kwanza hongera kwa kupata mtoto, lakini fanya hivi
1. Usifanye siri hili jambo kwani ipo siku litajulikana tu.. mpeleke Iryn na mtoto nyumbani kwenu kumtambulisha wamjue damu yako.
2. Mwambie ukweli mama J kuwa una mtoto umezaa na Iryn na usimfiche chochote. mwache yeye aamue kuolewa au aache kuolewa na wewe..usimuoe bila yeye kufahamu hili jambo na aridhie mwenyewe kuwa kuna mke mwingine.
3. Mwambie mama J kuwa utafunga ndoa ya serikali na pale kuna option ya wewe kuwa na wake wawili au zaidi ili umlinde Iryn na watoto utakaozaa naye, watoto wote wana haki kwa baba yao.. Mama J anatakiwa ajue kabisa kuwa anaolewa na wewe lakini kuna mke mwingine ambaye naye utafunga naye ndoa..
4. Usithubutu kumuoa mama J bila ya kumpa taarifa ya mke mwenzake ambaye ni Iryn..yani ajue kuwa anaolewa kama mke wa kwanza na pia kuna mke wa pili. usisahau kuwa huyo mama J ni mchaga na mtusamehe tu wanawake wa kichaga wengi huwa wanabaki wajane jiulize kwa nini.. na hasa akigundua mume wake ana wanawake wengine na watoto huko nje mawazo yao yote huwa ni kwenye mali na kuwamaliza waume zao.. tusije tukaanza kuimba parapanda bado tunakupenda Insider..
5. Mama J akikataa kuolewa na wewe kwa sababu ya kufahamishwa kuhusu Iryn basi pambana na hali yako na umuoe huyo Iryn na ikibidi uchukue mwanao ulee wote pamoja..nakuusia usifanye siri kwa mama J kwani madhara yake ni makubwa huko mbele labda kama huwajui wachaga..