Blessed Keinerugaba
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 4,754
- 4,746
Sasa mkuu na wewe utuanzishie hiyo hadithi yako. Inaonekana itabamba sana.ubarikiwe kiongozi,
kwahili sakata lako nasemaga linafanana na langu, baada ya kumaliza chuo nilijichanganya kwenye boda, dah kila unachoeleza mulemule me huyo mdada alikuwa anaeka mikono ndani ya tumbo langu
watu hawakuelewi kabisa wanaona chai ila tuliopitia tunaelewa
nishapewa saa ya lak 8 na huyo dada acheni tu tuna siri nzito.
Vijana wa humu ni wajinga sana asipo kuelewa hapa atajutaUsije ukawa umelewa mwamba?. Usijaribu kuwaita tu wana-JF walio karibu, halafu kweli wakaja ukajoin nao wakakufahamu na wakamfahamu na Mary,baadae wakakuletea unoko mwamba. Kaa mbali
Watu wa humu ni wapumbavu sana. Yaani unawapa kitu kwa nia njema tu ila watakacho kufanyia hutaaminiI know I was just kidding sina ham na wanajf kabisa kwa walichofanya
Mzee tumegee kidogoubarikiwe kiongozi,
kwahili sakata lako nasemaga linafanana na langu, baada ya kumaliza chuo nilijichanganya kwenye boda, dah kila unachoeleza mulemule me huyo mdada alikuwa anaeka mikono ndani ya tumbo langu
watu hawakuelewi kabisa wanaona chai ila tuliopitia tunaelewa
nishapewa saa ya lak 8 na huyo dada acheni tu tuna siri nzito.
Massage ya wabongo hafanyi mbona.ngoja tuone itakuwajeTanzania nchi yangu.
Watu wanafume weeee wakati Iryn anatoka kumfsnyia mtu massage!!! Na hiyo ni kawaida Iryn kukumbatiana na wateja wake. Shida iko wapi hapo?
Hii!!! We INSIDER MAN jamaniiiiiiiiii😏😏😏This week Ijumaa.
@INSIDER MAN ni mzanaki[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kabila la wazanaki kama GENTAMYCINE huwa wana wivu kwa michepuko yako a.k.a KITUNGO kuliko kwa wake zao[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Watu8 Naam, Kodi la INSIDER MAN litaingia vitani rasmi aidha kibarua kiote nyasi au utabiri wako utimie.
Insider Jana nilikua Dynasty Kisha Bara Beach na kumalizia ziara Bahari Beach (zamani leger hotel) ningejua upo Kidimbwi ningekutafuta. Tatizo sikuingia kwenye hii Tamthilia mapema...
Nimecheka sana, maumivu ya kumuona Iryn akiwa na mwanaume mwingine yalizidi Yale ungeyapata kama ingekua Mama J ndio unamuona na mtu mwingine?
Bila shaka maneno ya Lucy yaligonga kichwa Mara mbilimbili
@INSIDER MAN ni mzanaki[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kabila la wazanaki kama GENTAMYCINE huwa wana wivu kwa michepuko yako a.k.a KITUNGO kuliko kwa wake zao[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Lucy na sumaiya walikushauri uzuriEPISODE 50
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
Jumamosi jioni nilikwenda Ununio kwaajili ya kuonana na Mrs Pama na wakati niko njiani nilikuwa najiuliza maswali mengi sana.
“Ni nini ambacho Mrs. anataka kutoka kwangu? na muda huu niliwaza huenda likawa suala la Jane.”
Niliwasili Ununio na baada ya kupiga honi nilifunguliwa geti nikaingiza gari ndani nikapark. Nilisalimiana na jamaa mfanyakazi wa pale maana tunajuana na akanambia Mrs Pama yuko ndani. Nilikaribishwa ndani muda huu na baada ya kuingia nilikuta kuna watu wapo sebleni, nilisalimia na mimi nikakaa.
Baada ya dakika chache alitoka Mrs Pama na tukasalimiana na hii ndo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza tunazungumza na Mrs.
“Karibu sana Kijana uwe na amani, nashukuru sana kwa kutii wito wangu.”
“Ahsante sana mama nashukuru sana, hata hivyo hii sio mara yangu ya kwanza nakuja hapa. Mara nyingi nikija unakuwa haupo.”
“Nafikiri huwa tunapishana na pia mambo ya kazi.”
Na muda huu dada aliniletea juice kwenye kombe kubwa la glass.
“Dada nafikiri hii juice ipeleke pale nje kwenye hema tunatoka hapo. Kijana wangu nafikiri tutoke nje tukaongee maana hapa seblen kuna wageni itakuwa sio busara kuwatoa.” Mrs aliongea kwa sauti ya chini sana.
Tuliondoka seblen na tulikwenda nje kukaa garden na kulikuwa na hema pale. Na mida huu maongezi yaliendelea.
MRS. PAMA: “Mwanangu sitaki kukupotezea muda maana najua unamajukumu mengi sana.”
MIMI: “Usiwe na shaka na mimi mama.”
MRS. PAMA: “Kuna mambo nilitaka kukuuliza kuhusu Mzee, maana nimepata taarifa wewe ndo ulikuwa kama rafiki yake sana enzi za uhai wake. Nimepata taarifa hata hapa nyumbani ulikuwa unakuja na pia nilikuona msibani kule Tabora. Niseme ahsante sana kwa yote.”
MIMI: “Ni kweli mama Mzee alikiwa kama rafiki kwangu na alikuwa kama Mzee kwangu maana alinifundisha sana kuhusu maisha. Na sisi tulifahamiana kupitia Uber, mimi ni dereva wa Uber. Mara ya kwanza kukutana na mzee alinipenda ndo nikawa nafanya naye kazi nyingi sana.”
