LEARNED BROTHER
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 592
- 844
Bonge moja ya story, haichoshi kuisoma.
Yavutia mda wote
Yavutia mda wote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi tuna wavuta bange humu jamvini? Why insults always? What you gain after insulting? Shame on youWewe Fara.
Umeitwa hapa .
Mimi naongea na insider .
Siongei na mpumbavu kama wewe unayeleta mambo yasioleweka.
Kima wewe
Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
Muda huu mimi macho yangu yote yalikua yamelenga kwenye zile Box nijue Muajemi kaweka nini mle ndani?, japo zilikua hazinihusu ila nilitamani sana kujua ndani kuna nini.
Wewe unajua ni.mjinga Sana .Matusi ya mtt wa chekechea ,wewe umetoka Koo yenye matusi na unamiliki digrii ya matusi. Weka matusi Basi mazito. Unaiabisha mbona mkuu. Weka ambayo huwa nasikia wengine wanayaongea. Hutopata tenda msimu ujao. Demand Ni kubwa supply ndogo
Tulia kama haujui mada imeanzia wapi.Hivi tuna wavuta bange humu jamvini? Why insults always? What you gain after insulting? Shame on you
Hapa kwenye kula kimasihara kumenifanya nijenge imani kubwa ya hii story kuwa inaishi maisha ya Jf.Hapa ndo nikajua kumbe nilikua nimewekewa mtego kama ningekua natabia za kifisi kama wale wazee wa kula Kimasihara bhasi kibarua kingeota nyasi.
Wakuu tuseme umepata abiria masak Kwenda sehemu flan, ukifika malipo sianakuoa cash?? Sasa hao Uber pesa Yao wanaipata vp??EPISODE 16
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
Wakati nikiongea na Iryn kwa upande mwingine Mary naye alikua anapiga simu, nilitumia kama dakika 30 kumaliza mazungumzo na Iryn. Baada ya kumaliza mazungumzo naye, ikabidi nimpigie simu Mary Asap,
MARY : “Insider unaongea na nani usiku huu?”
MIMI : “Mama yangu”
MARY: “At this time of night?”
MIMI: “Ndio, kwani kuna time limit ya kuongea na mzazi?
MARY: “Siamini”
MIMI: “Niambie ulifanikisha?”
MARY: “Yeah, thank you. Insider can I ask you?”
MIMI: “Nakusikiliza Mary”
MARY: “What’s really going on between you and Prisca?”
MIMI: “Nothing, why are you asking me?”
MARY: “Naona ukaribu wenu unazidi kukua day after day.”
MIMI: “Mary bhana sasa si nilikuja kumwona Prisca alinambia anaumwa, ujue nyinyi ni Familia tayari afu nawachukulia kama washikaji zangu.”
MARY: “Insider Prisca kaondoka Ijumaa na hakurudi, amerudi jumamosi jioni anaumwa, kuna dalili zinaonesha mlikua pamoja.”
MIMI: “Mary unajua sikuelewi unachoongea, mimi nilikua na Prisca kivipi.”
MARY: “Prisca ni mdogo wangu na nina mjua vizuri sana, mimi na yeye tunashare mambo mengi sana ila kuhusu wewe amekua mgumu sana kushare na sio kawaida yake.”
MIMI: “Kama mnashare mambo mengi na mpaka sasa hajasema kitu, si manake mimi na yeye hakuna kinachoendelea.”
MARY : “Insider Prisca kaondoka Ijumaa na wewe ndo ulokuja mfata, baadae ananitumia message kwamba hatorudi home atalala hostel, Prisca halalagi Hostel weekend, na yule jamaa yake wameshaachana muda. Prisca Ijumaa alikua na wewe, maana nikijaribu kuunganisha hizi doti wewe ndo mwanaume kwa sasa ambaye unamchanganya Prisca.”
MIMI: “Mary mimi naona kama unajaribu kufanya guessing, na una uhakika gani kwamba Prisca wameachana na jamaa yake?”
MARY: “Prisca kaachana na jamaa yake kwasababu yako labda tu nikwambie hivo, she’s in love with you. Natoka Prisca arudi jumamosi usiku, amekua mtu wa kulalamika sana kuhusu wewe, you guys mlikua na usiku mzuri sana Ijumaa.”
MIMI: “Mary mimi nafikiri muulize Prisca vizuri alikua na nani maana mimi Ijumaa nimeshinda kwa Mamdogo wangu alikua anaumwa.”
MARY: “You guys mpo kwenye Mahusiano but you’re trying to sneak around”
MIMI: “Mary kama mimi natoka na Prisca hata nisingekuficha, kwanza ningependa kuwa na shemeji mzuri kama wewe.”
MARY: “Mmh mmmh sawa, unafanya nini?”
MIMI: “Naongea na mrembo Mary”
MARY: “Hahahaa Insider bhana”
MIMI: “Leo nitalala vizuri maana sauti yako ni nzuri sana.”
MARY: “Wanaume mnasifiaga hata kama kitu kibaya”
MIMI: “So you don’t trust me?”
MARY: “Alright nashukuru kama kweli”
MIMI: “Bye mimi nalala uwe na usiku mwema.”
MARY: “And you too.”
Muda ule nilikaa nikawaza kama Mary ameshajua mimi nimemla Prisca, amejuaje?, nikajiuliza au Aliona chats zetu na Prisca?. Lakini pia nikawaza Mary ni kama anatafuta ukweli kuhusu kinachoendelea mimi na Prisca. Mary pia alinekana ni kama mtu ambaye alipatwa na kawivu hivi.
Usiku huu pia nilichat sana na Prisca kupitia whatsapp na akawa ananitumia Picha zake alizopiga recently, nikawa namsifia sifia pale na nikalala zangu.
Nilichokifanya kwa sasa kwenye upande wa whatsapp nilifanya setting ambapo hata nikidownload picha inabaki mlemle kwenye whatsapp haijisave kwenye “camera roll”. Na pia nilikua nafuta chats palepale, nilijifunza kutokana na makosa.
*********
Asubuhi nilikua naamka 06:00 mapema kila siku, hii ndo ilikua time table yangu,nilikua naset na alarm kabisa. Na nilikua natumia dk15 kujiandaa na kutoka pale home na mara nyingi 06:30 ilikua inanikutia kwa Mama wa2. Nilikua namchukua Mama wa2 na mwanae then nitamdrop mwanae pale Mikocheni shule, then nitamchukua Maggy na kuwapeleka Posta.
Hizi ndo zilikua ratiba zangu za kila siku na hawa watu nilikua nimeingia nao mikataba hivyo nilikua sifanyi makosa.
Hii siku ilikua ni jumatano na niliamka mapema sana na nikaenda kumchukua mtoto wa mama 2 na baada ya kumuacha pale shuleni, nikaelekea kumchukua Maggy. Nilimpigia simu Maggy akanambia leo atachelewa kidogo, sababu nilikua sina jinsi ikabidi niende kwake kumsubiri.
Nilifika pale kwenye apartment anayoishi na muda huo Maggy alitoka kunifungulia geti, alionekana ni mtu ambaye ametoka kuamka muda huo.
MAGGY: “Insider samahani sana, jana nimetoka usiku sana ofisini, leo nitachelewa kuingia ofisni mpaka saa 3”
MIMI: “Sawa haina shida, acha nikusubirie tu.”
Mimi sikuwa na tatizo na akaomba nikamsubilie seblen kwake.
MIMI: “So hapa unaishi peke yako?”
MAGGY: “Ndio nitaishi na nani sasa?”
MIMI: “Hata na shemeji sio mbaya.”
MIMI: “Hahahaa Insider bhana, acha nikuandalie chai then tuondoke.”
MIMI: “Mimi sioni sababu ya kunywa chai asubuhi yote hii, wewe nenda kalale mimi nitakusubir hapa.”
MAGGY: “Nimeshamka hapa unafikir na usingizi tena?, ngoja nikukaangie hata mayai bhasi haitakua busara nikuweke bila kitu.”
Muda huo Maggy alikwenda jikoni na mimi nilikua niko seblen nimekaa. Na ndani ya muda mfupi alirudi na mayai ya kukaanga kwenye sahani na maziwa kwenye kikombe, akanipa na yeye akasema anakwenda kuoga.
“Maggy ni mwanamke ambaye tuseme ni wa kawaida yaani ana sura ya kawaida ila ana mahips , tuseme anafaa kuliwa vizuri kabisa.”
Na muda ule wakati Maggy akijiandaa nilimpigia simu Muajemi lakini hakuweza kupokea simu yangu, nikarudia tena ila hakuupokea. Nilitaka kumpa Muajemi taarifa mapema za kujiandaa na date.
Maggy alitoka akiwa amevaa surual ya kitambaa nyeusi na shati nyeupe alionekana kupendeza sana, na ilimchora Mahips yake, na mimi bila ya uchoyo nikampa sifa zake.
Mara nyingi tukiwa na Maggy story zetu nyingi sana zinakuwaga za maisha, Maggy ni aina ya wale wanawake ambao hawana mambo mengi na wako busy na mambo yao.
Nilimdrop pale ofisini kwake na muda huo ilikua saa4 asubuhi, nikatoka hapo nikaenda kupark gari pale pa sikuzote na nikawa nimeset destination ya kwenda Masaki.
Sasa nikiwa pale kijiweni tukiendelea na story na madereva wa Uber, story kubwa ilikua ni kuhusu Uber kutaka kufunga ofisi zao Tanzania. Sasa hapa kuliwa na pande mbili ambazo wanaunga hoja na wasio unga hoja.
“Uber wanaringa sana wanafikiri hata wakiondoka sisi tutalala njaa??, kamisheni yenyewe wanakata 25% hakuna tunachopata sisi.”
“Bolt ipo kwanza na wako tayari kupunguza kamisheni zao, Uber tumeichoka sisi kwanza Bolt ndo inawateja wengi kwa sasa.”
“Wewe fala unasema nini? Mimi nikipiga trip zangu ndefu 5 za Uber na pesa ya kutosha, huyo Bolt anawateja sababu anashusha sana nauli na tunaoumia ni sisi Madereva.”
“Sasa kwa taarifa yako nakwambia Uber wakifunga ofisi utaona jinsi Bolt watakavyoanza kuzingua, kwanza hawatujali Madereva kabisa.”
“Uber mimi imenipa connection sana asee naiheshimu, wateja wa Bolt ni maskini wanalia njaa sana.”
Yalikua ni mabishano ya madereva wa Uber na mimi nilikua nikichangia mada lakini nilikua upande wa Uber. Baada ya lisaa nilipata request ya mteja na alikua anakwenda pale Coco plaza.
Mteja alikua pale Exim Bank HQ, nikamchukua na tukaelekea Masaki na nikamdrop pale Coco plaza, mara nyingi sana wateja wa Bank huwa wanatumia card kwenye malipo.
Na mimi chap nilitoka nakwenda kuwachukua madogo ili niwapeleke majumbani kwao, ilikua ni kazi flani ya kitumwa lakini ndo mkono ulikua unakwenda kinywani kupitia hii kazi.
Wakati niko njiani Mzee wangu alinipigia simu kupitia Whatsapp call na akaniambia ananitumia namba za rafiki yake wa Dodoma ili tuwasiliane. Mzee akanambia ni rafiki yake sana hana shida na atanisaidia kwa kila hatua, na akanitoa wasiwasi. Baada ya mazungumzo na muda huohuo alikua kanitumia contact ikiwa inasomeka “Engineer Mollel”.
Na muda huo nilikua niko shuleni pale nimefika na nikawachukua watoto nakuanza safari ya kuondoka. Hawa watoto walikua wananipenda sana, wakiniona tu utaskia “Uncle Insider” where have you been?, sasa na mimi nilikuaga nawanunulia pipi, biscuits nawapa, walikua wananipenda sana.
Nilikua nawatoto wanne (4) ambao watatu walikua wakiume na mmoja wa kike. Kama kawaida niliwashusha wote akabaki mmoja ni wakike ambaye nilikua namshusha pale nyuma ya Budget kwa sikuzote.
Nikashuka kwenye gari nikagonga geti na akatoka dada mgeni ambaye nilikua namwona kwa mara ya kwanza.
Baada ya kufungua geti tukasalimiana pale,
DADA: “wewe ndo Insider?”
MIMI: “Ndo mimi kwema?”
“Dada Emmy huyu ndo Uncle Insider”
DADA: “Haya nenda ndani kabadilishe nguo nakuja. Kwema pole na kazi.”
MIMI: “Ahsante ndo nakuona leo wewe ndo dada na Caroline?” (Yule mtoto)
DADA: “Mimi ndo dada yake wa kwanza. Mama alikua anahitaji kuonana na wewe weekend, alinambia ukija nikwambie, pia alikua anahitaji namba yako ya simu.”
MIMI: “Yule dada anayefunguaga geti kila siku mbona anayo?”
DADA: “Yule kaondoka toka Jumapili, juzi na jana wewe hujaja, Carol alikuwa analetwa na mtu mwingine.”
MIMI: “Yeah sure, yule ni ndugu yangu hana shida. Gari yangu ilipata ajali ndomana sikuweza kuja.”
DADA: “Pole sana”
Nikampa namba yangu ya simu pale na sikujua Mama yake Carol alikua anataka kuongea nini. Na muda huo Iryn alikua akinipigia simu na palepale nikapokea,
MIMI: “Nambie Bossy wangu.”
IRYN: “Poa, upo wapi?”
MIMI: “Niko Bahari beach”
IRYN: “Nakusubiri uje tufanye ile kazi”
MIMI: “Soon nitakuwa hapo.”
IRYN: “Okay”
Muda huo ilikua saa 7 mchana hivyo niliamua kutoka pale na kwenda kwa Iryn. Nilitumia kama dk45 kufika pale, na yeye nilimkuta akiwa seblen na zile form akizipitia.
Nilikwenda jikoni kuangalia alichopika, nilikua na njaa sana na alikua kapika wali kwa kutumia rice cooker na mboga za majani na nyama. Nikapakua chakula nikaanza kula na muda huo alikua ananiangalia sana.
MIMI: “Vipi unanifananisha au?”
IRYN: “Unaonekana ulikua na njaa sana.”
MIMI: “Ndomana unaona nilipitiliza jikoni, kwa haya mapishi matamu unayopika unanishawishi nikuoe.”
IRYN: “Seriously? mapishi ndo yanakufanya unioe?”
MIMI: “Wewe unafikiri mimi naweza kumwoa Bossy wangu?”
IRYN: “Mapenzi ni upofu”
MIMI: “Yeah sure ila kuna vitu haviwezekani automatically.”
IRYN: “Impossible is Nothing, unaonekana hujiamini”
MIMI: “Umezipitia form zote tayari?”
IRYN: “Baadhi ndo nimezipitia hasa hizo za kampuni. Hizi zingine zinahitaji umakini nilikua nakusubiri wewe.”
MIMI: “Ngoja nimalizie kula, tuanze kazi.”
IRYN: “Hivi Insider una elimu gani?”
MIMI: “Bachelor ya Uchumi & Takwimu”
IRYN: “Nilihisi tu, maana kichwa chako kiko smart sana, watu wanaojua hesabu sikuzote utawajua tu.”
MIMI: “Hiki kichwa kina mambo mengi, hakina usmart wowote.”
IRYN: “No comment.”
Baada ya kumaliza kula tulianza kazi ya kuzipitia zile forms. Kwa ufupi, Mama yake alianza kazi na hii Organization “X” mwaka 1991 Ethiopia, mwaka 1992 ndo alihamishiwa Tanzania. Mwaka 2000 ndo alipewa parmanent contract na hii organization na alikua chini ya Idara ya Social protection.
Na kipindi hicho alikua analipwa mshahara wa $45,000 kwa mwaka. Lakini mshahara ulikua unapanda kila mwaka, ilivyofika mwaka 2012 ndo alipanda cheo na kuwa Coordinator wa Idara na mpaka anapatwa na umauti alikua analipwa $232,000 na point kadhaa kwa mwaka. Ukii Exchange hio amount na ukagawanya kwa 12 unapata mshahara wa si chini ya 45million kwa mwezi. Na pia nilishangaa wafanyakazi wa hii Organization hawalipi kodi wala hawana makato yoyote kwenye mishahara yao.
Nje na hapo nilikuja kujua mama yake alikua ni mtu mkubwa sana kwani kafanya na kuzisimamia project nyingi sana hapa Tanzania, East Africa na Africa kwa Ujumla, mpaka worldwide. Kufanya kazi na Organization kwa zaidi ya miaka 25 na kupewa Parmanent contract sio jambo rahisi kwa ile Organization.
Pia nikajua Mama yake alikua ni mwenyekiti wa hii Organization kwa upande wa Africa Mashariki kwenye mambo ya Social protection.
Tulipiga zile hesabu na mwisho wa siku tulipata kiasi ambacho kilikua sahihi kabisa na hesabu zao exactly. Nikajisemea ingekua Bongo ungekuta wahuni washapindisha hesabu muda mrefu sana.
Kwa zile hesabu niishie kusema Iryn alikuwa na uhakika wa kuingiziwa Pesa nyingi sana na yeye pekee ndo alitajwa kama mrithi wa kunufaika na mafao ya mama yake.
Mama yake pia alikua na mkopo Bank binafsi aliokuwa amekopa na ilionekana umebaki kama $191,000 kitu kama hicho ilikua around humo nakumbuka.
Tulimaliza lile zoezi na Iryn aliendelea kuzipitia zile documents za kampuni ambapo nilimwacha aendelee mimi kama dizaini zilikua hazinihusu.
Sikukaa sana pale nikamwaga mimi naondoka akanambia kesho saa4 asubuhi niwe pale ili twende kwa Mama Janeth, na mimi nikaondoka.
Niliwasha App nikaendelea na kazi yangu ya Uber kama kawaida. Sikupiga trip nyingi sana sababu ya muda na nilirudi home saa 1 usiku.
Na muda ule Muajemi alinipigia simu, nikapokea simu yake, (Maongezi yetu yalikua ni kwa kiingereza.)
MUAJEMI: “Bro mambo vipi.”
MIMI: “Salama Bossy wangu”
MUAJEMI: “Samahani sana ulinipigia simu asubuhi ila nilikua nimebanwa sana nikashindwa kukurudia ontime.”
MIMI: “Haina shida Bro!, nilitambua hilo”
MUAJEMI: “Nambie Bro!, sijui ulikua na habari gani.”
MIMI: “Jambo lako limekamilika Bro, ulinipa kazi nimeikamilisha.”
MUAJEMI: “Seriously?, Bro umenifurahisha sana kwa hizi habari.”
MIMI: “Nilikwambia siku ile mambo mazuri hayataki haraka, hutakiwi kuforce suala kama hili, acha aamue mwenyewe.”
MUAJEMI: “Kaka umetisha sana, nakupa respect kwa hili.”
MIMI: “Hata hivyo haikua kazi rahisi kaka, nimetumia mbinu nyingi sana mpaka kakubali yule mrembo.”
MUAJEMI: “Kaka nitakuongezea dau usijali, kwa hili umetisha sana.”
MIMI: “Sasa kesho ndo inatakiwa muonane Bro!, ikishindikana kesho kupata chance nyingine itakua ngumu sana, so do you have to do kesho muonane.”
MUAJEMI: “Bro kwa kesho timetable yangu iko vizuri tu kuanzia jioni, Bro siwezi fanya makosa yaani umehangaika kote umenipa assist then nishindwe kufunga goli?, siwez Bro! ninahamu sana na kesho ifike.”
MIMI: “Ok kesho asubuhi nitakupa timetable Bossy, ila naomba nikwambie jambo.”
MUAJEMI: “Jambo gani Bro.”
MIMI: “Iryn ni Mwanamke ambaye hana shida na Pesa, kama pesa anazo hivyo hakikisha unazungumza naye masuala ya Business, hakikisha unamfanya akuone wewe kama connection yake hasa huko dubai, ana mipango mingi sana ya biashara hakikisha unaifungua hii CODE ili akufungukie. Ukiweza ku-win hapa naamini yule Mrembo utampata.”
MUAJEMI : “ Kaka Ahsante sana kwa kunipa Mwanzo mzuri hilo kwangu ni suala dogo na nina kuhakikishia huyo mtoto nampata.”
MIMI: “Don’t force her, acha afanye maamuzi mwenyewe, kwa heri Bro! tutaonana kesho.”
MUAJEMI: “Ahsante kaka, nikimpata uyo mrembo utaishi maisha mazuri hapa mjini.”
MIMI: “Hayo ni wewe Kaka, kazi yangu nimemaliza uliyonipa sasa kazi imebaki kwako.”
Ilikua ni week kadhaa zimekata toka Muajemi anipe kazi, kwa upande mwingine niliwaza, Muajemi anatoa ahadi sababu anahitaji kumpata Iryn, hivyo amejua mimi ndo kama CODE ya kumpata. Ok nikasema sikuzote kwenye fursa ndo kuna fursa, cha muhimu nimepata kibunda changu hakuna shida, mimi najali Maokoto tu.
Nilimpigia simu Engineer Mollel wa Dodoma na tukaongea sana, tukakubaliana hii mipango ni bora kuipanga face to face. Na pia akanambia natakiwa kwenda Dodoma nikamwonyeshe kiwanja ili aweze kufanya estimation cost za ujenzi. Nikamwambia Jumapili nitakwenda kwaajili ya hilo swala, na akasema ramani tayari anayo akikiona kiwanja siku hiyohiyo atatoa hesabu.
***********
Alhamisi ilifika na baada ya kumalizana na kina Maggy, nilikwenda kwa Iryn na saa3 asubuhi nilikua pale kwake na nilimkuta alikua bado hajaamka. Nikampigia simu akaja fungua mlango,
MIMI: “Mpaka sasa hujaamka vipi unaumwa?
IRYN: “Insider jana nimechelewa kulala nilikua naangalia movie.”
Mimi nilikwenda jikoni kuandaa chai na yeye alikwenda kujiandaa, baada ya muda mfupi alitoka akiwa amevaa “skin jeans ya blue, kishati cha maroon na miwani, chini alivaa viatu skuna “muundo huu[emoji151]” na alikuwa kawaka sana.
IRYN: “Mbona unaniangalia hivyo?”
MIMI: “Kwamba umeanza kupoteza confidence kwangu?”
IRYN: “Insider mimi kama mwanamke pia na aibu, hayo macho yako yanafanya nikose kujiamini. Vipi nimezingua kuvaa hivi?”
MIMI: “Embu geuka nyuma nikuone, ewaaah umependeza sana kuliko siku zote.”
Ile skin ilikuwa imemkamata kisawasawa na ilikua imechora shepu yake.
Tulikunywa chai baada ya hapo tukaanza safari ya kwenda Masaki kwa Mama Janeth. Saa 4 asubuhi tulikua pale na tulikaribishwa ndani seblen. Mama Janeth alikua hajatoka muda huo alikua bado ndani, baada ya muda dada alileta korosho tukawa tunakula pale huku tukimsubiri Mama Janeth.
Baada ya dakika 10 mama Janeth alitoka akiwa ameshika funguo ya gari, akatusalimia.
MAMA JANETH: “Nafikiri tuanze Kigamboni afu tumalize na Masaki.”
IRYN: “Vyovyote tu sawa”
Na muda huo tulitoka nje Mama Janeth akasema tutumie gari yake “Audi Q7” na akanipa mimi funguo niendeshe, yeye alisema anataka atumie muda mwingi kuongea na Iryn.
Mimi nilipokea funguo japo sikuwai kuwa na historia ya kuendesha Audi nikasema leo niatendesha tu. Baada ya kuingia kwenye gari mama Janeth alikua bado kama anatoa maagizo kwa dada wa kazi, na muda huo nilitumia muda mchache sana kuisoma gari na nikawa nimeimasta.
Baada ya muda mfupi Iryn na Mama Janeth waliingia na wakakaa siti za nyuma ya gari, hao tukaondoka kuelekea Kigamboni.
Niseme tu Audi ni bonge la gari aisee, kuna gari unaendesha huku ukisikia raha kudrive, inakufanya usahau shida za dunia hii, gari inanukia vizuri afu inakiyoyozi flani hivi amazing. Hii Dunia kuna watu wanaishi asee na ile gari Mama Janeth aliinunua “0 km” yaani ni Brand new, afu ni new model.
Tulikwenda Kigamboni tukitumia Barabara ya Kilwa na tulipita pale darajani, muda huo Iryn na Mama Janeth waalikua busy sana wakiongea.
Tulikwenda mpaka Kigamboni kisiwani ambapo Mama Iryn alikua amejenga. Kwenye zile apartments kulikua na Mlinzi baada ya kumwona Mama Janeth alifungua geti na tukaingia ndani. Walizunguka kuzitazama zile apartments zote na kulikuwa na utulivu wa hali ya juu sana.
Zilikua ni Apartments tano (5) nzuri sana, apartments zenye vyumba vitatu zilikua 2 na apartment zenye vyumba viwili zilikua 3.
Kwa upande wa Iryn yeye ilikua ndio mara yake ya kwanza kufika kwenye hizi apartments. Na wakati wakiendelea na ukaguzi wao kuna sehem kulikua na garden mimi nikaenda kukaa pale, nikiwasubiri.
Baada ya kumaliza ukaguzi wa nyumba na kuzunguka kote mpaka nje, walikuja pale garden na mazungumzo yao yaliendelea.
IRYN: “Mama alianza kujenga lini hapa?”
MAMA JANETH: “Hizi apartments ujenzi ulianza 2019 na 2020 Februari watu walianza kuingia hapa.”
IRYN: “Baba alikua anajua kama mama anafanya hii Project?”
MAMA JANETH: “Hapana Baba yako hajui, Mama yako alifanya siri.”
IRYN: “Mama aliwezaje kuficha hili?”
MAMA JANETH: “Iryn unajua kuna mambo mengi yalikua yanatokea kati ya Mama na baba yako kipindi uko masomoni. Mama yako alihisi kuna mambo hayako sawa kwa upande wa Baba yako ndomana hakutaka kumshirikisha mambo yake.”
IRYN: “Bado una mawasiliano na Baba?”
MAMA JANETH: “Huwa tunawasiliana kwa nadra sana, tukifika home tutaongea vizuri mwanangu, tutakuwa na mazungumzo private”
Muda huu Mama Janeth aliniomba nikachukue bahasha kwenye gari ambayo ilikua ina mikataba ya wapangaji.
IRYN: “Hii ndo mikataba ya wapangaji.”
MAMA JANETH: “Hio ndo mikataba yao, na hizi apartments zote wanakaa foreigners.”
IRYN: “Ahsante Mama kwa yote.”
MAMA JANETH: “Iryn wewe ni kama bint yangu, Mama yako alikua ni more than friend, sometimes namkumbuka sana. Mimi na yeye tulikua na combination nzuri sana kazini na nyumbani.”
IRYN: “Mwanao Janeth anamaliza lini chuo.”
MAMA JANETH: “Janeth ndo kwanza yuko mwaka wa 1, yuko Scotland kwa sasa, nitampa namba yako akutafute uwe unampa ushauri kama dada yake.”
IRYN: “Kipindi kile alikua mdogo sana”
MAMA JANETH: “Na picha nyingi mlizopiga pamoja, utanikumbusha nikupe.”
Tulitumia kama masaa 3 pale na tuliondoka kurudi Masaki, tulipitia pale Ferry na Mama Janeth alinunua Samaki wabichi.
Tulipitia pale Dar Free market na tuliingia kwenye mgawaha kwaajili ya kupata lunch. Tulitoka pale na tulielekea nyumba ya pili, hii nyumba ilikua kama unatokea na “Samaki Samaki” kwenda “Village Market” kwa mbele kidogo kuna njiapanda, na ukifika pale njiapanda kuna baraba inakwenda kushoto na kulia. Barabara ya kushoto ndo inakwenda UN, na ya kulia unaweza itumia kwenda Coco Beach, ukishaingia hiyo ya kulia kwa mbele kidogo kulikua na hio nyumba.
Tulifika pale getini tukapiga honi na mlinzi alivyoiona gari akafungua tukaingia ndani.
Ulikua ni bonge la Mjengo wa ghorofa 1, nyumba ilikua ni nzuri sana kuanzia nje kwenye fensi mpaka ndani.
Iryn mwenyewe alishangaa sana, ni kama hakuwa akiamini mama yake ndo alikua akifanya yale maajabu.
Na muda huo walikuwa wakiongea na Mama Janeth;
IRYN: “Mama aliwezaje kufanya haya mambo bila mimi kujua?”
MAMA JANETH: “Iryn mwanangu Mama yako alikuacha usome kwanza hata kusomea Business Administration ilikua ni mpango wa mama. Mimi na mama yako tulikua na mipango mingi sana kwenye biashara nafikiri tutashare.”
IRYN: “Najiuliza Mama aliwezaje kumiliki nyumba nzuri kama hii na tena Masaki, bhasi kukaa kwangu mbali na Mama mambo mengi yalikua yakinipita.”
MAMA JANETH: “Kwamba unashangaa mama yako aliwezaje?, Mama yako nje na kazi alikua ni mtu mwenye deals nyingi sana, pia amewasaidia watu wengi hasa hizi NGO’s ambao walikua wanamlipa. Iryn mama yako alikua ni mtu mkubwa sana kwa upande wa Organization na alikua na connections worldwide.”
Iryn alijikuta akianza kulia pale ni kama Mama Janeth alimfanya amkumbuke Mama yake, maana hakuamini mama yake angefanya mambo yote kwaajili yake. Na Mama Janeth alikwenda akamkumbatia, wakaendelea kutembea.
Hatukukaa sana hapa na tuliondoka kurudi kwa Mama Janeth, na wakati tuko njian Mama Janeth alikua akimwambia Iryn kwamba nyumba zote kuna kampuni huwa anazitumia katika upangishaji. Na walikua wanaongea masuala mengine ambayo sikua nikiyafuatilia maana nilikua naona hayanihusu japo wanavyozungumza nilikua navisikia.
Baada ya kufika kwa Mama Janeth tuliingia ndani seblen na wao walitoka kwenda kibarazani, walikua na mazungumzo private. Dada aliniletea juice kwenye glass na korosho wakati mimi niko pale seblen.
Na muda huo tuliorudi kulikuwa na watoto wawili ambao ni watoto wake na alimtambulisha Iryn kama wadogo zake. Mtoto wa kwanza kwa kum kadiria umri wake ni kama miaka 12 na mtoto wa pili umri wake ni kama 6. Mkubwa alikua wa kike na mdogo alikua wa kiume.
Wakati niko pale sebelen Muajemi alipiga simu kuulizia tuko wapi na tunameet wapi, nikamwambia tuko Masaki ila Iryn bado hajamaliza mambo yake. Akanambia yeye yuko Msasani na yuko ready, tukikaribia kumaliza mambo yetu nimpe taarifa ili aanze kusogea.
Nikamwambia ndani ya muda mfupi nitakua nimeshampa tayari location, na pia nilimwambia akimalizana na Iryn aondoke mambo mengine tutawasiliana. Niliamua kufanya hivo ili Iryn asijue kuna something fishy kinaendelea kati ya mimi na Muajemi.
Mazungumzo yao yalikua marefu sana na yalichukua karibu saa zima, sikujua wanazungumza nini ila ili onekana ni kama suala la Baba yake.
Baada ya kumaliza mazungumzo yao walirudi seblen na muda huo walikua wakipanga mipango ya kuindeleza saloon hasa kwenye upande wa kutoa huduma. Iryn alikua akimwambia Mama Janeth kuna haja ya kuanzisha huduma za Massage pale, kwani watapata wateja wengi sana, na mama Janeth alilifurahia wazo hilo.
Mama Janeth alitoka pale seblen na nikachukua nafasi hio kumuuliza Iryn tunameet wapi na Muajemi na yeye akasema isiwe nje na Masaki.
Nikamtext Muajemi kupitia Whatsapp na nikamwambia asogee mpaka Masaki ndo watakutana huku. Kuhusu location nilimwambia yeye aseme wapi tutamkuta na sisi tutakwenda.
Baada ya dakika 20 muajemi akanitext;
MUAJEMI: “Bro niko Orchid cafe hapa nawasubiri.”
MIMI: “Nasisi soon tutakuwa hapo Bossy.”
MUAJEMI: “No problem.”
Saa 12 jioni ndo tulitoka pale kwa Mama Janeth baada ya mazungumzo yao kukamilika. Na wakati tumeingia kwenye gari ili tuondoke Mama Janeth alikuja na picha zilikua kwenye bahasha akampa Iryn.
IRYN: “Yuko wapi huyu mtu?”
MIMI: “Anasema yuko Orchid cafe.”
IRYN: “Ok twende ili tuwai kurudi maana leo nimechoka sana.”
MIMI: “Utabidi unifundishe ili niwe nakufanyia massage kama ukichoka kama hivi.”
IRYN: “Hahahaa Insider leo umenifurahisha sana.”
MIMI: “Au ndo mganga hajigangi?, unafanyia watu massage how about you? Au you don’t like?”
IRYN: “Nafanyaga lakini marachache ila nikienda nje na sio hapa bongo.”
MIMI: “Wewe ni expensive, hata hivyo kwa huo uzuri wako na hiyo ngozi yako laini bongo hakukufai, hawachelewi kukuweka ngeu.”
IRYN: “Insider umeanza mambo yako.”
MIMI: “Hivi kwanini hupendagi nikikusifia?, bhasi nitaacha kukusifia.”
IRYN: “Sijasema sipendi sometimes unanipa sifa ambazo sina ujue.”
MIMI: “Embu niambie ni sifa gani nimekupa afu hauna.?”
Iryn aliishia kunyamaza kimya ni kama vile alikosa cha kujibu na akaishia kunisonya kichwani kwa mkono. Na muda huo tulikua tumefika pale Orchid cafe, tulitumia kama dakika 5 hivi kufika pale.
******
Saa 12 jioni ndo muda ambao tulionana na Muajemi kama tulivyokubaliana tuonane pale, zilikua tayari kama dakika 30 zimepita toka Muajemi awasili eneo hili.
Wakati tunashuka pale Parking na kuingia mle ndani cafe, Iryn alikua akipigwa sana macho asee.
Unajua Warembo kama hawa kwa Tanzania hawaonekaniki mara kwa mara ni adimu sana, so wanavyo onekana machoni pa watu wanakuwa kama vivutio.
Tuliingia moja kwa moja na Muajemi alikua amekaa mwishoni kabisa, na mbele yake alikua na kikombe cha kahawa.
Tulifika mpaka pale tukasalimiana na muda ule dada alikua amekuja kutusikiliza tayari. Mimi niliagiza kahawa pale, nikawaacha pale nikawaambia natoka nje kuongea na simu.
Hii ni mbinu ya kibaharia, nilitaka kumwachia uwanja Muajemi awe huru kucheza mpira, dizaini kama Muajemi nayeye alikua kausoma mchezo. Nilitoka nje nikazuga zuga pale ndani ya dakika 10 nikarudi ndani.
Na mimi nilikwenda upande mwingine kabisa nikawaacha wakiongea, na ndani ya dakika mfupi dada alikua kaniletea kahawa.
Ndani ya dakika 10 dada alikuja tena akanambia Bossy pale amesema uagize chochote unachotaka, nikasema acha niagize chakula tu ili niendelee kumpa nafasi ya kuongea na Iryn. Na palepale nikacheki “Menu”nikaagiza beef na chips, maana nilikua sioni cha kuagiza pale, Menu ina majina ya ajabu.
Ndani ya dakika 10 nililetewa msosi wangu na nikaanza kula taratibu. Muda huo nilikua napiga macho ya kiwizi kuona kinachoendelea, na walionekana busy sana wakiongea na sometimes walikua wakicheka,
Nilimwona Muajemi akimwita dada na akampa funguo ya gari na alikua kama anampa maelekezo, baada ya dakika chache dada alikua karudi na kimfuko cheupe.
Tulikaa pale Orchid kwa saa 1 na baada ya hapo walinipa ishara tuondoke na wenyewe walikua wametangulia kwa mbele, na nilimwona Iryn akiwa ameshika kile kimfuko. Muajemi alituaga na akapanda kwenye gari yake Land Cruiser VXR akaondoka.
Mimi na Iryn tuliondoka lakini wakati tuko njiani Iryn akanambia twende “Pizza Hut” Mikocheni ana hamu ya kula Pizza.
Tuliwasili pale Mikocheni Plaza na tukatulia pale kwa nje ni kama dining tuseme, ni sehemu ambayo watu waki order wanapenda kukaa, hii sehem imetizamana na Parking.
Tulikaa pale mwishoni kabisa kwenye ki-ukuta na tulikuwa tunapiga story huku tunacheka.
MIMI: “Muajemi anasemaje?”
IRYN: “Anaonekana ana connection nyingi kwa Dubai, kuna kazi nimempa anisaidie kununua mashine za saloon, hapo ndo nitajua kama kweli ana connection au laah!”
MIMI: “Wewe unaona ni muongo?”
IRYN: “Anaonekana ni mtu mzuri ila usimwamini mtu usiyemjua Insider, kuwa makini.”
MIMI: “Sure, ila wewe moyo wako unasemaje?”
IRYN: “Naona ni mtu mzuri.”
MIMI: “Hiyo Pizza utakula mwenyewe mimi nimekula kule Orchid nimeshiba hapa.”
IRYN: “No utakula hata vipande 2 yaani mimi nile wewe uwe unanitizama?
MIMI: “Afu pia sipendagi haya mapizza kabisa na aleji nayo.”
IRYN: “Mnasemaga mwanaume rijali hatumii, Pizza, burger, na chips, na wewe upo hilo kundi?”
MIMI: “Obviously, mwanaume anatakiwa ale Donna ili awe na nguvu, haya si yanafanya uwe laini laini, hata show sidhani kama utaweza vumilia mikiki.”
IRYN: “Hahahaa jamani, Insider wewe unaonekana ni muhuni sana.”
MIMI: “Ningekua mhuni ile siku ningekua nimekufakamia.”
IRYN: “Aya bhana umeshinda”
MIMI: “Iryn mimi najitambua sana na pia najiheshimu.”
Na muda huu Mary alikua anapiga simu Nikapokea:
MARY : “Insider mambo”
MIMI: “Freshy mzima?”
MARY: “Niko poa, uko wapi?”
MIMI: “Niko Mikocheni, nambie.”
MARY: “Niko hapa stationery ulikonileta juzi, nasubir kazi,nafikiri ntachelewa sana kurudi home, njoo nipe kampani bhasi.”
MIMI: “Pole kwani walikua hawajamaliza?”
MARY: “Bado yaani, na kesho natakiwa kusubmit”
MIMI: “Sawa kama nitawai kurudi nitapitia hapo.”
MARY: “Okay, see you soon.” Na akakata simu
Muda huu Iryn alikua ananiangalia afu akatikisa kichwa kama mtu anayesikitika.
IRYN: “Insider appointment zako ni za usiku tu.”
MARY: “Kwani kuna shida?”
IRYN: “Nope ila sio vizuri
MIM: “Unajua mimi ni Uber hivyo nawateja wengi, sometimes huwa naamka hata usiku wa manane, unakuta mteja anakwenda Airport inabdi umpeleke tu, kama wewe ulivyotokea kupenda kufanya kazi na mimi hata wengine vivyo hivyo wanatamani kufanya kazi na mimi.”
IRYN: “Pole sana, hard work always pay off”
MIMI: “Ndo hivyo.”
Alimaliza kula na nikamrudisha kwake na muda huo ilikua kama saa 3 usiku kasoro. Nilipark gari nje ya fense na tuliingia ndani, na mkononi alikua ameshika kile kimfuko alichopewa na Muajemi pamoja na bahasha aliyopewa na Mama Janeth.
Alikaa kwenye kochi na aliingiza mkono kwenye ule mfuko na akatoa bahasha ya blue, akaifungua ile bahasha ya blue na ndani tena kulikua na box tatu (3) tofauti. Box moja lilikua kubwa limefungwa na bahasha ya purple na vibox vidogo viwili vilikua vimefungwa kwa rangi ya pink na orange.
Muda huu mimi macho yangu yote yalikua yamelenga kwenye zile Box nijue Muajemi kaweka nini mle ndani?, japo zilikua hazinihusu ila nilitamani sana kujua ndani kuna nini.
TO BE CONTINUED.
Wakuu tuseme umepata abiria masak Kwenda sehemu flan, ukifika malipo sianakuoa cash?? Sasa hao Uber pesa Yao wanaipata vp??
AlooooooooooIpo hivi kama mteja analipa kwa card huwa wanakata pesa yao palepale.
Kama unapokea cash tu, kamisheni ikifika 20,000 Hujalipa wanakufungia hupati request, mpaka ulipie.
Aloooooooooo
INSIDER MAN tupe ratiba.
tumechoka kuwa walinzi wa thread kila mda tunavizia kama umeachia episode.
kama ni kila siku jioni au usiku tujue.
Unafikiri watu wote wenye pesa wanapenda magari?Kuna mzee mmoja anahela ila hajui kuendesha gari na hataki hizo namboHivi isider ina maana huyo Dada mwenye biashara za mamilion alidhindwa kununua hata ka IST ka million 15
Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
Ni vzr sana mkuu kujua ratibaKesho tukutane jioni 19:00
NotedKesho tukutane jioni 19:00
Makasiriko ya nini?Wewe Fara.
Umeitwa hapa .
Mimi naongea na insider .
Siongei na mpumbavu kama wewe unayeleta mambo yasioleweka.
Kima wewe
Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app