Mi namuonea tu huruma dada wa watu Iryn na sijui kwanini kila mtu humu anamuona kama alikuwa anakosea sijui kisirani, mtu ambae hana ndugu wala rafiki zaidi ya mama Janeth akampata insider akamuamini na kumpenda kwa moyo wake wote akaamua kumfanya mtu wake wa karibu kabisa kama ndugu sijui pengine ndo hivyo labda alikuwa na hisia nae za mapenzi sina uhakika sana, maana kwa ninavyojua mwanamke amtake mwanaume kabisa na jinsi walivyokuwa close kulikuwa hamna cha kumzuia wala Insider sio kwamba alikuwa hamtaki bali alikuwa tu anashindwa jinsi ya kumuingia kwa kifupi alikuwa anamuogopa, kinyume chake akaona bora hata apate hela kupitia yeye bila kujiuliza kama Iryn atagundua itakuwaje
Hivi mlitegemea Iryn areact vipi kwa huyu mtu ambae alimthamini sana lakini yeye hakumrudishia hata nusu ya thamani ya utu wake, yaani kwamba anaweza kuchukua hela kwa Muajemi ili Iryn aliwe akititokea Muitaly nae akatoa hela atampeleka na huko pia, jarƬbuni kuvaa viatu vyake muone kama haviumi
Dada wa watu alijaribu angalau alijua amepata familia hapa na ndio maana mara ya mwisho alienda kuishi nao lakini aliambulia usaliti mkubwa ingawa pia insider hakuwa na nia mbaya wala hakumfikiria kwamba ni malaya ila sasa Muajemi jinsi alivyojieleza na kumbuka Insider alikuwa msiri anaficha mambo mengi na hata mara ya mwisho alivyopewa hela aliona na akamuuliza akamdanganya. Wakati mwingine sio hela ni kila kitu unaweza kupata hela sawa na ukapoteza kitu chenye thamani kuliko hiyo hela uliyopata INSIDER MAN