Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

@Watu8 njoo tufanya kikao Cha dharura hapa na kapten

Hahaha mkuu kwanza nimecheka sana baada ya kupitia comments za watu wenye hasira kali wanaolalamika kudanganywa kisa tu imeandikwa kwamba hii ni true story...

Kwa wasomaji wenzangu, masimulizi kama haya yenye kuandikwa true story, ijulikane ya kwamba kilicho ukweli huwa ni ujumbe wa story, mtunzi anaweza akaongeza mambo mawili matatu ili kujenga skeleton ya story yake...

Zaidi ya yote, tufanye kwamba hii sio story yenye visa vya kweli bali ni utunzi tu, Je kwa wanaoalalamika wanadanganywa ina maana hawaenjoy kusoma na kuguswa na kinachosimuliwa?
 
@Watu8 njoo tufanya kikao Cha dharura hapa na kapten

Mkuu sasa ngoja turudi kwenye kikao chetu cha dharura na INSIDER MAN...

Mwanamke yeyote ukishazoeana naye kwa kiwango kama ambacho yeye na Genevieve wamezoeana, huwa wanapenda kujua mipaka ya mazoea...

Ukimuonesha kuwa unampenda na kumtamani halafu unachelewa kufunguka, atakusubiri kidogo na ukichelewa zaidi ataendelea na mishe zake (lakini utaendelea kusalia moyoni tu)...

Sasa ndugu yetu kulingana na simulizi lake, bado hajaweka bayana kwa Genev...kwamba mahusiano yao mengine nje ya kazi yaweje na uzuri ni kwamba bibiye kampa chances kibao za kufanya hivyo tokea wanashinda wote enzi za apartments za Kijitonyama mtaa wa Grandvilla...

Katika hali waliyofikia hapo pa huyo bibiye kukasirika, sio kwamba kakasirika INSIDER MAN kuwa na mchuchu tofauti na Mama J, ila kilichomuudhi ni kwamba huyo mchuchu si yeye bali ni Prisca...

So Insider man kama atapata nafasi ya kuongea na Genevieve tena, kitu pekee anachoweza kufanya ni kufunguka kwake kwamba muda wote mtu aliyekuwa moyoni ni yeye isipokuwa aliona kama angeweza kuharibu uhusiano wao endapo angemfungukia na hakuwa tayari kuumiza moyo wake...

Pia amwambie kuwa yeye na Prisca walishaachana (amkandie kimtindo Prisca lakini sio ile sanaaaa)...
 
Sasa mbona unamtukana, nawewe kama unaona hii ni true story kaushia, soma kimya kimya , kwani akisema sio true story itabadilisha lipi kwenye akili yako. (Nb; Utakuwa mjinga sana ukishindwa kuelewa hii story ni ya kutunga)
SASA KAMA ANAKUOANGA MBONA UMEKAZA MAKALIO KUISOMA MUDA WOTE SI UNGEISHIA EPISODE YA 30 UKAAMSHA. KUTWA KUCHWA UMEKAZA MAKALIO KUIFUATILIA. KAMA CHAI UKIIONA IKAUSHIE USIIFUNGUE SIO HADI UCOMMENT HAPA UMELAZIMISHWA? PUMBAVU KABISA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti "Iryn unachochukia na kuninunia ni nini, wakati hatuna mahusiano yoyote Kati yetu"

Mkuu, umefeli Sana hapa, hii sio kauli ya kuitoa Kwa mwanamke ambaye inaonesha anakuelewa Sana.

Afu inaonekana Huwezi hata kubembeleza kidogo, Iryn anaamua Tu kusema muondoke hakuna Tena maongezi nawe unanyanyuka chap badala ungenishawish mkae akwambie alichokuitia.

Ivi serious? Eva mtoto mdogo aje alopoke vitu kma Ivo mbele ya Boss wako umetulia Tu unamsikiliza?

Aisee!! Unafeli pakubwa
 
Stor ni nzuri,lkn kuna maeneo insider anatuchanganya,...inakuaje kila wakati unapokua na issue sensitive na Iryn kuna jambo linaingia kuvuruga?...ulikwenda nae kwa lengo la kulala ukapigiwa simu na mama 2,unakwenda kwenye maongezi nyeti na Iryn mara Eva anaingilia...kwa matukio haya napata picha huna msimamo,huyu Eva alipokuita tu ungempiga stop ukiwa serious kwamba niko na mtu muhimu hapa tena ni boss wangu....lkn anakaa na ww una mtu mhm unamuacha anaongea mambo ambayo unajua yatamkwaza mtu uliye naye...kama mwanaume umefail pakubwa sana.
 
Stor ni nzuri,lkn kuna maeneo insider anatuchanganya,...inakuaje kila wakati unapokua na issue sensitive na Iryn kuna jambo linaingia kuvuruga?...ulikwenda nae kwa lengo la kulala ukapigiwa simu na mama 2,unakwenda kwenye maongezi nyeti na Iryn mara Eva anaingilia...kwa matukio haya napata picha huna msimamo,huyu Eva alipokuita tu ungempiga stop ukiwa serious kwamba niko na mtu muhimu hapa tena ni boss wangu....lkn anakaa na ww una mtu mhm unamuacha anaongea mambo ambayo unajua yatamkwaza mtu uliye naye...kama mwanaume umefail pakubwa sana.
Hapa kweli aliteleza .....na tunamushusha vyeo kadhaa
 
Ulizingua sana mkuu! kwahyo hujui kinachomliza Iryn au sio? Then unaondokaje unamuacha mwanamke analia? Alafu eti unamwambia kua huelewi analia nn wakat hamna mahusiano dah majibu ya kikatil sana man, wewe umeambiwa mara ngapi na Lucy kua boss wenu anakupenda?! Alafu mama wawil anapata wap ujasir wa kukupigia usiku simu na anajua ww mume wa mtu, otherwise unambie alikua anahitaj usafir( alikupigia kama dereva) . Leo nimeshindwa kucomment kimoyomoyo episode hiz mbili ulizingua sanaa yan
Kwa kweli mimi sio mtu anaeamini hii story ni ya kutunga lakini kuna vitu havimake sense kabisa hivi kweli mama wawili anakupigia simu saa 8 usiku mume wa mtu eti kwa sababu mtoto anaumwa, mbona hakumpigia baba wa mtoto si ni kwa sababu anajua ni mume wa mtu na anaheshimu hilo iweje wewe, na tena eti wewe ni mtu wake wa karibu ina maana kabla hajakutana na insider alikuwa hana rafiki wala mtu yeyote ambae angeweza kushirikiana nae kama hivyo.
Haya huyo Eva eti anasema alikuwa sahihi sio kweli hivi hata kama angekuwa rafiki yake wa kike best kabisa unamkuta sehem amekaa na mtu unaweza ukakaa tu na kuanzisha story bila wao kukukaribisha, angesalimia na kuondoka au kama angeona kuna ulazima sana kuongea nae basi hata angemuomba waongee pembeni kidogo na hapo
 
Maguire kama kawaida yake, ashachoma kibanda maniner!

Unanikera kifala sana mwanangu. Yani shida kuu kwenye mahusiano yako yote ni kukosa mipaka. Kwa lifestyle yangu, huyo Eva asingethubutu hata kuisogelea hiyo meza niliyokaa na Iryn!

Nimepoteza matumaini kabisa ya kushinda hii mechi. Maana foward butu, beki Maguire. Potelea mbali.

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] tusubri kaka kuna comeback ya Liverpool,Instanbul 2005
 
Ndugu zangu habari nina Ombi naamini kuna wazazi humu ndani.

Kuna tatizo sasa kuhusu NHIF hasa kwenye Bima za watoto masharti yameongezeka na utaratibu wa kuwaandikisha watoto umebadilika.

Kuna watoto 10 ambao Iryn alikuwa anawalipia bima sasa nimejaribu kufuatilia utaratibu imekuwa ngumu sana na bima zao zime expire tayari.

Kama kuna mtu anaijua kampuni ya bima inayoweza kukata Bima za watoto naomba msaada kwa hili, NHIF wamezingua sana nafikiri hawajaangalia upande wa watoto yatima ambao wanasaidiwa.
Kama wapo shuleni kwa sasa wanaandikisha kupitia shule zao wanaposoma kwa gharama zile zile but kama hawapo shuleni na ni yatima hiyo ni changamoto kubwa system imeamua kuwatenga pia
So sad🥲
 
Back
Top Bottom