SEASON 02
CHAPTER 17:
βA TRUE STORY BY INSIDER MANβ
PREVIOUS:
Baada ya kufungua na kusoma zile conversations zao ndo kujua hawa watu wapo kwenye mahusiano. Nilijikuta naanza kuumia maana sikuamini kama kweli Iryn ananicheat na ana mtu mwingine zaidi yanguβ¦.
CONTINUE:
Sikuamini ninacho kiona muda huu maana nilikuwa naona ni kama mapichapicha, Roho yangu iliendelea kuumia sana, niliona ni bora ninyamaze, nipotezee, nifanye kama sijaona kitu. Lakini sasa nikikumbuka mimba yake hapa nikawa naishiwa nguvu, niliwaza hata mtoto anaweza asiwe wangu pia.
Nilianza kuwaza mambo mazito sana muda huu na nilijisemea Iryn ni mwanamke mzuri sana ambaye kila mwanaume angetamani kuwa naye au kulala naye, ni ngumu sana kuchomoa au kukwepa mishale yote, kuna ambao utampata tu.
Mawazo yangu yalianza kunituma huenda yule jamaa tuliyekutana Seacliff hotel ndo anatoka naye kwasasa. Niliwaza kuhusu mienendo yangu kwasasa, nilifikiri huenda Iryn kaamua kutafuta mtu pembeni wa kupoteza naye muda maana mimi sitabiriki.
Nguvu ya kumuuliza iliniishia kabisa na niliona ni busara nikavunga like nothing happened ila nitafute sababu ya kuondoka hapa hotelini, hata hamu ya kuendelea kubaki sikuwa nayo.
Kwa upande wake alihisi something wrong kutoka kwangu na alikuwa akiniita, lakini kutokana na mimi kuwa deep kwenye mawazo, sikuwa namsikia. Alishuka kitandani akaja usawa wangu, nilikuwa nimekaa kwenye sofa one sitter na yeye alikaa juu yangu.
IRYN: βBaby, nakuita hata huitiki are you okay?β
Muda huu nilikuwa sina hamu naye kabisa, isingekuwa mimba ningekuwa nilishamzingua kitambo sana. Kwa kawaida akikaaga juu mapajani lazima mashine isimame ila kwa leo ilikuwa tofauti, alishangaa kuona hakuna kitu kigumu kinachomtekenya na alianza kunishika na mkono;
MIMI: βNiache bhana.β Nilikuwa mkali.
IRYN: βWhatβs wrong? Mbona ghafla umebadilika? Unashida gani?β
Simu yake ilikuwa pale mezani aliichukua, sasa baada ya kutoa lock ndo alikutana na zile chats zake, muda huu mimi nilikuwa kimya tu,
βAisee! Hiki ndo kimefanya ubadilike haraka hivi?, Darling, it wasnβt me, it was Samantha chatting with her boyfriend yesterday.β
MIMI: βDo you see me as a child? Even Junior is not deceived like this, your chats show everything."
IRYN: βNo, baby, I canβt cheat, Itβs Samantha who forgot to delete her chats on my phone.β
MIMI: βSamantha anafanya nini kwenye simu yako?β
IRYN: βSimu yake imeharibika na jana alikuwa anatumia simu yangu siku nzima.β
MIMI: βI donβt trust you maana nitakuvunjia heshima sio muda mrefu, inaonesha ni muda mrefu umekuwa unacheat, hata hio mimba naanza kuwa na wasiwasi nayo.β
Kwa upande wake alikuwa kapaniki tayari, alikwenda kukaa kitandani na alionekana ni mtu anayejutia kwa uzembe wake.
IRYN: βYou have to trust me, Iβm telling you the truth.β
MIMI: βUnajua sikuamini hata kidogo, kwanza haimake sense unipende mimi kapuku nafikiri kuna mipango yako ambayo siijui.β
IRYN: βInsider what are you talking about?β
MIMI: βSipendi kuongea mambo ya nyuma, tambua mimi sio mjinga nina akili zangu timamu.β
Alisimama tena akaja usawa wangu na alinipa simu yake niangalie tena;
IRYN: βI told you, hii conversation sio yangu lakini hunielewi, look mwanzo wa conversation alivyojitambulisha kwa boyfriend wake.β
Baada ya kuangalia kweli alikuwa ni mdogo wake Samantha, hapa ndo kidogo nikaanza kuhema vizuri na mapigo ya moyo yakaanza kurudi sawa. Licha ya yote Iryn alikuwa kashanikolea sana na Upendo wangu kwake ulikuwa unapanda kwa kasi kama graph za time series.
(Samantha ni mdogo wake wa Ethiopia anayeishi naye South Africa, nilishaandika nyuma kuhusu hili)
IRYN: βUmeongea mambo mengi sana but tuachane na haya, just know I love you, maneno uliyosema sijayapenda, najua ni hasira.β
MIMI: βUngekuwa ni wewe ungenielewa? Kama ambavyo hunielewi kwa Asmah, je ungekuta hizo chats?β
IRYN: βNdomana nimesema tuachane na haya tuongee mambo ya msingi.β
Maongezi yetu yalikuwa kuhusu kwenda huko Ethiopia maana nilijua lazima atakutana na upinzani wa hali ya juu sana, ukizingatia yeye ndo mtoto pekee aliyeachwa na mama yake.
Kwa mazingira ya kawaida ni ngumu sana mzazi akubali mtoto wake abebeshwe mimba bila kuwa na maelezo ya kueleweka. Kutokana na mimi kuwa na mke tayari, suala ka kumuoa Iryn lisingewezekana kabisa na hapa ndo kulikuwa na ukakasi, kila tukilijadili hili tulikosa majibu ya kueleweka.
Nilimwambia Iryn ajitahidi kuongea ili aeleweke maana yeye ndo alibeba mimba kwa interest zake tena bila kunishirikisha. Jambo lingine lililoibuka ni pale ambapo wangenihitaji niende Ethiopia itakuwaje? Nilimwambia Iryn kwasasa kwenda Ethiopia haitawezekana labda kwa baadae ndo nitafanya hivo.
Tuliongea kuhusu Organization aliyompeleka Asmah, na alisema ni moja ya umiliki wa mama yake na aliandika kwenye diary. Ishu ni kwamba kwa wafanyakazi wa hizi International organization hawaruhusiwi kabisa kumiliki hizi NGOs sababu ya conflict of interest, so wengi wanamiliki kwa kuwatumia watu wengine.
Aliyekuwa anaisimamia hii organization mwezi june ndo alitakiwa kuikabidhi kwa Iryn sababu muda wake ulikuwa umeisha tayari. Alimpeleka Asmah ili aanze kupata uzoefu taratibu na kufikia June awe na experience ya kutosha.
Uvumilivu ulinishinda kuhusu yule jamaa aliyempa $50,000 maana tulikutana Rotana hoteli, tena tukakutana seacliff nilihitaji majibu ya kueleweka. Iryn alicheka sana na alinambia yule jamaa alikuwa ni mteja wa mama yake, kuna vitu alimsaidia huko nyuma, kwahiyo kila mwaka ile ndo kamisheni huwa anaitoa.
Alikiri kwamba ni kweli jamaa anamtongoza sana, hata ile siku niliyokwenda kuchukua zile pesa alimwambia mimi ni ndo mpenzi wake ambaye nazifata zile pesa.
Kwa upande wake alionekana kuchoka sana na aliomba alale na kuhusu mambo mengine tutapanga asubuhi.
Asubuhi nilichelewa kuamka, lakini Iryn hakuwepo around, ikabidi nimpigie simu ili nijue aliko, ile kuchukua simu nakutana na ujumbe wake ambao ulisema niende restaurant nikiamka.
Nilisafisha kinywa changu pamoja na kunawa uso ndo kwenda huko restaurant na nilishangaa sana kwa mbali kumuona yuko na Asmah. Bhasi, mimi nilivuta kiti nikamsalimia Asmah na waliendelea na maongezi yao na kubwa ilikuwa ni mipango ya ofisi mpya.
Baada ya lisaa Iryn alimuaga Asmah kuwa ana kwenda room sababu muda huu ana online lecture na alituacha pale tukiendelea kuongea. Kwa upande wa Asmah alishangaa sana kujua Iryn ni mjamzito,
ASMAH: βMbona hujawahi kunambia kuwa Iryn ana ujauzito wako?β
MIMI: βSindo leo umejua? Hakuna tatizo mummy.β
ASMAH: βNimejisikia vibaya sana, laiti ningelijua hali ya Iryn hata nisingethubutu kufanya ule ujinga.β
MIMI: βKinachofanya ujilaumu ni nini?.β
ASMAH: βNimejisikia vibaya sana, kwa mambo anayonifanyia na mambo nayofanya mimi in return si sawa.β
MIMI: βTuachane na haya mummy, mbona umekuja bila kunipa taarifa?β
ASMAH: βHata mimi nashangaa kukuona hapa, jana alinipa taarifa nije hapa Serena tuzungumze, sikujua mpo wote.β
MIMI: βUmeshindwa jiongeza mimi nitakuwa naye? Sema hukutaka nijue tu.β
ASMAH: βKweli Insider sikuwa na mawazo kama utakuwepo hapa.β
Tuliendelea kupiga story na Asmah na taarifa aliyonambia ni kwamba anawaza kurudi shule kwaajili ya masters na ameplan kusoma MBA. Pia, nilimuuliza anatarajia kuanza kazi lini? Alisema kuanzia february anatarajia kuanza kazi kwenye ofisi mpya.
Baada ya dakika 40 kupita tangu Iryn atuache nilipokea ujumbe kutoka kwake ambao ulisema nirudi room mapema kwani anahamu sana na mimi. Niliusoma ujumbe wake nikaendelea kupiga story na Asmah, baada ya dakika 10 alituma tena ujumbe akiomba nirudi room haraka.
Maongezi yetu na Asmah yalikuwa yameisha na tuliagana pale restaurant na nilirudi room kuonana na Iryn. Nilimkuta amelala kitandani yuko naked na aliomba nimkande tumbo lake kwa maji ya vuguvugu, na kipindi nafanya haya yote alionesha kusikia raha sana.
Saa 11 jioni nilimpa kampani ya kwenda airport kwaajili ya safari ya Ethiopia, na baada ya kuwasili JNIA Terminal 3 tulikaa kwenye mgawaha wa nje kabisa. (Upo katikati koridoni kati ya Terminal 3 na Terminal 2).
Tuliamua kupumzika pale huku tunasubiri muda wa kucheck-in, nikiwa na Iryn huwa tunaongea sana. Yeye sio muongeaji ila tukiwa wawili, huwa tunapiga sana story, hata mama janeth huwa anashangaa sana kwa hili.
IRYN: βHili jambo likiisha nafikiria tupange mipango ya biashara, ila sasa unanipa wasiwasi sana, imani yangu kwako inapungua, lakini nina mipango mizuri sana ya kufanya pamoja.β
MIMI: βMummy ni jambo gani linafanya uanze kukosa imani na mimi?β
IRYN: βUnataka tuanze kubishana mambo unayofanya? Okay hata kama hufanyi bhasi kuwa na mipaka.β
MIMI: βKwa hili nimekuelewa mpenzi wangu, sijaelewa sababu ya kumuita Asmah pale hotelini.β
IRYN: βNilikuwa nina maongezi naye binafsi na kuhusu ofisi mpya.β
MIMI: βNaelewa plan yako imetimia tayari mimi sio mgeni na wewe. You wanted her to know youβre pregnant thatβs it.β
IRYN: βThat was not my plan, ni masuala ya ofisi tu.β
MIMI: βNa huko Ethiopia utatumia muda gani?β
IRYN: βNikimaliza kikao na familia nitarudi South Africa.β
MIMI: βSawa mummy naomba nilindie damu yangu hiyo, kadri siku zinavyokwenda nazidi kuwapenda.β
IRYN: βHili niachie hakuna kitakachoharibika.β
MIMI: βMama Janeth utampa taarifa lini?β
IRYN: βNikimalizana na familia nitampa taarifa.β
Muda wa kucheck-in ulikuwa umewadia na tulielekea ndani Terminal 3, tuliagana kwa kukumbatiana na mimi nikaondoka maeneo yale.
Kipindi narudi home nilikuwa nawaza sana kuhusu Asmah na niliona ni bora nikamwacha na maisha yake, ukizingatia mimi sina future naye, nitaishia kumchezea na kumwacha. Niliwaza kuhusu kitendo alichofanya Iryn cha kumuita pale hotelini, nilijua Iryn ana mipango yake kufanya vile kwa Asmah na leo amejua ni mjamzito.
Baada ya kurudi home ule usiku Muajemi alinicheki na alinipa taarifa ya kuja Dar es Salaam kesho na aliomba tuonane kwaajili ya mazungumzo.
*****
Kesho yake ambayo ni jumamosi mama Janeth alinipigia simu kunipa taarifa kwamba, kuna dada wa reception amempata na amempa maelekezo ya kuonana na mimi kwaajili ya interview. Sikuwa ofisini, hivyo nilifanya kuwasiliana na Hilda ili amfanyie interview, then afanye maamuzi kama anafaa au laah!.
Ile jioni nilimpa wife taarifa ya kuondoka wote na nilimwambia avae apendeze, kwani tunakwenda kupata dinna na tutachelewa kurudi. Ni muda mrefu sana sikuwa nimetoka na wife kwenda maeneo, niliona kwa leo acha nimsaprise niendelee kuongeza mapenzi kwake.
Saa 1 usiku ndo muda ambao tulikubaliana kuonana na Muajemi na alinipa taarifa ya kukutana pale Holiday-in Posta. Kabla ya kuondoka kwenda eneo la tukio, nilikumbuka kubeba vile vitu vyake kutoka kwa Iryn na tukaanza safari.
Baada ya kuwasili eneo la tukio tulikwenda straight upande wa Bar maana ndo alikuwa akinisubiri kule na ile kuingia nilimwona amekaa kwa kona. Baada ya kuifikia meza yake tulikaa, tukasalimiana pale na nilifanya utambulisho mfupi wa wife maana alikuwa hamjui.
MIMI: βBrother leo nimeamua kukusurprise, huyu unayemuona ndo my fiancee.β
MUAJEMI: βHongera sana kaka yuko vizuri na nimefurahi kumuona.β
Walisalimiana pale na nilimuomba wife atafute sehemu akae ili sisi tuongee mambo yetu ya kiume.
Dada alikuwa ameshakuja kunisikiliza muda huu na nilimwambia aniletee coke ya kuchanganyia hennessy maana nilikuta Muajemi anainywa na ilionekana kuwa nyingi kwenye chupa.
Maongezi yetu makubwa yalibase kwa Iryn na nilishindwa kuelewa kwanini jamaa anakuwa mgumu kumuacha Iryn na maisha yake?. Taarifa mbaya ni kwamba Muajemi alikuwa ana taarifa kwamba mimi ndo muhusika wa mimba ya Iryn.
Baada ya kunipa hizi taarifa ukweli nilishtuka na nilianza kujiuliza kajuaje? Lakini ni Iryn ambaye alimpa hizi taarifa kuhusu mhusika wa mimba yake;
MUAJEMI: βKaka siamini wewe ndo umempa mimba Iryn, na kwanini hukutaka kuniweka wazi mapema?β
MIMI: βKaka Iryn kakudanganya maybe hataki uendelee kumsumbua ndomana kakwambia hivyo, mimi sihusiki na hio mimba.β
MUAJEMI: βNilishangaa sana kusikia hivyo, ni kweli ni mjamzito?β
MIMI: βKaka ni kweli hakutanii sheβs pregnant, muache aendelee na maisha yake, Bro! youβre wasting your time.β
MUAJEMI: βKwa muda mrefu nilikuwa naamini ananidanganya, kwasasa acha niwe mpole, nimuache na maisha yake.β
MIMI: βUna pesa unaweza kupata mwanamke yoyote unayemtaka, kuhusu Iryn utapoteza muda kaka.β
Muajemi alikubali matokeo na tulianza story zingine, taarifa aliyonipa ni kwamba anataka kuichukua familia yake ya huku Tanzania kuipeleka Saudi Arabia. Nilitaka kujua kuhusu biashara zake za huku Dar itakuwaje? Kwa upande wake alisema, mke wake atakuwa anakuja kutembelea.
Ni maongezi yaliyokwenda zaidi ya lisaa na nilitoa vitu vyake nikamkabidhi, lakini aligoma akasema hawezi kuvipokea, kama Iryn kanirudishia bhasi nimpe wife. Nilimwambia wife anajua ni vitu vya Iryn, hivyo italeta shida, bado alikataa na akasema mimi nitajua kwa kuvipeleka.
Kipindi tunamalizia maongezi yetu ili tuagane dada mrembo mwenye asili ya uarabu alikuja usawa wetu na alivuta kiti akakaa. Muajemi alinitambulisha kama shem wangu na niliamua kuaga ili niondoke na alisema tutaendelea kuwasiliana.
Niliondoka na wife maeneo yale na safari yetu ilikuwa ni kwenda Masaki ili tukapate dinna na tumalizie sehemu usiku wetu. Nilimwambia wife leo haturudi home mpaka kesho, tuta-tafuta sehemu nzuri ya kulala, yeye hakuwa na usemi na alishia kufurahia maamuzi yangu.
Tulipitia Peninsula hotel kufanya booking ya room mapema na baada ya kupata chumba tuliondoka kwenda Levant kupata dinna. Kipindi tuko levant tunapata dinna nilimshirikisha wife kuhusu mipango yangu ya kutafuta kiwanja kwaajili ya ujenzi kwa huku Dar. Kwa upande wake aliunga mkono wazo langu na akasema kwahili tutashirikiana pamoja maana ni bora tukaanza ujenzi kama uwezekano upo.
Kwa ufupi hii siku wife alikuwa na furaha sana na nilikuwa na mtreat kama malkia. Kwa upande wake alikuwa bado haamini kama ndo mimi baba J ambaye nafanya haya yote bila ya aibu, japo yeye ana asili ya kuwa na aibu sana.
Baada ya kumaliza kupata dinna tulifanya kuhamia Samakisamaki kumalizia usiku wetu, inshort tuliinjoy sana, mida ya saa 7 za usiku ndo tukarudi hotelini kulala and the rest was history.
Jumapili nilikuwa na miadi ya kuonana na Kizoka kwaajili ya kukabidhiana gari na alikuja home. Kwa upande wake alikuwa kabeba documents zote muhimu pamoja na taarifa za wadhamini wake. Kwenye masuala ya kazi sinaga usela na ushikaji kabisa bora unichukie tu, ila lazima taratibu zote zifuatwe.
Kizoka alikuja home mida ya mchana na nilimwambia wife asogee eneo la tukio ili ashuhudie tunavyo andikishiana mikataba. Zoezi likikwenda vizuri sana maana jamaa alikuwa serious na kazi na alikuwa katembea na nyaraka zote muhimu.
Baada ya kumaliza kusainishana mikataba tulipata lunch ya pamoja na nikamkabidhi gari na pesa ya mafuta full tank kwaajili ya kuanza kazi, hakutaka kuendelea kupoteza muda home na aliaga akaondoka.
Baada ya Kizoka kuondoka niliwaza kununua gari ya kutumia na sikutaka gari yenye mambo mengi kwa kipindi hiki cha mpito, niliwaza niwe na gari simple tu.
Jioni niliondoka kwenda Mbweni kwa Jane na nilifanya kurequest bodaboda ya kunipeleka na nilitumia muda mchache sana kuwasili pale kwake.
Baada ya kuwasili, Vicky ndo alitoka kunifungulia gate na tulikaa nje kibarazani, lakini aliniaga anakwenda ndani kujiandaa ili tuondoke wote, kwani anataka kumpa kampani dada yake.
Baada ya nusu saa tuliondoka kwenda ukweni kuonana na mama mkwe maana alisema jioni ndo muda mzuri wa kuonana naye na tukazungumza.
Tulitumia muda mfupi sana kuwasili ukweni na tuliishia kukaribishwa ndani na shemeji zangu, mimi pale ni kama home na baada ya kuingia sebleni niliendelea kuongea na dada yake wife.
Mama mkwe alikuja seblen na nilifanya utambulisho mfupi kuhusu Jane na baada ya kufahamiana maongezi yakaanza;
MAβMKWE: βKaribuni sana wageni zangu, huyu mkwe wangu sio mgeni ni mwenyeji kama aliwakaribisha bhasi inatosha.β
JANE: βAhsante sana mama, mengi nadhani Insider ameshakwambia ndomana niko hapa kupata elimu.β
MAβMKWE: βKwanza nilitaka kujua mtaji wako ni kiasi gani na eneo umetarget wapi?β
JANE: βMama kuhusu eneo bado sijatafuta ila kwenye mtaji hakuna shida.β
MAβMKWE: βSiku zote tunavyoanza biashara huwa hatuingizi mtaji wote, tunaangalia kwanza hali ya hewa, kama inaridhisha ndo tunaongeza pesa tena.β
JANE: βNi kweli mama upo sahihi.β
MAβMKWE: βBiashara ya mini-supermarket ni nzuri kama utapata eneo zuri na inalipa.β
JANE: βKwahiyo mama nianze na mtaji wa kiasi gani kutokana na experience yako?β
MAβMKWE: βNashindwa kukupa makadirio halisi maana sijui frem utapatia wapi na gharama zake zitakuwaje.β
MIMI: βMama tupe makadirio ambayo ni nje na fremu.β
MAβMKWE: βKwa kuanza jitahidi uwe na 30M ili uanze vizuri, hapo jitahidi uwe na kila bidhaa na unakuwa unauza jumla na rejareja. Pale ambapo utakuwa umepata frem njoo kwa mara ya pili ili nikupe mchanganuo wa vitu muhimu vya kuanza navyo.β
Yalikuwa ni maongezi kama ya lisaa hivi, Jane alipata elimu nzuri sana kutoka kwa mama na alisema ananipa kazi ya kutafuta frem ya biashara.
Tuliwaaga pale na kipindi tuko kwa gari Jane alisema tunakwenda kwangu ili akapajue na aijue familia yangu maana mimi nakwenda kwake kila siku, lakini kwangu hakujui. Sikuwa na chakusema wala nguvu ya kukataa, hivyo tulianza safari ya kwenda home Mbezi beach.
Baada ya kuwasili home, niliwakaribisha ndani, kwa upande mwingine wife alikuwa jikoni akipika na alikuja kuwakaribisha wageni. Wife alikuwa anamjua Jane kwa kumuona kwa picha, sura haikuwa ngeni kwake na nilifanya utambulisho pale.
Jane aifurahi sana kumuona wife pamoja na Junior na maongezi mengine yaliendelea;
JANE: βWifi yangu leo nimefurahi sana kukuona live, niseme Insider anajua kuchagua.β
Wife aliishia kutabasamu pale,
WIFE: βAhsante sana wifi yangu, pia pole sana kwa matatizo yote na hongera kwa mtoto.β
Muda huu wife alikuwa kamshika mtoto na Junior alikuwa akimshangaa sana mtoto na alikuwa akifurahi kumuona;
JANE: βYote ni mipango ya Mungu, natakiwa kumshukuru pia.β
WIFE: βNgoja niwaache nikawapikie chakula ili mnavyoondoka muwe mmeshiba kabisa.β
Wife alituacha pale seblen akaenda jikoni na muda huu Jane alianza kumzingua Vicky maana alionekana kuwa kimya sana;
JANE: βMdogo wangu Vicky, unaona Insider ana mke? Huyu sio level yako becareful.β
Vicky aliishia kucheka tu pale maana hakuwa na usemi,
MIMI: βMuache Vicky kama ananielewa si namuoa na yeye tu, kwani kuna tatizo?β
JANE: βThubutu! Insider kama mke unaye mdogo wangu, the way nilivyomuona na maongezi yake anaonekana kujitambua sana, utulie sasa.β
MIMI: βUnaongea haya ili kumchoma Vicky?β
Na tuliishia kucheka wote kwa pamoja muda huu..,
Tuliendelea na maongezi kuhusu biashara anayotaka kufungua na nilimshauri atafute frem ya karibu na home na asiwe mbali na biashara maana kwa mwanzo biashara inahitaji usimamizi mkubwa.
Tulijadiliana sana mwishoni tukaona tutafute frem ya biashara Bahari Beach na akaendelea kunisisitiza nimsaidie kutafuta fremu, kwaajili ya kuanza biashara february.
Jane alikumbushia kuhusu zawadi nayotaka kutoka kwake na nilimwambia afanye atakavyoona sawa kwa upande wake, ila mimi siwezi kusema zawadi nayotaka na afanye atakavyoweza.
Saa 2 za usiku tulipata dinna ya pamoja, wife alikuwa kapika pilau kwa kuku na mazaga mengine ya kutosha. Wakati tunakula Jane alikuwa akimsifia mama J kuwa yuko vizuri sana jikoni, na waliendelea kupiga story na kubwa alikuwa anamtaka siku aende Mbweni.
Baada ya kupata dinna ilibidi watuage maana muda ulikuwa umekwenda sana, Jane alitoa laki 2 cash kwenye mkoba wake na akampa Junior kama zawadi.
Bhasi, baada ya Jane kuondoka mimi nilikwenda chumbani kuweka mipango yangu sawa kuhusu kununua gari ya kutumia, kama pesa nilikuwa nayo ya kutosha kwa account, sasa nilikuwa naendelea kujifikiria gari ya kununua.
Ajabu nilikuwa nakosa choice ya gari ya kununua maana nilikuwa nakosa maamuzi sahihi, nikapata wazo niazime gari ya Sumaiya kwa muda. Pia, niliwaza ninunue kiwanja kwa huku Dar ili nianze ujenzi wa makazi ya kuishi, kama uwezo wa kujenga nilikuwa nao.
β
Niliwaza pale kama mshahara nalipwa mzuri, akiba ninazo, bado naweza kukopa pesa Bank au kwenye kampuni, ni nini cha kunizuia kufanya ujenzi?. Ni mimi tu sijataka kufanya maamuzi juu ya hili, kama Dodoma nilifanikisha, na huku nitafanikisha. Pia, kuna haja ya kuanza kufungua biashara zangu, kuitegemea kampuni ni upumbavu wa akili ya maisha.β
Baada ya kumaliza kuplan ilibidi nimjulie hali Iryn nijue na maendeleo ya Ethiopia maana tangu tuachane ijumaa hatukuwa na mawasiliano. Nilimpigia simu na alisema nimpe dakika 10 atanipigia tuongee vizuri, kwani kwa sasa yuko jikoni anapika na mama yake mkubwa.
Niliendelea kuwaza pale kitandani kuhusu Iryn na niliona kwa sasa sitakiwi kumkera ili nifaidi matunda kutoka kwake. Kipindi tuko Airport alinambia anataka tufanye biashara nyingi hapa Tanzania ila tatizo langu, nina mambo mengi na hiki ndo kina mpa wasiwasi.
Baada ya dakika 10 ainipigia simu na nilipokea tukaanza maongezi;
MIMI: βNambie mke wangu unaendeleaje?β
IRYN: βNiko poa darling, nilikuwa napika nikashindwa pokea simu yako.β
MIMI: βUsijali mummy ni nini kinaendelea huko?β
IRYN: βBaby, jana tumeongea na mamkubwa kuhusu hili, nimemwambia hii mimba mhusika ni wewe butβ¦β
Nilimkatisha maongezi yake,
MIMI: βBut what?β
IRYN: βMamkubwa kalipokea negatively na amechukia sana jana mpaka sasa namwona bado kamind.β
MIMI: βNiliona hili mapema na nilikwambia.β
IRYN: βMamkubwa amemind kubeba mimba bila utaratibu, afu sijatoa taarifa mpaka mimba imekuwa kubwa.β
MIMI: βSasa mmefikia wapi?β
IRYN: βLeo ilibidi tuwe na kikao cha familia na ndugu wa upande wa mama, lakini imeshindikana mpaka jumanne sababu uncle hayupo.β
MIMI: βSawa mummy, ila usithubutu kuwaambia kuwa hio mimba wewe ndo uliamua kuibeaba itakuletea shida ni bora useme ilikuwa bahati mbaya.β
IRYN: βSawa baby, niko very smart kwa hili sitokuangusha.β
MIMI: βBye and takecare.β
****
Jumatatu nilihitajika kwenda ofisini mapema ili nikaonane na dada mfanyakazi mpya ambaye aliletwa na mama. Hilda alikuwa kanipa feedback kuwa yuko vizuri, lakini nilitaka na mimi nijithaminishe kama anafaa au laah.
Saa 3 asubuhi ndo nilikuwa nawasili pale ofisini na baada ya kuingia ndani pale reception kulikuwa na dada amekaa, nilimsalimia na nikaenda ndani ofisini. Baada ya dakika 10 Hilda alikuja kunipa taarifa kuwa dada amefika muda na alikuwa akinisubiri mimi ili tuongee naye na nikamwambia amuite.
Dada ambaye nilimuona pale reception ndo aliingia ndani muda huu maana mimi kipindi naingia nilijua atakuwa ni mteja. Nilimsalimia kwa mara nyingine tena na maongezi mengine yakaendelea kuhusu kazi na mimi nilitaka kujiridhisha. Na niseme kwenye upande wa kuchagua na kuzingatia standards, mama Janeth yuko vizuri sana, maana dada alikuwa yuko vizuri sana.
Kutokana na nature ya biashara yetu huwa tunahitaji kuwa na wafanyakazi wenye muonekano mzuri wa sura mpaka maumbile na kingine ni umri. Tunahudumia watu wenye hadhi na wengi ni foreigners wanaofanyia kazi kwenye organizations tofauti, makampuni na mabalozi mbalimbali hapa nchini.
Aina ya wateja tunaowahudumia ndo inapelekea kampuni kuhitaji kuwa na wafanyakazi wenye standard, wanaovutia na wenye muonekano mzuri wa kutoa huduma kwa wateja wetu.
Baada ya kujiridhisha na dada, nilimpa Hilda mamlaka ya kuendelea kumpa training na maelekezo mengine kuhusu kampuni, pamoja na kumpa mkataba wa kazi.
Mchana mzee wangu alinipigia simu kuwa yuko mkoani na anatarajia kuja Dar kesho mapema, hivyo lazima tuonane na atakuja home kuisalimia familia yangu.
Zilikuwa ni taarifa njema kwangu, ukizingatia ni muda mrefu ulikuwa umepita bila kuonana na mzee. Nilipanga nikirudi home badae nitampa taarifa mama J ya kuwa na ugeni kwa siku ya kesho, ikiwezekana hata chuo asiende.
Kama nilivyo waambia nyuma kwamba mzee wangu yuko Zambia ndo anafanyia kazi huko kwenye moja ya kampuni kubwa ya engineering. Sasa mara nyingi anakuja Tanzania kwa kuvizia sana na hata akija huwa hakai sana, kutokana na nature ya kazi yake.
Nilitoka kwenda kuonana na Sumaiya pale ofisini kwake na tuliishia kupiga story nyingi sana, kubwa alisema kidogo anajitahidi kuendesha gari na kufika mwisho wa mwezi atakuwa fiti. Nilimuomba aniazime gari yake kwa muda na alinikubalia bila kuwa na kinyongo na alisema tuongozane twende kwake tukaichukue.
Tuliongozana kwenda kwake kuchukua gari maana hakai mbali sana na Masaki, episode za nyuma niliandika anakoishi. Baada ya kuchukua gari tulipitia filling station, nikajaza wese full tank na nilimuachia gari aendeshe ili nipime uwezo wake.
Tulikwenda barabara za kule oysterbay maana hazinaga mwingiliano mkubwa wa magari na ni rahisi kumfundishia mtu. Sumaiya alikuwa bado ni lena kabisa na nilimpigisha kwa masaa 2 straight na kidogo alianza kuonesha improvement.
Baada ya kumaliza zoezi letu tulipitia Salt tukapata lunch ya kuchelewa maana muda ulikuwa umekwenda sana, saa ilikuwa inasoma ni 10 za jioni.
Tulirudi ofisini kwake kukaa na nilishinda pale mpaka usiku na hii siku tulizungumza mambo mengi sana na Sumaiya. Alisema kuna jambo kubwa siku atashare na mimi, nilijaribu kumbana sana, na yeye aliishia kusema niwe mpole atanambia.
Licha ya yote Sumaiya ni moja ya watu wangu muhimu sana ni kama ndugu kwangu, ukiacha matani yake anajua sana kuongea point pale ambapo mnakuwa serious.
Jumanne ndo siku ambayo mzee alikuja Dar, saa 4 asubuhi alinipa taarifa kuwa yuko Dar tayari na ikiwezekana saa 6 mchana tuonane pale Mwenge. Mimi nilikuwa ofisini na baada ya kutimia 11:30 nilianza safari ya kutoka Masaki kwenda Mwenge kuonana na mzee.
Mzee alikuwa Puma filling station akinisubiri kwenye gari ya rafiki yake na baada ya kuonana tulianza safari ya kwenda home Mbezi beach. Tukiwa njiani tulikuwa tunapiga story mbalimbali za kuhusu maisha na huko Zambia kwa ujumla na yeye alisema kuna siku atanitumia nauli ili niende huko nikatembee.
Baada ya kuwasili home kwa upande mwingine pale nje alionekana Elena na Junior wakicheza na mzee baada ya kumuona mjukuu wake alimbeba. Muda huu Junior alikuwa anafurahi tu, na tangu Junior azaliwe mzee hakuwahi kumwona live zaidi ya kumuona kwa picha tu.
Baada ya kuingia ndani wife alikuja pale seblen kuonana na mzee pamoja na kumkaribisha na alianza kuandaa chakula cha mchana na alitukaribisha.
Tuliongea mambo mengi sana kuhusu maisha na alisema badae anatarajia kuondoka kurudi Zambia na kilichomleta Dar ni kuja kunisalimia kijana wake wa kwanza pamoja na familia yangu.
Mzee aliulizia kuhusu suala la ndoa tumefikia wapi na ni lini tumeplan kufunga? maana muda unakwenda sana tangu tuchumbiane. Mzee ni muelewa nilimchana suala la ndoa bado tunajipanga, mpaka mama J amalize chuo ndio tutaanza na mipango ya ndoa.
Saa 11 jioni mzee alisema tuondoke tusogee maeneo ya karibu na Mwenge huku akimsubiri jamaa yake waondoke kwenda zambia. Kabla ya kuondoka alitoa bunda la pesa lenye thamani ya tshs million moja na akampa wife kwaajili ya Junior.
Tuliamua kwenda kutulia pale Mlimani city Samakisamaki tukimsubiri jamaa yake, huku tunapiga vinywaji taratibu na story kwa sana. Mzee kwa upande wake alinipa hongera za kuweza kupambana na maisha ya Dar na kufanikiwa maana sio rahisi. Pia, alinipa wosia wa kuhusu maisha na alinisihi sana nitulie na mama J maana hatapenda kusikia nina chepuka na wanawake wengine pembeni.
Mida ya saa 12 jioni tuliachana maana jamaa yake alikuwa akimsubiri waondoke kwenda Zambia na kabla ya kuondoka alilipa bill zote na tukagaana pale.
Mimi niliendelea kukimbiza chupa zangu taratibu na nilikuwa nawaza kuwasiliana na Iryn ili nijue wamefikia wapi kwenye kikao walichokaa. Muda huu walionekana warembo mbalimbali wakirandaranda maeneo haya na asilimia kubwa walikuwa ni waviziaji tu.
Nilipata wazo nikamtembelee Prisca nyumbani kwake changanyikeni ili nijue na maendeleo yake kwa ujumla, ukizingatia ilikiwa ni muda hatuja onana.
Saa yangu ilikuwa inasoma ni saa 2 za usiku, hivyo nilikwenda kwanza Shopperz kununua mazaga ya kumpelekea ndo nikaanza safari ya kwenda kwake. Nilitaka iwe suprise ndomana sikutaka kumpigia simu maana nilijua lazima nitamkuta kwake kwa siku za katikati ya wiki.
Baada ya kuwasili pale kwake, nilishaozea huwa nina fungua geti nakuingiza gari ndani, ila sasa ni muda mrefu nilikuwa sijakwenda pale niliona nimpigie simu. Niliamua kumpigia simu ili anifungulie geti, ajabu simu zangu 3 nilizopiga hazikupokelewa ila Roho ilikuwa inanambia huyu yuko ndani, labda amelala.
Nilipark gari pembeni vizuri ili wengine waweze kupita na nilisogea mpaka getini na kwa mbali nilimuona jirani yake ambaye namfahamu na alikuja akanifungulia geti. Tulisalimiana maana ilikuwa ni kitambo sana hatujaonana na alinambia kamuona Prisca dakika 40 zilizopita akianua nguo zake.
Nilisogea mpaka usawa wa apartment yake na kwa mbali nilikuwa naisikia sauti ya TV ambayo ilikuwa kwa chini sana, taa ya seblen ilikuwa imewashwa pia.
Niligonga geti kwa sarafu β
Nke! Nke! Nke!β na nilimkia akisema β
Karibuβ na akatoka kufungua mlango. Nafikiri kwa mawazo yake alikuwa anajua ni jirani, sasa ile kuniona ni mimi alishtuka sana na alionekana kuanza kupatwa na wasiwasi, ofcourse nilikuwa nikishuhudia mabadiliko yake pale;
PRISCA: βInsider, usiku huu?β
MIMI: βKuna shida? Saa 3 hii bado mapema sana au nimekuja muda mbaya?, nifungulie bhasi niingie ndani.β
Nilimuona Prisca akisitasita kufungua geti na mimi nilijiongeza nikajisemea hapa kuna kitu hakipo sawa, acha nimpe mzigo wake niondokee.
βNaona unasitasita na hujiamini, sikujua kama nimekuja muda mbaya, fungua geti nikupe mzigo wako mimi niondoke, ndani siwezi kuingia tena.β
PRISCA: βInsider sijamaanisha uondoke.β
MIMI: βWhy take so long?β
PRISCA: βSijategemea ujio wako muda huu na simu hujanipigia.β
MIMI: βAngalia simu yako nimepiga mara ngapi? Na mbona excuse zimekuwa nyingi sana leo?.β
Alifungua mlango na akapokea vile vitu, sasa wakati namuaga, nilimuona dogo jamaa akitokea chumbani kwake,
MIMI: βOhh! Kumbe ndomana unakuwa mgumu kufungua mlango, mimi naondoka sijaja hapa kukuharibia na sikujua kama una ishi na mtu humu ndani maana hujanipa taarifa, naomba nisamehe kwa hili.β
Muda huu jamaa alikuwa kafika pale getini na alikuwa kasimama nyuma ya Prisca, alikuwa ni mtu ambaye anataka kujua kinachoendelea pale.
Niliwaza kwa haraka kuendelea kubaki hapa ni tatizo acha niondoke tu kabla hali ya hewa haijachafuka maana nilikuwa nimeingilia code za watu tayari. Muda huu Prisca alikuwa kanyamaza kimya, nilimuaga na nikaondoka zangu eneo lile, ile nataka kuwasha gari nilisikia geti likifunguliwa na alianza kuja speed usawa wa gari na nilishusha kioo;
PRISCA: βInsiderβ¦ subiri.β
MIMI: βUnafanya nini huku nje?β
PRISCA: βYule sio mtu wangu bhana, amekuja tunajisomea wote.β
MIMI: βSio mtu wako na ametokea chumbani kwako serious? Afu sijui kwanini una wasiwasi, mimi sina shida ni vile nimekuja bila taarifa na nimefurahi kuona ume move on.β
PRISCA: βKweli sio mtu wangu, kesho tuna test ndomana.β
MIMI: βUsimkatae boyfriend wako sio vizuri, kama anakupenda kweli tulia naye na usiwe na wasiwasi, ushikaji wetu utaendelea kama kawaida hili ondoka shaka.β
PRISCA: βSiwezi kumove on kama wewe bado upo hai, nimeshindwa kwa hili naomba niwe mkweli, sitamani kuwa na mwanaume yoyote yule.β
MIMI: βNenda ndani kuendelea kuwa hapa na boyfriend wako yupi sio vizuri, tutawasiliana.β
PRISCA: βNaomba ijumaa tuonane Insider.β
MIMI: βSawa nitakucheki Mummy, usiku mwema.β
Tuliagana pale na nikaondoka kurudi home, ukweli kwa lile tukio la Prisca kiaina nilipata kawivu, hasa pale napokumbuka utamu wake ndo nilikuwa nazidi kuumia, kwa upande mwingine nilifurahi kuona amemove on.
Baada ya kufika home sikutaka kuingiza gari ndani, hivyo nilipark gari pembeni ili niongee kwanza na Iryn nijue kinachoendelea maana alikuwa bado hajanitafuta kabisa na hii ndo ilikuwa inanipa wasiwasi.
Nilimpigia simu na baada ya kupokea hatukuongea sana ila alisema tutaongea kesho vizuri alikuwa kalala tayari. Habari kubwa aliyosema ni kwamba maamuzi yaliyochukuliwa na familia yake ni magumu sana na sijui kama mimi nitayaweza na hili ndo linampa mawazo kwani anajua fika mimi sitowezaβ¦.
CHAPTER 18
chini ya comments za watu inaonesha watu ambao wanawatch thread husika kwa mda huo. asante