SEASON 02
CHAPTER 09
“BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Niliona sometimes kama mwanaume inatakiwa kuwa na maamuzi magumu, nibora mama ajue mapema kinachoendelea before it’s too late na maamuzi yafanyike mapema. Kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na kucheki ni Iryn alikuwa anapiga na nikajisemea leo namchana ukweli siendi Ethiopia.
CONTINUE:
Niliamua kuipotezea simu yake kwanza na nilichukua maamuzi ya kuondoka maeneo haya. Wakati nimeingia kwenye gari nilikuwa nikitafakari namna ya kuongea naye ili aweze kunielewa. Unajua niliwaza Iryn ni kama mke tayari, pia yale maongezi yake na Claire alionesha kuwa side yangu, hivyo mpaka akaomba twende Ethiopia ni kweli anahitaji kampani yangu, sasa mimi nafanyaje?.
Kumpa jibu kuwa siendi niliona sio jibu zuri, hivyo inabidi nitafute namna ya kuongea naye na anielewe ili amani iendelee kuwepo. Baada ya kufikiri sana niliona nimpe conditions zangu na kama atakubaliana nazo bhasi nitaenda huko Ethiopia na kama atagoma bhasi kwangu itakuwa sherehe.
Muda ulikuwa umekwenda sana maana nilikuwa niko kwa zaidi ya masaa 3 pale Coco beach. Niliondoka mitaa ile kwenda ofisini kuangalia maendeleo na sikukaa sana nikaondoka kwenda kuonana na Sumaiya maana alikuwa anahitaji sana kuonana na mimi.
Baada ya kufika pale ofisini kwake tulipanda juu kabisa ghorofani ili tufanye mazungumzo yetu na taarifa kubwa alizonipa ni kuhusu kununua gari na alisema ataanza na hiyo Toyota Ist. Nilimpeleka Morocco ili tukaangalie gari zilizopo na kama kuna gari ataipenda, bhasi aweke booking mapema maana alisema kufikia ijumaa atakuwa amekamilisha.
Tulikwenda palepale kwa jamaa niliye fahamiana naye kupitia mzee Pama na baada ya kuwasili pale alituonesha Ist tano (5) na zote zilikuwa ni kali, lakini Sumaiya aliipenda moja yenye rangi ya dark blue. MBaada ya mazungumzo ya muda mrefu Jamaa alitupunguzia mpaka kufikia 14.5M, ukweli ilikuwa ni Ist ya moto sana.
Bila kuchelewa Sumaiya alifanya malipo ya 12M kwa kutransfer na balance inayobaki alisema atamalizia Ijumaa, then akabidhiwe na gari yake. Niliagana na Sumaiya pale na nikarudi home kupumzika, wakati niko njiani nilikuwa nafikiri namna ya kudeal na suala la Iryn.
Ndani ya muda mfupi nilikuwa niko home na Elena aliniambia mama amelala, hivyo nili kwenda kukaa nje kibarazani maana kichwa changu kilikuwa na vitu vingi sana. Ulishawaza mpaka kichwa kinauma na bado hupati majibu? Bhasi ndo hali niliyokuwa nayo mimi Insider maana nilikuwa dilemma na sijui nifanye maamuzi gani.
Baada ya nusu saa mama alitoka pale nje kibarazani na baada ya kusalimiana tulianza maongezi,
MAMA: “Mwanangu upo sawa kweli? Nimekuona muda mrefu upo kwenye mawazo shida ni nini?”
MIMI: “Mama hata usijali niko sawa ni mambo ya kazini yananiumiza kichwa.”
MAMA: “Kweli mwanangu? Nakujua vizuri sana na kama unanidanganya mimi mama yako naelewa.”
Niliwaza pale sijui nimwambie tu ukweli wa kinachoendelea? Lakini nikaona hapana nitakuwa nimefanya maamuzi ya haraka sana,
MIMI: “Kuna shot imetokea huko ofisin ndo inanipa mawazo hapa kuwa imeenda wapi?maana hesabu zote ziko sawa ila balance ndo inagoma.”
MAMA: “Pole sana inabidi utulize akili hapo na ikitokea hujui inakuaje?”
MIMI: “Nakatwa mshahara maana mimi ndo top natakiwa kufuatilia kila mauzo ya siku, nilifanya kauzembe.”
MAMA: “Na pale Salon ndo ofisi yako iliko?”
MIMI: “Ile ni branch yetu ila ofisi kuu ipo Masaki, ni karibu na tulikokwenda jana usiku ndo ipo kule.”
Muda huu Junior alisikika akilia na mama alikwenda kuangalia shida ni nini? na aliniacha pale kibarazani.
Baada ya dakika 20 hivi, Iryn alipiga simu tena na mimi nilipokea kwa haraka sana na tukaanza mazungumzo,
MIMI: “Hey mummy za wewe?”
IRYN: “Safi darling, pole na kazi.”
Kwanza nilishangaa kuona Iryn kawa mpole maana angeanza na kulalamika why sijapokea simu zake?,
MIMI: “Mimi niko poa just tired, what’s new?”
IRYN: “Ijumaa tunatakiwa kwenda Ethiopia na sikuelewi elewi baby.”