MRS. PAMA: “Nilitaka kujua kama mzee kuna jambo lolote on-going alikuachia, maana nimejaribu kufuatilia nimeona mara ya mwisho alikuingizia kiasi cha Pesa milion 6. Hiki ni kiasi kikubwa sana kama kuna jambo lolote naomba niambie.”
MIMI: “Ni kweli mama hicho kiasi mzee alinitumia. Ila alinitumia baada ya kuongea naye na kumwambia biashara ya Uber imekuwa ngumu, pia aliniahidi angenitafutia kazi. Hiyo pesa alituma inisaidie pale nilikokwama bad news baada ya siku 3 nikapata taarifa za kifo chake.”
MRS. PAMA: “Haina shida nilitaka kujua kama kulikuwa na suala lolote linaendelea kati yenu. Na vipi kuhusu Jane mlifahamiana lini?”
MIMI: “Jane tumefahamiana toka mwaka jana.”
MRS. PAMA: “Ulikuwa unajua kama Mzee anajenga nyumba Mbweni?”
Niliona Mrs ameanza kuvuka mipaka maana maswali aliyoanza kuuliza ni kama anatafuta ushahidi.
MIMI: “Hapana mama hayo mimi sijui kwakweli.”
MRS. PAMA: “Okay kijana mimi ni hayo tu nilikuwa nayo niseme Ahsante sana kwa kuitikia wito, karibu tena hapa ni nyumbani.”
MIMI: “Ahsante mama pia poleni sana kwa msiba.”
Ni maongezi yaliyochukua kama nusu saa hivi na niliondoka pale Ununio. Ukweli sikujua dhumuni la Mrs Pama kuniita maana niliwaza kwa yale maswali ni kama alikuwa anatafuta jambo alijue. Na pia alionesha kutoridhika na majibu yangu, ni kama alikuwa anataka kumjua Jane vizuri ila mimi nilikuwa mgumu kuingilika.
Muda huu saa yangu ilikuwa inasoma saa 11 jioni hivyo nikaamua niende Mikocheni nikaonane na Maggy. Nilitumia kama dakika 40 kuwasili pale kwa Maggy na baada ya kupark gari niligonga mlango wake na akatoka kunifungulia mlango.
“Insider sikutegemea kama ungekuja leo maana wewe unamambo mengi sana.”
“Remember nilikwambia leo nakuja kwaajili yako, leo ukitaka hata tulale wote nitalala kwaajili yako.”
“Utaweza kulala wewe? Vipi yule mrembo wako anaendeleaje?”
“Yule ni Bossy wangu kama ulivyo wewe hapa, sema ndo unakimbia.”
“Insider leo sijapika kabisa ngoja nikajiandae ili tukitoka hapa tukapate na dinna kabisa afu tutoke out.”
Maggy aliingia ndani kujianda na aliniacha nimekaa seblen. Baada ya nusu saa alitoka akiwa amewaka sana na mimi kama kawaida yangu nikamsifia pale na yeye akaishia kufurahi tu.
Saa 1 usiku ndo tulitoka pale kwake na tuliamua kwenda Golden fork kupata dinna. Baada ya kuwasili pale tuliagiza chakula na tulitumia kama lisaa tukaondoka kuelekea samaki samaki.
Mapema sana tulikuwa tumewasili pale na tulizama ndani. Muda huu ulikuwa mapema sana hata watu walikuwa ni wa kuwahesabu. Tuliagiza vinywaji lakini mimi hii siku sikutaka kunywa kabisa maana nilikuwa na ratiba za kwenda church asubuhi ili nikatoe na shukrani.
Kwa upande wangu niliagiza heineken 3 tu lakini Maggy aliagiza backet ya Savanna. Hii siku tuliongea mambo mengi sana na Maggy na mimi nilimtakia mema kwenye maisha yake mapya pamoja na kazi yake mpya. Hata kunitoa out ilikuwa ni kama farewell na alikuwa anatarajia kuondoka jumatano kwenda Dodoma.
Saa 6 usiku wakati mziki umeanza kuchanganya tuliondoka na nilimpelea Maggy kwake na mimi nikarudi zangu home kulala. Kwa upande mwingine mama J alikuwa ameshazoea time table zangu za kurudi hata zile kelele zilikuwa hazipo tena.
******
Jumapili niliamka mapema sana ili niwai misa ya saa 1 asubuhi. Hii siku niliweza kutoa na sadaka zangu za shukran kwa mambo yote Mungu aliyonitendea. Kwa upande mwingine mama Junior ni mwalimu wa watoto “Sunday school”.
Baada ya kutoka church niliwasiliana na Mary nikampa ratiba za kwenda kwa Prisca. Na tulikubaliana twende saa 6 mchana tukamtembelee.
Saa 5 nilitoka home nikaenda kwa Zena kumpitia Mary na hao tukaanza safari ya kwenda Changanyikeni. Kwa upande mwingine sikumwambia Prisca kama nitakwenda na dada yake nilitaka iwe surprise kwake. Pia sikumwambia Mary kama tunakwenda Changanyikeni.
Tulivyofika Mlimani city Mary alisema tuingie ndani ili anunue vitu kwaajili ya mdogo wake na mimi niliona ni jambo jema. Baada ya kupark gari tulikwenda pale Shoppers tukafanya shopping ya vitu na mimi nilinunua mazaga kama mafuta, sukari, maziwa, kuku, nknk.
“Insider mbona sikuelewi haya yote kwaajili ya Prisca?”
“Wewe twende utaona.”
