Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Wee, mimi nilimfuma aliyekuwa mume wangu live lakini hata sikumdhuru mtu. Nilimuacha sababu ya utapeli na akili kisoda. Wala sikuhangaika na mtu mie, nilienda mahakamani nikavunja ndoa. Na maisha yameendelea tena vizuri tu.

Mko wa chache wa aina Yako. Hata hivyo inaonekana Kuna vitu jamaa yetu alikupitisha ukafikia hiyo hatua. Awali sio rahisi sana.

Hongera Kwa maamuzi thabiti na pole Kwa misukosuko
 
kwanza hongera kwa kupata mtoto, lakini fanya hivi
1. Usifanye siri hili jambo kwani ipo siku litajulikana tu.. mpeleke Iryn na mtoto nyumbani kwenu kumtambulisha wamjue damu yako.

2. Mwambie ukweli mama J kuwa una mtoto umezaa na Iryn na usimfiche chochote. mwache yeye aamue kuolewa au aache kuolewa na wewe..usimuoe bila yeye kufahamu hili jambo na aridhie mwenyewe kuwa kuna mke mwingine.

3. Mwambie mama J kuwa utafunga ndoa ya serikali na pale kuna option ya wewe kuwa na wake wawili au zaidi ili umlinde Iryn na watoto utakaozaa naye, watoto wote wana haki kwa baba yao.. Mama J anatakiwa ajue kabisa kuwa anaolewa na wewe lakini kuna mke mwingine ambaye naye utafunga naye ndoa..

4. Usithubutu kumuoa mama J bila ya kumpa taarifa ya mke mwenzake ambaye ni Iryn..yani ajue kuwa anaolewa kama mke wa kwanza na pia kuna mke wa pili. usisahau kuwa huyo mama J ni mchaga na mtusamehe tu wanawake wa kichaga wengi huwa wanabaki wajane jiulize kwa nini.. na hasa akigundua mume wake ana wanawake wengine na watoto huko nje mawazo yao yote huwa ni kwenye mali na kuwamaliza waume zao.. tusije tukaanza kuimba parapanda bado tunakupenda Insider..

5. Mama J akikataa kuolewa na wewe kwa sababu ya kufahamishwa kuhusu Iryn basi pambana na hali yako na umuoe huyo Iryn na ikibidi uchukue mwanao ulee wote pamoja..nakuusia usifanye siri kwa mama J kwani madhara yake ni makubwa huko mbele labda kama huwajui wachaga..
INSIDER, TAFADHALI SANA CHUKUWA HAYA MAANDISHI, PRINT NA UYAWEKE KWENYE LAMINATION ILI UWE UNAKUMBUKA KLA SIKU. HUU NDIO UKWELI AMBAO HAUNA CHENGA YA UNAFKI. KUMBUKA MAMA J ALIONDOKA KWA SABABU YA MSG ZA PRISCA, IMAGINE AKISIKIA UNA MTOTO TENA UMEZAA NA IRYN.
 
Wee, mimi nilimfuma aliyekuwa mume wangu live lakini hata sikumdhuru mtu. Nilimuacha sababu ya utapeli na akili kisoda. Wala sikuhangaika na mtu mie, nilienda mahakamani nikavunja ndoa. Na maisha yameendelea tena vizuri tu.
Doh aisee pole sana en kudos kwa kumoveon.....honestly binafsi ikinikuta hiyo hali sitamdhuru mtu ila lazima ntafanya jambo ili angalau akihisi nilichopitia
 
Eti bro Watu8 katiba ya kibazazi inasemaje? Amchane mama J kabla hawajaanza process za kubariki ndoa au akaushe mpaka watakapofunga ndoa aje agundue tu mwenyewe kwamba jamaa ana familia nyingine na Iryn?? Ila wanaume mna siri daaahh🙌🙌


Ndio maana tunakufa mapema
 
Ni kuambie kitu, hakuna kitu kizuri kama ku move on bila kulipiza kisasi, utapata amani ya moyo
Wanasema your tolerance over something ndo inafanya watu waku treat vipi......anyways siku yakinikumba i'll remember your advice[emoji120]
 
Mimi bora mtu aniambie mapema tu kuliko kunificha. Toka niujue ukweli kwamba ni asilimia moja tu ya wanaume ambao hawachepuki nimeshakubaliana na ukweli kwamba hakuna mwanaume wa peke yako. Ukianza sijui ohh naachana naye labda ubaki single maisha, ila kwa hawa wanaume wa kibongo sidhani kama utampata ambaye sio mchepukaji.
Ewaaaaaa nachosema mimi ni ule ukweli tu na uwazi ili mtu ajue ndoa anyoiingia ina jambo hili hili na lile... mapemaaaaaa
 
Ningekua mimi ndo mama J. Bora usiniambie mpaka mtoto atakavyokua mkubwa maybe miaka 10 huko tukiwa tushakuwa watu wazima zaidi tunafikiria majukumu zaidi.

My dad alimficha mama kwamba ana mtoto. Mama akaja kujua mtoto akiwa 20yrs, akamwambia tu baba amlete mtoto amuone.

Ila sasa hivi mapenzi bado ni moto moto, mimi nashauri usimwambie mama J. Kuhusu kuwaambia wazazi hapo labda wenzangu wakusahauri. Ila mzazi wako anaweza kukwambia mwambie mkeo na tunarudi pale pale.
 
Back
Top Bottom