Umetukaushia mazimaHamjambo?
NakupendaHatimaye😎
SEASON 03
CHAPTER 1
A TRUE STORY BY INSIDER MAN
Inaendelea ilipoishia Season iliyopita:
Baada ya kuwasili Dar es Salaam, nilijikuta nikihitaji muda wa kutulia kabla ya kuendelea na safari nyingine ya Dodoma. Nilielekea moja kwa moja BAO Café, iliyopo ndani ya Terminal 3, nikajipatia kikombe cha kahawa ya moto huku nikijaribu kupunguza uchovu wa safari. Hali ya ukimya ilikuwa imetanda sana katika aneo hili hata zile movement za abiria zilikuwa kama zimetulia kwa muda.
Muda huu nilikuwa kwenye dimbwi kubwa la mawazo kuhusu hatima yangu na Iryn pamoja na mtoto. Nilijikuta nikirudi nyuma, nikikumbuka misukosuko yote tuliyopitia pamoja hadi kufikia hatua ya yeye kujifungua. Kila kumbukumbu ilikuwa ni muhimu kama sinema inayoendelea kucheza akilini mwangu.
Lakini zaidi ya yote, nilianza kuwaza kuhusu hatua zinazofuata. Nilihisi kuna kitu muhimu sana kinahitaji kufanyika mapema-kuhakikisha wanangu wanajuana, wanajenga ukaribu na kutengeneza bond ambayo itadumu maisha yao yote hata mimi nisipokuwepo. Niliwaza kwamba Bond ya watoto inatengenezwa wakiwa bado watoto maana wakishakua wakubwa ni ngumu sana kuwa na umoja na ushirikiano. Nilijiona nina hatia kubwa sana ya kuhakikisha hili linafanikiwa kwa njia yoyote ile, ingawa ni jambo ambalo lilionekana kuwa gumu sana kufanikisha.
Simu yangu ilianza kuita ghafla kupitia WhatsApp. Nilipoangalia, niliona ni yule agent niliyezungumza naye jana kuhusu tiketi ya ndege ya kwenda Dodoma. Nilijua hii inaweza kuwa habari muhimu ukizingatia nilikuwa nasubiri tiketi, nikapokea haraka.
Agent alinieleza kuwa amefanikiwa kupata ticket ya ndege na alinihitaji nifanye malipo mapema na nisogee karibu na eneo la tukio ili kuendelea na taratibu nyingine. Nilijikuta nikitabasamu kwa sababu ilikuwa habari nzuri sana. Sikutaka kumshirikisha dada Tyna, sababu kubwa ilikuwa sitaki ajue mambo yangu na kuanza kuniuliza maswali. Zaidi ya hapo, dada yangu alikuwa amenishauri kwamba nikirudi Dar niwe makini na hata nisijaribu kuonana naye.
Muda huo huo nilitumia kubadili fedha ili nipate noti za Kitanzania. Bila kupoteza muda, nikafanya malipo ya tiketi na kuanza kusogea taratibu kuelekea Terminal 2, nikikokota begi langu mdogo mdogo.
Baada ya kufika Terminal 2, nilimpigia dada yangu simu kumjulisha kuwa tayari nimewasili Dar es Salaam. Wakati tulipokuwa Cape Town, tulikubaliana kwamba atakuja Dar kwa ajili ya kuweka mambo sawa kati yangu na mama J. Hata hivyo, bahati mbaya hakuwa online, hivyo niliamua kumtumia ujumbe mfupi wa taarifa.
Kwa upande mwingine, wakati bado nikiwa Airport, Iryn alinipigia video call. Lengo kubwa lilikuwa kuhakikisha kama nimefika salama.
IRYN: “Baby, naona bado upo Airport… ndo umewasili?”
MIMI: “Nimewasili saa moja iliyopita, lakini nilikuwa nasubiri tiketi ya kwenda Dodoma,” nilijibu kwa utulivu.
IRYN: “Baby, Dodoma kuna nini tena?” aliuliza kwa ukali, akionekana kushangaa.
MIMI: “Ni muda mrefu sana sijaenda kufuatilia miradi yangu, hata sijui maendeleo yake. Bora niende sasa kuliko nirudi nyumbani, maana itakuwa ngumu kutoka.”
Alinyamaza kidogo kisha akavuta pumzi,
IRYN: Ok, sawa. Hakuna tatizo… ila najikuta nakuwa nina wivu sana na wewe. Tafadhali,… don’t cheat.”
MIMI: “Kwa nini nifanye hivyo? Nakupenda wewe tu na Aria.”
Tulitumia takribani dakika 20 tukiongea tu na baada ya kumaliza maongezi yetu tuliagana pale.
Kipindi nikiwa nasubiri kuondoka, sister alinipigia simu. Nilimjulisha kuwa tayari nimerudi Dar es Salaam, lakini nikamwambia kabla sijaenda nyumbani natakiwa nipitie Dodoma mara moja. Kwa upande wake alisema atakuja Dar kesho, siku ya Jumamosi, na akaahidi atanijulisha mara tu atakapoanza safari yake.
Safari ya kuelekea Dodoma ilipoanza, mawazo yangu yote yalielekea sehemu moja tu, kuhusu kampuni ya baba yake Iryn, ile ambayo wahuni walikuwa wameipora. Nilikaa kimya nikitazama nje ya dirisha huku akili yangu ikipanga hatua za kuchukua. Nilijua hili jambo halitakuwa rahisi, lakini nikajisemea lazima nifanikishe. Nilihisi hii ndiyo nafasi ya pekee ya kurudisha shukrani kwa Iryn kwa yote aliyonifanyia, ni kuhakikisha kampuni inarudi mikononi mwao na kuwapeleka wahusika wote mbele ya sheria.
Iryn hakutaka kumshirikisha mama Janeth kwenye suala hili. Alipendelea libaki siri kati yetu wawili, na kwa sababu hiyo alinipa baraka zote. Alinikabidhi nyaraka zote muhimu za kampuni ambazo zilikuwa ushahidi wa msingi, nilihisi niko kwenye nafasi nzuri ya kupambana na kesi hii.
Muda huu akili yangu ilikuwa makini sana huku nimefocus kwenye hili suala, kisha nikajua ninachopaswa kufanya, nilifikiri kuonana na kaka yangu ambaye ni mwanasheria. Yeye ni mmoja wa watu ninaowaheshimu na kuwamini sana, ni mtu ambaye kila ninapohitaji msaada wa kisheria ndiye wa kwanza kumfikia. Nilijua fika kupitia yeye, nitakuwa nimeanza safari ya kulipigania hili jambo kwa nguvu zote.
Baada ya kuwasili Dodoma majira ya saa 6 kasoro mchana, nilielekea moja kwa moja nyumbani. Nilipofika, ndipo nikakumbuka kuwa nilikuwa nimeacha funguo zangu Dar es Salaam. Nilijikuta nimesimama nje nikiwaza kidogo, kisha nikawaza kuwasiliana na Juma-yule dogo niliyempa makazi kwenye lile gheto ambalo nilifikia awali. Bila kusita, nilimuomba uber simu yake na nilipiga simu ofisini na nikaomba Juma aje home na funguo ya gheto lake.
Baada ya dakika kumi, dogo aliwasili nyumbani na kunikabidhi funguo za gheto ambalo nilimkabidhi awe anakaa (Gheto alilofikia Mary). Nilikuwa nimechoka sana na sikutaka mazungumzo marefu, hivyo nilimwambia aniache nipumzike kwanza na tulikubaliana kuwa tutakutana jioni ofisini kwa maongezi ya kina kuhusu biashara.
Kabla hajaondoka, nilimuomba anisaidie kubadilisha vitasa vya milango kwani sikuwa na namna nyingine ya haraka. Pia nilimwomba msaada wa kusajili laini ya muda kwa kutumia kitambulisho chake.
Jioni ilipofika, nilitoka kwenda kukagua miradi yangu. Nilianza na safari ya kwenda kuonana na dada wa dukani, na nilifurahi kuona kila kitu kikiwa sawa. Kwa upande mwingine, Dullah alikuwa msaada mkubwa sana kipindi nikiwa South, ndiye aliyekuwa akihakikisha mizigo inafika Dodoma kwa wakati. Tayari nilikuwa nimepanga nikirudi Dar, mtu wa kwanza kuonana naye atakuwa ni yeye, ili nimshukuru kwa yote.
Baada ya kuagana na dada, nilielekea moja kwa moja kwenye ofisi nyingine kwa ajili ya ukaguzi. Baada ya kushuka kwa bajaji, nilikwenda straight ofisini kwa Sanchi ili nimsalimie maana nilikuwa nimem-miss sana. Sanchi hakuwa na taarifa yangu ujio wangu Dodoma zaidi tulikuwa tunawasiliana kupitia whatsapp na nilimwambia niko South Africa.
Sanchi alikuwa anaongea na simu na baada ya kuniona alisimama na akaanza kuniangalia kwa makini ni kama alikuwa haamini macho yake na alitoa kelele ya furaha na kuja kunikumbatia kwa nguvu;
SANCHI: “Bossy! Ndo nini hivi kuja kimya kimya?”
MIMI: “Nilitaka nikusuprise au hujapenda?”
SANCHI: “Na ungekuta sipo?”
MIMI: “Ningekuja kwako kwa mara ya kwanza.”
Sanchi aliishia kufurahi huku akionesha tabasamu lake waziwazi;
SANCHI: “Kwanza hongera kwa kupata mtoto, hukunambia ni jinsi gani.”
MIMI: “Hivi sikukwambia?”
SANCHI: “Wewe huyo- hata message zangu hujibu kwanza.”
MIMI: “Ni wa kike boss wangu.”
SANCHI: “Hongera sana nioneshe hata picha nikaone jamani! maana katakuwa kazuri sana.”
Nilitoa simu nikampa aangalie picha za Ariana, kisha nikamuacha na nikatoka nje ili nikaendelee na jambo ambalo lilikuwa limenipeleka pale.
Nikiwa na vijana wangu tulizungumza masuala mbalimbali kuhusu biashara kwa ujumla na biashara ilikuwa ikienda vizuri. Baadae tulishauriana kufanya baadhi ya marekebisho kwenye ofisi ikiwemo kununua baadhi ya mashine kubwa na za kisasa ili kuongeza ufanisi wa kazi zetu. Ukweli ushauri wao ulinigusa, maana ulikuwa ni mzuri sana ukijikita kuleta mapinduzi na maendeleo ya biashara yetu.
Baada ya mazungumzo ya kina na vijana wangu, nilipita kumuona dada niliyemuajiri kama cashier. Yeye ndiye anayehakikisha fedha zinapokelewa kwa usahihi, risiti zinatolewa, na taarifa zote muhimu za ofisini zinaandaliwa kwa umakini. Nilijisikia fahari kuona jinsi alivyokuwa anasimamia majukumu yake kwa ustadi.
Baada ya kuridhika na kila kitu, nilielekea tena ndani kwa lengo la kuonana na Sanchi, nimshukuru kwa jinsi alivyonisimamia ofisi kipindi nikiwa South.
SANCHI: “Insider mtoto wako ni mzuri sana, mpe hongera sana Iryn.”
MIMI: “Usijali zitafika japo hana imani na wewe”
SANCHI: “Kwanini?”
MIMI: “Anasema hakuna mwanaume asiyependa makalio, anaamini labda kuna siku nitashawishika juu yako!”
Wote tulianza kucheka pale…
SANCHI: “Pamoja na uzuri wote alio-nao bado hajiamini?”
MIMI: “Adui wa mwanamke ni mwanamke umesahau?”
SANCHI: “Na vipi kuhusu Mary, anaendeleaje?”
MIMI: “Mary sijamuona since niko Dar but she’s fine. Unajua nimetoka direct south kuja Dom?”
SANCHI: “Aisee kumbee! Na umezidi kuwa HB plus kunenepa. Ukweli South imekupenda sana.”
MIMI: “Ahsante sana, mimi nakushukuru sana kwa kuniangalizia biashara yangu na nimekuletea zawadi sema nimesahau home.”
SANCHI: “Kesho jumapili niko free nitazifuata ili nipajue na kwako.”
MIMI: “Sawa karibu, badae nitakupeleka dinner Golden Fork, maana unasemaga mimi ni bahiri.”
SANCHI: “Mmhh hapana, kwa lile bata la muda mfupi ulilonipa Dar nakupa heshima bossy wangu.”
Tuliishia kucheka wote kwa sauti ya juu…
Tangu nilipowasili Dodoma, upande mwingine Aggy hakuwa na taarifa yoyote kuhusu ujio wangu. Nilijaribu kumpigia simu mara mbili, lakini hakupokea. Hatimaye niliamua kumtumia ujumbe ili kumpa taarifa, hasa kwa kuwa nilikuwa natumia namba mpya na nilijitambulisha.
Muda wa saa 1 usiku ulipofika, nilitoka na Sanchi kwenda kupata dinner Golden Fork. Ilikuwa ni sehemu ya ahadi yangu kwake na pia njia ya kutoa shukrani na kutambua msaada wake. Tulikaa muda mrefu tukizungumza, na mazungumzo yetu mengi yalijikita kwenye masuala ya biashara na maisha kwa ujumla. Nilifurahi jinsi alivyokuwa akinipa mawazo mapya ya kukuza biashara yangu na mipango yake binafsi ya kimaendeleo.
Wakati bado tuko mezani, sister alinipigia simu. Alinipa taarifa kuwa kesho mchana ataingia Dar es Salaam. Pia alinishauri nisirudi home mara moja, bali nisubiri angalau siku mbili, ili mama J asije kuhisi kama yote haya ni mchezo. Ushauri wake ulikuwa ni mzuri, hivyo nikapanga kuondoka Dodoma jumanne.
Tulitumia takribani masaa mawili tukifurahia dinner pamoja na story zilikuwa haziishi. Baada ya chakula, tuliagana kwa makubaliano ya kukutana tena kesho, ambapo angekuja nyumbani.
Kwa upande mwingine, tangu siku ile tulipokutana Dar na nikampeleka Masaki kupata lunch, nilihisi heshima yake kwangu imeongezeka maradufu.
Mara baada ya kurudi nyumbani, nilipokea simu kutoka kwa Aggy. Aliniambia kuwa alikuwa kwenye seminar na akaomba tuonane kesho. Nilipokata simu, mawazo yangu yakahamia kwa Mary-nilianza kumkumbuka siku alipoamua kuja Dodoma na kufikia kwangu. Tulianza kwa kukaa wote gheto, na baadaye tukahamia nyumba mpya pamoja. Mary alikuwa ameniachia historia kwenye maisha yangu na nilihisi kuna jambo muhimu lililobaki kati yetu, hasa kuhusu suala la mtoto. Nilijisemea moyoni kuwa mara tu nitakaporudi Dar, nitamtafuta ili tuzungumze uso kwa uso na kumaliza mazungumzo yetu muhimu.
Kwa upande mwingine, nilipokuwa nikipanga vitu kwenye kabati, macho yangu yaliangukia mkufu wa Iryn aliouacha nyuma, pamoja na hereni zake alizokuwa akizipenda sana. Nilivihifadhi kwa umakini na nikajiambia, “Siku nikisafiri kwenda South nitam-suprise navyo, na najua atafurahi sana.”
Kabla sijalala, nilimpigia simu kujua maendeleo yake pamoja na ya mtoto. Mazungumzo yetu yalikuwa ni marefu kidogo na kubwa alitamani kujua nina mpango wa kurudi lini Dar es Salaam. Pia, alitaka kujua maendeleo ya miradi yangu na nilikofikia maana alikuwa ana wasiwasi sana juu yangu.
*****
Asubuhi ile niliamka mapema kwa lengo la kusalimia majirani na pia kujua maendeleo yao. Ni desturi yangu kuhakikisha uhusiano wangu na majirani unadumu, hivyo nilizunguka nyumba chache nikibadilishana salamu na maongezi mafupi.
Niliporudi ndani nilikuta simu yangu ikiwa na missed call tatu kutoka kwa Sanchi, nikakumbuka nina miadi naye, hivyo bila kupoteza muda nilimpigia simu. Baada ya kupokea simu, sauti yake ya upole ilisikika ikiniomba nimwelekeze mahali ninapoishi kwa sababu alikuwa njiani anakuja kuniona.
Saa nne asubuhi, Sanchi aliwasili pale home na nilitoka nje kwenda kumkaribisha. Nilipofungua mlango, macho yangu yalikutana na Sanchi aliyesimama pembeni akiwa amependeza sana na alianza kutabasamu. Nilimkaribisha ndani kwa furaha, lakini aliniambia hatakaa muda mrefu kwa sababu alikuwa na ratiba nyingine baadaye.
Ndani ya nyumba kulikuwa na vinywaji baridi vilivyokuwa vimebaki kipindi niko Dodoma, hivyo nilichukua chupa ya wine nikamimina kwenye glasi mbili. Tukaanza kunywa huku tunapiga story mbalimbali na mimi nilimwambia leo atashinda na mimi hadi niridhike. Dakika zilivyokuwa zikisonga, mazungumzo yetu yalizidi kupendeza zaidi. Sanchi ni muongeaji mzuri sana, mwenye uwezo wa kugeuza mazungumzo ya kawaida kuwa yenye kuvutia na kufanya maongezi yetu yawe ya vicheko na utani wa hapa na pale.
SANCHI: “Kuna jambo naomba nikuulize, ila tafadhali usinielewe vibaya. Hivi kati ya Iryn na Mary, ni nani uliyeanza naye mahusiano ya kwanza?”
MIMI: “Iryn ndiye wa kwanza kabisa kuanza naye mahusiano, na hata kufahamiana naye pia.”
Sanchi alitabasamu kidogo, macho yake yakionekana kama yanataka kujua zaidi.
SANCHI: “Aah! Natamani kujua, mlikutana wapi na Iryn? Maana si rahisi kabisa kukutana na mrembo kama yule kwenye sehemu isiyo na hadhi.”
MIMI: “Hahahaa! Mishe mishe tu ndiyo zilitukutanisha, na baadaye tukajikuta tumeanza mahusiano.”
SANCHI: “Wewe mwanaume unabalaa kweli... na Mary je?”
MIMI: “Mary nilifahamiana naye kupitia mdogo wake. Yote yalianza kama urafiki wa kawaida tu.”
Sikutaka kuendelea kulizungumzia lile suala la awali, hivyo nilibadili gia ghafla. Nikaamua kumuuliza kuhusu maisha yake ya mahusiano, maana kwa muda wote tuliokuwa tukifahamiana, hatukuwahi kukaa chini na kuzungumza kwa mapana. Nilijua ana mtoto mdogo wa takribani miaka sita, lakini nilitaka kusikia kutoka kwake mwenyewe kuhusu baba mtoto na hali yake ya sasa kwa ujumla.
MIMI: “Kuna kitu kimoja siku zote nimekuwa nikitaka kuuliza… kuhusu mahusiano yako. Najua una mtoto mdogo, ila sijawahi kusikia ukiongelea upande wa baba mtoto. Mkoje kwa sasa?”
Sanchi alishusha pumzi taratibu,
SANCHI: “Baba mtoto yupo, lakini hatuko intouched sana kutokana na tabia zake. Kila nikimpigia simu kuhusu pesa za matumizi ya mtoto, badala ya kujali mtoto anaanza kuomba game… na kumbuka ana mke hapo nyumbani.”
Maneno yake yalinishtua kidogo;
MIMI: “Ilikuwaje ukaingia kwenye mahusiano na mume wa mtu?”
SANCHI: “Sikujua kabisa kama ni mume wa mtu. Nilikuja kujua baada ya kuwa na mimba tayari, ndipo akanieleza ukweli kwamba ana mke nyumbani.”
MIMI: “Aisee, pole sana kwa kupitia yote hayo…”
Lakini kabla sijaendelea, alinikatisha,
SANCHI: “Nashukuru Mungu nina kazi, naweza kumhudumia mwanangu mwenyewe na maisha yanaendelea freshy. Sina budi kuwa imara kwa ajili yake.”
MIMI: “Pole sana… kwa hiyo sasa hivi upo single, taken, au complicated?”
SANCHI: “Hahahaa… niseme tu ni complicated. Wanaume hamtabiriki bwana.”
Simu yangu ambayo ilikuwa juu ya meza ilianza kulia ghafla. Nilipoitazama screen, jina lililosomeka lilikuwa “Aggy”. Bila kuchelewa nilipokea ili kumsikiliza. Aggy aliuliza nilipo, na baada ya kumjibu kuwa niko nyumbani, akasema kwa haraka:
“Basi nakuja mpaka home sasa hivi.”
Sikuwa na jinsi ya kumkatalia, hivyo nikamwambia:
“Karibu, utanikuta tu hapa.”
Dakika chache mbele Aggy alifika na alinipigia simu kunijulisha, nami nikatoka nje kwenda kumfungulia geti. Nilimkaribisha ndani na ile kufika seblen alishtuka kidogo kukutana na Sanchi amekaa, aliishia kunipiga jicho na story zikaendelea.
Aggy hakukaa sana pale sebleni, alisimama akaaga anakwenda kupumzika chumbani, akituacha mimi na Sanchi tukinywa na kuendelea na mazungumzo yetu ya awali.
Baada ya muda mfupi, niliamua kumfuata chumbani. Nilihisi kuna haja ya kuzungumza naye faragha na pia kumpa zawadi zake nilizokuwa nimeandaa. Nilipoingia tu ndani, kabla hata sijafungua mdomo, Aggy alianza na maswali yake moja kwa moja:
AGGY: “Insider, Sanchi anafanya nini kwako?”
MIMI: “Si kaja kunisalimia tu..,kuna shida?”
AGGY: “Mmh! Na mnakunywa kabisa mpo wawili seblen?”
MIMI: “Kama kungekuwa na shida nisinge hata kukaribisha home, ningeishia kukudanganya tu.”
AGGY: “Na kwanini ulikuwa hujibu text zangu?”
MIMI: “I’m sorry… nilikuwa busy sana. Ndomana hata baada ya kutua Dodoma nilihakikisha nakupigia simu. Usimind, nimekuletea zawadi kwa ajili yako.”
Nilitoa mfuko mkubwa wa zawadi niliokuwa nimeuandaa kwa ajili yake. Ndani kulikuwa na raba kali za Nike, coat la reza, perfume yenye harufu ya kipekee, handbag maridadi, tracksuit, pamoja na hereni, saa na mkufu. Zilikuwa zawadi nzuri kwa kweli, na uso wa Aggy ulianza kuchanua furaha mara tu alipoviona.
Aggy hakukaa sana na aliaga akaondoka kwa makubaliano ya kuonana badae kwenda kupata dinner ya pamoja.
Hii siku nilikaa na Sanchi hadi jioni ilipofika muda wa kuondoka. Kabla hajaondoka, nilimkabidhi zawadi zake ambazo zilijumuisha chaji ya simu, vipodozi, perfume, na mkufu. Alifurahi sana na alinishukuru kwa dhati. Baada ya hapo, nilimsindikiza hadi alipopanda bodaboda na kuondoka na mimi nikarudi ndani kujiandaa kwaajili ya kwenda dinner na Aggy maana alisema atanipitia.
Kwa upande wa Dar es Salaam, sister alikuwa ameshawasili nyumbani na alinijulisha kwa kunitumia ujumbe kupitia WhatsApp. Baada ya kusoma ujumbe wake, nilianza kuchati nae na haikuchukua muda akanipigia simu WhatsApp. Alitaka kujua nitarudi lini Dar?, nami nikamwambia kufikia Jumanne nitakuwa tayari nimerudi. Alisisitiza sana nihakikishe kweli narudi siku hiyo kama nilivyomwambia.
Baada ya kutoka dinner usiku huo nilijikuta nikiwa bize sana na laptop nikipanga mipango yangu ya mbele. Kitu kikubwa kilichokuwa kinanijia kichwani ni suala la kurudi shule. Nakumbuka mara ya mwisho kuonana na Mzee Juma, alinielekeza niandae ripoti kamili inayoonesha gharama zote za chuo hadi nitakapomaliza masomo, ikiwemo ada, chakula, kodi ya nyumba na matumizi mengine muhimu. Alinisisitiza kuwa hataki niteseke nikiwa nasoma ili niweze kutoa matokeo mazuri.
Wakati nikiwa bize kuandaa bajeti yangu ya shule, simu yangu ilianza kulia kwa video call-ilikuwa ni Iryn. Bila kusita hata kidogo, niliipokea haraka sana. Kipindi hiki alikuwa akionekana anadeka sana, nami sikusita kumdekeza kwa moyo wote, maana alikuwa amenipa heshima kubwa kwa zawadi aliyonipa, zawadi ya mtoto.
Mazungumzo yetu yaliendelea kwa furaha, tukipiga story nyingi hadi akaniambia habari kubwa kwamba wiki ijayo anatarajia ugeni mkubwa kutoka Ethiopia na alinihakikishia atanijuza kinachoendelea. Kisha akagusia kwenye mada ya ahadi niliyompa kuhusu Aria kwenda kwa bibi na babu yake. Niliona macho yake yakibeba maswali mengi, hivyo sikusita kumtoa wasiwasi nikimhakikishia nitashughulikia hilo mapema iwezekanavyo.
Baada ya kuagana na mama mtoto, nilibaki nikiwa nimetulia kimya, nikitafakari uzito wa jambo hili maana lilihitaji mipango makini na maamuzi ya haraka. Nilifarijika kidogo pale nilipokumbuka kuwa dada yangu yupo Dar es Salaam akinisubiri, kwani moyoni nilijua atakuwa mtu wa kwanza kunipa ushauri mzuri kuhusu hili suala nyeti.
Kesho yake, siku ya Jumatatu, niliamua kuitumia vizuri kwenda kutembelea plot yangu ya Iyumbu. Nilipofika, nilitembea eneo lote nikihakikisha kila kitu kiko sawa. Baada ya kuridhika na mazingira, niliamua kuondoka na kuelekea ofisini kwangu kushinda.
Pale ofisini, kama ilivyozoeleka, nilikuwa na Sanchi tukipiga story nyingi huku tukicheka sana. Wakati tunazungumza, alinieleza kuwa anatarajia kuja Dar mwisho wa mwezi huu na akaahidi atanicheki ili tupate nafasi ya kukutana na kula bata kidogo.
Jioni ilipokaribia, nilielekea kumsalimia Maggy pamoja na kukagua nyumba yangu. Nilikuwa nimemtaarifu mapema kuhusu ugeni wangu, na yeye kwa upande wake alinieleza kuwa atawahi kutoka ofisini ili tuweze kukutana. Maggy ni mtu ambaye namchukulia kama ndugu, ndiye anayeniangalizia nyumba yangu na kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza mara kwa mara. Tulishinda pamoja hadi usiku, tukipiga stori na hata kupata dinner pamoja, kabla sijaanza safari ya kurudi kwangu ili kujiandaa na safari ya Dar es Salaam.
Usiku huo nilipanga mambo yangu vizuri. Kwa kuwa ningewasili Dar mapema, nilijiambia sina budi kwenda kumsalimia Jane pale Mbweni. Roho yangu ilikuwa inaniuma juu yake, ilikuwa imepita wiki bila kuwasiliana kutokana na ubusy niliokuwa nao. Nilihisi ni busara kwenda kumuona ili kujua maendeleo yake na ya mtoto, hasa kwa sababu pia nilikuwa nimepewa jukumu hili na mzee Pama. Nilishika simu yangu nikitaka kumpigia, lakini nilipogundua muda umeenda sana, niliamua itakuwa vyema nimcheki asubuhi kabla ya kuanza safari.
*****
Jumanne asubuhi, mbele yangu zilikuwa begi mbili kubwa tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam. Aggy hakuwa mbali, alifika kunipa kampani ya kwenda Airport na kabla ya kuelekea Airport, tulipitia kwanza ofisini kwa kuwa nilikuwa na maelekezo muhimu ya kuwapa timu yangu.
Nilitumia takribani nusu saa tukipanga mambo ya kazi na niliwaaga pale na pembeni Sanchi alikuwa akinisubiri ili tuweze kuongea. Nilitumia dakika 10 kuongea naye nikimpa maelekezo hasa juu ya mafundi watakaokuja kufanya marekebisho ya ofisi yangu kwa kufunga vifaa vya kisasa. Muda ulikuwa umeenda sana na nilimuaga Sanchi na tuliishia kwa kukumbatiana-akinitakia safari njema.
Niliporudi kwenye gari nikakutana na uso wa Aggy akiwa amekunja sura. Nilijua nilikuwa nimemuweka muda mrefu sana pale;
AGGY: “Insider, sikuelewi sana siku hizi… na huyu dada.”
MIMI: “Hutuelewi kivipi?”
AGGY: “Jana alikuwa na wewe pale kwako, na huu ukaribu wenu unazidi kunipa mashaka. Na jinsi alivyo… lazima kuna jambo linaendelea.”
MIMI: “Hujui natumia mbinu za kijasusi ili awe ananiangalizia biashara yangu?”
AGGY: “Kwamba hulitamani lile tako?”
MIMI: (nikicheka) “Kwa level niliyofikia hakuna manzi wa kunipagawisha wala kusumbua akili yangu.”
AGGY: “Unaniona mtoto sana.”
Tuliendelea na stori nyingine njiani. Aggy akanifungukia kuhusu mpango wake wa kurudi shule kusoma masters, hivyo tulibadilishana mawazo na ushauri hadi tulipofika Airport. Nilikuwa nje ya muda sana, hivyo hata baada ya kuwasili tuliagana na mimi nikaenda kucheck-in ili kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
Baada ya kutua Dar es Salaam, nilipanda Uber kuelekea Mlimani City kwa sababu Dullah alikuwa akinisubiri kwa hamu kubwa. Safari haikuchukua muda mrefu na ndani ya saa moja nilikuwa nimefika pale Mlimani City. Nilimpigia simu mara moja, naye alikuja haraka kufungua gari yake ili niweze kuweka mabegi yangu salama.
Baada ya kusalimiana kwa furaha ya kuonana tena, tuliamua kwenda kuchill SamakiSamaki kwa ajili ya kupata lunch. Dullah alionekana kabisa kuwa na shauku maana macho yake yalikuwa yanauliza maswali kabla hata hajafungua kinywa. Alionekana ni ambaye Alitaka kwa hamu kusikia kila kilichotokea kule South Africa.
Mara tu tulipokaa mezani, dada mhudumu
alitukaribisha kwa tabasamu kali;
DADA: “Karibuni sana, sijui mnataka lunch au vinywaji?”
DULLAH: “Lunch kwanza, tupe dakika mbili tucheki menu alafu urudi.”
DADA: “Sawa, karibuni.”
Dullah alinigeukia na kunitazama kwa uso wenye furaha.
DULLAH: “Insider, hongera sana kwa kupata mtoto. Kwanza kabisa, umebadilika sana! Hata mwili umejipanga, umenepa kidogo, umekuwa wa kimamton kabisa.”
MIMI: “Hahaha… kila mtu ananiambia hivyo, lakini mimi sijayaona hayo mabadiliko.”
DULLAH: “Hebu nioneshe kwanza picha ya mtoto, nataka nione mwenyewe.”
Nilitoa simu yangu na kuanza kumwonyesha picha za Ariana. Dullah aliangalia kwa umakini, kisha uso wake ukaanza kutoa tabasamu.
DULLAH: “Insider, hii damu yetu kabisa! Naona kabisa mmefanana na huyu dogo.”
MIMI: “Watoto wanabadilika kaka, acha tuone kwanza.”
DULLAH: “Aaah, huyu wa kike atafanana na wewe kila kitu, amini hilo. Nikuulize… sasa hivi nikuite baba nani?”
MIMI: “Baba Ariana.”
DULLAH: “Hongera sana mzee wangu.”
MIMI: “Nitaangalia namna, next time twende wote South Africa.”
DULLAH: “Hapo utakuwa umetisha sana. Afu, umewasiliana na Ghati?”
MIMI: “Ukweli, tangu niende South Africa sijawasiliana naye kabisa.”
DULLAH: “Aisee, Ijumaa alinitafuta kaka. Alikuwa analalamika sana kwamba hupatikani, hata WhatsApp husomi meseji zake. Alikuwa na hofu kubwa, alihisi labda umepata matatizo. Nikamlainisha nikamwambia umepata emergency ya kikazi na umeenda nje ya nchi.”
MIMI: “Dullah, unajua kule South simu nilikuwa naiweka mbali sana. Nilikuwa bize na malezi ujue.”
DULLAH: “Najua, ndio maana sikutaka hata kukuletea stress. Lakini, kaka, fanya juhudi umcheki Ghati. Huyu dada alijitoa sana kwako kipindi kile upo polisi, alikusaidia bila kuchoka. Usimtupe hivihivi na ananitafuta sana kukuulizia.”
MIMI: “Of course lazima nimtafute. Ghati alinisaidia sana, siwezi kusahau wema wake.”
DULLAH: “Sawa, basi jitahidi hata zawadi ndogo umpelekee. Halafu mambo mengine, usimfiche, mchane ukweli kwamba una mke na mtoto. Usije ukasababisha maumivu yasiyo ya lazima, maana asije akawa na malengo yake moyoni.”
MIMI: “Upo sahihi kabisa, nitafanya hivyo.”
Yalikuwa ni maongezi marefu sana kati yangu na mshikaji wangu Dullah, tukipata vinywaji huku tukicheka na kufungua stori nyingi. Tulikaa pale SamakiSamaki kwa takribani masaa manne bila hata kuhisi muda ukipita. Baada ya kuagana naye, nilipanda Uber kuelekea Mbweni kuonana na Jane.
Safari kutoka Mlimani City ilikuwa kimya. Dereva alitumia barabara ya chini (Mwaikibaki) na mimi nilibaki nikitazama mandhari nje ya dirisha nikiwa nimezama kwenye mawazo mazito. Kila dakika kichwa changu kilikuwa kinapishana na maswali mengi ambayo majibu yake nilikosa, ilikuwa kama vita ya kimya ndani ya nafsi yangu.
Nilipowasili kwa Jane, nje ya geti lake, magari yalikuwa yamejaa, yakipark kwa mpangilio usio wa kawaida. Nilishuka kwenye gari na nilisimama kimya kwa sekunde chache, nikibaki nayaangalia magari, haikuwa kawaida.
“Ni nini kinaendelea hapa?” nilijiuliza nikiwa bado nimekamatwa na mshangao.
TO BE CONTINUEDwelcome back brother
Edo kissySEASON 03

TO BE CONTINUED

Umecheza kama konami na free epic😂😂
Daaah😂😂Umecheza kama konami na free epic😂😂
Hatari 😂🙌Daaah😂😂
Unaweza kunitumia boss?View attachment 3356898
Hii Story kwa upande wangu nimeiweka kwenye PDF maana haichoshi kuisoma kwa kuirudiarudia pindi unapokuwa bored na ukiwa na nafasi.
Ongeeni na INSIDER MAN akiruhusu nitawawekea hapa.
Biashara Gani hiyoMkuu ahsante.
Kama hutojali nipe pia wadau wanaouza oils na vilainishi mbalimbali kwa jumla.
Peterson 007SEASON 03