Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Hii ndo Zawadi ya Mzee Juma. The moment napewa hii PC bei yake ilikuwa 5M. Hadi sasa ina 2 years, ni moja ya PC nzuri sana.
 

Attachments

  • IMG_4180.jpeg
    564.9 KB · Views: 93
  • IMG_4179.jpeg
    1 MB · Views: 87
  • IMG_4176.jpeg
    699.2 KB · Views: 77
Hongera sana INSIDER MAN kwa hatua mpya katika maisha yako, kila la kheri bro. Asante pia kwa mafunzo uliyojitoa kutupatia vijana wenzako. Salute 🫡
 
Hii ndo Zawadi ya Mzee Juma. The moment napewa hii PC bei yake ilikuwa 5M. Hadi sasa ina 2 years, ni moja ya PC nzuri sana.
Hivi ni wewe ulikuwa pale makao makuu T R A...na kama ndio wewe basi shikamoo..pia Kuna code moja kama naifungua hivi...inanuhusu Nuru japo kwenye story umemtaja kwa jina lingine
 
Sina jibu la kukujibu huenda wewe ndiye unayetamani maisha ya kimaskini
Hujanielewa , ni kuwa wewe unayaona hayo Maisha aliyo ni Kama akafika inawezekana kwake bado hajafika na halali usiku na mchana anawaza namna ya kumiliki apartments huko New York, Paris, Singapore, Sydney, London , Dubai ama hata maghorofa hapo upanga , masaki na Oster bay,
 
Sawa mkuu
Psychological mtu hutamani kidogo na akikupata kidogo hutamani tena zaidi na zaidi

So alipokuwa maskini huenda alitamani apate tu hela ya kula na kodi basi maisha yaende wakati anaendesha uber ila alipofanikiwa kidogo kama sasa huenda anatamani zaidi kama hayo uliyosema

Binadamu huwa haridhiki
 
SEASON 03
CHAPTER 11

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:

Kadri nilivyoendelea kuwaza, ndivyo nilivyozidi kuhisi kukutana naye hakutaleta maana yoyote. Niliona ni jambo lisilokuwa na faida, bali linaweza kufungua ukurasa mwingine wa matatizo. Baada ya muda wa tafakari ndefu, nilichukua uamuzi wa kukata mawasiliano naye kabisa. Nilihitimisha kuwa kwasasa Muajemi hana msaada wowote tena kwangu, na kilicho muhimu sasa ni kuendelea na maisha yangu.

CONTINUE:
Niliamua kuingia bafuni kuoga, nikiwa najipanga kwa safari yangu ya kwenda kuonana na Sanchi. Kwa upande wa Muajemi, nilimdanganya kwamba nimepata dharura ya kikazi, ninahitajika kwenda Zanzibar kufuatilia mzigo. Muajemi, kwa upande wake, aliniambia kuwa kesho siku ya Jumapili angeondoka kuelekea Kenya, na akaongeza kuwa atarudi tena Tanzania mwezi Desemba.

Saa kumi na moja jioni nilitoka nyumbani, nikiwa nimevaa jeans nyeusi, hood ndefu ya rangi ya maroon, viatu vya Airforce vyeusi, na saa yangu mpya ya Apple Watch mkononi. Kichwani nilivaa cap safi, bila kusahau kujipulizia unyunyu unaonukia vizuri ukitambulisha uwepo wangu. Nilielekea Mnazi Mmoja, Peacock Hotel, kumchukua Sanchi kama nilivyokuwa nimemuahidi awali.

Wakati huo huo, mama Janeth alinipigia simu akiniomba nimsaidie kuwachukua wageni wake JNIA kesho jumapili na kuwapeleka nyumbani. Mama alisisitiza kwamba wageni watakuwa na mizigo, hivyo nikachukue gari kubwa pale kwake. Kwa kuwa nilikuwa njiani kuelekea Mnazi Mmoja, niliona ni bora nipitie Masaki kwanza kubadilisha gari, ili kesho nisihangaike tena kwenda huko, niunganishe moja kwa moja hadi Airport.

Nilipofika Masaki, nilikutana na Jessie, aliyenikaribisha kwa tabasamu na kunipatia funguo za gari. Tulianza kupiga story za hapa na pale na mara nyingi huwa anapenda sana kunitania;

JESSIE: “Hii gari ya mke wako si ungekuwa unaitumia tu? Maana huwa haiendeshwi kabisa.”

MIMI: “Hata wewe umeshindwa kuiendesha?”

JESSIE: “Sina driving licence, lakini mbona leo umependeza sana? Unaenda wapi?”

MIMI: “Mind your business.”

JESSIE: “Ngoja nimpigie simu mke wako.”

MIMI: “Thubutu! Ila naona siku hizi umeanza kuongea Kiswahili vizuri.”

JESSIE: “Iko, najifunza taratibu.”

Nilimwambia tunaonana keshi, kisha niliondoka pale haraka kuelekea kwa Sanchi, ambaye alikuwa akipiga simu mfululizo. Sikutaka kupokea simu zake, hivyo niliendesha gari kwa mwendo wa kasi kuelekea Mnazi mmoja.

Baada ya kuwasili hotelini, nilielekea moja kwa moja mapokezi na nikajitambulisha kwa mhudumu aliyekuwa zamu. Baada ya maelezo mafupi, akanionyesha room number ya Sanchi na kuniambia niende ghorofa ya pili. Nilipanda taratibu, sikuwa nimemwambia kuwa nimefika, nilitaka iwe surprise.

Nilipofika mbele ya mlango wake, niligonga taratibu mara tatu. Kulikuwa na kimya kifupi, kisha nikasikia sauti ya miguu ikikaribia. Mlango ulipofunguliwa, Sanchi alijitokeza taratibu, akitazama kwa tahadhari kama mtu anayechungulia kuona ni nani. Wakati macho yetu yalipokutana, alishikwa na mshangao, kisha uso wake ukajaa tabasamu.

“Wewe!” alitamka kwa mshangao, kisha akacheka kidogo na kunikaribisha ndani.

Nilipoingia, nilihisi pumzi yangu ikibadilika ghafla baada ya kumtizama kwa makini. Alikuwa amejifunga taulo pekee, mapaja yake yakiwa wazi, na makalio yake makubwa yalichoreka barabara, kiasi cha kunifanya nisiseme neno kwa muda. Nilijaribu kujizuia, nikavuta pumzi ndefu na nikakaa kwenye sofa lililokuwa pembeni, nikimwangalia kwa jicho la pembeni huku akitoa nguo kwenye begi lake.

MIMI: “Ulipiga simu mara nyingi, nikadhani ushajiandaa kabisa.”


SANCHI: “Nilijua umenidanganya maana wewe mwanaume una pilikapilika sana.”


MIMI: “Basi jiandae, leo nataka nikutoe stress zote. Nitakupeleka sehemu ambapo mwanaume wako hajawahi kukupeleka.”

Sanchi aligeuka taratibu, macho yake yakinitazama kwa utulivu huku yakiwa na mshangao na hamu, tabasamu jepesi lilichanua usoni mwake.

Baada ya muda mfupi, alimaliza kujiandaa na akaanza kuniita pale. Mimi sikuwa namsikia, maana mawazo yangu yalikuwa mbali kabisa, aliponiita kwa sauti ya juu zaidi, ndipo nilipogeuka kumtazama...

SANCHI: “Insider mbona uko mbali, hivyo unawaza nini?”

MIMI: “Kuna wanaume wanakojolea pazuri asee! Bwana wako anafaidi sana.”

Sanchi aliishia kucheka tu maana hakuwa na jibu la kunipa na aliendelea kujiremba taratibu.

Baada ya takribani dakika kumi, tuliondoka. Kwa upande wake, alionekana kupendeza sana kuanzia mavazi yake, kila kitu kilikuwa kimetulia kwa ustadi wa kuvutia. Tulielekea moja kwa moja hadi kwenye sehemu ya maegesho ambako nilikuwa nimepark gari. Tulipofika pale, uso wake ulijaa mshangao aliponiona nikiwa na gari nyingine;

SANCHI: “Insider another car?”

MIMI: “Ooh! Hivi hujawahi niona na hii gari eeh!”

SANCHI: “Mara ya mwisho kukutana ulikuwa na Benz.”

MIMI: “Usipagawe ni vitu vya kawaida tu bossy wangu.”

Na nilimwambia aingie ili tuanze safari ya kwenda Masaki. Baada ya kuingia ndani ya gari, bila kuchelewa tukaanza safari pale;

SANCHI: “Dodoma kipindi tunafahamiana nilijua wewe si mtu wa kawaida ila ulikuwa unapretend sana kujifanya local.”

MIMI: “Hahaha! Mimi ni mtu wa kawaida tu mbona, siko hata unavyonifikiria.”

SANCHI: “Mtoto na mama yake wazima lakini?.”

MIMI: “Nashukuru Mungu wote wako salama, juzi tu hapa nilikuwa huko kuwasalimia.”

SANCHI: “Insider, unamwanamke mzuri sana dear wangu, kama pisi kweli unayo. Na ninachompenda wifi, hana dharau kabisa yuko poa sana. Ila vipi wifi yangu Mary? Nime-mmiss sana jamani, maana alinichukiaga sana kipindi tuko Dodoma, hasa baada ya kunikuta na wewe Rainbow.”

MIMI: “Habari mbaya ni kwamba hatuko kwenye maelewano mazuri na Mary. Tumeenda wiki sasa bila kuwasiliana.”

Sanchi alinyamaza kwa muda, macho yake yakinitazama kwa makini. Baada ya sekunde chache, akauliza kwa sauti ya upole lakini yenye shauku:

SANCHI: “Lakini imekuwaje sasa, mlitofautiana nini?”

Nilicheka kidogo, na nilinyamaza kwa muda sababu nilikuwa kwenye eneo la hatari ambalo lilihitaji nifocus na usukani. Na nilishia kumpa sababu za uongo sitaka kufunguka kuhusu yaliyokuwa yamejitokeza kati yangu na Mary.

Tuliendelea na mazungumzo kwa utulivu huku gari ikiendelea kukata mitaa ya Masaki kimya kimya. Nilihisi ni wakati muafaka kumwambia ukweli kuhusu maisha yangu kuhusu kile ambacho kwa muda mrefu nilikuwa nikikificha. Nilimgeukia taratibu, nikavuta pumzi ndefu kisha nikasema kwa sauti tulivu:

MIMI: “Sanchi, nataka ujue kitu kimoja kabla hatujaendelea zaidi. Ukiachana na Iryn, nina mke na tumebarikiwa mtoto mmoja, na huyu ndiye mke wangu mkubwa.”

Alinigeukia kwa mshangao, macho yake yakiwa wazi kana kwamba hakuamini kile alichosikia, lakini nikaamua kuendelea kusema ili kila kitu kiwe wazi;

“Ndio, Iryn ni kama mchepuko tu! na Mary naye vivyo hivyo. Wote wanajua ukweli kuhusu mimi kuwa na familia na Mary anajua Iryn ni mke wangu pia.”

Baada ya maelezo hayo, Sanchi alibaki ameduwaa. Alishindwa kuelewa kabisa ni kwa namna gani mwanamke mzuri kama Iryn angekubali nafasi ya kuwa mchepuko. Lakini kilichomchanganya zaidi ni Mary. Huyu naye, kwa akili yake yote na kwa kujua ukweli mzima kuhusu kila mtu kwenye mzunguko huo, bado alikubali kuwa mchepuko.

Sanchi alikuwa na maswali mengi sana wakati huu na aliuliza maswali mengi kwa wakati mmoja ambayo nilikuwa nashindwa kuyajibu. Tulikuwa tunakaribia Seacliff, ambapo nilipanga kumpeleka Sanchi Karambezi Café. Hili suala lilikuwa tayari nimelipanga, lakini ikinilazimu nimwulize ili kumalizia topic tuliyoianza:

“Nikupeleke sehem gani?”

SANCHI: “Wewe nipeleke sehemu yoyote nzuri.”

MIMI: “Nakupeleka Karambezi ni sehemu nzuri na ninamini utapafurahia.”

Tulipofika Seacliff, nilipaki gari upande wa baharini kisha tukashuka taratibu. Mwanga hafifu wa jioni ulimfanya Sanchi aonekane kuvutia zaidi kuliko kawaida. Alikuwa amevaa suruali iliyomkaa vyema, ikichora kwa ustadi umbo lake hadi kiunoni, huku juu akiwa amevalia shati jepesi lililombana vizuri. Rasta zake zilikuwa zimefungwa kwa ustadi, zikionekana nadhifu na zenye mvuto. Uso wake ulipambwa na miwani ya kisasa, na miguuni alivaa raba nyepesi za Nike zilizoongeza mvuto wake.

Tulipokuwa tukielekea ndani, makalio yake yaliyokuwa yamejitokeza kwa ustadi yalivutia macho ya wengi. Wanaume waligeuka kumtazama waziwazi, wengine wakijifanya wanapiga simu ilhali macho yao yamekwama kwake. Nilicheka kimoyomoyo, maana mbinu hizo za mafisi nazifahamu vyema. Hata baadhi ya wanawake walimwangalia kwa wivu wa kimya, wakipima uzuri wake kwa macho ya siri.

Mazingira ya restaurant yalikuwa yenye msisimko na pilikapilika nyingi. Watu wa kila rangi na asili walionekana hapa kuanzia, wazungu, wahindi, waarabu na ngozi nyeusi, wote wakichanganyika kwa utulivu na sauti nyororo za muziki wa nyuma. Hali ilikuwa ya kuvutia, yenye hewa na upepo wa baharini na harufu nzuri ya restaurant iliyoenea kila kona.

Mhudumu alikuja kutupokea kwa tabasamu pana na kutuongoza hadi sehemu tuliyopata kona tulivu, pembeni kidogo, mahali palipokuwa pazuri kwa mazungumzo ya faragha. Baada ya Sanchi kupitia menyu nzima kwa makini, kila mmoja wetu aliagiza chakula alichokitaka. Mimi nikaagiza wine, nikapendekeza tuletewe mapema ili tutumie wakati tunasubiri chakula chetu.

Mazungumzo yetu yakaanza kwa utulivu, tukijadili mambo muhimu ya kazi na maisha. Nilimshukuru Sanchi kwa moyo wa dhati kwa jinsi anavyonisaidia katika kusimamia biashara yangu kule Dodoma ni kweli alikuwa msaada mkubwa sana. Nilimweleza pia baadhi ya mipango yangu ya siku zijazo, naye akaonesha kunielewa na kuniunga mkono kwa maneno ya kutia moyo.

Baadaye mazungumzo yakahamia katika maisha yake binafsi. Nilitamani kujua zaidi kuhusu malengo yake, hasa upande wa mahusiano. Ndipo alipofunguka akanieleza kuwa bado yuko kwenye mahusinao na mwanaume yuleyule ambaye pia ni bosi wake, mtu aliyemteua kuwa meneja wa tawi la kampuni upande wa Dodoma. Kwa sauti ya upole na uso uliochanganyika na huzuni, alisema jamaa huyo ni mume wa mtu.

Sanchi alikiri kuwa si kwamba anampenda sana, bali hali na mazingira yalimfanya aingie katika uhusiano huo. Jamaa huyo, mwenye asili ya Kiarabu lakini aliyekulia hapa Tanzania, ndiye aliyempa nafasi nyingi za kimaendeleo.

Siku hii Sanchi alionekana mwenye furaha isiyo ya kawaida. Alifunguka zaidi, akiniambia kwamba licha ya jamaa yake kuishi Dar es Salaam, hajawahi hata siku moja kumtoa out. Mara nyingi hukutana hotelini tu, kisha kila mtu huendelea na shughuli zake. Nilimsikiliza kimya, nikihisi namna ambavyo alikuwa anazungumza kwa uchungu uliofichwa nyuma ya tabasamu lake.

Kwa upande wangu sikupenda kuendelea na hii mada sababu nilihisi ikimuumiza na kuibua hisia mbalimbali juy yake.

Ilipofika saa mbili usiku, Dullah aliniuliza tutaonana kiwanja gani na akaniambia yuko na Ghati. Kwa kweli sikufurahishwa na uwepo wa Ghati, lakini sikuwa na jinsi. Baada ya kushauriana na Dullah, tulikubaliana tukutane Samaki Samaki, sehemu tulivu yenye muziki mzuri. Nilimwambia afanye utaratibu wa reservation mapema ili tusiwe na usumbufu, naye akasema tayari alikuwa amefikiria hivyo.

Nilimgeukia Sanchi na kumwambia kwa sauti ya upole,

MIMI: “Tukitoka hapa, tunaenda Samaki Samaki kumalizia usiku.”

SANCHI: “Naisikiaga na kuiona instagrama ni pazuri?”

MIMI: “Yeah utaenjoy sana. Unakumbuka nilikuahidi kukulisha bata siku ukija Dar? Sasa leo natimiza ahadi yangu.”

SANCHI: “Wifi yangu hawezi kuchukia ukirudi usiku?”

MIMI: “Anajua niko na wewe, nilimpa taarifa mapema. Kesho njoo nyumbani ushinde, sawa?”

SANCHI: “Nitakuja kwa kweli, maana safari yangu hii nimeipanga kwa ajili yako ndomana nikaja mapema.”

Baada ya muda, Dullah alinipigia tena kuniambia tayari wamewasili na Ghati. Baada ya dakika ishirini hivi, tuliondoka kuelekea Samaki Samaki.

Tulipofika, Sanchi alishindwa kuficha furaha yake. Alikuwa akiangalia mazingira ya pale kwa mshangao na tabasamu. “Hapa pazuri sana!” alisema kwa msisitizo, macho yake yakizunguka kila kona kutizama. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika pale, na hakusita kusifia kila kitu kuanzia mwanga wa usiku hadi muziki wa nyuma uliokuwa unachezwa kwa ladha.

Tulipoelekea kwenye meza ambayo Dullah na Ghati walikaa, Ghati ndiye aliyekuwa wa kwanza kutuona. Niliona jinsi alivyobadilika ghafla, baada ya kumuona Sanchi, ni kama alipatwa na mashaka. Dullah, kwa upande wake aliishia kumtazama Sanchi kwa jicho la wizi na la kifisi.

Baada ya salamu na utambulisho mfupi, tulikaa mezani. Tukaagiza vinywaji zaidi, na nikamwambia Sanchi achague chochote atakachotaka kunywa. Muda wote alionekana mwenye furaha, akitabasamu kila wakati.

SANCHI: “Nimependa sana hapa, kila nikija Dar, nataka tuje hapa tena.”

Nilitabasamu nikamwambia,

MIMI: “Next time tutakwenda kiwanja kingine, nikufahamishe vizuri uzuri wa Dar.”

Nilikuwa nimezama kwenye mazungumzo na Sanchi, tukicheka huku tukibadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali. Dullah naye alikuwa na Ghati upande wa pili wa meza, wakionekana kufurahia usiku wao kwa mazungumzo na vicheko vyao. Mara kadhaa tulijikuta tukijumuika wote kwenye maongezi ya pamoja, tukicheka kwa sauti na kufanya meza yetu kuwa busy.

Hata hivyo, nilihisi mabadiliko fulani kutoka kwa Ghati. Nilijua kitendo changu cha kuwa karibu sana na Sanchi kiliigusa hisia zake. Licha ya yeye kuwa karibu na Dullah, akicheka na kuonekana mwenye furaha, bado alikuwa akiangalia upande wetu mara kwa mara kwa macho ya mtu anayehangaika kuficha jambo moyoni.

Baadae nilipata ujumbe kutoka kwake na ulisomeka;

GHATI: “Naomba tuongee kwa faragha kidogo.”

Nilikaa kimya kwa sekunde chache nikitafakari, kisha nikamjibu kwa kukubali;

MIMI: “Sawa haina haina shida, tangulia parking nakuja nyuma yako.”

Baada ya muda mfupi, niliondoka meza yetu kwa utulivu, nikimfuata nje hadi eneo la parking, pale nilipokuwa nimepaki gari langu.

MIMI: “Nambie mumy nakusikiliza.”

GHATI: “Insider yule dada ni nani? Na kwanini umeshindwa kunitambulisha mimi ni mpenzi wako?.”

Nilimueleza Ghati kwa utulivu kuhusu uhusiano wangu na Sanchi, nikimwambia kuwa sababu kuu ya kutomtambulisha kama mpenzi wangu ni kwa kuwa anamfahamu mke wangu. Nilihofia kwamba jambo hilo lingeonekana kama usaliti na lingeweza kunipotezea heshima mbele ya wote wawili. Nilizungumza kwa uwazi, nikijaribu kumfanya aelewe kuwa haikuwa rahisi kwangu kusimamia hali hiyo.

Baada ya maelezo yangu, Ghati alitulia taratibu. Uso wake ulionekana kuonyesha mchanganyiko wa huzuni na kuelewa. Mazungumzo yakageuka kuwa ya kawaida zaidi tulianza kuzungumza mambo mengine hata hivyo, bado alionesha kutamani tuondoke pamoja usiku huo. Nilimwambia kwa upole kuwa hilo halitawezekana, kwa kuwa nilipaswa kurudi nyumbani. Nilimwahidi kuwa kesho tutakutana mapema, ili tuweze kufurahia siku pamoja kwa utulivu zaidi.

Nilizungusha mikono yangu taratibu kwenye kiuno chake na nikamvuta kuja usawa wangu tukawa tumebana vizuri na nikaanza kumbembeleza pale na hatimae tukaanza kubadilisha lita kadhaa za maji.

Tuliendelea kuzungumza kwa utulivu pale parking, Ghati alinitazama kwa muda kisha akasema kwa sauti ya upole lakini yenye msisitizo:

“Basi baby, tutaondoka wote.”

Nilijua ndani yangu nilichokuwa nimepanga, kwani nilitaka kuhakikisha Sanchi anarudi hotelini salama, huku Ghati akiondoka kwa usafiri wa Uber. Baada ya kusema anataka tuondoke wote pamoja, sikutaka kumuumiza wala kumpa taswira mbaya juu yangu. Nilijua maneno ya kumkatalia yangemuumiza zaidi na angeweza kuhisi kuna something fishy kinaendelea kati yangu na Sanchi.

“Sawa, tutaondoka wote, lakini safari yangu haitakuwa Mbweni na nitakuacha Mbezi Beach, kisha utachukua Uber.”

Ghati alifurahi baada ya kusikia maneno haya kutoka kwangu na akaishia kutabasamu huku akijibebisha. Tulitumia kama nusu saa kukaa pale na hatimaye tukarudi ndani kuendelea kujumuika na kina Dullah.

Sanchi alikuwa amekunywa Moët nyingi kiasi kwamba alionekana kulewa, ingawa bado alikuwa anajitambua. Ilipofika mida ya saa saba kasoro, aliniambia kuwa amechoka na anataka kwenda hotelini kulala. Aliongeza kuwa asubuhi angekutana na jamaa yake, hivyo aliona ni bora aende mapema ili kuepuka maneno, kwani alisema jamaa yake ni mwenye wivu sana.

Tuliondoka wote hadi kwenye parking huku tukiendelea kuzungumza. Wakati huo nilikuwa tayari nimesharequest Uber wa kumpeleka hotelin. Tukiwa pale tunaendelea kupiga story, nilipokea ujumbe kutoka kwa dereva wa Uber akisema ameshafika, na akaomba tufanye haraka kutokana na foleni iliyokuwa eneo la Samaki Samaki.

Nilimtazama Sanchi, nikamwambia kwa upole,

“Twende basi, gari limefika.”

Aliendelea kunitazama kwa muda, kana kwamba hakutaka kuondoka haraka. Badala yake, alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu sana. Mimi, nikiwa kama mwenyekiti wa vikao vya wanaume na nisitake kuonekana dhaifu, nilimkumbatia pia na mikono yangu ikazunguka kiunoni kwake, na nikashusha hadi kwenye makalio yake. Baada ya mkumbatio ule, nilifeel joto kali sana na nilitamani niendelee kumkumbatia.

Sanchi akatabasamu kidogo, kisha kwa sauti ya upole akasema:

“Insider, thank you so much. Leo nime-enjoy sana, na ninafuraha kwa ajili yako.”

Nikamjibu, “Hata mimi nashukuru, hasa kwa kunilindia biashara yangu.”

Baada ya hapo, alipanda kwenye gari la Uber lililokuwa likisubiri. Nilisogea upande wa dereva, nikampa nauli yake na kumwomba ahakikishe Sanchi anafika salama hotelini. Kisha nilirudi upande wa nyuma, nikafungua mlango na kumuaga tena. Kabla sijaendelea kuongea, alinibusu shavuni taratibu huku akitabasamu.

“Insider, bye…” akasema, kisha gari likaanza kuondoka taratibu.

Mara ghafla, Masai mmoja ambaye ni mshikaji wangu wa muda mrefu alinijia pale akiwa na tabasamu usoni. Alikuwa akishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea na Sanchi, alianza kuuliza pale;

MASAI: “Yeloh! Hii shem yetu?”

Nilijikuta nikicheka tu bila kujibu, lakini kabla sijatoa neno, Masai akaongeza tena huku akitikisa kichwa:

MASAI: “Tajiri, hii mali sana.”

Sote tukacheka kwa pamoja. Mimi nilinyamaza, nikabaki nikitabasamu tu. Ukweli ni kwamba Masai wa hapa Samaki Samaki hasa wa Masaki ni washikaji zangu wa ukweli. Wananijua vizuri, wanajua pisi zote ambazo huwa naingia nazo maeneo haya, na hata magari yangu yote wanayafahamu. Sijawahi kukosa parking hata magari yajae namna gani, mimi nikiingia Samaki Samaki au Wavuvi, najua napata parking bila shida na bado huwa wananilindia gari yangu.

Nawapa hii code ishini vizuri na Wamasai, hawa watu wanajua vitu vingi sana, kwa wale ndugu zangu wa chini, hawa jamaa wanaweza kukuunganisha na pisi yoyote kali na ukala kwa bei chee. Mfano, kwenye maeneo mengi ya starehe kwa Masaki mademu wengi sana bei zao ni 1M hadi 500k hizi ndo bei zao elekezi. Ukiongea vizuri na Masai ile pisi kali ambayo inataka 1M unaweza ipata na kuichapa kwa 100k, hawa watu wana connection sana na wanaaminika, msiwadharau.

Baada ya kurudi ndani, hata sisi hatukukaa muda mrefu. Tuliamua kuondoka mimi nikaondoka na Ghati, huku Dullah akiondoka peke yake. Tukiwa njiani, simu yangu ikaita ilikuwa ni Sanchi. Aliniambia kuwa tayari amefika salama hotelini na hata ameoga. Sauti yake ilisikika ikiwa na utulivu, tofauti na ile ya awali. Kabla hatujaagana, tulikubaliana kwamba kesho tutaonana saa saba mchana. Yeye akaongeza kuwa akishamaliza kuonana na bwana wake, atanijulisha mara moja.

Barabarani kote hadi nakuja kupark gari Mbezi Beach karibu na flats za BOT, mikono ya Ghati ilikuwa haichoki kuchezea maiki ndani ya suruali yangu. Kwa upande wake hakuwa hanaelewa kitu muda huu na alikuwa kalegea sana. Macho yake yalikuwa yamelegea sana, bustani yake ilikuwa imelowa vya kutosha, nilitamani sana kwenda kulala naye, lakini sikuwa na huo uwezo.

Saa yangu ilikuwa inasoma ni saa saba za usiku, na nilipiga hesabu kali na za haraka sana juu ya hatima yake. Kwa eneo la barabara ya Mbezi chini, Kwa siku za weekend huwa kunakuwa na movement kubwa sana ya magari. Niliwaza pale nikaona wacha nimfanyie maunyama, sometimes mwanamke anatakiwa akukumbuke kwa mambo mazuri na mabaya pia.

Nilisogea mbele kidogo, kana kwamba naelekea kwenye kituo cha mafuta cha Oryx. Kabla sijafika, nikakata kona kulia kuelekea mtaa wa Upepo Avenue, barabara ya mkato kwenda Upepo Garden. Niliendelea kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu, nikatafuta sehemu tulivu kando ya barabara na nikapaki gari karibu na mti mkubwa.

Nikavuta pumzi ndefu kisha nikafungua mlango wa gari taratibu na kushuka. Nilizunguka upande wa pili, nikamwangalia kwa utulivu, halafu nikamwambia kwa sauti ya upole:

“Shuka, njoo upande wangu.”

We had a fling there kwa karibu dakika 15 hadi ana cum na aliishia kurusha maji mengi sana hadi mkono wangu wa kushoto ukalowa.

Baada ya hapo nilimrequestia Uber wa kumpeleka kwake, mimi nilirudi nyumbani moja kwa moja kupumzika. Nilipofika, nikaingia chumbani nikiwa nimechoka lakini bado na hisia za usiku ule. Niliposhika kitasa na kufungua mlango, nikamkuta wife wangu amekaa kitandani, akichezea laptop yangu mpya HP. Sikutegemea kabisa kumkuta bado macho muda huu.

“Swahiba, hujalala?” nikauliza kwa mshangao.

Akanitazama moja kwa moja machoni, uso wake ukiwa na mchanganyiko wa tabasamu na lawama:

“Napataje nguvu ya kulala na hujarudi hadi sasa hivi?”

“Swahiba, si nilikuaga mapema kwamba nitachelewa kidogo kurudi?”

“Sawa, naomba laptop moja, Baba J.”

“Hiyo moja ni ya masuala yangu binafsi na shule, na MacBook ni ya kazi za ofisini.”

“Huo ni uchoyo! Unaweza kutumia PC moja tu na ukanipa moja.”

Nikauliza kwa utani, “Sasa hapo umeipenda ipi?”

Akanijibu haraka bila kusita, “MacBook! Nimeielewa sana, na nimeshazoea kuitumia.”

Nikamtazama, nikatabasamu:

“Alright, nipe muda nitakununulia yako mpya kama hiyo, yangu ni ya 2021, nitakununulia latest ya 2022.”

Uso wake ukang’aa kwa furaha. Akaniambia kwa sauti ya upole iliyojaa mapenzi:

“Sawa, ahsante. Twende tukaoge, maana nimekumiss.”
*****

Jumapili saa tatu asubuhi, niliondoka nyumbani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kuwapokea wageni wa mama Janeth na kuwapeleka nyumbani kwake Oysterbay. Nilifika mapema uwanjani, hivyo nikalazimika kusubiri takriban saa nzima kabla ya wageni hao kuwasili.

Walipowasili, niligundua walikuwa jumla ya watu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja. Baada ya kusalimiana kwa furaha, niliwasaidia kubeba mizigo yao hadi kwenye gari lililokuwa limeegeshwa sehemu ya maegesho, kisha tukaaanza safari kuelekea Oysterbay.

Wakati wa safari tulijikuta tukiingia kwenye mazungumzo marefu. Wageni hawa walikuwa wanatua Tanzania kwa mara ya kwanza, hivyo walikuwa na shauku kubwa ya kujua mambo mbalimbali kuhusu nchi yetu. Mmoja wa wale wanawake wazungu alionekana kuwa na roho ya urafiki sana, tulielewana haraka, na tangu siku hiyo tumekuwa marafiki wakubwa. Hadi sasa, kila anaporudi Tanzania, huwa hakosi kumtembelea Junior kumjulia hali.

Baada ya kuwafikisha salama nyumbani kwa mama Janeth, niliendelea kubaki hapo kwa muda kidogo nikizungumza na Jessie. Alionekana mwenye wasiwasi, akilalamika kuwa Iryn hajibu jumbe zake wala kupokea simu. Nilimfariji nikimwambia huenda Iryn amekuwa bize na malezi, na kumtia moyo asiwe na wasiwasi kwani kwa hakika atampigia pindi atakapopata nafasi.

Baada ya maongezi mafupi na Jessie nilimuaga, nilielekea kuangalia kazi iliyokuwa ikifanywa na mafundi kwenye apartments za mama. Niliamua kuanzia Masaki, ambapo nilifurahi kuona kazi imekamilika kwa kiwango kizuri. Baada ya kujiridhisha, nikaondoka kuelekea Kijitonyama kukagua upande mwingine. Huko nilikuta mafundi bado wanaendelea na kazi zao.

Nilipoingia ndani, nilienda kukaa na Rose, tulikuwa jikoni, nami nikaishia kushangaa ustadi wake wa kutengeneza keki. Kumbuka, nilishawahi kuwaambia kwamba Rose ni mtaalamu sana wa kutengeneza keki na ana biashara yake ya bakery inayohusisha kutengeneza keki, mikate, na bites mbalimbali.

Tulipokuwa tukiendelea na mazungumzo, Rose alinikumbusha kuhusu Iryn. Alinishauri niwasiliane naye kwa kuwa hata namba yake nilikuwa nimeisahau kumwachia. Kwa upande wangu, Iryn hakuwa amenitafuta tangu jana tulipopiga simu tukiwa wote na mimi pia sikuwa nimemtafuta tena.

Hatimaye nikaamua kumpigia tena simu na haikupokelewa, ingawa niliona alikuwa online kwa sababu ujumbe niliomtumia ulifika, lakini hakusoma. Wakati nikijiuliza shida ni nini, nilipigiwa simu na Sanchi, ambaye alinijulisha kuwa yuko tayari na ananisubiri nimchukue. Nilimweleza achukue Uber aje Kijitonyama, nikimwambia atanikuta hapa nikimsubiri.

Wakati huo huo, Ghati naye alikuwa akinipigia simu mara kwa mara. Baada ya kumalizana na mazungumzo ya Sanchi, nikaamua kumpigia haraka. Nilikumbuka mara moja kuwa nilikuwa nimemuahidi kwenda kwake, lakini sikupata muda kutokana na ratiba zangu kuwa ngumu. Nikamueleza ukweli, nikifafanua jinsi nilivyokuwa bize na ukaguzi wa mafundi, jambo ambalo tayari alilifahamu.

Hata hivyo, Ghati hakupendezwa sana na maelezo yangu. Aliendelea kusisitiza anataka kujua ni muda gani hasa nitaenda, akinikumbusha ahadi yangu. Nilipoona Ghati anaendelea kusisitiza ni lini nitakwenda kwake, niliamua kusema ukweli wangu bila kuficha chochote.

MIMI: “Ghati, ukweli ni kwamba kila ninapofikiria kuja kwako, huwa nakosa amani ya moyo kabisa.”

Kulikuwa na ukimya wa sekunde chache, kisha nikasikia sauti yake upande wa pili wa simu ikiniuliza kwa mshangao:

GHATI: “What do you mean?”

MIMI: “Ninahisi kama una mwanaume mwingine. Tafadhali, niambie ukweli kama ambavyo mimi nimekuwa mkweli kwako.”

GHATI: “Huwezi kuwa serious, na kwanini unanambia hivi au sababu ya mimi kujirahisha kwako unafikiri ni malaya?”.

MIMI: “ Sijamaanisha hivyo, naona unataka kufanya kikao hiki kiwe kirefu zaidi. Mimi siko huko sababu sisi bado sio wapenzi, hatuko kwenye mahusiano rasmi- we are just having a fling.”

GHATI: “What? Kwamba haya yote tunayofanya pamoja unamaanisha hatuko kwenye mahusiano?.”

MIMI: “Mahusiano ni mipango na sio kukurupuka, ni lini mimi na wewe tulizungumza na kupanga kuhusu hili.?”

GHATI: “Insider thank you.” Na akakata simu.

Baada ya kuzungumza na Ghati, nilitabasamu kidogo kisha nikarudi ndani kuendelea na mazungumzo na Rose. Aliniuliza ikiwa kuna usalama, nikamkonyeza kidogo kwa utani. Baada ya takriban dakika 10, Sanchi alinipigia simu akiniarifu kwamba tayari wamefika Makumbusho. Nikamwambia wanisubiri kidogo kwenye kituo cha daladala cha Sayansi, ndipo nikaondoka.

Nilimuaga Rose, na kabla ya kuondoka, aliniambia nisubiri anifungie cake za kula njiani, kisha nikaondoka kwa spidi kuelekea kituo cha Sayansi. Nilipofika, nikaona Uber imepark mwanzoni mwa kituo, ikiwasha double hazard, na mimi nikasimama mbele kabisa ya kituo. Nilimpigia simu Sanchi, nikamwambia ashuke na aje mbele tuondoke.

Nilimwona Sanchi kupitia side mirrors, akiwa amevalia gauni refu lililokuwa wazi juu, akitembea kwa mwendo wa taratibu. Baada ya kufika, alifungua mlango na kuingia ndani ya gari. Baada ya salamu fupi na tabasamu, tukaanza safari kuelekea nyumbani. Nilikata kona ya kulia kwenye mataa ya ITV kuelekea Mikocheni, lengo langu nije kutokea Mwaikibaki Road, hii ndo njia rahisi ya kwenda nyumbani.

Tukiwa njiani, nilianza kumuuliza kuhusu hali yake ya jana. Alisema yuko poa kabisa, na hakusikia hangover za pombe kama ilivyokuwa kwa siku zingine. Baada ya kurudi hotelini na kuoga, alikuwa sawa kabisa.

MIMI: “Unajua kwanini huna hangover? Ni kwa sababu ulikunywa vinywaji vya gharama ndomana, sasa uko freshy.”

SANCHI: “Hili ndo najua kutoka kwako. Lakini huku Kijitonyama ulikuwa na mishe gani, maana wewe mwanaume, kwa pilikapilika sikuwezi.”

MIMI: “Huku nilikuja kuangalia maendeleo ya kazi, kuna marekebisho ya security mafundi wanafanya kwenye apartments za mama yangu, ambaye ni mkurugenzi kwenye kampuni ninayofanyia kazi. Na kabla hujaondoka, itabidi uje ofisini, pia naweza kukupa zawadi.”

SANCHI: “Lazima nije naondokaje bila kukuaga, bossy wangu?. Halafu nina swali, hivi yule mwanamke wa jana usiku ni nani? Maana kuna muda mlitoka nje pamoja na mkatumia muda mrefu sana.”

MIMI: “Kampuni ambayo inafanya marekebisho kwenye hizi apartments ni mfanyakazi wake, naye ndiye nilimpa kazi hii. Wana service nzuri sana, na ninafikiria kuja kufunga kwenye biashara zangu Dodoma.”

SANCHI: “Ooh, kumbe she is so beautiful.”

Nilicheka tu kwa sababu sikutegemea Sanchi aseme hivyo. Baada ya hapo, nikabadilisha kauli yangu kidogo na kuanza kumuuliza kwa utani sababu ya kuvaa gauni refu, naye akajibu:

“Ni kwa sababu nataka viungo vyangu vipumue wewe unanionaje?”

Baada ya kauli hii tuliishia kucheka wote kwa pamoja na maongezi mengine mafupi yakaendelea.

Sanchi alionekana kuvutiwa sana na mazingira ya Mwaikibaki Road, hasa baada ya kuvuka roundabout ya Kawe. Alifurahia sana utulivu wa eneo hili na upepo mzuri unaotoka baharini, jambo lililomfanya awe na furaha zaidi wakati wa safari yetu.

Baada ya kufika nyumbani, nilishuka kufungua geti. Baada ya kuingiza gari ndani, nilirudi tena kufunga geti na nikashangaa kuona Junior amesimama kibarazani, akiniita pale. Hii ni tabia ya Junior akisikia geti linafunguliwa, huangalia dirishani na kuthibitisha kama ni gari la baba, kisha lazima atoke kunipokea.

Sanchi alimnyanyua juu na kuanza kuongea naye kwa furaha, wakati mimi nikiendelea kumkaribisha ndani;

SANCHI: “Insider, una mtoto mkubwa hivi na mmefanana kila kitu, hapa kweli ulikaza sana kiuno asee, hongera sana.”

MIMI: “Hahaha ahsante, huyo ndo first born wangu, dume la mbegu.”

Mama Junior hakuwa mbali, alikuja sebule pale kumsalimia Sanchi. Bila kuchelewa, nikafanya utambulisho rasmi. Wakati nikiwa katika utambulisho huo, tuligundua kuna ugeni mwingine ni dada yake mama J alikuja pia kutusalimia, na alikuwa akipika jikoni.

Baada ya kumaliza utambulisho wa Sanchi, ilibidi nifanye utambulisho wa pili wa shem wangu, kisha tuliwaacha mama J na Sanchi wakiendelea na mazungumzo, huku sisi tukienda jikoni kuzungumza na dada yake, tukichanganya vicheko, utani na mazungumzo ya heshima.

Baada ya kupiga story chache, baadaye wife na Sanchi walikuja jikoni. Niliona ni muda mzuri wa kwenda chumbani, hivyo nikaamua kuwaachia uwanja. Nikiwa chumbani, nilimkumbuka sana Mary, na tamaa ya kusikia sauti yake ilinifanya nikumbuke jinsi ya kuwasiliana naye. Hapo nikapata wazo la kumpigia kupitia namba yangu nyingine.

Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na niliporudia kupiga tena, bado haikupokelewa. Hatimaye, nikaamua kumuandikia ujumbe mfupi nikaeleza hisia zangu na kumwambia kwamba nampenda sana, nime-mmiss, na niko tayari kuzungumza naye kuhusu yote na kujibu maswali yake kama atanipa nafasi hiyo.

Nilipiga simu ya Iryn kwa mara nyingine tena, lakini hakupokea. Wasiwasi ulianza kunikumba muda huu na nilijiuliza kwa nini hapokei simu zangu, kuna nini kinaendelea?. Mtu wa kuwasiliana na kujua afya ya Iryn alikuwa ni Samatha, lakini sikuwa na namba yake. Sababu Iryn alikataa kabisa mimi kuwa na mawasiliano na mdogo wake, hivyo nikaamua kumcheki Lucy.

Baada ya kumpigia Lucy na kusalimiana, alinipa taarifa kuwa wanajiandaa kurudi Dar es Salaam jioni na kila kitu kimeenda sawa. Baada ya maongezi mafupi, nikaenda moja kwa moja kwenye suala lililonifanya nipige simu ni kuhusu Iryn. Nilimuuliza kama wamekuwa na mawasiliano na Iryn siku ya jana na leo, akasema hapana.

Baada ya kuona Lucy anaanza maswali, nilikata simu na kumpigia Jimmy (shem wangu), lakini naye hakuwa anapokea simu. Nikamtumia ujumbe nikimwomba anipigie pindi atakapoona simu zangu.

Niliwaza sana pale kitandani, nilihisi huenda Iryn amekumbwa na matatizo, maana si kawaida yake kuwa kimya hivi. Kwa kawaida, Mama Aria huwa ananitafuta asubuhi, mchana, na usiku, mara nyingi tukiwasiliana kupitia FaceTime au whatsapp.

Nilipata wazo lingine la kuwasiliana na Mama Janeth. Niliiona kama uamuzi mzuri, lakini muda mzuri wa kuongea naye ungekuwa kipindi ninapo-mpa mrejesho wa kazi yake, na hapa ndiyo nitaingizia suala la Iryn.

Baadae nikahamishia mawazo yangu kwenye biashara yangu ambapo nilikuwa nikitafakari mipango ya kupanua biashara yangu na kuanza kuomba tenda kwenye taasisi za serikali pamoja na zile za binafsi. Nilijua huu ulikuwa wakati sahihi wa kusajili kampuni yangu rasmi na kupata VAT, ili niweze kushiriki kwenye zabuni kubwa na kupanua zaidi wigo wa biashara. Nilihisi ari mpya ndani yangu, hamasa ya kupeleka ndoto zangu mbali zaidi.

Wakati bado nikiwa katika tafakari hizo, simu yangu ilianza kuita. Nilipoangalia, niliona jina la Dullah liking’aa kwenye skrini. Niliamua kuipotezea kwa muda, nikijua fika kwamba lazima lingekuwa jambo linalomhusu Ghati na sikutaka kushughulika nalo kwa wakati huo. Alipiga tena mara ya pili, kisha akatuma ujumbe mfupi, akiniomba nimtafute baadaye. Niliahidi moyoni nitafanya hivyo, lakini si wakati ule.

Wakati huo, wife aliingia chumbani akiwa na tabasamu, akaniambia,

“Njoo dining, chakula kipo tayari.”

Tulielekea mezani ambapo kila kitu kilipangwa kwa ustadi meza ilikuwa imejaa vyakula vya kila aina, harufu ya pilau, wali, kuku na tambi bila kusahau juisi ya matunda. Wakati tunakula, mazungumzo yalikuwa mengi na yenye furaha. Ilikuwa moja ya siku zile ambazo familia yote inaonekana kuwa katika hali ya utulivu na maelewano.

Baada ya muda, nilimwambia wife kuhusu mipango ya jioni, ambapo tungeenda na Sanchi ‘The Whitesands Hotel’ kupumzika kidogo na kupata chakula cha jioni. Pamoja na vinywaji.

Sanchi alionekana kushangazwa na kufurahishwa kwa wakati mmoja. Alitabasamu kwa furaha na akashukuru kwa moyo wa dhati. Kwa upande wa shemeji yangu, dada wa mke wangu, alisema hangeweza kuungana nasi kwani alikuwa na ratiba nyingine muhimu kwa siku hiyo.

Baada ya chakula, tulikaa sebleni tukibadilishana mazungumzo ya hapa na pale. Nilijikuta nikifurahia kuona jinsi Sanchi na mama J walivyoanza kuelewana. Kwa mbali niliweza kuhisi urafiki mpya ukiota mizizi polepole, kwani mazungumzo yao yalikuwa ya kirafiki, na yenye hali ya uelewano.

Jioni ilipowadia, tuliondoka kuelekea The White Sands Hotel. Tulikuwa watatu tu ambao ni mimi, wife, na Sanchi. Junior pamoja na dada zake tuliwaacha nyumbani; tuliona hakuna ulazima wa kuambatana wote.

Tulipowasili hotelini, tulipokelewa na mandhari ya kuvutia na upepo mwanana wa Bahari ya Hindi ukipuliza taratibu. Tulitembea taratibu hadi Jet Bar, sehemu ambayo imejengwa ndani ya bahari.

Sanchi, aliyekuwa akifika maenao haya kwa mara ya kwanza, alishindwa kuficha furaha yake. Macho yake yalikuwa yakizunguka kila upande kwa mshangao, akifurahia utulivu na uzuri wa mazingira.

Baada ya kupata sehemu nzuri ya kukaa, tuliagiza vinywaji na kuendelea na mazungumzo. Nilimwelezea mama J kuhusu nafasi kubwa ambayo Sanchi anayo katika kusimamia biashara zetu kule Dodoma, na jinsi alivyochangia mafanikio mengi tuliyoyapata.

Wife alikuwa tayari anasikia mengi kuhusu Sanchi, lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kumwona uso kwa uso. Alimshukuru kwa mchango wake mkubwa, akionyesha upendo na heshima ya dhati. Kisha akapendekeza, mwisho wa mwezi tutoke wote kwenda Dodoma, tuone biashara zetu huko.

Mazungumzo yalikuwa ni mengi sana, pia hali ya utulivu na ubaridi unaotokana na upepo wa Bahari ulituvuta pamoja na kufanya story ziwe tamu zaidi huku tukipata ladha ya muziki wa mbali.

Ilipofika saa nne usiku, tulipanga kuondoka. Sanchi alionekana mwenye furaha kubwa sana na alishukuru kwa nafasi ya kumwona mama J na kumfahamu, na aliahidi kwamba kila anapokuwa Dar es Salaam kwa shughuli za kampuni, atahakikisha anampitia kumsalimia.

Tuliondoka pale, nikianza kumshusha mama J nyumbani. Baada ya hapo, nikaondoka kumpeleka Sanchi hotelini. Njiani, alionekana kimya, akiniangalia kwa makini kama mtu aliye na kitu cha kuzungumza lakini hawezi kupata maneno.

Tulipofika hotelini, nilimsindikiza hadi kwenye room yake. Alinikaribisha ndani, kisha akasema kwa upole lakini kwa uthabiti:
“Usiondoke subiri.”

TO BE CONTINUED ON TUESDAY
 
Ila insider banah ni mnafiki eti

"Usiondoke subir".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…