwa nina wasiwasi sana na Sumaiya nilikuwa simwamini kabisa.
Baada ya kufika pale saloon nilipark gari na nikamwambia Jane narudi ndani ya muda mfupi. Niliingia ndani kwanza nikaanza kufanya ukaguzi wa ndani then nikatoka nje lakini sikuridhika na mazingira ya pale nje na muda huu Sumaiya alikuwa katoka pale nje.
SUMAIYA: “Unavyokuja himaya za watu uwe unatoa taarifa.”
MIMI: “Yaani Bossy wako atoe taarifa kwako?”
SUMAIYA: “Sawa Bossy bora umekuja nipate na Lunch.”
MIMI: “Msimamizi unakosa pesa ya lunch? au una kiben ten unakihudumia?”
SUMAIYA: “Mimi mwenyewe hapa nataka kuhudumiwa, ila Insider hapa pagumu sana CCTV camera kila kona, na bado mteja akilipia unampa risiti ya EFD unaanzaje kujiongeza?”
MIMI: “Hamna bonus hapa?”
SUMAIYA: “Inategemea na mauzo ya mwezi kama target imefika na Queen ndo aliye tuanzishia bonus.”
MIMI: “Kumbe Iryn anawapenda sana, sasa kinachofanyaga humpendi ni nini? Au sababu kakuzidi uzuri?”
SUMAIYA: “Tuachane na haya, vipi Queen umempata?”
MIMI: “Yeah yuko somewhere safe.”
SUMAIYA: “Fyooh! eti somewhere safe, Queen anagongwa huko wewe unamtetea hapa shauri zako.”
MIMI: “I wish ayasikie haya maneno uyoongea hapa, sijui kama utaendelea na kibarua hapa.
SUMAIYA: “Labda wewe umwambie, nakuona naye close sana vipi na wewe unaweka pale?”
MIMI: “Ile sio level yangu, wewe ndo level yangu sasa.”
SUMAIYA: “Acha kuwa kama Aristote kazi kuzurura na kina Uwoya na kushika mikoba, Insider wewe unaonekana ni mhuni kabisa, mzalishe Queen au hutaki kupata mtoto awe na mama mzuri kama yule?”
MIMI: “Sio kila kinacho ng’aa ni Almasi fala wewe.”
SUMAIYA: “Huenda kaamua kwenda kupunguza ny*ge sababu wewe unashindwa hii kazi, but remember not everyone in this life gets a second chance.”
Na muda huu alisogea upande wangu kama ananinong’oneza
“Hakikisha unamkula Queen akirudi, bora umtongoze akukatalie kuliko kukaa kimya utafikiri sio mwanaume bhana”. Na akaingia ndani kwa madaha akiniacha pale nje bila majibu.
Nilitumia kama dakika 15 pale Saloon na tukaondoka kuwachukua madogo shuleni na safari ya Mbweni ikaendelea. Muda huu tulikuwa tunapiga story na Jane pia yeye alikuwa makini sana kuniangalia navyo drive gari.
JANE: “Insider hawa watoto wanakupenda sana, unawapaga nini?”
MIMI: “Hahaa naishi nao vizuri tu ndomana.”
JANE: “Ukiona watoto wanakupenda hivi jua nyota yako ni nzuri sana.”
MIMI: “Mmmh kweli?
JANE: “Sure my mama told me.”
MIMI: “Maybe, mtoto ukiwa naye karibu always atakupenda. Hivi Mzee Pama mlifahamianaje?”
JANE: “Hahahahaa mzee tulikutana Serena Hotel ndo tukabadilishana namba mpaka leo nina mimba yake.”
MIMI: “Aisee hongera sana umelamba bingo kubwa sana, vijana wangeishia kukuchafua tu.”
Jane aliishia kucheka tu hakuwa na neno lolote, na baada ya kuwasili kwake nilimshusha na mimi nikaondoka maeneo yale.
Wakati niko njiani nilimpigia simu Prisca lakini akaendelea na ujeuri wake wa kutokupokea simu na mimi nikasema sitamfuti tena, niliwaza huenda Prisca hana mimba yangu ila anatafuta attention tu kutoka kwangu.
