INSIDER MAN
JF-Expert Member
- Nov 7, 2018
- 2,005
- 19,579
- Thread starter
- #5,141
EPISODE 49
“Insider kuna jambo naomba tuongee ila uwe honesty na mimi. Hivi kwanini ulikuwa unanitumia mimi kupata pesa kutoka kwa Muajemi?. Ulishawai hata sikumoja kunambia unashida nikakunyima? Kwanini ukaona utu wangu haufai kwako?.
CONTINUE…
MIMI: “Iryn unajua sikuelewi kabisa maneno unayosema, embu nambie ni nini kinaendelea.?”
IRYN: “Its okay Insider I got this, don’t worry.”
MIMI: “Ndo unambie tatizo ni nini, ukisema hivyo utakuwa unanikosea sana kwakweli, niambie kuna nini?”
IRYN: “Insider tuachane na haya maana hakuna umuhimu ya kuendelea kuyaongelea maana Muajemi ni best yako.”
MIMI: “Ni sawa Muajemi ni best yangu lakini sio kuyaamini maneno anayosema, tell me what’s really going on?”
IRYN: “I trusted you remember?”
MIMI: “Umejaribu kuwaza kama Muajemi anataka kutugombanisha? Naomba niambie Muajemi amesema nini?”
Na muda huu ilibidi nimsogelee karibu yake ili nimbembeleze,
IRYN: “Insider stop touching me.”
MIMI: “I am Sorry.”
Na mimi ilibidi niwe mpole tu maana niliona Iryn hasira zimepanda mpaka uso wake ulianza kuwa mwekundu. Hii ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona Iryn akipandwa na hasira hivi.
IRYN: “Kesho itabidi uende ukachukue mzigo Posta utawasiliana na dada nitakuingizia pesa kwaajili ya logistic.”
MIMI: “Sawa haina shida Bossy.”
Na mimi sikutaka kuendelea kubaki hapa maana niliona nimeyatibua tayari, niliona bora niondoke maeneo haya. Nilimuaga Iryn kuwa naondoka lakini hakunijibu wala nini.
Wakati niko njiani niliwaza huenda Muajemi ameyachomesha huko, niliwaza pia Iryn hajanambia mpaka sasa kama kaonana na Muajemi, kingine Muajemi hajanipigia simu na sio kawaida yake kabisa. Muda huu niliamua kumpigia simu Muajemi lakini hakupokea, nilipiga tena kwa mara nyingine lakini haikupokelewa.
Niliamua kurudi zangu home mapema sana maana nilikuwa na mawazo. Kwa upande mwingine toka Iryn anipe simu nilikuwa bado sijaanza kuitumia. Hivyo baada ya kurudi home nilitoka na ile simu nimeishika mkononi na nikaingia ndani.
Nilivyoingia ndani nilimkuta Mama J akiwa seblen anamnywesha uji Junior, nikaishia kumsalimia pale.
MAMA J: “Usinambie na wewe umenunua macho 3 hongera zako.”
MIMI: “Usinambie na wewe umeitamani simu yangu.”
MAMA J: “Sijaitamani nimekupongeza tu kwa maendeleo.”
MIMI: “Ahsante umepika nini kwanza naskia njaa hapa.”
Baada ya kula nilikwenda chumbani kuoga na nilikaa kwenye kiti nikipanga mipango yangu ya maendeleo.
Nilipiga hesabu za pesa nilizonazo nikapata jumla ya 15.8million, hizi ni pesa zote kuanzia alizonipa Mzee, Jane, mshahara, Muajemi, udalali na akiba zangu binafsi.
Nikajisemea milion 3 nitalipa deni kwa Mama wa2 afu kiasi kitakachobaki nitaendelea na ujenzi Dodoma kwaajili ya kuendelea na finishing. Niliwaza kufanya Jambo kama ukumbusho wa Mzee Pama hivyo nikapanga Madirisha ya Aluminium yatakuwa kama ukumbusho wangu kwa mzee kila navyo yaona.