Tulitoka pale Mlimani city na tukaendelea na safari yetu na nilitumia njia ya geti maji huku unapita Coet. Sasa baada ya Mary kuona nakata kona kuelekea UDBS alianza kuongea,
“Insider Hall 4 si unakatia pale Contena? Au tunakwenda kuoanana naye wapi?”
“Wewe kuwa mpole utaona.”
Mary aliendelea kuwa na maswali na mimi nilikuwa kimya hata sikuwa namjibu ilibidi Mary awe mpole tu.
Baada ya kuwasili pale Changanyikeni kwa Prisca nilishuka nikafungua geti na nikaingiza gari ndani nikapark. Tulipiga hodi na alitoka Eva kutufungulia mlango lakini alishangaa baada ya kumwona Mary.
EVA: “Ooh da Mary mambo sikutegemea kama ungekuja.”
MARY: “Ahsante sana nimeona nije nimsaprize huyo dogo maana hataki kurudi home.”
Muda huu tulikaa kwenye coach na Prisca alitoka chumbani akiwa amejifunga khanga shingoni, na alvyomwona Mary alishtuka. Na mimi nilimsogelea nika-mhug na nikamkiss mdomoni.
Kwa upande mwingine Prisca tumbo lake lilikuwa la kawaida tu kwa mtu ambaye hana experince ni ngumu kumtambua kama anamimba.
PRISCA: “Karibuni, da Mary nimekumiss.”
MARY: “Unajua Unazingua home kila mtu anawasiwasi na wewe unashida gani?”
PRISCA: “Si unajua na mitihani? afu mimi nishakuwa mtu mzima sio kunifuatilia kama Ivy.”
MARY: “Mzee ndo anakuulizia shida unashindwa hata kuja kusalimia, unajua Ivy amekumiss sana?”
PRISCA: “I know hata hapa nimetoka kuongea naye kupitia simu ya mama.”
EVA: “Ngoja mimi nikawapikie chakula wageni zangu.”
MARY: “Acha tu tutatoka kula lunch pamoja. Kwahiyo ndo umeamua kupanga kabisa, Insider remember I told you that day.”
MIMI: “Eva naomba tupishe tuna mazungumzo kidogo hapa Seblen unaweza kwenda hata chumbani, samahani.”
EVA: “Kuwa na amani shem.”
MIMI: “Prisca nimeamua kuja na Mary sababu hali uliyonayo kwasasa huna haja ya kuendelea kuficha huyu ni dada yako, pia ndo msaada wako na…..” Mary alinikatisha maongezi yangu,
MARY: “Mbona siwaelewi kuficha nini?”
MIMI: “Mary subiri nimalize kuongea kwanza sawa?, ipo hivi Prisca unavyomwona hapo ana ujauzito wangu wa miezi 2. Na aliamua kuondoka nyumbani ili kuficha hii siri mpaka atakapomaliza mitihani ndo angewapa taarifa. Kwakuwa wewe ni mtu muhimu sana kama shem wangu nimeamua kukupa hii siri mapema, ila usithubutu kusema chochote mpaka aseme mwenyewe.”
MARY: “Aisee kumbe, hongera Prisca nafikiri hata home watakua surprised na taarifa hii maana nilijua hu……”
PRISCA: “Da Mary stop no need to talk about this.”
MIMI: “You guys mnahide nini mbona siwaelewi?”
MARY: “Nothing, Insider umempa mdogo wangu mimba unampango gani naye?”
MIMI: “Subiri arudi home itafahamika tu hapohapo.”
MARY: “Prisca me sidhani kama ni shida hii as long as Insider amekubali mimba ni yake unaweza kurudi home na ukawaambia wazazi.”
PRISCA: “I know subiri kwanza nimalizane na UE, haya mengine yataendelea.”
MARY: “Guys mimi sina tatizo nimefurahi kusikia hili ila Insider nakuomba usimchezee Prisca, remember I told you this before.”
MIMI: “I remember twende tukale lunch, mama kijacho wangu anasikia njaa hajala mchana.”
MARY: “Sawa Baba kijacho, Prisca mshtue Eva ili tuondoke.”
Tuliondoka pale na tulikwenda kupata lunch pale “Down Hill” restaurant ambayo ipo opposite na Mlimani City.
Wakati tumefika pale tukisubiri chakula nilipigiwa simu na Mama Janeth na alikuwa anaomba niende kwake kama nina nafasi. Alisema ana wageni hivyo anahitaji niwapeleke Airport wanatakiwa kuondoka na ndege ya saa 12 jioni. Kwa upande wangu sikuweza kumkatalia na nikamwambia nitakwenda kwake ontime.
Tulipata lunch ya pamoja pale huku story zikitawala na muda huu Mary alikuwa busy sana akiongea na Prisca kuhusu maendeleo yake. Na mimi nilikuwa busy na Eva tukipiga story na hii siku niliweza kuchukua namba yake ya simu.
Saa 9 mchana ilitukutia pale na mimi niliwaaga nimepata emergence natakiwa kwenda Masaki, kwa upande mwingine Mary alisema anatashinda na Prisca navyorudi nitampitia ili tuondoke wote.
EVA: “Shem unamambo mengi wewe nakupa nyota zako.”
MIMI: “Hamna Eva nikilala mtoto atakuja kukosa pampass.”
EVA: “Sawa shem wewe wahi tu.”
Na mimi nilifanya malipo nikaondoka maeneo yale na break yangu ilikuwa Masaki kwenye nyumba mpya ya Mama Janeth. Nilifunguliwa geti na nikaingiaza gari ndani na niliwaona mama Janeth na wageni zake wakitoka ndani.
“Mwanangu za jumapili naomba uwapeleke wageni wangu hawa Airport, afu unavyorudi kuna mtu atakupa samaki wabichi nakupa namba ya simu muwasiliane.”
“Sawa mama haina shida.”
Na mimi muda huu nilikuwa ninasaidia kuyaweka mabag kwenye gari kwaajili ya kuondoka maeneo yale.
Baada ya dakika 5 tuliondoka Masaki na tulianza safari ya kwenda AirPort, uzuri kwa Jumapili hakunaga foleni kabisa hivyo ndani ya nusu saa nilikuwa nimewasili pale tayari JNIA. Nilipark gari vizuri pale Terminal 3 na niliwasaidia kubeba mabag kwenye kibaiskeli na tukaingia ndani.
Baada ya kuwapeleka ndani niliwaaga na mimi nikafanya mawasiliano na mtu wa samaki na alinambia nisogee mpaka Ferry sokoni ndo tutaonana pale.
Baada ya kuwasili pale Ferry jamaa alinikabidhi samaki wakiwa kwenye ndoo dogo ya lita 10 na mimi nikaondoka kurudi Masaki.
Ndani ya lisaa nilikuwa nimekamilisha mambo yote na muda huu nilikuwa nimerudi tayari kwa mama Janeth. Nilimkabidhi ndoo yake ya samaki na kwa upande wake alikuwa kafurahi sana, maana alishangaa nimemaliza majukumu yangu kwa muda mfupi sana.
“Mwanangu itabidi unipeleke pale Saloon na baada ya hapo tutafute sehemu tukae tuzungumze maana bado sikujui vizuri.”
“Sawa mama haina shida kwasasa sina chakufanya.”
Mama Janeth aliingia ndani na Ilimchukua kama dakika 5 kutoka na tukaanza safari ya kwenda Saloon. Hatukutumia muda mrefu na ndani ya dakika 5 tulikuwa maeneo yale na alikwenda ndani.
Baada ya dakika 30 Mama Janeth alitoka akiwa ameongozana na Sumaiya walikuwa wanaongea. Walikuja mpaka usawa wa gari yangu na Mama Janeth akaingia ndani, siku hii Sumaiya hakuonesha sign yoyote zaidi ya kunipa salamu tu.
“Unaonaje tukienda maeneo ya beach tukapata na upepo wa Bahari?”
“Sawa haina shida kwahiyo twende Cocobeach.?”
“Lakini tutakwenda ule upande mwingine wa hotelin.”
Tulitoka pale Saloon tukaelekea Beach na baada ya kuwasili pale tulitafuta sehemu nzuri tukakaa. Kama mnavyojua Watanzania wakiona Mzungu wanavyokimbilia chap. Baada ya dada kuja kutusikiliza mimi niliagiza heineken 3, kwa upande wa Mama Janeth aliagiza Kilimanjaro lager 3 na Pweza samaki akasema akatwe katwe vipande.
Kwa upande mwingine Mama Janeth alishangaa sana kuona natumia beer ni kama hakujutia kampani yangu. Kwa ambao ham-wajui wazungu hawa watu hawapendagi unafiki kama wewe ni mnywaji jiachie usianze kujifichaficha, kama wewe unatumia marijuana wewe mwambie hawana noma.
Dada alianza kwanza kutulutea vinywaji na tukaanza kunywa pale taratibu.
MIMI: “Mama wewe ni mpenzi wa local beers?”
MA’ JANETH: “I like hii mnaita Kilimanjaro ndo beer yangu pendwa.”
MIMI: “Mimi hii ndo beer yangu pendwa.”
MA’ JANETH: “Heineken sijawahi kuipenda kwakweli. Hivi mwanangu una elimu gani?”
MIMI: “Mama mimi nina bachelor ya masuala ya Uchumi.”
MA’ JANETH: “Ooh kumbe tuna Mchumi kwenye kampuni yetu bhasi naamini tutaanza kupata supernormal profit.”
MIMI: “Kwa hili hata msijali nina mpango wa kuandaa budget ya kampuni kwa mwaka mzima, pia ninaweza kuandaa Financial statements, na masuala mbalimbali ya kodi.”
MA’ JANETH: “Kama hivi unaweza kufanya nafikiri tukupe haya majukumu wewe sababu namlipa consultant pesa nyingi sana kwa mwaka. Tukikupa haya majukumu wewe itasaidia kupunguza gharama na tutaangalia namna ya kukuongezea mshahara. Nitaongea na Iryn nione anasemaje kuhusu hili jambo.”
Kwa upande wangu nilijua Iryn hawezi kunichomolea kabisa kwenye hili deal. Pia mama Janeth aliniona smart sana kwa jinsi nilivyokuwa nampa mipango pale, alinikubali sana.
Mida ya saa 1 usiku Iryn alinipigia simu na nilikuwa bado niko na Mama Janeth pale tukiendelea kunywa na tukipiga story. Na mimi nilipokea simu yake, na toka jumanne nipeleke document za mizigo tulikuwa hatujaonana hata kwake sikwenda kabisa.
MIMI: “Hello Bossy.”
IRYN: “Insider Mama Janeth alikuwa anakuulizia vipi ulionana naye?”
MIMI: “Yes na bado niko naye hapa.”
IRYN: “Sawa unategemea kutoka sangapi huko?”
MIMI: “Sijajua lakini kwenye saa 2 hivi naweza nikatoka.”
IRYN: “Bhasi ukiwa unatoka nambie nataka unipitie hapa Palm Village au una ratiba zako?”
MIMI: “Hapana sina nitakupitia navyorudi.”
IRYN: “Ok” na akakata simu pale.
Tuliendelea kukaa na mama Janeth mpaka saa 2 usiku ndo tuliondoka maeneo yale na nilimpeleka kwanza kwake.
Wakati natoka Masaki nilimpigia simu Iryn lakini hakupokea, na nilipiga kwa mara nyingine tena lakini hakupokea. Wakati nimefika Msasani Ubalozi wa Marekani alinipigia simu na nikamwambia nakaribia kufika alipo na yeye alisema nikifika nimjulishe.
Niliplan nikionana na Iryn niongee naye ili nijue tatizo ni nini mpaka kanibadilikia vile na pia niliwaza nianze kumjasusi kuhusu sakata la Muajemi.
Ndani ya dakika 10 nilikuwa pale Palm village na nilimpigia simu kumpa taarifa kuwa nimefika, aliuliza nimepark wapi gari na mimi nikamuelekeza, akanambia anakuja.
Nilisubiri pale kwa dakika 30 lakini hakuna dalili za mtu kutokea nikawaza nimpigie simu tena lakini nikasita. Baada ya dakika 5 alinipigia simu akanambia nikamfate upande wa parking za ndani kabisa ground floor.
Ilibidi nitoke pale niingie ndani kwenye parking za wakazi wa pale. Baada ya kuingiza gari ndani nilimpigia simu kumpa taarifa kuwa nimefika, akanambia anashuka yuko kwenye lift.
Nilishtuka kumuona Iryn kaongozana na mshikaji wakija usawa wangu na walisimama. Muda huu macho yangu yalishuhudia wakikumbatiana na jamaa live na wakiwa zero distance.
Moyo wangu ulipiga paaah!, Moyo uliniuma sana, niliumia sana jamani. Hakuna siku ambayo niliumia kwenye maisha yangu kama hii na nilipatwa na hasira sana.
Muda huu mawazo yangu kichwani yalikuwa yananiambia Iryn alikuwa analiwa haiwezekani aniweke zaidi ya nusu saa. Ahh k*m*nina niliishia kutukana tu muda ule.
TO BE CONTINUED
Ok hapo sawa. Maana mimate imewatoka kwamba watampata Mary kirahisi kupitia mgongo wako.I know I was just kidding sina ham na wanajf kabisa kwa walichofanya
mkuu binadamu wa siku hz wamekuwa zaidi ya umbwa, bora umfadhili mbwa maana atabweka huko nje kwako kuliko kumfadhili binadamu wa leo.Watu wa humu ni wapumbavu sana. Yaani unawapa kitu kwa nia njema tu ila watakacho kufanyia hutaamini
Kuna muendelezo?
Mimeupata upo. namba 4958 nilipoishia...natamani nisaidie kiweka link. Tatizo muda hautoshi mambo mengiNasubr jamaa anakuja saa ngap
Daaah ngoma ya wiz inanifanya nijihisi kama namfaham Mzee rest in peace mzeeEPISODE 45
IN LOVING MEMORY OF MR. PAMA (2022).
CONTINUE….
Taarifa za Jane kuhusu kifo cha Mzee Pama nilihisi kama utani hivi, niliwaza huenda Jane atakuwa kachanganyikiwa huko. Ni taarifa ambazo zilinishtua sana kwa upande wangu, nilikuwa nahisi kutetemeka.
“Mzee Pama nimeongea naye juzi tu leo hii awe amekufa haiwezekani, acha nitoke niende Mbweni kwa Jane.”
Nilitoka chumbani na niliwakuta Mama J na Iryn wako seblen wakipiga story na baada ya kuniona niko kimtoko, Mama J alianza kuniuliza,
“Baba Junior unakwenda wapi usiku huu?”
“Nimepata taarifa za msiba wa Mzee wangu mwenye hiyo gari.”
Ni taarifa zilizowashtua pale na zilionekana kuwagusa muda huu.
“Insider tunakwenda wote ngoja nikavae sweta” ilikuwa ni sauti ya Iryn akitaka tuondoke wote na mimi sikutaka kumzuia.
Tuliondoka pale nyumbani na tulitumia muda mfupi sana kuwasili pale Mbweni na tulifunguliwa geti, nikaingiza gari ndani.
Muda huu nilikuwa nikisikia sauti za vilio kwa mbali na tuliingia ndani seblen. Tuliwakuta Jane akiwa ameegemea kwa mama yake akilia na mama yake akimbembeleza mwanae. Niliona huruma sana kwa Jane maana Mzee Pama amekufa bado Jane ana mimba ndogo, ukweli iliniuma sana.
Nilitumia nafasi hii kuanza kumbembeleza Jane na Iryn naye alisogea karibu lakini ilikuwa ngumu sana wakati huu kumtuliza akilia. Na muda huu ilibidi nimsogelee mama nianze kuongea naye wamezipataje taarifa.
“Mama mmezipataje taarifa?”
“Kuna mtu amepiga simu toka saa 3 usiku na akampa Jane hizi taarifa.”
Ilibidi nimwambie mama amtulize Jane ili tupange mipango mapema kabla watu hawajaanza kujaa. Tulipanga tuandae ma-tent pamoja na mziki kwa asubuhi kukicha pamoja na suala la chakula.
Jane alitransfer kiasi cha milioni 3 kwenye simu yangu kwaajili ya kukamilisha hayo masuala yote muhimu. Baada ya kumaliza mipango yetu ilibidi tumwache Jane akapumzike maana alikuwa amelia sana kwakweli.
Baada ya lisaa walikuja wageni wengine watano na vilio viliendelea ilikuwa ni huzuni sana pale Mbweni. Saa 7 usiku Iryn aliondoka na aliniacha mimi pale Mbweni, sikuwa na jinsi ya kuondoka pale ilibidi nilale tu.
