kip-korir
JF-Expert Member
- Sep 5, 2023
- 309
- 500
KONGOLE kwako INSIDER MAN kwa kupata kijana mwengine kutoka kwa irene. Pamoja na kukiuka kanuni za kawaida za maadili, sina budi kukupongeza kwa kumpata mwanamke anayekupenda maana L O V E utayashinda yote yatakayotokea. BARIKIWA pia kwa kutupata uzoefu wako maishani. mimi ambaye nakaribia kwenye 50 niaona ulivyokuwa na ubongo mkali darasani na katika maisha. sisi tume toil sana kufika hapa tulipo kutokana na kutokuwa na maono na bahati ya kuzaliwa katika familia ambayo tayari imesimama (namaanisha familia ambayo haiwazii mahitaji matatu makuu-malazi,mavazi na chakula). Kila unapopambana, wazo linakujia kule villa bado hapajarekebika, Baba na Mama hawana mavazi, dogo hajalipiwa ada, kaka mkubwa anaumwa anatakiwa kupelekwa matibabu yaani ni msururu wa majukumu na ukiacha kuya attend nafsi inakusta mno.We are lucky to welcome our second baby, a boy, and we have named him Adrian.
Kwa hiyo wenzetu mliozaliwa na working class kidogo mnao unafuu wa kufikia viwango vya juu kimaendeleo kutokana na kutokuwa na pulling back strings. Hata hivyo, vijana wa 2000 bado wanayo kazi ya kufanya kuuepuka ujinga wa teknolojia mpya ya simu na social media. Simu na social media ndiyo utumwa mpya ambao mzungu anatutumikisha nao muda huu. Tujitahidi kuushinda huu uraibu ambao ni mbaya kuliko utumwa wenyewe.
yote kwa yote Kongole tena kwako INSIDER MAN


