Nikiri wazi huu uzi umenifanya najiona dhaifu sana.
Story ya jamaa na prisca ni exactly same na story yangu na demu fulan. Insider na prisca jinsi walivo, tabia na mahusiano yao hata mimi ni hivo hivo.
Nimeoa nna mtoto 4yrs.
Na nna demu ambaye last yr ndo amegraduate chuo. Tabia zake na mahusiano yetu yanafanana na prisca almost kila kitu. Tatizo linalonitatiza ni moja.. Insider ameweza kumpa kibuti prisca. Lkn wakuu mimi nashindwa kabisa..
Moyoni siyataki mahusiano haya, nachukia kabisa, tatzo nashindwa namuachaje huyu demu. Sina ujasiri wa kupiga kibuti km alivofanya Insider.
Mfano leo hii tuna appointment. Demu anataka tuonane falagha.. Yaan toka asubuh sina raha kabisa.. Sipendi kuonana nae wala sina hamu naye. Na nshamkwepa sana hapo kati kila tukitaka onana naibua sababu za uongo mpaka nmeishiwa sababu.
Basi nashindwa kumuacha sababu najua ataumia sana, atapata stress.. Inanicost sana