*******
Alhamis nilifanya kazi ya kuzikagua Saloon zote, maana kesho Ijumaa Iryn alikuwa anarudi. Asubuhi baada ya kumdrop Jane niliamua kwenda Masaki kwanza kukagua, na baada ya kufika pale niliweza kuonana na Sumaiya.
Niliuliza kama kuna tatizo lolote la kiofisi, kama kuna mashine mbovu na tatizo lolote, lakini hakukuwa na tatizo lolote kulikuwa sawa. Kutokana na mazingira ya nje kuwa mabaya ilibidi nimtafute mtu wa kupruni maua na miti ili yawe na mpangilio mzuri.
Usafi wa nje ulifanyika kikamilifu na mazingira yalipendeza sana muda huu,
SUMAIYA: “Insider……”
MIMI: “Mimi ni Bossy wako embu nipe heshima yangu.”
SUMAIYA: “Sawa Bossy, leo sijakuelewa Queen anarudi lini?”
MIMI: “Kufanya usafi ni kazi yangu sio mpaka Iryn arudi haya ndo majukumu yangu.”
SUMAIYA: “Kwa leo umeupiga mwingi sana acha nikupe sifa zangu.”
MIMI: “Nikajua unanitunuku” tulikuwa tunaongea huku tumesimama pembeni ya gari hivyo nikamsogelea nikambana kwenye gari vizuri.
SUMAIYA: “Insider acha ujinga huoni tuko Parking hapa.”
MIMI: “Ujanja wote kumbe hujiamini, sasa twende wapi?” Na mimi nikamwachia muda huu.
SUMAIYA: “Hakuna mjanja kwenye ny*ege afu Insider wewe ni mhuni sana.”
MIMI: “Unaonesha kama umependa hivi,“
Na mimi muda huu nilikuwa naingia kwenye gari ili niondoke,
SUMAIYA: “Sijapenda wala nini, naomba hela ya lunch bossy.”
MIMI: “Pesa zangu unataka kumbe.”
SUMAIYA: “Bhana Insider unanipa hunipi?”
Nilitoa noti mbili za elfu 10 nikampa muda huu,
SUMAIYA: “Ahsante, ukiendelea kuwa hivi utafanya nikutunuku.”
MIMI: “Hata usijaribu.”
Always mimi ni mtu wa utani sana hasa kwa watu wanaonizunguka ndomana akina Sumaiya, Lucy walikuwa watani zangu sana. Maana matukio yote ya kiutendaji walikuwa wanaripoti kwangu kasoro mauzo tu.
Na mimi nikaondoka maeneo haya kuelekea Posta kumchukua Jane ili nimpeleke Mbweni. Nilianza kuwachukua madogo pale shuleni nikaenda Posta kumchukua Jane hao tukaanza safari.
Baada ya kumalizana na Jane nilichoma mafuta kuelekea Sinza ili niendelee na kufanya ukaguzi wa Saloon, niliamua kuanza na Sinza then nimalizie na Mikocheni.
Baada ya kuwasili pale Sinza niliwasalimia na niliwauliza kama kuna tatizo wakasema taarifa zote anazo Lucy. Baada ya kuridhika na mazingira ya pale ofisini nilikwenda Mikocheni na niliweza kuonana na Lucy, ofcourse Lucy alikuwa serious sana na kazi yake ndomana Iryn alikuwa anampenda sana. Hata kupewa simu ilikuwa halali yake kabisa, alikuwa anajituma sana.
MIMI: “Nimetoka Sinza pale wanasema maagizo yote yapo kwako.”
LUCY: “Sure tunahitaji makeup, Peruvian hair nknk.”
MIMI: “Ok sawa ila kwa Iryn nafikiri vitakuwepo.”
LUCY: “Sawa tutakwenda wote kuangalia.”
MIMI: “Ok tuondoke.”
LUCY: “Bossy ndo anarudi kesho?”
MIMI: “Yeah ndo alisema hivo.”
LUCY: “Hajakutafuta tena?”
MIMI: “Bado nafikiri atanicheki badae nijue ata-land muda gani.”
LUCY: “Utanambia alikuwa wapi akikwambia.”
