Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 18

Baada ya kusoma ile text ya Iryn na ilikua imetumwa muda mrefu nilisema kuna kitu kibaya kimeshampata Iryn. Na muda ule nilijikuta nikijilaumu sana kwa kulala kwangu kwenye gari na muda uleule nilitoka kwenye gari haraka na kuelekea Reception.

Na hapo nilikua nikimpigia simu Iryn lakini ilikua haipokelewi kabisa. Nilifika pale reception nikamkuta dada na nikamsalimia.

MIMI: “Dada mambo, Bossy wangu amenitumia message yuko in danger na amenitumia Room No.222, ni muda mrefu toka ametuma hii text, naomba twende tukaangalie anashida gani maana kwa sasa hata simu hapokei.”

RECEPTION: “Yule dada alikuja hapa nakumbuka si mweupe? na alisema anakwenda Room hio na alijiandikisha hapa ni iryn eeh.” (Baada ya kuangalia kwenye visitors register)

MIMI: “Ndio dada ndo huyo naona unachelewa twende haraka.”

Na muda huo dada alimwita mlinzi na tukaelekea usawa wa hiyo room ilipo, na muda huo alitumia kuwasiliana na manager. Room ilikua floor ya 2 na tulivyofika pale mlangoni tulisikia kama purukushani ni kama kuna ugomvi ulikua unaendelea pale.

Upande mwingine kuna dada oppositie na chumba hicho alikua katoka kama mtu mwenye mishe zake, lakini alivyomwona mlinzi na tuko pale mlangoni alisogea karibu ili ajue kinachoendelea pale.

Na tukiwa pale mlangoni tulikua tukisikia sauti ya Iryn,

“Leave me alone, I said leave me alone”

“You want to rape me?”

Na muda uleule Mlinzi aligonga mlango, lakini ulikuwa haufunguliwi, ilibidi mlinzi atumie vitisho ndo jamaa kufungua mlango.

Baada ya kufungua ilibidi tuingie wote ndani na wakati huo alionekana Iryn akiwa anahema sana, alionekana ni mtu aliyekuwa amechoka sana kama alikua jogging.

Kwa upande mwingine ni kama alikua haamini macho yake kama sisi tuko pale, na pant yake ya jeans ilionekana imefunguliwa nzipu na chupi yake ya pink ilionekana kwa mbali, pia upande wa juu alikua na brass kama ungeendelea kumwangalia ungeishia kudindisha tu kwa ule uzuri wake na alivyokuwa vile.

Iryn alikuja haraka kwangu na akanikumbatia na alianza kulia palepale, na dada Manager alikua kafika eneo la tukio tayari, na akaanza kuhoji ni nini kinaendelea pale.

MANAGER: “Ni nini kinaendelea hapa, maana matukio yanayoonekana hapa ni kama ubakaji, kaka shida ni nini?”

Jamaa alikua kimya na ikabidi dada ahamie Upande wa Iryn.

IRYN: “Dada mimi najishughulisha na masuala ya body therapy hii ndo kazi yangu, na ninafanya kwa wateja wengi sana. Huyu mteja tuliwasiliana toka juzi hata chats zetu hizi hapa (muda huu Iryn alikuwa ameshika simu yake Iphone 13 Pro Max ambayo ilionekana kuweka crack kubwa kwenye kioo na akamwonesha zile chats manager).

MANAGER: “Haya ndo makubalino yenu, endelea nakusikiliza”

IRYN: “Tulikubaliana ninafanya massage na sio zaidi na alikubali, nimemaliza kazi yangu naomba malipo akasema hawezi…..”

Dada Manager alimkatisha Iryn na alimwuliza swali,

MANAGER: “Malipo mlikubaliana kiasi gani?”

IRYN: “Tulikubaliana $1500”

MANAGER: “Okay Endelea”

IRYN: “Nilivyomaliza kazi yangu niliomba malipo yangu lakini alianza kuomba sex, nilimwambia I can’t do sex ni nje na makubaliano yetu na nilimkumbusha we had a deal, akanambia ataniongezea $1000, lakini nilimkatalia na nilimwambia hata apandishe dau kiasi gani siwez fanya sex. Na yeye akasema bila sex hanilipi na mimi sikutaka kubishana naye nilivyotaka kuondoka nilishindwa fungua mlango sababu ya card, na yeye akagoma kufungua mlango, nikaomba card ili nifungue mlango lakini hakutaka kunipa wala kunifungulia.”

SHAHIDI: “Pole sana dada huu ni ubakaji.”

IRYN: “Muda huo akanivuta kwa nguvu na akanisukumia kitandani akanambia siwezi kutoka mpaka tusex. Muda huu nilikua sijui cha kufanya maana nilipiga kelele lakini hakuna msaada wowote niliopata. Ilibidi nimwambie atafute condom bila hivyo sitoweza na alikwenda kuchukua kwenye bag. Mimi muda huo ndo nikapata nafasi ya kutuma text kwa dereva wangu huyu hapa. Alivyorudi akanambia nivue nguo zangu lakini nilimgomea sababu nilikua najua dereva wangu atakuja haraka kunisaidia. Alinishika kwa nguvu akanivua brauz yangu na tukaanz purukushani kwa zaidi ya dk 20 sasa, inamaana msingekuja leo ningekua raped.”

Maneno ya Iryn yalifanya tusijikie vibaya wote muda ule na kila mtu alikua anashangaa kwa lile tukio. Jamaa alikua anaforce kula mzigo tena kwa kutaka kubaka.

Kiukweli hata mimi ningeforce muda ule yaani uwe na mrembo kama yule umwache aende ni inataka moyo sana. Jamaa kimuonekano alikua ni lightskin na alikua ni mtu wa Uingereza.

Muda ule jamaa alianza kuomba msamaha kwa kile kilichotokea na alikiri alikosea sana, upwiru ndo ulimplekea kufanya vile.

SHAHIDI: “Kaka nadhani mpaka sasa ushahidi upo na wewe umekiri nafikiri sheria zinaweza kuchukuliwa.”

Jamaa alimfata Iryn na alimwomba sana msamaha maana nadhani alikua anajua kwa UK raping na harassment ni kesi kubwa sana.

Kwa upande mwingine Manager naye hakutaka mambo yafike mbali na alikua akijaribu kutafuta solution na Mlinzi, maana wao ile ni biashara isingeleta picha nzuri kama kesi ingefika mbali.

MANAGER: “Dada naomba haya mambo yaishe hapahapa please nakuomba sana.”

IRYN: “Dada hivi unavyoomba haya mambo yaishe kirahisi hivi ningebakwa je? Ungesema hivi?”

SHAHIDI: “Dada mimi nimerecord maongezi yake akiwa ameconfess alichofanya nafikiri nenda kashitaki huu ni unyanyasaji.”

Kwa upande mwingine jamaa alikuwa haamini macho yake na alionekana kuwa na wasiwasi sana. Na pia alikua akijutia kwa alichofanya muda ule na aliendelea kuomba yale mambo yaishe kwa namna yoyote. Kilichoniuma sana kuona jamaa kapiga magoti akiomba msamaha, kama mwanaume nilijiskia vibaya sana kuona baharia anapiga magoti.

Mimi niliteta na Iryn pembeni nikamwambia amsamehe Jamaa, sababu hajamfanya kitu chochote zaidi ya kumharras afanye kusamehe tuendelee na mambo mengine maana kwa Tanzania kesi kama hizi ni kupoteza muda. Iryn alinambia anaweza mpigia simu Mama Janeth na akaisimamia kesi na sheria ikachukua mkondo wake. Mimi nikamwambia cha muhimu jamaa amlipe simu yake, pesa ya simu mpya na usumbufu, mengine amwachie Mungu tu, na Iryn alikubali kufanya hivo.

“Insider nasamehe kwa sababu yako, ila alichonifanya siwezi kusahau ni udhalilishaji na unyanyasaji.”

IRYN: “Manager kutokana na masuala yenu ya kibiashara nitajali hili maana kuna siku nitarudi tena hapa ila ninauwezo wa kuiendesha hii kesi vizuri kabisa. Naomba nilipwe pesa ya simu mpya, hii imecrack sababu yake, anilipe pesa yangu $1500 na ninataka $4000 za usumbufu, simu ni kama $1800 kama yuko tayari kutoa $7500 mimi nitasamehe.

SHAHIDI: “Dada kwanini unamsamehe kirahisi hivyo wakati ushahidi upo na atakulipa pesa kibao, usiwe na haraka naweza kukusaidia Mwanasheria.”

IRYN: “Dada ni kweli unachosema ila sisi sote ni Binadamu kuna kesho, nina Mama yangu yuko Organization X ningempa taarifa hii kesi ingeisha haraka, ila nimeamua kusamehe tu.”

Jamaa ni kama hakuamini Iryn ameamua kumsamehe na jamaa aliomba alipe $6500 maana yuko Tanzania kikazi. Iryn aliamua kukubali na jamaa akafanya kutransfer hiko kiasi kwenda kwenye account ya Iryn

RAPIST: “You have an account in french bank?”

IRYN: “Yeah, transfer that amount to my account number.”

Pale wote tulibaki tunashangaa hata jamaa kama hakuamini kuona Iryn anamiliki Account kwenye moja ya bank za kifaransa, hata mimi nilishangaa maana Iryn hakuwai nambia hili, lakini pia sikuwaza sana maana nilikuambuka Iryn kasoma kule Ufaransa asingekosa kuwa na bank account kule.

Baada ya kutransfer Iryn alipata ujumbe kwenye email kuonesha pesa imeingizwa na akaaga tuondoke maana hakutaka tuendelee kukaa pale.

Na muda ule Manager alifurahi sana kuona jambo limeisha na alitusindikiza mpaka parking na muda huu walikua wakiongea na Iryn, mimi niliingia kwenye gari na nikatoa 50,000 nikampa mlinzi na alishukuru sana.

“Kaka Ahsante sana ila Bossy wako ni pini asee ni ngumu sana kuwa na mrembo kama huyu Getto afu umwache, ni balaa sana hii Dunia ina warembo wengine tunaishia kula kwa macho.”

Niliishia kucheka pale na tukaagana na jamaa pale. Manager aliendelea kuongea na Iryn na baada ya dakika 5 Iryn aliingia kwenye gari.

IRYN: “Insider lets go, twende home tu nikalale sina mood now.”

Tulianza kuondoka na muda ule kutoka eneo lile.

MIMI: “Iryn am so sorry for being late, nilikua nimelala yaani kitendo cha kupiga simu ndo nilishtuka”

IRYN: “I thought umelala that time hata hivyo thank you so much Insider ungechelewa kidogo ningebakwa. Kitendo cha kupiga simu ndo kilipelekea simu kuvunjika nilipambana sana.”

MIMI: “Nisingejisamehe maisha yangu yote kama jambo baya lingetokea, It was my fault”

IRYN: “It wasn’t your fault Insider, don’t be”

MIMI: “Yule ni nani na mlikutana wapi?”

IRYN: “Isabella ndo kani connect na huyu mtu, na mimi namuamini sana Isabella hata wateja anaonipaga sinaga shida nao.”

MIMI: “Pole sana Mummy unaonekana kupoteza so much energy”

IRYN: “Insider nimepambana sana usiione hivi kumbuka yule mwanaume ananguvu kuliko mimi.”

MIMI: “Ilishawai kukutokea kama hii before?”

IRYN: “Hii ya leo ni too much, ilishawai nitokea ila sio kama ya leo, wengi nilokutana nao walikua hawanilipi.”

MIMI: “Pole sana najiskia vibaya ujue.”

IRYN: “Ni moja ya changamoto za kazi.”

MIMI: “Pole sana Mummy.”

IRYN: “Hii weekend sitotoka usiku maybe next week.”

Sikutaka kabisa kuleta utani hii siku maana Iryn alikua kabadilika sana na hakuwa mtu wakuongea. Na muda huu yule jamaa alikua anampigia simu Iryn, lakini Iryn hakutaka kupokea simu yake.

Tulipitia pale Mikocheni kwa Osama na nikamnunulia Iryn chips yai “zege” nilijua lazima ana njaa, tukaendelea na safari yetu ya kwenda kijitonyama.

Tulifika pale kwake na muda huo saa 6 usiku ilikua tayari, na nikampeleka mpaka ndani na nikamwaga naondoka nitamcheki .

IRYN: “Insider…”

MIMI: “Naam Mummy”

IRYN: “Thank you for today bila wewe ningeweza pata jambo baya sana.”

MIMI: “Usijali Iryn sisi ni Familia tayari.”

IRYN: “Naomba nipe account yako ni transfer Pesa, sina cash ya kukupa.”

MIMI: “No usifanye hivo.”

IRYN: “Why? you saved me today.” Iryn alikua mkali kidogo.

MIMI: “Have you forgotten our agreement?”

IRYN: “I remember”

MIMI: “So don’t, byee”

Muda huo Iryn hakujua aseme nini aliishia kuniangalia nikipotea machoni pake, na mimi nilitoka hapo nikarudi home kulala.

###########

Jumamosi ndo siku ambayo nilikua na miadi na Mama wa2 kama tulivyokuwa tumekubaliana mwanzoni mwa week. Nilifika kwake saa4 kasoro asubuhi na baada ya kufika pale, nilimpigia simu niko nje akasema sawa.

Hapa alipokuwa anakaa Mama wa2 ni apartment ambayo ina nyumba 2 tu, tena za kujitegemea kwenye compound moja.

Baada ya dakika chache alikuja dada wa kazi na akanifungulia geti akanambia amesema dada uingie ndani. Niliingiza gari nje kwake parking na nikaingia ndani seblen, sikuwa na wasiwasi sababu nilikua najua hana mme.

Upande mwingine alionekana dada akiandaa chai dining, na muda mfupi mama wa2 alikua katoka na amependeza sana.

MAMA WA2: “Insider mambo!”

MIMI: “Salama Mama mkwe , umependeza sana.”

(Alikua amevaa kipensi cha jeans na tishirt nyeupe zile za kubana)

MAMA WA2: “Eti eeh, karibu chai bhasi”

Na muda huu alikua akielekea dining na mimi nikamfuata kwa nyuma,

Mama wawili akaniandalia chai pale na tukaanza kunywa. Ilikua ni chai ya maziwa, chapati za maji, na maini ya roast.

MIMI: “Rachel yuko wapi? Simwoni”. (Rachel ni yule mtoto wake wa pili ambaye nampelekaga shule)

MAMA 2: “Rachel kalala bado.”

MIMI: “Muamshe mke wangu bhana.”

MAMA 2: “Yule akilalaga anamka mwenyewe.”

Baada ya ya kupata breakfast nilimshukuru Mama wa2 kwa chai na yeye alikwenda chumbani akatoka na mkoba, akasema yuko tayari kwa safari tuondoke.

Tukitoka pale kwake ilikua saa 4 na tukaanza safari ya kwenda Bagamoyo “The horizon”.

MAMA 2: “Insider itabidi tuingie ATM ya CRDB nitoe pesa sawa?”

MIMI: “Sawa bossy wangu, kuna ATM nitakupeleka.”

MAMA 2: “Nilishakwambia mimi sio Bossy wako.”

MIMI: “Sawa mama mkwe.”

MAMA 2: “Unakujua tunakokwenda?”

MIMI: “Ondoa hofu mimi ndo Insider.”

Tulitumia barabara ya Mwaikibaki ya Mbezi beach chini na tukaingia na ile barabara ya Mwamunyage, tukaja tokea kunduchi road hao tukaunga na Bahari beach.

Kabla hujafika Budget mbele kidogo ya Jambo supermarket kuna ATM za “NMB & CRDB upande wa kushoto wa barabara kama unakwenda Budget. Niliingia pale ili Mama wa2 aweze kutoa hela kama alivyokuwa ameomba.

MIMI: “Toa pesa nyingi bhasi tupate na hela ya mafuta.”

MAMA 2: “Leo nitakupa offa ya mafuta full tank”

MIMI: “Mvua itanyesha, unafanya kazi bank ila ni mbahili balaa.”

Muda huo alikua ameshuka kwenye gari ili aingie kutoa hela, lakini kulikua na foleni hivyo ilibidi asubiri mpaka ile foleni iishe na yeye ndo aingie. Si unajua mambo ya weekend tena, foleni ya kutoa pesa ilikua kubwa kubwa.

Mama wa2 alitumia kama dakika 5 mpaka anatoa hela na hao tukaondoka kuendelea na safari yetu.

MAMA 2: “Insider ukiona sheli ingia tuweke mafuta.”

MIMI: “Mama mkwe kumbe ulikua serious?”

MAMA 2: “Ulifikiri utani?, sasa subiri uone”

MIMI: “Leo unaonekana una vibe sana.”

MAMA 2: “Insider sijatoka muda mrefu sana, sijui ndo kuzeeka?”

MIMI: “Bado mbichi kabisa wewe, na unawazidi watoto wa 2000 mbali sana.”

MAMA 2: “Hahahaaa! Insider ningekua nimeolewa kama unayosema ni kweli, ona nimeishiwa kuzalishwa tu.”

Na muda huu tulikua tumeingia sheli ya ORYX pale Bahari Beach.

Na muda huu nilikua namsikiliza mama2 aseme tuweke mafuta ya shilling ngapi, na dada pale sheli alikua kaja upande wa dirishani kutusikiliza.

MAMA 2: “Dada weka full-tank”

Gari yangu ilikua na bar 2 tu za mafuta, sasa nilivyosikia full tank, nilifurahi sana.

Baada ya kujaza gari full tank, mama wa2 alilipia na nikaomba risiti kwa dada, nilikua siachi risiti baada ya kujaza mafuta.

MAMA 2: “Umeona eeh, leo nimekupa offa maana sjawai kukupa offa, japo wewe unanipaga offa sana.”

MIMI: “So unalipiza?”

MAMA 2: “Hamna narudisha fadhila tu.”

Ukweli ni kwamba licha ya kuingia mkataba na Mama wa2 ila bado nilikuaga nampa offa mfano, sometimes kama niko Posta nataka rudi home nilikuaga nina mpigia simu afu nampick nampeleka kwake for free, sababu tulikua tunakwenda njia moja.

Tulikwenda moja kwa moja na Bagamoyo road tulivyofika kijiji kinaitwa Zinga kuna sehemu tuliingia kulia, ilikua ndo njia ya kwenda “The Horizon”.

Muda tuliotumia kutoka Mbezi Beach mpaka tunafika Horizon ilikua ni kama saa 1 na nusu, na tulikwenda kuna sehemu moja ilikua imetulia na imejitenga.

Alikuja kaka ambaye ni mhudumu wa pale kutusikiliza na mama wa2 aliomba apewe mocktail na mimi niliagiza mocktail pia. Mocktail niliyoagiza mimi inatengenezewa ndani ya nanasi. (Nanasi linatobolewa afu mixers zinawekwa humo, ni nzuri sana)

Mama wa2 alinonekana kulipenda eneo hili jinsi ya utulivu wake na pia kulikuwa na watu wastaarabu sana maeneo haya.

Tulitoka hapo tukaenda sehemu ya Range (kupiga shabaha), mama wa2 akawa anapiga shabaha zake pale na mimi nilimwacha mimi nikarudi kukaa.

Muda huu Mary alinipigia simu na nikapokea simu yake haraka;

MIMI: “Hi Mary”

MARY: “Salama uko poa?”

MIMI: “Niko poa Mary, siku yako inakwendaje?”

MARY: “Leo ni weekend uliahidi tunatoka out.”

MIMI: “Yes nakumbuka ila niko Bagamoyo kuna mteja nimemleta huku namsubiri kama nitawai rudi nitakucheki sawa?”

MARY: “Sounds like today’s impossible.”

MIMI: “No I can’t break my promise.”

MARY: “Insider sema hutaki tu, hauko Bagamoyo wala nini.”

MIMI: “Mpaka nikutumie Location ndo uniamini?”

MARY: “I don’t trust you.”

Baada ya kumaliza kuongea naye nilimtumia palepale Location na Mary alionekana kukasirika sana. Sasa baada ya kumtumia Location kwa whatsapp na palepale alinipigia simu tena;

MARY: “Insider Horizon uko na nani?”

Hapo ndo nikakumbuka kumbe location niliyomtumia imeniumbua.

MIMI: “Nimemleta mteja Mary, si nimekwambia lakini?”

MARY: “Insider acha kuniona mimi mtoto, yaani umepeleke mteja Horizon na umsubirie tu, from nowhere?”

MIMI: “So you don’t trust me?”

MARY: “Insider mimi sio mtoto, huko upo na demu mnakula bata not more, anyway mimi sio mtu muhimu Kwako na nilishaliona hili.”

MIMI: “Mary huko unafika mbali sasa, nyie ni washikaji zangu sana.”

MARY: “Prisca akiomba date muda wowote unamkubalia ila mimi naomba kwa mara ya kwanza unani avoid.”

MIMI: “Mary si nimekwambia nikirudi nakucheki? Usinilaumu wakati siku haijaisha, kumbuka hii ni kazi yangu.”

MARY: “Insider bye have a good time there”
Na mary akakata simu.

Mary alionekana kuwa na hasira sana alikua kama mtu aliyepaniki na mimi nikampotezea sikutaka kujihangaisha naye kabisa.

Na baada ya saa mama wa2 alirudi kutoka range na alikuwa anahema sana;

MIMI: “Vipi kulikoni?

MAMA WA2: “Insider nimepatia shabaha 2, hahahaah” alikua akicheka

MIMI: “Muda wote huo ulotumia ndo umepata shabaha 2 tu?”

MAMA WA2: “Eeh Insider.”

MIMI: “Unachezea hela tu.”

MAMA WA2: “Afu kwanini umenikimbia?”

MIMI: “Niliona michezo ya kitoto ile.”

MAMA WA2: “Eeeh mimi nimeupenda mzuri kweli.”

MIMI: “Sawa bhana”

Na muda huo alikuja jamaa mmoja akasema kama tunataka kwenda kisiwani kuna boti inatoka beach sa10 na gharama zake ni 10,000 kwenda na kurudi kwa kichwa. Na mama wa2 alifurahi hizo taarifa na akalipa 20,000, alinilipia na mimi.

Na muda huo tuliagiza chakula maana ilikua ni mchana saa7 tayari imefika na njaa zilikua zikiuma sana. Tuliendelea kupiga story pale na tulikua tukizungumza sana mambo ya maisha, Mama wa2 alikua ni mtu ambaye alikuwa na mipango mingi sana.

Kupitia mazungumzo yetu niliweza kujua kwamba Mama wa2 anajenga nyumba Madale, pia anabiashara ya kutoa huduma za kifedha kwa simu na Bank. Hivyo akanambia anampango wa kufungua biashara ya mapazia na urembo wa nyumba.

Aliniuliza mipango yangu pia na sikusita kumwambia baadhi ya mipango yangu, nilimwambia kesho ambayo jumapili ninakwenda Dodoma kwaajili ya mambo ya ujenzi. Na alinipongeza sana akanambia kama nitahitaji mkopo kutoka bank nimwambie atanisaidia kupata kwa haraka na bila masharti mengi.

Tulizungumza mambo mengi sana na alikua pia akiniuliza sana kuhusu origin yangu na kuhusu familia yangu na maisha yangu kwa Ujumla.

MAMA WA2: “Hivi Insider unakaa wapi?”

MIMI: “Mbezi Massana kule juu.”

MAMA WA2: “Kumbe hutokei mbali.”

MIMI: “Sio sana ila kuna kaumbali.”

MAMA WA2: “Kidogo kule kumechangamka sana.”

MIMI: “Sababu ya Hospital naona pia ni kama kacentre flani hivi.”

MAMA WA2: “Chuo umesoma wapi?”

MIMI: “Chuo X “

MAMA WA2: “Mtoto wa mjini wewe, ndomana baada ya kumaliza chuo hukutaka kurudi home.”

MIMI: “Niliamua kuhustle hapahapa mjini. Hivi kwanini huna mpango wa kumiliki gari.?

MAMA WA2: “Nilikua na gari mbona, mwakajana nilipata ajali mbaya sana Insider na gari ilikua haifai. Nashukuru Mungu nilitoka salama kabisa, niliitengeneza ila gari na nikauza, sitak kusikia tena habari za gari, ila nikimaliza ujenzi nitanunua.”

MIMI: “Pole sana na ilikua gari gani?”

MAMA WA2: “Harrier, na nilichukuaga mkopo kisa gari.”

MIMI: “Pole sana Mama mkwe.”

MAMA WA2: “Ahsante, gari hata mwaka haikufikisha ikala mueleka.”

Na baada ya kumaliza kula tuliagiza wine na tukaendelea kunywa taratibu pale huku story zikiendelea.

Mida ya saa 10 jioni tulitoka na kwenda Beach kwaajili ya kwenda kisiwani, sasa kama unakwenda kupanda boti beach kuna kidaraja cha mbao kizuri sana na watu wanapendaga sana kupiga picha pale. Na pale Mama wawili alinipa simu yake nimpige picha na mimi sikuwa na hiyana nikampiga picha za kutosha.
(Kwa mtu anayekwenda Horizon lazima apige picha pale)

Tulipanda kwenye boat na kwenda kisiwani, Boat lilikua kubwa na tulikua kama watu 30 mle ndani. Kilikua ni kisafari cha kama dakika 20 mpaka kufika kisiwani. Muda huo kila mtu alikua na simu yake akichukua self wengine wakichukua video na wengine wakipigana picha, ilikua ni burudani kwakweli.

Tulifika kisiwani na tuliwakuta watu wengine kule, yaani kulikua na watu kibao pale kisiwani. Ni kisiwa kadogo sana wala sio kikubwa kihivyo. Na mle kisiwani kulikuwa na michezo kibao kama mpira wa miguu, na wanawake walikua wakicheza netball, ilikua ni burudani sana asee.

Tulikua watu wazima mle kisiwani na full vibe wanawake walionekana na vichupi, wengine taiti nknk, wanaume wapo waliokuwa na boxer na wengine bukta. Mimi nilikua nimevaa track nikavua nikabaki na boxer, kwa upande mwingine nilimwona mama wa2 kwa mbali akiwa na taiti alivua kile kipensi chake.

Tulitengeneza timu za watu sita (6) na zilikuwepo team 3 sasa ilikua ni mtoano. Tulilisakata kabumbu pale na kila mtu alikua na vibe sana mle kisiwani. Hakuna sehemu ngumu kusakata kabumbu kama Beach asee unatumia sana energy watu walikua wanaflop balaa.

Kuna muda tulipumzika na Mama wa2 akaomba twende upande wa2 wabahari na akaomba nimpige picha.

Tulikaa pale mpaka saa 12 ndio tukaanza kutoka pale kisiwani, wakati tumepanda kwenye Boat, Nahodha aliuliza kama wote tumefika kabla hatujaondoka na seat zote zilikuwa zimeenea.

Tulitumia kama nusu saa hivi kuwasili pale Beach na tulirudi tukakaa na tuka order vinywaji, muda huu palionekana kupendeza sana maana kulikuwa na watu wengi wakinywa, wakienjoy maisha.

Mama wa2 aliagiza Savannah na mimi niliagiza Heineken kinywaji changu pendwa. Muda ule hata mimi nilikua nahamu ya kuvibe, maana sikuwa na miadi na Iryn. Nilichungulia simu yangu na nikakuta, Prisca, Mary na Mama J wamenipigia simu.

Nilishangaa sana kuona Mama J kanipigia simu na alikua kanitumia text ambayo ilisomeka

“Naona nimekupa chance ya kuwa na Malaya wako ndomana hunitafuti.”

Palepale nilitabasamu nikasema Mama J tayari hasira zimeisha. (Mama J ni mtu ambaye hapendagi kufosiwa huwa anataka maamuzi afanye mwenyewe ndomana mimi na yeye tukigombana, huwa namuacha atulie kwanza au anitafute mwenyewe hapo ndo tunayajenga).

Nilimuaga Mama wa2 naenda kwenye gari maramoja ili nimpigie simu, na nilitumia muda huo kumpigia Mama Junior lakini hakupokea simu, nilipiga mara3 lakini hakupokea simu zangu.

Muda huo nikampigia simu Prisca na alipokea muda uleule ni kama mtu ambaye alikua akisubiri simu yangu kwa hamu sana.

PRISCA: “Hi Insider”

MIMI: “Safi tu, now uko sawa?”

PRISCA: “Yeah, ulisema tuonane tuongee”

MIMI: “Ndio nafikiri tufanye J3 Prisca maana kwa leo itakua ngumu si unajua leo ni weeknd kazi ni nyingi?”

PRISCA: “Jumatatu ni mbali sana why not tomorrow?”

MIMI: “Kesho nasafari ya Dodoma ndomana nikasema nitakuona Jumatatu.”

PRISCA: “Insider unaondoka hata hunambii are you serious?”

MIMI: “Sorry hata hivyo safari imetokea haraka tu, haikuwa kwenye mipango yangu.”

PRISCA: “Unakwenda kufanya nini Dodoma?”

MIMI: “kuna kazi mzee amenituma nikaifanye.”

PRISCA: “Kazi gani.?”

MIMI: “Prisca sijajua bado ila nikienda ndo nitajua maana kuna mtu nitaonana naye nikifika.”

PRISCA: “Na unarudi lini?”

MIMI: “Prisca si nilikwambia narudi jumatatu na tutaonana? Nitatumia ndege ili niwai.”

PRISCA: “Okay nilisahau na unaondoka muda gani?”

MIMI: “Natakiwa kuchek-in saa 2 asubuhi naondoka saa4”

PRISCA: “See you later, byee.”

Kuhusu Mary sikutaka kuhangaika naye hata kumpigia maana nilikua sina cha kumwambia muda ule, zaidi ningemdanganya tu.

Muda ule nilirudi kwa Mama wawili na tukaendelea kunywa pale, Mama wa2 akaanzisha maongezi,

MAMA WA2: “Vipi ulienda kuomba ruhusua nini?”

MIMI: “Hahaahaa nilikwenda chukua chaji ya simu na muda huu nilikua nimeishika mkononi.”

MAMA WA2: “Kama wamekupigia simu sema bhana tuondoke.”

MIMI: “Wewe ukisema tuondoke ni sawa mimi sina shida kabisa. Nikalale mapema kesho nasafari asubuhi.”

Nilikaa pale tukaendelea na story na muda ule Mama wawili alinonekana na furaha sana,

MIMI: “Mama mkwe naona leo unafuraha sana kuliko siku zote.”

MAMA WA2: “Leo nimeinjoy sana kule Beach honestly huku nitakuja tena, nilikuona unasakata kabumbu upo vizuri sana.”

MIMI: “Mpira ni kipaji changu sana, nimechezea team ya shule wakati niko form4 na 6.”

MAMA WA2: “Nilikuona asee unakimbiza balaa.”

MIMI: “Si unajua life is too short, If you get a chance celebrate.”

MAMA WA2: “You only live once”

MIMI: “Vipi lakini kuhusu mwanao Pili anaendeleaje na masomo?

(yule mtoto wake wa kwanza ambaye yuko Advance).

MAMA WA2: “Yuko salama kabisa na jana nimeongea na Matron wao yuko vizuri.”

MIMI: “Anasoma wapi?

MAMA WA2: “Yuko hapo Kerege Marian Girls.”

MIMI: “Sasa mbona hukusema tupitie kumsalimia?”

MAMA WA2: “Insider kuna tarehe special za visiting, pia watapewa likizo kwaajili ya Easter.”

MIMI: “Hongera sana kwa kuwa na bint mkubwa, soon utaanza kula matunda yake.”

MAMA WA2: “Insider sipendi bint zangu waje kuwa kama mimi mama yao.”

Na muda huu tuliongeza vinywaji vingine na mama wa2 alikua akitawala mchezo katika maongezi.

MIMI: “Kwanini? Maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.”

MAMA WA2: “Insider you know sometimes sisi wanawake tunapitia vipindi vigumu sana, kuna mwanaume kukuoa na mtoto ni ngumu sana. Mimi siwezi kuwa na mume tena mpaka kufa kwangu.”

MIMI: “You never know, sometimes Mungu anakua na mipango yake huwezi jua kakupangia nini na amekuepusha na nini.”

MAMA WA2: “Unajua sometimes tunamwonea Mungu, kwamba alipanga mimi kuwa single mother?. Unajua Mwanamke bila mume hajakamilika, hakuna mwanamke asiyependa kuolewa Insider. Mwanaume ni kama kiongozi kwenye mahusiano au familia, unafikir najiskiaje kuona wanangu hawawaoni baba zao? Mwanaume mpaka ajiskie ndo anakuja kumwona mtoto atlist rachel anamwona Baba yake mara kwa mara ila Pili anaenda mwaka hajamwona Baba yake.”

MIMI: “Aisee pole sana, unakidonda kikubwa sana Mama mkwe.”

MAMA WA2: “Usione tunavaa tunapendeza tunacheka lakini nakidonda kikubwa sana moyoni. Nashukuru Mungu na kazi ambayo inanipa kipato napata pesa ya kuishi na Familia yangu.”

MIMI: “Kwani Baba yake na Pili yuko wapi?”

MAMA WA2: “Yuko Mwanza ni moja ya wanaume ambao wamesababisha mimi leo kuwa hivi.”

MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”

Kwa kifupi kutokana na maelezo ya Mama wa2 alisema alikutana na Baba Pili mwaka 2003 mwanza wakati anafanyia kazi kampuni moja huko. Baada ya hapo wakaanza mahusiano na Baba yake Pili ni mfanyabiashara, hatimaye akapata mimba ya Pili ila baadae alikuja kujua jamaa ana mke na watoto wa2. Na kipindi hicho alianza kupata vitisho kutoka kwa mke wa jamaa, na pia kutokana na kuwa na mimba kampuni ikamwachisha kazi ikabidi afanye mchakato wa kurudi kwao Moshi kwa Mama yake.

Baada ya kuzaa alikaa kama miaka 2 kwao akimlea mtoto na hicho kipindi chote Baba mtoto hakuwai mtafuta wala kujua hali yake. Baada ya hapo alianza kutafuta kazi na akapata moja ya shirika pale Moshi na alifanya kazi mpaka 2012 ndo akapata connection na moja ya wateja wake. Anasema kwenye lile shirika alikuwa akilipwa mshahara kidogo sana na kipindi hicho alikua anakaa kwao. Huyo mtu alimuunganisha Mama wa2 na huyu mtu ambaye ndo Baba yake Rachel kwa sasa.

Baada ya kupewa namba za Baba Rachel aliwasiliana naye na akamtumia CV yake, Baada ya Mwezi alimpigia simu aende Dar es salaam kwaajili ya training. Mama wa2 anasema alishangaa sana maana hata hakufanya Interview yoyote, jamaa alifanya kumsaidia tu. Alifika Dsm na alikutana na Jamaa ambaye alimpokea na baada ya kumaliza training alipangiwa kazi hapahapa Dar es Salaam. (Baba yake Rachel ni moja ya watu wakubwa sana kwenye hiyo Bank hapa nchini na ni moja ya Directors anaonekana sana kwenye TV).

Baada ya hapo Jamaa alimtongoza kutokana na jamaa kumsaidia hakusita kumkatalia sababu ndo aliyemsaidia kupata kazi. Lakini Jamaa alimwambia kuwa ana mke tayari na wakakubaliana akipata mtu sahihi awe huru kuolewa naye. Waliendelea kuwa na mahusiano ya siri mwisho wa siku akapata mimba ya Rachel, hakutaka kutoa mimba ikabidi azae tu ndo kupata mtoto wa pili.

MIMI: “Aisee yule ndo Baba yake Rachel?”

MAMA WA2: “Ndio yule ni Baba yake Rachel, Nashukuru anampenda sana mwanaye huwa anatafuta muda sana wa kukaa ba Bint yake japo ndo siri mke wake hajui lolote.”

MIMI: “Kama anajali mtoto sio mbaya, vipi kuhusu Baba Pili ndo alitelekeza mtoto.?”

MAMA WA2: “Baba Pili alikuja kunitafuta wakati Pili ana miaka 2 ndo kidogo akaanza kutuma Pesa za matumizi na kumwona.”

MIMI: “Mama mkwe ulipitia kipindi kigumu sana, pole sana.”

MAMA WA2: “Ahsante kipindi niko pale Moshi na lile shirika nilipata mwanaume ambaye alinipenda sana na alikua tayri kunioa ila nilivyomwambia nina mtoto alikimbia nduki na hakuwai nitafuta tena, kwa ujumla nilipata wanaume 3 lakini wakisikia habari ya mtoto ndo inakua tiketi ya kuondoka.”

MIMI: “Muda bado Mama Mkwe utapata tu wa kukuoa usiwe na wasi wasi umri bado unaruhusu.”

MAMA WA2: “Insider Mwanaume kamili aliyekamilika ambaye hatumii hisia kwenye maamuzi hawezi kukubali kuoa mwanamke aliyezalishwa na Mwanaume mwingine. Insider wewe uko tayari kuoa mwanamke ambaye amezalishwa na mwanaume mwingine?”

MIMI: “Hapana kwakweli siwezi.”

MAMA WA2: “Sasa unaona! Mimi huwa nawashangaa sana vijana wanaoa single mothers hata kama ni kupenda ila ni Risk sana.”

MIMI: “Aisee kwamba hutaki Single mothers waolewe?

MAMA WA2: “Hapana ila kwa Mwanaume hakikisha Baba mtoto amekufa na akuonyeshe kaburi otherwise hesabu maumivu. Ila wapo wanawake single mothers wanajitambua ila ni wachache sana.”

MIMI: “Unachosema ni kweli na upande wa Single fathers?”

MAMA WA2: “Tofauti wanaume anaweza kuzaa na mwanamke yoyote yule, wanaume wana tamaa tofauti na mwanamke anazaa na mwanaume anayempenda regardless kama anapendwa au laah!”

MIMI: “Naona leo umenipa lecture ya Mapenzi.”

Na muda huu tulikua tunaendlea kunywa bia kwa wingi sana kama ratiba za kurudi home zilipotea hivi,

TUTAENDELEA!

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
.
 
Vitu anavyopendelea INSIDER MAN
IMG_3702.jpg
 
EPISODE 21

“Insider……. Nimekubali option ya kwanza kwa zile mbili ulizonipa.”

ENDELEA……..


Na muda huu nilitumia kusogea pale kitandani na kumsogelea karibu maana alikua amekaa kitandani.

“Prisca kwahiyo umekubali kuwa mchepuko?”

Prisca alijibu kwa kutingisha kichwa kuonesha yuko tayari kufanywa kuwa mchepuko wa Insider.

“Kwanini unataka nikufanye mchepuko? Nafikiri option 2 ingekua nzuri zaidi, tuwe washikaji tu.”

“Ulinipa choice sasa nimechagua option ya 1. Nimeridhika hivyo kwa maamuzi yangu.”

“Okay haina shida kama umeamua hivyo ila…..” Prisca alinikatisha wakati nikiendelea kuongea.

“Insider, nioneshe picha za mke mkubwa bhasi nimjue hata kwa picha na mtoto wangu.”

Nilichukua simu ambayo ilikua mezani na nikaanza kumwonesha picha za Mama Junior, pamoja na zile za Junior.

“Insider umefanana sana na mwanao copyright.”

“Risasi zangu mimi ni genuine grade A”

“Hivi na mimi nikipata mimba si tutapata mtoto mzuri sana, tena atakuwa wa kike.”

Yaani tuseme Prisca alikua tayari karidhika kuwa mchepuko kiukweli nilishangaa sana, na bado akaanza kuleta story za kushika mimba, nilimwona mwanamke wa ajabu sana.

“Upate ujauzito na mme wa mtu, are you serious?”

“Insider najikuta natamani kupata mtoto, Junior ni mzuri sana. Najikuta natamani na mimi nipate mtoto.”

“Embu nenda kaoge tuondoke maana ulisema unataka kurudi mapema home au tulale hapahapa?”

“Natamani ila Mzee Mapembe yupo leo, acha nikaoge tuondoke.”

Ile anashuka kitandani nika muwasha kibao cha kalioo “Paaah”

Nilijiona Alpha kwakweli nikasema sasa huyu nitampa sheria zangu ili asije kuleta sintofahamu huko mbeleni, lazima nimcontol kama remote, maana nikifanya makosa tu itakula kwangu.

Na muda huu niliwaza asajili namba mpya ila kwa jina lingine, na pia nitampa ratiba za kuwasiliana naye pamoja na kuchat na mimi.

Na wakati huo alikuwa katoka kuoga kajifunga taulo kuanzia usawa wa matiti kushuka chini, na mimi nilivyomwona tena akiwa vile nikaanza kusisimuka. Na palepale nikamsogolea nikampiga kingine cha kuondokea nyumbani.

Nilimrudisha kwao saa 6 usiku na mimi nikaondoka kurudi kulala.

**********

Asubuhi Muajemi alinipigia simu na akaniomba niende kwake saa4 asubuhi kuna sehemu twende wote, na mimi niliikubali ile offa sikutaka kumkatalia Tajiri.

Saa4 ilipowadia nilikwenda kwa Muajemi na yeye alikua anakaa msasani unaingilia kushoto kabla hujafika Tanesco Mikocheni. Na alikuwa hakai mbali sana na maeneo yale.

Nilifanikiwa kufika pale anapoishi maana alikuwa kanitumia location kupitia Telegram, Muajemi alikua anatumia sana huu mtandao sijui kwanini.

Ilikua ni nyumba ya ghorofa 2 na ilikua nzuri sana na alikua anakaa na mke wake (Mke mdogo) na alikuwa amezaa naye watoto wawili (2).

Mlinzi alinifungulia geti na nikapark gari langu, alitoka dada wa kazi kunikaribisha, na ndani ya dakika chache Muajemi alikua ametoka na tulikaa garden.

MUAJEMI: “Bro! Hapa ndo naishi, jiskie upo nyumbani.”

MIMI: “Ahsante sana”

MUAJEMI: “Dada tuletee chai tunywee hapahapa na Insider.” Nilishangaa kuona dada anajua kuongea kiingereza.

MIMI: “Bro! shemeji yuko wapi?”

MUAJEMI: “Yuko mishemishe anachacharika”

MIMI: “Na watoto?”

MUAJEMI: “Watoto wako shule”

Tulikaa pale na Muajemi tukipiga story mbalimbali na moja kubwa alilisema ana mpango wa kufungua Filling stations hapa Tanzania, ila bado anakutana na upinzani mkubwa sana hasa kutoka kwa wenye mamlaka.

Saa 5 ndo muda tuliotoka pale na tulitumia gari yake Range sport nyeusi. Mimi nilikua sijui tunakwenda wapi lakini tulikwenda mpaka Kigamboni “South Beach hotel”.

Aliniacha na alikwenda kuonana na watu wake na alitumia masaa 3 wakatoka. Baada ya hapo tulikwenda Kurasini kwenye ofisi za Puma, na tukaondoka pale tukarudi Posta.

Tulikwenda kwenye duka moja kubwa la simu ambalo ni la mke wake alinambia hivyo, tukaenda mtaa wa India kwenye maduka ya Jewerly na tukaingia moja ya duka kubwa pale, alinambia nalo ni la mke wake.

“Insider ukitaka pete ya uchumba, pete za harusi, necklaces kila kitu kipo hapa”

“Bro! hizi bei mimi siwezi kwakweli.”

“Wewe utapewa discount usijali.”

Hapo ndo nikajua kumbe zile zawadi alizompa kwa Iryn alizichukua madukani.

Tulitoka hapo tukaenda pale Holliday inn tukapata chakula japo ilikua jion tayari. Na wakati tuko pale tulikuwa tukizungumza mambo mengi sana.

MIMI: “Tanzania una muda gani toka umeanza kuja?”

MUAJEMI: “Bro! Tanzania nimeanza kuja since 2008, kampuni yetu inafanya kazi karibu nchi zote za Africa, tunauza hizo pumps za mashine za sheli, tunauza lubricants za aina zote. Kwa upande wa mafuta kampuni yetu ina deal kama middle man, kwa ufupi tunaingia mikataba na serikali na makampuni mbalimbali hasa kwa Africa.”

MIMI: “Na kuhusu lubricants?”

MUAJEMI: “Bro! sisi ni exporter ila kila nchi tuna Madalali wetu tunaofanya nao kazi, ndo biashara zinavyokwenda hapa duniani, middle man huwezi wakimbia. Mfano tuna export contena 20 za lubricants kuja Tanzania kwa Agent yetu (middle-man) yeye anasupply kwa agents zake.”

Muajemi aliniambia siri nyingi sana hasa kwenye mafuta alisema watu wanapiga sana hela hasa hawa viongozi wa serikali, sitaki kufungua code kabisa. Muajemi alisema viongozi wa Africa wengi ni ma middle man wanakula sana hela huko, invoice zinachezewa balaa, ila mnaoumia ni nyinyi watumiaji wa mwisho.

MIMI: “Vipi mnawasiliana na Iryn?”

MUAJEMI: “Bro hata jana nimempigia simu, nikamwambia mzigo wake umefika tayari, aliniambia nimtumie account yangu anitumie pesa. Nimeshangaa sana na nimeona dharau sana kwangu.”

MIMI: “Hahahaha wewe ulifanyaje?”

MUAJEMI: “Nilimwambia nimempa offa tu, alinambia pia hakuna cha bure hapa duniani”

MIMI: “Unajua nini, we fanya kumwomba mtoke out, uendelee kumsogeza karibu.”

MUAJEMI: “Badae nitaongea naye, ukisha mpelekea mzigo wake.”

Tulitumia kama nusu saa pale na tulielekea Upanga na kuna mtu tulikutana naye ambaye ni Muajemi alikuwa, akatutolea ile mizigo kwenye Box, na zilikua box 7.

Kijana alipanga kwenye buti vizuri na tukaondoka kurudi Msasani, na muda huo ilikua giza limeanza kuingia.

Tuliwasili pale kwake na akanambia jumapili anakwenda Saudi Arabia hivyo lazima aonane na Iryn haraka iwezekanavyo. Mlinzi alikuja akatoa ile mizigo kwenye gari na akaipanga kwnye gari yangu.

Nilimuaga Muajemi pale na alitoa hela mfukoni akanikabidhi mkononi, alizitoa bila kuhesabu. Nilimshukuru pale na nilivyofika kwenye gari na kuhesabu zilikua ni 420,000/=.

Niliwasiliana na Iryn muda ule akasema nitamkuta kwake, nilifika pale nikafungua geti nikaingiza gari ndani. Na muda huo jirani alikua pale nje amekaa kibarazani.

MIMI: “Jirani nakuona umepumzika huna baya.”

JIRAN: “Jirani nimechoka tu.”

MIMI: “Huonekani siku hizi, ulikuwa umesafiri nini?”

JIRANI: “Mimi au wewe? Maana mimi nipo wewe ndo umetutenga bhana.”

MIMI: “Ngoja nikasalimie ndani, badae bhasi.”

JIRANI: “Wahi baba, atakua amekumiss.”

Niliishia kucheka tu nikasema lait Jirani angelijua hata asingesema hivi.

Niliingia ndani nikamkuta Iryn kalala kizembe pale seblen, maana alikua kavaa vile vibukta vifupi sasa mimi nikawa namwangalia pale kwa macho ya kifisi.

IRYN: “Insider vipi mbona sikuelewi?”

MIMI: “Unalalaje kizembe hivo.”

IRYN: “Sasa ulitaka nilalaje?”

MIMI: “Na mizigo yako kutoka kwa Muajemi ipo kwenye gari.”

IRYN: “Wow jana alinambia imefika, ila hataki nimtumie hela yake.”

MIMI: “Muajemi amekupa offa wewe unaleta habari za malipo”

IRYN: “There is no free meal in this world”

MIMI: “What do you mean?”

IRYN: “Twende tukatoe kwenye gari.”

Tulitoka nje na yeye alikuwa na kibukta chake vilevile tukasaidiana kutoa ile mizigo na tukaweka pale nje kibarazani. Na muda huo Jiran alikuwa akituangalia sana.

MIMI: “Hivi hapa kibarazani hawawezi kuiba?”

IRYN: “I don’t think so.”

Bhasi baada ya kumaliza kuweka zile box pale ambazo zilikua no vifaa vya saloon, kutokana na Iryn alisema zile mashine ni advanced kwenye upande wa saloon pia ni ghali. Na alisema zile mashine zimecost $24,000 mpaka kodi pale bandarini na zitakwenda Masaki.

Na wakati huo muda ulikuwa umekwenda sana, ilikua usiku tayari.

“Insider kesho uje mapema twende Posta nikanunue nguo maana nina hitajika kwenda kwenye ofisi ya mama.”

“Unakwenda muda gani?”

“Saa 7 mchana.”

Bhasi na mimi sikukaa pale kabisa nikaaga nikaondoka kurudi home maana nilitaka kurudi mapema nikaongee na Mzee Mollel nijue hata Ujenzi unakwendaje kule Dodoma.

*********

Ratiba zangu za asubuhi zilikuwa vilevile lazima nikawachukue wateja zangu lakini hii week ilikua tofauti kidogo toka nitoke Dodoma. Mtoto wa Mama wa2 naye alikuwa kaanza likizo ya Easter, hivyo nilikua namchukua Maggy tu.

Baada ya kumpeleka Maggy Posta ilibidi niende Kijitonyama mapema kwa Iryn kama tulivyokubaliana. Nilifika pale kwake na alikuwa bado kalala, nilimpigia simu na akatoka kunifungulia mlango.

Tulisalimiana pale na yeye akasema anakwenda kuoga ili tuwai kwenda mapema Posta.

Baada ya kuwasili Posta kuna duka tuliingia la nguo “special”. Iryn alinunua nguo nyingi tu pale za kiofisi ikiwemo suti ya suruali na alikua anajaribisha palepale.

Tulirudi haraka Kijitonyama na alijiandaa pale kwa haraka na alitoka akiwa amependeza sana. Alikuwa kavaa suti ya dark blue na ilionekana kumpendeza sana mrembo Iryn.

Tukaondoka kuelekea Masaki kwenye hio Organization. Muda huo ilikua saa 7 mchana na nilimshusha nje ya geti la Organization.

“Insider nitakupigia nikiwa tayari sawa?” na yeye akaingia ndani.

Mimi nilitoka hapo na nikatafuta chimbo kwa mbele nikapark gari langu.

Lengo kubwa la kwenda kwenye hii Organization ni kufanyiwa interview na kusaini forms, Iryn alisema wanamfanyia interview ili wajue zile pesa atazifanyia nini maana ni nyingi sana kwa umri wake.

Wakati niko kwenye gari nilikua nikiperuzi peruzi kwenye social medias nikiangalia mambo yanayoendelea na kutrend. Na muda huo Mary alinipigia simu, nilishangaa sana kuona akipiga simu.

MIMI: “Mary mambo.”

MARY: “Salama za kunisusa?”

MIMI: “Mimi au wewe ndo umenisusa?”

MARY: “Mimi sijakususa ila uliniboa, na unajua sababu.”

MIMI: “Ok am sorry, sindo unataka kusikia hivi?

MARY: “Insider juzi ulikuwa na Prisca?”

MIMI: “Why?”

MARY: “Insider ulikuwa na Prisca, don’t lie”

MIMI: “Afu Mary mimi sikuelewagi ujue, you keep asking me everyday. Mdogo wako akichelewa kurudi unaniuliza mimi badala umbane Prisca, this behavior has to stop”

MARY: “It’s okay, upo wapi?.”

MIMI: “Niko masaki now, unahitaji usafiri?”

MARY: “Kama utakuwepo Posta, jioni utanambia.”

MIMI: “Sawa Bossy wangu”

Na muda huo alikata simu [emoji3513]

Ukweli ni kwamba nikizurura hivi na Iryn nilikuwa naingiza pesa nyingi tu, sikosi laki, laki2 itadepend na yeye hio siku ana mood gani, japo kuna baadhi ya trip nilikua nakataa pesa zake.

Nilisubiri pale kwa almost saa zima nikimsubiri atoke na muda huo ndo alinipigia nisogee ili tuondoke.

Wakati nimesogea pale karibu nilimwona akiwa na Mama Janeth na wakapanda kwenye gari.

“Insider twende Levant tukale nafikiri ni sehem nzuri ambayo imetulia.”

Kutoka kwnye ile Organization hata sio mbali na ndani ya muda mfupi tulikuw pale Levant.

Na kila mmoja aliagiza msosi anaojua yeye na Mama Janeth na Iryn waliendelea kuongea, maana toka tukiwa kwenye gari walikuwa wakiongea sana, ni kama walikuwa wanaendeleza mazungumzo yao.

IRYN: “Mama ndo hivyo kama nilivyokwambia zile mashine zimefika tayari, utaziona ni nzuri sana na zitatusaidia.”

MAMA JANETH: “Na suala la massaji tutapata wataalamu na wakuaminika?”

IRYN: “Mama hata mimi nitawafundisha niko vizuri sana.”

MAMA JANETH: “Sawa mwanangu uwepo wako umekuwa baraka sana.”

IRYN: “Director muda ule alikuwa anasema Organization itanipa sponsorship ya Postgraduate, ni muda gani ita expiry?”

MAMA JANETH: “Hio ni wewe tu sidhani kama ina kikomo, vipi kwanini hutaki kufanyia kazi Organization?”

IRYN: “Mama si nitabanwa sana, na biashara zikayumba?”

MAMA JANETH: “Mbona mama yako alikuwa busy na mambo yalikuwa yanakwenda vizuri tu.”

IRYN: “Mama labda baadae kwa sasa hapana.”

MAMA JANETH: “Pale home unaishije? Maana sijaja na muda.”

IRYN: “Salama ila nafikiri mwezi ujao niondoke, ili uweke mtu ile ni biashara yako. Kipindi kile nilikuwa mgeni ila sasa nishayazoea mazingira, Insider ananisaidia sana.”

MAMA JANETH: “Hata mimi nakuona kuna utofauti mkubwa sana ulikuwa unajifungia tu ndani. Ila pale ni nyumbani unaweza kuendelea kukaa tu mwanangu hata usiwe na wasiwasi.”

IRYN: “Nataka nibadilishe mazingira pia.”

MAMA JANETH: “I understand.”

Tulitumia kama dakika 45 pale Levant na tukaondoka pale, tulimrudisha Mama Janeth kazini na sisi tukaondoka kurudi Kijitonyama.

Na wakati tunarudi tulitumia Kimweri Ave Road, hii barabara inakuja kutokea pale Mikocheni, Mwaikibaki road.

MIMI: “Iryn muda ule nilisikia mkiongea na Mama Janeth kuhusu kuhama pale Kijitonyama.”

IRYN: “Ndio Insider nataka kuhama pale, sikukwambia kama zile Apartments ni za mama Janeth?.”

MIMI: “Hapana hujawai kunambia.”

IRYN: “Ni Apartment zake, wakati nimerudi Tanzania kutoka Ufaransa nilifikia kwa Mama Janeth. Niliona nakosa uhuru wa kutoka usiku na kufanya kazi zangu, ndo nikamwambia nataka kupanga ndo akanionesha apartments mbili ya Mikocheni na hii ya Kijitonyama. Mimi niliipenda ya Kijitonyama ndo akaninulia vitu vyote unavyoviona mle ndani.”

MIMI: “Aisee kumbe”

IRYN: “Insider kukutana na wewe ni kama Baraka kwangu maana nilikuwa mtu wa kujifungia ndani tu.”

MIMI: “Nilikuahidi kukupeleka kula kitimoto na pia nitakupeleka ukale Biriani la selebonge.”

IRYN: “Week tayari hujatimiza ahadi.”

MIMI: “Better late than never.”

IRYN: “Don’t make Promises you can’t keep.”

MIMI: “Sema tumekula tayari, tena leo Ijumaa ningekupeleka pale kwa Selebonge tukale biriani.”

Tulitumia muda mchache kufika pale kwake baada ya kupark gari yeye aliingia ndani na mimi nikaenda kufunga geti.

Niliingia seblen na nikakaa kwenye coach na kwenye meza kulikuwa na kitabu kama magazine tuseme, kilikuwa ni cha mambo ya fashion, nilikuwa nakipitia nakiangalia yaliyomo ndani.

Wakati nikiendelea kuangalia picha za mle ndani nilisikia Iryn akiniita kutoka chumbani kwake,

IRYN: “Insider………”

MIMI: “Nambie mummy”

IRYN: “Come in please.”

MIMI: “In your room?”

IRYN: “Yes are you afraid? Njoo bhasi haraka.”

MIMI: “Okay am coming.”


TO BE CONTINUED

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Now
 
EPISODE 22

“A TRUE STORY BY INSIDER”

Na mimi muda huo niliinuka kuelekea chumbani kwake sikutaka kubisha, niligonga mlango na akasema niingie.

Nilifungua mlango na yeye alikuwa kajilaza kitandani, na muda huo macho yangu yote yalikuwa yakimwangalia Mwanamke mrembo aliyejilaza pale kitandani. Maana alikuwa na kibukta kifupi kinachoishia mapajani katikati, na upande wa juu alikuwa kavaa sport bras.

Sasa ule uzuri wake na vile alivyokuwa nikiona maungo yake vizuri tena live kwa macho nilijikuta nataka kupagawa na mimi sikutaka kuendelea kumtizama maana mnara ulishaanza kusimama wima.

MIMI: “Umeniita nakusikiliza”

IRYN: “Insider nataka unisaidie kutoa vitu humo kwenye makabati, nataka tuvipange vizuri.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

IRYN: “Afu Grizmann anakuja mwezi huu, anakusalimia.”

MIMI: “Msalimie pia, mwambie aje na mazaga bhasi.”

Room yake ilikuwa na zile kabati za kutengeneza moja kwa moja. Nilifungua kabati na droo zote moja kwa nyingine.

Sasa kila nikifungua droo nilikuwa nakuta simu na vitu vingine kama chaji, earpods, apple watches na saa. Baada ya kumaliza kukagua drow zote nilihesabu jumla ya idadi za simu na zilikuwa simu 14 ambazo ni Samsung na iphone. Samsung Galaxy S22 ultra (2), Iphone 12 Pro Max (3), Iphone 13 Pro (3) na Iphone 13 Pro Max (6).

Nilishangaa sana asee yaani mtu anakaa na simu nyingi vile ndani na zote zilikuwa ni brand new hakuna hata moja ilofunguliwa. Muda ule nilitamani niibe hata simu moja nifiche lakini ilikuwa ngumu kwa upande wangu. Kuomba simu pia nilikuwa siwezi maana nilipewa simu na Iryn na hakuwai niuliza kuhusu ile simu, nilimpa Mama J na nikachukua simu yake, tulifanya kuexchange na Mama J.

IRYN: “Insider hizo simu zipo ngapi?”

MIMI: “Jumla ziko 14, unakaaje na duka la simu ndani?”

IRYN: “Insidier hizo simu nilipewa kama zawadi tu na watu tofauti, kama hizo iphone 12 Pro Max nilipewa muda mrefu sana toka zinatoka.”

MIMI: “Aisee unabahati sana, unajua uzuri wako unawapagawisha sana wanaume.”

IRYN: “Insider umeanza tena, hizo iphone 12 kuna dada nitawapa saloon, wanani-furahisha sana.”

MIMI: “Na hizo zingine? Si bora hata uuze upate hela maana thamani zinazidi kushuka, na mwaka huu iphone 14 inatoka.”

IRYN: “Sasa naziuzia wapi?”

Nilitamani kumwambia aongee na Muajemi maana anaduka la simu lakini nikaona haitakuwa good idea, Muajemi angejisikia vibaya sana yaani kapeleka zawadi ya simu afu mtu anasimu kibao ndani.”

MIMI: “Niachie hili mimi, nitatafuta mtu wa kumuuzia.”

IRYN: “Okay sawa, nataka now nitumie na Samsung Ultra maana wanaisifia sana.”

Samsung S22 ultra ilikuwa released February lakini Iryn alikuwa nayo tayari tena mbili (2).

MIMI: “Sawa Bossy.”

Alinipiga jicho kali sana maana alikuwaga hapendi kusikia nikimuita hili jina.

MIMI: “Una nipiga jicho na hayo macho yako ya kirembo.”

IRYN: “Insider njoo angalia.”

Na muda huu alikuwa akinionesha picha zake na video mbalimbali alizokuwa Ufaransa.

MIMI: “Ulikuwa unashiriki fashion?”

IRYN: “Niligombea Miss college.”

MIMI: “Ikawaje?”

Na muda huu Iryn alikuwa akitafuta picha ya kunionesha,

IRYN: “Ona nilikuwa wa2, sikushinda. Huyu dada alishinda.”

Huyu dada aliyekuwa akinionesha ambaye ndo alishinda, alikuwa ni mhindi.

MIMI: “Ni kisu hatari.”

IRYN: “Kumbe hata wewe umeona, alishinda huyu alikuwa anasoma Finance.”

MIMI: “Hata hvyo ulijitahidi kuwa wa2 sio kitoto.”

IRYN: “Kupitia haya mashindano ndo nili-miti na Grizmann, kipindi hicho yeye alikua Masters.”

MIMI: “Everything happen for a reason.”

IRYN: “Yeah sure”

MIMI: “Hivi huko Ufaransa Grizz hakucheat kweli?”

Muda huu Iryn aliniangalia akaanza kucheka, ni kama hakutegemea lile swali.

IRYN: “Ana mke na watoto 2.”

MIMI: “Aisee na wewe umeridhika kuwa mchepuko?”

IRYN: “Insider Grizz kuna mambo ananisaidia mengi sana, sometimes we don’t have a choice.”

MIMI: “Ni kweli unachosema ila naona anakupenda sana.”

IRYN: “Yeah he loves me but ni mme wa mtu.”

Sikutaka kuendelea kumwuliza sana kuhusu Grizz na muda huo yeye alitoka kwenda Seblen akiniacha pale chumbani nikiendelea kumpangia vitu vyake.

Wakati amekwenda seblen Mary alikuwa akinipigia simu na Iryn alisikia simu ikiita.

IRYN: “Insider somebody Mary is calling.”

MIMI: “Njoo na simu bhasi.”

Muda huo nilitumia kuongea na Mary, alikuwa akiniuliza kama nipo around ili nikampick ila nikamwambia niko Kijitonyama. Mary pia aliomba kama tutaweza onana muda ule na nikamwambia maybe jumapili nitamcheki.

Na muda huo wakati nikiongea na Mary, kwa upande mwingine Iryn alionekana kuwa makini sana kusikiliza maongezi yetu.

IRYN: “Insider nani huyo?”

MIMI: “Kila nikiongea na mwanamke lazima uulize ni nani.”

Na Iryn kama hakufurahishwa na hili jibu nilimwona kamind flani hivi. Pia kama alijiona ananikosea sana kufuatilia calls zangu.

IRYN: “Ok Insider am sorry”

MIMI: “Usijali najua huna nia mbaya, huyu ni mshikaji wangu.”

IRYN: “Ngoja nikapike chap”

Na mimi nilitoka nikakaa pale seblen na muda huo nilikuwa nikiangalia Tv utafikiri ni Baba mwenye nyumba. Na mimi niliamua kwenda Jikoni kumsaidia kupika muda ule.

“Unanipikia nini Mummy?”

“Nilitaka kupika ndizi na nyama ila nimeona uvivu kumenya ndizi.”

“Si ungesema nikusaidie? Mimi niko kwaajili yako”

“Kesho nitapika usijali.”

“Sasa unapika nini?”

“Tambi za maini.”

Na muda huu mimi niliamua kutengeneza juice ya nanasi na story zikiendelea.

IRYN: “Insider Muajemi anataka twende Zanzibar kutembea”

MIMI: “Aaah mnakwenda lini?”

IRYN: “Ndo najifikiria hapa”

MIMI: “Wewe unapenda?”

IRYN: “Kwenda napenda, ila yule mtu simwamini bado.”

MIMI: “Kwamba unaogopa atakuteka?”

IRYN: “Hamna sio rahisi, anyway nitaangalia.”

MIMI: “Si unakwenda na mimi hapa Bodyguard wako.”

IRYN: “Hahahaah Insider huishiwi vituko”

MIMI: “Nimekwenda jeshini wewe cheka, sikutaka kuwa mjeshi tu.”

Na muda huo nikamwonesha cheti changu cha JKT kile cha Mujibu wa sheria, Iryn haya mambo hajui hivyo alishangaa sana, maana alikuwa haamini kama nilikwenda jeshini.

IRYN: “Insider kumbe umekwenda Jeshi, upo vizuri ndomana mambo yako ni chap sana, na unajali sana muda.”

MIMI: “Nitakulinda kila unakokwenda na hakuna wa kukuzingua.”

Iryn alishiia kufurahi tu muda huu hakuwa na chakusema, pia alisema kesho ambayo ni jumamosi angeenda kuonana na Muajemi. Na mimi niliunga mkono hili jambo kwa asilimia mia kabisa, maana Iryn angekua karibu na Muajemi mimi ningeendelea kufaidi matunda.

MIMI: “Vipi kuhusu kutoka usiku kwenye kazi zako.”

IRYN: “Tutaendelea next week nataka kudeal na wateja wa web tu kwasasa tena ambao wana offa nzuri tu.”

MIMI: “Sawa Bossy Lady.”

Baada ya kumaliza mapishi tulikula chakula na nikamshukuru kwa Dinna, nikamuaga nasepa muda ule, lengo langu ilikuwa kwenda barabarani kuendelea na majukumu ya kusaka pesa.

Wakati nataka kuondoka Iryn aliniita

IRYN: “Insider…. Leo tumeanza mwezi mpya, nikiwa nakulipa naomba upokee hela sijisikii vizuri kuona unakataa hela hata kama tulikuwa kwenye makubaliano.”

MIMI: “Sawa haina shida mummy”

IRYN: “Byee Insider takecare”

Nilitoka pale ilikuwa saa2 usiku tayari na mimi nikaendelea kupiga kazi non-stop, kama mnavyojua kwa Dar weekend ndo watu wanatoka out kutumia hela.

Nilipiga kazi mpaka saa 7 usiku na niliamua kurudi baada ya kupata mteja aliyekuwa anaelekea Mbezi Beach.

*********

Jumamosi niliamka asubuhi sana kama kawaida yangu na nilipiga sana kazi hii siku. Ile Asubuhi kwenye saa5 Msomali alinipigia simu na aliuliza niko wapi nikamwambia niko tabata Baracuda.

Msomali akasema kama nitakwenda mjini nimpigie simu anataka twende Mbweni na alisisitiza sana.

Saa 12 jioni ndo muda ambao nilionana na Msomali na alikuwa pale CBD hotel Gerezani.

Tulitoka hapo kwanza tulianza kupitia Mlimani city kuna mtu alikwenda meet naye na nilisubiri kama 1 hour. Baada ya hapo sasa tukaanza safari ya kwenda Mbweni na tulipitia Barabara ya Mwaikibaki ili kukimbia foleni ya Bagamoyo Road.

MSOMALI: “Insider gari yako ni safi sana na inanukia vizuri.”

MIMI: “Si unajua ofisi lazima iwe safi muda wote, hata hapa umekuta Gari ni chafu.”

MSOMALI: “Kwa hili unajitahid sana hongera.”

MIMI: “Ahsante sana Bossy wangu I really appreciate.”

Saa 3 tulikuwa tumefika Mbweni na tulifika sehemu anayokwenda tukaingia ndani na mimi nilikwenda msubiri kwenye garden

Msomali alitumia kama masaa 2 pale na akatoka akanambia tunakwenda Sea cliff hotel Masaki, ndo nitamwacha pale.

Wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story mbalimbali hasa za Maisha na mademu.

MSOMALI: “Insider kwa kipindi kifupi tulichokutana nimetokea kukubali sana, kuna deal nitakushirikisha by next week, au umeridhika na maisha ya Uber?”

MIMI: “Hapana Bossy sijaridhika maana hii kazi sometimes ni mateso ila ndo hivyo tunapambana kibishi. Kama deal zuri mimi napiga kwasasa nachoangalia pesa tu.”

MSOMALI: “Sawa haina shida Bro!, nitakupigia simu.”

MIMI: “Sawa Bossy nasubiri na nitashukuru sana.”

Tulifika pale Sea cliff na nikamshusha Msomali pale.

MSOMALI: “Bro nikupe kiasi gani? Maana hatukuelewana kabisa.”

MIMI: “Bossy wewe nipe utakayoona haitoniumiza mimi, si unaona wese limepanda bei? Vita ya Ukraine na Russia ndo imeleta majanga.”

MSOMALI: “Ni kweli Bro! vita ya wakubwa hizo sisi wengine ni watizamaji tu, wewe ongea kuwa huru.”

MIMI: “Ok kutoka Posta mpaka Mlimani city 15,000, kutoka Mliman mpaka Mbweni 25,000 na kutoka Mbweni mpaka hapa utanipa 30,000 unipa 70,000 sio mbaya.”

MSOMALI: “Haina shida Bro ngoja nikupe na offa ya bia maana leo weekend”

Msomali alinipa 100,000 na akaondoka pale huku akiahidi kunitafuta kwa ajili ya hilo deal. Na muda huo niliwaza Msomali atakuwa na deal gani?

Na muda huu nilipata request ya mteja alikuwa anakwenda Airpot na alikuwa palepale Sea cliff.
Na huyu mteja alikuwa kauzu sana nakumbuka, maana tulitoka pale Sea cliff mpaka Terminal 3 bila kuongea njiani.

Nilipiga kazi mpaka saa 9 usiku ndo nikarudi kulala, maana nilikuwa na usingizi hatari.

*******

Jumapili saa 4 asubuhi Mama Junior alirudi home na aliletwa na Mamdogo wake home. Niliwapokea na tulishinda na mamdogo pale home mpaka tukala chakula cha mchana na yeye akaaga.

Hii siku nilicheza sana na Junior maana nilim-miss sana, na Junior alikuwa mtundu sana kipindi kile mpaka sasa ni mtundu balaa huyu mtoto.

Mchana Iryn alinipigia simu akasema kama nitapata muda niende kwake ili nipeleke ile mizigo (mashine za saloon) kule Masaki kwa Mama Janeth.

Jioni saa10 nilitoka home na nikamwaga Mama J natoka ila nitawai kurudi tutoke out. Mama J alifurahi sana kusikia hizi taarifa maana ni kama alikuwa amemiss kutoka out na mimi mme wake.

Nilifika kwa Iryn ila sikuingia ndani na niliitoa ile mizigo kibarazani na kuiweka kwa gari. Muda huo nilihisi Iryn atakuwa amelala hivyo sikutaka kumsumbua kabisa. Kwasababu nilikuwa najua ile mizigo inakwenda kwa Mama Janeth nikasema acha niipeleke tu, nikirudi ndo nitamcheki.

Nilipeleka ile mizigo kwa Mama Janeth Masaki, baada ya kufika Mlinzi alinifungulia geti na nilimkuta yuko nje akipanda maua . Nilimsalimia nikamwambia nimeleta mizigo na nikaitoa nikaingiza ndani.

“Mwanangu Ahsante sana.”

Nilimwaga Mama Janeth na mimi nikaondoka kurudi kwa Iryn, na wakati niko njiani Iryn alipiga simu.

“Insider kumbe umepeleka mizigo kwa Mama Janeth.”

“Yeah, wakati nafika hapo ulikuwa umelala, sikutaka kukusumbua.”

“Nilitaka twende wote bhasi lakini.”

“Niko njiani soon nitakuwa hapo.”

Wakati narudi nilitumia njia ya Heilasie Road ambayo inakuja kutokea Bagamoyo Road, kwangu naonaga hii barabara ni rahisi, maana hainaga mambo mengi.

Nilitumia kama dakika 15 kufika Kijitonyama kwa Iryn na nilipark gari nje ya fensi getini, sikutaka kukaa sana pale. Lengo langu lilikuwa nirudi home mapema ili nitoke out na wife.

Niliingia ndani na nilimkuta seblen akichezea laptop yake ya Macbook, nilimsalimia na nikaenda kukaa kwenye kiti.

“Insider…….”

Iryn aliniita na mimi nikamtizama kumsikiliza anataka kusema nini;

“Naam mummy”

“Huyu ni mwanao?

Iryn alikuwa akionesha picha ambayo nilikuwa nimeipost whatsapp status nikiwa na Junior.

TO BE CONTINUED

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Now
 
EPISODE 25

“A TRUE STORY BY INSIDER”

Mary hata hakutusemesha bali aliomba nifungue gari ili atoe mkoba wake ndani ya gari. Na baada ya kuchukua mkoba wake aliondoka eneo lile.

MIMI: “Hivi Mary anajua kinachoendelea kati yetu?”

PRISCA: “Hapana hajui ila leo kajua na kuprove kabisa. Si unakumbuka nilikwambia kuhusu da Mary?”

MIMI: “Sawa bhana kazi kwako na dada yako. Mimi naondoka naomba utanambia kinachoendelea na urudi home mapema sawa?”

PRISCA: “Sawa haina shida”

Na mimi niliondoka eneo lile kurudi zangu nyumbani kulala, kwa upande mwingine nilifurahi Mary kufahamu kinachoendelea kati yangu na mdogo wake.
***

Jumatatu asubuhi Msomali alinipigia simu na akaniuliza maamuzi niliyoyachukua kuhusu lile deal na mimi nilimdanganya kuwa sipo na niko mkoani mara moja, hivyo nikirudi ningemcheki. Na yeye alisema hakuna shida ananipa muda wa mimi kuendelea kufikiria ili nifanye maamuzi sahihi.

Kwa upande wa wateja zangu nao wabeba, ambao tulikuwa na mikataba, nilikuwa na Mama wa2 na Maggy tu kwa kipindi hiki, maana hata madogo wa kule shule Masaki walikuwa likizo ya Pasaka.

Baada ya kuwapeleka wateja zangu Posta muda ule nilimpigia simu Prisca ili nijue kama walirudi home salama. Na baada ya kumpigia alipokea simu na tukaanza maongezi,

PRISCA: “Hi baby”

MIMI: “Umeamkaje na Unaendeleaje?”

PRISCA: “Niko salama Insider hofu wewe.”

MIMI: “Jana mmerudi sangapi?”

PRISCA: “Tulikaa mpaka saa 8 usiku.”

MIMI: “Aiseeh, yale mambo uliyokuwa unafanya jana bila aibu unakumbuka?”

PRISCA: “Hahahaa kwani vibaya Insider?, Wale ni watu wazima washajua kinachoendelea. Siwezi kuficha hisia zangu kwako kisa wao.

MIMI: “Sawa bhana umefanya vizuri, see you letter. Nilitaka kukujulia hali.”

PRISCA: “Ahsante Insider I love you.”

MIMI: “Byee”

Hii jumatatu pia niliongea kwa simu na Muajemi kupitia Whatsapp na yeye alikuwa bado yuko Saudi Arabia na alikuwa akinijulia hali. Muajemi aliendelea kunisisitiza niendelee kuongea na Iryn ili waende Zanzibar akitoka huko, na alisema hataki kwenda nyumbani ikiwezekana aunganishe moja kwa moja mpaka Zanzibar. Na alisema angerudi mwisho wa mwezi huu April, kwa upande wangu sikutaka kumwambia chochote kinachoendelea kati yangu na Iryn.

Biashara ya Uber ilianza kuwa ngumu hasa upande wa request maana abiria walikuwa wa tabu sana. Kilichokuwa kinanisaidia kipindi hiki ni wale wateja zangu wa bank kuwapeleka sehemu mbalimbali. Wateja wengi walikimbilia kwenye bajaji ili kupunguza gharama za maisha, maana nauli zilikuwa juu sana.

Jumatano Mama wa2 alinipigia simu na akaomba tuonane kwake usiku nikiwa natoka kwenye mishe zangu bhasi nipitie pale nyumbani kwake, na mimi niliukubali ule wito.

Baada ya kumaliza mishemishe zangu saa 2 usiku nilikuwa nimewasili kwa mama wa2 na nilikaribishwa ndani nikakaa seblen na yeye alikuwa jikoni. Na muda huu Pili alikuja seblen na alinisalimia pale,

“Shikamoo.”

“Marahaba mke wangu nimekuja hapa kwaajili yako ujue.”

Pili alionekana kuwa na aibu sana maana hta kuniangalia alikuwa anashindwa. Na wakati huu mama wa2 alikuwa dining akiandaa chakula mezani.

MAMA WA2: “Pili umemwona mme wako? anasema anasubiri umalize shule akuoe.”

Pili hakuwa na chakusema maana alishikwa na aibu sana, nilihisi huenda pili ni Virgin bado sio kwa zile aibu na pia alionekana kujipenda sana, Mama wa2 alikuwa na binti mzuri sana.

MIMI: “Mama mkwe mbona Pili ana aibu hivi? Ana umri gani?”

MAMA WA2: “Sema anakuonea aibu wewe hana lolote. Mwaka huu september anafunga miaka 18.

MIMI: “Pili unasomea nini?”

PILI: “PCB”

MIMI: “Nice kumbe nitaoa doctor.”

Na muda huu Pili alionesha kutabasamu, ila ni lile tabasamu la aibu.

Na muda huu nikaribishwa dining kwaajili ya kula dinna na sikuweza kukataa, japo nilisema nitakula kidogo ili nikirudi home nisigombane na Mama J.

Mimi ndo nilikuwa wa kwanza kumaliza kula na Mama wa2 alishangaa sana.

MAMA WA2: “Insider ongeza chakula hata kidogo maana nilipika kingi kwaajili yako.”

MIMI: “Mama mkwe hata usijali na unanijua vizuri mimi, ukweli ni kwamba navyotoka huko nilikuwa nimekula tayari.”

Nilikwenda kukaa seblen na baada ya dakika 10 Mama wa2 alikuja ili tuongee na alikuwa na bahasha mkononi.

MAMA WA2: “Insider mzigo wako huo hapo.”

Aliiweka ile bahasha mezani na mimi nikaichukua na nilivyoifungua nikaona kuna hela ndani.

MIMI: “Mama mkwe nilijua nina jaza mafomu ya mikopo.”

MAMA WA2: “Insider mkopo mdogo huo huna haja ya kujaza forms nimekusaidia kwa njia nyingine na hakuna riba. Wewe utarejesha hio hio amount, kama utakuwa unakwama marejesho bhasi uwe unasema tujue tunasaidianaje kurejesha.”

MIMI: “Ahsante sana mama mkwe, mimi sikujua unaniitia hili kabisa.”

MAMA WA2: “Kuwa na amani Insider”

Sikutaka kabisa kuuliza maswali sana, niliendelea kukaa pale huku tukipiga story mbalimbali na alisema weekend hii tutakwenda kuangalia nyumba yake anayoijenga Madale.

Niliaga pale kwake na nilimshukuru sana Mama wa2 kwa lile jambo na nikaondoka kurudi nyumbani. Wakati niko njiani nilikuwa na furaha sana kwakweli sikutegemea kupata kile kiasi cha pesa kwa haraka vile.

Habari mbaya kwenye hii week ya kwenda Pasaka, Uber walisitisha huduma za usafiri wa TAX kwenye Application yao, ila huduma za Bajaji na Bodaboda zilikuwa zikiendelea kama kawaida na ilikuwa 14/04/2022 alhamis kitu kama hicho, ila waliendelea na wateja wa Card tu na kampuni ambao walikuwa wameingia nao mikataba.

Hizi zilikuwa ni habari mbaya sana kwa madereva tulikokuwa tukitumia hii App. Kitendo cha Uber kusitisha huduma kwa upande wa magari kilinipa stress sana maana kwa Tanzania wateja wengi wanalipa kwa cash, nikawaza hapa itabidi nitumie Bolt ambayo nilikuwa siipendi.

**********

Ijumaa jioni Mzee Pama alinipigia simu na akaomba jumamosi jioni tuonane kwani ana mazungumzo muhimu na mimi, nilimkubalia na akasema tutakutana pale Budget Bahari Beach. (Mzee wa Ununio mwenye mchepuko wake Kigamboni)

Ijumaa mimi nilikomaa na Bolt na nilipiga kazi mpaka saa8 usiku ndo nikarudi kulala, biashara ilianza kuwa ngumu sana wateja walikuwa wakuokoteza sana. Yaani unaweza kaa hata saa2 bila ya kupata request na hapa ndo nikapata wazo la kununua bajaji, maana nilikuwa nikiwasiliana na madereva wa bajaji walikuwa wanasema kwa kipindi hiki wanapiga sana hela.

Nikakumbuka wife ana pesa kwa Baba yake na kuna kipindi alitaka kuzichukua nikamkatalia, nilimwambia aziache kwanza Baba yake azitunze. Baba yake aliahidi kumpa milion 5 ili zimsaidie kwenye mambo yake. Mzee wake alimwambia zile pesa ambazo anampa zilikuwa ni ada zake za masomo, sababu aliamua kuolewa bhasi atampa zimsaidie kwenye mambo yake.

Nikaplan nitaongea na wife ili tununue Bajaji na itakuwa ya kwake pesa itakayokuwa inapatikana itaingia kwenye mfuko wake. Niliona pale ni wazo zuri maana kama jambo litafanikiwa bhasi nitaweza kupunguza gharama nyingi sana.

Jumamosi ndo siku ambayo nilikuwa na miadi na Mzee Pama, niliamka saa11 asubuhi na hii siku nilipiga sana kazi na angalau pesa niliipata, japo Bolt niikuwa siipendi ila nilikuwa sina jinsi.

Saa11 jioni nilikuwa niko pale Magufuli stand mbezi mwisho nikisubir request na hapo nilikuwa nimeset destination ya Bahari Beach ambako nilikuwa nina miadi na Mzee.

Nilisubiri sana pale lakini sipati request na kuchoma mafuta kutoka mbezi mpaka Bahari beach niliona ni mbali sana afu hasara. Nilisubiri kwa saa 1 na nusu hivi ndo nikapata mteja alikuwa anaelekea Tegeta nyuki karibu na shule ya Canossa.

Baada ya kumshusha abiria nilikwenda na ile barabara ya nyuki inayokuja kutokea Bahari beach ndo nikaunga kwenda Budget.

Nilifika pale saa 2 kasoro lakini kwa upande mwingine mzee alikuwa bado hajafika, na ilimchukua dakika 20 Mzee Pama kufika eneo lile. Mzee Pama alifika moja kwa moja nilikokuwa nimekaa maana nilimuelekeza,

MZEE PAMA: “Nimeona gari yako hapo parking nikajua umefika muda sana, kwanza nisamehe kwa kukuchelewesha najua bado upo kazini.”

MIMI: “Usijali Mzee wangu kuwa na Amani kabisa.”

MZEE PAMA: “Kulikuwa na foleni kali sana pale Africana mpaka najuta kwanini sikupita barabara ya chini.”

MIMI: “Leo ni weekend lazima pawe na foleni, za siku na pole na majukumu Mzee wangu.

MZEE PAMA: “Ahsante sana kijana, kazi zinaendelea vipi kwa upande wako?”

MIMI: “Mzee kwa upande wangu ni ngumu, maana juzi tu hapa Uber wamefunga ofisi yao na wateja wamekimbilia bajaji, nauli ziko juu sababu ya kupanda kwa mafuta.”

MZEE PAMA: “Kweli kabisa bei za Petrol na diezel nimeona ziko juu sana hii ni hatari sana.”

Na muda huu dada alikuwa amefika kutusikiliza, wakati mara ya kwanza amekuja nilimwambia asubiri kidogo.

MZEE PAMA: “Kijana unaweza agiza chochote unachotaka kuwa huru.”

MIMI: “Dada naomba mchemsho wa Kuku na maji ya kunywa”

MZEE PAMA: “Niletee windhock na kuku choma nusu.”

Dada aliondoka na sisi tuliendelea na mazungumzo yetu,

MIMI: “Mzee uliniambia una jambo muhimu unataka kuniambia.”

MZEE PAMA: “Kuna jambo nilitaka unisaidie maana nalifanya kwa siri na sitaki ndugu au mtu yoyote wa karibu yangu alijue. Kwa muda mfupi tuliofanya kazi nimetokea kukuamini sana kijana na wewe ndo unajua siri yangu ya ule mchepuko hakuna anayejua mwingine zaidi yako.”

MIMI: “Kumbe! ni jambo gani mzee usiwe na wasiwasi mimi nitakusaidia kama litakuwa chini ya uwezo wangu.”

MZEE PAMA: “Ile nyumba ya Mbweni nayojenga bila shaka utakuwa unaikumbuka, tulikwenda wote kabla ya kwenda Kigamboni.”

MIMI: “Naikumbuka vizuri kabisa hata sasa naweza kukupeleka, ile mitaa yote ipo kichwani.”

Na muda huu mzee alicheka sana,

MZEE PAMA: “Kijana uko vizuri, sasa ile nyumba ni ya yule mke mdogo, niliamua kumjengea Mbweni ile niwe naye karibu ili hata nikitaka kumwona iwe rahisi. Kwasasa iko kwenye finishing kuna vitu vya kumalizia (kama kuweka makabati jikoni, masink, taa za ndani na nje, kuweka pavings, tiles, kupaka rangi na kutengeneza bustani nknk). Nataka wewe unisaidie kusimamia mpaka finishing ikamalike maana mimi ninasafari na nitarudi 26/04.

Nilishangaa kuona ule mjengo mkali ni wa yule mchepuko wake wa Kigamboni.

MIMI: “Mzee hilo halina shida ni jambo dogo sana kwangu nitalisimamia vizuri kabisa na wewe utafurahi.”

MZEE PAMA: “Sasa nitakukabidhi pesa na nitakupa list ya vitu na material nayohitaji kuweka mle ndani, nakuomba usimamie manunuzi na usitoe hela mpaka kazi iwe imefanyika, Constructor wa kwanza tuligombana alikuwa muhuni huyu ni mpya simwamini bado.”

MIMI: “Mzee hilo ondoa shaka kila kitu kitakwenda vizuri”

MZEE PAMA: “Ahsante sana gharama zako tutaongea nikirudi wewe usiwe na wasiwasi.”

MIMI: “No problem Mzee wangu.”

Tulimaliza maongezi pale na mimi nilikuwa nimemaliza kunywa soup yangu, alifanya malipo na tukaongozana kwenda kwenye gari yake, ilikuwa ni Fortuner mpya kabisa na namba zake za usajili zilisomeka DY.

“Kijana fungua mlango ingia”

Nilivyoingia ndani Mzee alifungua drow na akatoa bunda za pesa ambazo alisema jumla ni 37 million.

MZEE PAMA: “Makubaliano yetu ni 36.5 million, hapo itabaki laki 5 hiyo itakusaidia mafuta, chakula na mambo mengine.”

Na muda huu akatoa karatasi ambayo imeandikwa mahitaji ya kununua kwaajili ya ujenzi.

MZEE PAMA: “Na haya ndo mahitaji yenyewe naomba uwe makini sana kwenye hizi materials, huku ndo tunakopigwa hela sana na unaweza wekewa fake, hakikisha fundi hakuzidi ujanja.”

MIMI: “Mzee hili halina shida kwangu wewe fahamu umekutana na mtu sahihi.”

MZEE PAMA: “Nikirudi tutaonana na ujenzi unaendelea kule, jumatatu unaweza kwenda kuanza kukagua, nitampa namba yako na wewe nitakupa namba ya fundi, mimi naondoka kesho ila tutakuwa tunawasiliana kwa whatsapp”

Mzee alinipa namba ya simu ya constructor na alitoa bahasha ili niweke zile pesa na tukaagana muda huo.

Mimi nilikwenda kwenye gari yangu na nikaziweka zile Pesa kwenye drow na nikaanza safari ya kurudi home. IST ilikuwa imebeba pesa za kununua wenzake kama watatu hivi, zilikuwa Pesa nyingi sana na sikuelewa kwanini Mzee Pama kaniamini sana vile.

Barabarani niliendesha gari kwa spidi sana maana niliogopa nisije kutekwa na Pesa za watu muda ule, na mapema tu nilikuwa nimefika home.

Na huu usiku Mama wa2 alinipigia simu akafanya booking ya gari kwaajili ya kesho ambayo ni Pasaka na tukakubaliana tuonane kwake 08:00 asubuhi.

********

Asubuhi nilimka mapema nikafanya mazoezi ya viungo kwa ujumla na baada ya hapo nikaingia bafuni kuoga na muda huo mama J alikuwa amelala bado.

Wakati navaa ndo nasikia Mama J akiniita,

WIFE: “Baba J asubuhi yote hii unakwenda wapi? Inamaana hujui leo kuna sikukuu?”

MIMI: “Mke wangu nakwenda kutafuta hela si unajua leo sikukuu kazi ni nyingi, hata leo na kazi na mtu.”

WIFE: “Sawa ila sisi tunakwenda kula sikukuu nyumbani.”

MIMI: “Mimi sina tatizo kama umeridhia ni jambo jema kuwa na familia labda unambie utahitaji kiasi gani cha pesa nikupe.”

WIFE: “Tutatoka out pia wewe utakayoona inatosha sawa tu.”

MIMI: “Afu naomba tuongee jambo ili ukienda huko nyumbani uone unafanyaje.”

WIFE: “Jambo gani?”

MIMI: “Nataka tununue Bajaji maana Uber imekuwa ngumu kwa sasa wateja wamekimbilia Bajaji. Ulisema kwa mzee wako kuna hela kama unaweza ongea naye akupe hizo hela, lengo langu hio bajaji iwe yako na Pesa itakayokuwa inapatikana itaingia kwako. Nataka kupunguza gharama si unaona tuna ujenzi kule na pesa zinaishia kule?. Ukifanikisha hili sasa hapo nitakupa mpango mzima.”

WIFE: “Sawa ni jambo zuri sana nitaongea na Mzee na nitakupa mrejesho badae nikirudi.”

MIMI: “Ila usiseme lolote kwa Mzee, wewe angalia ni namna gani utaongea naye ili akupe hizo hela, usiongee masuala yoyote.”

WIFE: “Nimekuelewa Baba J usiwe na wasiwasi.”

Nilitoa laki moja nikampa zimsaidie kwenye matumizi yake ya sikukuu na mimi nikaondoka kuelekea kwa Mama wa2.

Nilifika mapema kabisa pale nyumbani na nilikuwa getini pale nje, nilipiga honi na Mama wa2 alitoka haraka ni kama alikiwa akinisubiri na alitoka na mwanae Pili wakaingia kwenye gari.

“Insider mambo, nataka twende sokoni sasa sijui twende wapi nahitaji na Kuku wa kienyeji wawili wakubwa”

“Hapa uhakika na soko kubwa twende Tegeta nyuki naamini utapata unachotaka.”

“Sawa twende bhasi chap.”

Tulikwenda Tegeta Nyuki sokoni kufanya manunuzi na siku hii soko likikuwa na wateja sana hata parking zilikuwa za shida. Tuliingia sokoni kufanya manunuzi na mimi nilikuwa nikimsaidia kufanya manunuzi na kupeleka mizigo kwenye gari.

Mimi hata niwe smart vipi kwenye suala la kuwasaidia wateja nilikuwa active sana, na hiki kilifanya wateja wanipende sana.

Tulitumia kama 1 hour hivi mpaka kumaliza manunuzi na baada ya hapo tulirudi home.

MIMI: “Mama mkwe mbona leo umenunua vitu vingi sana?”

MAMA WA2: “Na wageni leo ndomana, kuna rafiki zangu wa kazini wanakuja na pia kesho nina ugeni wa mdogo wangu kutoka Moshi.”

PILI: “Mama kumbe mamdogo Joana anakuja kesho.”

MIMI: “Kumbe una mdogo wako hongera sana.”

MAMA WA2: “Ehh Pili anakuja kesho…..Insider kesho tutakwenda AirPort kumpokea wote.”

MIMI: “Sawa haina shida Mama mkwe.”

Tulirudi pale kwa Mama wa2 na nikawasaidia kutoa vitu kwa gari na nikaingia ndani kupata Breakfast.

Na wakati niko kwa Mama wa2, Maggy pia alinipigia simu kuniwishi Pasaka na akanambia kama sitojali niende kwake maana hana kampani.

Mama wa2 hii siku alionekana kuwa busy sana na mimi sikutaka kuendelea kukaa pale na nilitamani sana kuondoka.

MIMI: “Mama mkwe kuna kazi yoyote ya mimi kufanya? Nataka nikukimbie.”

MAMA WA2: “Insider kwakweli hakuna nilitamani sana twende kule Madale ila tutakwenda kesho. Unataka kuondoka na hujala? Subiri chakula.”

MIMI: “Usijali nitakula kesho acha nikawasalimie ndugu zangu.”

Nilitoka pale kwake ilikuwa saa 7 mchana na wakati niko kwenye gari nilimpigia simu Prisca kumuwish sikukuu ya Pasaka. Na pia hii siku nilitamani sana ningeimaliza na prisca.

MIMI: “Hi bae, happy Easter”

PRISCA: “Thank you honey nilikuwa naogopa kukupigia maana nilijua upo nyumbani na mke mkubwa.”

MIMI: “Yeah sure ulifanya vizuri.”

PRISCA: “Honey karibu home bhasi hapa napika vitamu kwaajili yako, are you coming?”

MIMI: “Mmmh hata wewe unajua kupika? Hahahahahaha.”

PRISCA: “So unanicheka kwamba sijui kupika?, Insider hizo dharau has to stop.”

MIMI: “Baby utani tu unachukia, nilitaka kuspend na wewe leo vipi it’s possible?”

PRISCA: “Kwa leo ngumu maana mzee yupo na amesema tutatoka out kama family badae, pia niko period hapa mwenzako.”

MIMI: “Oohh sawa haina shida have funny mummy.”

Niliona Prisca hana deal tena kaanza kuniletea story za period tena na nikasepa zangu kwenda kwa Maggy Mikocheni.

Baada ya kufika Mikocheni kuna duka niliingia nikanunua wine na soda na mazaga mengine huyo nikaelekea kwake. Nilivyofika pale kwake nilifungua geti na nikaingia ndani na nikapark gari usawa wa apartment yake.

Niligonga mlango haikuchukua muda alitoka kufungua lakini alishangaa baada ya kuniona mimi ni kama hakuamini hivi.

MAGGY: “Yaani Insider sikujua kama unakuja ujue.”

MIMI: “Unipe mwaliko afu nisije? haiwezekani kabisa.” Na muda huu nilikuwa nampa ule mfuko.

MAGGY: “Waow! Umenunua nini?, Jamani thank you, karibu ndani.”

Niliingia ndani akafungua ile wine na akaniletea glass.

MAGGY: “Insider wewe endelea mimi napika huko jikoni. Nimefurahi kukuona maana nilikuwa bored hatari kuna best yangu kanipiga chini.”

MIMI: “Wewe endelea usijali.”

Maggy alionekana kufurahi sana muda huu ni kama nilimsaprize sana kwa upande wake. Na mimi nilikaa seblen nikaona acha niende jikoni tukaendelee na story.

MIMI: “Nakuona upo busy mwenyewe.”

MAGGY: “Nataka nimalizie kupika chap hapa vitu vingine nilikuwa nishapika tayari.”

MIMI: “Leo nitaonja mapishi yako kwa mara ya kwanza.”

MAGGY: “Hahahaa hivi hujawai eeh”

MIMI: “Sijawai zaidi ya mayai ya kukaanga”

MAGGY: “Usijali mimi niko vizuri sana jikoni. Insider nimefurahi sana ujio wako ujue maana niliona siku ishaanz kuwa mbaya.”

MIMI: “Usijali mimi nipo na wewe mpaka majogoo kama utataka, I’m not going anywhere.”

MAGGY: “Badae itabidi tutoke out bhasi au unaonaje.”

MIMI: “Nishasema nipo hapa kwaajili yako wewe utakachosema mimi nitakusikiliza leo.”

MAGGY: “Umetoka kazini?”

MIMI: “Hapana leo sikukuu napumzika, pesa zipo tu.”

MAGGY: “You are right.”

MIMI: “Ukiwa jikoni unaonekana kuwa sexy sana.”

MAGGY: “Mmmh Insider kweli? mimi naona unanizingua tu hapa.”

MIMI: “Kweli you look so sexy”

MAGGY: “Mmhh”

Tulipiga sana story hii siku na Maggy ila kwenye mazungumzo yetu nilikuwaga sithubutu kabisa kuongelea suala la mahusiano yake. Maana ningempa greenlight ya kuuliza mahusiano yangu na mimi sikutakaga wateja zangu wajue maisha yangu.

Saa 11 jioni tulitoka na tulikwenda “Cape Town Fish Market” tulikaa pale mpaka saa 5 usiku. Sikutegemea kuona Maggy kuwa mnywaji mzuri wa pombe kiasi kile na alizipeleka Savannah 8. Kwani nilikuwaga namchukuliaga mwanamke ambaye yuko busy na mambo yake. Maggy alionekana kulewa sana hii siku.

Tulitoka pale Capetown mpaka saa 6 usiku kasoro na nilidrive mpaka Mikocheni anakoishi. Nilifungua geti na nikaingiza gari ndani, na muda huu Maggy alioneka kalewa sana tofauti na wakati tunatoka kule Capetown. Japo alikuwa anajitambua, nilimsaidia kumtoa kwa gari na tukaingia ndani.

TO BE CONTINUED
Nitarud
 
Unatembea nazo hawa watu sijui wanabisha nini wakati utaratibu ni kudeclare ila sasa wewe mtanzania kubeba million 50 ni mzigo kwanza na hizo pesa unazipeleka wapi?

Kwa dollar ni simple sana hata kuzicarry unaweza weka dollar $50k kwenye surual freshy kabisa.
Extra ya USD 10 000 ni lazima ku declare. Watu wanabeba sana kwa magendo.
 
Kuna sehemu BROKE BOYS kaeleza vizuri. Na ndio utaratibu ulivyo. Kuna kiwango cha pesa huulizwi kusafiri nacho ila kiwango kinachozidi lazima kiwe na maelezo kuzuia utakatishaji wa fedha. Hii ni kutia ndani kiwango cha pesa kichotumwa au kuingia kupitia Bank toka nje ya nchi.
Na hii sheria imewekwa ili kukabiliana na illicit financial flows.
 
Back
Top Bottom