Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Pamoja na kwamba Insider alishindwa kutumia nafasi yake kwa Irene lakini hata Irene hajatumia busara kwenye haya mahusiano yake mapya. Hakukuwa na haja ya kumuonyesha Insider au kukumbatiana mbele yake. Anachofanya Irene ni kumkomoa Insider ili amuumize. Sidhani hata kama huyo jamaa anapendwa na Irene na mapenzi ya hivi huwa hayadumu. Na usishangae Irene akamuacha huyo mwanaume akaanza tena kujipendekeza kwa Insider au akaenda kwa mwanaume mwingine.

Nilichojifunza kwenye mapenzi ni usifanye kwa kumkomoa mtu. Mapenzi ya kumkomoa mtu mwingine huwa hayadumu na mwisho wake utajikuta unajilaumu kwa uliyoyafanya. Na mara nyingi huyo unayemkomoa unakuwa unampenda sana na unafanya hivyo kumuumiza na kumbe ndio unaharibu mazima na mwisho unaishia kuumia zaidi kwa sababu na huyo unayemkomoa hatakutaka tena na huyu uliyezuka naye unajikuta humpendi basi unabaki unajilaumu. Na hichi ndicho kitakachompata Irene. Nasemea hivi kwa uzoefu wangu mwenyewe
 
Kweli mkuu. Picha inaonekana iryn atakuja umizwa na huyo mwamba mbelen nahisi tu. Ila acha tunywe mtori itafahamika
 
EPISODE: 51

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Muda huu mawazo yangu kichwani yalikuwa yananiambia Iryn alikuwa analiwa haiwezekani aniweke zaidi ya nusu saa. Ahh k*m*nina niliishia kutukana tu muda ule.

CONTINUE…

Jamaa hakuishia hapo akamkiss Iryn kwenye forehead yake na mambo yote yalikuwa yanafanyika huku mimi nashuhudia live. Muda huu nilihisi kuishiwa nguvu kabisa, niliishia kuumia tu moyoni na niliona Iryn kama alitaka kunifanyia makusudi.

Iryn alikuja kwenye gari na akaa siti za nyuma na sio kawaida yake kabisa. “What the f*ck” nilishia kutukana tu na hapa sasa nikajua Iryn ametoka kuliwa maana angekaa mbele ningemshtukia.
Alinisalimia na mimi nilimjibu fresh kabisa hata sikutaka kumwonesha sign yoyote ile. Muda huu niliongeza sauti ya mziki kwenye gari na album ya Kendrick Lamar “Mr. Morale & The Big Steppers” ndo ilikuwa kwa playlist.

Nilitoka na gari mle ndani kwa kasi sana mpaka mlinzi aliishia kushangaa tu pale mlangoni. Baada ya kufika Mikocheni Plaza Iryn alianza kuniuliza kuhusu yaliyojiri na mama Janeth lakini mimi nilijifanya kama sijamsikia, nilijifanya niko busy na kurap ngoma ya Kendrick lamar “N-95” muda huu ndo ilikuwa ikisikika.

Baada ya kuwasili kwake niliingiza gari ndani mpaka usawa wa apartment yake na akashuka. Na mimi hata sikutaka kupoteza sekunde pale, bali niligeuza gari huyo moto nikaondoka.

Ukweli mwili wangu ulikuwa mzito sana muda huu. Nilipatwa na hasira sana tena zile za wivu, maana sikutegemea kama kuna siku nitakuja kumwona Iryn akiwa na mwanaume katika mazingira kama yale.

Niliwaza pale hivi kama mimi nimeumia hivi, vipi kuhusu Mary ile siku Kidimbwi? Niliwaza pia ni mara ngapi nimemuumiza Iryn hasa suala la kujua nina mke na mtoto?. Niliishia kujilaumu tu na maneno ya Lucy yalianza kunijia

“Iryn hajataka kumpa uchi mwanaume mwingine ila akija kupata mwanaume nakuambia utakuwa umempoteza mazima.”

Niliishia kulaumu tu, baada ya kuwasili nyumbani nilishuka kwenye gari na nilikuwa mpole sana hata wife alivyoniona alihisi something wrong.

“Baba J mbona hivyo upo sawa kweli?”

“Yeah niko sawa mke wangu leo niko hovyo sana.”

“Pole, hakuna jambo lingine lolote limetokea?”

“Hamna kwakweli ningelikuambia mbona?.”

Nilikwenda ndani chumbani na muda huu simu yangu ilianza kuita ile kucheki alikuwa ni Mary akipiga, nikakumbuka nilimuahidi kwenda kumchukua kule Changanyikeni.

“Mary mambo.”

“Insider mbona hukuja kunichukua na uliahidi?”

“Sorry Mary mambo yaliingiliana nikashindwa kukupa taarifa ndo naingia hapa home now.”

“Its okay nilirequest usafiri, mbona hivyo are you ok?”

“Yeah I am good. Don’t worry about me Mary.”

“Okay have a good night.”

Niliingia bafuni kuoga na baada ya hapo nilipanda kitandani nikalala maana nilipitiwa na usingizi palepale.

*******
Asubuhi Iryn alinipigia simu na akanipa maagizo ya kwenda kufanya ukaguzi kwenye ofisi mpya ya Mikocheni kabla ya kuhamia.

Nilikwenda kuonana na Lucy na alinipa kampani mpaka ofisi mpya maana nilikuwa sijui ipo location gani. Ofisi mpya haikuwa mbali sana na chuo cha kodi (ITA) na pia haikuwa mbali na Palm Village. Ofisi ilikuwa ni kubwa kwakweli ni kama house na Iryn aliplan kuongeza huduma zingine kama massage lakini kwa upande wa wanawake tu.

Ofisi ilikuwa imekamilika kwa kila kitu na kimuonekano kwa ndani haikuwa tofauti na ya kule Masaki. Muda huu nilipata wazo la kutengeneza mazingira ya nje maana yalikuwa hayaridhishi kabisa. Nilitafuta mtu wa kutengeneza bustani pamoja na mazingira ya nje pamoja na kupanda miti na maua.

Nilishinda pale Mikocheni mpaka jioni ndo kila kitu kilikuwa sawa, kutokana na jinsi ofisi ilivyo nilipata wazo la kuajiri mtu wa usafi awe anamwagilia na maua.

Kwa upande mwingine niliwaza kutokana na sintofahamu inayoendelea kati yangu na Iryn niliona ni bora kujidhatiti katika kampuni pamoja na kuongeza ubunifu. Akili ilinijia ninunue mapambo kama Canvas za kuweka ukutani ili ofisi ipendeze na pia nitengeneze T-shirts za kampuni kama sare.

Usiku niliandaa report na nikamtumia Iryn kupitia kwa email na nilikuwa nimeandika na idea ya kuajiriwa kwa mtu wa usafi na mazingira kwa ujumla. Baada ya kutuma report haikuchukua muda mrefu Iryn alini reply na ujumbe uliosomeka “Nice work”.

Kwa cost zote ambazo nilikuwa natoa pesa zangu mfukoni, nilikuwa naziandikia afu kila mwisho wa mwezi nalipwa pamoja na mshahara.

Jumanne asubuhi baada ya kuachana na mama wa2 nilikwenda Kariakoo kuonana na mtu wa printing. Mtashangaa kwanini Mama wa2 tu? Maggy alikuwa ameacha kazi tangu 30/06 hivyo alikuwa anasubiri kuondoka kwenda Dodoma kwenye kazi yake mpya.

Nilikwenda Kariakoo mtaa wa Nyamwezi karibu na Sunderland towers, sasa maduka ya underground pale kuna mshikaji wangu sana ni Home boy anaprint sana hizi T-shirts.

Baada ya kuonana nilimpa mpango kazi wa kudesign logo ya kampuni pamoja na kuprint T-shirts. Kwa idadi ya wafanyakazi ilikuwa 15 lakini Iryn alikuwa anampango wa kuajiri wengine 4 kwa Masaki na Mikocheni, hivyo idadi ingekuwa 20 pamoja na mtu wa usafi.

Mipango yangu ilikuwa kuprint T-shirts za rangi nyeusi na blue, baada ya kushauriana na jamaa tuliona tuprint ziwe 48 kwa blue 24 na Black 24.
Jamaa alishauri atengeneze logo za kushonea ndo imara na zinadumu pia alishauri tshirt za form 6 ndo zitakuwa nzuri.

Gharama zote zilikuwa ni 650,000/=, baada ya kumalizana na masuala ya T-shirt nilikwenda Kijitonyama kuonana na mtu wa Canvas. Hesabu zangu kichwani niliona idadi ya canvas 20 zingetosha kabisa kwa Masaki na Mikocheni.

Jamaa baada ya kuongea naye vizuri alinifanyia Tshs 600,000/= kwa zote maana zilikuwa na ukubwa tofauti. Nilimpa kazi jamaa na akasema ndani ya siku 2 atakuwa amekamilisha kazi tayari.

*******
Jumatano Maggy aliondoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kuanza kazi mpya na makazi mapya. Saa 2 asubuhi niliwasili pale kwake kwaajili ya kumpa kampani na yeye alikuwa anatarajia kuondoka saa 5.

Muda huu Maggy alikuwa amesha jiandaa tayari na tulikuwa tumekaa seblen tukiongea.

“Insider nitakuachia key, hivi vitu kuna mtu atakuja kuvibeba jumamosi.”

“Sawa haina shida mimi unaniachia nini kama ukumbusho?”

“Anayekuja kuvichukua ni mdogo wangu ili akaanze maisha wewe usiwe na wasiwasi na mimi.”

“Sawa haina shida Maggy wangu ila nasikitika sana mteja wangu anaondoka nitakufa njaa.”

“Insider wewe usiwe na wasiwasi ukikwama unakuwa unapiga simu tunasaidiana sisi ni ndugu.”

“Poa Maggy na hizi key nazo nitampa dogo?”

“Kuna mtu nitampa namba zako atakucheki.”

Tuliondoka pale na tulianza safari ya kwenda AirPort na njian tulikuwa tukipiga sana story za mwisho mwisho. Niliwasili pale terminal 2 na nilimpa kampani Maggy mpaka ndani na tuliendelea kukaa pale nje kwenye bench tukipiga story mbalimbali.

Muda ulifika wa kucheck-in aliniaga na akatoa bahasha kwenye mkoba wake na akataka kunikabidhi.

“Insider mshahara wako huu maana ndo tarehe zenyewe.”

“Maggy keep it. No need to pay, mimi mwezi huu nilikupa offa, hata usiwe na wasiwasi.”

“Insider umechoma mafuta yako for nothing?”

“Elewa hivyo tumefanya kazi nyingi sana sioni sababu ya kukulipisha, keep it baadae unaweza kuja kuwa msaada kwangu, kama sio mimi hata watoto wangu.”

Tuliishia kukumbatiana na Maggy muda huu na aliondoka kwenda kucheck-in. Na mimi nilifanya kumtafuta dada Tyna ili nimsalimie na alisema nimsubiri.

Baada ya dakika 15 dada Tyna alikuja na tukakaa pale BAO cafe tukipiga story. Tuliongea mambo mengi sana na kubwa alisisitiza sana kwenda kwake kumsalimia. Tuliongea kama dakika 20 hivi tukaachana na mimi niliamua kwenda Mbweni kwa Jane ili tukaendelee na mafunzo yetu.

Saa 7 mchana nilikuwa nimewasili pale Mbweni na nilipark gari nje getini nikaingia ndani. Nilimkuta Jane seblen anaongea na mgeni na baada ya kuniona mimi alifurahi sana.

“Shem bora nimekuona maana nahamu ya kuendesha gari sana.”

“Ndo kilichonileta hapa kama ulikuwa hujui.”

“Shoga wewe si upo? acha nikaendelee na shule mwenzio.”

Tuliondoka na Jane na baada ya kufika kwenye gari nilimpa funguo ya gari.

“Insider tunakwenda wapi leo?”

“Upo vizuri? Nataka twende mpaka Mlimani city. Tutapita njia ya juu kwenda na kurudi tutapita ya chini.”

“Sawa haina shida.”

Lengo langu kubwa kuona Jane akizoea mazingira ya barabara tofauti ili aendelee kupunguza uoga. Tuliondoka pale na tulianza safari yetu na tulikwenda kuingia Bagamoyo road tukitokea Mbweni road pale Boko.

Tulikwenda moja kwa moja mpaka Mlimani city pale roundabout tukageuza kurudi tulikotoka. Wakati wa kurudi tulipita barabara ya chini kupitia Cocacola road mpaka tukaunga na Mwaikibaki.

Barabarani Jane alikuwa anajitahidi sana kudrive, alikuwa kila siku anabadilika ni vitu vidogo sana vilikuwa vya kumuelekeza. Njiani tulikuwa tunapiga sana story na Jane alikuwa muda wote anatabasamu tu.

“Insider nishauri ninue gari gani?”

“Subiri kwanza uzoee barabara hapo sasa tutaangalia suala la gari.”

“Hata mimi ndo ilikuwa mipango yangu. Nafikiri utanisaidia kwenye hili suala la kununua gari.”

“Usiwe na wasiwasi kwa hili.”

Baada ya kuwasili pale kwake alishuka na nikamwambia hii week nzima tutakuwa pamoja tunafanya mafunzo mpaka awe fit na yeye aliishia kufurahi tu.

Alhamisi na ijumaa hizi siku pia nilizitumia sana kufanya mafunzo na Jane. Ijumaa tulikwenda mpaka Msata na alikuwa anaendesha gari mwenyewe. Nakumbuka Kiwangwa tulipigwa mkono sababu ya over speed na tuliandikiwa tsh 30,000.

Kwa upande mwingine Jane alikuwa tayari kawa Dereva tayari na ile Ijumaa niliamua kumuachia gari yangu Ist aendelee kuitumia.

********
Jumamosi tulikuwa tunahamia ofisi mpya kwa Mikocheni na kulikuwa na kazi ya kupeleka vitu na baadhi ya mahitaji. Na hii siku niliweka zile Canvas pale ofisini na ofisi ilipendeza sana kwakweli na ilikuwa inavutia.

Nilisimamia show nzima nikiwa na Lucy kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, pia Lucy alikuwa na team yake wakipanga vitu kwa mpangilio mzuri.

Baada ya mimi kuona mambo yanakwenda vizuri nilimuaga Lucy na niliondoka na fundi kwenda Masaki na zile Canvas. Baada ya kuwasili pale ilikuwa jioni hivyo tukaziweka zile canvas sehemu zote na ofisi ilipendeza sana.

SUMAIYA: “Bossy leo umetisha sana ofisi imependeza sana.”

MIMI: “Thanks for your compliments lady.”

SUMAIYA: “Insider leo weekend naomba nitoe out.”

MIMI: “Kama baada ya hapo nitakukula sawa niko tayari.”

SUMAIYA: “Ili unifanyie kama siku ile? thubutu.”

MIMI: “Leo siku yangu mbaya sana unajua nilikuwa nakazi ya kuhamia ofisi mpya so nimechoka sana.”

SUMAIYA: “Wewe jishaue tu hapa.”

Kwa upande mwingine Sumaiya alikuwa ameanza kuwa na heshima hata ule utani wake alikuwa hana tena. Baada ya kumaliza kuweka zile Canvas, zilibaki 3 hivyo nikapata wazo, moja nitaondoka nayo, moja nitampa mama Janeth na nyingine nimpe Iryn.

Nilimpigia simu Mama Janeth ili kumpa taarifa naenda kwake na yeye alisema yupo niende tu hakuna shida. Baada ya kuwasili kwake nilitoa Canva moja nikaweka kwa bahasha kubwa na ilikuwa inapicha ya mwanamke wa kiafrica ilikuwa nzuri sana.

Baada ya kushuka kwa gari nilikaribishwa ndani na nilikuwa nimeshika ile bahasha. Ndani ya dakika kadhaa dada alikuja na korosho kwenye bakuli pamoja na juice na mimi nikaendelea kula huku namsubiri mama Janeth.

Baada ya dakika 10 mama Janeth alitoka na mimi nilisimama nikamsalimia.

MA’ JANETH: “Karibu sana my son.”

MIMI: “Ahsante sana, Mama mimi hata sikai maana nilikuwa ofisini nikasema nikuletee hii zawadi.”

Na muda huu nilimkabidhi ile canva na yeye akaifungua bahasha akaitoa ndani ilikuwa ni kubwa ya square.

MA’ JANETH: “Mwanangu Ahsante sana what a gift? I really like it na unisaidie kuiweka mwenyewe.”

Mama Janeth aliingia ndani akatoka na mashine nikadrill nikaweka ile picha, ofcourse canva ilikuwa kali sana hata yeye aliipenda sana na akanipa kazi nimtafutie zingine 3.

Wakati tunaendelea kuongea pale, Mama Janeth alipigiwa simu na Sumaiya na alikuwa anampa shukran kwa kupendezesha ofisi, alifikiri mama Mama Janeth ndo kahusika.

MA’ JANETH: “Insider kumbe umeweka mpaka kule ofisini?”

MIMI: “Ndio mama.”

MA’ JANETH: “Let’s go nikaone maana Sumaiya amesema Ofisi imependeza sana.”

Muda huu ilibidi tuongozane na mama Janeth mpaka pale ofisini tena na baada ya kuingia ndani aliishia kufurahi tu muda huu. Tulitoka pale ofisini na kwa mbele kidogo kama mita 100 kuna sehem wanauza vinywaji, tulikwenda kukaa pale na tukaagiza juice.

MA’ JANETH: “Mwanangu leo umenifurahisha sana kwakweli itabidi Iryn akurudishie cost zako.”

MIMI: “Mama no need nimefanya kama ukumbusho kwa ofisi kama siku sipo.”

MA’ JANETH: “Hapana hiyo ni kazi ya kampuni Iryn atalifanyia kazi hili. Lile suala lingine nilishaongea na Iryn atakutafuta muongee, kuna jambo lingine nataka kukushirikisha kama utaona lina manufaa kwako.”

MIMI: “Sawa mama wewe nishirikishe tu nakusikiliza.”

MA’ JANETH: “Mara nyingi nakuwa na wageni tofauti wa ofisi na binafsi ni kuwachukua Airport na kuwapeleka, kama unakuwa free kwa jioni na weekend uwe unafanya hii kazi. Unaonaje hili wazo kwa upande wako unakuwa unapata pesa za pembeni hutegemei mshahara tu.”

MIMI: “Mama haina shida tena nitashukuru sana kwa hili.”

MA’ JANETH: “Sawa haina shida mara nyingi huwa nawapeleka mimi au Dereva wangu au Uber. Kama wewe utakuwepo nitakuwa nakutumia wewe kwenye hili.”

MIMI: “Ahsante sana mama mimi niko tayari. Wewe muda wowote niambie hata usiwe na wasiwasi.

MA’ JANETH: “Ahsante sana mwanangu nitakuwa nakupa ratiba mapema ili ujiandae mapema.”

Nilimuaga mama Janeth pale maana nilikuwa natakiwa nikaonane na Lucy kwaajili ya kuchukua funguo then nikamkabidhi Iryn. Nilidrive gari kwa spidi sana na nilitumia muda mfupi kufika pale ofisini na nilimkuta Lucy akiwa peke yake.

“Mbona upo alone?”

“Wamendoka maana hakuna cha kufanya. Nilikuwa nakusubiri wewe nikupe key.”

“Kazi nzuri sana nafikiri Iryn atafurahi sana.”

Baada ya kuachana na Lucy nilimpigia simu Iryn kuhusu Key na akasema nimpelekee kwake pia anataka nimpeleke Capetown.

Na mimi nilitoka kwenda mpaka kwake na baada ya kufika nilipark gari usawa wa apartment yake na nikampa taarifa niko parking, sikutaka hata kuingia ndani kwake.

Ilimchukua dakika 20 Iryn kutoka ndani na baada ya kuingia kwenye gari alikaa siti za nyuma.

“Bossy sikuhizi hujali muda kabisa ni nini kimekukuta.?”

“Insider sorry kuna mtu nilikuwa nawasiliana naye ndomana.”

“Sawa wewe ni Bossy wangu mimi hata nikikesha sina shida ilimradi nalipwa mshahara.”

“Lets go tuwahi.”

Tulitoka pale na uelelekeo ulikuwa ni Capetown Fish Market sasa wakati tumekaribia Mikocheni plaza, Iryn akasema tupitie kwanza Palm Village. Na mimi nilihisi lazima tutakuwa tunampitia yule jamaa yake.

Baada ya kuwasili pale nilipark gari na muda huu Iryn alikuwa akiongea na simu. Alikuwa ana muelekeza jamaa tuliko park gari, na muda huu Iryn alishusha kioo na akampungia mkono jamaa kama kumpa ishara. Jamaa alisogea mpaka tulikopark gari akafungua mlango na akakaa siti za nyuma na Iryn.

TO BE CONTINUED
Kimekupata kitu 🤣🤣
 
Wadau eee jogoo mwenzetu uku mambo yamemchachia uwanja umeinama a.k..a ameingia Kwenye mfumo
 
zebri na mimi nilichojifunza kwenye hii story ni kwamba tusijifanye watabiri,huenda huyo ni mteja wake wa faida sana kwamaana iryn uzungu mwingi hata wateja wake pia, kwahiyo ....
 
EPISODE: 52

CONTINUE….

Jamaa alikuwa ni lightskin na urefu wa wastani lakini ukimtizama anaonekana ni foreigner kabisa. Ofcourse jamaa alikuwa yuko vizuri sana Handsome na Gentleman na alionekana kuwa very caring kwa Iryn.

JAMAA: “Bro! how are you?”

MIMI: “Am fine.”

IRYN: “This is my driver call him Insider.”

JAMAA: “Oooh, Insider good to know you Bro!.”

Na mimi sikujibu chochote mudaa huu niliamua kunyamaza kwanza niliona Iryn kazingua sana kwa kitendo cha kunitambulisha kama dereva kwake na sio operation manager, niliona zile ni dharau, nilijisemea kweli Iryn kanichoka tayari.

Na muda huu walikuwa wakiongea na lugha waliyokuwa wanatumia ni kifaransa hivyo ilikuwa ngumu kuelewa wanachoongea. Muda huu niliishia kuwatazama kupitia mirror ya katikati ya gari, maana hii unaweza itumia kuangalia kwa upande wa seat za nyuma. Na walionekana kuwa close sana na mimi niliishia kutukana tu kimoyomoyo, ofcourse jamaa alikuwa yuko vizuri na alikuwa na hadhi ya kutoka na Iryn.

Baada ya kuwasili pale Capetown nilisogeza gari mpaka mlangoni ili washukie pale karibu, kwa upande wangu nilikuwa sawa hata sikuonesha sign yoyote ila kwa ndani nilikuwa naumia sana sema unajikaza kiume tu.

IRYN: “Insider nilijua unapark gari tushuke wote.”

Niliona Iryn ameanza dharau yaani mimi niongozane nao ili wawe wanapenzika mbele yangu na mimi nawaona?, si ningeishia kuwa mpiga picha tu pale.

MIMI: “No mimi siwezi ingia naenda Masaki ofisini wewe ukiwa tayari nijuze nije chap.”

JAMAA: “Bro we need your company, please join us.”

MIMI: “Thank you Bro! Don’t worry about me.”

Walishuka kwa gari na niliishia kuwaangalia wakiingia ndani huku wameshikana mikono na wakitembea mwendo wa taratibu sana. Daah maanninnerr niliishia kutukana tu kimoyo moyo na muda huu nilishtushwa na honi ya nguvu ya gari tena ile ya hasira maana jamaa aliona kama napoteza muda tu pale.

Na mimi muda huu niliamua kuondoka maeneo yale na nilikwenda mpaka Cocobeach kupoteza muda. Baada ya kuwasili pale nilikwenda kukaa sehemu ambayo mara ya mwisho nilikuwa na Iryn.

Nilitafuta angle nzuri nikakaa na niliagiza heineken 2 za kunywa. Muda huu nilikuwa kwenye mawazo sana, kwanza niliona Iryn kama ananifanyia dharau

“Hivi Iryn ananionaje? yaani mimi kuwa dereva wa kumpeleka batani na jamaa yake? No haiwezekani kwakweli.”

Kwa upande mwingine nilikuwa sina maamuzi maana nilisign mkataba wa kazi, hivyo nilikuwa sina ujanja.

“Nafikiri kwa sasa nifocus na maisha yangu, Iryn sio mpenzi wangu na mimi ni mme wa mtu haina haja ya kuingilia faragha zake. Kwasasa nitafocus na maendeleo ya kampuni tu na nitafanya kazi kwa bidii sana.”

Nilijua kabisa mwanamke akikuchoka inatakiwa uanze kuwa adimu machoni pake ili aanze kukumbuka, pia niliwaza hata kwake nitaacha kwenda kabisa.

Wakati nikiwa deep kwenye mawazo nilishutka baada ya mtu kunishika mkono na mbele yangu alionekana dada mzuri tu mwenye asili ya uarabu na alikuwa kajifunika mtandio mwepesi kichwani.

“Kaka mambo?, naweza kukaa hapa?”

“Ndio unaweza kukaa, karibu.”

“Ahsante mbona hivyo? unashida gani? Au ni mapenzi?, nimekusalimia naona kimya mpaka nikaamua nikushtue kwa kukushika.”

“Hamna bhana ni maisha tu ndomana yanafanya niwe hivi.”

“Pole sana maana nimekuonea huruma sana, hata mimi back 2 weeks ago nilikuwa hapa na mawazo kama wewe.”

“Shida nini kwa mrembo kama wewe kuwa na mawazo?”

“I had a boyfriend ambaye tulidate kwa miaka 7 lakini nilikuja kufound out ana mahusiano mengine. Unajua kaka niliumia sana, I cried nikaamua kuja hapa kupoteza mawazo.”

“Kwanini sasa ulie kisa mapenzi?”

“Kinachoumiza ni kupoteza muda kwa mtu ambaye tayari mlikuwa na malengo ya kufika mbali.”

“Pole sana ila kwa uzuri wako naamini utapata mtu sahihi.”

“Upo sahihi but am 29 yrs now kwa kipindi chote ambacho nimepoteza muda si ningekuwa mbali sana.”

“Sometimes remember everything happen for a reason. Huwezi jua mipango ya Mungu juu yako ni ipi.”

“Ni kweli, vipi hapa ndo unapendeleaga kukaa?”

“Yeah sometimes but ni rare sana ila ndo maeneo yangu. Jina lako nani dada?”

“Naitwa Sia na wewe?”

“Naitwa Khalid”

Niliamua kumdanganya tu jina maana mimi nikikutana na stranger maeneo kama haya huwa sitaji jina langu halisi.

“Ok kaka nimefurahi leo kukufahamu.”

“Shukuru Mungu stress ndo zimenileta hapa otherwise tusingejuana.”

Na muda huu dada aliishia kucheka tu ni kama alikuwa surprised na jibu langu. Tulipiga story nyingi sana muda huu hata yale mawazo yangu ni kama yalipotea.

Muda huu nilipigiwa simu na Dullah na alinambia yuko Samaki samaki amemshusha abiria kama nitakuwa around tuonane. Saa yangu ilikuwa inaonesha saa 4, kwa upande mwingine Iryn alikuwa hajanirudia bado, hivyo nikaona bora nikapoteze muda na Dullah.

Nililipa bill zote pamoja na ya dada lakini hakujua kama nimemlipia na mimi nikamuaga nikaondoka pale.

“Sia mimi nakukukimbia nafikiri ipo siku tutaonana tena, byeeh.”

“Ahsante sana kaka kwa kampani yako leo.”

Niliwasiliana na Dullah na akanambia amepark gari mbele ya Jackies na mimi nikaenda kupark gari pale. Nilishuka kwa gari na tukaanza kupiga story na Dullah kwa pale nje,

DULLAH: “We ms*nge usinambie yule mrembo anakuhonga sana mpaka umedaka chuma mpya asee.”

MIMI: “Hahaha kuwa mpole kijana mimi ndo next level hata U-senior inabidi niurithi sasa.”

DULLAH: “Daah hongera sana Man hii Dualis ni kiwembe sana, na ile Ist vipi si nikupe hela tu.”

MIMI: “Ile siwezi uza asee nafikiri kununua nyingine tena ile nitampa mama watoto wangu.”

DULLAH: “Huna njaa ndomana, kwanza pole sana kwa msiba wa Mzee. Nilikuwa simjui ila mpaka umeacha Uber kweli alikuwa muhimu sana kwako.”

MIMI: “Ndo hivo Mzee baba kila kitu ni mipango ya Mungu. Tuingie hapo Jackies nikupe offa ya dinna.”

DULLAH: “Daah sawa bwana mimi sina usemi.”

Tulichil na Dullah pale Jackies na tuliagiza msosi na maongezi yetu yaliendelea pale. Kubwa zaidi ni suala la kumuoa mrembo wake Latifah na alisema november watafunga harusi.

Kwenye mida ya saa 6 kasoro simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Iryn na baada ya kupokea alinambia nisogee wanataka kuondoka. Nilimuaga Dullah na mimi nilikwenda pale Capetown kuwachukua.

Na baada ya kuwachukua tuliondoka maeneo yale na wakati tuko njiani Iryn alisema niwapeleke moja kwa moja mpaka kwake. Njiani walionekana wakiongea na wakiwa kwa ukaribu sana kwa upande wangu nilikuwa busy na kusikiliza music like someone I don’t care.

Baada ya kuwasili pale kwake walishuka kwa gari na walini-wish usiku mwema wakaondoka.
Nilijisemea pale “huu mwaka hakuna rangi nitaacha kuona kama jamaa ameanza kuingizwa kwenye apartment ya Iryn bhasi siku zangu zinahesabika tu.”

Nilikuwa naumia ila sasa sikuwa na jinsi ilibidi nijikaze tu kama mwanaume.

******

Jumatatu huduma zilikuwa zinaanza kutolewa ofisi mpya ya Mikocheni na ofisi zote za Sinza na Mikocheni zilifungwa. Wafanyakazi wa Sinza nao walikuja pale kuungana na wale wa Mikocheni na kufanya jumla yao kuwa 8 pamoja na Lucy.

Kwa upande wangu niliona wafanyakazi wanatosha na ule mpango wa Iryn wa kuongeza wafanyakazi nilimshauri ausitishe kwanza ila afanye kuajiri mtu wa usafi tu. Pia nilimshauri afunge internet fiber tuwe tunalipia kwa mwezi kidogo itasaidia kuvutia wateja na pia wafanyakazi watapost sana product zetu na kuitangaza kampuni. Iryn aliunga mkono wazo langu na akanambia nitafute mtu wa kufunga internet pamoja na mtu wa usafi.

Na mimi sikuchelewa kuna mtu nilikuwa nafahamiana naye kipindi kile nakaa kwa Uncle alikuwa jirani. Yeye alikuwa anafanyia kazi kampuni moja inadeal na haya mambo ya telecom bhasi nikampa ile kazi na akafunga internet kwaupande wa Masaki ilikuwepo. Baada ya internet kufungwa niliona dada pale ofisini wakifurahia free Internet kama iliwaongezea morale ya kazi, hata Lucy alinipongeza kwa hili.

Kwa upande mwingine kuna baadhi ya vitu vilibakia saloon za Mikocheni na kule Sinza maana havikuwa na kazi tena hivyo tulifanya kuviuza na Lucy na tulipata milion 3 na ushee, tukagawana. Kwenye Saloon mpya kila kitu kiliwekwa kipya ni vitu vichache sana ambavyo vilitoka kwenye hizi saloon zilizofungwa.

Ratiba zangu pia zilibadilika kuanzia hii week, kwa ile asubuhi nikimpeleka mama wa2 kazini nilikuwa napitia Masaki kwanza naangalia kama kila kitu kipo sawa kuanzia mazingira, usafi, maji na umeme then nakwenda kumalizia Mikocheni. Nikimaliza ukaguzi na kujihakikishia kila kitu kipo sawa nilikuwa narudi zangu home mapema kucheza na Junior.

Kwa upande wa watoto wa kule Masaki shuleni, hii week walikuwa wamefungua shule na taarifa mbaya ni kwamba madogo wawili waliamishwa shule akiwemo Carol. Hivyo walibaki watoto wa2 tu wa kuwapeleka na mimi nikaamua kuachana na hili dili maana niliona kwangu ingekuwa hasara tu.

Jumatano nilikwenda Kariakoo kuonana na jamaa niliyempa kazi ya kuprint Tshirts na nilikuta amemaliza tayari na alifanya kazi nzuri sana.

Nilitoka Kariakoo na nilikwenda moja kwa moja mpaka Masaki na nilimpa T-shirts Sumaiya ili azigawe kwa wafanyakazi wake maana zilikuwa kwa size tofauti. Baada ya hapo nilitoka nikaenda Mikocheni nikaonana na Lucy nikampa T-shirts awape wafanyakazi wake. T-shirts zilikuwa ni nzuri na ziliwapendeza sana na waliishia kunishukuru na kunipongeza.

Muda huu niliamua kuondoka pale Mikocheni na nilirudi home kupumzika pamoja na kucheza na Junior. Lakini baada ya kurudi home nilikuta Junior hayupo na dada akanambia Iryn alikuja akaondoka naye.

“Dada una uhakika ni Iryn aliyekuja?”

“Ndio kaka ni yeye na amekuja na gari nyeusi, amekaa hapa akampa na uji akasema anaondoka naye atamrudisha badae, mmepishana kidogo tu.”

Nilivyosikia gari nyeusi ilibidi nishtuke kwanza, maana Iryn hana gari. Ilibidi nimpigie simu Iryn ili nicomfirm kama ni kweli alikuja mchukua Junior, na baada ya kuwasiliana naye alisema yuko naye na atamrudisha badae.

Nilikumbuka kwa mama Janeth kuna Range nyeusi hivyo Iryn atakuwa aliamua kuifuata ile gari iliyokuwa ya mama yake. Na muda huu nilijisemea,

“Daah! Iryn mpaka kaenda kuchukua gari kweli hataki usumbufu na mimi.”

Baada ya kukuta Junior hayupo niliamua kwenda zangu kwa Prisca ili nikapoteze muda pia nilikuwa nimem-miss sana. Kipindi hiki walikuwa wako kwenye mitihani na ilikuwa ni week ya mwisho na alikuwa anasubiri mtihani wa mwisho ijumaa.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 7 kasoro za mchana wakati nawasili pale kwake na nilimkuta akiwa na Eva wanasoma Sebleni. Niliwapa hi! na mimi nikaenda zangu chumbani kulaa, lakini baada ya dakika 5 nikiwa chumbani Prisca alikuja,

PRISCA: “Honey are you okay? Seems like you’re not ok.”

MIMI: “Niko poa swirry please come.”

PRISCA: “Nataka nikakupikie chakula.”

MIMI: “Mimi nataka ugali na kitimoto, wapi wanauza hapa kitimoto? Ugali nitakusaidia leo kupika.”

PRISCA: “Ngoja nimpigie simu bodaboda alete.”

MIMI: “Mara hii ushawajua bodaboda?”

PRISCA: “Baby mara nyingi namtumia kwenda sokoni na kuniletea vitu.”

MIMI: “Ni sawa ila pia sitaki kukuona ukipanda bodaboda not safe.”

PRISCA: “Sawa honey ngoja nikaandae mboga ya majani.”

Na mimi sikuchukua muda nilikwenda jikoni kumsaidia kupika ugali na muda huu Eva alikuwa yuko busy anasoma.

MIMI: “Shem nakuona upo busy unatafuta 1st class nini?.”

EVA: “Shem acha nasoma hizi statute za sheria zinanichanganya tu hapa. Mwenzangu Prisca coursework yake ni nzuri hana stress kama mimi.”

MIMI: “Pole sana, utatoboa usijali.”

PRISCA: “Honey tukimaliza paper si unatutoa out? Twende hata Tips.”

MIMI: “Wewe na hali hiyo bado unataka kutoka out? Si ulitaka kuwa mama? Utabaki hapa mimi nitatoka na Eva.”

PRISCA: “Honey nimeacha kutumia alcohol nitakunywa hata mocktail, kidogo nitoe hangover za mitihani.”

MIMI: “Sawa haina shida nitawatoa mka-enjoy.”

Na muda huu nilikwenda jikoni kumsaidia Prisca na yeye alikuwa akikata kata viungo vya mboga.

Alikuwa amevaa kigauni kifupi ambacho kiliishia chini ya usawa wa makalio sasa akiinama mambo yote nyuma yalikuwa hadharani.

MIMI: “Baby kwanini huvai pichu?”

PRISCA: “Honey hutaki mwanao apumue?

Na mimi niliishia kunyamaza tu muda huu, nikakumbuka hata mama Junior alikuwa hapendelei kuvaa pichu enzi za ujauzito wake.

Hii siku nilishinda na Prisca mpaka usiku, wakati naondoka niliamua kumpa cash tsh. 300,000/= kwaajili ya matumizi na yake binafsi.
*******

Ijumaa Prisca alimaliza mitihani yake lakini baada ya kutoka kwa mtihani alianza kuumwa. Nilipigiwa simu na Eva na akanipa taarifa hizi na nikamwambia atangulie Kairuki hospital nitawakuta huko.

Nilichelewa kuwasili pale na nilikuta tayari wameonana na doctor na majibu ya vipimo yalionesha ana homa. Tuliondoka pale hospital kurudi kwake na nilishinda naye siku nzima pale kwake tukiwa na Eva.

Kwa upande mwingine Prisca alinambia kesho jumamosi atarudi kwao na pia akaongee na wazazi kuhusu suala la mimba. Mimi niliona ni jambo jema kurudi kwao na kutoa taarifa ili wazazi wajue kinachoendelea.

Hii siku hatukutoka kama tulivyopanga sababu ya kuumwa kwa Prisca, hivyo wakati naondoka ile jioni nilimwambia Eva tuongozane ili nikawanunulie vinywaji.

Wakati niko njiani na Eva tulikuwa tunaongea mambo mengi tu likiwemo la Prisca, na kubwa alitaka kujua nimejipangaje kwenda kwa kina Prisca. Pia alikuwa anashangaa kuona silali pale kwa Prisca ni kama alikuwa ananipeleleza ajue kwanini. Niligundua Eva hajui chochote na hakuna ambacho Prisca kamwambia na mimi nilishia kumpa sababu za uongo.

Niliingia na Eva pale Mlimani city kununua vinywaji na baada ya hapo alirequest Uber ya kumrudisha Changanyikeni.

Tuliachana pale na mimi nilikwenda Parking nilikopark gari ili niondoke lakini wakati nimeingia kwenye gari niliangalia siti ya pembeni yangu na nikaishia kumkumbuka Mzee Pama muda huu.

Nilikumbuka mara ya mwisho wakati nampeleka Airport alikuwa amekaa pembeni yangu tunaongea. Muda huu niliwaza kumpelekea gari Jane, niliona ni muda sahihi wa kumkabidhi gari yake.

“Mzee najua haupo kimwili lakini kiroho tupo pamoja. Hukutaka kipindi kile kumpa gari Jane sababu alikuwa bado hawezi kuendesha. Kwasasa anaweza hivyo ni wakati sahihi wa mimi kumkabidhi gari yake. Rest In Peace Mzee.”

EPISODE 53[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Pamoja na kwamba Insider alishindwa kutumia nafasi yake kwa Irene lakini hata Irene hajatumia busara kwenye haya mahusiano yake mapya. Hakukuwa na haja ya kumuonyesha Insider au kukumbatiana mbele yake. Anachofanya Irene ni kumkomoa Insider ili amuumize. Sidhani hata kama huyo jamaa anapendwa na Irene na mapenzi ya hivi huwa hayadumu. Na usishangae Irene akamuacha huyo mwanaume akaanza tena kujipendekeza kwa Insider au akaenda kwa mwanaume mwingine.

Nilichojifunza kwenye mapenzi ni usifanye kwa kumkomoa mtu. Mapenzi ya kumkomoa mtu mwingine huwa hayadumu na mwisho wake utajikuta unajilaumu kwa uliyoyafanya. Na mara nyingi huyo unayemkomoa unakuwa unampenda sana na unafanya hivyo kumuumiza na kumbe ndio unaharibu mazima na mwisho unaishia kuumia zaidi kwa sababu na huyo unayemkomoa hatakutaka tena na huyu uliyezuka naye unajikuta humpendi basi unabaki unajilaumu. Na hichi ndicho kitakachompata Irene. Nasemea hivi kwa uzoefu wangu mwenyewe
Hata Insider alifanya mambo mengi ya kumuumiza Iryn ikiwemo kufinya na wakina Sumaiya mara wakina Mary wamnunie Iryn na anawapakiza pamoja abiria wake.
 
TO BE CONTINUED.
Dah, pole sana Insider man, Iryn nae ameamua kukulipiza kama ulivyokuwa unamjibu wakati akikuukiza kuhusu Marry, naamini next time ukipata nafasi nyingine kua na ukatibu nae kamwe hutafanya jambo la kumuumiza tena!
 
Story hii nafikiri ni moja ya story bora kabisa kuwahi kuandikwa hapa JF.

Nampongeza sn Mkuu INSIDER MAN kwanza kwa uandishi wake wa viwango vya hali ya juu ukizingatia kwamba anayapanga matukio katika hali ambayo inamfanya msomaji awe na suspense ya kujua nini kinafuata kwenye mtiririko wa hii story.

Nimetumia siku 4 kuanzia eposod ya kwanza mpk hapa alipoishia huyu mwamba, nimesoma huku nikifuatilia matukio kama kuna sehemu either kajichanganya lkn to be honest sikuona. Na hii ndiyo inaonesha kuwa hii ni true story cos anakwenda day after day, week after the same etc. etc.(according to my analytical eye) kwa hii story.

KILICHONIVUTIA
1. Sehemu nyingi za ukanda wa kuanzia Posta kurudi kaskazini yote ya Dar nimezunguka sn maeneo yale na barabara zote pamoja na maeneo mengi anayoyaeleza msimuliaji nimekuwa nikiyapita so nilikuwa naenda naye bampa to bampa.

2.Msimuliaji ana bahati sn ambayo ni 'unique' hizi bahati zinawapata watu wachache sana. It's God given!

3.Kuna mtu humu amekuwa akicomment hii story na neno lake moja tu la 'NUKTA ' yeye hana maneno mengi kwenye coments zake kiasi ambacho naye amekuwa kivutio...

4. Kuna wajuba walimshukia Ndg INSIDER kwa nguvu ya 5G kuwa mwandishi anayoadithia ni 'Chai' kiasi ambacho kilipelekea uzi kuchafukwa na mwandishi kutaka kuwithdraw ila nguvu ya wana JF iliwazima kama moto wa kibatari.

USHAURI:
Mkuu INSIDERMAN napenda niungane na wana JF wachache waliodokeza kuwa weka kitu hiki kwenye kioo( TV) utengeneze hela. Nahakika na kwasababu unatembea na bahati usishangae unapiga hela kupitia contracts na wadau wa tamthilia kama Dstv or Azam
Mwanangu Mimi jina lako lazima nilianzishie uzi, eti bendera ya bati. Hahahaha!!!
 
Urafiki na ukaribu uliokuwa nao na Iryn ulikuwa unapendeza na kufurahisha kwa kweli ila ndo hivyo uliharibu kwa kuchukua hela kwa Mwarabu ili kumuunganishia ampate Iryn, kwa lugha nyingine Iryn aliona ni kama unamuuza wakati mara nyingi alikusisitiza anakuamini sana
 
Back
Top Bottom