Kwa hii pesa nilijua kabisa nakwenda kufanya finishing ya nyumba, hivyo vingebaki vitu vidogo sana vya kumalizia. Niliwasiliana na Mzee Mollel muda huu kuhusu kuendelea na ujenzi na yeye alisema ataandaa vijana wake waendelee.
******
Jumanne asubuhi baada ya kuwapeleka akina Maggy Posta, nilikwenda kuonana na dada Agent ofisini kwake na tuliongea kuhusu mzigo.
Kwa upande mwingine nilikuwa na mipango ya kuanza kujiongeza ili niwe napata pesa za ziada. Maana niliwaza nimeacha biashara ya Uber hivyo inabidi nitafute sana Pesa. Kwa upande mwingine nilijua dada lazima anacheza mchezo mchafu tu, niliplan kumbana kuhakikisha tunakula wote.
Baada ya kuonana na Dada alinambia niende jioni kwaajili ya mzigo na kila kitu kitakuwa sawa, na mzigo utakuwa ushapelekwa store tayari.
Baada ya kutoka Posta nilikwenda moja kwa moja mpaka Kairuki Hospital kuonana na Prisca sababu alikuwa amekwenda kujiandikisha kwaajili ya kuanza clinic. Ilibidi niende pale kama Baba mtoto kwajili ya kujaza taarifa zangu.
Baada ya kuwasili pale nilionana na Prisca na alikuwa ameongozana na Eva. Tulikwenda kuonana na Doctor tulijiandikisha na akatuchukua vipimo vyote mpaka damu.
Kwa upande mwingine maendeleo ya Prisca yalikuwa ni mazuri mpaka ukuaji wa mimba ulikuwa ni mzuri sana. Hivyo Doctor alisisitiza sana Prisca awe anapata utulivu wa kutosha pamoja na kula lishe bora.
Prisca alinambia anatarajia kuanza mitihani ya final exams (UE). Na alisema akimaliza hategemei kurudi kwao lakini nilimwambia hili suala hatakiwi kulificha sana amwambie hata mama yake. Baada ya kumaliza taratibu zote ilibidi niwaage na wao walifanya kurequest usafiri wa kuwarudisha chuo.
Baada ya kutoka Kairuki mimi nilikwenda mpaka Mikocheni kushinda na Lucy ili niendelee ku-buy time ya kwenda Posta kufuata mzigo. Baada ya kuwasili pale niliweza kuonana na Lucy.
LUCY: “Insider mida ya lunch hii twende Golden fork nikakupe offa leo, pia nina mazungumzo na wewe.”
MIMI: “Sawa Lucy mimi sina tatizo kabisa.”
Tuliondoka pale na break ilikuwa parking za pale Golden fork. Baada ya kupark gari tulishuka na tukatafuta angle nzuri tukakaa. Mhudumu alikuja kuchukua odda na baada ya kila mtu kuagiza chakula tuliendelea na story zetu.
MIMI: “Nambie Bossy wangu.”
LUCY: “Insider unatoka na Sumaya?”
MIMI: “Hapana achana na yule mropokaji.”
LUCY: “Mhh unajua ile siku Iryn alibadilika sana niliona hata hamu ya kuendelea kubaki pale ilimkata.”
MIMI: “Nilishamwambia mapema Sumaiya ni mropokaji asipende kumsikiliza.”
LUCY: “Kuwa naye makini sana acha mazoea naye ya kijinga atakuharibia shauri zako. Anyway nimefurahi kuona kwasasa ninatuma report kwako sasa huu ni wakati wa sisi kupata hela.”
MIMI: “Kwanini unasema hivyo mummy?”
LUCY: “Insider hapa unaponiona ninategemea hii kazi kupata kula na mahitaji mengine. Unajua pia ninaishi na mama yangu namuuguza anaumwa umwa, bado namsomesha mdogo wangu yuko form 6. Baba yetu alikufa so tumebaki watatu tu pamoja na mama. Pia nina mpango mwaka huu kurudi chuo nikajiendeleze kusoma na bachelor naona muda unakwenda sana, lakini nitakuwa nasoma evening classes.
