Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mfano wewe ndio ungekua dada yake mwandishi; kwa situation aliokua nayo kaka yako UNGEFANYAJE?
Hakuna dada anayeweza mkataa kaka, atalamika mwisho wa siku atanyamaza. Dada insider alisema, Jamaa kazingua ila hawezi mkataa mtoto sababu ni damu yao.

Usicheze na ndugu asee, unaweza pendwa na wifi zako afu wakakutaa mwishoni.

Dada alikuwa sahihi kumpa kampani Iryn.
 
Dada yuko sahihi asee, mtoto ni Damu yao. Kuhusu mme wa dada hawezi kuingilia mambo ya ndugu, inaonesha Insider na dada yake wanabond nzuri sana, tena ya kusaidiana kwenye shida na raha.

Ulitaka dada amkatae kaka kisa mama J? Hakuna dada wa aina hii aseee
 
🙄🙄🙄 mama j anatoka..?
 
Asingeandika kabisa hiko kipande, acha tuone
Hata kwa Irene alikuwa anaandika hivyo hovyo episode ijayo utasikia simu alikuwa anachatia mdogo wake na mpenzi wake. Hawezi kukubali kama mama J anacheat itakuwa ni udhaifu atachekwa mno na haters wake humu.
Episode ijayo utaona eidha alikuwa anaongea na rafiki yake au ndugu wa kike na ndio walikuwa wanatoka out wote ngoja tusubiri tuone.
 
Sijasema amkatae kaka kisa mama J i said angemsapoti kulea damu yake but asingekuwa involved kiasi cha kwenda kumlea uzazi Irene kwani hana ndugu zake hadi aende??

Kweli mume hawezi kuingilia mambo ya ndugu lakini je wewe ungekuwa mume ungemfikiria vipi huyo dada anayeenda kulea mchepuko wa mdogo wake??
 
Dada anaenda kwaajili ya mtoto na sio mchepuko. Hatuwezi sema Iryn ni mchepuko sababu bado hajaoa. Naamini Hata dada yako angefanya hivyo, hata mama yako angefanya.
 
Dada yuko kwenye wakati mgumu sana, mwisho wa siku damu ni nzito kuliko maji. Na hii ndo maana ya ndugu wa shida na Raha.
 
Ndugu zake si ndio hao walioendekeza mila wakataka mimba itolewe? dada yupo sahihi kulingana na situation iliyotokea maana ni almost wamkose mtoto
 
Kabisa yaani am sure hii mimba angekuwa nayo Asmah dada mtu wala asingehangaika nae na angemshauri kabisa Insider ajitahidi kuficha mama J asijue. Wadada tutafuteni hela jamani mawifi wakunyenyekee.
Hivi nyie story mnaisoma vizuri kweli? Si kuna mwanamke mwingine Insider alipitaga nae na mama Jr alijua na mgogoro hu ulitatuliwa na huyu huyu sister? Someni story mkiwa na positive mind, msisome mkiwa tayari mna majibu yenu kichwani au chuki or mapenzi kwa mtu. Kule volume 1, kuna watu walikua tayari wana team, yaani team mama J na team Iryn, sijui walikua wanawake or wanaume. Hi story according to mwandishi ni matukio ya nyuma, yaliisha pita, we are not sure kama bado wanaendelea na boss lady or not though ile Benz aliopewa kama zawadi it sound bado anayo, kaulizia spear hapo juu. Tuburudike, tujifunze. Ningekua bado kijana ningeokota madini mengi sana humu, mojawapo ni hi, "Uaminifu ni MTAJI" pia jifunze kusamehe waliokukosea, ukiwa na chuki kwa waliokukosea ni kama kujiadhibu mwenyewe, check tukio la mama wawili but mwamba kaenda kwa mama wawili, kamchukua Pili na katoka nae out na zawadi kamnunulia kama alivo ahidi, sasa hvi deni na gilt imebaki kwa mama wawili. Ukijikita kwenye mapenzi tu; hutapata kitu cha kujifunza.
 
Umeandika episode ndefu ya kukidhi haja ya moyo. Hongera sana ndugu mwandishi, sikudai...
 
Kwenye kuchambua story kila mtu ana namna yake wewe umeichambua positive mimi nimeielewa kwa namna nyingine negative, after all kila mtu ana uhuru wa kuweka maoni yake kutokana na uelewa wake mimi sijamuelewa dada mtu, kuna wengine hawajamwelewa Irene, Mary nk.
Nadhani kila mtu achambue anavyoona yeye
 
HII STORY NI YA UKWELI KABISA INGEKUWA NI YA UONGO TAYARI INSIDER MAN ANGEKUWA AMESHAJICHANGANYA. NA LAZIMA MJUE KWAMBA KILA MTU ANA KUSUDI LAKE HAPA DUNIANI. MWENYEZI MUNGU KAMBARIKI JAMAA KWA VITU VINGI TU. UAMINIFU, UCHAPAKAZI, AKILI, MOYO WA HURUMA NA KUWAJALI WENGINE BILA KUSAHAU JAMAA ANA UPENDO. HII SIMULIZI IWE CHACHU KWA VIJANA WENGINE KUBADILIKA KIFIKRA,KIMAWAZO NA KIMTAZAMO.
TUNAONA VILE INSIDER MAN ANAWAVUA SANA WADADA NA ANAMSALITI MPAKA MAMA JR NA HUO NDIO UHALISIA WA MAISHA YETU WANADAMU. trudie , cocochanel PUNGUZENI KUHUKUMU. HII SIMULIZI SIO KWAMBA INABURUDISHA TU PIA INAFUNDISHA WATU . MAANA MPAKA X HUKO WANATANGAZIANA KUHUSU HII SIMULIZI. INSIDER MAN UMEBARIKIWA SANA MKUU CRITICISM ZA WATU WASIOJIELEWA ACHANA NAZO, ENDELEA KUTULETEA SIMULIZI YAKO.
 
Na wanawake huwa wanajua kulipiza vibaya hatari. Hapo maji utaita mma.
Kuna jamaa mmoja alioa na kazaa na mkewe watoto 3 ila jamaa alikuwa kicheche kama Insider hivi.
Mke wake alikuwa mzuri mpole, ila sasa yule mwanamke alivyochoka na mauzauza ya jamaa, alimbwaga mazima. Sasa hivi huyo mama kaolewa na mzungu kabisa jamaa hadi leo anajuta.
Wanawake huwa wanavumilia sana ila wakichoka malipizo yake ni balaa nyengine
 
Tatizo la waja wanataka tufanane mawazo, stori ukishaiweka public jiandae kwa positive na negative critism so far hata INSIDER MAN mwenyewe anajua kuna pande mbili za maoni na mpaka leo anazipokea zote bila kuchukia wala kulalamika. Refer waleta story wengine ukienda kinyume na wanachotaka kusikia wao huwa wanazira kabisa ila its been a year bado anaileta tena kwa uhalisia wake bila kuwaplease baadhi ya watu.

So sio kwamba tunahukumu bali tunatoa maoni kutokana na tulivyoelewa sisi kamwe wote hatuwezi kuwa na maoni yanatofanana sometime angle yako unaweza kuona ni namba 9 ila mimi naona ni namba 6 ila wote tukawa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…