Muda huu nilikuwa nakumbuka matukio yote ambayo nilikuwa na Mzee kwa vipindi tofauti. Nilikumbuka ile siku ambayo tuliongea na Mzee Pama na akanitumia milion 6, niliwaza huenda ilikuwa ni kama farewell Mzee alikuwa ameona kifo chake. Pia na suala la kunisisitiza sana kumwangalia Jane nilihisi Mzee alikiona kifo chake Mapema sana. Niliwaza pale Mzee alikuwa anasumbuliwa na nini? Maana alikwenda India mara mbili.
Usiku nilikesha tu pale seblen kwakweli maana nilikuwa nahisi kama niko Dunia nyingine kabisa nilikuwa siamini kama kweli Mzee Pama amekufa, nilikuwa naona kama utani.
Asubuhi mapema sana nilikwenda kutoa taarifa kwa Mjumbe wa nyumba 10 kuhusu msiba na aliweza kunipa connection ambapo nitaweza pata matents na viti. Baada ya kufanya mawasiliano na hao wanaokodisha matent nilikwenda Boko Magengeni kuonana na mhusika ndo alikuwa anapatikana maeneo yale. Nilifanikiwa kupata matent mawili na viti 50 na pia nilifanikiwa kupata mtu wa mziki kupitia jamaa wa matent.
Tuliondoka Boko na kwenda Mbweni na nilimwacha jamaa akiendelea kutengeneza na mimi nilikwenda kutafuta vitu vingine kama vinywaji na mahitaji mengine. Kuhusu mtu wa chakula nilimpata mama mmoja alikuwa anakaa kulekule Mbweni. Mpaka kufika saa 3 asubuhi kila kitu kilikuwa kipo sawa tayari na DJ alishakuwa ameanza kuplay nyimbo.
Nilipata wazo la kuwasiliana na Mary na nilimpa taarifa za msiba wa Mzee maana alikuwa anamjua. Kwa upande wa Mary taarifa hazikuwa nzuri kwakweli na aliishia kuhuzunika tu, na Mary alilsema ndani ya muda mfupi atakuwa amefika eneo la tukio hivyo nimtumie location tu.
Saa 4 asubuhi Mary alikuwa kawasili tayari pale Mbweni hivyo kidogo nikawa na mtu wa kunipa kampani. Baada ya Mary kuwasili pale alianza kulia pale nje na mimi niliishia kumkumbatia na kumfuta machozi.
MARY: “Insider chanzo cha kifo ni nini?”
MIMI: “Kwakweli sijui mara ya mwisho kuongea na mzee ilikuwa jumatano na alisema anakwenda India. Nafikiri tutajua tu, nahisi mzee alikuwa anaumwa.”
MARY: “Yeah itakuwa hivyo, Mzee alikuwa ni mtu mzuri sana. Mungu amlaze mahali pema peponi.”
Mpaka muda huu nilikuwa sijui kifo cha Pama kimesababishwa na nini lakini Roho ilikuwa inaniambia ni ugonjwa. Kwa upande mwingine wageni walikuwa wakizidi kuingia taratibu na ilivyofika saa 5 Iryn alikuja pia.
Hii siku ukweli nilikuwa busy sana ni kama nilikuwa operation manager simu zote za wageni zilikuwa zinapigwa kwangu. Nilikuwa nakazi ya kuwalekeza wageni mpaka Mary akanipa wazo la kutengeneza mabango ya kuelekeza direction ya msiba ulipo.
Kwenye mida ya saa 6 mchana kuna wageni niliwapokea na walijitambulisha kwangu kama marafiki wa mzee Pama, na walisema wana mazungumzo private na Jane. Ukweli wote tulikuwa hatujui kilicho kuwa kinaendelea kuhusu taratibu zote za mazishi. Mipango na kila kitu vilikuwa vinafanyika Ununio kwa mke mkubwa, Jane alikuwa ni mchepuko tu.
Jioni nilikaa na Iryn akanambia kutokana na msiba hataondoka kwenda kwenye apartment yake mpya mpaka mambo ya msiba yaishe. Jioni Iryn aliomba kuondoka na mimi sikuona sababu ya yeye kuendelea kubaki maeneo haya hivyo nikafanya kurequest Uber impeleke home.
Mary alikuwa kampani yangu kubwa sana kipindi hiki na alikuwa akijituma sana asee, ungemwona usingekubali kama ni mtoto wa kishua. Mary alikuwa ananikosha sana mpaka nikaanza kujuta kwanini nilidate na Prisca?. Mary alikuwa kama wife material asee akiwa na khanga yake kiunoni.
Saa 4 usiku Mary aliniaga na akanambia asubuhi atakuja mapema, na mimi nikampa kampani ya usafiri mpaka kwao.
*******
Jumatano mwili wa marehem ulikuwa unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kutoka nje. Kwa upande mwingine ndugu wengi wa Mzee Pama walikuwa wanakuja kutoa pole kwa Jane.
Mzee Juma rafiki wa Pama alikuja Mbweni hii siku na tuliweza kuongea na kubwa alinambia ana maelekezo kutoka kwa Mzee Pama, hivyo taratibu zote za msiba zikikamilika tutaonana. Mzee Juma alinishukuru sana kwa jitihada zangu na jinsi navyojitolea pale msibani.
Jioni walitoka na Jane kwenda Airport kwaajili ya mapokezi ya Mwili wa marehem na ulikuwa unatarajiwa kuwasili usiku. Na taarifa nilizo zipata ni kwamba alhamis itakuwa ni siku ya kuaga mwili kwa hapa Dar na baada ya hapo utafirishwa mpaka Tabora na mazishi yatafanyika huko kwao.
Ile jioni nilimwambia Mary nitakwenda Tabora kwaajili ya mazishi na yeye akasema tutakwenda wote, na mimi sikuweza kumzuia. Niseme mimi na Mary tulikuwa bega kwa bega mpaka watu walikuwa wanafikiri sisi ni wenyeji wa pale.
Alhamis ndo ilikuwa siku maalumu ya kuaga mwili wa Mzee Pama pale kwake Ununio. Mwili ulikuwa unatarajiwa kuagwa saa 5 asubuhi na jioni ungesafirishwa kwenda Tabora.
Mimi na Mary tuliwasili mapema sana eneo la tukio tukitokea Mbweni. Hii siku kulikuwa na watu wenye hadhi, wakubwa na baadhi ya viongozi wa serikali hadi wastaafu. Mzee pama alikuwa ni mtu ambaye anajulikana sana na watu, hadi wazungu na foreigners walikuwepo hii siku.
Kwa upande mwingine Jane naye alikwenda mpaka Ununio kwaajili ya kuaga mwili na nilisikia kulikuwa na mke mwingine tena wa Mzee Pama alikuja pale.
Muda huu zilikuwa zinaonekana nyuso za huzuni sana, jinsi gani kifo cha Mzee Pama kilishika hisia za watu. Kila mtu alikuwa akimwongelea Mzee Pama kwa mazuri na pia aliwasaidia watu wengi sana enzi za uhai wake.
Mazingira yote ya pale kwa Pama zilionekana gari kali tu nazungumzia VX, V8, Range rovers, Jeeps, BMW, nknk. Gari zilijaa karibu mitaa yote ya karibu. Mzee Pama hakuwa mtu mdogo kabisa na eneo hili lilikuwa chini ya ulinzi mkali sana.
Mpaka saa 7 mchana zoezi la kuaga mwili lilikuwa limekamilika na mimi nilirudi Mbweni kwaajili ya kuweka mambo sawa kabla ya safari ya kwenda Tabora. Kwa upande mwingine Mary naye alikwenda home kujiandaa kwaajili ya safari ya baadae.
Ilibidi nirudi Mbweni ili kuweka mazingira vizuri kabla sijaondoka na lengo ilikuwa niwatambue watu ambao walikuwa wanabaki pale kwaajili ya usalama. Na watu waliobaki pale walikuwa ni ndugu wa Jane na baadhi ya rafiki zake. Na muda huu nilipata wazo nitafute Mlinzi wa kukaa pale getini kwaajili ya ulinzi.
Baada ya kuweka mambo sawa nilirudi home kubadilika na kuchukua baadhi ya nguo. Wakati naondoka nilimuaga Iryn naondoka kwenda Tabora na yeye alinitakia safari njema na akanikumbatia.
“Insider nawish nikupe kampani lakini itabidi nibaki kwaajili ya uangalizi wa biashara.”
“Usijali kuwa na amani mpaka sasa mchango wako umeonekana.”
Ilinibidi niache gari na nilirequest Uber ya Bajaji na wakati nasubiri pale kibarazani uliingia ujumbe wa TIGOPESA na kucheki Iryn alikuwa kaniingizia 500,000/=. Nilitabasamu ni kama alijua sina hela, ukweli ni kwamba nilikuwa nimetoboka sana hizi hela ndogo ndogo zilikuwa zinanitoka balaa pale msibani, hata ile Pesa aliyokuwa amenipa Mzee nilikuwa nishapunguza million 2 tayari kwenye masuala ya msiba.
Nilimpitia Mary pale kwao na alikuwa yuko tayari na alikuwa kavaa nguo full black kuanzia raba, T-shirt na miwani, kasoro skin jeans ilikuwa ya blue. Pia alikuwa kaninunulia miwani meusi na mimi kama zawadi.
Saa 9 alasiri tulikuwa pale Ununio kwajili ya kupata usafiri na tuliikuta costa moja tu imebaki na ilikuwa imejaa tayari. Wakati tukiendelea kushangaa pale na kuwaza namna ya kuondoka tulibahatika kupata gari landcruiser V8 ambayo ilikuwa inakwenda msibani na ilikuwa na seat 2 tu zimebaki.
Tuliondoka pale Ununio saa 10 jioni na Ilikuwa ni safari ya masaa 10 mpaka tunafika wilaya moja ya huko Tabora. Nakumbuka tulifika saa 8 usiku na baada ya kuwasili pale wilayani mjini tulikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Mzee Pama, uzuri hakuwa mbali na pale mjini.
Mzee alikuwa amejenga bonge la mjengo na lilikuwa ni eneo kubwa sana ambalo alikuwa anaishi mama yake na baadhi ya ndugu zake. Ndani ya mjengo kulikuwa na garden kubwa na mazingira mazuri sana na yenye kuvutia.
Tulivyofika pale tulikuta msiba unaendelea na watu wengi walikuwa wame wasili tayari na wengine walikuwa wakiwasili. Mary aliingia ndani kuonana na Jane na sisi tulikaa pale nje tukiendelea na mkesha.
Story zilizokuwa zinasikika hapa ni pamoja na utajiri wa Mzee Pama, nilijua Mzee Pama alikuwa ni mstaafu moja ya kampuni kubwa ya uchimbani madini. Pia Pama alikuwa ana miliki vitalu vya dhahabu, bado alikuwa na kampuni ya madini. Alikuwa na mali na Pesa chafu bado alikuwa anamiliki mahotel na nyumba kibao, ila sasa ungemwona Pama jinsi alivyokuwa, alikuwa anaonekana wa kawaida sana.