MIMI: “Aisee pole sana unamajukumu mazito sana rafiki yangu.”
LUCY: “Ndomana huwa nawaza kama Iryn akifunga biashara nitakuwa kwenye hali gani, yaani sijui.”
Ukweli nilipatwa na huruma sana muda huu, sikutaka hata kumwambia kama Iryn atarudi South Africa mwezi octoba. Maana ningeishia kumchanganya tu.
MIMI: “Usiwaze riziki anatoa Mungu na sio mwanadamu. Nambie una mpango gani unataka nishirikisha?”
LUCY: “Insider ipo hivi mimi nina watu wa kuwauzia hizi wigi hasa Brazilian na Peruvian na aina zingine kibao za nywele nina wateja wengi sana. Unajua wigi za Iryn ni nzuri zinapendwa sababu ni OG, sasa msala nikiuza nyingi nje hapa ofisini mzigo utakwama, na Iryn akiona zinaisha kwa haraka atapata wasiwasi maana pia tutaua brand yake ya biashara.”
MIMI: “Sasa wewe ndo unashinda hapa ulikuwa na mpango gani dear?”
LUCY: “Insider kwa wigi moja kama nitauza minimum sikosi 30k, kama ntauza wigi 100 hapo ni 3m hatukosi hata kwa mwezi, tunagawana half utakuwa na shida gani?. Sasa hili litakuwa ngumu kama mzigo utakuwa constant hapo inatakiwa ufanye juu chini Iryn aongeze mzigo. Ukifanikisha hili tutapiga hela sana mimi naweza pambana kwa mwezi tukauza hata wigi 100 kwa watu tofauti na nikaendelea tafuta wateja wengine.”
MIMI: “Nawaza namna ya kumuingia Iryn japo alisema anataka kuniachia suala la mizigo niwe nafatilia mimi yeye atakuwa analipia tu.
LUCY: “Insider fanya kutembea na Iryn ukithubutu hili naamini utaweza kumcontrol na tukapiga sana hela. Tambua Iryn amekupa majukumu mapya sababu anakuamini sana. Ukifanikiwa kumla naamini kila utakacho mwambia atakuwa anakubali kama suala la Sinza amekubali kufunga kwasababu yako na mimi alinigomea unafikiri nini?”
MIMI: “Ok nimekuelewa sasa kwani ukiuza wigi zote nje kuna shida? Maana mzigo huwa unakuwepo store.”
LUCY: “Ni sawa kumbuka mzigo ukija Iryn anakadiria wa kutumia mwezi au miezi kumbuka kuna Saloon 3. Sasa kama nitauza kwa magendo hapa ofisini mzigo utakata afu pia tutaacha maswali kwa Iryn, maana atashtuka kuona mzigo kuisha haraka. Sitaki tufike huko utanifukuzisha kazi hapa njia nzuri wewe mshawishi aongeze Supply tu. Kumbuka pia tunakwenda ofisi mpya itakuwa na CCTV camera hali itakwenda kuwa mbaya zaidi.
MIMI: “Nimekuelewa hili niachie mimi nitalifanyia kazi sawa?”
LUCY: “Insider Iryn anakupenda sana wewe hujui tu, unaweza kumfanya kuwa side chick wako na maisha yakaenda ikiwezekana mzalishe kabisa. Umepata bahati ya kuwa karibu na mwanamke mwenye Pesa ila naona hutaki kutumia hii opportunity, wewe pretend tu cha muhimu unapata pesa. Kuna siku utakuja kujuta kwa kuchezea bahati kama hizi, unajua hata hapa ofisini wanakusifia sana kuwa na pisi kali? Sasa wakijua wewe ni mshika pembe tu watakudharau sana.”
MIMI: “Naona lecture yako ya leo imeniingia sana kwakweli. Itabidi nianze kufanya jambo leo umeongea point tupu.”
LUCY: “Insider najua huo uwezo unao ila shida yako unaleta ubossy kwenye suala kama hili. Unasahau hata Iryn naye ni binadamu na wewe ndo kampani yake. Iryn hajataka kumpa uchi mwanaume mwingine ila akija kupata mwanaume nakuambia utakuwa umempoteza mazima.”
MIMI: “Lucy inatosha kwa leo mama.”
LUCY: “Sisi sote tuna makujumu na ni washikaji ukifanikisha kuwa karibu na Iryn naamini hata mimi nitakuwa na maisha mazuri. Ni hayo tu Insider usizingue tu, acha mimi niwahi saloon pale kuna mteja ananisubiri.”
Baada ya kuachana na Lucy nilikwenda Posta kwaajili ya kuchukua mzigo. Baada ya kuwasili Posta nilikwenda kuonana na dada ofisini kwake na aliomba nimsubiri kwa dakika kadhaa kuna documents anaziandaa ili tuondoke.
Na muda huu nikiwa nimekaa nikimsubiri nilikuwa nawaza namna ya kumwingia lakini nikasema acha kwanza.
Dada alitumia kama dakika 20 ndo tukatoka kuelekea kwenye store yao kule kurasini. Ulikuwa ni mzigo mkubwa ambao nilipakia kwenye canter na baada ya kumaliza alinipa documents zote. Na mimi muda huu nilifanya kuzikagua document zote na niligundua kuna document zina miss.
Nilikuwa natambua dada anafanya michezo kwenye kodi sababu Iryn hajui haya mambo na ingekua ni ngumu kuyajua, yeye alikuwa analipa tu na kupiga simu. Na pia nilijua anampiga sana Iryn kwenye storage fees, nikasema huyu lazima tule sahani moja.
Nilipanga kwanza kumchekecha Iryn then next time nitampandia ofisini kwake tuliweke sawa hili jambo. Nilisubiri kwanza Iryn anipe madaraka kwanza ya kufuatilia kodi za mizigo na masuala mengine.
Baada ya kumaliza process zote tuliondoka na nilipeleka ile mizigo yote Masaki saloon. Ofisi ya masaki ilikuwa kubwa kama nyumba hivi so kulikuwa na store kubwa sana. Mizigo iliingizwa ndani na mingine baadhi niliweka kwa gari nikapeleka Mikocheni.
Baada ya kutoka Mikocheni nilikwenda kuonana na Iryn kwake na nikampa documents za mzigo. Lakini kwa upande mwingine alikuwa kama mtu ambaye hayuko sawa hata maongezi yetu yalikuwa mafupi mafupi sio kama tunavyoongea siku zote.
MIMI: “Kwanini ulibadilisha Agent Bossy.”
IRYN: “Yule mjinga alianza kunisumbua ndomana niliamua kuachana naye.”
MIMI: “Ulisema utaniachia haya majukumu kidogo nipe elimu hapa kwenye kuagiza na mambo mengine.”
IRYN: “Kuagiza hili nitafanya mimi kazi yako wewe ni kuwasiliana na agent baada ya mimi kufanya malipo na nitakuwa nakupa documents. Kazi yako wewe kufuatilia mzigo mpaka unafika na masuala ya kodi yote yatakuwa chini yako ukishirikiana na Agent.”
MIMI: “Hapa nimekuelewa Bossy. Unapika nini leo?”
IRYN: “Insider wewe si unaona hapa nakata nyama.?”
Baada ya kumsoma maongezi yake niliamua kunyamaza kimya. Nilihisi Iryn bado hayuko sawa ana kinyongo na mimi na mawazo yalikuwa yakinituma ni Muajemi ambaye kaongea mambo siyo kwa Iryn.
Niliamua kumuaga Iryn lakini hakuonesha kunifurahia kabisa na mimi nikapotea maeneo yale. Njiani niliamua kumpigia simu Muajemi lakini alikuwa hapatikani kabisa, nikamcheki kwa whatsapp lakini wapi hakuwa online.
Nilianza kuwa njia panda kwakweli maana nilianza kujiuliza ni nini kinaendelea? Mbona toka Iryn aonane na Muajemi kwa siri amenibadilikia ghafla hivi? Na kwanini Muajemi hajanitafuta?. Ofcourse nilianza kuingiwa na wasiwasi muda huu, nilihisi Muajemi kuna maneno kaongea kwa Iryn.
Nilikuwa natamani sana kujua kilichoendelea kwenye mazungumzo yao ya Jumapili lakini Muajemi ndo hapatikani. Muda huu niliwaza kumpeleleza Iryn ili nijue, maana kama Muajemi angekua alifananikiwa lazima angenambia tu, ukimya wake ulikuwa unanipa wasiwasi sana.
*******
Ratiba zangu za asubuhi zilikuwa zinaendelea kama kawaida na baada ya kumshusha mama wa2 nilikuwa napiga story na Maggy kuelekea ofisini kwake.
“Insider nimepigiwa simu tayari, Jumapili nitaondoka hivyo naomba Jumamosi tuonane.”
“Sawa Maggy this week lazima tuonane.”
“Insider wewe unamambo mengi sana huchelewi kunikataa. Naomba Jumamosi kwenye ratiba zako unikumbuke na mimi.”
“Maggy I promise lazima tuonane weekend hii.”
Niliachana na Maggy na nilikwenda kuonana na dada wa clearing Agent. Baada ya kufika pale ofisini kwake ilibidi nimchane ukweli kuhusu kula wote na yeye hakuwa na noma kabisa. Maana nilimwambia ukizingua natafuta Agent mwingine najua uhuni unaotumia. Tulikubaliana na dada atakuwa ananipa 40% ya kitakachokuwa kinapatikana. Niliona kwa hizo percent hata sio mbaya ni kubwa kwa upande wangu.
********
Ijumaa ndo siku ambayo nilikuwa nina miadi na Jane ya kwenda Bagamoyo na ilikuwa tumeanza July tayari.
Hii siku Mary alinipigia simu asubuhi na akanambia anamaoengezi muhimu sana na mimi. Sababu nilikuwa nakwenda kwanza kuonana na Jane nilimwambia nitamcheki jioni nikiwa natoka Mbweni.
Saa 5 asubuhi nilikuwa nimewasili tayari pale Mbweni na nilipark gari nje getini nikaingia ndani.
Baada ya kuingia ndani nilimkuta mama akiwa seblen na tulisalimiana pale. Muda huu dada alinikaribisha chai na nikaenda dining kunywa. Mbweni palishakuwa nyumbani tayari na mazingira nilikuwa nisha yazoea tayari.
Na muda huu nikiwa dining Jane alitoka akiwa amevaa surual ya track na jaz ya Arsenal na chini alikuwa na raba sport.
“Nambie Insider, nakusubiri wewe tu ili tuondoke maana nina hamu sana ya kudrive leo.”
“Sawa dereva acha nikupe funguo kabisa utangulie mimi nakuja.”
Baada ya kunywa chai nilimuaga mama na nikaondoka pale seblen. Baada ya kutoka nje nilimkuta Jane amekwisha geuza gari tayari ananisubiri mimi tu. Na mimi niliingia kwenye gari muda huu,
“Usinambie umejua kugeuza gari tayari.”
“Insider unaniona lena sana eeh haya twende sasa, mimi leo ndo Dereva wako.”
“Mimi sikufundishi njia utajiongeza mwenyewe huko barabarani.”
Muda huu Jane alianza kudrive taratibu kuelekea Bagamoyo japo alikuwa anaonesha ulena ila alikuwa yuko vizuri hata break za haraka/papohapo zilikuwa zimepungua sana. Na mimi nilikuwa makini sana nikim-monitor kwa kila action barabarani.
Tuliingia Bagamoyo road na Jane alionesha umahiri mkubwa sana hata sikutegemea kuona Jane akiendesha gari vizuri na kwa utulivu sana. Na huku njiani nilikuwa namfundisha sheria za barabarani kama sehemu anayotakiwa ku-overtake, kuangalia vibao vya speed limit na sheria nyingine mbalimbali.
Aliendesha gari mpaka kibao cha kuingia Pwani ndo tulipigwa mkono. Traffic alikuja upande wa Jane na alikuwa anakagua leseni, uzuri alikuwa nayo na baada ya kujiridhisha akaturuhusu kuendelea na safari.
Jane aliendesha gari mpaka Bagamoyo na tukaizunguka ile roundabout kurudi tulikotoka. Lakini njiani nilipata wazo nimpeleke pale Horizon ili tupumzike kidogo tupate na lunch.
Baada ya kuwasili pale “The Horizon” tulitafuta sehemu nzuri tukakaa na haikuchukua muda mhudumu alikuwa kafika tayari kutusikiliza.
JANE: “Insider unakula nini? Utakachokula
wewe na mimi nitakula.”
MIMI: “Kaka leta Chips kavu na portion ya mbuzi choma.”
JANE: “Kaka mbuzi hawatoi ile harufu.?”
MHUDUMU: “Hapana dada wako vizuri hata usiwe na wasiwasi.”
MIMI: “Kama vipi kula kuku tu.”
JANE: “Nitakula Mbuzi Insider, Kaka usisahau na limao ya kutosha.”
Na muda huu niliendelea kupiga story na Jane na kikubwa aliomba ushauri kwani anataka kufungua biashara. Na mimi nilimshauri afungue mini-supermarket na awe anauza vitu kwa jumla na rejareja kwani zinafaida sana.
JANE: “Insider na vipi kuhusu mtaji na location?”
MIMI: “Mtaji ni wewe tu ila ukianza na million 30 utakuwa upo vizuri sana, hapa unapata frem ya uhakika na mzigo wa kutosha. Kuhusu location wewe usiwe na shaka kama utakuwa tayari mimi nitaongea na mama mkwe wangu na nitaweza kukutanisha naye akupe elimu juu ya hii biashara.”
JANE: “Insider kumbe una mke? ni Mary au?”
MIMI: “Hahahaha hapana Mary ni mshikaji wangu tu.”
JANE: “Mimi nilikuwa najua ni wifi yangu sio kwa kunicare kule jamani kumbe ni mshikaji tu, bhasi ni mchepuko wako.”
MIMI: “Hamna najua huwezi amini ila ndo ukweli wewe siku muulize.”
JANE: “Aisee hii ni noma bhasi she is in love with you. Mtoto wa watu kamuelewa mme wa mtu kama ilivyokuwa mimi tu.”
MIMI: “Hamna bhana wewe unaona hivyo ila Mary hana noma kabisa.”
JANE: “Sasa Insider nafikiri hii idea umenipa nzuri pia acha nikae chini nifikirie. Kwa upande wangu niliwaza kufungua biashara ya home decoration mpaka maofisini.”
MIMI: “Hio idea pia nzuri unaweza fanya hapo baadae, kwa hali yako hii kwasasa itakuwa ngumu maana inabidi uwe mfuatiliaji sana kwa mwanzoni. Ifikirie hii nilokupa maana unakaa dukani tu na mfanyakazi wako mmoja, idea yako unaweza ukaiacha kwa muda ukijifungua ukaendelea nayo.”
JANE: “Yeah ni kweli, umenipa idea nzuri sana, acha nitulize akili.”
Kwa upande mwingine Jane hakuwa na stress na maisha maana mpaka sasa alikuwa na pesa kibao kwa bank. Maana Pama kabla ya kifo chake alimuingizia Jane Pesa za kutosha sana. Bado pia alipewa pesa kwenye kikundi cha Pama na ile michango ya msiba bado alipewa so alikuwa vizuri sana.
Tulikaa pale mpaka saa 9 mchana ndo tukaondoka pale maana tulikuwa tumeongea mengi sana. Jane alikuwa na furaha sana hii siku kwani nilimpeleka mpaka kwenye kile kidaraja maarufu cha pale Horizon akapiga picha za ukumbusho.
Tuliondoka pale na aliendelea na usukani mpaka tunafika Mbweni. Na baada ya kuwasili pale Mbweni tuliingia ndani na nilimshauri Jane afuge Mbwa kwaajili ya ulinzi na yeye aliona ushauri wangu ni mzuri.
“Insider wazo lako zuri hili nitakuachia wewe udeal nalo.”
“Haina shida maana Mzee alijenga nyumba yao kabisa ni kununua na kuwaweka tu.”
Na mimi sikukaa pale nilimuaga Jane na nikaondoka maeneo yale. Muda huua akili yangu ilikuwa kumpigia Mary ili tuonane nimsikilize ana jambo gani.
Ilikuwa ni jioni tayari na baada ya kumpigia Mary simu alisema tuonane Upepo Garden, yeye yuko home nikiwa nakaribia nimwambie ili nimpitie pale kwa Zena.
Nilitumia kama nusu saa kuwasili pale kwa Zena na nikamchukua Mary tukaelekea Upepo garden.
Baada ya kuwasili pale tulikwenda kukaa kwenye chimbo ambalo huwa napendelea sana kukaa na Prisca.
MIMI: “Mary mimi leo sikai sana na wewe maana nimechoka hatari si unajua nilikuwa na Jane?”
MARY: “Waow! Wifi yangu maendeleo yake yakoje?
MIMI: “She is doing great for sure.”
MARY: “Nimefurahi kusikia hivyo baadae nitampigia.”
MIMI: “Nambie una jambo gani kwanza maana ulinisisitiza sana.”
MARY: “Okay, Insider unawasiliana na Prisca?”
MIMI: “Yeah mke wangu lazima tuwasiliane, vipi kuna tatizo?”
MARY: “Prisca sijui anashida gani maana ana weekend 2 hajarudi kabisa home na sio kawaida yake. Na tunakwenda week ya 3 sasa hajakanyaga home, Insider what is really going on? Au unaishi naye?”
MIMI: “Hapana Mary, Prisca alinambia soon wanaanza UE hivyo atakuwa kabanwa na masomo si unajua mwaka 2 ni mgumu sana?”
MARY: “I know ila naona ya sasa kama too much sometimes nahisi kama karudiana na yule jamaa yake.”
MIMI: “Mmhh sidhani ila itabidi nianze kumchunguza.”
MARY: “Anza kumfuatilia Insider maana mimi hata kwenda kumwona hataki anasema yuko busy hiki nacho kinanipa mashaka sana.”
MIMI: “Usijali nitaanza kumfuatilia ila leo kanambia anajiandaa na mtihani so yuko busy sana na kusoma.”
MARY: “Sawa kesho muombe muonane afu twende wote Insider.”
MIMI: “Sawa haina shida nitafanya hivyo ila wewe usimwambie chochote.”
Niliwaza pale Prisca anaficha suala la mimba lakini ataficha mpaka lini? Ikitokea kapata shida itakuwaje?. Niliona sio busara kuendelea kuficha hivyo niliona ni busara Mary atambue mapema kinachoendelea kwa faida yake.
Tulikaa na Mary pale Upepo Garden mpaka saa 2 usiku ndo tukaondoka maeneo haya. Mary alirequest bodaboda na mimi nilindoka kwenda nyumbani.
Wakati nimefika home niko kibarazani nikivua viatu simu yangu ilianza kuita lakini niliipotezea. Wakati nafungua kamba za kiatu cha kulia simu iliita tena bhasi nikasema acha niangalie ni nani anayepiga. Baada ya kutoa simu mfukoni ilikuwa ni namba ngeni ya Vodacom na nikaopokea ile simu.
MIMI: “Hello habari nani mwenzangu.”
ANONYMOUS: “Haujambo Kijana wangu mimi ni Mrs. Pama wa hapa ununio. Naomba kesho Mungu akijalia uhai tuonane hapa nyumbani, kwani nina maongezi na wewe very important.”
Naam! Ilikuwa ni simu ya Mrs. Pama akiomba tuonane, Je alikuwa anataka nini kutoka kwangu?.
EPISODE 50[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu