Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Acha ule majonzi sasa jamaa atamdinya hapo hapo kwenye gari 🤣🤣🤣
 
Pamoja na kwamba Insider alishindwa kutumia nafasi yake kwa Irene lakini hata Irene hajatumia busara kwenye haya mahusiano yake mapya. Hakukuwa na haja ya kumuonyesha Insider au kukumbatiana mbele yake. Anachofanya Irene ni kumkomoa Insider ili amuumize. Sidhani hata kama huyo jamaa anapendwa na Irene na mapenzi ya hivi huwa hayadumu. Na usishangae Irene akamuacha huyo mwanaume akaanza tena kujipendekeza kwa Insider au akaenda kwa mwanaume mwingine.

Nilichojifunza kwenye mapenzi ni usifanye kwa kumkomoa mtu. Mapenzi ya kumkomoa mtu mwingine huwa hayadumu na mwisho wake utajikuta unajilaumu kwa uliyoyafanya. Na mara nyingi huyo unayemkomoa unakuwa unampenda sana na unafanya hivyo kumuumiza na kumbe ndio unaharibu mazima na mwisho unaishia kuumia zaidi kwa sababu na huyo unayemkomoa hatakutaka tena na huyu uliyezuka naye unajikuta humpendi basi unabaki unajilaumu. Na hichi ndicho kitakachompata Irene. Nasemea hivi kwa uzoefu wangu mwenyewe
 
Kweli mkuu. Picha inaonekana iryn atakuja umizwa na huyo mwamba mbelen nahisi tu. Ila acha tunywe mtori itafahamika
 
Kimekupata kitu 🤣🤣
 
Wadau eee jogoo mwenzetu uku mambo yamemchachia uwanja umeinama a.k..a ameingia Kwenye mfumo
 
zebri na mimi nilichojifunza kwenye hii story ni kwamba tusijifanye watabiri,huenda huyo ni mteja wake wa faida sana kwamaana iryn uzungu mwingi hata wateja wake pia, kwahiyo ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…