MIMI: “Mummy naomba nikupe conditions zangu za kwenda huko Ethiopia.”
IRYN: “Go ahead, nakusikiliza.”
MIMI: “Moja sitalala kwenu naomba nitafutie hotel, naomba usije kuja kulala hotelini mpaka tunaondoka na utalala home. Pili, naomba usifanye utambulisho wowote kwenu wala kuonesha signs zozote za mimi na wewe tuko kwenye mahusiano. Mwisho, sitakaa wiki na wewe nafikiri siku 3 zinatosha mama yuko home na biashara inategemea usimamizi wangu.”
IRYN: “Done.”
MIMI: “What?”
IRYN: “I said done, Ijumaa nitakuja Dar then tutaondoka wote kwenda huko.”
MIMI: “Sawa mummy no problem.”
Baada ya kuachana na Iryn nilishangaa sana kuona akikubali matakwa yangu bila kusumbuana na muda huu nilianza kuwaza gia ya kutokea pale home.
***
Asubuhi nilipigiwa simu na namba ngeni na alijitambulisha vizuri, akanambia niende Ubalozi wa Ethiopia nikiwa na passport yangu. Sikutaka kuuliza maswali kabisa maana nilijua yatakuwa ni maagizo kutoka kwa Iryn na mimi nilijiandaa nikaondoka kuelekea Masaki.
Nilimpigia simu Iryn na kumpa taarifa juu ya kupigiwa simu na yeye alisema huyo mtu amempa maagizo hivyo nimpe ushirikiano maana muda umekwenda tayari. Break yangu ya kwanza ilikuwa ni pale ubalozini na baada ya kuonana na huyo mtu kuna documents nilizijaza chap. Nilijaza nakwenda Ethiopia kwaajili ya utalii na baada ya kumaliza kuzijaza, akanambia atanipigia simu na mimi ndo kuondoka.
Niliondoka kuelekea ofisini na nilimkuta Asmah amelala kwenye coach, ile kalalia tumbo makalio yako juu na mimi nilimuwasha na kibao cha kalio “PAAH” na alianza kulalamika pale,
“Insider mbona unatabia mbaya hivi?”
“Wewe unalalaje hivyo ofisini? Au unataka kunipa stim!?”
“Ulitaka nilalaje sasa?”
“Ningekuja kukuonesha sema umelala kimitego sana.”
“Insider una matatizo ya akili wewe.”
Tuliendelea kufanya kazi huku tunapiga story za hapa napale na utani mwingi. Mida ya mchana Hilda alikuja kutushtua tukapate lunch.
Hii siku nilishinda ofisini maana nilikuwa ninaandaa maripoti ya hesabu za mwaka afu nilikuwa napunguza makazi hata nikiondoka mambo yaende. Sikuona sababu ya kumficha Asmah na nilimpa taarifa kuwa nitasafiri mara moja kwenda Ethiopia na nitamuachia ofisi iwe chini ya usimamizi wake.
Mida ya jioni Allen alinipigia simu na akanambia tuoanane Samakisamaki ili tucheki na game kabisa. Hii siku kulikuwa na match ya nusu fainali kati ya Argentina na Croatia na mimi sikuona sababu ya kwenda home mapema hivyo tulikubalina tutaonana pale. Wakati naongea na Allen kwa upande mwingine Asmah alikuwa makini sana kusikiliza maongezi yetu na yeye alisema tutaenda wote kuangalia mpira.
Mida ya saa 2 usiku tulitoka kuelekea maeneo kwa upande mwingine Allen alikuwa amefika muda mrefu na alikuwa kashanipa taarifa amefika tayari. Baada ya kuwasili tulijumuika naye na yeye hakutegemea kama ningeenda na Asmah na nilifanya utambulisho na story zingine zikaendelea.
Game iliisha kwa Argentina kushinda 3 bila na nilikuwa na furaha sana hii siku kwakweli maana tulifuzu kwenda fainali. Baada ya game nilimpa Asmah kampani ya usafiri mpaka kwake Upanga na baada ya kuwasili kwake nilipark gari pembeni. Muda huu tulikuwa tukiendelea na mazungumzo yetu na kubwa nilitaka kujua yeye na Iryn walikuwa na mazungumzo gani?
MIMI: “Asmah embu niambie Iryn amekwambia nini alivyorudi Dar?”
ASMAH: “Hakuna chochote alichoongea zaidi ya story za kawaida.”
MIMI: “Mbona ulikuwa unaonekana kumwogopa sana? Au unanificha?”
Asmah alikosa majibu ya hili swali langu alinyamaza kimya, nilivyoona yuko kimya nilipitisha mkono wangu wa kushoto nyuma yake na nikanza kukipapasa kiuno chake,
ASMAH: “Insider stop! please!”
MIMI: “Kipindi kile unaumwa mguu ulikuwa unanifunulia mwenyewe sahivi unanipa masharti sindio?”
ASMAH: “No! sijamaanisha hivyo but sija-do muda mrefu sana utanipa majaribu bure na sitaki chochote kitokee baina yetu.”
MIMI: “Kwahiyo kukushika kiuno nakupa majaribu? Bhasi una matatizo jitathmini.”
Na muda huu nilifungua kifungo cha skin jeans yake kwa haraka sana taah! Na ile nataka kutalii kwenye bustani alinishika mkono, na akaendelea kulalama,
ASMAH: “Insider stop this please, wewe umesha lewa na hizi sio akili zako.”
MIMI: “Asmah niachie mkono wangu ndo utafanya nikukamie kweli.”
Asmah ilikuwa mpole maana nguvu ya kunikazia alikuwa anaitolea wapi kwanza? Na aliniachia nifanye nachotaka. Ile kuingiza mkono daah! Bustani yake ilikuwa imeshamwagiliwa vizuri.
MIMI: “Kidogo tu uko hoi stage uliyofikia ni mbaya sana.”
ASMAH: “I told you before hukutaka kunielewa.”
MIMI: “Mara ya mwisho ku-do ni lini?”
ASMAH: “Nikikwambia hutanielewa tatizo, utasema nakudanganya.”
MIMI: “Nitakuamini maana ukweli nimeushuhudia kwa macho yangu.”
ASMAH: “Sijakutana na mtu mwingine zaidi yako kipindi kile.”
MIMI: “Nenda kalale kesho saa 4 asubuhi tutakwenda Posta wote.”
Asmah aliniangalia na akaondoka na mimi sikutaka kupoteza muda nikaondoka kurudi home maana wife alikuwa kashaanza kupiga simu kwa fujo. Kipindi niko njiani nilikuwa nawaza kuhusu Asmah na niliona kuna haja ya kumuhudumia maana stage aliyofika ni mbaya sana. Hata mimi kwa upande wangu nilikuwa naingiwa na tamaa ya kutamani kumla kwa mara ya pili.
Baada ya kurudi home ile kuingia ndani nakutana na mama yuko seblen pamoja na wife na aliishia kunipiga jicho kali sana, mimi sikujali na niliwasalimia nikapitiliza kwenda chumbani kuoga.
Mawazo yangu makubwa yalikuwa ni namna ya kutoka pale home na kwenda huko Ethiopia na niliwaza nitumie mbinu gani? Ambayo itamake sense na isilete maswali. Niliwaza nikiwaambia nakwenda Zanzibar kufuata mzigo mwisho wa siku nitapigiwa simu afu sipatikani italeta shida, ni bora nidanganye nakwenda Kenya hata nisipopatikana ni freshy.
“Sasa niwaage ijumaa nakwenda Kenya kuna mzigo umefikia kule hivyo inabidi nikaufuate pamoja na kufanya clearing mapema, hii sababu ita make sense.”
Asubuhi nilitoka mapema kwenda ofisini maana nilikuwa na ratiba ya kwenda Posta na Asmah. Niliendelea kuandaa documents ambazo Iryn alikuwa kanitumia za mzigo na nikaendelea kumsubiri Asmah. Haikuchukua muda Asmah naye aliwasili pale ofisini na alionekana kuwa na aibu kidogo, nilijua ni ile ishu ya jana usiku.
Tulisalimiana then tukaondoka kuelekea Posta na ile baada ya kuingia kwa gari nilianza kumzingua tena,
“Naona unanionea aibu mummy.”
“Insider ulichofanya jana sio heshima, umenikwaza.”
“Sawa mummy sitakukwaza tena usijali.”
Nilikuwa nakwenda na Asmah Posta ili aendelee kupata uzoefu taratibu hata kama sipo awe anajua pakuanzia na kutokea, si mnajua mambo ya custom yalivyo na complications?, na ukisema umuachie kila kitu agent utakuwa unapigwa.
Kipindi niko njiani nilifanya kuwasiliana na dada wa clearing ili tuonane na tufanye malipo yote kwa pamoja. Kwa kila stage tunayoanza na kupita nilikuwa namuelekeza Asmah na yeye alionesha kuwa makini na kuelewa.
Kwenye mida ya saa 7 mchana tulikuwa tumekamilisha kila kitu na tulikwenda kupumzika moja ya mgahawa pale Posta tukipata lunch. Baada ya lunch tuliondoka na nilipitia ofisini kwa mama wa2 maana alikuwa ameniomba kama nitapita Alli Hassan road nipitie tuonane.
Baada ya kuwasili pale ofisini kwake tulikwenda moja kwa moja mpaka reception kumsubiri na nilikuwa nimempa taarifa tayari. Baada ya dakika 10 mama wa2 alitoka kuja pale reception tukaendelea na maongezi.
MIMI: “Mama mkwe leo umewaka sana.”
MAMA WA2: “Ooh jamani! Nimefurahi kukuona japo unakesi za kujibu.”
MIMI: “Kesi gani hizo mama mkwe.”
MAMA WA2: “Wake zako kule home wanakuulizia sana, ulisema utakuja mchukua Rachel mpaka leo kimya.”
MIMI: “Hao nitakuja kuwasilimia haina shida, afu sijakwambia mama yangu yuko home.”
MAMA WA2: “Mbona hujanambia nije kumwona mama mke mwenza, jumapili nitakuja na kina Rachel.”
MIMI: “Bad news ijumaa na safari nakwenda Kenya one time ila sitokaa, nikirudi tu nitakupa taarifa uje.”
MAMA WA2: “Insider kwa mishemishe sikuwezi na huyu dada ni nani? Hujanitambulisha bado.”
MIMI: “Huyu anaitwa Asmah ni HR wa kampuni.”
Na mama wa2 alifanya kusolimiana na Asmah maana walikuwa bado hawajasalimiana na aliomba tukae pembeni ili tuongee. Kuna mchongo mama wa2 alikuwa ananipa ambao na mimi ningepata commission na baada ya maongezi ya muda mrefu tulifikia makubaliano na niliukubali mchongo. Tuliagana pale na mama wa2 na tukaondoka na Asmah maeneo yale kurudi ofisini, lakini wakati tuko njiani Asmah alikuwa ananipiga sana maswali,
ASMAH: “Insider huyu mama ni nani?”
MIMI: “Unataka kusema ni lishangazi langu sindio?, huyu ni mtu wangu wa karibu kama wewe.”
Asmah alicheka na akaendelea kuongea,
ASMAH: “Hapana sijamaanisha hivyo, last time nilikuuliza umefahamianaje na Iryn lakini hukunipaga majibu ya kueleweka.”
MIMI: “Nilikujibu sema umesahau.”
ASMAH: “Ulinijibu kimkato sana, kama uliweza kufahamiana na Iryn na akakuzoea na bado amekuwa mpenzi wako, una nyota.”
MIMI: “Mbona wewe hujisifii sasa? Kwahiyo mimi kufahamiana na wewe sio nyota?”
ASMAH: “Insider mimi kwa Iryn sio kitu, kujifananisha na yeye namkosea heshima.”
MIMI: “Asmah tatizo lako ni moja tu hujikubali, lakini wewe ni moja ya wanawake warembo hapa duniani.”
ASMAH: “Napata wapi ujasiri wa kujilinganisha na Iryn? kwanza kanizidi kipato, kanizidi uzuri bado kaniajiri.”
Ilibidi nicheke maana Asmah alikuwa kaongea ukweli mtupu na muda huu tulikuwa tumeshawasili ofisini na maongezi yaliishia hapo.
Niliendelea kukaa pale ofisini na nilipata wazo la kwenda kwa Jane kumpa taarifa kwamba sitokuwepo kwenye arobaini ya mtoto. Niliwaza ni busara nikaenda Mbweni kuonana na Jane ana kwa ana kuliko kupiga simu na kutoa taarifa.
Saa 12 jioni nilikuwa nimewasili pale kwa Jane na Vicky ndo aliyenifungulia gate na baada ya kupark gari niliendelea kupiga story na Vicky pale nje then nikaingia ndani. Kwa upande mwingine pale seblen palikuwa na mama Jane na pindi anaponiona huwa anafurahi sana na nilimsalimia tukawa tunaongea.
Jane alitoka ndani na kama kawaida yake alinipa ishara na tulikwenda kukaa garden kwaajili ya mazungumzo,
MIMI: “Shem maandalizi yanakwendaje ya 40 ya mtoto?”
JANE: “Unafikiri kuna maandalizi bhasi? Bado hata tulichoanza.”
MIMI: “Mary bado anakuja hapa home?”
JANE: “Toka uje weekend hajaja tena ila aliniambia atakuja ijumaa hii.”
MIMI: “Shem mimi nimekuja kukupa taarifa sitokuwepo hio jumamosi maana nimepata emergence na ninaondoka ijumaa hii kwenda Kenya.”
JANE: “Jamani! Mbona hivyo shem? Kuna shida gani imetokea ifanye usiwepo?”
MIMI: “Ni masuala ya kiofisi tu ndomana na sina mtu wa kusema aende zaidi yangu, natamani sana ningekuwepo ila naamini hakuna kitacho haribika.”
JANE: “Insider ulipaswa uwepo shem, kuna zawadi nilikuwa nimekuandalia nikukabidhi hio siku kama mchango wako kwangu kwa kipindi chote, sasa nitafanyaje?”
MIMI: “Naelewa shem na naomba samahani kwa hili maana ni suala ambalo limekuja haraka na sina jinsi. Kuhusu zawadi unaweza mpa hata Mary ili nirahisishe mazingira ya kuonana naye na tuyamalize.”
JANE: “Uwasiliane naye na umpe taarifa.”
Niliagana na Jane kuondoka kurudi home na kipindi niko njiani nilijisikia vibaya sana kuondoka na kuikosa arobaini ya mtoto, ukizingatia uwepo wangu ungekuwa ni muhimu sana. Kwa upande mwingine Jane alionekana kutozipokea vizuri taarifa zangu ni kama nilikuwa nimemkatili na hakutegemea.
Nilitoa simu nikampigia Mary lakini ilikuwa inatumika na nilipiga kama mara 3 bado namba inatumika. Baada ya dakika 10 nilipiga tena lakini bado niliambiwa inatumika na nikapark gari pembeni ili nimtumie ujumbe kwenye whatsapp. Baada ya kufungua whatsapp nilibaini ameniblock na hapa ndo nilishangaa sana nikajisemea kweli Mary yuko serious hataki mazoea na mimi this time.
*****
Ijumaa ilikuwa ndo safari ya kwenda Ethiopia na maamuzi niliyoyachukua niliona ni ya busara ukizingatia Iryn ni kama mke wangu. Niliona sometimes ni bora ujifanye mjinga ili mambo yaende maana Iryn amenipa heshima kubwa sana. Zawadi kubwa ya kumpa sina hata kumpeleka Ethiopia iwe mtihani? Niliona mambo kama haya ndo yatafanya mapenzi yake kwangu yaendelee kuongezeka.
Kuhusu home niliwapanga kuwa nimepata emergence ya kwenda Kenya kuna mzigo nakwenda kuufata na umefikia bandari ya Mombasa. Home hawakuwa na shida kabisa maana waliona ni suala la kazi, hivyo sinabudi kwenda huko. Yule mtu wa Iryn pale ubalozini alikuwa kanicheki jumatano na alinipa visa yangu kwaajili ya safari.
Nilinunua zawadi ya ua kwaajili ya kumpa Iryn na nilikwenda JNIA maana yeye alikuwa anatarajia kuingia saa 9 za mchana. Saa 10 jioni aliwasili na baada ya kuonana alikuja akanikumbatia na alikuwa amependeza sana. Kwa upande wetu sisi tulikuwa tunatarajia kuondoka na ndege ya saa 12 jioni na tulikaa pale Bao cafe tukipiga story.
Kwa upande wake alionekana kuwa sawa tu maana wasiwasi wangu ulikuwa kwenye tumbo lake, na lilikuwa la kawaida tu. Nilitoa zawadi ya ua nikamkabidhi pale na alifurahi sana, na yeye alitoa zawadi ya simu akanipa ilikuwa ni iphone 14 pro.
IRYN: “Darling leo tutalala wote hotelini then kesho tutakwenda home.”
MIMI: “Mhh! si watakushtukia umelala hotelini?”
IRYN: “Hapana nimewambia naingia kesho so it won’t be a problem.”
MIMI: “Na tunakwenda lini kwenye kaburi la mama?”
IRYN: “Jumapili ndo kumbukizi ya mazishi yake.”
MIMI: “Na vipi kuhusu mimba unaonaje haiwezi kuleta shida? Na wasiwasi watajua hali yako.”
IRYN: “Mara nyingi usiku ndo inanisumbua ila haitakuwa tatizo niko makini I promise. Mama mkwe wangu hajambo? Na wish sana nimuone hata kwa mbali tu.”
MIMI: “Usijali utamwona kuwa na subira baby.”
IRYN: “Lini hiyo? Maana chance ndo sasa au utanipeleka mkoani?”
MIMI: “Wewe usijali nipe muda niendelee kuandaa mazingira sawa mummy?”
IRYN: “Sawa darling no problem.”
Tulicheck-in na safari ya kwenda Ethiopia ikaanza, kimbembe tuko kwenye ndege mahaba yalikuwa motomoto hata hatukujali kama watu. Nilianza kumuuliza maswali Iryn kuhusu mila zao maana nilitamani sana kuzijua ili nisizingue huko Ethiopia.
IRYN: “Mama yangu ana mixer ya Mursi na Oromo tribe maana babu ni Mmursi na bibi ni Oromo. Babu alikufa mama akiwa mdogo sana na kupelekea kulelewa na bibi miaka yote na hii ikapelekea sisi kubase kwenye Oromo tribe. Bibi yangu yupo home utamwona na kama unavyoniona mimi tumefafana kila kitu wewe utaona nitakutambulisha.”
MIMI: “Sawa haina shida nifundishe na namna ya kusalimia watu ili nisizingue huko.”
IRYN: “Nitakufundisha baadhi ya maneno muhimu ya kuongea just in case”
Na alianza kunifundisha pale taratibu na mimi nilikuwa makini sana kumsikiliza maana sikutaka kuzingua huko,
How are you?- Isin attam?
I’m fine-Nagaa
What is your name?- maqaan ke eenyu?
And you?- ati ho?
Where are you from?- Biyyi ke eessa?
I’m from Tanzania-Biyyo ko Tanzania.
How old are you? -umuriin ke waggaa meeqa?
I'm good -Fayyaadha
Do you speak english?- Afaan Ingiliizi beekta?
Thank you- Galatoomi
“Baby nafikiri haya ndo muhimu endelea kuyapitia uyajue yatakusaidia kwa kiasi chake. Baby ondoa wasiwasi ukoo wetu ni wakarimu sana hata watu wote kwa ujumla ni wakarimu hawana shida kabisa. Utauona ukoo wetu wote kesho na naomba uwe na amani hata usiwe na wasiwasi I know you’re confident.”
MIMI: “Naona unanipa matumaini lakini kwa mwanaume kuja ukweni kwa mara ya kwanza tena bila washenga ni kipengele. Nimekuja sababu ya mama na sio wewe, naomba usioneshe sign zozote zitakazo onesha tuko kwa mahusiano.”
Saa 4 za usiku tuliwasili Addis Ababa lakini hatukushuka maana safari yetu ilikuwa kwenda Bahir Dar. Huu ni mji ambao upo kaskazini mwa Addis Ababa na ndo Lake Tana liliko, na umbali wa kutoka Addis mpaka Bahir ni kama 600km hivi haina utofauti sana wa Dar na Dodoma.
Tulikaa kama nusu saa pale Addis na tukaondoka kuelekea Bahir na tulitumia nusu saa tukawa tumewasili. Muda ambao tuna land mji ulionekana kuwa mzuri sana kwakweli na baada ya kushuka kwa ndege tuliondoka kwenda hotelini.
Muda huu mimi nilikuwa kimya hata yeye alikuwa kimya mpaka tunawasili hotel ya Blue nile na ipo karibu na lake Tana. Wakati tumefika hotelini huku njiani nilikuwa napishana na warembo visu balaa, nilijikuta naanza kushangaa aisee ni hatari.
Nilisikia Iryn akisema,
IRYN: “Baby, keep walking. Wha the f*ck are you looking at?”
Nilinyamaza kimya maana nilikuwa nimezingua na nimesahau uwepo wa Iryn na aliendelea kuongea,
“You said mimi ni mwanamke mrembo hapa duniani umeona warembo sasa? Nafikiri mpaka tunaondoka huku utakuwa umeona hali halisi kuwa mimi ni wa kawaida tu.”
Kauli aliyosema Iryn ilikuwa ina ka ukweli ndani yake maana pisi niliyokuwa nimepishana nayo ilikuwa ni hatari tupu.
MIMI: “Mummy wewe ni mwanamke mrembo bado sijaona wa kukuzidi.”
Na nilisikia akini fyonza,
IRYN: “Fyoooooh! umepagawa na dada wa watu mpaka ukageuka, hii ni hotel ya kitalii na most ya watalii wanafikia hapa, utakutana na warembo wengi sana. Sijui kwanini nilikuleta hii hotel utaweza kuvumilia kweli?”
MIMI: “Sasa baby kwanini umenileta hapa kama unajua haya yatatokea? Anyway mimi najitambua siwezi fanya ujinga unaouwaza.”
IRYN: “Insider wewe ni mtu mzima tayari fanya lolote ambalo unaona litakupa furaha, huenda naongea na mtu ambaye bado hajataka kujua majukumu yake.”
MIMI: “Baby kwanini unasema maneno hayo? Ni nini maana ya kuja huku?”
Muda huu tulikuwa tuko room yetu tayari na nilikuwa nafikiri kwanini Iryn anaongea maneno kama haya? Na toka aje Dar niliona mabadiliko yake, nikahisi kuna jambo haliko sawa. Nikawaza acha leo nimuoneshe ukichaa wangu maana haujui, mazoea yanazidi sasa ngoja nimuoneshe. Yeye alikuwa amekaa kitandani, haraka nilimkamata nikambana kitandani ile tunaangaliana na alikuwa hawezi kufurukuta, maana nilimbana kisawasawa,
“Leo utanambia siri zote zinazoendelea kati yako na Claire, lasivyo nitakuharibu hapa na uzuri niko kwenu tuone utanifanya nini.?”
Nilikuwa nimembadilikia na alianza kuogopa,
IRYN: “Insider, stop this. You’re disrespecting me.”
MIMI: “Ndo uongee sasa nadhani hunijui vizuri, unaniletea dharau zako za kiseng*seng* leo nakuonesha mimi ni kichaa, afu tuone kama utanipeleka police.”
IRYN: “What's wrong with you? You forgot I'm pregnant?”
Na aliendelea kufurukuta ili ajinasue lakini wapi nilikuwa nimemdhibiti vizuri,
MIMI: “Naelewa ila naomba uniheshimu na sio kunipangia nini cha kufanya hili sio ombi ni lazima, shenzi zako. Na umwambie Claire aache usnitch wake kabla sijamfanya mbaya I know what is really going on na mimi sio mtoto, kwanza nimekuzidi miaka pumbavu.”
Na nikamwachia pale,
IRYN: “Don’t dare ever touch me like that again.”
Na mimi nilianza kucheka kwa dharau pale na yeye aliishia kununa akalala bila kuoga na kula akasahau.
Asubuhi baada ya kuamka alikuwa kanuna sana, nilimpa salamu lakini hakuijibu na baada ya kujiandaa tulikwenda kupata breakfast. Wakati tunapata breakfast yeye alikuwa busy na simu yake na mimi nilikuwa busy na simu yangu. Mida ya saa 5 asubuhi tuliondoka pale hotelini kwenda kwao na tulitumia muda mchache sana kuwasili kwa makadirio ya haraka kutoka pale hotelini mpaka kwao ni kama 10km.
Baada ya kushuka kwa Tax mbele yangu ilikuwa inaonekana nyumba kubwa nyeupe nzuri na Iryn alisema hapa ndo home na haikuchukua muda tulifunguliwa gate tukaingia ndani. Kwa upande mwingine niliona mama mtu mzima akija na dada watatu kwa spidi sana usawa wetu na wakamkumbatia Iryn. Yule mama mtu mzima nilimgundua ni mama yake mkubwa maana nilikuwa namuona kwa picha tu.
Baada ya kuingia ndani Iryn alifanya utambulisho pale na alianza kunitambulisha mama yake mkubwa na alisema wale ni wadogo zake kasoro mmoja ndo alikuwa ni dada yake. Kwa upande wangu Iryn alinitambulisha kwa ndugu zake mimi ndo manager wake ambaye nasimamia kampuni zote alizoacha mama yake. Wenyeji walionesha kunifurahia na haikuchukua muda bibi yake alitoka ndani na alifurahi sana kumuona Iryn, na kweli walikuwa wamefanana sana.
Asilimia kubwa ya maongezi yaliyokuwa yanatumika hapa ni lugha yao, mimi nilikuwa kimya maana sikuwa naelewa chochote. Seblen nilikuwa mpole sana maana nilikuwa kama nimetengwa hivi na Iryn alionekana kuwa busy sana na ndugu zake.
Baada ya nusu saa Jimmy aliingia na alifurahi sana kuniona na hapa kidogo nikawa na amani maana alikaa pembeni yangu tukawa tunapiga story. Baadae tulitoka nje kukaa na tukaendelea na story zetu na kubwa nilishangaa akiniambia anajua kila kitu kinachoendelea kati yangu na Iryn na alinitoa wasiwasi. (Kuhusu Jimmy ref Season1 Epsode 56)
Mida ya saa 1 jioni mimi niliamua kuondoka na nilimwomba Jimmy anipe kampani, lakini kabla ya kuondoka nilimwomba aniitie Iryn ili niweze kumuaga mke wangu. Baada ya dakika 10 alitoka na tulizungumza kidogo sana maana alikuwa bado kaninunia na nikajisema kumbe alichukulia serious, wakati mimi nilifanya kwa utani tu na sisi tukaondoka.
Hotelini nilikuwa peke yangu maana sikuwa na kampani yoyote, hivyo nikapata wazo la kwenda kupoteza muda kwenye bar ya pale hotelin. Wakati natoka Tanzania nilitembea na $2,000 kama amergence na nilitoa noti 3 za dollar 100 nikaweka mfukoni, huyo nikasogea eneo la tukio.
Ethiopia wana sarafu yao wanaita birr sasa baada ya kufika pale bar nilimuuliza mhudumu kama naweza kulipa kwa dollar? Akanambia naweza kulipia, Japo nikosa kisheria maana nilitakiwa kufanya exchange. Nilimwambia nitampa dolla 10 ya usumbufu yeye atanisaidia kufanya exchange kwa muda wake, kwanza mhudumu mwenyewe ni pini balaa.
Niliagiza wine yangu na nikaanza kuinywa taratibu kwa upande mwingine nilikuwa nazi-zoom pisi za kihabeshi oyaa ni hatari sio poa mpaka nikaanza kudata. Nikakumbuka ule msemo unaosema “tembea uone” pisi ambazo zilikuwa zinaranda randa ni balaa. Kama pisi ikaja bongo ukafanikiwa kuimiliki unaweza kuhonga mpaka bandari na ukaipa Kigamboni kama kifungashio.
Nilimuuliza mhudumu kama nataka pisi ya kulala nayo iliyonyooka niandae kiasi gani? alinambia inategemea na quality ila kwa pisi kali wastani ni $100 tu. Aliuliza kama nahitaji nimtajie room namba yangu then mrembo atakuja naye mtaka kutokana na offa yangu. Sikutaka kuingia tamaa za kijinga na nilirudi room kulala maana niliona kuendelea kubaki pale ningeshawishika tu!, warembo niliokuwa nawaona ni balaa.
Baada ya kurudi room nilianza kuchati na Asmah maana alikuwa kanicheki na kuuliza kama nimefika salama. Tulichati sana huu usiku ni kama alihisi sina kampani na kwa mara ya kwanza Asmah alinifungukia kuwa ananipenda toka muda mrefu na alikuwa anategema labda kuna siku nitakuja mfungukia.
Asmah aliendelea kufunguka kuwa kwasasa hataki matatizo na Iryn maana amemuwahi na anabariki mahusiano yetu. Kwa upande mwingine aliendelea kukazia kuwa hajapenda Kitendo nilichomfanyia ile siku usiku na nisirudie tena.
***
Asubuhi Jimmy alikuja kunichukua pale hotelini hatukwenda home bali tulikwenda moja kwa moja makaburini. Tulitumia kama dakika 40 kuwasili makaburini na hapo tulikuwa spidi balaa ni sawa na mwendo wa kutoka Mwenge hadi Bagamoyo.
Tuliwakuta baadhi ya watu wamewasili pale na baada ya dakika 20 hivi akina Iryn waliingia na jumla ya watu ilikuwa kama 50 hivi. Ilifanyika ibada pale makaburini na baadae watu walianza kuweka mashada na maua kama kumbukizi na nilimuona Iryn akilia kwenye kaburi la mama yake.
Daah! Nilijisikia vibaya na niliumia sana kuona Iryn akilia vile, katika siku zote ambazo nimeishi na Iryn sikuwahi kumuona akilia namna ile. Nilitamani sana kwenda kumpoza lakini niliona mazingira sio rafiki na niliishia kuumia ndani kwa ndani. Niliwaza pale kama Iryn analia vile kwaajili ya mama yake bhasi kuna haja kubwa sana ya kuwapenda wazazi wetu wakiwa hai.
Saa 8 za mchana tulirudi home kwaajili ya kuendelea na ratiba zingine na baada ya kuwasili pale home tulipata chakula cha pamoja. Jimmy alitoka ndani na alikuja kunipa kampani pale nje maana tulikuwa garden tumetengenezewa hema na viti kwaajili ya wageni.
Nilitumia nafasi hii kumuuliza maendeleo ya Iryn na akanambia yuko sawa kwa sasa na ametulia. Japo nilitamani sana ningepata hata nafasi ya kuongea naye lakini niliona itakuwa ngumu kutokana na yale mazingira. Jimmy alikuwa ananipa historia ya Iryn na mama yake na alinambia kwamba walipendana sana enzi za uhai wake na kumuona Iryn akilia vile ni kawaida. Jimmy aliendelea kuongea na alinambia nimefanya kazi kubwa sana kumuweka Iryn sawa maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana tangu afiwe na mama yake.
Kwa upande mwingine pale home palionekana kuwa na wageni wengi sana na asilimia kubwa walikuwa wakinishangaa maana waliona mimi ni kama mzamiaji. Mida ya saa 11 jioni tuliondoka na Jimmy pale home na kwenda moja ya bar/lounge kwaajili ya kuangalia fainal ya kombe la Dunia.
Mimi na Jimmy wote tulikuwa mashabiki wa Argentina na baada ya kuwasili pale lounge, tulitafuta angle nzuri tukakaa na game ilianza saa 12 jioni kamili kama bongo tu. Katika fainali ambayo nilikuwa naangalia kwa presha ni pamoja na hii maana zilirudi goli 2 dakika za mwisho. Bado tukaenda extra time tukapata goli la tatu, bado likarudi tena aisee ilikuwa ni bonge la fainali.
Muda wa penalty mimi nilisema siangalii maana nilijua tumeshakosa ubingwa tayari lakini Mungu alisaidia tukashinda kombe. Nilikuwa na furaha sana hii siku kwakweli na Jimmy aliagiza moet tukaendelea kuinywa maana ilikuwa ni shangwe na furaha kwa mashabiki wa Argentina.
Baadae kuna pisi yake kali sana ilikuja kutupa kampani pale na Jimmy alinitambulisha kuwa yule ni mpenzi wake. Nje na kelele za furaha, lakini eneo hili lilionekana kuwa na warembo sana, pia wazungu walikuwa wengi ni kama unavyoona vile Samaki samaki.
Kwenye mida ya saa 5 za usiku Jimmy alinipa taarifa kuwa Iryn ananiulizia maana amekuja hotelini hajanikuta na amemwambia tuliko. Ndani ya dakika 15 Iryn aliwasili pale na alimpiga Jimmy jicho kali sana bila hata kumsemesha na akaniomba tutoke nje ili tuongee,
MIMI: “Mummy unaendeleaje kwasasa?”
IRYN: “Niko poa, nimekuja hotelini sijakukuta kumbe umetoka na Jimmy.”
MIMI: “Yeah! Shem wangu kanitoa maana niko peke yangu tu hana kampani sina.”
IRYN: “Sitaki kukuona unatoka na Jimmy.”
MIMI: “Kwanini tena? Ni shem wangu shida iko wapi?”
IRYN: “Sizipendi tabia zake za kupenda wanawake ni hajatulia, angekuwa anakuheshimu hata asingeleta mwanamke pale.”
MIMI: “Amenitambulisha ni mpenzi wake sasa shida iko wapi?”
IRYN: “Mwanamke wake yuko pale home na mtoto wake, kamuacha kaja huku kuonana na malaya zake, naomba tuondoke twende hotelini please!.”
MIMI: “Sisi tumekuja kuangalia match bhana, ngoja nikamuage tuondoke.”
Ile nataka kwenda kumuaga alinivuta kunikataza na tukaondoka pale kurudi hotelini. Baada ya kurudi hotelini kwa upande wangu nilikuwa nina mizuka yangu, sasa ile kumshika si akani push kuonesha hataki dudu na nilishangaa sana.
“Sasa mummy unenitoa kwa Jimmy kisa wivu wako, unanirudisha hotelini hata kunipa utamu ni shida si ungeniacha tu kule mimi niendelee kupoteza muda?”
Iryn aliniangalia na hakujibu kitu aliishia kunyamaza kimya, na mimi niliendelea kuongea,
“Hii safari sijui why nimekuja huku maana Roho yangu ilikuwa haitaki, haya ndo matokeo ya kuforce. Anyway kesho mimi naondoka maana sioni faida ya kuendelea kubaki huku kama unaninunia.”
Mimi nilikwenda kuoga na baada ya kutoka washroom nilikuta Iryn hayupo na mimi nilijua ameondoka kurudi kwao, ni wivu wake ulikuwa una msumbua. Pale kitandani kulikuwa na karatasi nyeupe ameiandika na niliichukua ili nisome alichoniandikia.
CHAPTER 10
Arsenal akichukua ubingwa J2, nitapost picha nikiwa na Iryn kwa dakika 1 na nitaifuta. Otherwise tukutane kesho kwa chapter 10 ✅ Tuambizane na muda mkuu ili tutazame kwa timing!... All in all aaaaasante Kwa kutenga muda wako na kutufurahisha sie waja chochole
www.jamiiforums.com