EXTRA EPISODE 07
BY INSIDER MAN
Biashara ya Uber ni moja ya biashara nzuri sana maana inakukutanisha na watu wengi sana wenye hadhi āstatusā tofauti, foreigners, matajiri na maskini nknk.
Hii biashara niliiacha baada ya kifo cha Mzee Pama kwasababu ya kumuenzi kifo chake, Pama nilikutana naye kupitia hiihii Uber. Kwasasa hii biashara naifanya kwa kuajiri vijana na ninazo Uber mbili na dereva zangu wanafanya vizuri sana hakuna ujinga wanaofanya na wale wateja zangu wote nimewaunganisha nao.
Hii biashara imenikutanisha na watu wengi sana niwe mkweli, wengi sijawaandika kabisa kwenye hii story na wengi wao bado tuna wasiliana sana maana walikuwa wateja zangu na wana niamini. Nimekutana na watu wengi sana kupitia Uber kama watu maarufu, celebrities, wanasiasa nk, kipindi nafanya hii biashara na ndo iliyonipa connections na kutoboa maisha.
Just imagine bila Uber nisingekutana na Iryn, Mzee pama, Jane, Mzee Juma, Mama wa2, Mama Janeth, Sumaiya, Lucy, Prisca na Mary nknk. Kupitia Iryn ndo niliwajua hao wengine wote, kupitia Pama nilimjua mzee Juma na Jane. Hapo unaona connection moja inafungua au inaongeza connection zingine.
Dunia hii jinsi inavyokwenda tajiri rafiki zake ni matajiri, maskini rafiki zake ni maskini, dereva rafiki zake ni madereva, mfanyabiashara rafiki zake ni wafanyabiashara, vivyohivyo kwa mkulima, mwalimu, mwanafunzi, mlevi nknk.
Sasa kama wewe maskini ufanye nini ili uweze kukutana na matajiri? kwa mtizamo wa haraka utaona ni ngumu but ni very simple, the question is how?.
Ukifuatilia kwa makini utagundua matajiri wanaingia sehemu expensive na zenye thamani kama hadhi yao, ni ngumu sana kumkuta tajiri anakula kwa mama ntilie ni kitu ambacho hakiwezekani. Matajiri wengi utawakuta wakienda kupata lunch/dinner kwenye mahotel makubwa kama Serena, Hyatt, au kwenye migahawa mikubwa na ya kisasa.
Siku mojamoja jenga utaratibu wa kutembelea haya maeneo hata sio ghali kuingia kupata dinner au lunch ni vile uoga wetu. Nenda viwanja vikubwa kama Samakisamaki nknk huko utakutana na watu wenye hadhi tofauti, mtu anayeingia Samakisamaki actually hata kipato chake si kidogo. Na ukienda maeneo kama haya kuwa mtu wa kujichanganya usipende kukaa kivyako vyako hii itakusaidia kupata watu wapya. Kwa upande wangu toka nianze kwenda haya maeneo nakutana na watu wengi sana tofauti na wana status nzuri sana.
Maeneo ya hadhi kama haya ukiingia, ukakutana na mtu yoyote kwanza atakuheshimu ataona wewe si mtu wa kawaida. Ukijenga tabia ya kutembelea haya maeneo naamini utapata connections nyingi sana na utakutana na watu wenye hadhi.
Biashara ya Uber pia ni sehemu ambayo ni rahisi sana kukutana na matajiri sababu asilimia kubwa ndo usafiri wao, mtu kama anatoka point A to B ni ngumu kutumia usafiri wake ataishia kurequest. Kama Dereva uwe unapiga nao story hawa watu acha kujikuta kauzu msome kwanza mteja ukiona ni talkative anza kupiga naye story, hii itasaidia kufungua milango mingine.
Kwa upande wa Posta/Masaki kuna ofisi nyingi sana na utawabeba Ma-Hr, Managers, C.E.Oās nknk, jitahidi uwe unafanya engagement nao usiwaogope, tengeneza connection. Mimi Insider ningekuwa nataka kuajiriwa kipindi kile bhasi ningekuwa nilipata kazi muda sana.
Cheki conversations yangu na moja ya mteja niliyekutana naye Posta,
INSIDER: āBossy wangu naona umependeza sana na pigo za Ki-HR.ā
CUSTOMER: āMhh kaka naonekana kama HR?ā
INSIDER: āExactly nambie kama nimekosea.ā
CUSTOMER: āHahaha hamna bhana, mimi ni mtu wa kawaida tu mbona.ā
INSIDER: āOoh sawa kama kweli wewe ni HR naomba connection ya mchongo, napambana na Uber angalau mkono uende kinywani, lakini huku ni kugumu sana.ā
CUSTOMER: āJamani lakini sio mbaya Mungu atakusaidia, una elimu gani kaka?ā
INSIDER: āNina degree ya Uchumi naweza kuisaidia kampuni kwenye mambo mengi sana, kama itatokea chance naomba nikumbuke bossy wangu.ā
CUSTOMER: āKaka usijali utanipa namba yako afu utanitumia na CV kabisa incase imetokea nafasi nikupambanie.ā
Sasa ukituma CV kwa watu 20 hapo unakuwa na Probability kubwa ya kupata mchongo na ukiwa na qualifications nzuri, kutoboa ni haraka sana. Hawa watu wamenitafuta sana honestly, na last week kuna dada kanipigia simu nilimtumiaga CV mwakajana nilikuwa nimemsahau, sasa kanipigia simu ili anipe connection lakini nilimwambia nimerudi shule kusoma. Unaona ni muda mrefu lakini still alikuwa na CV yangu akanikumbuka, mimi nilikuwa nimesahau kabisa.
Suala la kupata wateja Private ni juhudi zako za kupambana na kuwa mbunifu, kumbuka Uber ni biashara na mpo wengi na wengi gari zao ni nzuri, inabidi uwe mjanja sana kuwapata hawa wateja wa Private.
Ukiwa smart unajiweka vizuri, gari yako ni safi nje na ndani, gari full AC na inanukia vizuri. Naamini huwezi kosa wateja wa private na asilimia kubwa ya wateja utakao wapata ni wanawake, kingine cha muhimu mtangulize Mungu pale unavyotaka kwenda mzigoni, just pray.
Mteja mpaka anaamua kukutumia private anaangalia vitu vingi sana kutoka kwako ukiachana nakuwa na gari kali, pia customer care nayo ni muhimu sana ili kuwavutia. Wanaume hawana shida ila kwa dada zetu wanapenda sana ukiwapa customer care nzuri sana, pamoja na kuwasifia sifia yaani wanapenda sana.
Kitu kingine ambacho Uber wanafeli sana, unakuta umemchukua mteja kutoka Posta kwenda Masaki. Baada ya kumdrop unamwacha aende badala ya kumuuliza kama anarudi tena Posta ili umrudishe wewe unamuacha aende kwa hapa mnafeli sana, wengi wenu mnapishana na hela.
INSIDER: āDada samahani unarudi tena Posta? ili nikusubiri?ā
CUSTOMER: āYes narudi ila nitachelewa kidogo, kuna customer namuattend.ā
INSIDER: āUnaweza tumia muda gani maximum.ā
CUSTOMER: ā30 minutes maybe.ā
INSIDER: āMimi nitakuwa around kama utakaribia kumaliza just text me nianze kusogea.ā
CUSTOMER: āSawa usijali.ā
30 minutes sio nyingi kwa kumsubiri customer maana kuna muda request zinakuwa shida afu biashara ni ushindani sana, lazima uwe mjanja na mbunifu. Kumbuka pia sio kila mteja atakwambia umsubiri ni wewe ujiongeze tu, sasa mteja kama huyu ukimrudisha Posta lazima atasave namba yako na ataanza kukutumia.
Kingine ukimshusha mteja kwa destination ongea naye kama atakuwa na kazi Private awe anakutumia, tengeneza na Business card zako unakuwa unawapa wateja. Ukiwapa wateja 30 business card yako kuna ambao watakutafuta tu mfanye kazi, na kumbuka ukifanya kazi na mmoja anafungua baraka ya kukuunganisha na wengine, circle yako inazidi kutanuka inafika stage unawateja wengi.
Mimi binafsi kuna stage ilifika hata Uber nikawa siwashi, yaani ile asubuhi nikiwa drop akina mama wa2 na Maggy, unakuta nina booking ya kufanya kazi na loan officers na hapo inakuwa kazi ya siku nzima.
Nilifanya kazi na hawa loan officers wa CRDB, NMB, EXIM, KCB nknk ni wengi mno nimefanya nao sana kazi, na wao kwa wao ndo walikuwa wanapeana connection wananitafuta. Malipo yanakuwaga kwa card ila sasa ikitokea wamepiga mshindo walikuwa wananipa sana hela.
Ukija kwa mtaani wengi walikuwa wananitafuta si unajua wanawake hawapendagi shida? Kama anasherehe bhasi atanitafuta tunakubaliana bei ya siku nzima afu tunafanya kazi, Dullah nilimpa connection ya mtoto wa bank na baadae kaja kuwa mke wake halali.
Nimefanya kazi nyingi sana yaani kuna muda nilikuwa napiga pesa mpaka ukiniletea story za kuajiriwa nakuona mchawi. Narudia tena kama upo smart ukifanya uber unapata kazi kwa haraka sana na maana utakutana na watu wengi wenye status tofauti.
Kitu kingine cha muhimu kwenye Uber ni uaminifu hata ukiona kitu cha thamani mteja amekisahau wewe mrudishie itakupa sifa nzuri sana. Nimekutana na simu nyingi sana kwenye gari wateja wamesahau, wallets, pochi nknk lakini nilikuwa nawarudishia kwa uaminifu na sikuwahi kuwa na tamaa.
Kitu kingine usikatae request hata kama mteja anakwenda sehemu ya mbali kama upo kazini wewe nenda cha muhimu ongea na mteja muone mnasaidianaje maana yeye anataka usafiri wewe unataka Pesa. Kama ni usiku na mteja anaingia ndani ndani sana, mchukulie bodaboda kwaajili ya usalama wako na uwe makini sana hasa kwa nyakati za usiku.
Huwa nawashangaa sana madereva wa Uber wanaolalamika kuwa biashara ni ngumu kwakweli huwa siwaelewi kabisa, kwa mwaka jana wakati Vita ya Russia/Ukraine imeanza kupamba moto kweli biashara ilikuwa ngumu sababu nauli zilipaa sana, ila kwa dereva wa Uber kutegemea request ni umaskini wa akili. Tumia Uber kukupa connections za kupata wateja wa private na sio kutegemea requests hapa utafeli tu na kuishia kulalamika biashara ni ngumu.
Jambo lingine madereva wa Uber 80% hawajatulia ni malaya, sasa ukiendekeza pussy hesabu maumivu, utaishia kuwapakia mademu bure kila wanakokwenda. Mademu wa Dar wajanja sana they know hot to manipulate a Man, hapo akikupata ana uhakika wa free Uber ya kumpeleka kwenye mishe zake. Hii tabia mpaka madem waliojariwa wanayo maana akikupata ana uhakika wa usafiri wa asubuhi, hakuna dem anayependa kupanda daladala asubuhi na kubanana hakuna.
Utakutana na mademu wengi sana kwenye hii biashara ila ukikosa self control utaishia kutembea nao na kuwagongea kwenye gari. Asilimia kubwa ya madereva wa Uber gari zao ni guest, nyie mnaotumia huu usafiri kuweni makini sana. Hawa jamaa wanagongea mademu au mashoga humo humo ya gari, usipendelee kukaa seat za nyuma ni hatari sana.
Umaskini ni mbaya sana ndugu zangu maana utakuwa unakubali kushawishika kwa vitu vidogo, sahivi mashoga asilimia kubwa wanaliwa na madereva wa Uber sababu ya njaa. Hawa watu sijui wanatoa wapi pesa kwakweli, lakini ndo kwanza wanakaa sehemu nzuri kama mbezi Beach, Mikocheni nknk.
Ukiwapakia hawa watu ni wasumbufu sana wata kutongoza sana, nimekutana nao sana hawa watu na wengi wamenisumbua sana mpaka kero, kukuwekea offa ya laki 5, million kwao ni kawaida. Sasa kwa dereva ambaye ana njaa hapa hatoboi ataishia kuwala tu, bad news mpaka mastar nao hamna kitu, kuna msanii huwa siamini kama na yeye ni chakula yaani daah! hali ni mbaya sana. Kuna presenter maarufu kanisumbua sana na niliishia kumblock lakini bado akaendelea kunitafuta kwa namba nyingine, mpaka nikamwambia nitaavujisha chats zako ndo akatulia ila hali ni mbaya sana Mungu atusaidie.
Ukiwa HB na unajipenda hawa wanawake watakutongoza sana na hasahasa wamama wanasumbua sana āmashangaziā. Mademu watakusumbua sana, nyakati za usiku utapakia mademu ambao hawajielewi wamelewa na kama unatamaa utaishia kuwala.
Dar ni mkoa mchafu sana hasa kwa nyakati za usiku, ukitaka kuamini hili wewe jaribu kutembelea maeneo ya Sinza, Masaki ndo utaona ushenzi unaofanyika. Nyakati za usiku kwa Sinza mashoga kibao wanazagaa, Masaki kuna Malaya wengi sana. Kwa Mbweni ukisikia illegal issues ndo ziko huko kama sembe, utapeli bhasi huko ndo HQ yake kwa hapa mjini. Hii Dar ione hivihivi lakini ni chafu sana, mimi Dar naijua yote hakuna kitu utakacho nidanganya na ninazifahamu chocho zote.
Mimi nilikuwa natafuta hela na sikuzote pesa utazipata kwenye mambo ya hovyo, mfano mimi nilikuwa na connection za kuwapata madem wa kizungu, kichina, kihindi nknk, kupitia Masai-Ellias na pia kuna chocho ziko Posta unawapata wazungu ni hela yako tu. Mfano madem wa kizungu minimum Price wanacharge kuanzia $300 mpaka $1,000 inadepend na quality ya mwanamke, hapo ukimuanganisha kwa tajiri hukosi hata $100-200 ya kuweka mfukoni. Mimi nashida gani? kwenda kumchukulia foreigner demu na kumplelekea hotelini na kujipatia $100 kuna kazi hapo?.
Ukiwa kwenye hio biashara utakutana na vishawishi vingi sana ukiachana na mademu, pia kuna vishawishi vya kuingia kwenye dili za kikubwa kama sembe, kusafirisha wazamiaji nknk, point hapa kuacha tamaa maana unaweza ambiwa kila kichwa cha mzamiaji ni 2M afu uwapeleke Bagamoyo hapo ukipiga hesabu una 10M, ni wachache ambao wanaweza kuikataa hii offa.
Ishu ya mwisho na muhimu kwa Dereva wa Uber ni kuzingatia usafi wako binafsi, vaa pendeza chomekea kama vile unakwenda ofisini, pulizia na unyunyu wako freshy. Kwa weekend mimi nilikuwa nakula pamba safi nimetupia jeans na t-shirt afu chini nina raba yangu kali freshy.
Usishangae haya mambo kazi ya Uber ni ngumu sana na inataka moyo, wapo watakao kudharau, kupewa kejeli ni jambo la kawaida sana, muhimu hapa wewe mind your business usipende kubishana au kugombana na wateja itakucost, kubali kuonekana mjinga ila kwa faida yako.
Katika vitu ambavyo nilijitahidi sana kuvizuia ni pamoja na wife kupanda ile Ist, maana niliona natengeneza mikosi kwa mke na mtoto. Ndomana nilikuwa nikirudi break ya kwanza ni bafuni kuoga kutoa nuksi ndo mambo mengine yaendelee, lingine nilikuwa najitahidi sana kufanya usafi wa gari.
Biashara ya Uber ni rahisi sana kukutana na watu wapya na kupata Connection nyingi sana kama utakuwa smart. Maana huku ni easy kukutana na foreigners, Celebrities , pisi kali nknk. Just assume wastani kwa siku unabeba abiria 10 mara 30= 300, zidisha mara miezi 12= 3,600. Huu ni wastani tu nimetumia, sasa kwenye hawa watu 3,600 utakosa connection hapa???.
Dereva wa Uber ukilalamika Biashara ngumu bhasi jua wewe upo kundi hili,
1. Unategemea request tu
2. Umeendekeza Mademu/Starehe
3. Hujiongezi.
Wewe utaishia kulalamika Biashara ngumu.
insiderman1@yahoo.com