INSIDER MAN ...achana na mambo ya kumtambulisha Iryn na mtoto Kwa wazazi wakati huu. Mama Yako ni mtu makini sana, anawezakukupa maelekezo yatakayokuweka mahali pagumu sana.
Kumbuka unatarajia kufunga ndoa(kubariki ndoa) muda SI mrefu, hizi habari za mtoto zitatibua na kuibua mambo mengine. Kwa maoni yangu, ungekamilisha Hilo zoezi la ndoa kwanza, huku ukisikilizia mambo yanaendaje.
Mie nilisha ambiwa, siku ikitokea taarifa za ujauzito au mtoto wa nje ndio mwisho wa mahusiano na wife. Akasema Yuko radhi kumtambulisha watoto wengi wajae fuso ila kama walipatikana kabla ya kufahamiana nae ila sio tukiwa wote.
Inabidi uongeze sasa Mdogo wa hao watoto Kwa Mama Jr. Naona Iryn ndio anamoto wa kukyzalia mtoto mwingine asije akasawazisha na kuongoza ligi...
Ni kweli hautaki kuendelea kulipwa mshahara kwenye kazi za Iryn, lakini hauoni kuondoka kwako inaweza kusababisha mambo yakayumba kibiashara mkapoteza wote?
Unaweza kufanya mambo mengine lakini ukaendelea ku oversee hizo biashara.
Kwenye extra episode 06 haujagusia suala la Mama Janeth na mtoto wa Iryn, hajawahi kujua wewe ndio baba wa huyo mtoto?
Kingine unakibarua kizito sana, tena sana Cha kukaa mbali na akina Mary, Mdogo wake Jane, mtoto wa Mzee Juma na walimbwende wengine, siku ukijichanganya, ikathibitika pasi shaka umechepuka, Kwa akili za Iryn zilivyo, hasira zake anaweza kumshirikisha Mama Jr kuhusu hizo tabia hata kama na yeye atakua matatani lakini hatakua na Cha kupoteza. Usiwaumize mioyo hao wake zako, Iryn akijua unachepuka ni Bora ukajifiche Gaza.
Mwisho wa siku maamuzi unayo wewe kiongozi.