MIMI: “Sidhani kama atasema ukweli maana hata mimi kanikera.”
LUCY: “Sasa unakereka nini wakati sio mpenzi wako?”
MIMI: “Kitendo cha kuondoka bila taarifa, hivi si ningekuwa matatizoni sana, mpaka wewe ujue.”
LUCY: “Yeah sure hapa alikukosea sana, mimi nahisi alikuwa na huyo Muajemi au alikuwa Ufaransa kwa bwana wake.”
MIMI: “Maybe, hivi Lucy Biashara ya Sinza inafanya vizuri kama hii Mikocheni?”
LUCY: “Sio sana atleast, unajua sisi tunauza wigi original na bei zake zimemechangamka kidogo, si unajua wabongo hawapendi vitu OG? afu Wateja wetu asilimia kubwa wanatoka nje na sio Sinza.”
MIMI: “Ok sawa nimekuelewa.”
Tuliwasili pale kwa Iryn na baada ya kuingia ndani Lucy aliingia chumba kingine na alifanikiwa kuvipata vile vitu na akaondoka akiniacha mimi pale.
Muda huu niliamua kwenda chumbani kulala maana nilikuwa najisikia uchovu sana. Lakini niliendelea na upekuzi wangu kama kawaida na nilifungua drow iliyokuwa na handgun. Baada ya kutoa lile box kwa chini kulikuwa na Notebook nzuri sana yenye kava linalovutia.
Nilianza kuifungua ile notebook lakini kwenye page ya kwanza mwanzoni ilikuwa imendikwa
“MY DEAR DAUGHTER IRYN”.Nilipata shauku ya kujua ndani kuna nini na niligundua ilikuwa ni kama diary ambayo mama yake alikuwa anaiandika toka akiwa mjamzito. Mama yake alindika mambo mengi sana toka Iryn akiwa anazaliwa mpaka kifo chake, na aliandika azikwe Ethiopia kwao.
Nilijua siri nyingi sana kupitia diary japo nilikuwa nakosea kusoma lakini sikuwa na jinsi muda huu. Kwenye diary mama yake aliandika mali zote alizokuwa anamiliki kuanzia nyumba na Biashara na Pesa anazomiliki Bank zote kwa Tanzania mpaka Ethiopia pamoja na mafao aliyoacha kazini. Pia nilijua mama yake alikuwa na duka la nguo Posta, Iryn hakuwai kunambia hili na pia alikuwa na Organization kubwa Ethiopia ambayo pia Iryn hakuwai nambia hili.
Jambo lingine nilijua mama yake aliacha gari aina ya Range Rover lakini aliandika apewe Mama Janeth kama ukumbusho wa urafiki wao. Pia aliandika Mama Janeth ndo awe kama mama kwake kwa kila jambo na amuheshimu sana, aliandika pia ndugu zake wa kuwatembelea na pia aliandika maadui zake. Pia niliona picha za zamani za Iryn akiwa mtoto mama yake alikuwa amezibandika kwenye ile Diary.
Waraka ambao ulinitoa machozi ni siku aliyoandika kabla ya kifo chake, aliandika mambo mengi sana kwa bint yake na alimsisitiza sana kuishi vizuri na watu, azisimamie biashara zote vizuri na ajitahidi kwenda kuwatembelea watoto yatima na wote wenye uhitaji.
Na alimaliza kwa kuandika hivi, japo aliandika mengi ila haya ndo yalikuwa ya muhimu.
“Iryn wewe ndo Bint yangu pekee niliyefanikiwa kukupata nakuona kama dhahabu kwangu, naumia kukuacha bado ukiwa unanihitaji sana lakini mama yako safari imewadia hivyo sina budi kukuaga. Nimekutengenezea misingi mizuri ya maisha na niliwasaidia wengine pia, naomba na wewe ufanye zaidi ya nilichofanya mimi. Naomba uishi vizuri na watu hapa duniani na umuheshimu kila aliye mbele yako. Kama kuna sehemu nilikukosea naomba unisamehe hata Baba yako nimemsamehe natumaini Baba yako na mama Janeth watakuwa na msaada kwako. Mimi nitakufa kimwili ila kiroho tutakuwa wote, nitakuona tena mwanangu. GOODBYE MY DAUGHTER I LOVE YOU.”
Ni diary ambayo ilikuwa imeandikwa kwa kiingereza, Ukweli ni Diary ambayo ungeisoma ungeishia kulia tu, mama yake aliandika mambo mengi sana ya siri ambayo siwezi kuyaandika hapa. Pia nilijua Iryn anamchukia Baba yake lakini sio mpango wa mama yake kufanya hivyo.
Nilijifunza kuna umuhimu wa kuwaandikia watoto Diary kama ukumbusho ni muhimu sana kwa future. Nilikaa mpaka jioni pale na nikaondoka kurudi home maana muda ulikuwa umekwenda tayari ilikuwa saa12 jioni.
Mida ya saa 2 usiku nikiwa home nimetulia zangu chumbani Iryn alinipigia Whatsapp Video call.
IRYN: “Hi Insider.”
MIMI: “Am good Mummy you look great.”
IRYN: “Thank you and you too, I have missed you.”
MIMI: “Me too, you look so happy today”
IRYN: “Yeah Insider thanks God I’m great, hope to see you tomorrow.”
MIMI: “Mimi nipo Bossy wangu nambie unarudi muda gani.”
IRYN: “Ndege ita-land 12:30 mchana mida hiyo uwe around.”
MIMI: “Sawa Bossy wangu unaonekana kuwa mzuri zaidi.”
IRYN: “Thank you I have gifts for you, Mama J and my husband Junior, byee Insider.”
MIMI: “Byee have a good night.”
*********
Ijumaa ndo Iryn alirudi Tanzania alikuwa wapi? mimi nilikuwa sijui kabisa, haya maswali nilikuwa nasubiri afike ili nimwulize.
Niliwasili pale JNIA mapema na 12:30 mchana ilikuwa imenikutia pale. Katika ujinga niliofanya nilisahau kumwuliza Iryn atakuja na ndege gani. Nilishuka kwenye gari na niliingia moja kwa moja mpaka upande wa Arrival door nikaingia ndani.
Nilijaribu kuitext ile namba tuliyowasiliana na Iryn kupitia Whatsapp jana lakini haikuwa online na last seen ilikuwa toka asubuhi saa2. Nilimpigia simu Tyna kumuuliza ndege za kimataifa zinazo tarajia kutua muda huu mpaka saa7 mchana akanambia kuna Qatar Airways na Ethiopian Airlines.
Nilikaa mle ndani mpaka 13:15 nilivyoona kimya hakuna hata dalili nikatoka zangu pale nje nikakaa kwenye kiukuta na nilikuwa usawa wa arrival door na macho yangu yalikuwa yako focused na mlango.
Nilimpigia tena simu Tyna nikamwuliza kama kuna habari yoyote akanambia Ethiopia Airlines imesha land kama dakika 10 zilizopita na Qatar airways ita land baada ya dakika 5. Ndani ya dakika 10 watu walianza kutoka kwa wingi na mabag yao pale mlangoni na mimi macho yangu yalikuwa makini sana muda huu, lakini sikuona sura ya Iryn.
Niliendelea kukaa pale pale nje na baada ya dakika 20 watu walianza kutoka pale mlangoni na kuna watu walionekana kuja kuwapokea ndugu zao.
Macho yangu yalikuwa makini sana muda huu maana nilijua lazima Iryn anatoka soon. Niliamua kuingia ndani ili iwe rahisi kumwona Iryn, sasa kumbe yeye ndo alokuwa wa kwanza kuniona.
Nilisikia naitwa
“Insider……..” ile kugeuka mtu akaja haraka akani-hug kwa nguvu utafikiri watu ambao hatujaonana kwa muda mrefu. Na aliendelea kunikumbatia bila kuniachia na watu mle ndani walikuwa wakilishuhudia tukio hili live bila chenga, hata Mama Janeth ilibidi ashangae maana sio kwa ule mkumbato.
Iryn alimgeukia mama Janeth akamwambia ataondoka na mimi maana kuna watu walikuwa wamekuja wapokea na walikuwa wameshika mabag yao muda huu.
EPISODE 40[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu