Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sorry nilikuwa namquote mtu mwingineBoss labda unieleweshe
INSIDER MAN msaidie huyumazee kwa upendo wenu naomba mniambie tu season 02 ep1 ni page namba ngapi maan naaslide iz page sioni ata dalili naombeni mniambie page number tu ntashukuru sana
INSIDER MANmazee kwa upendo wenu naomba mniambie tu season 02 ep1 ni page namba ngapi maan naaslide iz page sioni ata dalili naombeni mniambie page number tu ntashukuru sana
Thank youSEASON 02:
CHAPTER 18
“BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Nilimpigia simu na baada ya kupokea hatukuongea sana ila alisema tutaongea kesho vizuri alikuwa kalala tayari. Habari kubwa aliyosema ni kwamba maamuzi yaliyochukuliwa na familia yake ni magumu sana na sijui kama mimi nitayaweza na hili ndo linampa mawazo kwani anajua fika mimi sitoweza….
CONTINUE:
MIMI: “Nafikiri ni heri ukanambia kidogo ni maamuzi gani mmechukua na familia yako.”
IRYN: “Baby wameongea mambo mengi sana kuhusu wewe mpaka nimejisikia vibaya, they don’t care kwamba wewe ndo mwanaume pekee uliyeweza kuwa nami kwenye kipindi cha mpito.”
MIMI: “Nenda straight kwenye point wanasemaje?”
IRYN: “Wanataka uje Ethiopia wakufahamu na wajue mipango yako juu yangu, then ijumaa nakuja Dar tutaongea na kujadiliana vizuri kihusu hili.”
MIMI: “Sawa haina shida kama unakuja tutayajenga mke wangu.”
IRYN: “I love you Insider.”
MIMI: “I love you too.”
Baada ya maongezi mafupi niliamua kuingiza gari ndani na nilikwenda moja kwa moja chumbani kuoga.
Kipindi naoga Prisca alikuwa anapiga simu, na wife baada ya kugundua anayepiga simu ni Prisca alipokea simu yake, lakini hawakuongea Prisca alikata simu. Mnakumbuka kipindi kile nyuma wife alizioteaga chats zangu na Prisca mpaka akaondoka kwenda kwao? Na ndo nikapata sababu ya kumla Prisca kwa mara ya kwanza sababu ya hasira??.
Ipo hivi, wife anatabia ya kunote namba za wanawake ambao huwa anahisi tuko kwenye mahusiano, sasa akigundua bado tunawasiliana huwa kina nuka. Sasa, baada ya kunidaka kipindi kile, tulikubaliana na Prisca asajili namba nyingine ambayo tungekuwa tuna wasiliana ili wife asijue.
Baada ya kuachana na Prisca, mawasiliano yetu yalikata kabisa na alianza kunicheki kwa namba yake ya zamani na mimi ndo kuisave kwa mara nyingine. Sasa hili lilikuwa ni kosa kubwa sana maana wife alikuwa ameikariri namba ya Prisca mpaka jina lake.
Tuendelee, sasa baada ya kutoka kuoga nilimkuta wife amekaa kitandani huku ameshika simu yangu mkononi na alianza kuongea;
“Baba J, hivi huyu mwanamke wako bado mnawasiliana?.”
Mimi nilikuwa sijui kinachoendelea kwakweli na ilibidi nianze kumshangaa;
“Mwanamke gani gena mbona sikuelewi?”
“Huyu Prisca anakupigia simu unafikiri sikuikariri namba yake? Na inakuaje anakupigia simu usiku huu? Na ametuma ujumbe kuuliza kama umefika salama, kuonesha mlikuwa wote.”
“Mama J kitendo cha kupiga simu sio kigezo ni mwanamke wangu hapana, nilimpigia ili anipe namba za dada yake, si unaona nimechange simu? Nimepoteza contacts nyingi sana na kipindi nampigia hakupokea, nafikiri amenicheki baada ya kuona missed call zangu.”
“Baba J hivi unanionaga mimi ni mtoto sana? Kwanza umerudi na spidi umeingia bafuni kuoga, hivi unanichukulia mimi kama nani humu ndani?”
“Wewe ni mke wangu nakuheshimu na siwezi kuwa na mwanamke mwingine zaidi yako.”
“Baba J nimeshachoka na hizi drama zako, kama umenichoka ni bora ukanambia mapema nijue, ili nikupe nafasi ya kufanya mambo yako kwa uhuru.”
Wife aliondoka na aliniacha bado nimesimama nimebong’aa, ukweli Prisca alikuwa kazingua sana na nilijisemea huyu kesho nitamuwashia moto kwa upuuzi aliofanya.
Nilijiona kama nina mkosi na Prisca na kuendelea kuwa naye karibu nitazidi kuleta mafarakano kwenye familia yangu, niliona ni bora nikae nae mbali, afu hana umuhimu wowote kwangu zaidi ya kunipa matatizo. Hata mzuka wa kwenda kula ulinikata na nilipanda kitandani nikaendelea kuwaza kuhusu future ya maisha yangu. Niliendelea kufikiri namna ya kumaliza huu msala wa Iryn, maana sikuwa na budi ya kufanya hili kwaajili ya mtoto.
Nilifikiri kuhusu kumshirikisha mzee wangu na dada yangu, lakini niliona ni busara nikongea kwanza na sister, afu kuhusu wazazi mpaka Iryn atakapo jifungua.
Kwa upande mwingine niliwaza kumshirikisha Dullah na Allen kuhusu hii ishu ili nione mawazo yao kwenye hili jambo. Allen ni kama kaka kwangu na tulitokea kukubaliana sana, licha ya yote pia ni auditor na ni mzuri sana kwenye kutoa mawazo na ushauri, niliona anaweza kuwa msaada kwangu.
*****
Asubuhi nilikuwa nina ratiba za kuonana na dalali kwaajili ya fremu ya biashara, nilikuwa nishaanza process za kutafuta fremu kwaajili ya Jane. Dalali alikuwa ameshanipa taarifa ya kwenda kuziangalia fremu zilizokuwa zimepatikana na tulikubaliana tuonane saa 4 asubuhi.
Baada ya kupata breakfast niliondoka kwenda Bahari Beach kuonana na Dalali na tulikutana pale Mtongani kituoni, karibu na police, tukaendelea na safari.
Dalali alikuwa ana frem 3 za kunionesha na baada ya kuziangalia zote, hakuna hata moja ambayo ilinivutia na alinambia kuna frem ya mwisho amepigiwa simu tukaingalie na haikuwa mbali.
Baada ya kuiona fremu kwa upande wangu niliipenda, kwani ilikuwa kubwa sana saizi ya double fremu na ilikuwa location nzuri, parking kubwa na mazingira kwa ujumla ni mazuri.
Niliipiga picha na nikazituma kwa Jane ili aione na yeye kwa upande wake alitoa recommendation nzuri na alisema kaipenda, hivyo tuendelee kuongea kuhusu kodi.
Dalali alisema gharama ya fremu ni laki sita, lakini maongezi yapo kama tutakuwa serious, bhasi ataongea na mmiliki atupunguzie kodi. Niliomba anipe namba za mmiliki ili niongee naye mwenyewe na tulikubaliana mwisho ni laki 5 na alikuwa akitaka kodi ya miezi 6.
Nilimpigia tena simu Jane kuumpa mrejesho na alisema kesho tutamaliza ili naye aione frem, niliagana na dalali kwa makubaliano ya kukutana kesho tena kwaajili ya kulipia na kuandikishana mkataba.
Kipindi niko njiani nilimpigia simu Dullah ili tuonane na alisema niende Makumbusho stand ili nikalione na goli lake la chakula. Baada ya kuongea na Dullah, nilipigiwa simu na mzee Juma kupitia whatsapp na alinipa taarifa nionane na binti yake Cami, na alisema kuna maelekezo ya kunipa. Baada ya kuagana na mzee sikuchelewa nikampandia hewani Cami na tukakubaliana tuonane kesho jioni kwaajili ya kufanya maongezi.
Nilitumia kama lisaa mpaka nawasili Makumbusho na nilikwenda kuonana na Dullah maana alinielekeza ofisi yake ilipo. Nilikwenda straight mpaka kwenye goli lake na yeye ndo alikuwa anasimamia, tuliishia kusalimiana, na nikaagiza msosi;
MIMI: “Senior hongera sana, na imekuaje upo hapa na sio Sinza?”
DULLAH: “Baada ya kupata hapa kule nikaachana nako.”
MIMI: “Hapa umetisha huwezi kosa hela movement ya watu ni kubwa sana.”
DULLAH: “Namshukuru sana Allah, kama hivi mapambano yanaendelea taratibu.”
MIMI: “Biashara ya Uber ndo umeacha kabisa?”
DULLAH: “Naachaje biashara iliyonitoa? Nimepa mtu wa mkataba aniletee hesabu, vipi wewe gari yako ushapata mtu?.”
MIMI: “Tayari mzee baba, Sasa nimekuja tuongee jambo bro! Unipe ushauri ndugu yako maana sielewi.”
DULLAH: “Shida nini bro?”
MIMI: “Kaka nimemtia mimba mhabeshi na mimba inakwenda mwezi wa nne sasa, navyozungumza na wewe hapa huko kwao wamemind sana na wanataka mimi niende huko.”
DULLAH: “Nilijua tu lazima hili litokee lilikuwa ni suala la muda tu, wazazi wake wapo sahihi hasa kwa mila na desturi za kiafrica ni lazima ungehitajika wakufahamu na uwape assurance ya ndoa kwa binti yao.”
MIMI: “Kaka unajua kabisa nina mke tayari na hii mimba alibeba kwa interest zake bila kunishirikisha.”
DULLAH: “Kaka tambua hio damu ni yako lazima uilinde kwa namna yoyote na ukileta masikhara utamkosa mtoto. Hao watu wa Ethiopia wana ubaguzi sana, shukuru Mungu dada anakupenda, hawa watu wanapenda kuoana wao kwa wao.”
MIMI: “Sasa kaka unanishauri nini?”
DULLAH: “Bro! Mistake zinatokea ni kawaida kwa wanaume hata usijilaumu sana, Mama J bado hujamuoa na huyu tunapambana tupate damu yetu, wewe nenda Ethiopia, uzuri ulishaenda before, sahivi haiwezi kuwa shida wewe nenda, usipokwenda wataona ni dharau na mtoto unaweza mkosa.”
MIMI: “Kaka ndo ushauri gani huu? Yaani niende nijipeleke? Sina kampani yoyote yakwenda nayo mpaka sasa, na kumuoa haiwezekani.”
DULLAH: “Kaka kama kweli unamtaka uyo mtoto fanya hivo kabla hawajafanya maamuzi magumu juu ya mtoto, hawashindwi kufanya jambo baya kwa mtoto na wewe sio kabila lao, hawana cha kupoteza. Labda nikuulize swali, unataka mtoto au laah?.”
MIMI: “Bro swali gani hilo, nataka mtoto.”
DULLAH: “Kama kweli unataka mtoto nenda huko Ethiopia, masula ya ndoa unaweza kuwaambia bado mnajadiliana na mama mtoto, kitendo cha kwenda ni busara tosha, ndoa ni majaliwa.”
MIMI: “Senior sio rahisi kama unavyozungumza hapa, mambo sio simple hivyo.”
DULLAH: “Unaweza kubadili dini ukawa muislam na ukaoa wote wawili bila shida.”
MIMI: “Hapo nitakuwa nimebadili dini kwaajili ya kuoa na sio kutoka moyoni.”
DULLAH: “Bro jambo lako ni gumu sana, niachie niendelee kutafuta options na nitakupa mrejesho soon.”
Tuliendelea kuongea masuala mengine kuhusu harusi yake na kubwa ilikuwa ni maandalizi na yeye kwa upande wake alisema mambo si mabaya na anahitaji sana sapoti yangu.
Nilishinda na Dullah mpaka jioni, kwa upande mwingine alikuwa amenipa hamasa ya mimi kuanzisha biashara zangu na nilimpongeza sana kwa maamuzi na hatua aliyokuwa ameichukua. Muda ulikuwa umekwenda sana maana giza lilikuwa limeanza kuingia tayari na niliondoka kurudi home mapema.
Usiku nikiwa home Ghati alinipigia simu na habari kubwa aliomba nimkopeshe kiasi cha pesa sababu alipata short kazini na alihitaji pesa before mwisho wa mwezi. Kiasi alichohitaji ni million 7 na alisema atarudisha ndani ya wiki 2 na anaweka bond gari yake mpaka atakapo rejesha hicho kiasi. Niliwaza na kuwazua kwa haraka nikaona nimpe, afu niendelee kuitumia Crown yake, hivyo nilimwambia nitampa hiko kiasi kesho.
Wife alikuwa bado kaninunia kuhusu suala la jana kuhusu Prisca na nilijitahidi sana kumuelewesha bila mafanikio maana hakutaka kunielewa. Prisca sikumtafuta kabisa niliona ni bora nikamwacha ila nichukue hatua madhubuti za kumweka mbali zaidi na mimi.
Asubuhi baada ya kuamka nilikutana na missed 2 za Jane na missed call za Dalali, hivyo nilianza kwanza kumpigia Jane na tukakubaliana tuonane Bahari Beach, kisha nikampigia dalali kumpa taarifa tuonane saa 4 asubuhi.
Saa 4 ontime nilimiti na Jane eneo la tukio na baada ya kuliangalia frem pamoja na mazingira yake yote, kwa upande wake alilipenda na akasema tufanye malipo haraka ili process zingine ziendelee.
Kufikia saa 8 mchana tulikuwa tumekamilisha malipo pamoja na kuandikishiana mkataba wa pango na nilitafuta fundi wa kudesign shelves mle ndani. Jane mipango yake ilikuwa kufikia february lazima awe ameanza biashara ndomana alikuwa anataka kuona mambo yakienda haraka.
Tulimwacha fundi akiendelea na vipimo, na tuliondoka kwenda kupata lunch pale budget, mimi ndo nilikuwa nimetangulia mbele, na Jane alikuwa akinifuata kwa nyuma. Baada ya kupark gari nilimsubiri Jane apark gari yake maana alikuwa bado ana ulena.
Tuliongozana kuingia ndani na nilishangaa kumuona Mary amekaa akitusubiri na alikuwa akituangalia wakati tunaingia. Ofcourse kwa upande wangu sikutegemea kama ningeonana na Mary muda huu maana ilikuwa ni surprise kwakweli.
Baada ya kukaa nilimwangalia kwanza Jane then nikamgeukia Mary, na alionekana kuwa mrembo zaidi, ilikuwa ni muda umepita bila kuonana,
MIMI: “Mary mambo, nimekumiss kipenzi changu na nimefurahi kukuona.”
Mary alionesha tabasamu,
MARY: “Thank you Insider, nimekumiss pia ni muda mrefu hatuja onana leo ni kama surprise sikutegemea ningekuona.”
Muda huu mhudumu alikuwa ameshafika kutusikiliza na kila mmoja aliagiza chakula anachotaka kula;
JANE: “You guys narudi soon ngoja niende kwenye gari nikambadilishe pampas mtoto.”
Nilijua Jane kafanya makusudi ili atupe nafasi ya kuongea,
MIMI: “Naona umezidi kuwa mrembo sana.”
MARY: “Mimi naona niko vilevile mbona, sema hatujaonana muda ndomana.”
MIMI: “Unajua kwa muda mrefu nimekuwa mtu wa kujuta sana juu yako, leo imekuwa bahati tumeonana naomba nikwambie ukweli. Najua nimekukosea sana naomba nisamehe tuanze page mpya, na utambue wewe ni moja ya wanawake muhimu sana kwangu.”
MARY: “Insider mimi nilishakusamehe muda mrefu na sina kinyongo na wewe, hata mimi niliplan siku nikutafute tuyamalize, nashukuru Mungu leo tumekutana hapa.”
MIMI: “Really?”
MARY: “Nilikaa chini nikaona naweza kukublame kumbe kweli unakuwa kwenye majukumu ya kutafuta riziki. Unajua wewe Insider una mke na mtoto na pengine una watu wengine wa karibu ambao wanakutegemea, mimi bado nakaa home bado sijajua nini maana ya maisha.”
MIMI: “Wakati wako utafika tu, na mimi nakuombea kwa Mungu upate mwanaume bora ambaye atakujali na kukuheshimu na sio kukuchezea.”
Jane aliingia na baada ya kutuona tunapiga story alifurahi sana na alianza kuongea,
JANE: “Nimefurahi sana kuwaona vipenzi vyangu mkicheka kwa mara nyingine, nilikuwa nawish sana mrudi kama zamani.”
MARY: “Usijali dada Mary tumeyamaliza tayari.”
Chakula kililetwa na tukaanza kula huku story zimetawala juu yetu na kila mtu alionesha kuwa na furaha sana. Muda huu simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ni Ghati alikuwa akipiga simu, ndo kukumbuka nina miadi naye maana muda ulikuwa unasoma saa 9 mchana.
Baada ya kumaliza kula nilimpigia simu ili nijue tunakutana wapi na alisema niende ofisini kwake, ili akanioneshe na products zao, before aliniambia anafanyia kazi kampuni inayodeal na masuala ya internal controls technology.
Sikuona umuhimu wa kuendelea kubaki na kina Jane na niliwaaga pale na nilimpa Mary ishara ya kumcheki kwa simu bila Jane kujua na nikaondoka kwenda Victoria kuonana na Ghati. Ulikuwa ni mwendo wa dakika 40 mpaka nawasili Victoria na nilikwenda straight kwenye ofisi yake, alikuwa kashanielekeza toka niko njiani.
Baada ya kufika kwenye ofisi yake nilikaa reception nikimsubiri na alitumia kama dakika 10 kuja kuniona, tulisalimiana na tukaendelea na mazungumzo;
“Insider karibu sana bossy wangu, hii ndo ofisi yetu.”
“Ahsante sana inabidi nizione na products zenu ikitokea kazi niwe nakupa.”
“Nashukuru, naona umetembea na gari, hii utaondoka nayo vipi?.”
“Siondoki na gari yako mama, mimi nakuamini cha muhimu ni uaminifu tu maana hizi pesa nazokupa ni za ofisi pia.”
“Ahsante sana, nilipata mtu wa kunikopesha haraka ila kwa riba, sema ndo ana riba kubwa sana.”
“Pole matatizo kila mtu anapitia, usiwe na wasiwasi mama, leo kwako kesho kwangu.”
“Inabidi nikufahamu kwako, wewe kwangu unakujua.”
“Sawa haina shida karibu sana.”
Tulikwenda kuziona products zao na nilitokea kuvutiwa nazo na nikaona kuna umuhimu wa baadhi ya controls kuziweka ofisini kwetu. Tuliongea mambo mengi sana na alizidi kubold suala la kuja kwangu na mimi nilimwambia muda wowote akiwa tayari aniambie.
Nilitumia kama dakika 40 na nikaondoka, lakini nilipata wazo la kupitia Mikocheni ofisini ili nikaangalie na maendeleo. Lucy hakuwepo na alikuwa amekwenda chuo na baada ya kufanya naye mawasiliano alinambia kuna barua yangu ililetwa na Landlord na alisahau kunipa taarifa.
Barua ilikuwa mezani na nilianza kuisoma pale na habari mbaya barua ilikuwa inasema tunapewa miezi 3 ya kutafuta eneo lingine la biashara sababu nyumba inauzwa.
Zilikuwa ni taarifa mbaya ambazo zilinishtua na nilifanya maamuzi ya kumpigia simu Landlord ili tuongee vizuri. Nilifanikiwa kufanya naye mazungumzo na nilimuomba anipe muda wa siku 3 ili niongee na wahusika ikiwezekana tununue sisi.
Iryn alikuwa anakuja ijumaa kutokea Ethiopia, hivyo niliona ni busara kuongea naye pindi atakapokuja Dar, kuhusu bei ya kuuza jamaa alisema tukiwa tayari ndo tutaongea kuhusu hilo.
Niliwasiliana na Cami ili tuonane kwaajili ya maagizo ya kutoka kwa Mzee, lakini alisema tuonane kesho ambayo ni ijumaa. Kwa upande wangu ilikuwa ngumu kuonana sababu ya Iryn alikuwa anakuja na nilimwambia tuonane jumapili.
Usiku niliwasiliana na Iryn akasema atawahi kuja Dar na alinisisitiza sana niwahi kwenda mapema kumpokea. Pia nilimpanga wife kuwa ninakwenda Zanzibar kufuatilia mzigo na nitarudi jumapili, lakini hakunijibu na alionesha kuwa I don’t care.
****
Asubuhi nilifanya mawasiliano na Iryn ili anipe taarifa za muda wa kuwasili Dar niandae mazingira mapema na baada ya kuwasiliana, alinambia saa 7 mchana atakuwa amefika, niwe around pale JNIA.
Niliondoka home kwenda Masaki ofisini ili nikaangalie na maendeleo ya Nollie mfanyakazi mpya pamoja na kuanda taarifa zake kwenda bank na NSSF.
Baada ya kuwasili pale ofisini Nollie alikuwa pale reception na nilikwenda nikamsalimia japo alionekana kuwa sio muongeaji na nilimwacha nikaingia ofisini kuonana na Hilda.
Pengo la Asmah lilikuwa limezibwa tayari na Hilda maana alikuwa yuko sharp sana kwenye kutuma ripoti na usimamizi wa pale ofisini ulikuwa mzuri. Nilimuuliza maendeleo ya Nollie akanambia anaendelea vizuri na ni quick learner, na mimi nikandelea na majukumu yangu.
Mchana mida ya saa 6 nilimuaga Hilda na nikaondoka kwenda Airport kumpokea Iryn, barabarani kulikuwa na foleni sana hii siku, kwanza kulikuwa na msafara, pili barabara inatengenezwa hilo foleni ni balaa.
Nilitumia masaa mawili na madakika kufika pale JNIA terminal 3, kwa upande wa Iryn alikuwa amewasili tangu saa 7 mchana na alikuwa amekaa cafe akinisubiri. Baada ya kuingia ndani na kumuona, nilimsalimia kwa kumkiss mdomoni pamoja na kumpa pole ya safari na nikaanza kumuuliza maendeleo yake kwa ujumla.
Baada ya kumaliza kunywa juice yake sikuona sababu ya kupoteza muda hivyo nilimwambia tuondoke ili tukaendelee na maongezi yetu hotelini. Kwa upande wake alionekana kuchoka sana hata tumbo lilikuwa linazidi kuonekana kubwa.
Iryn alizidi kuonekana kuwa mrembo zaidi maana alizidi kung’aa kama almasi na aliteka sana attention za watu pale airport maana macho yote yalikuwa kwake na mimi nilikuwa nikimsifia jinsi alivyokuwa mrembo, na yeye aliishia kutabasamu tu.
Tulivyofika parking nilishtuka kuona akiniuliza kuwa gari nayotumia ni ya Sumaiya? Nilijiuliza inamaana Sumaiya kashamwambia Iryn kuwa natumia gari yake?,
MIMI: “Yes baby ni ya kwake, ameshakupa taarifa kuwa natumia gari yake?”
IRYN: “Sumaiya ana siri? Ameniambia umemsaidia kupata gari na unaitumia wewe, kwani gari yako iko wapi mpaka unatumia ya Sumaiya.?”
MIMI: “Sina gari ya kutumia kwasasa unataka kuninunulia?”
IRYN: “Unataka gari gani?”
MIMI: Gari nzuri kama wewe mke wangu.”
Bhasi, aliniangalia afu akanyamaza kimya na mimi nikaendelea kukimbiza gari kwenda Serena Hotel. Hii ni moja ya hotel yake pendwa pamoja na Coral hotel na hafikiagi hoteli nyingine zaidi ya hizi mbili.
Baada ya kuwasili pale hotelini tulipokelewa mabag na tulikwenda kwanza restaurant kupata chakula maana alikuwa analalamika anasikia njaa.
Muda ambao tuko restaurant tukipata chakula tulianza maongezi kuhusu huko Ethiopia maana nilikuwa na shauku kubwa sana ya kujua kinachoendelea. Kwa upande wangu sikutaka kuona Iryn akiteseka kuhusu hili suala na moja ya maamuzi niliyoamua ni kufanya kila litakalowezekana kuhakikisha yeye na mtoto wanakuwa salama.
MIMI: “Mummy nafikiri tuendelee na maongezi yetu wakati tunakula ili tukifika room nikuache upumzike.”
IRYN: “Hili jambo nimekuwa nalitafakari toka niko kwa ndege, lakini sioni future ya hii mimba.”
MIMI: “Unamaanisha nini kusema hivi?.”
IRYN: “Sometimes huwa najuta kwa maamuzi niliyoyachukua, you was right nilikuwa naendeshwa na hisia na sio akili.”
MIMI: “Jambo ulilofanya ni la kheri ndomana huoni nakulaumu kwa haya maamuzi uliyoyachukua, ndomana nilikwambia waambie bahati mbaya ilitokea.”
IRYN: “Baby, unajua nimesemwa sana kikao cha 2hrs kilikuwa moto sana, kila mtu alikuwa against mimi kasoro bibi tu ndo alikuwa akinitetea.”
MIMI: “Mpaka Jimmy alikuwa against na wewe.?
IRYN: “Hapana, Jimmy hata nguvu ya kuongea alikuwa anaitolea wapi? Hata yeye aliwekwa kati na ameambiwa ahakikishe anamuoa Amara na aache uhuni. Kwanza yeye ndo wanamlaumu kwamba ndo amesababisha na mimi nimeiga tabia zake za umalaya mpaka nikapata mimba.”
MIMI: “Nina wasiwasi utakuwa ulishindwa kujielezea mummy, maana kwa jinsi wanavyo kutreat huko napata wasiwasi.”
IRYN: “Baby, hayo yote nimewaeleza lakini wanapata ukakasi kuwa hii mimba ni planned nasio bahati mbaya maana mimi ni mtu mzima na nina elimu.”
MIMI: “Tuachane na hayo, wanatakaje?”
IRYN: “Wanataka uende Ethiopia haraka iwezekanavyo, najua ni suala gumu kwako lakini kwa usalama wangu na mtoto you have to go.”
MIMI: “Wanataka assurance ya ndoa wala sio kitu kingine hata usizunguke.”
IRYN: “Ishu ni kunitengenezea mazingira mazuri na familia yangu hata wakati wa kujifungua niende huko, ile ndo familia yangu. Unajua fika siwezi kujifungulia South, mamdogo wangu hawezi kuwa na upendo na mimi kama nikienda Ethiopia kwa mamkubwa.”
MIMI: “ Naelewa, niachie hili suala nijifikirie maana linahitaji busara na sio kukurupuka.”
IRYN: “Haina shida mpaka namaliza mitihani utakuwa ushafanya maamuzi.”
Baada ya kupata lunch tulikwenda room kupumzika na alionekana kuchoka sana hata baada ya kuingia room aliishia kujitupia kitandani na aliniomba tulale wote.
Saa 2 usiku baada ya kuamka Iryn hakuwepo kitandani na hakuonekana maeneo ya room, lakini kwa mbali nilimsikia akiongea na simu na amesimama upande wa balcon. Baada ya kumuona akiongea na simu niliendelea kulala pale kitandaani maana nilikuwa bado nina maluweluwe ya usingizi. Ilipita nusu saa lakini bado anaongea na simu, ilibidi nimfuate hukohuko maana nilipatwa na kawivu jinsi alivyokuwa anachukua muda mrefu kuongea na simu, nilipatwa na wasiwasi.
Nilisogea mpaka usawa wake na nikamuuliza kwanini anatumia muda mrefu sana kuongea na simu? na anaongea na nani?, matokeo yake hakunijibu na akaendelea kuongea na muda huu alibadilisha lugha akaanza kuongea kifrench.
Nilipatwa na hasira kuona namuuliza afu hanijibu na anabadilisha lugha, palepale nilimvuta kwa nguvu kuja usawa wangu,
“Nakuuliza unaongea na nani afu unanyamaza kimya huoni ni dharau hizi?”
“Insider mbona unakuwa na mambo ya kitoto sana?.”
“Mimi nina mambo ya kitoto?”
Nilimtia kibao cha nguvu kwenye shavu lake la kushoto ‘’PAAAH!” mpaka simu yake ikandoka chini, hasira zikaanza kumpanda na machozi yalianza kumtoka.
“Insider wewe ndo wa kunipiga namna hii? Ni kosa gani nimekufanyia?”
Mimi nilinyamaza kimya, ofcourse nilikuwa nimezingua kwakweli na hii siku ndo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumpiga Iryn na nilianza kujiona mjinga kwa jambo nililofanya.
“Nipe simu yako.”
“I can’t and don’t ever touch me again.”
Nilimkamata kwa nguvu na nikamnyang’anya simu, mtoto laini yule asingeweza kunisumbua kabisa. Uzuri Passcode za simu yake nazijua, hivyo haikuwa shida kwangu kutimiza lengo langu, na baada ya kuangalia nilibaini alikuwa akiongea na Grizzman na hapa ndo nikapandwa na hasira tena.
“Malaya mkubwa wewe kumbe unaongea na bwana wako Grizz kwa muda mrefu, ni wewe ambaye ulisema hauna contact naye na huyu ni nani sasa?”
Kwa upande wake hakuwa akitoa majibu bali aliendelea kulia na nilimsogelea maana alikuwa amekaa kitandani,
“Si naongea na wewe au unataka nikupe vibao vingine ili uongee?”
“Insider naomba niache please, ushanipiga na kuniita malaya juu, sasa kuna haja gani ya kuongea na mwanaume katili kama wewe?”
“Malaya mkubwa wewe hata huyo mtoto na wasiwasi itabidi tupime DNA sina imani na wewe kabisa.”
Actually nilikuwa nina hasira sana yaani nilitamani nimtie vibao vingine, nikaona italeta shida pale hotelini, nikampotezea. Kwa upande
wake alivaa gauni akatoka mle chumbani na aliniachia simu yake maana ana simu mbili. Sikutaka kuendelea kuikagua ile simu sababu niliona naweza kukutana na mambo mengine ya ajabu afu nikamfanya kitu mbaya ukizingatia ni mjamzito.
Muda huu nilikuwa kwenye mawazo kutokana na jambo lililotokea, kuna Roho ilikuwa inanambia nilichofanya nimekosea na Roho nyingine ikawa inanambia niko sahihi, kwani sometimes wanawake wanahitaji surprise kama hizi ili wasijisahau.
“Iryn atakuwa kwenye mahusiano na Grizz? Hata huko Ufaransa anakokwenda nina wasiwasi huwa wanakutana. Kwanini baada ya kuniona akaswitch lugha na kuanza kutumia french? Maana yake hakutaka nijue wanachozungumza, hapa kuna something fishy kinaendelea.”
Baada ya kupita dakika 30 nilipata wazo nimuangalie Iryn restaurant, lakini hakuwepo na nilishuka reception nikamuuliza dada akanambia alimuona amekaa pale reception na akaondoka.
Nikajiuliza sasa huyu mwanamke atakuwa amekwenda wapi? Nilitoka pale nje nikamuona mlinzi amesimama sehemu ya kupakia na kushushia customers na baada ya kumuuliza alisema ametoka na uber nyeupe, dakika 20 zimepita tayari.
Nilimpigia simu kwa whatsapp haikuwa hewani na niliona kuna haja ya kumtafuta maana anaweza fanya jambo baya kwa hasira zake. Niliwaza huenda atakuwa amekwenda kutulia sehemu na mawazo yangu ya haraka nilihisi atakuwa amekwenda Cocobeach, Karambezi, Capetown, Coral na kama nitamkosa bhasi atakuwa amekwenda kwa mama Janeth au kwa Claire, niliwaza nikipita humu lazima nimpate.
Nilitoka nje barabarani “Ohio road” na nilifanikiwa kupata bodaboda na haraka tukaanza safari ya kwenda Cocobeach kumtafuta.
Ndani ya muda mfupi sana tuliwasili pale Coco na nilimuomba dereva anisubiri ili kama nitamkosa twende sehemu nyingine. Boda alikuwa na wasiwasi labda nataka kumtapeli pesa yake maana alitaka tulipane kabisa. Kwa upande wangu sikuwa na cash kabisa zaidi ya Tigopesa, lakini nilimtoa wasiwasi na akakubali.
Nilikwenda kumuangalia pale kwa sikuzote ambako huwa tunakaa lakini hakuwepo na nilimuuliza jamaa akasema hajamuona. Tukaondoka kwenda Karambezi cafe na pale hakuwepo pia, tukaenda Coral beach hotel nako hakuwepo, tukaenda Capetown nako hakuwepo.
Nikawa nimebaki na option 2 ya kwenda kwa Claire na kwa mama Janeth, niliona nianze kwanza kwenda kwa Claire then kama nitamkosa ndo nifanye utaratibu wa kwenda kwa mama kumcheki.
Sikumwambia Claire kama nakwenda kwake, baada ya kuwasili pale Marina apartments nilimpigia simu kuwa nakuja kumsalimia na yeye alinikaribisha akasema yupo. Baada ya kuonana na Claire nilimuuliza kama Iryn yuko pale kwake na akasema hajakwenda na hajui kama yuko Dar, nilimbana sana lakini aninisisitiza na kunihakikishia kuwa Iryn hayupo kwake;
MIMI: “Claire una uhakik hayupo hapa? niambie ili niondoke kesho nimfuate, kwa hali yake afu na mazingira aliyoondoka pale hotelini inanipa wasiwasi.”
CLAIRE: “Shem, trust me Iryn hajaja hapa hata nisingetaka uhangaike. Ni nini kimetokea mpaka ameondoka? Usije ukawa umeshampiga matukio best yangu.”
MIMI: “Ni tofauti za kawaida zimetokea na ni jambo la kawaida kwenye mahusiano, acha nikuache see you.”
CLAIRE: “Wait twende wote tutamtafute naamini yuko somewhere.”
MIMI: “Haina haja wewe endelea na mambo yako,afu usiku sahivi nikimpata nitakwambia.”
Claire hakufurahishwa na maamuzi yangu lakini hakuwa na jinsi, nilimuaga nikaondoka maeneo yale, na baada ya kushuka chini nilitoa simu nikampigia mlinzi wa mama Janeth pale home na alisema hajamuona Iryn akiingia na kama atamwona atanambia.
Bodaboda kwa upande wake uvumilivu ulimshinda na aliniuliza ni nini kinaendelea? Maana tunazunguka sana mpaka anaanza kuwa na wasiwasi na usalama wake. Nilimpa mkanda mzima na yeye alishauri turudi tena tukimungalia sehemu tulizotoka huenda tulipishana njiani.
Tuliamua kuanza upya tena kumtafuta na kipindi hiki nilipita maeneo yote ya starehe kwa Masaki lakini hakuonekana na niliamua kurudi hotelini, niliwaza huenda atakuwa karudi.
Baada ya kuwasili hotelini kwa bahati mbaya sikumkuta na hapa sasa nikaanza kuwa na wasiwasi, na swali langu kubwa Iryn kaenda wapi? Ukimcheki whatsapp hapatikani.
Nilikaa kama nusu saa hivi nikisubiria kama kutakuwa na muujiza wowote lakini ilikuwa tofauti na hapo saa inaonesha ni saa 5 za usiku. Kuendelea kukaa hotelini niliona si sawa ni bora nitoke niende maeneo mengine kumtafuta na wazo langu kichwani niende Hyatt na Johari hotel.
Nilibadilika chap nikachukua funguo ya gari na nikatoka kwenda parking na nilimpigia simu Lucy maana niliwaza huenda akawa naye, hata baada ya kuwasiliana na Lucy alisema hawajawasiliana na hajui kama yuko Dar.
Niliwasha gari na nikaanza safari ya kwenda Hyatt na nilikwenda pale Level 8 lakini sikumwona na nikakata tamaa kabisa, niliwaza nimuache atarudi hotelini mwenyewe ila wasiwasi wangu ni ujauzito wake na kuwa mazingira ya nje usiku, ukizingatia na urembo wake niliona wahuni wanaweza wasimuache salama.
Sikuwa na option nyingine maana maeneo yote anayopenda kwenda au kwenda kote hakuwepo na nilipata wazo la kwenda Mlimani city na nikafanya mawasiliano na Bob ili tuoane pale Samakisamaki.
Niliendesha gari kwa kasi sana na wakati nipo Vodacom HQ simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ni wife alikuwa akipiga, ilibidi niingize gari pale Oryx kituo cha mafuta li tuongee maana nilijua atakuwa anauliza kama nimefika au laah!.
Muda huu simu ilikuwa imeita mpaka imekata na nilimpigia simu kwa haraka sana na haikuchukua muda alipokea,
“Nambie mke wangu unaendeleaje?”
“Hujanambia kama umefika salama.”
“Nimefika salama sema mambo mengi ila ningekuambia mke wangu.”
“Iryn amekuja home kutusalimia na yuko sebleni anacheza na Junior.”
Nilishtuka sana kupewa hizi taarifa na wife na nilijiuliza amekwenda kufanya nini home na lile tumbo lake?, kwanza sikuwa na wazo kwamba atakwenda home na nilianza kuingiwa na wasiwasi, na jasho lilianza kunitoka…”
Absolutely [emoji817]. Ana utoto mwingi sana huyu kijana af anajiona yuko sawa tuu.INSIDER MAN you need to differentiate the way you handle local girls and the woman whom you entirely depend on for living.
LalaMuendelezo vipi
Kesi ndogo sana hii mimi wife alitumiwa picha nimelala na kichanga pembeni..huo msala nilipambana nao na kuumaliza mimi mwenyewe bila kuhusisha watuSEASON 02: