Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

You said it all, am afraid kuna namna tu asipoweka sawa huyo mke lazima atafute kisasi tena kikubwa

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kuna shida kwenye hii thread, naambiwa Error. Nitaleta Extra Episode.
Asante sana mkuu kushare nasi. Tumeburudika. Huna baya mwanangu. Mimi nakutakia kila la kheri ufanikiwe sana mwamba. Kwa jinsi ulivyo mvumilivu,unavyopanga mipango yako. Usivyo na papara. Jinsi unavyojibu,yaani niseme tu elimu yako imekusaidia mwamba. Hongera na Asante sana INSIDER MAN .

Umezalisha kitu kipya vichwani mwa wengi waliopitia hii tred. Binafsi ilikuwa kila nikisoma,hasa hii epsode ya mwisho nilikuwa najiona kama ni mimi vile,kama ndoto fulani nzuri. Nasema umezalisha kitu kipya ksbb inakuwa kila nikipitia hii story najiona imara fulani,hata kama napitia matatizo fulani najiona mpya mwenye kuweza kuyashinda hivi.
Asante sana
 
Ukweli mchungu
 
Ni kweli kuficha ficha haitasaidia. Atafute muda amuambie mama J ukweli, then mama ataamua kusuka au kunyoa mapema.
Good advice kama mtoto keshazaliwa na no way mama j asije kujua Cha kufanya ni Bora Insider akamueleza yeye mwenyewe kwamba ana mtoto na bi dada Iryn na anataka kumfanya kuwa mke mdogo najua mwanzo ata mind lakini atatulia .
 
Kmmmk
 
INSIDER MAN ...achana na mambo ya kumtambulisha Iryn na mtoto Kwa wazazi wakati huu. Mama Yako ni mtu makini sana, anawezakukupa maelekezo yatakayokuweka mahali pagumu sana.

Kumbuka unatarajia kufunga ndoa(kubariki ndoa) muda si mrefu, hizi habari za mtoto zitatibua na kuibua mambo mengine. Kwa maoni yangu, ungekamilisha Hilo zoezi la ndoa kwanza, huku ukisikilizia mambo yanaendaje.

Mie nilisha ambiwa, siku ikitokea taarifa za ujauzito au mtoto wa nje ndio mwisho wa mahusiano na wife. Akasema yuko radhi kumtambulisha watoto wengi wajae fuso ila kama walipatikana kabla ya kufahamiana nae ila sio tukiwa wote.

Inabidi uongeze sasa mdogo wa hao watoto kwa Mama Jr. Naona Iryn ndio anamoto wa kukuzalia mtoto mwingine, angalia asije akasawazisha na kuongoza ligi...

Ni kweli hautaki kuendelea kulipwa mshahara kwenye kazi za Iryn, lakini hauoni kuondoka kwako inaweza kusababisha mambo yakayumba kibiashara mkapoteza wote?

Unaweza kufanya mambo mengine lakini ukaendelea ku oversee hizo biashara.

Kwenye extra episode 06 haujagusia suala la Mama Janeth na mtoto wa Iryn, hajawahi kujua wewe ndio baba wa huyo mtoto?

Kingine unakibarua kizito sana, tena sana cha kukaa mbali na akina Mary, Mdogo wake Jane, mtoto wa Mzee Juma na walimbwende wengine, siku ukijichanganya, ikathibitika pasi shaka umechepuka, Kwa akili za Iryn zilivyo, hasira zake anaweza kumshirikisha Mama Jr kuhusu hizo tabia hata kama na yeye atakua matatani lakini hatakua na cha kupoteza. Usiwaumize mioyo hao wake zako, Iryn akijua unachepuka ni bora ukajifiche Gaza.

Mwisho wa siku maamuzi unayo wewe kiongozi.
 

kwanza hongera kwa kupata mtoto, lakini fanya hivi
1. Usifanye siri hili jambo kwani ipo siku litajulikana tu.. mpeleke Iryn na mtoto nyumbani kwenu kumtambulisha wamjue damu yako.

2. Mwambie ukweli mama J kuwa una mtoto umezaa na Iryn na usimfiche chochote. mwache yeye aamue kuolewa au aache kuolewa na wewe..usimuoe bila yeye kufahamu hili jambo na aridhie mwenyewe kuwa kuna mke mwingine.

3. Mwambie mama J kuwa utafunga ndoa ya serikali na pale kuna option ya wewe kuwa na wake wawili au zaidi ili umlinde Iryn na watoto utakaozaa naye, watoto wote wana haki kwa baba yao.. Mama J anatakiwa ajue kabisa kuwa anaolewa na wewe lakini kuna mke mwingine ambaye naye utafunga naye ndoa..

4. Usithubutu kumuoa mama J bila ya kumpa taarifa ya mke mwenzake ambaye ni Iryn..yani ajue kuwa anaolewa kama mke wa kwanza na pia kuna mke wa pili. usisahau kuwa huyo mama J ni mchaga na mtusamehe tu wanawake wa kichaga wengi huwa wanabaki wajane jiulize kwa nini.. na hasa akigundua mume wake ana wanawake wengine na watoto huko nje mawazo yao yote huwa ni kwenye mali na kuwamaliza waume zao.. tusije tukaanza kuimba parapanda bado tunakupenda Insider..

5. Mama J akikataa kuolewa na wewe kwa sababu ya kufahamishwa kuhusu Iryn basi pambana na hali yako na umuoe huyo Iryn na ikibidi uchukue mwanao ulee wote pamoja..nakuusia usifanye siri kwa mama J kwani madhara yake ni makubwa huko mbele labda kama huwajui wachaga..
 
Umetoa mawazo mazuri sana.
 
Nenda kaongee na wazazi wako pamoja na ndugu zako kuhusu kuzaa na Iryn. Toa msimamo wako kuwa utaendelea nae. Mtaitisha kikao pande zote mbili kuzungumza hili.
Mama J ataamua kuolewa nawe au la. Mwanzo utalaumiwa sana ila baadae utaonekana mwanaume jasiri. Lakini kumuoa bila hii taarifa utakuwa umemlaghai.

Sikushauri kabisaaa umwambie mama J mkiwa wawili tu; yaani wewe na yeye. Maamuzi anayoweza kuchukua hujui.
 
Sio kwamba ata kataliwa kumuoa mama j hapana. Ila kwenye ukristo hakuna wake wawili so ndoa itafungwa vizuri ila shida inaanza wewe kutaka kulazimisha uhalali wa wake wawili.

Kibinadamu tupo sawa mana ni nature ya wanaume kuwa na watot wengi toka enzi ila utashindana na imani yako mpk kufa kwako, unless uwe muslim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…