*******
Ijumaa ndo siku ambayo Mzee Pama alilazwa kwenye Jumba lake la milele na mazishi yalianza mapema sana. Watu wa Tabora waliaga maiti na hata wengine wa Dar ambao hawakufanikiwa kuaga nao waliaga na wale waliotaka kuaga kwa mara ya mwisho walipewa nafasi.
Muda huu kulikuwa na vilio kila kona yaani daah moja ya siku ambayo siji kuisahau ni hii, watu walilia sana huku Tabora vilikuwa ni vilio na huzuni.
Kwa upande mwingine Mzee alikuwa kaandika waraka ambao aliwatambulisha wake zake wote kuanzia mke mkubwa, Jane na alikuwepo mke mwingine ambaye alikuwa na watoto 2 ambao wote ni wa kike. Mzee pama alikuwa na bahati sana na watoto wa kike ni Jane pekee ambaye alikuwa na mimba ya mtoto wa kiume.
Mzee Pama aliandika mambo mengi sana na mwisho kabisa alisema ameandika barua kuhusu mirathi itakavyogawiwa kwa wake zake, watoto na ndugu. Pia aliwataja baadhi ya marafiki zake akiwemo Mzee Juma wawe waangalizi wa Familia yake na baada ya kumaliza kusoma ule waraka kila mtu alibaki na huzuni. Ulikuwa ni waraka mrefu ambao ulikuwa umegusa sana hisia na mioyo ya watu.
Baada ya sala na kila kitu Pama aliingizwa ndani ya Jumba lake la milele. Ni kaburi ambalo lilikuwa limejengwa ndani na likafunikwa kwa nzege juu.
Familia ya Pama ilikuwa na makaburi yao na yalikuwa palepale kwake kwa upande wa nyuma na yalikuwa ndani ya uzio/fense. Makaburi yalikuwa na uzio wake ambao umeungana na nyumba na gate la kuingilia makaburini lilikuwa kwa nyuma linajitegemea na upande wa nyumba.
Kwa upande wa Familia ya Pama walizaliwa watoto wa4 tu kwa Baba yao, Pama alikuwa wa kwanza kuzaliwa, aliefuatia ni dada yake, watatu alikufa na wa mwisho alikuwa ni mdogo wao wa kiume. Baba yao alikufa na walikuwa wamebakiwa na mama yao tu, mpaka kifo cha Pama walikuwa wamebaki watoto 2 na Mama yao.
Hii siku pia nilibahatika kuwaona watoto wote wa Mzee Pama mpaka yule Binti yake wa kwanza mkubwa wa Canada na yule anayesoma Australia.
Mpaka saa 8 mchana mazishi yalikuwa yamekwisha na taratibu zote zilikuwa zimekamilika. Baada ya hapo tulirudi nyumbani kwaajili ya chakula huku taratibu zingine zikiendelea.
Baada ya kumaliza mazishi ule usiku watu walikuwa wamekaa kwenye magrupu wakinywa bia. Kulikuwa na bia za kila aina na nyama choma za kutosha maana kuna gari ilileta vinywaji na nyama kwa wingi, mbuzi na ng’ombe. Kama mnavyojua wabongo wakisha maliza kuzika wanasahau wanaanza kunywa ili kupunguza stress.
Na mimi muda huu nilikuwa nimekaa na watu wazima tukipigia story mbalimbali. Kwenye group letu kulikuwa na wazee na wababa ni mimi pekee nilikuwa kijana. Story zilizokuwa zinapigwa hapa ni siasa na biashara ofcourse nilipata idea nyingi sana za biashara ila shida maokoto tu ndugu zangu.
Mary alikuja akaliunga na sisi pale na story zilikuwa zikiendelea na kila mtu alikuwa anaelezea jinsi alivyokutana na Mzee Pama mpaka kifo chake. Mary alionekana kuchoka sana na aliishia kulala kwenye mapaja yangu.
Huu usiku pia niliweza kuongea na Mzee Juma na tukaagana maana alisema kwa kesho tusingeweza kuonana atakuwa busy na kikao. Mzee Juma alisema ataendelea kubaki pale kwa siku mbili na tutaonana Dar akirudi kwa ajili ya mazungumzo zaidi. Alinipa pesa ya nauli kwaajili ya kurudia Dar na baadae kuja kuhesabu ilikuwa ni laki 3.
Ile Jumamosi asubuhi watu wengu walianza kuondoka pale kwa Mzee Pama na mimi nilimwambia Mary tutaondoka na ileile V8 tuliyokuja nayo.
Saa 6 mchana tulitegemea kuanza safari ya kurudi Dar na kabla ya kuanza safari nilitumia kuongea na Jane. Jane alishukuru sana kwa kujitoa kwangu kwake na alisema yeye bado ataendelea kubaki mpaka vikao vya familia vitakapo kwisha.
Kwa upande mwingine aliniomba niendelee kumwangalizia nyumba yake maana kule alikuwa amebaki mama yake. Mnajua Jane alikuwa amelia mpaka sauti yake ilikauka na macho yalikuwa mekundu sana.
Saa 6 mchana mapema kabisa tulianza safari ya kurudi Dar na njiani tulikuwa hatujui vibao vya 50 ilikuwa ni spidi tu. Saa 4 usiku tuliwasilia Dar na walituacha pale Ubungo mataa wao walikuwa wanaelekea Tabata. Nilifanya kurequest usafiri kwaajili ya Mary na mimi nilichukua bajaji kwenda Changanyikeni kulala kwa Prisca.
Wiz khalifa ft Charlie Puth- See you Again. [emoji444]
CONTINUE
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu