SEASON 02
CHAPTER 34
“BY INSIDERMAN”
PREVIOUS:
Wakati tukiendelea na maongezi, nilimuona Iryn akija mahali tulipokuwa na alikuwa amependeza sana. Sister alimuona na alianza kumuangalia kwa makini, kwani alihisi kwamba ndiye Iryn. Iryn, baada ya kutufikia, alianza kumwangalia sister kwa umakini. Sister aliamua kusimama, na wakaanza kuangaliana kwa kimya, bila hata mmoja kuzungumza na mwingine.
CONTINUE:
Sister alibadili mwelekeo wa macho yake, akalenga macho yake kwenye tumbo la Iryn kwa umakini mkubwa. Ilikuwa kama haamini kile anachokiona sasa hivi.
Iryn ndiyo alikuwa wakwanza kuongea pale;
IRYN: “Hi wifi.”
SISTER: “Iryn, ni vizuri kuona umerejea salama, lakini ulituacha na wasiwasi mkubwa. Kwanini ulikuwa hupatikani, hasa ukiwa katika hali kama hii?.” Na alimpa ishara ya kuketi.
IRYN: “Nisamehe sana wifi, nilikuwa katika kipindi kigumu sana, na nilihisi kama natakiwa kujitenga kwa muda, nilihitaji muda wa kutafakari mambo.”
SISTER: “Umejua jinsi tulivyokuwa na wasiwasi? Tulikuwa na hofu kubwa kwa sababu ya hali yako, ilitubidi kuja Afrika Kusini kukutafuta!"
IRYN: “Naelewa kabisa, na najuta kwa kile kilichotokea. Hivi sasa, nipo tayari kuelezea kila kitu na ninaomba msamaha kwa maumivu yote niliyowasababishia."
SISTER: “Tunakupenda na tunakujali, hatuwezi kukaa kimya wakati hatujui ulipo na hali yako."
IRYN: “Nashukuru sana kwa juhudi zenu, sikutaka kuwafanya mtaabike. Nilikuwa nikihangaika na mambo mengi, lakini sasa najua kuwa nilikosea kutowasiliana nanyi.”
SISTER: “Tuna furaha kwamba umerejea salama, lakini tafadhali, usitufanye tena kuwa na hofu kama hii. Siku nyingine usijitenge kiasi hicho, nipo hapa kukusaidia changamoto yoyote unayopitia."
IRYN: “Afadhali ningekuwa nakujua ningeweza kuja kwako unisaidie, nimejifunza, na ninaahidi kwamba sitafanya hivyo tena. Nawashukuru kwa uvumilivu wenu na kwa upendo wenu. Naomba mnipokee tena, tuwe na amani."
SISTER: “Embu niambie tatizo lilikuwa ni nini? Brother kwa upande wake alifunguka vya kutosha, ningependa kusikia kutoka kwako, tatizo lilikuwa ni wapi?.”
Baada ya kuona sister yuko serious sana, ilibidi niwaage ili niwape uhuru wa kuongea na nikaondoka kwenda room.
Baada ya kufika room nilimpigia simu Mary maana alikuwa kanipigia sana, kipindi niko na Sister, hivyo nilitamani sana kumsikia alichotaka kuzungumza nami. Nilimpigia simu na kwa haraka alipokea tukaanza maongezi pale na alionekana kununa;
MIMI: “Hi my baby.”
MARY: “Why didn’t you pick up the phone?”
MIMI: “Sorry bae, nilikuwa naongea na sister, I miss you.”
MARY: “Please! Insider, tell me the truth, do you really love me?”
MIMI: “Yes, I do love you. Why are you asking me this?”
MARY: “Since Iryn karudi, huna mapenzi tena kwangu, you know, I feel bad.”
MIMI: “Don’t be my love, nikirudi Dar es Salaam tutaspend vya kutosha, just me and you.”
MARY: “Unarudi lini?”
MIMI: “Kufikia jumapili nitakuwa nimerudi, pia nataka tuongee suala la mtoto.”
MARY: “Don’t be too late, I miss you badly.”
MIMI: “Bye, see you then.”
Baada ya kuongea na Mary, nilimpigia simu Hilda maana tangu Iryn aje Dodoma hatukuwa na mwasilino yoyote. Hilda aliniomba msamaha kwa kumpa Iryn namba yangu ya simu, lakini nilimwambia alifanya jambo jema, hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.
Hilda alinipa taarifa kwamba mama Janeth kasafiri tena. Vilevile, Asmah na Sumaiya wananiulizia sana. Nikiwa na hayo akilini, niliendelea kumsisitiza Hilda kwamba asije thubutu kuitoa namba yangu.
Baada ya lisaa kupita, Iryn alinitumia ujumbe uliosomeka;
“Darling, sisi tumehamia kwenye rooftop. Kwenye begi langu kuna simu mpya, naomba uje nayo. Pia, niambie nikuagizie nini?”
Nika reply;
“Seafood 😋😋”
Nilifungua begi lake nikaona simu mpya ya iPhone 14 Pro Max, nikajisemea kuwa hii lazima itakuwa zawadi ya dada. Nilitafuta bahasha, nikaiweka na kuelekea huko. Kwa mbali niliwaona wakiongea na kucheka, nami nikavuta kiti nikakaa.
Muda huu walikuwa busy sana wakipiga story mbalimbali kuhusu Ethiopia na tamaduni zao. Kwa upande wa dada yangu, alikuwa akishangaa sana kumuona Iryn akijitahidi kuongea Kiswahili. Ingawa Iryn anaongea Kiswahili, sio fasaha kabisa, kuna baadhi ya maneno yanamsumbua, kama vile neno “ugali” ambalo yeye anasema “ungali.”
Muda wote wakiongea mimi nilikuwa kimya, kwani sikutaka kuingilia maongezi yao. Nilitoa ushirikiano pale nilipohitajika tu. Sister alipendekeza kwamba jumapili twende Serengeti kutalii na turudi jumanne, na Iryn alifurahi sana kusikia mapendekezo haya kutoka kwa dada yangu.
Muda ulikuwa umeenda, hivyo sister alituaga na aliniomba sana niende nyumbani kesho ili nikamsalimie na shemeji. Kabla ya kuondoka, Iryn alimpa dada ile zawadi, na sister alishukuru sana, akasema ataifungulia mbele ya safari.
Tulimkampani sister mpaka nje kwenye parking alikokuwa amepark gari yake. Walikumbatiana kwa hisia, nami nikamalizia kwa kumkumbatia pia. Baada ya hapo, sister akaondoka.
Iryn alikuwa na furaha sana baada ya kuonana na sister yangu, na alisema nimebahatika sana kuwa na dada anayejitambua na kuongeza kwamba amempenda sana dada yangu. Kwa upande wangu, sikutaka kumuuliza walichoongea na dada, kwa sababu nilijua kuwa ningemwona dada yangu kesho.
Baada ya kufika chumbani, alinivuta kitandani kwa haraka. Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kisha akapanda juu yangu, akianza kuvua gauni lake. Ndani, alikuwa hajavaa chochote, na alichukua mikono yangu miwili akaiweka tumboni mwake, akionyesha jinsi alivyotaka niwe nalichezea tumbo lake. Kisha, alinyanyuka kidogo, akaikamata magazine, na kuanza kuiingiza taratibu, kwa ajili ya kutengeneza njia ya mtoto. Baada ya kazi ndefu alichoka sana na aliishia kulala palepale juu yangu.
Saa nne asubuhi, nilienda nyumbani kwa sister Sakina. Bahati nzuri, nilimkuta shemeji naye aliishia kunikaribisha, kwani ilikuwa muda mrefu hatujaonana. Kwa upande mwingine nilikuwa nikiwashangaa madogo kwani walionekana kukua sana, kwa sababu ni muda mrefu sana tangu nilipowaona mara ya mwisho.
Sister aliaga anakwenda jikoni kupika na alituacha pale seblen na shemeji yangu. Tulijadili mambo mengi, kuanzia changamoto za maisha ya kila siku hadi ndoto zetu za baadaye. Mazungumzo yetu yalikuwa na mvuto na yalijaa hekima, na nilipokea maoni ya thamani na muhimu kutoka kwake.
Kwa upande wangu, nilimkaribisha kwa moyo mkunjufu aje kwangu kusalimia pale atakapokuwa Dar es Salaam. Aliahidi kuja, lakini aliongeza kuwa tatizo langu ni kwamba huwa namtenga sana.
Baada ya kupata chakula cha mchana, tulitoka nje mimi na dada yangu na tukakaa kibarazani kwa ajili ya maongezi. Kitu kikubwa nilichotaka kufahamu ni maongezi yao ya jana akiwa na Iryn;
SISTER: “Mke wako hajakwambia?”
MIMI: “Sikutaka kumuuliza, nilijua leo tutaonana, hivyo nitajua.”
SISTER: “Tuliongea mambo mengi sana, mengi tulishaongea siku ile. Ukweli ulizingua sana, una bahati sana ni vile dada anakupenda.”
MIMI: “Nakusikiliza dada yangu.”
SISTER: “Yeye anasema wewe huna hatia, yeye ndo aliamua kuibeba mimba bila kukushirikisha. Amenifungukia kwamba anakupenda sana ndomana aliamua kubeba mimba na hayuko tayari kuharibu mahusiano yako na mama J.”
MIMI: “Mmh sawa, mama J atakuwa tayari kukubaliana na hili jambo?”
SISTER: “Nimemwambia huoni umefanya maamuzi ya haraka ambayo yatapelekea mafarakano kwenye mahusiano yake na mama J?”
MIMI: “Akasemaje?”
SISTER: “Ameahidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba siri hii itabaki kuwa yenu pekee. Bro! hali hii tayari imetokea, na lazima ukubali kwamba ulikosea sana. Mimi kama dada yako siwezi kukulaumu sometimes inakuwa ni mipango ya Mungu. Mtoto ni damu yetu, hatuwezi mkataa, hivyo inabidi niendelee kuwa naye karibu aone tuko pamoja.”
MIMI: “Vipi kuhusu home kwa mama na mama J tutawaambiaje?”
SISTER: “Tunawaambia au utawaambia wewe? Naona umeshaanza kuniingiza taratibu kwenye msala wako.”
MIMI: “Nakutegemea sana kwa hili maana bila wewe siwezi.”
SISTER: “Subiri kwanza ajifungue, then mambo mengine yaendelee, usiwe na haraka.”
MIMI: “Sawa dada yangu nashukuru kwa hili.”
SISTER: “Usijali tutapanga, ila sasa utulie sitaki kusikia umemzalisha mwanamke mwingine au unachepuka tena, tutagombana.”
MIMI: “Sawa dada yangu.”
SISTER: “Kama mwanamke umempata kwa hili acha nikupe sifa kaka yangu.”
Tuliishia kucheka wote na kuendelea na mipango mingine kuhusu Iryn. Nilishinda pale nyumbani kwa dada yangu hadi jioni, kisha nikaondoka kurudi hotelini kwa sababu Iryn alikuwa anapigia simu sana.
*****
Asubuhi na mapema ya Jumapili, sister alifika hotelini tayari kwa safari ya kuelekea Serengeti. Gari la kukodi kwa ajili ya tour lilikuja kutuchukua hotelini, na tulianza safari yetu saa 4 asubuhi.
Ilikuwa safari ndefu ya takriban masaa saba hadi tulipowasili Serengeti National Park, na tukafikia Four Seasons Safari Lodge. Kufikia muda huo, giza lilikuwa limeingia, hivyo tuliamua kupumzika, tukisubiri siku inayofuata kwa shauku ya kuanza safari yetu ya kutalii.
Asubuhi na mapema, baada ya kupata kifungua kinywa kizuri, tulianza safari yetu ya kwenda kuanza utalii. Tulikuwa na hamu kubwa ya kuona mandhari na wanyama wa porini. Bahati nzuri, tulikuwa na mwenyeji mzuri ambaye alituongoza na kutuelekeza mbugani kwa ufanisi mkubwa.
Tulitembea huku tukifurahia kila hatua, tukiona wanyama mbalimbali kama vile simba, tembo, na twiga. Hali ya utulivu ilitawala, na tulikuwa na amani kwani mwenyeji wetu alitufanya tujisikie salama. Hatukuwa na wasiwasi hata kidogo, kwani kila kitu kilipangwa kwa uangalifu. Kila kona ya mbuga ilitupa uzoefu mpya na wa kipekee, na tulifurahia kila dakika tuliyokuwa huko.
Tulitumia siku mbili za kipekee pale Serengeti, tukifurahia uzuri wa mandhari na wanyama wa porini. Kila siku ilikuwa na jambo jipya la kuvutia, na muda ulionekana kupita haraka. Siku ya jumatano asubuhi, tuliondoka Serengeti na tukarudi Arusha kwa ndege ya binafsi.
Tulipofika Arusha, tulijiandaa kwa safari nyingine ya kurudi Dar es Salaam. Hapo ndipo tuliagana na dada yetu. Alikumbatiana na Iryn kwa hisia nyingi, na kisha akaondoka huku akitabasamu. Ilikuwa siku yenye hisia mchanganyiko, furaha kwa muda mzuri tuliotumia pamoja na huzuni kidogo kwa kuagana.
Katika zile siku mbili tulizotumia Serengeti, jambo la kufurahisha zaidi lilikuwa kuona jinsi Iryn na dada yangu walivyotokea kuelewana sana. Ingawa mwanzoni walikuwa hawafahamiani sana, muda tuliotumia pamoja uliwapa fursa ya kuzungumza na kufahamiana zaidi. Walikuwa wakicheka, wakishirikiana mawazo, na hata kupanga mambo ya baadaye kwa furaha kubwa.
Kila wakati tulipokuwa tukifanya utalii, mara nyingi walikuwa wakiendelea na mazungumzo yao ya ndani, wakionekana kufurahia urafiki mpya uliokuwa ukichanua kati yao. Ilikuwa faraja kwangu kuona jinsi walivyojenga uhusiano wa karibu kwa muda mfupi.
Tulipofika Dar es Salaam, tulielekea moja kwa moja Coral Hotel. Wakati tuko njiani, Iryn aliniambia angependa twende tena Zanzibar kwa mara nyingine. Hata hivyo, kutokana na hali aliyokuwa nayo, nilimkatalia kwa upole na kumwambia, 'Kwa sasa hapana, tulia tu, upo kwenye kipindi muhimu cha karibu kujifungua, hivyo unapaswa kupumzika.'
Tulipokuwa hotelini, tulipanga kutafuta apartment ya kuishi kwa muda wa kipindi hiki atakachokuwepo Dar es Salaam, kabla ya kurudi Afrika Kusini. Alisema tutakaa kwa wiki mbili, kisha ataondoka kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujifungua.
Kesho yake, tulipoamka, tayari tulikuwa tumeanza mwezi mpya wa sita. Kwa upande wa Iryn, hali yake ya ujauzito ilikuwa imeendelea sana. Tumbo lake lilikuwa kubwa, na alikuwa akionesha dalili za kuchoka, hali iliyokuwa ya kawaida kwa hatua aliyokuwa nayo. Nilipomuangalia, niligundua pia kuwa alionesha ishara za karibu za kujifungua muda wowote.
Siku hiyo, tuliondoka hotelini mapema ili kwenda kuonana na dalali, tukiwa na lengo la kuangalia apartments. Tulitembelea apartment tatu, kila moja ikiwa na sifa tofauti. Hata hivyo, apartment iliyotuvutia zaidi ilikuwa ile iliyokuwa nyuma ya Coco Plaza. Ilikuwa na mandhari nzuri na ilikidhi mahitaji yetu kikamilifu. Baada ya kuitazama kwa umakini, hatukusita kufanya uamuzi. Tulifanya malipo palepale bila kuchelewa, tukiwa na furaha kwa kupata sehemu nzuri ya kuishi.
Baada ya kumalizana na dalali, tuliondoka kuelekea ofisini. Tulipofika, tulikuta mazingira yakiwa kimya sana, kana kwamba kila mtu alikuwa bize au hapakuwa na shughuli nyingi. Tulipoingia ndani, Nollie alikuwa pale kwenye mapokezi, na aliponiona, alishangaa sana na alikuja kunisalimia.
Haikuchukua dakika nyingi, Hilda akaja kwa kasi na kunikumbatia kwa furaha. Hapo ndipo hali ya utulivu ilibadilika kabisa, ndani ya muda mfupi, lobi ilijaa watu. Wafanyakazi walikusanyika huku sura zao zikionyesha furaha kubwa. Kila mtu alionekana kufurahi kuniona, lakini kilichonigusa zaidi ni jinsi Winny alivyoonyesha furaha ya pekee. Alionekana kweli mwenye furaha kuniona, hasa kwa sababu hawakuwa na taarifa zangu kwa muda mrefu. Siku hiyo ilikuwa ya kipekee, ilijaa shangwe na hisia za kukutana tena na watu wa karibu.
Nilitoka nje kukaa kibarazani nikiwa na Hilda na tukaanza maongezi na alionekana kufurahi sana;
HILDA: “Insider nimefurahi sana kukuona, pia naona furaha yako imerudi tena,”
Nilicheka kwanza;
MIMI: “Soon naenda kuwa baba wa watoto wawili lazima niwe na furaha.”
HILDA: “I’m sorry nilishindwa kuvumilia nikampa namba Iryn, lakini nimefurahi mmeyamaliza.”
MIMI: “Usijali Hilda, ulifanya jambo zuri sana.”
HILDA: “Weeh! Hapa ofisini kila mtu anakusifia hawaamini kama kweli Iryn kakubali kuzaa.”
MIMI: “Achana na wanawake wa humu ndani, ndomana Asmah alikuwa anajifungia ndani.”
HILDA: “Umenikumbusha, halafu Asmah anakuuliza sana, ana wasiwasi sana juu yako, naomba umtafute.”
MIMI: “Nitamcheki, nafikiri tutaenda ofisini kwake.”
HILDA: “Ndo umerudi mazima? Nikukabidhi ofisi yako.”
MIMI: “Wewe endelea Hilda, ushachukua kiti changu, sina jeuri ya kukutoa, pia kwasasa na mambo mengi siwezi kurudi ofisini.”
HILDA: “What? Najua utarudi tu, Iryn anakutegemea.”
MIMI: “Naona una simu mpya kitu fourteen.”
HILDA: “Zawadi kutoka kwa wifi yangu Iryn.”
MIMI: “Hongera sana unastahili pongezi kwakweli hata mimi nitakupa zawadi.”
HILDA: “Zawadi gani?”
Kwa kumnong’oneza;
MIMI: “D*ck.”
Hilda aliishia kunipiga kwa ngumi ya mgongo kwa utani, kisha tukaendelea na mazungumzo mengine. Baadae Iryn alitoka na akasema tuondoke twende Mikocheni kumwona Lucy.
Nilirequest Uber ili atupeleke Mikocheni, na ndani ya muda mfupi tuliwasili na kisha tukaingia ndani. Tulipofika, wafanyakazi wa pale walishangilia kwa furaha baada ya kuniona. Ilikuwa ni furaha ya kukutana tena, na niliendelea kupiga nao stori huku tukicheka na kushirikiana mawazo.
Hata hivyo, kelele zetu zilimvuta Lucy kutoka ofisini kwake. Alipotuona, alimkumbatia Iryn kwa furaha, lakini mimi hakutaka hata kunisalimia. Japokuwa hali hiyo ilinifanya nijisikie vibaya kidogo, nilijaribu kuweka hali ya utulivu kwa muda huo.
Iryn aliusoma mchezo mzima ulitokea pale na aliishia kunikonyeza. Nilijua kilichomchukiza Lucy ni suala la kutopatikana kwa simu, hivyo nilipanga kuongea naye pembeni, ili tumalize tofauti zetu.
Mchana tuliamua kutoka kwenda Golden Fork kwa ajili ya kupata lunch ya pamoja na timu nzima ya pale ofisini. Ilikuwa ni chakula cha pamoja, ambapo kila mmoja alionekana kufurahia muda huo. Baada ya kumaliza, tulirudi tena ofisini tukiwa na hali ya kuridhika.
Muda ulipokwenda, niliona ni bora nijaribu kuongea na Lucy ili tuondoe ule ukimya na kutoelewana. Hata hivyo, jitihada zangu hazikufanikiwa. Lucy alionekana kukerwa na hakutaka kuongea nami kabisa. Aliniambia moja kwa moja kuwa hataki kuniona. Maneno hayo yalinichoma, lakini nilijua kuna jambo kubwa zaidi lililokuwa likimtatiza, hivyo niliamua kumpa nafasi ili apate utulivu.
Hatukutumia muda mrefu pale ofisini, hivyo tuliondoka kurudi Masaki. Tulianza kwa kupitia Coral Hotel kuchukua mabegi yetu, kisha tukaelekea kwenye apartment. Baada ya kufika, tulikaa na kutulia kwenye balconi, tukipiga story kwa utulivu;
IRYN: “Baby, please twende Zanzibar tukatembee hata siku mbili, umenikatalia kufanya Baby shower hata Zanzibar?”
MIMI: “Hali yako si unaiona? Nina wasiwasi ndomana.”
IRYN: “Mimi kujifungua bado, I think kuanzia tarehe 20 huko, ndo kwanza tarehe 1.”
MIMI: “Unaona hata wewe huna uhakika unaonaje tukienda kujihakikishia hospital?”
IRYN: “No problem, na kama niko sahihi tutaenda sindio?”
MIMI: “Deal.”
IRYN: “Badae nitaenda kumsalimia Mama J, nipe namba zake niawasiliane naye.”
MIMI: “Usijaribu wala kuthubutu kwenda kuonana naye, utaleta matatizo tu.”
IRYN: “Why? Hivi hujui kwamba nisipoenda ndiyo atazidi kuamini anachowaza ni kweli?. Acha niende nikamsalimie nijifanye kama sijui kinachoendelea, hii itasaidia kumuweka sawa, trust me.”
Niliwaza pale nikaona anachoongea ni sahihi,
MIMI: “Sawa, lakini mpigie simu mwambie uko Dar unataka kwenda home kumsalimia, uone atajibu nini.”
Nilimpa namba ya mama J, na bila kusita akampigia simu. Kwa kuwa alitumia namba ngeni, alijitambulisha kwanza, kisha wakaanza mazungumzo. Walizungumza mambo mengi, na baadaye akamweleza nia yake ya kwenda nyumbani, na mama J wangu akamkubalia.
Kipindi chote wanaongea sikio langu lilikuwa makini sana likidaka mawimbi, baada ya kumaliza kuongea, alinigeukia;
IRYN: “I told you, sasa nitafanya jambo moja muhimu sana, nikifika pale home nitaweka sawa hili jambo linalomsumbua.”
MIMI: “Sawa.”
Nilipanga kwamba Iryn akienda kuonana na mama J, bhasi na mimi nitumie muda huu kuonana na Mary ili tuyajenge.
Saa 11 jioni tulienda SALI Hospital kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujauzito kwa ujumla. Tulipofika, vipimo vilichukuliwa kwa umakini, na muda mfupi baadaye matokeo yalitolewa. Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani kwangu, kwani nilijihakikishia kuwa mtoto alikuwa wa kike. Pia, daktari alituambia kwamba Iryn angeweza kujifungua kuanzia tarehe 24, jambo lililonifanya nijisikie zaidi kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo muhimu. Tafrija na msisimko kuhusu ujio wa mtoto wetu yalikuwa wazi kwetu sote.
Kwa ujumla, daktari alisema maendeleo ya mtoto ni mazuri, pamoja na afya ya mama, jambo lililotupa utulivu zaidi. Alinipa pia ushauri wa umuhimu wa kuwa karibu na Iryn wakati huu wa mwisho wa ujauzito, kwani ni kipindi nyeti kinachohitaji uangalizi wa karibu. Maoni yake yalinifanya nione uzito wa jukumu langu la kumsaidia na kumfariji zaidi tunaposubiri siku ya kujifungua.
Baada ya hapo, Iryn aliondoka kwa Uber kwenda home kuonana na mama J, nami nilitoa simu mfukoni, kisha nikampigia Mary. Simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa na nikapiga tena kwa mara ya pili, haikupolewa. Wakati nikijifikiria cha kufanya, yeye ndo alinipigia na nikapokea pale;
MIMI: “Mke wangu upo busy? Au ndo bado umenichukia?”
MARY: “Nilikuwa mbali na simu.”
MIMI: “Niko Dar naomba tuonane. Upo wapi now?”
MARY: “Niko home, tukutane wapi?”
MIMI: “Triple 7 pazuri zaidi kwa kukutana.”
MARY: “After 30 minutes nitakuwa nimefika.”
MIMI: “Sawa nami naanza kutoka hapa.”
Nilirequest uber wa kunilipeleka Triple 7 na baada ya kufika nilimkuta Mary kawasili tayari akinisubiri. Nilivuta kiti nikakaa, kisha nikamsalimia na tulianza kuangaliana pale;
MIMI: “Nimekumiss sana mummy.”
MARY: “Ulisema unarudi jumapili na leo ni alhamisi unaona jinsi ulivyo muongo?”
MIMI: “Sorry, nadhani nilikwambia kinachoendelea. Iryn kaniganda sana kwa kipindi hiki naomba uwe uvumilivu, akiondoka kwenda South tutaenjoy.”
MARY: “Sawa baby, mimi nakumiss sana ndomana unaona nakusumbua.”
MIMI: “I know mpenzi wangu, vipi kuhusu lile jambo letu? Bila shaka umeshajifikiria vya kutosha.”
Mary aliniangalia muda huu, nami nilimshika lips zake nikawa nazichezea;
MARY: “Utawezaje kutumudu wote? Iryn karudi soon atakuwa na mtoto wako, mama J ana mtoto mkubwa, still bado unataka na mimi nikuzalie.”
MIMI: “Sijakuelewa hapa, kuwamudu kivipi? Kipesa au?. Mpaka nikasema hivi nimeona naweza, lakini sio lazima ndomana nikakupa muda wa kujifikiria juu ya hili. Pia tambua hustahili haya maisha mummy, you need someone better atakayekupenda na kukuoa kabisa.”
MARY: “Bora niwe na mwanaume nayempenda kuliko kuwa na mwanaume nisiyempenda. Sipendi kufake juu ya hili, maana mahusiano ni suala nyeti sana, sitaki kuharibu future ya kijana wa mtu sababu ya hili.”
MIMI: “Upo sahihi, but naamini utampata hata mimi utanisahau.”
MARY: “Maybe, Baby nimekuona natamani tukafanye.”
MIMI: “Are we discussing this today at this time?”
MARY: “Yes! Please.”
Niliwaza pale, na ukweli alionesha kuhitaji sana game, lakini nilifikiri nikaona si sawa, niende nikalale na Mary then nirudi tena kwa Iryn?. Hapana, haiwezekani.
MIMI: “Mummy nisikilize kwa makini sana, naomba uvumilie Iryn soon anaondoka, tutaenda Zanzibar tukaenjoy sawa?”
MARY: “Baby, really? Even for just 1 hour? It’s impossible.”
MIMI: “Naomba nielewe Mary wangu, kutokana na hali ya Iryn kwasasa, kufanya na wewe si sawa..”
Mary alikubali kwa shingo upande, Japo alionesha kuchukia, lakini sikuwa na jinsi maana ningekuwa ni mpumbavu kama ningemkubalia na tuliagana pale akaondoka kwenda home, nami nikarudi Masaki.
Nimerudi kwenye apartment, lakini Iryn bado hajarudi wala hakuna dalili yoyote ile, nikaanza kupatwa na wasiwasi juu ya Iryn. Niliwaza nimpigie simu, nikaona ni wazo baya, hata kumtumia ujumbe niliona niache. Muda huu nilimpigia simu Lucy, lakini naye hakupokea nikaamua kumpotezea maana niliona anafanya utoto sasa.
Iryn alirudi home saa 4 za usiku na alianza kunipa mkasa mzima wa kilichokuwa kinaendelea kule Mbezi beach akiwa na mama J.
Baada ya kuachana na hospitali, Iryn alielekea nyumbani ambapo alielekezwa na mama J hadi alipoifikia makazi mapya. Alipofika, alikaribishwa vizuri na kupokelewa kwa furaha.
Iryn alifurahi sana kumuona Junior, alimpigia kelele kwa furaha na kumnyanyua juu. Junior alionekana kufurahia sana kama kawaida yake, na Iryn alishangaa kuona jinsi alivyokuwa akikua kwa kasi. Utundu wa Junior ulikuwa umeongezeka zaidi tofauti na zamani, jambo lililomshangaza na kumfurahisha Iryn kwa pamoja.
Walianza maongezi pale seblen na wife alizidi kumshangaa Iryn kuwa na tumbo kubwa sana;
MAMA J: “Karibu sana Iryn ni muda mrefu sana umepita bila kuonana.”
IRYN: “Ni kweli nilikuwa busy na masomo na nikaenda ufaransa kwa baba mtoto kutulia, si waona hali yangu ilivyo kwasasa?”
MAMA J: “Naona, sijui niseme pole au hongera maana soon unakuwa mama kamili.”
IRYN: “Hahahahaa soon tu hata sio mbali. Insider hapatikani kwenye simu na pia kaacha kazi, amekwambia?”
Iryn alianza kutafuta gia ya kumuingia mama J;
MAMA J: “Hapana hajanambia kama kaacha kazi, lakini anapatikana kwa namba nyingine na yuko Dodoma.”
IRYN: “Na hii ndo sababu ya mimi kuja Dar, maana nashindwa kuelewa kwanini aache kazi na hakuna jambo lolote baya tulilomfanyia.”
MAMA J: “Suala la kuacha kazi, mimi ndo nalisikia kwako, alinambia yuko Dodoma kuna project ameenda zianza na atarudi mambo yakikaa sawa.”
IRYN: “Okay! Mimi nimekuja kuwasalimia, nilihisi atakuwepo na yeye, kama hayupo bhasi utanipa namba zake nitampigia simu.”
Baada ya maongezi mafupi anasema waliingia jikoni wakapika chakula pamoja, kisha wakala na waliendelea na story za hapa na pale. Habari njema Iryn alimuahidi mama J kuwa watashirikiana pamoja katika kufanya biashara ya vipodozi, pindi tu atakapo maliza chuo.
Kwa upande mwingine lengo lake halikifanikiwa sababu mama J hakutaka kufunguka kabisa kuhusu ugomvi wetu. Iryn anasema kwa asilimia kubwa aliweza kumuweka sawa kisaikolojia.
Tulianza kupanga mipango ya kwenda Zanzibar kwaajili ya mapumziko na maandalizi ya ujio wa mtoto wetu. Kwa upande wake alitamani sana twende Nungwi na tutafute hotels ambazo ziko karibu na maeneo ya kule.
Bila kupoteza muda, nilianza mara moja kufanya utaratibu wa kuandaa usafiri, huku yeye akiangalia hoteli ya kufikia. Kwa upande wangu, nilifanikiwa kupata boti ya saa 3 asubuhi.
Asubuhi tuliondoka kuelekea Posta, lakini tulianza kwa kupitia maduka ya nguo. Tulinunua nguo kadhaa na vitu vingine vingi. Baada ya hapo, tulikwenda KADOO kufanya exchange ya pesa, kisha tukaelekea ferry kwa ajili ya safari.
Safari ya kuelekea Zanzibar ilianza kwa utulivu, mawimbi madogo ya bahari yakigonga pembeni mwa boti yetu. Tulipowasili, upepo wa baharini ulitukaribisha huku tukiona gari ya hoteli ikitufikia kwa haraka, tayari kutupeleka Nungwi. Nilikuwa na shauku ya kujua zaidi, tunafikia hotel gani maana sikupata taarifa kutoka kwake juu ya hotel aliyopata.
“Tunaenda Riu Palace Hotel," Iryn alisema kwa tabasamu laini, baada ya mimi kumuuliza tutaenda wapi. Jina hilo lilinifanya nitafakari. Nilikuwa sijawahi kuisikia hoteli hiyo kabla, na hata nilipokumbuka safari zangu zote, haikuwa kwenye orodha ya sehemu nilizowahi kufikiria kutembelea.
Nilitabasamu kisha nikamuuliza tena. “Ni wapi huko?” Nilimuuliza huku nikimwangalia kwa udadisi. Aligeuza uso wake na kutazama nje ya dirisha, upepo ukicheza na nywele zake. "Subiri utaona," alijibu kwa sauti ya upole.
Ulikuwa ni mwendo wa lisaa na nusu maana tulikuwa tunaenda taratibu sababu ya hali yake, hivyo dereva alikuwa makini sana. Tuliwasili kwenye hoteli ya Riu Palace, mahali pazuri tulipopumzika na kufurahia mandhari ya bahari. nilianza kushangaa mazingira ya hotel maana ni mazuri sana na baada ya kuingia reception tulipokelewa vizuri sana na tukapelekwa mpaka room yetu.
Room ilikuwa ni private nzuri afu kubwa, kitanda kikubwa, kuna sofa kubwa mbili pamoja na TV kubwa ya inch 65 ikiwa juu ya showcase, bila kusahau min bar. Ukitoka nje unakutana na terrace kubwa yenye private pool kubwa, na sun loungers. Nilibaki nikiishangaa ile room maana ilikuwa ikivutia sana nami niliwaza kwa haraka nikajisemea hapa lazima mama kijacho wangu ametoboka sana;
MIMI: “Baby, mbona umechukua room kubwa sana utafikiri tunakaa mwezi?”
IRYN: “Yeah si waona hali yangu, nahitaji nafasi na faragha ndomana nimechukua hii. Twende swimming kwanza tukapoteze muda then, tukale.”
MIMI: “Tukale kwanza hapa nilipo nina njaa balaa.”
Tulienda kwenye moja ya restaurant ya pale hotelini, na macho yangu yaliendelea kuangaza huku na kule, nikishangazwa na uzuri wa mazingira. Ukimya wa bahari na upepo laini ulijaza kila pembe ya mahali pale, huku mandhari yakitufanya tusahau kabisa uchovu wa safari. Ilikuwa ni sehemu iliyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila kipengele kilionekana kuakisi uzuri wa asili ya pwani ya Zanzibar.
Mhudumu alifika kwa tabasamu, akatusikiliza kwa upole. Bila kusita, tuliagiza sahani za seafood, samaki waliokaangwa kwa ustadi, kamba, na chaza safi, na kinywaji tuliagiza fresh juice.
Baada ya chakula, tulirejea chumbani kupumzika kidogo, na kuhusu swimming, nilimwambia asijali, kwani muda bado upo. Aliniegemea kwa upole, akitabasamu kwa shukrani, kisha akalala kitandani huku nami nikifikiria kuhusu kile kilichokuwa kimesalia kwenye siku yetu.
Usiku ulipoingia, baada ya kupata chakula cha jioni tulirejea chumbani. Kulikuwa na utulivu wa kipekee, sauti ya mbali ya mawimbi ikipiga kwenye pwani. Tulikaa kwa muda mfupi, tukipumzika, kisha wazo la kwenda kuogelea lilinijia.
"Nadhani huu ni muda mzuri wa kupoteza muda kwa kuogelea," nilimwambia Iryn, naye akatabasamu, akakubali bila kusita.
Tulifika kwenye swimming pool, mwanga wa usiku uking'aa juu ya maji, ukitengeneza mandhari tulivu. Tulijitosa kwenye maji, hali ya baridi ikitufanya tuhisi kama tumekumbatiwa na dunia. Tuliongea kidogo, tukicheka, na kupoteza muda kwa furaha, tukisahau kila kitu kingine nje ya wakati huo. Ni kama dunia yote ilikuwa kimya, tukabaki sisi wawili tu, tukifurahia usiku wa pwani ya Zanzibar. Tulitumia muda mwingi sana tukiswim pamoja na kupeana mahaba motomoto na, baadae tulirudi kulala.
*****
Ilikuwa Jumamosi tulivu tulipoamua kutembea kando ya ufukwe, karibu na hoteli. Mawimbi laini yaligusa miguu yetu kwa upole, huku tukitembea tukishikana mikono. Upepo mwanana ulituzunguka, ukibeba hewa safi ya bahari na kutufanya tusahau dunia nzima.
Baada ya muda, tulianza kucheza majini, kama watoto wadogo tukiwa wenye furaha. Nilichukua picha nyingi za kumbukumbu pamoja na video, tukifurahia wakati huo wa kipekee. Upekee wa kila picha ulikuwa na hadithi ya uhai wa furaha yetu.
Katikati ya mchezo wetu, tulikutana na kundi la wazungu, wanawake wawili na mwanaume mmoja. Walivutiwa na sisi, na mazungumzo yakaanza kama marafiki wa muda mrefu. Walituambia kuwa walikuwa Zanzibar kwa kazi na kufikia hoteli ileile tuliyofikia. Mazungumzo yaliendelea, na ingawa tulikuwa wageni kwao, upendo wao kwetu ulionekana dhahiri. Siku iligeuka kuwa nzuri zaidi, kwa furaha na urafiki usiotarajiwa.
Siku nzima tuliitumia ufukweni, na mwishowe tulirudi hotelini tukiwa tumechoka lakini wenye furaha tele. Tulifika saa moja usiku, tukaoga ili kuondoa uchovu wa mchanga na maji ya bahari, kisha tukajiandaa kwenda kupata chakula cha jioni.
Baada ya chakula, tuliamua kwenda bar kupoteza muda na kufurahia usiku. Kama kawaida, niliagiza Heineken, huku Iryn akiagiza mocktail. Hewa ya usiku ilikuwa ya utulivu, na sauti za mbali za muziki zilifanya eneo hili kuvutia sana.
Saa 6 za usiku tulirudi room kulala sababu Iryn alionesha kuchoka sana, hivyo sikuwa na budi ya kumrudisha kulala. Baada ya kurudi Iryn alinambia tumbo linamuuma, hivyo nimsaidie kumkanda kanda kwa mbali. Nilichukua maji ya vuguvugu nikawa namkanda kwa juu, taratibu na baadae akalala.
Asubuhi baada ya kuamka niliamua kutoka nje na kwenda kukaa kwenye sun lounger nikipata jua tamu la asubuhi pamoja na upepo wa bahari. Nilikuwa mtu ambaye nimetulia sana nikifikiri mambo mengi sana kwa wakati mmoja.
“Naenda kuwa baba wa watoto wawili, soon Iryn atajifungua. Hivyo, majukumu kwangu yanaongezeka kuanzia matunzo ya mtoto na mama yake.”
Nikiwa nimendelea kutulia nilisikia sauti laini ya mama kijacho wangu Iryn, ikiniita;
“Darling.”
Na ile kugeuka namuona akielekea kwa swimming kuogelea, nami niliinuka nikamfuata ndani ya swimming.
“Baby si jana tu ulikuwa unalalamika tumbo linauma?”
“Ndio, lakini sasa niko good. Ni maumivu ya kawaida ambayo kila mwanamke huwa anayapitia hasa kabla ya kujifungua.”
Iryn alionekana kuwa na nguvu sana, mpaka nilishangaa licha ya kuwa na mimba ya miezi 8, lakini bado alikuwa anatembea vizuri, hakuwa akideka kabisa. Ukiachana na hayo bado alizidi kuonekana mzuri, umbo lake likikuwa linavutia barabara.
Tuliishia kuogelea wote mle ndani ya swimming na bila wasiwasi wowote tulianza kuwekana. Ni private room yenye terrace kubwa, hakuna mtu wa kusogea wala kutuona na kutufuatilia, It was just a part of our private life. Baadae tulienda kulala kwenye sun loungers na tuliendelea kupiga story pale;
IRYN: “Baby nilikuona umetulia ulikuwa unawaza nini?”
MIMI: “Nilikuwa nawaza kuhusu maisha, naenda kuwa baba wa watoto wawili soon na wote watahitaji matunzo.”
Iryn aliniangalia kisha akanishika kidevu changu kwa mahaba;
IRYN: “Darling, hili ndo linakufanya uwaze, like seriously?”
MIMI: “Yes! Hata kama una pesa bado matunzo ya mtoto yananihusu kama baba, hio ni damu yangu lazima niijali na kuitunza.”
IRYN: “Sawa nafurahi kuona una mipango juu ya huyu mtoto. Naomba tuongee mambo muhimu kuhusu future yetu na mtoto.”
MIMI: “Sawa mummy nakusikiliza.”
IRYN: “Kwanza nakuhitaji pale ofisini uendelee kuwa manager. Mali zangu zote za huku Dar naomba uendelee kuwa msimamizi, pia nampango wa kufungua restaurant na kampuni ambayo wewe utakuwa Director wa hii kampuni mpya.”
MIMI: “Suala la kurudi ofisini mimi sina shida, kwanza naomba uyamalize na mama.”
IRYN: “Jumatatu tukirudi Dar tutaenda kuonana naye.”
Tulirudi ndani kujiandaa kwaajili ya kwenda kupata lunch na Iryn alivaa gauni nzuri ya kujisitiri na alionekana kupendeza zaidi kuliko kawaida. Ujauzito wake ulimfanya awe na uzuri wa kipekee, na kila tulikopita, watu walikuwa wakimshangaa na kumtazama kwa furaha na shauku.
Hii restaurant tuliyoenda ilikuwa ya wazi halafu kulikuwa na watu wengi sana wakila na kupiga story na asilimia kubwa ni foreigners. Muda huu tukipata lunch kwa upande mwingine Mary alikuwa anapiga simu na nilimtumia ujumbe kuwa nitamcheki baadae.
Haikuchukua muda akareply kwa kutuma emoji;
MARY: “😭😭😭”
Nilireply kwa kumuandikia;
MIMI: “Mummy nitakupigia simu mpenzi wangu niko na mama kijacho hapa.”
Iryn alianza kuongea muda huu;
IRYN: “Baby unachat na nani?”
MIMI: “Dada wa dukani kanicheki kuhusu mzigo, halafu sijatuma odda kwa supplier, ndiyo nimemwambia anitumie namba za mzigo ulioisha.”
IRYN: “Alright, tukirudi Dar tutaongea kuhusu na hii biashara yako. Kingine nataka kama kampuni tukupangie nyumba uishi Masaki uwe karibu na ofisi.”
MIMI: “Nyumba ya kuishi mimi na familia nitahitaji vyumba viwili au vitatu. Na bajeti yake si chini ya $1000. Hizo pesa ni bora mnipe tu ili nijenge nyumba yangu ya kukaa.”
IRYN: “Utajengea wapi kwa Dar es Salaam?”
MIMI: “Nina kiwanja nilinunua Mapinga, nitaenda kujenga kule.”
IRYN: “Mapinga ndiyo wapi?”
MIMI: “Iko pwani kama unaenda Bagamoyo.”
IRYN: “Kutoka city centre mpaka huko kuna umbali gani.”
MIMI: “Kutokea Mwenge mpaka Mapinga ni kama 30km.”
IRYN: “Mbali sana, kwanini usijenge Kigamboni, ni kuzuri sana. Yule kaka agent wetu wa real estate alisema ana viwanja sehemu nzuri sana na atanipa kwa bei poa, unaonaje?”
MIMI: “Tatizo la Kigamboni kumekaa kushoto sana hasa kwa mimi mtu wa mishemishe siwezi kuishi kule. Daraja liko mbali na vivuko vinazingua sana, Kigamboni labda kwa uwekezaji sawa ila kuishi hapana.”
IRYN: “Tafuta kiwanja sehemu yoyote utakayoipenda, then niambie ili tuanze ujenzi. Tafuta ramani nzuri ya nyumba unayoipenda pamoja na makadirio ya gharama za ujenzi, halafu utanipa feedback.”
MIMI: “Are you sure?”
IRYN: “You don’t trust me now?. Sikutegemea kabisa kama ungekataa kuishi Masaki na badala yake umesema tukupe pesa ili ufanye ujenzi, hii inaonesha ni jinsi gani unawaza future na mimi kama mama mtoto wako nitakusaidia kwa hili, na naomba usijisikie vibaya, sijakuhonga ila ninafanya kwa upendo wangu.”
MIMI: “Ahsante sana mummy, sikutegemea kama kuna siku utanisaprize kama leo.”
IRYN: “Baby, hivyo ni vidogo tu, na vingi vinakuja na utafurahi. Toka tufahamiane hujawahi kunipiga vizinga, kuniibia, wala kuwa na tamaa ya kitu chochote kutoka kwangu. Wewe ni mwanaume wa tofauti sana, licha ya mambo yote yaliyo tokea kwenye kampuni still uliendelea kuipigania kampuni na hujaonesha tamaa. Nafikiri hujui what do I feel about you right now, mapenzi yangu kwako yameongezeka, nimegundua nina mwanaume sahihi ambaye ni mpambanaji.
Nilimkatisha;
MIMI: “Baby, huna haja ya kusema hayo yote ni wajibu wangu kama manager na pia wewe ni kama mke kwangu, hii kampuni ni yote sote.”
IRYN: “Nitakuwa mwanamke wa ajabu sana kama nitashindwa kurudisha fadhila kwa haya yote uliyofanya.”
Iryn alionekana mwenye furaha isiyoelezeka. Nilitazama tabasamu lake na nikahisi furaha yangu kuwa naye, tukijua kuwa hivi karibuni tutakuwa na furaha nyingine ya kumpokea mtoto wetu. Ilikuwa siku ya kukumbukwa, tuliyohisi kuwa karibu zaidi na tayari kwa safari mpya ya maisha yetu.
Usiku tulianza kupanga nguo kwaajili ya safari yetu ya kurudi Dar es Salaam. Muda huu Sister alinipigia simu tukaongea na baadae akaomba kuongea na Iryn na habari kubwa alikuwa akimjulia hali pamoja na maendeleo yake kwa ujumla.
Jumatatu, tuliondoka kutoka hotelini, ambapo kama ilivyo ada kwa Iryn, alitoa shukrani kwa wahudumu waliotuhudumia kwa huduma bora waliotupatia. Gari ya hotel ilitupeleka mpaka bandarini kwaajili ya safari ya kurudi Dar es Salaam.
Tuliondoka saa sita mchana kwa kutumia boat, na tulifika Dar es Salaam saa nane mchana. Baada ya kufika, nilirequest usafiri wa kutupeleka Masaki. Mara baada ya kuingia kwenye apartment yetu, tulipumzika kwani tulikuwa na uchovu mkubwa kutokana na safari.
Saa moja usiku, Iryn aliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuonana na mama Janeth. Alipendekeza twende wote, lakini nilimwambia kuwa kwa sasa ni bora aende peke yake. Nilimwambia kwamba baada ya kumaliza huko, nitakuwa na nguvu ya kuonana na mama pia.
TO BE CONTINUED.